Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis akitoa taarifa kwa waandishi wa habari. Video na taarifa kwa hisani ya Munir Zakaria
Kitu kinachosadikiwa ni bomu (mfano wa sausage) kimerushwa na watu wasiojulikana katika duka la Sahara Store liliopo eneo la Darajani majira yasaa nane za usiku wa kuamkia leo na kusababisha taharuki, mshtuko na moshi mzito katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Maghrib Mkadam Khamis Mkadam amewaeleza waandishi wa habari leo ofisini kwake kuwa watu hao wakiwa ndani ya gari aina ya Pick Up (namba hazijapatikana) walirusha kitu hicho wakati wakitokea Bwawani kuelekeaMkunazini, na walipofika katika duka hilo walipunguza mwendo na kurusha kitu hicho katika makreti yaliyopo mbele ya duka hilo na baadae kutokomea kusikojulikana.
Aidha Kamanda Mkadam amesema baada ya kurusha kitu hicho, mlinzi wa duka hilo (Amour Kassim Amour) alichukua kitu hicho kilichokuwa kikitoka moshi na kukirusha barabarani ambapo kiliripuka na kusababisha mshtuko mkubwa, taharuki pamoja na uharibifu wa barabara, ambapo POLISI imefanikiwa kupata mabaki ya unga unga pamoja na kokoto zilizotokana na athari za mripuko huo.