Na Miza Othman Maelezo-Zanzibar 8/12/2013
Serikali Jamii na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zimeombwa kushughulikia suala la udhalilishaji wa kijinsia kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba suala la ukatili wa kijinsia linaondaka kabisa Visiwani hapa.
Hayo yameelezwa leo huko Eacrotanal na Mkurugenzi wa Maendeleo Wanawake na Watoto Rahma Ali Khamis ikiwa ni maadhimisho ya siku ya 16 za wanaharakati wakupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema kwamba Wizara imetayarisha mpango wa utekelezaji wa kisekta zidi ya udhalilishaji wa kijinsia ambao unalengo la kuweka mtandao wa sekta na kuunganisha jitihada za kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Aidha Mkurugenzi Rahma Ali amesema kwani hivi sasa kumeshapitishwa sheria ya mtoto dhidi ya udhalilishaji iliyopitishwa mwezi Machi 2011 uliozingatia upatikanaji wa haki, fursa na ulinzi wa mtoto wakiwemo wakike kupitia taasisi husika na jamii kwa ujumla.
Wizara kwa kushirikiana na taasisi husika imefanyia mapitio sheria ya mahakama ya kadhi ya mwaka 1985 ili kubaini mapungufu yake katika kutoa haki kwa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wakijinsia, alisema Mkurugenzi Rahma Ali.
Nae Msaidizi Afisa Watoto Mohammed Jabir Makame amesema endapo mtoto amefanyiwa ukatili wa kijinsia hupata athari ya ulemavu wa viungovya kawaida na uzazi,kushindwa kusoma vizuri,kuongezeka kwa mimba zisizo tarajiwa na kuongezeka kwa virusi vinavyosababisha ukimwi.
Hata hivyo amesema ni vyema wazazi kuwa na wawasiwasi wa mara kwa mara na kuchukuwa jitihada za makusudi kwa kufuatilia nyenendo za watoto wao wakati wanapo kwaenda Skuli, Chuoni na hata wanapokwenda kucheza na wenzao.
Kongamano hilo lilijumuisha vitengo mbali mbali wakiwemo Askari, Daktari na Maafisa kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja,Kusini Unguja na Mkoa wa Mjini.
Ujumbe wa mwaka huu ni Amani ya Duniani huanzia Nyumbani tupigane na vitendo vya utumiaji wa nguvu zidi ya wanawake na watoto.
MWISHO.
IMETOLEWA NAIDARAYA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.