Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36208 articles
Browse latest View live

Wanafunzi Kengeja wakabidhiwa zawadi

$
0
0
 
OFISA Mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais Pemba, Amran Massoud Amran, akimkabidhi mmoja kati ya wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Kengeja wilaya ya mkoani, sare na fedha taslimu kama zawadi zilizotolewa na mzaliwa wa kijiji hicho dk, Omar Dadi Shajak, kwenye hafla iliofanyika skulini hapo, ambapo wanafunzi hao ni wale waliofaulu mitihani yao ya darasa la saba na darasa la kumi na tatu mwaka 2013/2014 (picha na Haji Nassor, Pemba)


MWENYEKITI wa skuli ya sekondari ya Kengeja wilaya ya mkoani Pemba, Hassan Abdalla akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi za sare na fedha kwa wanafunzi waliofaulu ngazi na michepuo na darasa na kumi na tatu mwaka 2013/2014, zilizotolewa na mzaliwa na Kengeja dk Omar Dadi Shajak, katikati ni mjumbe wa kamati hiyo Said Khalifan Amour akifutiwa na Ofisa mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais Pemba Amran Massoud Amran (picha na Haji Nassor, Pemba)    

Mke wa mfalme Mswati atembelea Shamba la Viungo Kizimbani

$
0
0
 Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula kulia  akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo kuhusu Mmea wa Mchaichai na faida zake wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
 Mmea wa Mmanjano kama unavyoonekana ambao ni miongoni mwa mimea yenye faida kubwa ambao hupatikana sehemu ya Kizimbani Zanzibar.
 Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula Katikati akipata maelezo kuhusu Mmea wa Mmanjano na faida za Manjano Kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
 Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akishika Mmea wa Mvuje na kupata maelezo yake kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo wakati alipotembelea katika Shamba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
 Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akiuluza maswali kuhusu karafuu, kama anavyoonekana pichani kushika karafuu hio wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akipata maelezo kutoka kwa Mtembezi wa Watalii Shaaban Ali Hassan kuhusiana na Kima Punju alipotembelea katika maeneo ya Jozani Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Dk Shein awaambia waathirika wa ujenzi wa Barabara Wete - Gando: Tutawalipa fidia

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                  08 Julai, 2014
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi walioathirika na ujenzi wa barabara ya Wete-Gando na Gando-Ukunjwi kuwa watalipwa fidia lakini wanapaswa kufanya subira kwa kuwa tathmini ya athari za ujenzi huo itafanyika kwa ukamilifu baada ya ujenzi kukamilika ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
 
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Raha, wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo wakati akikagua ujenzi wa barabara hizo, Dk. Shein aliwaambia wananchi hao kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kufanya malipo yoyote hadi hapo ujenzi utakapokalimika na kufahamu hasara kamili aliyopata kila mwananchi.
 
Wananchi wa kijiji cha Raha walilalamika kuwa ujenzi wa barabara hizo umeathiri nyumba zao pamoja na mazao na kuwa pamoja na Serikali kufanya tathmini Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano hadi sasa imeshindwa kuwalipa fidia.
 
Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo ya Waziri wa Wizara hiyo Rashid Seif malipo ya fidia yalifanywa kwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao tu wakati ujenzi ulipoanza na kwa wale ambao nyumba zao hazikuvunjwa zitatathminiwa mwishoni mwa mradi kwa kuwa bado athari itaendelea wakati ujenzi haujakamilika.

 
Kwa hivyo Dk. Shein aliutaka uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuweka mpango maalum wa kulipa fidia wananchi walioathirika na ujenzi wa barabara hizo hususan kwa walioharibiwa miti yao ambao ni miongoni mwa waliotoa malalamiko.
 
Akijibu malalamiko ya Bwana Bakari Rajab Bakari kuhusu kutofahamu lolote kuhusu fidia ya miti yao iliyokatwa kupisha ujenzi huo ikiwemo mikarafuu, minazi, mishelisheli na miembe, Dk. Shein aliusisitizia uongozi wa Wizara hiyo kufanya mikutano ya pamoja na wananchi ili kuwapa taarifa za mara kwa mara kuhusu hatua zilizofikiwa kuhusu malipo yao.
 
Katika hatua nyingine Dk. Shein alilazimika kuzitembelea nyumba zilizodaiwa kuathirika za baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ili kumaliza ubishi kati ya wananchi hao na wizara kuhusu malalamiko kuwa nyumba zao hazikutembelewa wala kutathminiwa huku viongozi wa wizara wakisisitiza kuwa wamezitembelea.
 
