Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36229 articles
Browse latest View live

Jamii yahamasishwa kupima TB

$
0
0
Na Zainab Anuwar
WASTANI ya watu 64,000 huugua kifua kikuu kila mwaka nchini Tanzania, sawa na wagonjwa 176 kwa kila siku.
Hayo yalielewa na Daktari Damana wa hospitali ya Kuu ya Mnazi Mmoja katika kitengo cha maradhi ya kifua kikuu na ukoma,Ali Ahmad, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mnazi Mmoja .
Alisema watu wengi wanapata maambukizo ya maradhi ya kifua kikuu na ukoma kwa sababu ya kutogundua mapema dalili zake na jinsi ya kujikinga.
Alisema hadi sasa kuna jumla ya wagonjwa 685 wanaoendelea na matibu katika hospitali za Unguja na Pemba.
Hivyo, aliwataka wananchi wanapoona wana dalili za kifua kikuu wafike hospitalini mapema kwa sababu ugonjwa huo unatibika.
Alisema watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo ni watu wanaoishi na VVU na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Kundi jengine ni la wazee walio na umri wa kuanzia miaka 65, watu wenye magonjwa wa muda mrefu kama vile kisukari, saratani pamoja na watoto wenye utapiamlo.

Daktari huyo alisema wanakabiliana na changamoto mbali mbali katika kupunguza ugonjwa huo ikiwemo jamii kuuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina. 

Katuni wa Leo na Ujumbe wake huoo.....

Harakati za Maandalizi ya Sikukuu Pemba

Taarifa vya Vymbo vya Habari

$
0
0
Na Himid Choko BLW. 
DAR ES SALAAM                                                                                          July 14, 2014
 Kamati ya mashauriano ya bunge Maalum la Katiba  inatarajiwa kukutana  kutathmini kazi zilizofikiwa za  utungaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Kamati hiyo inatarajiwa kukutana kwa siku mbili  kuanzia tarehe 24 mwezi huu katika ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Daresalaam.
Taarifa iliyotolewa na katibu wa bunge  maalum la katiba Yahya Khamis Hamad imeeleza kuwa kamati hiyo inawajumuisha wajumbe thelathini walioteliwa na Mwenyekti wa bunge hilo Mh Samwel Sita kwa kushirikiana na Makamu wake Mh Samia Suluhu Hassan.
Uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo ya mashauriano ya bunge hilo ni kwa mujibu wa   masharti ya kanuni ya 54(4) na (5) ya kanuni  za Bunge Maalum za mwaka 2014.

Taarifa hiyo imewaomba wajumbe walioteuliwa kuhuduhria kikao hicho kwa lengo la kufanikisha kazi waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Watanzania.

Kinyikani wahimizwa kudhibiti unyanyasaji

$
0
0
Na Shemsia Khamis, Pemba
OFISA Elimu na Mafunzo ya Amali wilaya ya Wete, Khamis Said Hamad, amesema, vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, havipaswi kunyamaziwa 

Alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Kinyikani wilaya ya Wete, katika mkutano maalumu wa kuhamasisha jamii namna ya kuyaripoti vitendo hivyo uliondaliwa na wananchi hao.

Alisema kumeundwa taasisi mbali mbali zinazoendesha mapambano hayo, lakini bado jamii haina mwamko wa kutoa ushahidi pale wahusika wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimekithiri katika jamii hivyo kina mtu ana wajibu wa kukabiliana navyo.


Kwa upande wake, Mratibu wa wanawake na watoto shehia ya Kinyikani, Muwa Siad Khamis, alisema katika shehia yake kuna baadhi ya watu wanavifumbia macho vitendo hivyo na kushindwa kutoa ushirikiano.

Sheha wa shehia ya Kinyikani,Mussa Rashid Said,alisema licha ya wanaharakati kuwa mstari wa mbele kupinga udhalilishaji, bado jamii yenyewe haijataka kubadilika.

