Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36229 articles
Browse latest View live

ZECO yailipa TANESCO 500m/- kila mwezi

$
0
0
Na Mwandishi wetu
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi, amekanusha tuhuma za Shirika la Umeme (TANESCO) kwamba linaidai Zanzibarkiasi cha shilingi bilioni 47 kutokana na matumizi ya umeme.

Alisema wamekuwa wakipokea shilingi milioni 500 kila mwezi kutoka Shirika la Umeme Zanzibar, ikiwa ni malipo ya umeme  unaotumiwa Zanzibar.

Maswi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwasilisha mada kwa Wahariri na waandishi wa habari kuhusu mikakati inayochukuliwa kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa umeme utakaokidhi matakwa ya Mradi wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaotazamiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi ujao hadi mwaka 2033.

“Kwanza niwaambie (waandishi wa habari),deni hili ni la zamani sana ila ,SMZ imekuwa ikilipa kila mwezi na hata hivi sasa tumepokea  shilingi milioni 500 za malipo ya umeme kwa Zanzibar tu,” alisema.


“Nawaambia mkawaambie wote wanaosema kwamba Zanzibar inadaiwa na TANESCO kuwa huo ni uongo na kama mtu hajafanya utafiti hana haki ya kuzungumza,” alisema.

Pia,aliwataka wananchi kutowasikiliza watu aliodai kuwa ni wanafiki kutokana na kuamua kuzungumzia mambo ya TANESCO  nje bunge.

Aliwataka wanasisasa  wanaosema kuhusu nishati na madini kuhakikisha  hawapotoshi ukweli.

Aidha alisema TANESCO na  Wizara ya Madini na Nishati, zimekubaliana kutekeleza mipango waliyojipangia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha umeme unapatikana kwa uhakika na kwa bei nafuu ili ifikapo 2025  na asilimia 75 ya Watanzania  wawe wanatumia nishati hiyo.

Alisema,Juni 30 mwaka huu,wataipatia  TANESCO shilingi bililioni 80 ikiwa ni ruzuku kuhakikisha inapata uwezo wa kujiendesha.

Magazetini Leo Tz Bongo.

Harakati katika Soko la Mwanakwerekwe Mwezi wa Ramadhani leo.

$
0
0
Wananchi wa Mji wa Zanzibar wakiwa katika harakati za mahitaji ya manunuzi ya Futari katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Ubguja. Bei za bidhaa katika soko hilo zilikuwa juu katika siku ya leo nazi moja katika Soko la Jumla imeuzwa kwa shilingi 700/= fungu la mihogo liliuzwa katiki ya shilingi 1000/= Boga Shs 2500/= , ndizi ya Mkono mmoja iliulwa kati ya shilingi 1000/= na 2500/= kwa dole moja


Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Wajumuika katika Futari na Watoto wa Yatima ya Nyumba ya Watoto Mazizini na SOS.

$
0
0
Keki maalum walioandaliwa Watoto Yatima wa Kijiji cha SOS na wa Nyumba ya Serekali ya Watoto Yatima Mazizini kusherehekea miaka 48 ya Benki ya Watu wa Zanzubar tangu kuazishwa kwake mwaka 1966 Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakiwa katika futari waliowaandaliwa watotoyatima wa nyumba ya watoto yatima mazizini na wa Kijiji cha SOS Mombasa ikiwa na kuadhimisha miaka 48 ya Benki ya Watu wa Zanzibar tangu kuazishwa kwake mwaka 1966 Zanzibar.
                                        Vijana tuleni futari imeandaliwa kwa ajili yenu hii.



               Mambo ya Futari na Watoto Yatima Zanzibar. kuadhimisha miaka 48 ya PBZ.
Watoto wetu tuleni ndivyo inavyoonekana Wafanyakazi wa PBZ wakizungumza na Watoto Yatima wa Nyumba ya Mazizini na SOS wakati wa futari ilioandaliwa kwa ajili yao na PBZ.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi Viwe akijumuika na Watoto wa Kijiji cha SOS katika futari ilioandaliwa na PBZ kwa Watoto hao ikiwa ni kutimiza miaka 48 ya PBZ, hafla hiyoimefanyika katika Nyumba ya Watoto yatima Mazizini Zanzibar. 