Baada ya kufaya hivyo Dk. Shein aliwataka viongozi wa wizara na mkoa Kaskazini Pemba kuwatembelea wananchi hao ili kuweka mambo yote sawa ili kuepuka malalamiko wakati malipo yatakapowadia.
 
Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza na Mapinduzi alieleza kuwa kumekuwepo na mabadiliko tangu alipozitembelea barabara hizo mwanzoni mwa mwaka huu.
 
Kwa hivyo amesisitiza Mkandarasi kumaliza ujenzi kwa mujibu wa ratiba mpya ambayo ujenzi umepangwa kukamilika mwezi Disemba mwaka 2014.
 
Alieleza matumaini yake kuwa kila upande utatimiza wajibu wake na kuona barabara hizo zitakamilka kama ilivyopangwa.
 
Awali akitoa maelezo kwa Mhe Rais, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk. Juma Malik Akili alieleza kuwa ujenzi wa barabara za Wete- Gando hadi Ukunjwi na Wete-Konde ambazo ujenzi wake ulisimama kutokana na changamoto mbalimbali unatarajiwa kumalizika mwezi Disemba mwaka huu.
 
Barabara hizo ambazo awali zilitarajiwa kumalizika mwaka 2012 zinajengwa kwa fedha kutoka BADEA, SAUDI FUND na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hadi sasa alieleza kuwa utekelezaji umefikia asilimia 75.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi yuko kisiwani Pemba kwa ziara ya siku tatu ambapo kesho anatarajiwa kuzindua ununuzi wa zao la karafuu,kutembelea mashamba ya karafuu pamoja na miradi ya ufugaji wa samaki.
 
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameuhimiza uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kusogeza huduma za umeme katika vijiji vya Mlima Sudi, Buyuni na Mkote katika shehia ya Ukunjwi, wilayaya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 
Dk. Shein ametoa agizo hilo wakati akijibu ombi la wananchi wa vijiji vya jirani ya kijiji cha Raha wakati alipokuwa akikagua barabara za Wete-Gando na Gando-Ukunjwi.
 
Alieleza ni muhimu kuwapelekea huduma hiyo ambayo tayari inapatikana katika kijiji cha Raha ambapo ni karibbu na vijiji hivyo ambapo kwa kufanya hivyo kutalipatia shirika mapato zaidi na kujijengea uwezo.
 

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

Dk Shein akagua ujenzi wa Barabara kisiwani Pemba

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Juma Malik Akili,wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo leo,[Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya Mecco Tanzania Abdulkadir Sheikh Bujet akitoa maelezo kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo leo,[Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
 Mkandarasi msimamizi wa Kampuni ya J.Burrow ya Dar es salaam Mohamed Hussein akitoa maelezo kuhusu utengenezaji wa barabara wakati Rais  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo leo,[Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelekezo kwa watendaji kampuni ya Ujenzi wa barabara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde-Wete-Wete Gando na Gando –Ukunjwi,alipotembelea kuona maendeleo ya kazi zinazofanyika katika ziara ya Mkoa huo leo,[Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Raha Shehia ya Ukunjwi,Jimbo la Gando Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijiorodhesha wakati walipotakiwa Wananchi walioathirika na Nyumba zao kutokana na Ujenzi wa Barabara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde-Wete-Wete Gando na Gando –Ukunjwi,wakati Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipofanya ziara leo katika Mkoa huo . [Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa kijiji cha Raha Shehia ya Ukunjwi,Jimbo la Gando Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofanya ziara leo katika Mkoa huo ya kutembelea  maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi, [Picha na Ramadhan Othman Pemba.]
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa  maelekezo kwa Afisa Mdhamini wa Wizara Mindombinu na Mawasiliano Pemba   Hamadi Ahmed Baucha kuhusu malipo ya fidia ya Nyumba ya Mzee Mohamed Waziri Mbwa Mkaazi wa Kijiji cha Raka (katikati) wakati alipotembela ujenzi wa barabara tatu za Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi, Mkoa waKaskazini Pemba. [Picha na Ramadhan Othman Pemba.]