Akizungumza katika mkutano kama huo uliofanyika shehia ya Kiungoni,mwanaharakati kutoka Wizara ya Wanawake na Watoto, Dina Juma Makota, alisema watoto wana haki yao


Mikutano hiyo ilifanyika chini ya ufadhili wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA).

Magazetini Tz Bongo

ZECO yakaribia kuuza umeme kwa simu

$
0
0
Na Kauthar Abdalla
SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO) linaendelea kuchukua hatua za kuimarisha huduma zake ili kuwapunguzia usumbufu wateja wake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msaidizi Ofisa Uhusiano wa shirika hilo,Haji Juma Chapa, alisema utaratibu ambao ulikuwepo mwanzo umeshapitwa na wakati na shirika linafanya kila jitihada kuhakikisha linarekebisha hitilafu zilizopo ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati.

Akizungumzia ununuzi wa umeme kupitia simu ya mkononi, alisema huduma hiyo haijaanza kutumika kwa sababu taratibu bado hazijakamilika kwa sababu mfumo unaotumika kuuzia umeme umeshapitwa na wakati.


Alisema shirika limeona ipo haja kwa mara ya kwanza kuanza kutoa huduma kwa kutumia mtandao wa Zantel kwa sababu wanannchi wengi wa Zanzibar wanatumia huduma za kampuni hiyo na baadae watafikiria kujiunga na mitandao mengine ya simu.


Aidha alisema kabla ya huduma hiyo kuanza kutumika kutakuwa na kipindi cha majaribio ambapo kuna idadi ya watu watatumiwa kuanza kutumia huduma hiyo kabla ya kuingizwa sokoni.

Donge walia na wizi wa mazao

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga.
WAKATI mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiendelea wakulima wa vijiji vya Donge Vijibweni na Donge pwani,wamelalamikia tabia ya wizi wa mazao iliyoshamiri, kitendo kinachowarejesha nyuma wakulima.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wanavijiji hao walisema mazao kama  muhogo, ndizi, viazi, mananasi,miwa na mapapai na mbegu za mihogo ndiyo yanayoibiwa kwa wingi.
Walisema mara nyingi mazao hayo kuibiwa nyakati za usiku wakati wakulima tayari wakiwa wameshaondoka.
Walisema kutokuwepo polisi jamii ndiko kulikosababisha ongezeko la wizi huo.
Naye sheha wa shehia ya Donge vijibweni, Abdalla Abrahman Machano, alikiri kuwepo kwa matukio hayo na kusema vijana wa mitaani ndio wanaoshiriki wizi huo.

Aliwashauri wakulima kushirikiana ili kuhakikisha wanakabiliwa na wizi huo pamoja  na mifugo inayoharibu mazao yao.

Ujumbe wa Katuni wa Leo Huoooo.............

AU yataka uchaguzi huru

$
0
0
Na Mwashamba Juma
UMOJA wa Afrika (AU), umeitaka Tanzaniakushajiisha masuala ya jinsia katika uchaguzi ujao  ili kutoa ushiriki mzuri kwa wanawake na makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu.

Msaidizi Mkuu, kitengo cha demokrasia na uchaguzi wa AU, Shumbana Karume, aliyasema hayo kwa niaba ya Kamishna wa masuala ya siasa wa umoja huo, Dk. Aisha Abdullai akizungumza hoteli ya Serena wakati akifungua mafunzo ya wiki moja yaliyohusu jinsia na uchaguzi.

Alisema katika kufanikisha uchaguzi huru na wa haki pamoja na ushiriki wa kila mlengwa, AU imeona haja ya kuchagua kipengele cha jinsia kwenye uchaguzi ili kuyafanya masuala ya jinsia kuwa ya kwaida katika harakati za uchaguzi ujao sambamba na kutoa fursa ya ushiki wa kila mmoja hasa wanawake na wenye ulemavu.

