Mkurugenzi wa Kampuni ya Ekika inayoshughulikia matengenezo wa uwekaji wa nyasi bandia katika uwanja wa amani Bwana Ben Mush akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juhudi zinazochukuliwa na kampuni yake kuendeleza ujenzi huo ili kuwahi kwa wakati.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishuhudia mitaro ya uwanja wa amani ilivyofanyiwa matengenezo na kuwa katika kiwango kinachokubalika.Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Hoteli ya Uwanja wa amani kuhakikisha kwamba matengenezo yanayofanywa katika hoteli hiyo yanamalizika kwa wakati ili hoteli hiyo iwahi kutoa huduma wakati wa mashindano ya kombe la Mapinduzi.
Meneja wa uwanja wa Amani Maalim Khamis akimuonyesha Balozi Seif marobota ya nyasi Bandia ambazo tayari zinasubiri kuwekwa katika uwanja wa amaji Mjini Zanzibar.
Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.