Dk Shein afutarisha wananchi wa Pemba

$
0
0
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akiwakaribisha Mashekhe katika futari  aliyoiandaa kwa Wananchi  waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Viwanja vya Ikulu ya Wete jana.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na akinamama   na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Baadhi ya  akinamama mbali mbali wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari aliyowandalia na Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (aliyesimama) alipokuwa akitoa shukurani pamoja na kuomba dua baada ya kumaliza kufutari wananchi waumini wa Dini ya kiislamu,futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiitikia Dua iliyoombwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete ,[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiagana na  akinamama   mbali mbali na Viongozi waliohudhuria katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Maalim Seif afutarisha watendaji wa CUF nyumbani kwake

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Sheikh Mohd Khamis (aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Mjini, baada ya futari aliyowaandalia watendaji wa CUF nyumbani kwake Mbweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji, kabla ya futari aliyowaandalia watendaji wa CUF nyumbani kwake Mbweni.
 Sheikh Mohd Khamis akiongoza Sala ya Magharibi nyumbani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Mbweni Zanzibar.
Watendaji wa CUF wakipata futari waliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya futari ya pamoja na watendaji wa CUF nyumbani kwake Mbweni. Kulia ni Mkurugenzi wa Habari na mawasiliano ya umma (CUF), Salim Bimani. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Dk Shein azindua ununuzi wa karafuu 2014-2015

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia zao la karafuu alipotembelea katika shamba la Bw.Said Sinani  (hayupo pichani) Shumbageni Kusini Pemba akiwa katika ziara maalum.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Bw.Said Sinani (kulia) baada ya kulitembelea shamaba lake la mikarafuu leo akiwa katika ziara Mkoa wa Kusini Pemba,(kusho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizindua ununuzi wa karafuu kwa msimu wa mwaka 2014-2015  katika kituo cha ZSTC Mkoani Pemba,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda  na Masoko Nassor Ahmed Mazrui ,zoezi hilo lilifanyika leo.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Grand Malt yakabidhi vifaa Timu za Ligi Kuu ya Zanzibar

$
0
0
 


 
MENEJA wa Kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam akitoa maelezo katika makabidhiano ya vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt yaliofanyika katika uwanja wa Amaan.(Picha na Haroub Hussein).

 
RAIS wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina akizungumza katika makabidhiano ya vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt yaliofanyika katika uwanja wa Amaan.(Picha na Haroub Hussein).

 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Zanzibar Grand malt, kulia Meneja wa Kikwaji cha Grand Malt, Consolata Adam na kushoto Rais wa ZFA , Ravia Idarous. Makabidhiano hayo yalifanyika katika uwanja wa Amaan.(Picha na Haroub Hussein).

 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk akimkabidhi vifaa Afisa Michezo wa Mafunzo , Khamis Ali wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Grand Malt.(Picha na Haroub Hussein).

 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk akimkabidhi vifaa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi , Issa Ahmada Jogoo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Grand Malt.(Picha na Haroub Hussein).
 

 



Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi

$
0
0
Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi
 
Raia unayo haki ya:-
 
*Kumwomba Askari ajitambulishe kwako....
-Muulize Jina lake.
-Muulize namba yake ya Uaskari.
*Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa.
*Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU.
*Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo.
*Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo.
*Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako.
*Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo.
*Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni.
Haki za Raia Kupekuliwa
*Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo.
*Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume.
*Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na:
(a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani.
(b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika.
(c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa.
 
Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act).
 
Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale.
 
Share na marafiki zako!!!
 
Tundu Lissu via Face Book

Chezea mfungo wa Ramadhaan Machomanne!

$
0
0
Vijana wakipata joto ya jiwe baada ya kukutwa mchana wa Ramadhaan Machomanne Chake Pemba wakifanya mambo kinyume na maadili ya mwezi mtukufu.( Picha kwa hisani ya Abdi Suleiman, Pemba)
 
Elimu bado inahitajika kwa waumini kuweza kufahamu na kuelimishwa kuhusiana na funga kwani licha ya kuwa ni amri kutoka kwa Allaah Subhaanahu Wata'ala pia ni moja katika nguzo kuu tano za dini yetu ya kiislamu.
 
Kula kwa makusudi au kufanya jambo litakalobatilisha funga kwa makusudi mchana wa Ramadhaan si kwamba kunabatilisha funga tu bali kunaweza kukutoa katika dini pia kwa mujibu wa baadhi ya Maulamaa kwa kuikana moja katika nguzo za kiislamu.
 