Alisema masuala ya  jinsia kwa nchi wanachama wa AU ni mambo yanayopewa kipaumbele na kusisitizwa zaidi na Mwenyekiti wa AU, Dk. Dlamini Zuma, katika karakati za maendeleo hususan kwa wanawake na wenye ulemavu.


Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuujengea uwezo uongozi wa Bodi za uchaguzi Tanzania (EMBs) ili kutekeleza kivitendo uchaguzi ulio huru na wa haki katika kuifikia demokrasia ya kweli.

Aliongeza AU itatoa wataalamu watakaofanya kazi na bodi hizo katika hatua za matayarisho katika kukabiliana na uchaguzi mkuu wa 2015.

Aidha aliuagiza uongozi huo kutoa taafa kwa AU ikiwa watahitaji msaada wa teknolojia na kwamba umoja huo uko tayati kuisaidia Tanzaniakatika kufanikisha chaguzi zake.

Alisema Kamisheni ya Umoja wa Afrika kupitia kitengo cha demokrasia na uchaguzi iko tayari kuisaidia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufanikisha uchaguzi mkuu ujao na kuongeza kuwa mafunzao hayo yatafuatiwa na mengine kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ambapo Tanzania itakuwa nchi ya tatu kunufaika na misaada ya AU kwa mwaka ikitanguliwa na Bukina Faso na Madagascar.

Aidha mataifa kama Guinea, Cameroon, Ivory Coast, Jamuhuri ya Afrika ya Kati na visiwa vya Comoro pia zinatarajiwa kupokea misaada ya kiufundi kutoka AU katika chaguzi zao.

Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujikubalisha kushiriki kikamilifu ili kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni mtiririko wa makubadiliano baina ya Tanzaniana AU katika kuunga mkono juhudi za maandalizi ya uchaguzi ujao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jesha Salum Jecha, alisema uchaguzi ujao 2015 unatarajiwa kutoa ushiriki zaidi kwa watu wenye ulemavu na wanawake ambao kwa kawaida hupata nafasi ndogo na kosesha haki zao za msingi.

Nae mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mwanajuma Zahor Abeid ambae pia ni Katibu Mkuu Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ), alisema anatarajia mafunzo hayo yatawajengea uwezo hasa kwa viongozi wa jumuiya yake na kwamba taaluma hiyo itawafikia walengwa kwa wakati ili kuwapa uwezo wa kupiga kura zaidi.

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa chama cha ADC, Juma Said Sanani, alisema anatarajia vyama vya siasa  vitabadilika baada ya mafunzo hayo.

Mapema Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Salum Kassim Ali, alisema mafunzo yatawasaidia wadau wengi kwenye uchaguzi ujao na kutoa uelewa wa uhuru na haki kwa mpiga kura.

Ufungaji wa Mapembea Pemba Waendelea Kiwanja cha Watoto Kibirizi.

Ziara ya Makamu wa Rais Mkoani Kigoma.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Dini na Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati alipofanya ziara ya siku moja Mkoani humo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa kigoma Mhe. Issa Machibya kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi na Viongozi wa Mkoa wa kigoma kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo.(Picha na OMR)

Dk Shein Amwambia Balozi wa Kisamba Kuimarisha Uhusiano na Russia kwa Kupanua Maeneo Mapya ya Ushirikiano.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF  THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                             15 Julai, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi Mheshimiwa Luteni Generali Wynjones Mathew Kisamba.
Balozi Kisamba alifika Ikulu kujitambulisha na kumuaga Mheshimiwa Rais tayari kutumikia wadhifa wake huo mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Jaka Mwambi ambaye amestaafu.
Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza Balozi Kisamba kuwa uhusiano wa Tanzania na Urusi ni wa miaka mingi na umekuwa wa kirafiki kwa hivyo azma ya Serikali wakati wote ni kuona uhusiano huo unaimarika kwa kupanua maeneo ya ushirikiano hususan biashara, uwekezaji na utalii.
Alimpongeza Balozi Kisamba kwa kuteuliwa katika wadhifa huo na kumshukuru kwa kukubali uteuzi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubainisha kuwa hiyo ni heshma kubwa kwake kuitumikia nchi yake nje ya nchi.
Kwa hiyo alimkumbusha kuitekeleza vyema Sera ya Tanzania ya diplomasia ya uchumi wakati wote akiwa nchini humo na kueleza kuwa hiyo ni nafasi pekee kwa Tanzania kutangaza fursa za kiuchumi kuvutia biashara na uwekezaji.
Dk. Shein alifafanua kuwa hivi sasa Urusi ni moja kati ya mataifa yanayotoa watalii wengi duniani lakini watalii wa nchi hiyo si wengi wanaotembelea Tanzania hivyo ubalozi wa Tanzania nchini humo hauna budi kufanya jitihada kuonesha kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio na kuwafanya raia wa Urus  i kuja Tanzania.  
Kwa upande wa uwekezaji, alieleza kuwa Urusi hivi sasa inafanya vizuri hasa katika ya nishati ikiwemo gesi na mafuta hivyo ipo haja Ubalozi huo kuwahamasisha wawekezaji wa nchi hiyo kuja Tanzania.

Katika mazungumza hayo Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimueleza Balozi Kisamba haja ya kuendeleza jitihada za kupata fursa zaidi za masomo nchini humo kwa vijana wa Tanzania hasa ukizingatia kuwa gharama za masomo bado ni ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine barani ulaya.
Pamoja na kufanya hivyo alisisitiza haja ya Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi ya kuwapatia ushauri wa mara kwa mara wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini humo na nchi inazoziwakilisha, kuishi vizuri na kwa ushirikiano ili waweze kuhitimu masomo yao vyema.
Alimueleza Balozi huyo kuwa ni muhimu wanafunzi hao wakaelimishwa juu ya umuhimu wa kurejea nyumbani mara wamalizapo masomo yao na kuelewa wajibu walionao kushiriki katika ujenzi wa taifa.
 Kuhusu ushirikiano katika sekta ya afya, Dk. Shein alimtaka Balozi kufanya jitihada za kuangalia namna ya kufufua tena ushirikiano wa karibu katika sekta hiyo ikiwemo nafasi za mafunzo kwa watumishi wa afya nchini.
Alibainisha kuwa Taasisi za elimu ya afya za nchi hiyo zina uwezo mkubwa hivyo ni muhimu kwa Tanzania kuwa na ushirikiano wa karibu na nchi hiyo katika sekta hiyo kwa manufaa ya nchi.    
Kwa upande wake Balozi Kisamba alimueleza Mhehimiwa Rais kuwa ni kweli kwamba wako watanzania wengi wanaosoma nchini Urusi katika vyuo mbalimbali na matarajio ni kuwa wanafunzi wengi zaidi wataendelea kwenda nchini humo kwa masomo.
Kwa hivyo alisema ipo haja ya kuimarisha uratibu wa wanafunzi wanaokwenda nchini humo kwa kuwa si wote wanaopitia serikalini bali wengine wanakwenda kupitia mawakala.
Alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumpatia fursa ya kukutana naye na aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yake.          
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 


Kampuni ya Superior Financing Solution LTD,Yakabidhi Tiketi kwa ya Safari ya Kijana Mwanaidi Saleh, kwenda India kwa matibabu.

