Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi : Uzinduzi wa kituo cha umeme Zoni ya Kaskazini

$
0
0

 
Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa kituo cha umeme Cha Zoni ya Kaskazini.

 
Wasoma utenzi, Asha Haji kulia na Mwajuma wakighani katika ufunguzi wa kituo cha umeme  Zoni ya Kaskazini - Gamba

 
Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman akijiandaa kukata utepe na kufungua rasmi kituo cha utoaji huduma za jamii cha zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba, Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano, Mhe: Rashid Seif Suleiman akisalimiana na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk alipowasili katika ufunguzi wa kituo cha Zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba, Mkoa wa Kaskazini Unguja.



Na ZECO

WANANCHI wamepewa elimu ya kununua taa (bulb) zenye kutumia umeme mdogo (energy server) ili kupunguza matumizi makubwa ya umeme na kupunguza gharama kubwa ambayo wananchi wanaitumia kwa kulipia umeme.

Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman aliyasema hayo wakati akifungua kituo cha umeme cha zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuwa, ghara za umeme wakati mwengine huongezeka zaidi kutokana na wananchi kutumia taa zenye kutumia umeme mkubwa ambazo taa moja unaweza kutumia kwa taa nyingi zenye kutumia umeme mdogo (energy server) inagawaje bei yake iko juu zaidi.

“Na sisi wananchi tuwapige chenga ZECO kwa kutumia balbu zinanzotumia umeme mdogo, ingawaje bei yake ni ghali zaidi kuliko zile zinazotumia umeme mkubwa lakini tuweke kidogo kidogo kwani balbu moja ya bei rahisi unaweza kutumia balbu takriban saba (7) zinazotumia umeme mdogo hii itapunguza gharama”. Alisema Mheshimiwa Waziri.

Aliwaeleza wananchi wa Mkoa wa Kaskazini kuweza kikitumia kituo hicho kilichopo Gamba ili kukipa uhai kituo hicho na kusema ya kuwa matumizi ya umeme ni nafuu sana kulikoni ya nishati nyengine.  

Aidha, Mheshimiwa Waziri aliwataka wananchi kuweka kumbu kumbu za risiti za malipo yao ili kuondoa migogoro kwa wananchi na Shirika la umeme.

Kwa upande mwengine Mheshimiwa Rashid ametoa ahadi ya kuishuhulikia bara bara ya njia hiyo kutoka Chaani Kikobweni hadi Gamba kipande ambacho kinaonekana kimekuwa kibovu kwa kuwa na mashimo mengi.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Mustafa Aboud Jumbe amesema kituo hicho kimerejeshwa kutoa huduma baada ya kusita kutokana na kuwosogezea karibu wananchi wa Mkoa huo huduma za umeme.

Nao wananchi wa Mkoa huo wamelipongeza Shirika la Umeme kwa kufungua kituo hicho kwani kimeweza kuwapunguzia masafa ya kufuata huduma mjini.

Kituo hiki kinatoa huduma za kiufundi za umeme, malipo ya umeme kwa mita za kawaida na huduma za kuwasajili wateja wapya.

Shirika la Umeme (ZECO) katika kuadhimisha miaka hii 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar limeweza kufungua miradi mitano (5) tokea shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 zianze. Miradi iliyofunguliwa ni mitatu kwa upande wa kisiwani Pemba na miwili kwa upande wa Zanzibar.

Miradi hiyo ni uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa njia mpya ya umeme kisiwa cha Makoongwe, ufunguzi wa mradi wa umeme kijiji cha Kichaka, ufunguzi wa ujenzi wa njia mpya ya umeme Ukunjwi ambayo yote hii ni kwaupande wa Pemba na ufunguzi wa kituo cha utoaji huduma za kiufundi kwa jamii zoni ya Kusini (Makunduchi) na zoni ya Kaskazini (Gamba).

 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>