Tusichoke kuwakumbusha ndugu zetu umuhimu wa kujitambua na kujielewa kwamba ni Waislamu kwanza na tutaulizwa na Muumba siku ya siku

Dk Shein ziarani Kusini Pemba

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mshauri wa Rais Uwekezaji Bw.Abrahman Mwinyi Jumbe (kushoto) akipotembelea shamba la ufugaji wa samaki la kikundi cha Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi wa  wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki Mwambe kusini Pemba jana,wa Pili (kulia) Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Watoto wa Kijiji cha Mwambe  mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa  wanakikundi cha Ufugaji wa Samaki cha Hakiliki  jana,alipofanya ziara katika Mkoa wa Kusini Pemba. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Chake Chake  Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Kusini Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Chake Chake. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Pemba Mwanajuma Majid katika futari iliyowaandalia wananchi wa Vijiji mbali mbali vya mkoa wa Kusini Pemba hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Ikulu ya Chake Chake. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Baadhi ya akinamama wa Mkoa wa kusini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari waliyoandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Ikuu ya Chake chake jana, [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
 

Maalim Seif afutarisha na kutembelea wagonjwa Donge

$
0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika kijiji cha Donge Muwanda kufutari na wananchi wa kijiji hicho.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akijumuika na wananchi wa kijiji cha Donge Muwanda katika futari ya pamoja.
 Mzee Abdulhakim Muhsin Abeid wa kijiji cha Donge Muwanda, akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho baada ya kufutari  pamoja  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya kumjuilia hali mzee Foum Denge (kushoto) wa kijiji cha Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwafariji baadhi ya wananchi katika ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na wazee mbali mbali katika kijiji cha Bumbwini, baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja. (Picha na Salmin Said, OMKR).

Biashara ya Nguo Kipindi cha Mwezi wa Ramadhan hushamiri sana.

$
0
0
Vijana wajasiriamali kisiwani Pemba wakiwa katika biashara yao wakisubiri wateja wao, kipindi hichi cha mfungo wa Ramadhan

Wananchi wa Donge wahimizwa kuendeleza umoja na mshikamano

$
0
0
Na Hassan Hamad OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amejumuika pamoja na wananchi wa kijiji cha Donge Muwanda katika futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa kijiji hicho.
 
Akitoa nasaha zake baada ya futari hiyo, Maalim Seif amewahimiza wananchi wa Donge kuendeleza umoja na mshikamano walionao, na kamwe wasikubali kugawanywa kwa sababu zozote zikiwemo za itikadi za kisiasa.
 
Maalim Seif ambaye baada ya futari hiyo aliungana na waumini wa kijiji cha Donge katika sala ya Isha na Tarawehe, amewasisitiza wananchi hao kuendeleza utamaduni wa kufutari pamoja ambao uliasisiwa tokea wakati wa enzi za Mitume, na kwamba kufanya hivyo kutakuza mshikamano na mapenzi miongoni mwao.
 
Amewashukuru wananchi hao wa Donge Muwanda kwa kukubali kuungana nae katika futari hiyo, kitendo ambacho amesema kimempa faraja na matumaini ya kuendelea kwa mshikamano uliopo nchini.
 
Mapema akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Donge Muwanda, Mzee Abdulhakim Muhsin Abeid, amempongeza Maalim Seif kwa uamuzi wake wa kufutari  na wananchi wa kijiji hicho.
Amesema kitendo hicho kimewaleta pamoja wananchi mbali mbali wa kijiji hicho, na kuomba utamaduni huo uendelezwe ili kukuza mshikamano na maelewano miongoni mwa wananchi.
 
Akizungumzia kuhusu historia ya kijiji hicho cha Muwanda, Mzee Abdulhakim amesema kijiji hicho kina historia ndefu tokea wakati wa ukoloni na harakati za kupigania uhuru.
 
Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Katika ziara hiyo Maalim Seif amewatembelea wagonjwa na kuwafariji wafiwa katika vijiji vya Matemwe, Donge, Kitope na Bumbwini, ambapo anatarajiwa kuendelea na ziara hiyo kwa Mikoa yote ya Unguja na Pemba, ndani ya kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

KONGAMANO LA NNE LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA (TAPSEA) LAFUNGULIWA LEO JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana 
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda.Picha na Othman Michuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu pamoja na Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki wakati wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza Picha na Othman Michuzi.