$
0
0
Meneja Mikopo wa Kampuni ya Superion Finacing Solution Ltd Tawi la Zanzibar Ndg Emmanuel Magazi, kulia akimkabidhi Tiketi ya Mgonjwa Bi Mwanaid Saleh, Msimamizi Madeni wa kampuni hiyo Ndg Khamis Pandu, Kampuni hiyo imechangia Tiketi kwa Bi Mwanaidi kwenda India kwa matibabu zaidi ya majeraha yake ya kuungua kwa moto Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo tawi la Zanzibar Jengo la Zakaria Majestic. 
Msimamizi Madeni wa kampuni hiyo Ndg Khamis Pandu, akimkabidhi tiketi hiyo Mdau wa Blog ya Zanzinews.com Ndg Othman Maulid, akiwa ni mmoja wa msimamizi wa safari hiyo ya Bi. Mwanaid, kwenda India kupata matibabu zaidi ya majeraha ya kuunguwa kwa moto miezi mitano iliopita na kujitokeza Wasamaria wema kutowa michango yao na kufanikisha safari hii ya kwenda katika matibabu.

 Bi Mwanaidi  anatarajiwa kuondoka leo Zanzibar kuelekea India kwa Ndege ya Shirika la Oman Air mchana huu.  

Uhamiaji kubadilisha tena paspoti

$
0
0
Na Mwandishi wetu
IDARA ya  Uhamiaji itabadilisha tena hati za kusafiria kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya yanayofanywa na baadhi ya wananchi.
 Akizungumza kwenye banda la uhamiaji katika viwanja vya maonesho ya 38 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayofanyika  Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa idara hiyo, Tatu Buruhani, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika wananchi wengi wanafanya udanganyifu.
 Alisema, wananchi wengi wamekuwa wakiwatumia mawakala maarufu kama vishoka wa idara hiyo kwa nia ya kupatiwa huduma hiyo kwa haraka na hivyo kuwasababishia wengi wao kutapeliwa ikiwa ni pamoja na kubadilishiwa vyeti vyao.

“Kinachotokea hapa ni kwamba, mwingine anachukua ile pasipoti anakwenda kuweka rehani, mwingine anauza, halafu anakuja kukwambia kwamba imeibiwa. Katika uchunguzi tuliofanya tumebaini kuwa haziibiwi bali wanazitumia vibaya pasipo kutambua umuhimu wake,” alisema.

Alisema utaratibu wa kubadilisha hati za kusafiria ulianza  mwaka 1961 kutokana na changamoto kama na mabadiliko mengine yalifanywa mwaka 1992 na ya mwisho kufanywa ilikuwa mwaka  2005.    

Polisi waanzisha operesheni kusaka wezi wa mazao

$
0
0
Na Tatu Makame
JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, linafanya operesheni ya kukabiliana na wezi wa mazao katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Mkadam Khamis Mkadam, , alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  ofisini kwake Madema.

Alisema lengo la opereshen hiyo ni kuzuia wizi wa mazao ambao huongezeka zaidi katika kipindi kamahiki.

Alisema mazazo kama ndizi,muhogo,majimbi,viazi vikuu ndivyo vinavyoibiwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika kipindi cha Ramadhani, hivyo jeshi la polisi linataka kukomesha wizi huo.


Alisema operesheni hizo zinafanywa katika barabara kuu zinazotumiwa na gari za shamba kupeleka mazao masokonini.


Maeneo ambayo operesheni hiyo itafanywa ni Fuoni, Mwera na barabara nyengine zinazotumiwa kuingiza mazao mijini. 

30bn/- kujenga kiwanda cha sukari Pemba

$
0
0
Na ShemsiaKhamis, Pemba
UJENZI wa mradi mkubwa wa kiwanda cha sukari katika kijiji cha Kiuyu Mbuyuni wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba, utatumia shilingi bilioni 30.

Mkurugenzi wa kampuni ya Talon Sugar Group kutoka India, Dk. Hamza Hussein Sabri,  alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo ambalo mradi huo utajengwa.

Alisema kiwanda hicho cha kisasa kitawanufaisha wananchi wote wa Pemba, ambapo kampuni itawapatia miche ya miwa na pembejeo zote kwa ajili ya kilimo hicho na baadae miwa yao wataiuza kwa kampuni hiyo.

Aidha alisema ujenzi wa mradi huo utaanza Oktoba na na utaanza uzalishaji wa sukari mwaka ujao.