Watoto wa Nyumba za Watoto Yatima za SOS na Nyumba ya Watoto Yatima ya Serekali ya Mazizini, wakijumuika na Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar  katika futari ilioandaliwa na PBZ kwa ajli ya Watoto hao katika makazi yao Mazizini Zanzibar. 











Watoto wa Kijiji cha SOS na Wa Nyumba ya Watoto YatimaMazizini wakikata keki na kulisha kuadhimisha kutimia miaka 48 ya PBZ tangu kuazishwa wakifurahia na wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar baada kupata futari iliandaliwa kwa ajili yaWatoto.iliofanyika katika Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar.
Mfanyakazi wa PBZ akimlisha keki mmoja wa Watoto Yatima wakati wa kujumuika na Wafanyakazi wa PBZ katika futari walioandaliwa Watoto hao ili kujumuika kuadhimisha miaka 48 ya PBZ., katikati anayefurahia ni Mkurugezi Masoko wa PBZ Bi. Viwe akijumuika na Watoto hao katika makazi yao Mazizini Unguja. 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba afungua mafunzo ya siku 10 kwa wawezeshaji

$
0
0

 
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba,Mhe: Juma Kassim Tindwa, akifungua mafunzo ya siku 10 kwa wawezeshaji kuhusiana na kaya masikini kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa TASSAF Chake Chake Pemba(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Viongozi wa jimbo la Gando wakabidhi boti

$
0
0
 
MBUNGE wa Jimbo la Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe:Khalifa Suleiman akimkabidhi boti aina ya Faiba, mmoja wa wananchi wa Fundo, ambae jina lake halikupatikana, boti hiyo iliyotolewa na viongozi wa jimbo hilo, kulia ni mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe;Saidi Ali Mbarouk, hafla hiyo iliyofanyika huko Fundo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
VIONGOZI wa jimbo la gando, wakiwa katika faiba waliyowakabidhi wananchi wa kisiwa cha Fundi, wakiitumia kuvuka kutoka Fundo kwenda Wete.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

WANANCHI wa kisiwani Fundo jimbo la Gando wilaya ya Wete, wakiisukuma faiba yao waliyokabidhiwa na viongozi wa jimbo hilo, mara baada ya kukabidhiwa rasmi, ambayo itawasaidia katika kuwavusha wananchi kwenda mjini Wete kutafuta mahitaji.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Kamanda wa wa Polisi Mkoa wa Arusha Akipokea Taarifa kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda

$
0
0
Meneja wa NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akimkabidhi ripoti ya wanahisa kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas katika hafla ya kukabidhi pikipiki kwa jeshi hilo ofisini kwa kamanda sabas makao makuu ya jeshi hili mkoani hapa

Mahmoud Ahmad
Jeshi la polisi limepokea msaada wa pikipiki mbili kutoka kwa benki ya NMB katika hafla iliyofanyika makao makuu ya jeshi hilo na kuhudhuriwa na askari mbalimbali akiwemo mkuu wa upelelezi mkoa,afisa mnadhimu wa jeshi hilo mkoani hapa na wafanyakazi wa benki ya nmb.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilienda sambamba na kukabidhi taarifa ya gawiwo la mwaka la wanahisa lililokabidhiwa kwa kamanda wa polisi kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas na meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo katika ofisi za kamanda huyo

Akizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo kamanda wa polisi mkoani hapa alisema kuwa pikipiki hizo zimekuja wakati muafaka na zitasaidia katika kuweka hali ya usalama na kuwaraisishia kufika maeneo ya tukio kwa uraisi hivyo wakilishukuru benki hiyo na kuitaka kutoishia hapo.

Nae meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini alisema kuwa wametoa pikipiki hizo ili kuweza kulisaidia jeshi hilo katika kuhakikisha usalama na  ulinzi wa raia unaendelea kuimarishwa kwani hali ya usalama wa raia umeonekana kuimarika kwa siku za karibuni hivyo wakiwa kama wadau wetu tumeona kuwasaidia hichi kidogo tukijaa liwa tunaweza kuongeza zaidi.

