( حق المسلم على المسلم ست : إذا لقيته فسلم عليه ، و إذا دعاك فأجبه ، و إذا استنصحك فانصح له ، و إذا عطس فحمد الله فشمته ، و إذا مرض فعُده ، و إذا مات فاتبعه ) .
Kutoka kwa Abu Hurayrah, Allaah Amuwie radhi amesema. Mtume Swalla Alaahu ‘alayhi Wasallam amesema:
Haki za muislamu kwa muislamu mwenzake ni sita: Utakapokutana nae umsalimie, atakapokuita umuitike, atakapokunasihi umsikilize nasiha zake, atakapoenda chafya umuombee rehma ( yarhamuka Allaah – Allaah Akurehemu), atakapougua ukamkague (kwa kumtembelea na kumjuulia hali) na atakapofariki umsindikize (kwa kwenda maziko yake). Muslim