Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk Shein : Tuongeze kasi, bidii na ushirikiano kufikia malengo

$
0
0


STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

    Zanzibar                                                                     31 Disemba, 2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wazanzibari kuutumia mwaka ujao wa 2014 kwa kuongeza kasi, bidii na ushirikiano katika utendaji kazi ili Zanzibar iweze kufikia malengo ya maendeleo iliyojiwekea ifikapo mwaka 2015.


Amesema mwaka 2014 ni mwaka muhimu katika kuuweka mustakbala wa maendeleo ya Zanzibar kwa kuwa ifikapo mwaka 2015 Serikali itafanya tathmini ya utekelezaji wa mipango yake mikubwa ya maendeleo ukiwemo Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Awamu ya Pili-MKUZA II.


Akitoa salamu zake za mwaka mpya wa 2014 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amebainisha kuwa Zanzibar ikiyafikia malengo yake maendeleo sio tu kutachochea ari na hamasa kwa wananchi wake bali hata kwa washirika wake wa maendeleo na Jumuiya ya Kimataifa.


Kwa hiyo amewakumbusha wananchi wajibu wao wa kuitumika nchi pamoja na kuimarisha na kuendeleza umoja na ushirikiano, amani, utulivu na mapenzi baina yao.


Katika mnasaba huo ametoa wito kwa wananchi kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kwa watumishi wa umma wafanye kazi kwa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria ya Utumushi wa Umma na Kanuni zake.


Dk. Shein amesema amefurahishwa sana kuona katika kipindi hiki Zanzibar inaadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi wananchi wamekuwa wakionesha mshikamano, upendo na uzalendo bila kujali itikadi zao za kisiasa na ubaguzi.


Hali hiyo ameielezea kuwa ni uthibitisho wa kutosha wa mapenzi baina ya wananchi na kwa nchi yao.   


Kwa hiyo ametaka wananchi wazidi kuzingatia kuwa wana wajibu wa kuendelea kuyatetea, kuyalinda, kuyaenzi na kuyaendeleza Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964.


Katika salamu hizo Dk. Shein amewataka wananchi wajiandae pia kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yatakayofanyika mwezi April mwakani na kusisitiza kuwa Muungano huo ndio msingi wa kuimarisha udugu wa wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.


Ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika maonyesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ambayo anatarajia kuyazindua rasmi tarehe 2 Janauri, 2013 huko Beit el Raas 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>