Pichani ni meneja wa NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akimkabidhi ripoti ya wanahisa kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas katika hafla ya kukabidhi pikipiki kwa jeshi hilo ofisini kwa kamanda sabas makao makuu ya jeshi hili mkoani hapa

Maalim Seif Azungumza na Kituo cha ITV Dar-es-Salaam.

$
0
0
Na Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ameonya kuwa vitendo vya hujuma dhidi ya raia na wageni, vinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zanzibar.

Amesema Zanzibar ambayo imekuwa ikitegemea zaidi sekta ya Utalii kuendeleza uchumi wake na kukuza pato la taifa, imekuwa ikiguswa na matukio hayo ya hujuma, na kwamba yanaathiri uchumi, ustawi wa jamii na sifa ya ukarimu kwa Zanzibar.

Mhe. Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha ITV, Mikocheni Dar es Salaam.

Amesema katika kukabiliana na vitendo hivyo, serikali inakusudia kutekeleza mpango wake wa kuweka kamera za CCTV katika maeneo muhimu ya utalii likiwemo eneo la Mji Mkongwe, ili kuweza kuwabaini kwa urahisi wahusika wanafanya vitendo hivyo.

Kuhusu zao la karafuu kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibar, Maalim Seif amesema serikali imefanikiwa kudhibiti magendo ya karafuu baada ya kuongeza bei ya zao hilo na kuwashinda wanunuzi wengine wa Afrika Mashariki ambako karafuu hizo zilikua zikipelekwa.

Aidha amesema katika kuhakikisha kuwa ubora wa karafuu za Zanzibar unalindwa na kudhibiti wauzaji wengine, Serikali kupitia Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, itaweka nembo maalum “brand”, kuweza kuzitofautisha karafuu za Zanzibar na maeneo mengine.

Akizungumzia dawa za kulevya, Maalim Seif ambaye ofisi yake ndiyo inayohusika na udhibiti wa dawa hizo, amesema bado kuna kazi kubwa ya kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa hizo kutokana na jiografia ya visiwa vya Zanzibar.

Amefahamisha kuwa vita hiyo pia ni ngumu kutokana na uwezo mkubwa wa wafanyabiashara wa dawa hizo ambao wanaweza kuwarubuni watendaji kwa pesa nyingi na kuacha kutekeleza wajibu wao.

Amesema katika kupiga vita dawa hizo, ni lazima kuwepo na mashirikiano pamoja na uadilifu miongoni mwa watendaji, hasa wale wanaofanya kazi katika viwanja vya ndege, bandarini na vyombo vya ulinzi.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa GNU itaendelea kuwepo hata baada ya uchuguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa vile suala hilo ni la kikatiba na limewekewa misingi maalum.

Kuhusu mchakato wa katiba mpya, Maalim Seif amesema bado serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa katiba mpya inapatikana, ili kuendeza ustawi wa Taifa na kukidhi mahitaji ya wananchi.

Amesema tayari serikali imeshatumia fedha nyingi za wananchi, na kwamba kushindwa kukamilisha mchakato huo kwa wakati, itakuwa ni hasara kwa serikali na taifa kwa ujumla.

Hivyo amesema hakuna budi kwa serikali kutafuta njia mbadala za mazungumzo, kuhakikisha kuwa mchakato huo unaendelea na unafanikiwa kwa maslahi ya Taifa.

Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)

$
0
0
Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Jamii Zanzibar Ndg. Mussa Yussuf akitowa utaratibu wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Sita ya ZSSF, iliozinduliwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Oar Yussuf Mzee.  
  Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akizindua Bodi Mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ZSSF kilimani Zanzibar. 

Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akisisitiza jambo wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Sita ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ( ZSSF) uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa  ZSSF Kilimani Zanzibar. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg. Khamis Mussa,akizingumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliozinduliwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee. 
Maofisa wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF wakimsikiliza Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akizindua Bodi hiyo na kutowa nasaha zake kwa Wajumbe wa Bodi mpya ya ZSSF  

                               Maofisa wa ZSSF wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Sita
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadha ya Jamii Zanzibar Dkt.Suleiman Rashid Mohammed, akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa Bodi yao na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee, katika ukumbi wa ZSSF Zanzibar.
Mkugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg Abdulwakil Haji Hafish, akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kutowa maelezo ya uendeshaji wa Mfoko wa Hifadhi ya Jamii kwa wajumbe wa Bodi ya Sita ya ZSSF. 
Wajumbe wa Bodi ya Sita ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee na  Wafanyakazi wa ZSSF, wakiwa nje ya Jengo la ZSSF Kilimani Zanzibar baada ya uzinduzi wake.

Wajumbe wa Bodi ya Sita ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwake na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee.

Mwenyekiti wa Bodi ya Sita ya ZSSF Dkt. Suleiman Rashid Mohammed, akiaza kuongoza Kikao cha Bodi baada ya luzinduliwa leo na Waziri wa Fedha Zanzibar, kikiwa kikao cha kwanza.  


Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakipitia makabrasa yao kabla ya kuaza kwa Mkutano wa kwanza wa Bodi hiyo baada ya kuzinduliwa leo na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee.


Article 4

$
0
0
    MAKUTANO YA FIKRA JUU YA RASIMU YA KATIBA

Kama mjuavyo, mchakato wa kupata katiba mpya umekwama katika Bunge Maalum la Katiba kutokana na kushindwa kupatikana kwa theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono pendekezo la CCM kuhusu Rasimu ya Katiba. Kama hili halitoshi, ususiaji wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka kundi la UKAWA, umezidi kuathiri vibaya mchakato mzima wa kupata katiba mpya ya nchi.

Kwa madhumuni ya kutafuta njia zitakazosaidia kufanikisha jitihada za kupata katiba mpya, napenda kukujuilisheni kuwa ZIRPP, kwa ufadhili wa “The Foundation For Civil Society”, imeandaa mkutano wenye maudhui yaliyotajwa hapo juu na inakualikeni kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika mjadala utakaojitokeza katika mkutano huo ambao utafanyika siku ya Jumapili tarehe 06 Julai 2014 katika Ukumbi wa Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, hapo Vuga, Zanzibar, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana.

Ratiba ya mkutano pamoja na nyaraka nyingine zitatolewa siku ya mkutano.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo muhimu atakuwa Mheshimiwa Hassan Nassor Moyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano.

Natanguliza shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wako.


      (Muhammad Yussuf)
MKURUGENZI MTENDAJI



Mashindano ya Kuhifadhi Quran Juzuu 30

$
0
0

Mwanafunzi Salha Faki Khatib (17) akishiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur an juzuu 30 yalioandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhi Quran Zanzibar yaliofanyika ukumbi wa Skuli ya Haele Salasei na kuwashirikisha Wanafunzi wa Madrasa mbalimbali za Zanzibar.

              Mwanafunzi Asya Othman Juma (15) akishiriki mashindano ya kuhifadhi Quran juzuu 30
Wazee na Wanavyooni wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Quran Juzuu 30, yaliowashirikisha Wanafunzi wa Kike wenye umri tafauti.
Washiriki wa mashindano ya Quran Juzuu 30 wakisubiri kushiriki mashindano hayo wakimsikiliza mshiriki mwezao akisoma Quran.
Majaji wakifuatilia wasomaji wa Quran katika mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Quran Zanzibar.
                       Mwanafunzi Khadija Mwadini (14) akishiriki mashindano ya kuhifadhi quran juzuu 30.

