Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Timu ya Taifa ya Zanzibar Yaaza Vizuri Chalenji. 2--1

$
0
0
Timu ya Taifa ya Zanzibar leo imeaza vizuri kuiwakilisha Zanzibar katika Michuano ya Chelenji kwa kuifunga Timu ya Taifa ya Sudan ya Kusini kwa mabao 2-1, mchezo uliofanyika uwanja wa Nyayo nchi Kenya katika jiji la Nairobi.

Timu ya Zanzibar iliaza mchezo huo wa ufunguzi kwa mashambulizi m akali kupitia kwa washambuliaji wake Khamis Mcha (Viali) Sulemain Selemba na Kiungo mchezeshaji Masoud Ali (Chile)

Timu ya Zanzibar imepata bao lake la kwanza katika dakika ya saba ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake  Suleiman Kassin Selembe. 

Bao la pili limepatikana katika kipindi cha pili cha mchezo katika dakika ya 67 kupitia kwa mshambuliaji wake Waziri Salum.

Zanzibar ingeweza kuondoka na ushindi mkubwa kutokana na wachezeaji wake kumuliki mpira katika kipindi chote cha mchezo,kama washambuliaji wake wangekuwa makini akina Khamis Mcha Vialli na Ali Badru kupoteza nafasi nyingi langoni kwa timu ya Sudan.


Timu ya Sudan imepata bao lake katika kipindi cha pili kupitia mshambuliaji wake Fabiano Lako katika dakika ya 73 ya mchezo.    
  
Timu ya Zanzibar imewakilishwa na Abdalla Rashid,Salum Khamis,/Ally Khan,dk78,Waziri Salum,Shaffi Hassan,Mohammed Fakh,Sabri Ali , Masoud Ali, Suleiman Kassim, Awadh Juma,na Khamis Mcha Vialli / Amour Omar dk44, /Adeyoum Saleh dk62.

Timu ya Sudan Kusini imewakilishwa na Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Edomon Amadeo, Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas Jacob, Godfrey Peter, Francis Khamis/Fabiano Lako dk68 na James Joseph. 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles