Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

‘Wasomi, vyombo vya habari wanaharibu kiswahili’

$
0
0
Na Mwashamba Juma
WAKATI Zanzibar inaadhimisha  miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, lugha ya kiswahili imezidi kuimarika na kukua kutokana na juhudi zinazochukuliwa na sekali ya kuieneza lugha hiyo.
Katibu Mkuu wizara ya habari,utamaduni,utalii na michezo, Dk. Ally Saleh Mwinkai, aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la Kiswahili lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika kampasi ya chuo hicho,Beitras.
Alisema juhudi za serikali ya Zanzibar kukiimarisha kiswahili zilianza tokea mwaka 1964 baada ya rais wa kwasnza wa Zanzibar kutangaza kiswahili kitumike kama lugha rasmi katika shughuli za serikali.
Alisema katika kutekeleza juhudi hizo taasisi mbalimbali za kusimamia na kukienzi kiswahili kwa wakati huo ziliundwa zikiwemo Baraza la kiswahili, Baraza la sanaa, Idara za kiswahili katika vyuo vikuu na kituo cha kimataifa cha uatafiti na uendelezaji wa lugha ya kiswahili.

Alisema juhudi hizo kwa sasa zinaendelea baada ya kuanzishwa Kamisheni ya kiswahili ya Jumuiya ya Afriaka Mashariki ambayo ofisi zake zipo Zanzibar.
“Hapana shaka juhudi zinazochukuliwa na serikali ya SMZ zimeleta mafanikio makubwa miongoni mwao ni kukilea kiswahili sambamba na kuongeza wataalam katika ngazi zote za taaluma,” alisema.
Alisema kukua kwa kiswahili ni kuongezeka misamiati na matumizi ya kijamii, utamaduni, mazingira, sayansi na teknolojia pamoja na kutanuka kisarufi.
Alisema katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi,idadi ya waandishi wa vitabu vya fasihi na lughawiya hasa katika tanzu za mashairi, riwaya na tamthilia, imeongezeka ikilinganishwa na miaka ya nyuma na sasa vinatumiaka katika taasisi mbalimbali za taaluma za ndani na nje ya Zanzibar.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya wasomi hukipotosha na kukitumia vibaya kiswahili kwa kubuni maneno yasiyolingana na ufasihi unaostahiki.
“Kuna matumizi ya maneno yanachefua nyoyo kwa watambuzi wa lugha ya kiswahili wanapoyasikia yakitamkwa, cha kutisha ni kwamba wanaofanya hivyo ni wataalamu wetu na kwenye vyombo vyetu vya habari,” alisema.
Alisema hali hiyo haikiimarishi kiswahili bali inakipotosha na kurudisha nyuma juhudi za serikali kukikuza na kukiimarisha.
Alisema kuna haja ya kuendelea kuimarishwa kiswali kwani kila kinachokua hulazimika kuimarishwa ili kisife kama ilivyo kwa kiswahili.
Aidha alisema wasomi wengi hupendelea kutumia lugha za kingeni wanapokuwa kwenye mihadhara ya watu, warsha au makongamao, kwani wengi huona hawatotambulika kuwa wasomi, matokeo yake hukiacha kiswahili kitumike mitaani na baadhi ya sehemu za kazi.
Alisema jamii ina jukumu la kukienzi na kujivunia lugha yaona na wawe tayari kukizungumza mahala popote bila kuona aibu.

Barani Afrika kiswahili kinazungumzwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya,Uganda, Burundi,Rwanda, na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya  Congo kwa Afrika ya Kati. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>