Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanawake Zanzibar wataka serikali tatu

$
0
0
WANAWAKE wa Zanzibar wamesema suala la serikali tatu ni lazima liandikwe kwenye katiba za serikali ya Tanganyika na Zanzibar ili kuweka wazi mambo ambayo hayataingizwa katika Muungano.
Wanawake hao walitoa kauli hiyo juzi katika Kongamano la Wanawake wa Zanzibar kuhusu Katiba lililoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).
Akichangia mada kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya na hatma ya wanawake, Mariam Ahmed Omary, alisema alishauri wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiwa inaendelea na mchakato wake, ni vema zikaundwa nyingine mbili moja ikishulikia mambo ya Tanganyika na nyingine ya Zanzibar.
“Wanzanzibari sote tunataka serikali tatu, lakini ni vema kwanza kila nchi ikapata Katiba yake ili iweze kuundwa ya Muungano …huwezi kutaka mtoto mkubwa wakati hata mdogo huna na huwezi kuzaa kabla ya kupata mimba,” alisema Omary.
Alisema wanachokisubiri kwa hamu ni wakati wa kura ya maoni ya kukubali au kukataa hoja zilizotolewa kwa ajili ya kuandikwa kwa Katiba mpya ya Tanzania.
Sitti Mohamed Ally alisema kuanza kuandikwa kwa katiba za nchi mbili (Tanganyika na Zanzabar) kutasaidia na kuyaweka wazi mambo yaliyo na yasiyo ya Muungano ambayo sasa yanawakanganya.
“Kwa sasa hata hatuelewi kama masuala ya elimu, afya na kodi kama ni ya Muungano au siyo … lakini zikiwepo hizi Katiba mbili ndiyo ije ya tatu … kila suala litakuwa wazi tena kwa mapana,” alisema Ally.
Mtoa mada katika kongamano hilo, Lilian Wassira, aliwataka wanawake hao kukumbuka historia na matukio mbalimbali ambayo yanayotokea kutokana na kasoro nyingi zilizomo katika Katiba ya sasa hata kuundiwa tume tofauti bila mafanikio.
Wassira alisema kasoro hizo zilizojitokeza na zinazojitokeza mpaka sasa zimetengeneza chuki baina ya serikali ya Zanzibar na Tanzania, aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele wa kupigania Katiba mpya.
Awali akifungua kongamano hilo la siku moja, m chumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Josephine Mushumbusi, alisema suala la kupatikana kwa Katiba mpya si suala la mtu mmoja bali linawataka watu na makundi yote kushiriki kikamilifu katika kura ya maoni na hasa wanawake.
Chanzo - Tanzania Daima

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles