Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36203 articles
Browse latest View live

Magazetini Leo Tz Bongo


Jumuiya ya Kiislam ya Muzdalifat watoa Sadaka ya Ramadhani Zanzibar.

$
0
0
Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya Wefa kutoka Ujarumani wakipeleka Sadaka kwa watu mbalimbali wasiojiweza kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Kijiji cha Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mmoja kati ya Wazee wa kijiji cha Kilimani Tazari akipokea Sadaka iliotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya WEFA kutoka Ujarumani kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Zanzibar.




Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais, tawala za mikoa na idara maalum atembelea miradi ya JKU Pemba

$
0
0
 
AFISA Mdhamini Wizara ya Nchi Afisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Pemba, Mhe:Saleh Mbarouk Amour, akipata maelekezo ya Ramani ya jengo la kulala wageni, kutoka kwa Kamanda wa KJU Pemba, Ali Mtumweni Hamad, wakati alipotembela jengo hilo Gombani Pemba. (Picha na Said Abrahman, KJU Pemba.)

 
AFISA Mdhamini Wizara ya Nchi Afisi ya Rasi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Pemba, Mhe:Saleh Mbarouk Amour,akiangalia eneo linalotaka kujengwa madarasa ya kusomeshea Ufundi katika kambi ya JKU Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba. (Picha na Said Abrahman, KJU Pemba)

KIJANA wa Mujibu wa sharia katika kambi ya JKU Msaani, ambae hakufahamika jina lake mara moja, akiwa kenye kidungu akiinga ndege Mpunga katika bonde la JKU Msaani.(Picha na Said Abrahman, KJU Pemba.)

Balozi Seif afungua maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa

$
0
0
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuongeza kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoelekeza azma ya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati na unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.
 
Matumaini ya kufikiwa kwa malengo hayo yaliyowekwa na Serikali yatatokana na kuimarika kwa uzalishaji pamoja na uwekezaji katika viwanda vya msingi.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati akiyafungua maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya saba saba vya Mwalimu J. K. Nyerere Jijini Dar es salaam.
 
Balozi Seif alisema  juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii zinaendelea kuonesha mafanikio kutokana na kukua kwa pato la Taifa kutoka asilimia 6.4 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 7.1 mwaka 2013. 
 
Alisema  kiasi hiki cha ukuaji wa uchumi kimeiwezesha Tanzania kuongoza kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika { SADC }  zilizokua kwa wastani wa asilimia 4.3 mwaka 2012 na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizokua kwa wastani wa asilimia 5.1 mwaka 2012.
 
Balozi Seif alifahamisha kwamba kwa Tanzania, ukuaji wa Sekta ya Viwanda umeongezeka kutoka asilimia 5.5 mwaka 1998 hadi asilimia 7.7 mwaka 2013, wakati sekta ya kilimo inakua kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mwaka.
 
“ Ukuaji huu umechangiwa kwa kiwango kikubwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani, hususan viwanda vya vinywaji, saruji, bidhaa za chuma na usindikaji wa mazao ya kilimo “. Alifafanua Balozi Seif.
 
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwamba  mwenendo wa mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa kipindi rejea umeongezeka kwa asilimia kutoka asilimia 8.37 mwaka 1998 hadi asilimia 9.92 mwaka 2013.
 
Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania {TanTrade} kwa mpango wake wa kuwekeza katika miundombinu mipya ya kisasa ya maonesho unaokwenda sambamba na mahitaji ya nafasi ya kuoneshea. 
 
“ Nimefahamishwa kuwa idadi ya washiriki wote wa ndani na nje ya nchi imeongezeka kutoka makampuni ya ndani 1,601 mwaka 2013 kufikia makampuni 1,690 mwaka 2014, na makampuni kutoka nje 460 mwaka 2013 hadi 490 mwaka huu wa 2014 “. Alisema Balozi Seif.
 
Alisisitiza kuwa Ongezeko hili ni ishara inayoonyesha kwamba  maonesho hayo ya saba saba  yanakidhi viwango vya kimataifa na kudhihirisha kwamba yanaendelea kupata umaarufu. hivyo sasa ni kipindi muafaka kwa wazalishaji wazalendo kutangaza bidhaa zao kwa walaji wa ndani na nje ya nchi.
 
Balozi Seif alitoa wito kwa waandaaji kutumia maonesho hayo kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji kutembelea Maonesho haya kwa nia ya kujionea fursa hizo na hatimaye kupata ushawishi wa kuwekeza miradi yao.
 
Nimefahamishwa kuwa katika maonesho haya kuna nchi ambazo zinashiriki.  Aliwashauri washiriki wa ndani kwenye maonyesho hayo ya saba saba kutenga muda wa kutembelea mabanda na makampuni ya nchi wanachama wa EAC na SADCkuzungumza nao kwa ajili ya kujifunza.
 
Alisema hatua hiyo wapa muda wa kutengeneza mtandao wa pamoja ambao utawasaidia kutangaza bidhaa zao katika masoko hayo ya Kikanda na baadaye kuwa na nguvu za pamoja kwenda kwenye masoko makubwa ya Ulaya, Marekani, Mashariki ya Kati na Asia.
 
B kalozi Seif aliwaasa wale wote watakaopata oda wazifanyie  kazi ili malengo yao ya sasa na yale ya muda mrefu yaweze kutimia.
 
Zingatieni kuwa mmetumia muda mwingi na rasilimali nyingi katika maandalizi, hivyo ni vyema juhudi zenu hizi zikawa zenye manufaa endelevu.  Epukeni urasimu usiokuwa na faida, kwani urasimu siku zote unarefusha mchakato na kufikia makubaliano ya kibiashara “. Balozi Seif liwatahadharisha washiriki hao wa Maonyesho ya saba saba dar.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aidha aliushukuru Uongozi wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania {Tan-Trade} kwa ubunifu wao wa kuanzisha maonesho maalum yatakayokuwa yakifanyika kila mwaka yakiwemo Tamasha la Biashara, Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Maonesho ya Bidhaa za Utamaduni na Uhuru.
 
Balozi Seif alielezea matumaini kwamba Mamlaka hiyo itaendelea kuanzisha maonesho mengine kama hayo katika Mikoa mengine hapa nchini ili kuhakikisha maonesho ya Biashara yanatumika kikamilifu kama chombo cha kukuza biashara kwa nchi nzima.
 
Mapema Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Abdulla Kigoda aliwashukuru washirika wa maendeleo pamoja na Wananchi kwa ushiriki wao uliosaidia kufanikisha maonyesho hayo.
Mh. Kigoda alisema Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania{ Tan Trade } itaendelea kuimarisha  miundo mbinu itakayotoa fursa kwa mikoa mbali mbali NchininTanzania kufanya maonyesho ya biashara kila mwaka.
 
Alisema Wizara ya Viwanda na Biashara ya SMT imeandaa mpango maalum wa uwekezaji katika eneo hilo muhimu la maonyesho linalochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Kigoda alifahamisha kwamba utafiti uliofanywa na Taasisi za uchumi Kimataifa zimethibitisha kwamba maonyesho ni ni nyenzo inayoongoza katika kukuza uchumi na utoaji wa huduma muhimu za kijamii.
 
Washiriki wapatao 1,690 kutoka makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi wamehudhuria maonyesho hayo ya 38 ya Kimataifa  mwaka huu  idadi ambayo imeongezeka zaidi ikilinganishwa na makampuni 1,601  yaliyoshiriki mwaka jana.

Hotuba ya Balozi Seif alipofungua maoneysho ya 38 ya biashara ya kiamtaifa Dar

$
0
0


HOTUBA YA MHE. BALOZI SEIF ALI IDD, MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, WAKATI WA UFUNGUZI WA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM, 2 JULAI, 2014
 
Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara,
Waheshimiwa Mawaziri,
Mhe. Raymond Mushi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa,
Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, Bwana Uledi A. Mussa,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Bibi Sabetha Mwambenja,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Bibi Jacqueline Mneney Maleko,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini,
Ndugu Wanahabari,
Washiriki wa Maonyesho,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
 
Awali ya yote sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kukutana hapa tukiwa wazima na wenye furaha, kushuhudia ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.  Aidha, napenda kuchukua fursa hii adhimu kuishukuru kwa dhati Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania – Tan Trade kwa heshima mliyonipa ya kuwa mgeni rasmi.
Waswahili wanasema “mcheza kwao hutunzwa”.  Kwa hivyo, sina budi nami kuitunza kwa pongezi Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar pamoja na Taasisi mbali mbali za Serikali na sekta binafsi kwa kushiriki kwao ili kufanikisha maonesho haya.
Kwa namna ya pekee pia niwashukuru wageni waalikwa, Washiriki wa Maonesho haya pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kushiriki na kutembelea Maonesho haya makubwa, ambayo yanafanyika kila mwaka.  Nawapongeza waandaaji wa maonyesho haya ya sabasaba kuwa endelevu.  Kauli Mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni “Unganisha Uzalishaji na Masoko”. Kauli mbiu hiiinawataka wazalishaji wa mazao na bidhaa kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya soko ikiwa ni pamoja na kujitangaza.
 
Ndugu Washiriki na Wageni Waalikwa,
Nimefahamishwa kuwa idadi ya washiriki wote wa ndani na nje ya nchi imeongezeka kutoka makampuni ya ndani 1,601 mwaka 2013 kufikia makampuni 1,690 mwaka 2014, na makampuni kutoka nje 460 mwaka 2013 hadi 490 mwaka huu wa 2014. Ongezeko hili ni ishara kuwa maonesho haya yanakidhi viwango vya kimataifa na hivyo ni kipindi muafaka kwa wazalishaji wetu kutangaza bidhaa kwa walaji wa ndani na nje.  Ongezeko hili la washiriki, linadhihirisha ni kwa kiasi gani maonyesho yameendelea kuwa maarufu ndani na nje ya nchi.
 
Ni matarajio yangu kuwa maonesho haya yataendelea kuwa maarufu na jukwaa kubwa kupita yote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati la kutangaza biashara kwa bidhaa na huduma.  Natoa wito kwa waandaaji kutumia maonesho haya kutangaza pia fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini na hivyo kuvutia pia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutembelea Maonesho haya kwa nia ya kujionea fursa hizo na hatimaye kuwekeza. Nawapongeza pia TanTrade kwa mpango wa kuwekeza katika miundombinu mipya ya kisasa ya maonesho unaokwenda sambamba na mahitaji ya nafasi ya kuoneshea.  Suala la msingi hapa ni kupanga mradi huu wa ujenzi uwe kwa awamu ili kuhakikisha maonesho yanaendelea wakati wote wa ujenzi bila kuleta usumbufu kwa waoneshaji.
 
 
 
Ndugu Washiriki na Wageni Waalikwa,
Umuhimu wa kuendeleza maonesho kama fursa ya kutangaza na kutafuta masoko ya bidhaa unatokana na ongezeko la ushindani katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo na bidhaa za viwandani ndani na nje ya nchi.  Kwa Tanzania, ukuaji wa Sekta ya Viwanda umeongezeka kutoka asilimia 5.5 mwaka 1998 hadi asilimia 7.7 mwaka 2013, wakati sekta ya kilimo inakua kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mwaka.
 
Ukuaji huu umechangiwa kwa kiwango kikubwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani, hususan viwanda vya vinywaji, saruji, bidhaa za chuma na usindikaji wa mazao ya kilimo. Aidha, mwenendo wa mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa kipindi rejea umeongezeka kwa asilimia kutoka asilimia 8.37 mwaka 1998 hadi asilimia 9.92 mwaka 2013.
 
Ndugu Washiriki na Wageni Waalikwa,
Moja ya bidhaa za Tanzania ambazo zimekuwa zikivutia watu wengi kwenye maonesho haya ni bidhaa za ngozi.  Hii inatokana na jitihada za Serikali ikishirikiana na sekta binafsi ambapo Mkakati wa Kufufua na Kuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi nchini umeendelea kutekelezwa na kwa sasa Sekta Ndogo ya Usindikaji wa Ngozi imeongeza viwanda kutoka vitatu (3) vya awali hadi viwanda tisa (9) mwaka 2013/2014.  Viwanda hivyo vina uwezo uliosimikwa (installed capacity) wa kusindika vipande vya ngozi milioni 13.2 kwa mwaka kufikia hatua ya awali (wetblue).  Uwekezaji katika viwanda vilivyo chini ya Maeneo Maalum ya Kuzalisha Bidhaa za Kuuza Nje (Export Processing Zones- EPZ) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji Kiuchumi (Special Economic Zones-SEZ) nao vile vile umechangia katika ukuaji wa sekta ya viwanda.  Mathalani, katika mwaka 2013/2014, makampuni 31 yamepewa leseni za kujenga viwanda chini ya Mamlaka ya EPZ na makampuni 8 yameanza uzalishaji. Makampuni hayo yanatarajia kuwekeza mtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 458 na kuajiri watu 10,276.  Idadi hiyo inafanya jumla ya makampuni yanayozalisha chini ya SEZ na EPZ kufikia 98, jumla ya mtaji uliowekezwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 1.5 na jumla ya ajira za moja kwa moja kufikia 27,000.
 
Ndugu Wananchi,
Serikali inakusudia kuongeza kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ili kuakisi malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoelekeza azma ya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati na unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025. Matumaini ya kufikiwa kwa malengo tuliyojiwekea yanatokana na kuimarika kwa uzalishaji na uwekezaji katika viwanda vya msingi.
 
Aidha, juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii zinaendelea kuonesha mafanikio. Pato la Taifa limeendelea kukua kutoka asilimia 6.4 mwaka 2011 kufikia asilimia 7.1 mwaka 2013.  Kwa kiasi hiki cha ukuaji Tanzania inaongoza kwa nchi za SADC zilizokua kwa wastani wa asilimia 4.3 mwaka 2012 na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizokua kwa wastani wa asilimia 5.1 mwaka 2012.
 
Kasi nzuri ya ukuaji wa Pato la Taifa ilichangiwa pia na sekta zinazokua kwa haraka na zenye mtaji mkubwa hususan sekta ya mawasiliano iliyoongoza kwa ukuaji wa asilimia 20.6 kwa mwaka 2013, sekta ya huduma ya fedha asilimia 13.2, ujenzi,  madini asilimia 7.8, biashara asilimia 7.7 na uchukuzi asilimia 7.1.
 
Hata hivyo, sekta ya kilimo ambayo inayoajiri watu wengi zaidi imekua kwa kiwango cha asilimia 4.3 kwa mwaka 2013. Pamoja na ukuaji mdogo wa sekta hii, mchango wake kwa Pato la Taifa bado ungali mkubwa.  Mathalani, mwaka 2013, sekta hii ilichangia asilimia 24.7 ya pato hilo na asilimia 10.7 ya mapato ya fedha za nje. 
 
Ndugu Washiriki na Wageni Waalikwa,
Kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 (2011/12 – 2015/16), malengo yetu ni ukuaji wa wastani wa asilimia 8 wa Pato la Taifa. Ili tufikie huko, Serikali yetu kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 ilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).  Mpango huu unalenga maeneo ya kipaumbele katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5 ambayo ni Miundombinu, Kilimo, Maendeleo ya Viwanda, Rasilimali Watu, Utalii, Biashara na Huduma za fedha.  Ni matumaini yangu kuwa tutaanza kuona matokeo makubwa katika sekta za uchumi kutokana na ukuaji wa sekta ya biashara ya ndani na nje.
Ndugu Washiriki na Wageni Waalikwa,
Ukuaji wa sekta ya biashara unategemea mifumo ya soko la ndani pamoja na mikakati ya kuyafikia masoko ya nchi jirani. Hivyo, ili kunufaika na fursa za masoko zilizoko katika nchi jirani ni muhimu kutangaza na kuuza bidhaa zetu katika masoko hayo.
 
Nchi jirani ambazo pia ni Wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na SADC zimeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima na hivyo biashara baina ya nchi yetu na nchi hizo imeongezeka. Napenda niipongeze Serikali kwa kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na kurahisisha biashara za mipakani kwa kuanzisha Kamati za Pamoja za Mipakani na kujenga majengo yatakayowezesha ukaguzi wa mipakani kufanyika kwa pamoja.
 
Nimefahamishwa kuwa katika maonesho haya kuna nchi wanachama wa EAC na SADC ambazo zinashiriki.  Nawashauri washiriki wa ndani mtenge muda kutembelea mabanda na makampuni ya nchi hizi, muongee nao kwa ajili ya kujifunza na kutengeneza mtandao wa pamoja ambao utawasaidia kutangaza bidhaa zenu katika masoko haya ya Kikanda na baadaye muweke nguvu ya pamoja kwenda kwenye masoko makubwa ya Ulaya, Marekani, Mashariki ya Kati na Asia.
 
Naomba nitumie pia fursa hii kuwaasa wote mtakaopata oda, zifanyieni kazi ili malengo yenu ya sasa na ya muda mrefu yaweze kutimia. Zingatieni kuwa mmetumia muda mwingi na rasilimali nyingi katika maandalizi, hivyo ni vyema juhudi zenu hizi zikawa zenye manufaa endelevu.  Epukeni urasimu usiokuwa na faida, kwani urasimu siku zote unarefusha mchakato na kufikia makubaliano ya kibiashara bila ya sababu.
 
Naomba pia niwapongeze Tan-Trade kwa kuwa wabunifu kwa kuanzisha maonesho maalum yatakayokuwa yakifanyika kila mwaka yakiwemo Tamasha la Biashara, Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Maonesho ya Bidhaa za Utamaduni na Uhuru. Natumaini mtaendelea kuanzisha maonesho mengine kama haya kwenye Mikoa mingine hapa nchini ili kuhakikisha maonesho ya Biashara yanatumika kikamilifu kama chombo cha kukuza biashara kwa nchi nzima. Ni muhimu pia msimamie kikamilifu jukumu la kusimamia uandaaji wa Maonesho ya Kimataifa ili kuhakikisha kuwa Maonesho yote yanakidhi vigezo na masharti yaliyowekwa na Serikali.
 
Kwa kutambua mchango wa biashara katika uchumi wa nchi yetu, Serikali kupitia Wizara na Taasisi zake husika itaendelea kuunga mkono juhudi za sekta binafsi kwa kuboresha mazingira ya biashara nchini.
 
Ndugu Wananchi,
Mwisho, napenda kwa mara nyingine kuushukuru uongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na ule wa Tan-Trade kwa kuandaa maonyesho haya ambayo yamefana sana.  Najua kuwa wamefanya kazi usiku na mchana ili kuyafanikisha maonyesho haya.  Nawapongeza sana. 
 
Lakini pia naupongeza uongozi huo kwa heshima hii adhim walionipa ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho haya.  Heshima niliyopewa kwa mara ya pili, nitaendelea kuitunza, kuienzi na kuithamini siku zote.
 
Mabibi na Mabwana,
Baada ya kuyasema hayo, napenda kutamka kuwa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam sasa yamefunguliwa rasmi.
 
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Dkt Bilal afanya mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza

$
0
0
 




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza alipomtembelea Ofisini kwake Ikulu jijini Bujumbura jana Julai 02-2014.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Burundi Ikulu jijini Bujumbura jana ambapo alizungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi mbili hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya  Viongozi wa Serikali ya Burundi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura jana baada ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa nchi hiyo.      (Picha na OMR)
 
Julai 02, 2014: Bujumbura
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumatano Julai Pili, 2014 amekutana na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na kufanya naye mazungumzo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Rais Nkurunzinza iliyopo katikati ya jiji la Bujumbura.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano baina ya Tanzania na Burundi ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Nkurunzinza na watu wa Burundi kwa sherehe zilizofana za kutimiza miaka 52 ya uhuru. Pia alitumia nafasi hiyo kumtakia kila la heri Mheshimiwa Rais Nkurunzinza pamoja na  watu wa Burundi kufuatia kupiga hatua kubwa za kimaendeleo sambamba na kuweza kuwafanya wananchi wa Burundi kuwa wamoja.
Pia alimueleza Rais Nkurunzinza kuhusu umuhimu wa kuzidi kuifanya Burundi kuwa nchi moja kwa kuwaunganisha watu wake na akaeleza kuwa, Tanzania inafurahi kuona hatua kubwa za kimaendeleo zikipigwa nchini Burundi na kwamba ili hatua hizo ziwe madhubuti, upo umuhimu wa kuwafanya wananchi wa Burundi kubakia wamoja na wanaoshirikiana katika kuiendeleza nchi yao.
“Burundi ikifanya vizuri maana yake ni kuwa Afrika Mashariki imefanya vizuri. Tanzania tutafurahi na nchi zote za ukanda wetu zitafurahi,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza kuwa lengo la Tanzania siku zote ni kuona jirani zake wakiishi kwa utulivu na wakifanya mambo yao ya maendeleo katika hali ya amani.
Katika mazungumzo hayo Rais Nkurunzinza aliendelea kuishukuru Tanzania kwa uhusiano wake wa karibu na Burundi na akaongeza kuwa wananchi wa nchi yake wamefurahishwa sana kwa Tanzania kushiriki katika sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore jana. Pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania, sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Somalia na Waziri Mkuu wa Chad.
Msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais umeondoka leo jijini Bujumbura na kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa. Katika msafara huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
 
Imetolewa na:              Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 2, 2014 Bujumbura: Burundi

Magazetini Bongo Tz

Amuua mama yake baada ya kumpikia magimbi badala ya ugali

$
0
0
Na Rose Chapewa, Mbeya
MWANAMME aliyefahamika kwa jina la Kiswigo Anganisye (33) mkazi wa kijiji cha Ibungila, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga fimbo mama yake mzazi  sehemu ya kichwani na usoni na kisha kumnyonga shingo na kusababaisha kifo chake,baada ya kumpikia magimbi badala ya ugali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi, mwanamke  aliyeuawa ni Martha Kyando (73) mkazi wa kijiji cha Ibungila.

Alisema tukio hilo lilitokea Julai mosi mwaka huu  majira ya saa 6:30 usiku katika kitongoji cha Mpunguti kijiji cha Ibungila kata ya Malindo, tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni baada ya mama huyo kumpikia mtuhumiwa magimbi badala ya ugali, ambapo alichukia na kumpiga  mama yake.


Alisema  uchunguzi unaonesha mtuhumiwa huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa akili, na kwamba bado uchunguzi zaidi unaendeea, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Katika tukio jingine  watu wawili wanaodaiwa kuwa raia waMalawi wanashikiliwa kwa kosa la  kuingia nchini  bila kibali.


Aliwataja watu hao kuwa ni Thomas Juma (29) na Bonophace Chitete (29), na kwamba walikamatwa Julai 1 mwaka huu majira ya saa 5:15 wilayani Kyela baada ya jeshi hilokufanya msako maalumu.

Upasuaji warejea Chake Chake

$
0
0
Na Abdi Suleiman, Pemba
BAADA ya huduma za upasuaji kusimama kwa muda katika hospitali ya wilaya Chake Chake baada ya kuharibisha mashine ya dawa ya usingizi,(anaesthetic machine), hatime huduma hizo zimerejea baada ya mashine hiyo kongwe kutengenezwa.

Taarifa ya kuharibika mashine hiyo kwa mara ya kwanza ilichapishwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.
Huduma hizo zilizosimama tokea Juni 20 na kusababisha wagonjwa na wajawazito wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kuhamishiwa hospitali za Mkoani na Chake, zimeanza kurejea tena kuanzia Jumatatu ya wiki hii.

Zanzibar Leo imeshuhudia baadhi ya wagonjwa wakitolewa katika chumba cha upasuaaji wakiwa tayari wameshafanyiwa upasuaji.

Dk. Alawi Hamad Othman,alisema huduma hiyo imerejea baada ya masheine hiyo kufanyiwa matengenezo na mafundi wa wizara.


Hata hivyo, alisema mashine hiyo imeshachoka na wakati wowote inaweza kuharibika tena.

“Baada ya wandishi kuandika habari ya kuharibika mashine hii, fundi mkuu wa wizara alikuja na kuungana na fundi wa hospitali yetu kuitengeneza na imekubali na sasa tunaendelea kutoa huduma kama kawaida yetu, tunawashukuru (waandishi kwa kutusaidia),”alisema.

Mashine hiyo ambayo ni moja katika hospitali hiyo inayohutumia wagonjwa kutoka wilaya nzima ya Wete, ipo hospitalini hapo tokea 1992.

Baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, waliiomba serikali kuharakisha kupatikana mashine mpya.
Walisema kuharibika kwa mashine hiyo kumesababisha mateso makubwa kwao.


Ali Khamis mume wa Mariyam Kambi, aliyefanyiwa upasuaji, alisema walilazimika kukaa hospitali kwa muda wa wiki moja kusubiri mashine hiyo itengenezwe huku mke wake wakiwa na maumivu makali ya tumbo.

Mufti Simba awaonya wanaoteka misikiti

$
0
0
Na Joseph ngilisho, Arusha
MUFTI Mkuu wa Tanzania,  Shekh   Issa Bin Shaaban Simba, amewaonya Waislamu wanaosababisha migogoro misikitini na wakati mwengine kuteka viongozi wa misikiti.

Alitoa onyo hilo baada ya kutatua mgogoro wa uongozi katia mskiti mkuu uliopo Bondeni manispaa ya Arusha.

Alisema kuna baadhi ya Waislamu wamekuwa wakiitumia misikiti sehemu za migogoro na kupindia uongozi uliowekwa kisheria kwa sababu zao binafsi.

Alisema hali hiyo mbali ya kusababisha migogoro pia imeifanya misikiti kuwa na makundi mawili ya uongozi, jambo ambalo halikubaliki.

Alisema kutokana na hali hiyo amelazimika kufanya
ziara Mkoani Arusha na kukutana na viongozi wa serikali,viongozi wa  Bakwata wa makundi yote yanayokinzana, ili kujaribu kumaliza mvutano.


Mufti Simba, alisema viongozi waliokuwa wakishikilia msikiti huo hawana haki, badala yake wanaotakiwa kuwa viongozi ni  Sheikh wa mkoa, Shaban Juma Abdallah, Kaimu Katibu wa mkoa, Ustadhi Abdallah Masoud na Mwenyekiti wa halmashauri, Ustadhi Mohamed Juma Marawi.

