Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36208 articles
Browse latest View live

Waislamu watahadharishwa

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
KUMEIBUKA kundi la watu wanaowapotosha Waislamu kwa kuwataka wasiwapeleke watoto wao skuli na vyuo vikuu na  badala yake wasome Quran pekee, kwa madai kwamba elimu ya vyuo vikuu ni ukafiri.
Hayo yalielezwa jana na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Dk. Seif Sulley, wakati akizungumza na wakazi wa mjini Dodoma.
Aidha alisema kundi hilo limekuwa likiwahamasisha wanafunzi wa kiislamu walio vyuo vikuu kukatisha masomo yao.
"Kwa gharama yoyote ile nitajitahidi kupambana na kundi hili ambalo linaharibu maisha ya watu,” alisema.
Alisema watu hao wamekuwa wakipita vyuoni na kutoa kauli kama hizo misikitini na kuwaachisha masomo wanafunzi.

Aliwataka Waislamu kuwapiga vita watu hao kwa sababu hawana nia njema na Waislamu na wanapotosha Uislamu ambao umehimiza watu kusoma.

Taasisi za umma zadaiwa kufanya uharibifu Mji Mkongwe

$
0
0
Mwanrafia Kombo,MCC  na Zuleikha Abdalla
MAMLAKA ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe wa Zanzibar, imesikitishwa na hujuma zinazofanywa na baadhi ya taasisi na watu binafsi ndani ya mji huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ghafla katika maeneo katika maeneo yaliyohujumiwa,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Issa Sariboko Makarani, alisema mamlaka yake imesikitishwa na hujuma hizo zilizofanywa na taasisi binafsi kwa kushirikiana na taasisi za serikali.

Alisema katika kipindi hiki cha karibuni kumekua na matukio ya uharibifu wa viguzo vilivyowekwa maalum kwa ajili ya kuzuia gari zisifike maeneo ya ndani kwa lengo la kuzuia uharibifu wa nyumba katika eneo la mji huo.

“Tumekua tukiona uharibifu ukifanywa katika maeneo mbali mbali ya mji wetu ambapo sehemu nyengine hufanywa na watu binafsi na nyengine hufanywa na taasisi za serikali ambazo hufanya hivyo kwa lengo la kupata pesa bila ya kujali kuwa wanaweza kuhatarisha mji wetu kutolewa katika urithi wa kimataifa,” alisema.


Alisema uharibifu huo ni pamoja na ukataji wa miti ndani ya mji huo,kuharibu taa na viguzo vya vizuizi ambao umefanyika katika eneo la Shangani mbele ya hoteli ya Africa House, uharibifu wa taa katika eneo la Forodhani na ukataji wa miti uliofanywa eneo la Darajani.

Alisema walioharibu viguzo mbele ya hoteli ya Africa House ni dhahiri wameshirikiana na taasisi za serikali kwa vile walikwenda Mamlaka kutaka kibali cha kuviondoa na wakakataliwa.

Alisema baada ya mamlaka kukataa kutoa kibali ndipo wamiliki wa hoteli hiyo walipokwenda katika taasisi nyengine ya serikali kuchukua kibali vya kuviondoa viguzo hivyo, na bila kujali taasisi hiyo ilikubali kwa sababu tu itapata mapato.


Alishauri wafanyabiashara kuweka utaratibu wa kutumia maeneo mengine yalio nje ya mji huo kwa lengo la kuhakikisha msongamano unapungua.

Bidhaa bei juu Ramadhani Zanzibar.

$
0
0
Hafsa Golo na Habiba Zarali
LICHA ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, kuwataka wafanyabiashara kupunguza bei za bidhaa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, wafanyabiashara wamepuuza agizo hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazaeti hili umebaina bei za bidhaa zinazotumiwa na Waislamu kwa ajili ya futari, zimepanda mara dufu katika masoko yote makuu Unguja na Pemba.

Katika soko kuu la Mombasa, bei ya ndizi mbichi, magimbi, viazi vikuu, ndizi mbivu zimepanda karibu kwa asilimia 30.

Katika soko hilo ndizi mbichi aina ya mkono wa tembo inauzwa baina ya shilingi 30,000 hadi 50 na kidole kimoja kinauzwa baina ya shilingi 3,000 na 5,000 wakati fungu la viazi vitamu linauzwa shilingi 2000 na 5,000.