Ally Fereji Tamim mgeni rasmi Zanzibar Beach Soccer Bonanza, Agosti 2

$
0
0
 


Na Andrew Chale
TAASISI ya  Mwangaza wa buradani Zanzibar  (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja,  Zanzibar,  kupitia vyombo vya habari, imemtangaza rasmi , Raisi mstaafu wa  Chama cha Soka  Zanzibar, (Zanzibar Football Association-ZFA) Mzee Ally Fereji Tamim  kuwa mgeni rasmi kwenye michuano maalum ya soka la ufukweni  lijulikanayo kama  (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti  Mbili mwaka huu katika fukwe za  Nungwi.
Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo  kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa, michuano hiyo ya Zanzibar Beach Soccer inatarajiwa kuzikutanisha timu mbalimbali za Visiwani humo, Bara na nje ya Tanzania ambapo watakutana kwa pamoja na kushiriki kichuano hiyo maalum, kwenye fukwe hizo za Nungwi.

Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’  alisema  wamejisikia furaha kwa viongozi wa juu na wadau wa soka kuwaunga mkono, kwani inatia moyo katika kuendesha shughuli za kimichezo kama hizo. “Tunapongeza wadau wote, kikubwa  zaidi, ni Mzee wetu,  Ally Fereji Tamim kukubari  kuwa mgeni rasmi, pia milango ipo wazi kwa wadau wengine kujitokeza katika kufanikisha zaidi tukio hili ,muhimu” alisema Muslim Nassoro ‘Jazzphaa’.
Aidha, aliendelea kuwaomba  mashirika, makampuni, taasisi za Serikali na za watu binafsi na wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini Bonanza hilo la Zanzibaar Beach Soccer, ilikufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuifikia jamii na kuiweka pamoja.

Muslim  Nassoro ‘Jazzphaa’ aliongeza kuwa, Michezo hiyo yenye lengo ya kuweka watu pamoja, kudumisha utamaduni na kuhimalisha afya ya mwili, pia itakuwa na burudani mbalimbali. Lakini pia alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa beach soccer na kamati yote kwa ujumla katika kufanikisha jambo hilo.
Kwa upande wake, Rais wa beach Soccer Zanzibar,  Bwana Ally Sheikh Alhabshy  alipongeza Taasisi hiyo kuandaa michuano hiyo ambapo amesisitiza kuwa Wadhamini wasisitite kutoa udhamini wao na kuja kuona mchezo huo unavyochezwa.
Zanzibar Beach soccer Bonanza kwa  mwaka huu itakuwa ni ya mara ya tatu, kwa taasisi hiyo kuandaa michezo hiyo ya soka la ufukweni.
Michezo hiyo ya soka la ufukweni imekuwa maalufu katika nchi mbalimbali zenye fukwe, ambapo wananchi na wageni kutoka mataifa mengine ujumuika kwa pamoja.
Kwa mwaka huu pia kutakuwa na burudani kali na ya aina yake itayaoporomoshwa na dj mkali anayetikisa visiwani humo.

Rais wa Zanzibar Dkt Shein akutana na Mgombea Urais wa Chama cha Frelimo Ikulu Zanzibar.leo

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,filipe Jacinto Nyusi baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ukumbi wa wageni  Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,filipe Jacinto Nyusi baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar(Picha na Ramadhani Othman)

DK Shein Ataka Mazingira ya Skuli ya Mpya ya Sekondari Mkanyageni Yaimarishwe Kukamilisha Ujenzi Wake.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                         11 Julai, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameiagiza Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha Skuli mpya ya Mkanyageni inakuwa na mazingira mazuri yanayoizunguka pamoja na eneo la kutosha ili kukamilisha mradi mzima wa ujenzi wa skuli hiyo inayotarajiwa kuwa ya Wilaya.
 Agizo hilo amelitoa jana wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa skuli hiyo huko Mkanyageni Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba katika siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu kisiwani Pemba iliyoanza Jumanne iliyopita.
 Katika maelezo yake kwa Mhe. Rais, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee alisema kuwa baadhi ya huduma katika skuli hiyo ikiwemo kiwanja cha michezo zitakosekana kutokana na uhaba wa eneo la skuli.
Alifafanua kuwa ingawa eneo hilil ni shamba la Ser
ikali lakini wameshindwa kupewa kwa sababu baadhi ya wananchi wamelichukua na kudai ni lao na baadhi tayari wamejenga nyumba za makaazi.
 Kwa hiyo Mhe. Rais aliagiza utaratibu ufanyike kuwasiliana na wananchi waliopo katika eneo hilo ili kufahamu kama wapo kisheria au vinginevyo na kusisitiza kuwa taratibu za umilikaji wa ardhi lazima zizingatiwe na kufuatwa.
 Dk. Shein ambaye alikuwa amefuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alisisitiza kuwa skuli hiyo ambayo ni kati ya miradi mikubwa ya aina yake ya ujenzi wa skuli za sekondari Zanzibar ikiwemo ya Kibuteni kisiwani Unguja ujenzi wake lazima ukamilishwe kama ilivyopangwa ili kuipa haiba na hadhi iliyokusudiwa.
 Skuli za sekondari Mkanyageni na Kibuteni zinajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Benki ya Mendeleo ya Uarabuni(BADEA).

 Sambamba na agizo hilo Mhe. Rais aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuwasilisha serikalini taarifa rasmi ya hali halisi ya utekelezaji wa ujenzi wa skuli ya Mkanyageni ambayo kwa mujibu wa maelezo ya Ndg. Abdalla Mzee baadhi ya majengo hayakuweza kujengwa kutokana na uhaba wa fedha.
Mapema katika taarifa yake kuhusu ujenzi wa skuli hiyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alisema kuwa baadhi ya majengo katika skuli hayataweza kujengwa kutokana na uhaba wa fedha.
Katika maelezo yake hayo alisema kati ya nyumba 16 za walimu, zimejengwa 8 tu huku dakhalia kwa wanafunzi wa kiume haikujengwa kutokana na sababu hizo hizo.
Halikadhalika uhaba wa fedha umesababisha pia msikiti kutojengwa ingawa zipo dalili za kupata wafadhili wa kujenga msikiti huo.
Kwa hivyo alieleza lengo la skuli hiyo kuwa ya dakhalia kwa wanafunzi wote halitatekelezeka badala yake wanafunzi wa kike tu ndio watakaoishi dakhalia na kwa wanafunzi wa kiume watachaguliwa wale wanaoishi karibu na skuli tu hivyo kutotimiza lengo lililokusudiwa.
Hata hivyo alieleza kuwa majengo yalioyoachwa yanaweza kujengwa katika awamu ya pili kama Serikali itakuwa na fedha.
Naibu Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa wizara yake inakabiliwa na changamoto kubwa katika kukamilisha ramani ya ujenzi wa skuli hiyo upande wa barabara ambazo hazikuwemo katika bajeti ya ujenzi.
Kuhusu maendeleo ya ujenzi wa skuli hiyo ambao ulianza mwezi Agosti, 2012 na kutarajiwa kumalizika Julai 2013 Ndg. Abdalla Mzee alisema hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 78 na inatarajiwa ujenzi utakamilika mwezi wa Disemba mwaka huu.
Alifafanua kuwa kuchelewa kukamilika kwa wakati kulitokana na kucheleweshwa malipo ya mkandarasi kutokana na fedha kuchelewa kutolewa kutoka kwa mfadhili.
Akiwa kisiwani Pemba, Dk. Shein alizindua ununuzi wa karafuu kwa msimu wa 2014/2015 na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ufugaji samaki katika vijiji vya Pujini na Mwambe mkoa Kusini wan Pemba na ujenzi wa barabara za Wete-Gando,Gando-Ukunjwi na Wete –Konde. Mbali ya kukagua miradi hiyo alipata fursa ya kufutarisha wananchi kisiwani humo.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 


Rais wa Zanzibar Atembelea Skuli Mpya ya Sekondari Mkanyageni Pemba

Maalim Seif awafariji wagonjwa Mkoa wa Kusini Unguja

$
0
0





 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea na kuwafariji wagonjwa katika vijiji vya Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Na Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameendelea na ziara yake ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Ziara hii ni mfululizo wa ziara zake za kuwatembelea wagonjwa katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, ambapo Alkhamis iliyopita alitembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Akiwafariji wagonjwa hao, Mhe. Maalim Seif amewaombea wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kimaisha.
 
Nao wagonjwa hao wamemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuamua kuwatembelea na kuwafariji, na kwamba ziara yake inaweza kuwa chachu ya kupata nafuu.
 
Katika ziara hiyo Maalim Seif ametembea wagonjwa katika vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini Unguja vikiwemo Kitogani, Kajengwa Makunduchi, Kibele na Umbuji.
 
Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-hajj Maalim Seif Sharif Hamad, jana alijumuika na Masheikh mbali mbali wa Zanzibar katika futari iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni.
 
 
 

 

Viewing all 36208 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>