Quantcast
Viewing latest article 25
Browse Latest Browse All 35745

WAZIRI NDUMBARO ATAKA MIKAKATI YA PAMOJA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA

 Image may be NSFW.
Clik here to view.

Na Oscar Assenga,Tanga
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amezitaka familia, viongozi wa dini na uongozi wa mkoa wa Tanga kuweka mikakati ya pamoja ya kupambana na ukatili wa kijinsia ili kukomesha tabia hiyo ambayo kwa mkoa huo ni tatizo kubwa tofauti na mikoa mingine nchini.
Akizungumza leo katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa kisheria ya mama Samia (MSLAC), Waziri Dkt Ndumbaro alisema ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa linaloathiri jamii kwa njia nyingi, na ni muhimu kuwa na mikakati thabiti ya kutokomeza tabia hiyo ili kukomesha vikundi vinavyosababisha ukatili hususani kwa wanawake na watoto na hatimaye kuhakikisha kwamba wahanga wanapata msaada wa haraka.
Alisema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemtuma alete salamu katika uzinduzi huo ili kuhakikisha kuwa masuala hayo yanashughulikiwa katika Kampeni hiyo kwa kutoa msaada wa kisheria bure kwa timu hiyo.
Alisema kampeni hiyo ipo katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ibara ya 120-123 ambayo inaelezea suala la utawala bora hivyo wahanga wanapopata haki jamii itakoma kufanya mambo hayo.

"Ilani Ile haikuandikwa bure, ukatili wa kijinsia unaofanywa kwa watoto na wanawake tunatakiwa kila mmoja katika familia tuweke mkakati wa kupambana nalo," alisema Waziri Ndumbaro na kuongeza,
"Tanga ni mkoa wenye imani ya dini, tutumie taasisi zetu za dini kukemea masuala ya ukatili,".
Amewataka watendaji wanaohusika na masuala ya haki, wasiogope kuamua kesi za ukatili kwa kutumia taratibu, kanuni, Sheria na taratibu.
Waziri Dkt Ndumbaro alisikiliza malalamiko mbalimbali ya wananchi na kupanga kukutana nao kusikiliza pande zote ili kufikia muafaka na haki kwa pande zinazokinzana.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum, Wakili Msomi Amon Mpanju, alisema mkoa wa Tanga unaongoza kwa matukio ya ukatili ambapo jumla ya visa 7,320 yaliyoripotiwa mwaka jana mkoa huo ulikuwa na visa 457.
Mpanju alisema ili kupambana na matukio hayo viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuepusha migogoro ya kifamilia katika jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ustadh Rajab Abdarahman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutumia maono yake ya kuanzisha kampeni hiyo ambayo itasaidia wananchi katika utatuzi na haki zao.
Aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kutumia kampeni hizo kwa kuwa serikali imetumia fedha kuhakikisha migogoro ya kisheria inatatuliwa na wananchi kupata haki zao.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Balozi Dkt Batlida Burian, naye pia alimshukuru Rais Dkt Samia kwa mageuzi makubwa aliyofanya ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na ya kisiasa na kampeni ya mama Samia itasaidia kupunguza migogoro iliyokuwepo.

Mwisho

Viewing latest article 25
Browse Latest Browse All 35745

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>