         Mwanafunzi Hafsa Omar Kassim(14) akishiriki mashindano hayo ya kuhifadhi quran juzuu 30.
Majaji wa mashindano ya Quran wakifuatilia usomaji wa washiriki hao wa mashindano ya kuhifadhi Quran Juzuu 30.
Mwanafunzi Qasmat Machano (19) msindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Quran Juzuu 30, akiwa katika mashindano hayo. akisomo aya anazotajiwa na majaji.
Msimamizi wa Mashindano ya Kuhifadhi Quran Bi Zainab Thani,akizungumza katika hafla hiyi na kumkaribisha Mgeni Rasmin kutowa nasaha zake na kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kuhifadhi Quran juzuu 30.
Mgeni rasmin Bi Amani Abdallah Rajab. akitowa nasaha zake kwa Washiriki wamashindano ya kuhifadhi quran na kuwataka kuwa na bidii katika kuhifadhi quran na kujiendeleza katika elimu ya dini. 

Jaji Kiongozi akitowa matekeo ya washindi wa mashindano ya kuhifadhi quran kwa washiri wa mashindano hayo.
                        Washiriki wa mashindano ya kuhifadhi quran wakisikiliza matekeo ya mashindano hayo.
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi quran mwanafunzi Qsmat Machano akikabidhiwa zawadi zake na Mgeni rasmin Bi Amina Abdallah Rajab. baada kuwa mshindi wa mashindano hayo.
                                Mshindi wa Pili Mwanafunzi Asya Othman.akipokea zawadi yake.

Aliedaiwa kumpa ujauzito mtoto wa mkewe aachiwa huru

$
0
0
Asya Hassan na Khamis Amani
Mahakama ya Mkoa Mwera, imemuachia huru mshitakiwa,Nasu Kassim Chande (30) mkaazi wa Muyuni ‘C’ wilaya ya kusini Unguja, alieshitakiwa kwa kosa la kumuingilia mtoto wa mkewe, kutokana na ushahidi kutopatikana.

Hakimu wa mahakama hiyo, Hamisa Suleiman Hemed, alimwachia huru mshitakiwa huyo kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi kutobainisha ukweli wa kosa lililokuwa likimkabili.

Akitoa hukumu, hakimu huyo alisema  anamuachia huru mshitakiwa chini ya kifungu cha 219 cha sheria namba 7 ya mwaka 2004.

“Kutokana na kutokuwepo ushahidi wa kutosha ambao ungeweza kuishawishi mahakama kukubali shitaka dhidi yake, mahakama hii inamuachia huru mshitakiwa,” alisema.

Mshitakiwa huyo alishitakiwa kwa kosa la kumuingilia kimwili mtoto wa mkewe na  kumsababishia ujauzito, ingawa ushahidi wa daktari haukueleza kwamba ujauzito umepatikana  lini na kama ni wa mshitakiwa.


Sababu nyengine iliyosababisha mshitakiwa aachiwe huru ni makosa ya mashtaka, ambapo mshitakiwa alishtakiwa kwa kumuingilia maharimu wake wakati kifungu 160 namba 7 ya mwakja 2014, kinaeleza kwamba maharimu  ni mju kuu wa kike, dada na mama na wala sio mtoto wa kambo.

 “Mazingira ya kosa hili yapo yana utata kwa kuwa kesi hii ni kubwa ushidi wake pia ulipaswa uwe mzito na wa kuridhisha,” alisema.

Awali kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo ilildaiwa kuwa mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 29 mwaka 2012 kujibu shutuma hizo.


Ilidaiwa tukio hilo lilitokea mwezi usiofahamika ambapo mshitakiwa alimuingilia mtoto wa mkewe wa ndoa na kumsababishia ujauzito kitendo ambacho ni kosa kisheria. 

Biashara ya dagaa yasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira

$
0
0
Hakuna huduma za maji, wananchi wajisaidia fukweni

Na Mwandishi wetu
Uharibifu mkubwa wa mazingira umezikumba fukwe zote ambazo zinafanywa biashara ya upikaji na uanikija dagaa hasa maeneo ya kaskazini Unguja na eneo la Maruhubi mkoa wa mjini magharibi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa maeneo ya Fungu refu Mto wa Pwani, Bwekunduni, Muwanda na eneo la Maruhubi kwa kiasi kikubwa kumekuwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na kumwaga maji ya moto ya kuchemshia dagaa na hata mabaki ya dagaa waliooza.

