WANAFUNZI wa skuli ya Michakaeni B, darasa la kwanza na Pili, wakiimba wimbo maalumu wa kumkaribisha, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna (mwenye kofia kati katiu) wakati alipokuwa akiingia kwenye banda maalumu la TZ 21, katika maadhimisho ya kilele
cha Elimu bila malipo Pemba, kilichofanyika Gombani Kisiwani Pemba
cha Elimu bila malipo Pemba, kilichofanyika Gombani Kisiwani Pemba
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna mwenye kofia nyeupe, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mratib msaidizi wa mradi wa TZ 21 Hassan R. Libingai ndani ya banda la maonyesho ya vitabu vya masomo mbali mbali ya wanafunzi, huko Gombani katika
maadhimosho ya Kilele cha Elimu Bila ya Malipo
maadhimosho ya Kilele cha Elimu Bila ya Malipo
WANAFUNZI wa darasa la Kwanza na Pili skuli ya Michakaeni B, wakichora maumbo mbali mbali katika katika maadhimisho ya Elimu bila ya Malipo, yaliyofanyika huko katika uwanja wa Michezo Gombani kisiwani Pemba.
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna akisikiliza hadithi ya Ziro, iliyosomwa na wanafunzi wa skuli ya Michakaeni B, katika maadhimisho ya kilele cha Elimu Bila ya Malipo Pemba
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna, akiwakabidhi wanafunzi zawadi wanafunzi wa skuli ya Michakaeni B, waliosoma hadithi ya Zero, katika maadhimisho ya kilele cha Elimu Bila ya Malipo Pemba
WANAFUNZI wa skuli ya Alhamis Kempu, inayomilikiwa na JWTZ kisiwani Pemba, wakishiriki kwenye maandamano ya kilele cha maadhimisho ya Elimu Bila ya Malipo, yaliyofanyika katika kiwanja cha Gombani Pemba.
MIONGONI mwa wanafunzi walioshiriki katika maandamano ya kilele cha maadhimisho ya Elimu Bila ya malipo, wakiwa na bango lao maadhimisho hayo yaliyofanyika Gombani kisiwani Pemba
WANAFUNZI wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba, wakimsikiliza kwa makini waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna, wakati alipokuwa akiwahutubia katika kilele cha maadhimisho ya elimu bila ya Malipo, yaliyofanyika huko gombani kisiwani Pemba
WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wakishindwa kuzuwia hisia zao na kujikuta wakiimba wimbo maalumu wa kilele cha maadhimisho ya elimu bila ya malipo, yaliyofanyika huko gombani Pemba
WASOMAJI utenzi Fatma na Halima wakiuhani utenzi wao katika kilele cha maadhimisho ya elimu bila ya malipo, yaliyofanyika katika kiwanja cha michezo Gombani kisiwani Pemba
WANAFUNZI 20 wa kujitolea kutoka nchini Marekani, wanaosomesha skuli ya Tumbe, Sizini na Msuka wakiwa wamevaa nguo za kiasili za kizanzibari, ni miongoni mwa wageni waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya elimu Bila ya Malipo, huko Gombani kisiwani Pemba
MKUU wa mkoa wa kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya elimu Bila ya Malipo, yaliyofanyika Gombani kisiwani Pemba
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna, akiwahutubia walimu na wanafunzi kutoka skuli mbali mbali za mikoa mitano ya Zanzibar, katika kilele cha maadhimisho ya elimu bila ya malipo yaliyofanyika Gombani kisiwani Pemba.
(Picha zote na Abdi Suleiman, Pemba.)