Na Ali Issa Maelezo 3/4/2025.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wakilishi Hamza Hassan Juma amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwafanyia wema na kuwaombea dua viongozi waasisi walio tangulia kwa mola kwani ni sehemu yao kubwa ya maisha katika uhai wao walitumikia Taifa lao kwa uzalendo.
Ameyasema hayo huko kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Afisi Kuu ya CCM Zanzibar wakati wa ziara ya kumuombea dua Muasisi wa Taifa hili, Mwana Mapinduzi Marehemu Pili Khamis Mpera.
Amesema Marehemu Pili alikuwa ni kijana Mzalendo na imara ambae aliitumikia nchi kwa heshima na uzalendo jambo ambalo halitosahulika kamwe kwa viongozi wa sasa na kizazi kijacho.
Amesema utumishi wake ni chimbuko la kupatikana uhuru wa Zanzibar kwa kushirikiana na viongozi wezake jambo ambalo Zanzibar leo hii imefikia hatua kubwa kimaendeleo.
Aidha Mhe Hamza amesema Serikali ya Zanzibar kwa kuwajali viongozi wake imeweka utamaduni wa kuwaombea dua jambo ambalo ni jema na litaendelezwa.
Aidha Waziri Hamza alisema wasisi hao wamewapa funzo kubwa viongozi waliopo madarakani na kizazi kiliopo kwamba duniani ukifanya mambo mema naiwapo umekufa utatajwa kwa mazuri ulio fanya kama inavyo dhihirika wazi kwa waasisi na marehemu Pili Khamis Mpera.
Nae mwana familia wa Marehemu Hassan Khamis Mpera aliishukuru Serikali kuweka utaratibu wa kuwaombea dua wazee wao na kusema kuwa wameliridhia hilo kwa moyo mkunjufu.
Aidha aliishauri Serikali kuwaekea kumbukumbu wasisi wao kuwa watu marufu kwa kuyatuza majina yao kupitia majengo ya serikali,Barabara kama walivyo viongozi maarufu ili kizazi kijacho kufahamu asili ya majina ya viongozi waasisi.
Mapema Afisa Tawala wa Mkoa wa Mjini Said Mrisho akimkaribisha mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mjini Khamis Seif Said alisema dua alio ombewa Muasisi Pili Khamis Mpera ni muendelezo wa utaratibu uliowekwa na serikali kuwaombea dua viongozi wake wa sisi ili kuwakumbuka kwa mambo mema walio fanya viongozi hao katika uhai wao wa kilitumikia taifa lao.
Dua hiyo iliongozwa na Sheikh Sharief Abdulrahaman Muhidin kutoka ofisi ya Mufti Mkuu Znzibar alisema kuwa mtu anapokufa mambo yote hukatika isipo kuwa mambo matatu ndio yanayobakia nayo ni Mtoto Mwema Elimu yenyemanufaa na Sadakatul njaria.