Sambamba na hilo l pia imebainika kukatwa kwa mikoko mingi ili kutoa nafasi ya uanikaji wa dagaa katika maeneo hayo.

Aidha mashamba kadhaa ya maeneo ya Bwekunduni na Mto wa pwani yamevamiwa na maji chumvi baada ya kukatwa mikoko hiyo.


Mbali na hayo,gazeti hili pia limebaini kuwa hakuna huduma za vyoo katika maeneo ya bishara hizo jambo ambalo linasababisha watu wanaojishughulisha na biashara hiyo, kujisaidia pembeni mwa fukwe au sehemu za mikoko.

Pia katika eneo hilo kumekosekana maji safi na salama na kusababisha wanaoishi maeneo hayo kutumia maji ya kuokota.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima wa Mto wa pwani,eneo la Fungurefu kwa  masharti ya kutotajwa majina yao waliliambia gazeti hili kuwa eneo kubwa la mashamba limevamiwa na maji chumvi na hivyo kusitisha shughuli za kilimo.

“Kwa kweli nilikuwa nalima, mpunga viazi vitamu lakini kwa sasa nusu ya shamba langu limevamiwa na maji ya chumvi”, alisema.

Aidha alisema wakulima wanaolima karibu na eneo hilowamekuwa hawapati mavuno mazuri kutokana na kuingiliana na maji chumvi.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa Kamati ya Mazingira ya Mkoa wa Kaskazini Unguja (MECA), Hadia Ali Makame, alikiri kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira na kwamba taratibu zote za kuiarifa Idara husika zimefanywa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.

Aidha alisema k baada ya kuona hali mbaya katika eneo hilowalilazimika kupanda mikoko ili kurejesha uhalisia wake lakini wamevunjika moyo kutokana na miti yote kuhujumiwa.

Nae Msimamizi wa eneo hilo, Kaite Mwadini Haji, alisema hakuna uharibifu wa mazingira katika eneo hilo lakini alibainisha kukosekana kwa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na vyoo na maji safi na salama.

“Tunajaribu kudhibiti mazingira sana lakini nikiri kuwa watu wanajisaidia katika mikoko na maji safi hayapo mpaka tununue barabarani,” alisema.

Aidha mmoja wa waanikaji wa madagaa, Asha Nuru, alisema serikali lazima iwawekee mazingira mazuri kwani wamekuwa wakipata shida ya vyoo na maji.

Pia Fatma Ali na Mtumwa Ali, ambao wameajiriwa kwa ajili ya kazi ya kupika dagaa katika eneo la Maruhubi walikiri kuwa maji ya kuchemshia dagaa wanalazimika kumwaga maeneo yoyote tu kwa kuwa hakuna udhibiti wa mazingira sambamba na kwenda haja kubwa na ndogo.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Riziki Juma Simai, alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira katika eneo la Mto wa pwani fungu refu.

“Tayari tumekutana na wavuvi, matajiri, wapikaji na waanikaji wa madagaa wa maeneo yote na kukubaliana kupunguza eneo hilo utaratibu ambao kwa sasa uko mbioni na utakamilika hivi karibuni,” alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Sheha Mjaja, alikiri uharibifu huo na kwamba walifanya ziara ya makusudi katika maeneo yote ya uanikaji wa madagaa.

Mihangaiko ya ununuzi wa futari Pemba

$
0
0
 
BAADHI ya wafanya Biashara ya ndizi za aina mbali mbali, wakiwa katika mnada wa ndizi ndani ya soko kongwe la chake chake, ambapo bei ya bidhaa hizo katika mwezi huu wa Ramadhani zimepanda bei kupitia kiasi, mkungu mmoja uliokuwa ukiuza kati ya 8000 hadi 10000 upanda kufikia elfu 20000 hadi 30000.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
KUFUATIA mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufika, bidhaa ya ndizi mbivu aina ya mkono mmoja, zimepanda bei maradufu kidole kimoja kilichokuwa kikiuzwa shilingi 500 hadio 700 na kupanda hadi kufikia 1500 na 2000.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 
BIASHARA ya ndizi imeonekana kupendwa na wananchi wengi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, pichani mteja akinunua ndizi ya mkono mmoja katika soko la chake chake.(Picha na Bakari Mussa,PEMBA.)

