Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

DK. SHEIN:KAMATI ZA AJIRA ZIELIMISHE VIJANA HALI YA AJIRA NCHINI

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                       4 Disemba, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa moja ya wajibu wa Kamati za Ajira katika ngazi zote ni kuielimisha jamii hasa vijana juu ya hali ya ajira nchini na hatua zinazochukuliwa na Serikali.
Alisema kuwa kamati hizo ziwaelimishe vijana kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mhitimu na kufafanua mipango mbadala iliyoandaliwa na Serikali ili kuwawezesha vijana waweze kujiarjiri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alieleza hayo wakati alipokuwa akizungumza katika Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma kwa mwaka 2012/2013 na robo mwaka ya mwaka wa fedha 2013/2014.
Katika kikao hicho Dk. Shein aliitaka Wizara hiyo kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa kasoro zilizogunduliwa katika utafiti wa utumishi Serikalini uliofanywa na Ofisi hiyo yanarekebishwa.
Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Wizara na Idara za Serikali kuhakikisha zinafuata taratibu zote za uajiri ikiwa ni pamoja na kuwapatia watumishi mikataba ya ajira na kuweka kumbukumbu sahihi za watumishi.
Aliitaka Wizara hiyo kuimarisha Ofisi ya Nyaraka za Taifa iliyopo Kilimani kwa kuipatia huduma zote zinazotakiwa ili kuimarisha mazingira ya utunzaji nyaraka za taifa pamoja na kuhimiza umakini wa watumishi wa idara hiyo muhimu kwa Taifa.
Ameipongeza Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma kwa kufikia kiwango cha kati ya asilimia 71 na 100 cha utekelezaji Mpangokazi wake.
Hata hivyo alihimiza ushirikishwaji wa watumishi wote wa idara tangu wakati wa kupanga mpangokazi hadi utekelezaji wake ili kuimarisha utumishi wa pamoja katika idara na Wizara za Serikali.
Kufanya hivyo alieleza kunarahisisha kuleta ufanisi katika utendaji kwa kuwa watumishi wanafanya kitu walichokitayarisha wenyewe na hatime inaleta utulivu katika idara na Wizara za serikali.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alieleza umuhimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma kuweka katika Mtaala wake mafunzo ya uongozi wa utumishi wa umma ili kuanda viongozi katika utumishi wa umma nchini.
Alisema chuo hicho pamoja na mafunzo inayoyatoa hivi sasa kinapaswa kuwa chimbuko na tegemeo la nchi katika kuandaa viongozi katika utumishi wa umma.
Katibu Mkuu Kiongozi alisisitiza umuhimu wa Wizara kutilia mkazo na kuweka umakini zaidi katika kupanga malengo yanayotekelezeka ili kurahisha tathimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo.
Alibanisha kuwa malengo yakifafanuliwa vyema na shughuli za kufanikisha malengo hayo zikianishwa ipasavyo kazi ya kufuatilia na kutathmini utekelezaji inakuwa rahisi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mwalimu Haroun Ali Suleiman alieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 na mwaka 2013/2014 Wizara yake imepanga kutekeleza malengo 12.
Malengo hayo alisema yamekusudia kuimarisha mazingira kusaidia kupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa wananchi,kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sheria za kazi, kushaajihisha upatikanaji wa fursa zaidi za ajira na kuimarisha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi wa umma.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kujenga uwezo wa watumishi wa umma, Kuratibu, kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo, Kuimarisha utendaji katika utumishi wa umma, Kuongeza upatikanaji wa kazi za staha kwa wote  hususan vijana na Kuimarisha matumizi ya mifumo ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano.
Malengo mengine ni Kuimarisha uandaaji, utekelezaji na uratibu wa Sera, Mipango na Programu za Wizara, Kuimarisha hali ya usalama na afya katika sehemu za kazi, Kuogeza ufanisi katika utekelezaji wa Sheria za kazi, Kimarisha usimamizi wa nyaraka na kumbukumbu za Taifa na Kuweka miundo na taratibu nzuri za kuendesha Serikali.
Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara hiyo ilieleza kuwa mwaka wa fedha uliopita Wizara ilifanya uhakiki wa watumishi wa Serikali katika Wizara 14 ambapo jumla ya majalada binafsi 15,530 yalikaguliwa ambapo kwa Wizara mbili zilizobaki yaani Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Wizara ya Afya zitafanyiwa ukahikiki katika mwaka huu wa fedha.
Taarifa hiyo ilizidi kubainisha kuwa katika kuwajengea uwezo watumishi wa umma Wizara imo mbioni kukamilisha Rasimu ya Sera ya Mafunzo ya watumishi wa Umma  na pia Wizara inakamilisha uandaaji wa Muongozo wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>