Muhogo ambao uliozoeleka kuuzwa shilingi 1,000 kwa fungu moja, bei imebakia pale pale lakini wafanyabiashara wamepunguza ukubwa wa fungu.

Nazi zimepata bei ya kutisha kutoka shilingi 5000 hadi shilini 18,000 huku samaki wamekuwa adimu na hao wanaopatikana wanauzwa kwa bei kubwa hadi shilingi 10,000 kwa kipande.


Hata hivyo, bei ya nyama imebakia baina ya shilingi 8000 na 9000 kwa kilo moja.

Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara walisema wanalazimika kupandisha bei kutokana na wakulima kupandisha bei huku bidhaa zikiwa pungufu masokoni.

Mmoja ya wauza ndizi, Kihange Haji Juma, alisema wanalazimika kuuza bei ya juu kwa sababu ndizi zimekuwa adimu na hizo zinazopatikana wanauziwa bei kubwa.

Nae mfanyabiashara wa nazi, Abdi Mohammed, alisema nazi zimekuwa adimu na kwa jumla wananunua kati ya shilingi 1200 na 1600 kwa nazi moja.

Katika masoko ya Mwanakwerekwe na Darajani, hali ni mbaya zaidi hali iliyosababisha wananchi wengi kumiminika katika soko la Mombasa.

Kisiwani Pemba, pia hali sio nzuri kutokana na bidhaa nyingi kupanda bei na kusababisha wananchi kulalamika.

Katika soko kuu la Qatar, ndizi mbichi zinauzwa hadi shilingi 20,000 na kusababisha Waislamu wengi kukimbilia futari za nafaka.

Hassan Kombo (45), mkaazi wa Chake Chake, alisema wafanyabiashara wengi huweka mbele tamaa ya pesa ifikapo mwezi wa Ramadhani, bila ya kuzingatia hali za maisha ya wananchi ambao wengi wao ni maskini.

“Hali inatisha, wafanyabiashara hawana hata huruma, tunashindwa kununua bidhaa za shambani na tunakimbilia nafaka,” alisema.

Bibi Zuhura Khamis (33), mkaazi wa Wesha, alisema imekuwa kawaida kwa wafanyabiashara kuongeza bei ifikapo mwezi wa Ramadhani licha ya serikali kuwataka kupunguza bei.

Amour Juma (49), mkaazi wa Chake Chake, alisema mwezi wa Ramadhani si wa kufanyia uchumi, bali ni wa kusaidiana lakini wafanyabiashara wanashindwa kufahamu hilo.


Kwa upande wao wafanyabiashara kisiwani humo, walisema kupanda bei kwa vyakula katika mwezi wa Ramadhani kunatokana na kupanda ushuru.

Balozi Seif Akabidhi Cheki kwa Ajili ya Umeme Kisima cha Maji Kirombero

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kitop[e ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha kirombero kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu kutokana na ukosefu wa huduma ya maji safi yanayotarajiwa kupatikana muda si mrefu kijijini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu akitoa ufafanuzi kwa wananachi wa Kijiji cha Kilombero Wilaya ya Kaskazini “ B “ juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kisima cha maji safi na salama cha kijiji hicho.Ufafanuzi huo aliutoa wakati wa hafla fupi ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Sei Ali Iddi kukabidhi  hundi  ya shilingi milioni 14,000,000/- kwa ajili ya uwekwaji wa huduma za umeme katika Kisima hicho.
Balozi Seif akimkabidhi Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali Hassan Hundi ya shilingi Milioni 14,000,000,/- kwa ajili ya uwekwaji wa huduma za umeme kwenye kisima cha maji cha kijiji cha Kilombero.
Aliyepo kati kati yao ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B “ Nd. Khamis Jabir Makame.(Picha na Hassan Issa wa OMPR)


Na.Othman Khamis Ame
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Nd. Hassan Ali Hassan alisema shirika lake linakusudia kutumia rasilmali ilizonazo katika kuhakikisha huduma za umeme zinapatikana kwenye kisima cha maji cha Kijiji cha Kilombero ili kuwaondoshea usumbufu wa huduma za maji safi Wananchi wa Kijiji hicho.

Alisema kazi hiyo itakayoanza wakati wowote kuanzia sasa inatarajiwa kukamilika sambamba na ulazwaji wa mabomba ya maji utakaofanya na wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } kutoka kwenye kisima hicho hadi maeneo ya wakaazi wa Kijiji hicho.

Nd. Hassan Ali Hassan alitoa kauli hiyo mara baada ya kupokea hundi ya shilingi Milioni 14,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kupitia mfuko wa Jimbo ili kuanza kazi za kukipatia umeme kisima hicho kilichopo ndani ya shamba la ASP mashariki mwa Kijiji cha Kilombero.

Alisema licha ya gharama halisi zinazohitajika katika mradi huo wa umeme zinayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi Milioni 60,000,000/-  ikijumuisha nguzo, waya pamoja na transfoma lakini shirika litajitahidi katika kuona mradi huo unafanikiwa ili umeme upatikane katika kisima hicho.

“ Shirika litakuwa tayari kutumia rasilmali zake kidogo ilizonazo ili kuona mradi huu wa kuwafikishia huduma za umeme wananachi  wa Kilombero kwenye kisima chao unakamilika “. Alifafanua Nd. Hassan.

Meneja Mkuu huyo wa Shirika la Umeme Zanzibar alimpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif kwa jitihada zake anazoendelea kuchukuwa za kukabiliana na kero  zinazowasumbua  wananchi wake hasa zile za huduma za umeme na maji safi na salama.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu alisema kisima hicho tayari kimeshakamilika kwa muda mrefu sasa, lakini kilichobakia ni kusambazwa kwa mabomba kazi itakayochukuwa muda kidogo.


Dr. Garu alisema kisima hicho chenye uwezo mkubwa wa kusambaza huduma ya maji kwa  idadi kubwa ya wananchi kitahitajika  kuwekewa mabomba makubwa yenye upana wa  inchi nne ili kwenda sambamba na kasi ya maji yake.

Alisema hicho ni kisima cha pili kuchimbwa katika eneo hilo la kijiji cha kilombero badala ya kile cha awali ambacho hakikuwa na uwezo kamili wa kutoa huduma itakayotosheleza mahitaji  ya wananchi  hao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho cha Kilombero Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza wanakiji hao kwa ustahamilivu wao mkubwa wa kukosa huduma za maji safi na salama kwa muda mrefu.

Balozi Seif alisema nia ya uongozi wa jimbo hilo ilikuwa ni kuona wananchi hao wanafaidika na maji kutoka katika kisima hicho ndani ya kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, lakini upungufu wa vifaa vya kukamilishia miundo mbinu ya mradi huo ndio uliochangia tatizo hilo.

Alifahamisha kwamba eneo la kilombero limekuwa likikabiliwa na tatizo la muda mrefu la upatikanaji wa huduma za maji safi kiasi kwamba wananchi wake hasa akina mama wanatumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo badala ya nguvu zao kuzielekeza katika harakati zao za kimaisha.

Zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- zilizotolewa na Mbunge  wa jimbo la Kitope Balozi Seif zimetumika kugharamia ujenzi wa kibanda cha kisima hicho kilichochimbwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA }.

Mdahalo wa Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

$
0
0
Mwenyekiti wa Mdahalo wa kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye Mjumbe Mstaaf wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Tanzania Mhe. Mohammed Yussuf, akizungumza katika mdahalo huo ulioandaliwa na Zanzibar Institute for Research and Public Policy  kwa ufadhili wa Taasisi isiyo ya kiserekali ya The Foundation for Civil Society Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Lugha za Kigeni Vuga Zanzibar.  
Mgeni rasmin Mzee Hassan Nossor Moyo akitowa hutuba ya ufunzuzi wa Mdahalo la kujadili Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi za lugha za kigeni Vuga Zanzibar na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali Zanzibar.  
Washiriki wa Mdahalo wa Rasimu ya Katiba wakimsikiliza Mzee Moyo akizungumza katika mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya lugha za kigeni Vuga Zanzibar. 

                                                   Wananchi wakifuatilia mdahalo huo

Mshiriki wa Mdahalo huo Mzee Enzi Talib akichangia mada katika Mdahalo huo uliofanyika ukumbi wa Taasisi za lugha za kigeni Vuga. 

Mjumbe Mstaafu wa Tume ya Marekekebisho ya Katiba Tanzania Mhe. Ali Saleh akitowa ufafanuzi wa jambo wakati wa kujibu michango ya Wananchi walioshiriki mdahalo huo.

ZSTC yataka uadilifu ununu karafuu

$
0
0
Na Ali Mohamed
MKURUGENZI Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC),Mwanahija Almas Ali, amewataka Wakaguzi, Wapasishaji na Makarani wa shirika hilo, kufanya kazi kwa uadilifu na busara wanapowahudumia wakulima wa karafuu .

Akitoa nasaha kwa watendaji hao katika mkutano wa kutathmini utendaji wao katika msimu wa mavuno ya karafuu kwa mwaka 2013/2014, katika ukumbi wa Benjamin Mkapa Wete, Mkurugenzi huyo alisema pamoja na mafanikio ya shirika katika manunuzi ya karafuu bado kuna malalamiko kutoka kwa wakulima vituoni.

Alisema katika msimu wa 2013/2014 ZSTC imevuka makadirio katika manunuzi ya karafuu ambapo mafanikio hayo yanaongeza matumaini ya serikali na wananchi kwa shirika katika kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi kupitia zao la karafuu.

“Serikali na wananchi wana matumaini makubwa kwa ZSTC kupitia zao la karafuu katika kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi kwa sababu karafuu ni zao pekee Zanzibar lilochangia kwa asilimia kubwa pato la taifa hivyo watendaji tuwe makini ,” alisema.


Alisema ni lazima watendaji hao ambao wanaazimwa kutoka taasisi za serikali wawe waadilifu na kutumia busara zaidi wanapowahudumia wakulima katika vituo vya manunuzi .

Kwa upande wao watendaji hao walisema kwa kawaida huwa wanakabiliana na changamoto nyingi katika vituo vya manunuzi kutoka kwa wakulima na waliahidi kutumia busara na taaluma ya huduma kwa wateja katika kukabiliana na changamoto hizo.


Akitoa mada ya uadilifu katika biashara, Ustadh Omar, alisema kazi ni ibada hivyo ni vyema watendaji hao ZSTC wakazingatia adilifu katika vipimo ili kulifanya zao la karafuu kuendelea kuwa neema kwa wananchi. 

Maalim Seif Atembelea Watoto Yatima wa Kituo cha Muzdalifa Zanzibar.

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mwekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa wakati alipokwenda kuwatembelea Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya hio Amani Mjini Zanizbar.Katikati ni Katibu Mkuu wa Jumuiya Farouk Hamad.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea Zawadi ya Mas-haf kwa mtoto Khunayna Said kwa niaba ya Wototo wenziwe Mayatima wanao hudumiwa na Muzdalifat alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi akipokea Zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya yaKiislam ya  Muzdalifat Farouk Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa Abdalla Hadhar Bahasha yenye Sadaka kwa ajili ya Watoto yatima alipowatembelea watoto hao Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.

Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya ya MUZDALIFAT wakisoma kasda kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katikati akiwa pamoja na Viongozi wa Jumuia ya Kiislamu ya Muzdalifa wakiinua Mikono kuomba Dua kwa ajili ya Watoto na wote waliohudhuria alipowatembelea watoto yatima huko Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya  Farouk Hamadi na kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya Abdalla Hadhar( Picha na Yussuf Simai Maelezo)

Magazetini Leo Tz Bongo.


Katuni wa Leo na Ujumbe wakeb huoooooooo........

Mambo ya Mtandao wa Zanlink hayo

$
0
0
Wanafunzi wa Vyoo mbalimbali Zanzibar wanafaidika na huduma ya bure ya mtandao kupitia kampuni ya Zanlink hutowa huduma hiyo ya Bure ya Wifi katika maeneo ya Bustani ya Forodhani na Bustani ya Jamuhuri weles, wanafunzi wengi hunufaika na huduma hiyo kurahisisha kazi zao kwa kupitia katika mitandao, kama walivyokutwa na Mdua wakiwa katika makao makuu ya Ofisi hiyo majestik Zenj wakichati masomo yao kupitia taika mtandao.kutoka katika kampuni ya Zanlink majestic wakipata huduma hiyo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu akiwa katika mizunguko ya mitaani 

Wawaaa Uwanja wa Watoto Kariakoo. Huooooo....... hatua za mwisho.

$
0
0
 Uwanja wa Kufurahishia Watoto Kariakoo ukiwa tayari takribai asilimia nyingi kutokana na kuendelea na ufungwaji wa pembea katika uwanja huo na kutia matumaini Watpto wetu mwaka huu watakumbukia enzi zile za uwanja huu kwa burudani za pembea mbalimbali na huduma nyengine za michezo ya watoto kiwanjani hapo.


Maalim Seif Atembelea Masoko ya Bidhaa Zenj.

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei ya samaki, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.
Mfanyabiashara wa muhogo na majimbi, akitoa bei ya bidhaa hizo wakati Maalim Seif alipofanya ziara ya kutembelea soko la Mwanakwerekwe, katika soko hilo bei ya majimbo kwa fungu shilingi 2000/= na 5000/=
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia biashara ya mitumba katika kituo cha biashara Saateni, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.

Mfanyabiashara wa soko la matunda Mombasa, akimkabidhi boga Maalim Seif kwa ajili ya futari, wakati alipotembelea soko hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei ya samaki na pweza katika soko la darajani, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.(Picha na Salmin Said OMKR)

Maalim Seif Atembelea Marikiti kuangalia Bei za Vyakula.

$
0
0
Na Hasaan Hamad OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na uwepo wa vyakula na matunda yenye viwango kwa ajili ya mwezi mtuku wa Ramadhani.

Hata hivyo amesema bei zake bado ziko juu ikilinganishwa na kipato cha wananchi, na kwamba wananchi walio wengi wanashindwa kumudu kununua bidhaa hizo.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kutembelea masoko mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa na matunda, ambayo hutumika sana katika mwezi wa Ramadhan.

Amewashauri wakulima na wafanyabiashara kuzingatia hali za maisha ya wananchi, na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei, ili wananchi waweze kumudu kununua bidhaa hizo.

“Sitaki niwambie kuwa wauze kwa hasara, lakini wapunguze kuingiza faida nyingi ili kila mwananchi aweze kumudu kununua, na wakifanya hivyo inaweza kuwa sadaka nzuri kwao katika mwezi huu wa Ramadhan”, alisisitiza Maalim Seif na kuongeza,

“Nashkuru katika bidhaa nilizoziona ziko katika kiwango cha kuridhisha, na sijaona dalili ya ndizi au matunda mengine yaliyochomwa moto”, alisema.
Amesema Serikali imetoa fursa ya soko huria kwa wafanyabiashara, na kwamba upandaji wa bei kwa bidhaa hizo unayokana na wakulima na wafanyabiashara wenyewe.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa vitoweyo, Maalim Seif amesema hali hairidhishi, kwa vile samaki waliopo ni wachache, na hivyo kuuzwa kwa bei ya juu.


Kuhusu uvumi wa kuwepo kampuni inayotaka kuingiza samaki kutoka nje ya Tanzania na kuuzwa kwa bei nafuu, na kuwepo madai kuwa kampuni hiyo imezuiwa na Serikali, Maalim Seif amesema yeye hana taarifa hiyo, lakini ikiwa kuna ukweli wowote inawezekana kuwepo sababu za msingi kwa Wizara inayohusika kufanya hivyo.

Aidha Maalim Seif ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya soko la Mombasa ambalo linaendelea kufanyiwa matengenezo makubwa ambayo yatasaidia kutunza hadhi ya soko hilo la matunda.

Hata hivyo ameelezea kutoridhishwa na hali ya usafi katika soko la samaki Malindi, na kuliagiza Baraza la Manispaa kuweka utaratibu mzuri wa kulitunza eneo hilo la kuuzia samaki, ili liwe katika hali ya usafi wakati wote.

Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba serikali kuwawekea mazingira bora ya kufanya biashara zao, sambamba na kulalamikia baadhi ya wafanyabiashara waliorejea soko la Mwanakwerekwe baada ya kuhamishiwa katika soko la Mombasa.

Katika ziara hiyo Maalim Seif ametembelea soko la matunda Mombasa, soko Kuu la Mwanakwerekwe, Kituo cha biashara Saateni na Soko Kuu la Darajani.