~~
MFANYABIASHARA wa ndizi katika soko la Chake Chake, akimuuzia mtenja ndizi aina ya mkono mmoja, kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.(Picha na Wapiga Picha wetu, PEMBA.)

Magazetini leo Tz Bongo


Makamu wa Rais Dkt.Bilal Aiwakilisha Tanzania kwenye Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru wa Burundi.

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA SIKU YA UHURU WA BURUNDI
Julai 01, 2014 Bujumbura
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumanne Julai Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za kilele cha miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.
Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia kulikuwa na Makamu wa Rais wa Somalia, Waziri Mkuu wa Chad na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika. Sherehe hizo zilianza kwa Rais Pierre Nkurunzinza kuweka silaha katika eneo  maalum la Uhuru na kufuatiwa na maadhimisho yaliyoshirikisha wananchi mbalimbali katika uwanja wa Rwagasore.
Akizungumza baada ya kutoa tuzo mbalimbali za heshima, Rais Nkurunzinza aliwashukuru wageni wote waliofika katika sherehe hizo na akabainisha kuwa Tanzania ni rafiki wa Burundi hivyo anafurahishwa sana kuona ikiwa imewakilishwa na uongozi wa ngazi za juu katika sherehe hizo.
Burundi ambayo inategemea sana bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na hasa uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo linaiunganisha na Tanzania, inaadhimisha miaka 52 ya uhuru huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali kiuchumi sambamba na kisiasa kufuatia kuwa na miongo kadhaa ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sasa Burundi licha ya kukua kimaendeleo pia inaongezeka idadi ambapo inakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Uhusiano baina ya Tanzania na Burundi unabaki kuwa wa damu ambapo pia redio za nchi hii hutangaza vipindi kadhaa kwa kutimia Kiswahili sambamba na nyimbo za muziki za wasanii wa Tanzania hupata nafasi kubwa katika redio za Burundi.
Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai Mosi, 2014 Bujumbura: Burundi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mwa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza wakipokea maandamano ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi. 
 
 Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.  




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza walipokutana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014.  

Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi. 



‘Imani potofu yadhoofisha uzazi wa mpango’

$
0
0
Na Khamis Mohammed
UELEWA mdogo wa wanajamii pamoja na imani potofu walionayo baadhi ya watu kuhusu dhana nzima ya uzazi wa mpango, imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa inayopelekea wanawake wengi kutojitokeza kutumia uzazi wa mapango.

Hayo yameelezwa na Dk.Sebastian Macrice, wakati wa mdahalo  juu ya uzazi wa mpango kwa maendeleo, uliofanyika ofisi za Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Kidongochekundu mjini hapa.

Dk.Macrice, alisema, baadhi ya wanawake wamekuwa wakitaka kushiriki uzazi wa mpango, lakini, kutokana na kuwahofia waume zao, wamejikuta wakipata huduma hiyo kwa kujificha kinyume na malengo yanayokusudiwa.

Alisema, wanaume wengi si washiriki wazuri katika suala la afya ya uzazi, hatua inayosababisha wanawake wanaoamini uzazi wa mpango kuamua kutumia njia za usiri na hivyo kukosekana maridhiano baina ya pande hizo.


Alisema, suala hilolimefanya baadhi ya ndoa kuvunjika au kukumbwa na migogoro isiyotarajiwa ikiwemo tuhuma za kutembea nje ya ndoa.

Dk.Macrice, alisema, hivi sasa ni asilimia 27% ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na kwamba lengo linalokusudiwa ni kufikia angalau asilimia 60 ifikapo mwaka 2020.

"Safari bado ni ndefu, vifo vinavyotokana na uzazi ni vingi, lazima jamii ibadilike," alisema.

Alisema, lengo hilolinaweza kufikiwa  kwa kushirikiana na wanajamii katika kupata elimu sahihi juu ya uzazi wa mpango sambamba na kuepuka uzazi wa papo kwa papo.

