Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Miti Mikubwa katika Mji Mkongwe Zenj.

$
0
0
Moja ya Mti wa historia katika mitaa ya mji mkongwe ni Huu Mbuyu uliooko katikati ya Mji wa Unguja na kuwa kivutio kwa Wageni na Wananchi wanaotembelea katika Visiwa vya Zanzibar na kujiuliza Mbuyun huu umepandwa lini na una umri gani tangu kuota katika sehemu hii.

Mbuyu huu uko katika mtaa wa Mkunazini maarufu kwa Batashi huvutia watu wengi wanaopita katika eneo hilo na hasa wageni na kuchukua picha yake kuwa kumbukumbu yao wakati wakiwa katika ziara ya kitalii Unguja.

Sehemu hii iliwahi kufanywa eneo la kupumzikia kwa kupata viwanji kwa wageni (Mgahawa) na Mzee Riami enzi za uhai wake. Na sasa umeaza ujenzi wa maduka kando ya mbuyu huu na sehemu ya ndani kujingwa kwa ajili ya wageni kupata Viburudisho wakiwa katika matembezi yao Zenj.

Sehemu kama hizi ni moja ya vivutio vya Utalii wanaotembelea katika maeneo ya mji mkongwe ili kutunzwa na kuweza kuvutia wageni wanaofika Zanzibar na kupata historia ya mbuyu huu.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>