Wakati huo huo Mhe. Maalim Seif amewatembelea na kuwafariji watoto yatima wanaolelewa na jumuiya ya Muzdalifat katika eneo la Amani mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdallah Hadhir Abdallah ameishukuru serikali kwa mashirikiano waliyonayo kwa jumuiya hiyo, na kuiomba kuongeza misaada yake ili kuwaendeleza watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbali mbali vya Zanzibar.


ZEC Zanzibar yatowa mafunzo ya Jinsia na Uchaguzi Zanzibar yaliodhaminiwa na Umoja wa Afrika (AU)

$
0
0
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ndg. Jecha Salim Jecha akifungua mafunzo ya siku tano ya Jinsia na Uchaguzi, kulia Mkurugenzi wa Tume hiyo, ndg. Salum Kassim Ali na kushoto Msaidizi Mkuu wa Kitengo cha kusimamia Demokrasia na Uchaguzi Umoja wa Afrika (AU), ndg. Shumbana Amani Karume. Mafunzo hayo yameandaliwa na ZEC na kudhaminiwa na AU yanafanyika katika Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar
MKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) , Salum Kassim Ali akitoa maelezo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya Jinsia na Uchaguzi. Mafunzo hayo yameandaliwa na ZEC kwa udhamini wa Umoja wa Afrika (AU) yanafanyika katika Hoteli ya Serena Inn Mjini Zanzibar
Washiriki wa mafunzo ya Jinsia nacUchaguzi wakimsikiliza muwezeshaji akitowa Mada katika mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena Zanzibar.
 MSAIDIZI Mkuu wa Kitengo  cha Kusimamia Demokrasia na Uchaguzi katika Umoja wa Afrika (AU) Ndg. Shumbana Amani Karume akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano juu ya Jinsia na Uchaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  na kudhaminiwa na AU.


 MSAIDIZI Mkuu wa Kitengo  cha Kusimamia Demokrasia na Uchaguzi katika Umoja wa Afrika (AU) Ndg. Shumbana Amani Karume akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano juu ya Jinsia na Uchaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  na kudhaminiwa na AU.
Maofisa wa Umoja wa Afrika (AU) Wakifuatilia Mafunzo hayo katika ukumbi wa Mkutano hoteli yaSerena Inn Zanzibar 
Afisa Uhusiana wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bi Salh wa kwanza mwenye baibui akifuatilia mafunzo hayo akiwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa mafunzo hayo hoteli ya Serena Zanzibar.




Washiriki wa mafunzo ya siku tano ya Jinsia na Uchaguzi  wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Afrika na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.(Picha na Haroub Hussein)

Mke wa Kwanza wa Mfalme Mswati awasili Zanzibar kwa ziara ya Siku mbili.

$
0
0
Mke wa Kwanza wa Mfalme Mswati wa Swaziland Queen Nomsa  Matsebula akivishwa shada la maua baada ya kuwasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili,ambapo atatembelea sehemu mbalimbali ikiwa pamoja na Kizimbani,Shangani na Mji mkongwe wa Zanzibar.
Mke wa Kwanza wa Mfalme Mswati wa Swaziland Queen Nomsa  Matsebula katikati akifuatana na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar wakwanza kushoto baada ya kuteremka Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Mke wa Kwanza wa Mfalme Mswati wa Swaziland Queen Nomsa  Matsebula kushoto akibadilishana mawazo na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar katika Ukumbi wa Uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Wananchi Wamfurahia Rais Jk Uwanja wa Sabasaba Dar-es-Salaam alipofika kuona Maonesho ya Sabasaba.

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya  siku ya Jumamosi kutokana na muda. Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila mwaka. Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila mara alisimama na kuwasalimia. 
PICHA NA IKULU
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi alipofika viwanja vya Sabasaba Dar kuangalia maonesho ya Wafanyabiashara katika viwanja hivyo.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Watoto waliofika viwanja vya Maonesho Sabasaba mjini Dar.


Rais Kikwete akimsalimia mtoto aliyefika katika viwanja hivyo vya maonesho barabara ya kilwa Dar kujionea maonesho ya biashara katika viwanja hivyo. 

Makamu wa Rais Dkt Bilal Aiwakilisha Tanzania katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Malawi.

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika 
Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni Mama Asha Bilal
. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA MALAWI
Julai 06, 2014 Lilongwe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumapili Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Civo jijini Lilongwe.

Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia alihudhuria Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika.

Sherehe hizo zilianza kwa ibada ya misa asubuhi na kisha kuhamia katika uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur Peter Mutharika  alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka 50 na baadaye kulihutubia taifa.

Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Mutharika alisisitiza kuhusu umuhimu wananchi wa Malawi kuwa wamoja na akaeleza nia yake ya kujenga umoja kwa nchi zinazoizunguka Malawi pamoja na zile za Kusini mwa Afrika. Baada ya hotuba hiyo, sherehe hizo ziliendelea na mchezo wa soka baina ya timu ya taifa ya Malawi na Msumbiji.

Malawi ilipata uhuru wake mwaka 1984 ikiongozwa na Rais wake wa kwanza Dkt. Kamuzu Banda hadi mwaka 1994. Baada ya mwaka huo alifuata Rais Dkt. Bakili Muluzi aliyetawala kuanzia mwaka 1994 hadi 2004. 

Baaada ya mwaka huo alifuata Rais Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala hadi mauti yalipomkuta mwaka 2012. Dkt. Joyce Banda aliyekuwa Makamu wa Rais wa Mutharika alichukua madaraka na kukaa hadi mwaka huu 2014 ambapo Malawi iliingia katika uchaguzi mkuu na kisha Rais Profesa Arthur Peter Mutharika aliposhinda uchaguzi huo na hivyo kuwa Rais wa nne wa Malawi.

Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim na Mheshimiwa Makamu wa Rais amerejea nyumbani Tanzania Julai 07, 2014 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 06, 2014 Lilongwe: Malawi

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Azungumza na Mke wa Mfalme Mswati Ikulu Migombani Zanzibar.

$
0
0
Mke wa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza   la Mapinduzi Mhe Mama Mwanamwema Shein (kulia) akisalimiana na Mke wa Kwanza wa Mfalme Muswati wa Swasiland  Mama Nomsa  Matsebula,alipofika Ikulu ya Migombani  na ujume wake leo,akiwa katika ziara ya siku mbili nchini
Mke wa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza   la Mapinduzi Mhe Mama Mwanamwema Shein (kulia) akizungumza na Mke wa Kwanza wa Mfalme Muswati wa Swasiland  Mama Nomsa  Matsebula,alipofika Ikulu ya Migombani  na ujume wake leo,akiwa katika ziara ya siku mbili nchini,
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Harakati za Wananchi wa Mji wa ChakeChake Pemba hizoooooo.............

Maalim Seif afutarisha

$
0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa nasaha zake baada ya kujumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani katika futari ya pamoja aliyoindaa kwa ajili ya wanachuo hao.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani Dr. Hamed Rashid Hikman, akitoa neno la shukrani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kujumuika na wanafunzi wa Chuo hicho katika futari ya pamoja
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani, alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya futari ya pamoja na wanachuo hao.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani wakijumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. (Picha na Salmin Said, OMKR).
 
Na: Hassan Hamad (OMKR).
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amejumuika pamoja na wanafunzi na watendaji wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani katika futari ya pamoja, na kutaka utamaduni wa kufutarishana miongoni mwa waislamu uendelelezwe.
 
Amesema utamaduni huo ni muhimu na utapaswa kuendelezwa kwa vile unajenga mapenzi, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu, na kwamba hatua hiyo itavirithisha vizazi vijavyo utamaduni ulio bora.
 
Maalim Seif amewashukuru wanachuo hao kwa kukubali kujumuika nao katika futari hiyo ya pamoja, na kuwatakia kheri ya mfungo mtukufu wa Ramadhani.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dr. Hamed Rashid Hikman amemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuamua kujumuika na wanachuo katika futari hiyo ya pamoja.
 
Dr. Hikman amesema kitendo cha viongozi kujumuika pamoja na wananchi  katika shughuli za kijamii ikiwemo futari, ni jambo la msingi ambalo linajenga umoja na upendo  kati ya wananchi na viongozi.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameanza kuwafutarisha wanachuo hao, ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kufutarisha makundi mbali mbali ya kijamii yakiwemo ya wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi mbali mbali kupitia ngazi za Wilaya na vijiji, kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Viewing all 36208 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>