Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya MrishoKikwete, akikata utepe kuashiria kuzindua Alama za Usalama Barabarani kwa Watu Wenye Ulemavu, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu, huadhimishwa Duniani kote.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Usalama barabarani ya Watu wenye Ulemavu (NCPDRS) na mbunifu wa alama za barabarani kwa watu wenye ulemavu ,Bw. Jutoram Kabatelle,kabla ya kuzindua rasmi alama mpya kwa watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mabanda ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Bi. Lupi Maswanya kwa kutumia akitoa shukrani kwa lugha ya alama huku mfasili akitafsiri kwa sauti wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma risala kwa kutumia braille katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa cheti kwa niaba ya TBC Mtangazaji mahiri wa stesheni hiyo ya Taifa Bi. Amina Mollel katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Wartu Wenye Ulemavu Tanzania katika maadhimishi ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.