"Uzazi wa papo kwa papo unapelekea  kuregea kwa fuko la uzazi au wakati mwengine kupelekea kutoka damu nyingi kwa mama mjamzito, ni hatari", alieleza.

Aidha, alieleza, hata ulemavu wanaopata wamama ambao hawajajiandaa kubeba ujauzito nao unaweza kuepukika kwa kutumia uzazi wa mpangilio na hivyo  kupunguza vifo vya mama na watoto.

Dk.Macrice, alisema, uzazi wa mpangilio unatoa uhueni  kwa familia  katika kuwatunza  watoto hao pamoja na kuwapatia huduma nzuri, kwa vile panakuwepo na maandalizi ya kiuchumi kabla ya kupokelewa mtoto mpya.

Naye Sheikh Ismail Asaakher kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar, alisema, uislamu haukatazi uzazi wa mpango, lakini, inachosisitiza  ni njia ambazo hazitaleta athari baina ya wazazi.

"Bwana Mtume ametuhimiza  tuoane ili tuwe wengi, lakini, kwa kuwatimizia watoto mahitaji yaoya lazima," alisema.

Hivyo, alisema, ni juu ya wazazi kuridhiana  bila ya kupoteza haki ya mwengine na kwamba mtoto ni zawadi ambayo inatakiwa kupatiwa huduma.

Mapema, Mwakilishi kutoka UMATI, Mwanajuma Salum Othman, alisema, moja ya tatizo kwa nchi zinazoendelea  ni kuongezeka kwa idadi ya watu, hivyo uzazi wa mpango unatoa nafasi kudhiti hali hiyo.


Hata hivyo, alisema, jamii bado haijaelewa umuhimu wa uzazi wa mpango kulingana na rasilimali ndogo wanayowajibika nayo katika maisha ya kila siku. 

Dk. Mwinyi:Tutawasilisha mswada bungeni kudai maslahi ya Z’bar

$
0
0
Na Hafsa Golo
MBUNGE wa jimbo la Kwahani, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Zanzibarinakusudia kupeleka mswada bungeni kudai maslai yake kamamjadala kuhusu katiba mpya utashindikana kuendelea.

Awamu ya pili ya mjadala kuhusu katiba mpya unatarajiwa kuanza Agosti 5.

Dk. Mwinyi ambae ni  Waziri wa Ulinzi, alisema hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya jimbo la Kwahani.

Alisema mswada huo utazingatia suala la uchumi na maslahi ya Zanzibar ambapo mambo mbali mbali  ya msingi yatawasilishwa, ikiwemo suala la mafuta na gesi.

Alisema mswada huo huenda ukapelekwa katika bunge la kawaida mwezi Novemba, lakini iwapo katika mpya itashindikana.


Juzi Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Khamis Hamad, alisema mjadala wa katiba hautawezekana kuendelea bila ya kuwepo wa jumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao wanasusia mjadala huo.

Alisema hakuna sababu ya msingi ya kukosekana maslahi ya Zanzibarhasa hata kama katiba ya sasa itaendelea ikizingatiwa bunge ndio chombo kikuu cha maamuzi ya sheria za nchi.

"Naamini Zanzibar itakuwa na maslahi mazuri sina wasiwasi  hata kama bunge la katiba   halikukaa,"alisema.


Akizungumzia suala la kugombea uongozi alisema hajawa na maamuzi hasa akizingati bado ni mapema. 

Katuni wa leo na ujumbe wake

Hatua ya Umaliziaji Ujenzi wa Barabara ya Daraja Bovu Zenj Yakamilika

$
0
0
 Wananchi wa barabara ya daraja bovu wakiwa memevunja nyumba zao baada kukamilika kwa taratibu zote za kisheria ili kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo awamu ya mwisho ya ujenzi wake ili kukamilisha mradi huo kumalizika kwa kipande kilichobaki katika ujenzi huo wa barabara mpya ya daraja bovu Zanzibar.

Viewing all 36229 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>