Aidha alisema baraza la  Masheikh mkoa litaongozwa na  Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni,Sheikh Nassib Idd Nassib, Sheikh Hussein Said Ijunje,Sheikh Abdallah Hanafi Simba na Sheikh Abdulrahman Salum.

Aliwataja wajumbe wanostahili kuwepo kwenye halmashauri ya mkoa ni  Hassan Waziri Salum, Said Rashid Golugwa,Athuman Amir Yunus,Seif Juma Banka,Athuman Juma Luwuchu, Mohamed Kidange Laizer, Salim Rajab Majaaliwa na Rashid Kilavo Msuya.


Aliwahimiza Waislamu kuimarisha umoja na mshikamano kwa kuwa uislamu ni dini ya amani na sio ya mivutano.

Katuni wa Leo

PBZ Yafutarisha Wateja Wake Pemba.

$
0
0
 MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wa Benk ya watu wa Zanzibar, PBZ Tawi la Pemba wakati alipokuwa akiwasili katika futari maalumu iliyoandaliwa na Benk hiyo kwa wateja wake huko ZSSF Chake Chake Pemba.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Viongozi wa Serekali na wa PBZ, wakati wa futari Maalum ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, kwa Wateja wake Kisiwani Pemba, iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba jana.
 Wananchi na Wafanyabiashara Kisiwani Pemba wakipata futari maalum ilioandaliwa na PBZ kwa ajili ya Wateja wao walioko Pemba na kujumuika na Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Pemba, futari hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba jana. 
Wananchi wakipata futari maalum iliandaliwa na PBZ Tawi la Pemba katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Pemba.
Mkurugenzi Mtendajin wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Amour, akitowa shukrani kwa Wananchi na Wafanyabiasha wa Kisiwani Pemba baada ya kumaliza kupata futari ilioandaliwa kwa ajili yao katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Chake Pemba na kuhudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad.(Picha na Abdi Suleiman -Pemba)  

Balozi Seif Afungua Maonesho ya 77 Dar.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi tuzo Maalum Mkuu wa Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Tanzania { NSSF } Mhandisi Julius Nyamuhokya baada ya shirika lake kudhamini sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Saba saba yaliyoanza rasmi jijini Dar es salaam.
Balozi Seif akiangalia mabomba ya kusambazia maji yaliyotengenezwa na shirika la mabomba Tanzania kwenye maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya saba saba Jijini Dar es salaam.

Balozi Seif akiwa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania { Tan Trade } Bibi Sabetha Mwambenja akiingia ndani ya viwanja vya maonyesho ya saba saba ya Mwalimu j.k Nyerere kuyafungua maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara.
Mkuu wa Miradi wa NSSF Mhandisi Julius Nyamuhokya akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juu ya haraki za miradi yao ya ujenzi wa nyumba katika eneo jipya la Kigamboni.
Meneja mauzo wa shirika la Biashara  la la Taifa Zanzibar { ZSTC } Ndugu Issa Hamid akimpatia maelezo Balozi Seif kwenye banda la biashara la Zanzibar kwenye maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania { Tan Trade } Bibi SabethaMwambenja baada ya kufungua maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam.
(Picha na Hassan Issa wa – OMPR)

Mashindano ya Kuhifadhi Quran Juzuu 15 na 30 Masjid Nour Muhammad.

Rais Kikwete Akutana na Mwana Mfalme wa Japad Dar.

$
0
0
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki  Mwana Mfalme wa JapanPrince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo wakiwa katika ziara ya kutembelea Tanzania. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Asia Bw. Mblewa Kairuki kwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaamleo 
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazunzumzo na  Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. 

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha Simba waliotengenezwa Mwana Mfalme wa JapanPrince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea  jijini Dar es salaam


Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwatembeza Ikulu Mwana Mfalme wa JapanPrince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea  jijini Dar es salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea  jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi, balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome Sijaona na balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe Masaki Okada(Picha na Ikulu)

Alama hii Wazenj wanaweza Kusoma Lugha ya Kichina Michezani.

$
0
0
 Alama ya Tangozo  liliowekwa katika eneo linalojwengwa Mnara likiwa katika lugha ya Kichina Wazenji wanaweza kuisoma lugha hiyo na kutambua makusudio yake?

MwanaMfalme wa Japan Awasili Zanzibar leo Mchana.

