Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar akiiada timu ya Taifa ya Zanzibar, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikielekea Nchini Kenya kushiriki Michuano ya Kombe la Chalenji, inayoaza leo kwa kufungua dimba na timu ya Taifa ya Sudan ya Kusini. Ikiwa na Kikosi chake kilichokuwa kimejianda vya kutosha na kuahidi kurudi na ushindi ikiwa ni Zawadi kwa Wazanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dokta wa timu ya Taifa ya Zanzibar akimpatia huduma ya kwanza mshambuliaji wa timu hiyo Khamis Mcha Viali.wakati wakiwa katika mazoezi katika uwanja wa miembeni mnazi mmoja kabla ya kuondoa wakiwa katika maandalizi.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar Seif Bausi akiwa kibaruani akitowa maelekezo kwa Wachezaji wake katika mazoezi yao katika uwanja wa miembeni Unguja hivi karibuni.