$
0
0
Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na Mkewe Princess Akishino wakiteremka kutoka kwenye ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuanza ziara ya siku moja hapa Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mwinyihaji Makame akimlaki Mwana  Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na makewe Princess Akishino katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Chukwani Zanzibar
Mtoto akimvisha shada la Mauwa Mwana Mfalme wa Japan Akishino alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aamani Karume Zanzibar.kwa ziara ya iku moja kutembelea sehemu za historia ya Zanzibar. 
Mwana  Mfalme wa Japan Akishino akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
(Picha na Makame Mshenga)

Mwana Mfame wa Japan Akutana na Rais wa Zanzibar Dkt Shein Ikulu leo.

$
0
0
                                                       STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                        04 Julai, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema visiwa vya Zanzibar vimeendelea kuvutia wageni wengi kutokana na utajiri mkubwa wa historia yake na uthiri wa utamaduni wa watu wake pamoja na mazingira mazuri ya kuvutia.
Akizungumza na Mwanamfalme wa Japan Akishino pamoja mkewe Ikulu leo, Dk. Shein amesema pamoja na visiwa vya Zanzibar kubahatika kuwa na fukwe maridadi zinazovutia watalii wengi lakini nafasi yake katika historia iliyopelekea kutembelewa na watu kutoka nchi mbali mbali ulimwenguni kwa karne nyingi imevifanya visiwa hivyo kuwa maarufu hivyo kuendelea kuvutia wageni wengi.
Alimwambia mwanamfalme huyo ambaye yuko nchini kwa ziara maalum kuwa historia ya Zanzibar imeunganika na mataifa mengine ulimwenguni hivyo ni vigumu kuandika au kuzungumzia historia ya watu wake bila kugusia mataifa mengine.
Alitolea mfano mji mkongwe kuwa moja ya urithi wa uthibitisho wa makutano ya tamaduni kutoka nchi mbalimbali hadi sehemu hiyo ya mji wa Zanzibar kuwa uthiri wa dunia chini ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni ya Umoja wa matyaifa-UNESCO.
Katika mazungumzo hayo Dk. Shein ameishukuru pia Serikali na wananchi wa Japan kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiipatia Zanzibar na ametolea mfano sekta ya huduma za jamii na miundombinu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amempongeza Mwanamfalme Akishino na mkewe kwa kuitembea Zanzibarna amemueleza kuwa milango iko wazi kwa Mwanamfalme huyo kutembelea Zanzibar wakati wowote.
Dk. Shein alieleza matumaini yake kuwa ziara hiyo ya Mwanamfalme huyo itafungua njia kwa watalii wengi kutoka Japan kutembelea Zanzibar.
Kwa upande wake Mwanamfalme Akishino amemueleza Mhe Rais kuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea Zanzibar na anatarajia kujifunza mengi kuhusu Zanzibar kwa kutembelea sehemu mbalimbali.
Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Bi Hindu Hamad Khamis na Balozi wa Tanzania nchini Japan Balozi Salome Sijaona.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino  alipowasili Ikulu mjini Zanzibar leo akifuatana na Mkewe Princess Akishino na baadae kufanya mazungumzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akifuatana na Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino mara walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuonesha kitu  Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino  baada ya mazungumzo yao  alipotembelea Ikulu Mjini Zanzibar leo na Mkewe Princess Akishino,[Picha na Ramadhan Othman)

Rais Mstaaf Ali Hassan Mwinyi Afungua Masjid Huda Chamazi Mbagala.Jijijini Dae-es Salaam..

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB. Ndg. Said Salim Bakressa. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi,alipowasili viwanja vya Masjid Huda Mbagala Chamazi kwa ajili ya Uzinduzi wa Masjid Huda. 

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa  katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kulia) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjid Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam.

Mkundemba bye bye

$
0
0


Mtunda ambao ulipandwa Kundemba mnamo mwaka 1982-1983 na kubatizwa jina la Mkundemba Leo hii umetuaga rasmi kwa kukatwa kutokana na chini kuwa umeshaoza sana na kuhatarisha  usalama na amani kwa wakaazi wa hapo.

Mtunda huu ndipo lilipokuwa duka maarufu la Alwatan wa Kundemba Ali Kibanda.

Kwa wakaazi wa Kundemba walio ughaibuni ambao wanaufahamu vizuri sana mtunda huu ambao ulipandwa na Marehemu Hassan Wigi wakija kutembea  kwa leo wataona tofauti imetokea mtaani kwao

Viewing all 36203 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>