Aidha alisema kiwanda kitatoa fursa za ajira kwa vijana wa Pemba na kusaidia kupunguza pengo la ajira linalowaandamana vijana.


“Kiwanda chetu hakitalima mua,kitakachofanya  ni kuwapa wakulima fursa ya kulima miwa na baadae kiwanda kitanunua miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari,” alisema.

Kwaupande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho,Satish Purandare, alisema kiwanda hicho hakina uhusiano wowote na kiwanda cha sukari Mahonda kilichopo wilaya ya kaskazini B Unguja.

Nae, Ofisa kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA),Ali Shaaban Suleiman, alisema ujio wa wawekezaji hao wataleta faraja kwa wananchi wa Pemba.


Hicho kitakuwa kiwanda cha pili cha sukari Zanzibarkikitanguliwa na kile cha Mahonda na kitakapoanza uzalishaji kitaondoa uagizaji wa sukari kutoka nje.

Makamba awagonganisha wanaCCM

$
0
0
Na Kadama Malunde,Shinyanga
Kauli iliyotolewa na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba,kwamba Tanzania inahitaji rais kijana mwenye fikra mpya katika uchaguzi mkuu ujao, imechafua hali ya hewa ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Makamba alitoa kauli hiyo hivi karibuni nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini, Charles Shigino, alipinga vikali kauli ya Makamba na kusema anataka kuleta siasa za kibaguzi ndani ya chama hicho.

Alisema  CCM inapiga vita ubaguzi wa aina yoyote na kuongeza kuwa  kauli ya Makamba inaweza kuleta hatari kwa mustakabali wa chama na inaweza kuleta nyufa ya mshikamano uliopo.

Aidha alisema Makamba amelenga kuwabagua wazee  na kwamba  fikra zao hazifai na kuongeza kiwa ni  matusi ya kiungwana wanayotukanwa wazee hao na alipaswa kuwaomba radhi.


“Namwomba Makamba atambue kuwa ujana sio kigezo cha kuiongoza jamii ya kitanzania na hasa katika nafasi nyeti ya urais , kisiasa kijana huyu bado ni mdogo ni bora akajifunza kutoka kwa wazee waliokwishawahi kuiongoza  nchi ambao yeye amekuwa akiwadharau,” alisema.

Alimtaka kujipima  kama ana uwezo wa kuongoza nchi kabla ya kutamani kuwaongoza Watanzania.


Alisema alisema CCM ni chama kikongwe chenye wanachama wa kila rika hivyo alipaswa kuwaheshimu badala ya kuwakejeli.

Mwanaidi Safarini India Matibabuni India Leo Mchana Huo.

$
0
0
Tunatoa Shukrani kwa Wananchi Wote waliofanikisha Michango ya Kumchangia Bi Mwanaid Saleh Vuai, ili kuweza kwenda India kwa Matibabu.
Walioko Zanzibar  Tanzania na Ulaya kwa kuweza kufanikisha michango yao. 
Mama wa Mwanaidi akimsaidi Bi Mwanaid walipowasilinUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kwa safari yake ya kwenda India kwa matibabu zaidi, Baada ya kupata misaada kutoka kwa Wananchi mbalimbali wa Zanzibar na Nje ya Zanzibar kufanikisha safari yake. 
Tunatowa shukrani kwa Mwananchi wote waliofanikisha Safari yake kwa michango yao ya kumchangia na hatimai kufikia lengo lililokusudiwa kumpeleka India kwa matibabu.
Shukrani hizi ziwafikie Wananchi wote kwa michango yao kwa njia moja na nyegine ilioweza kufanikisha zoezi hili. Inshala Mwenyezi Mungu atawalipa kwa kila la kheri katika shughuli zenu na kuwaondolewa kila la shari na kuwapa kila la kheri na kuwaepushia na balla.
 Bi Mwanaidi ameondoka mchana huu kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Oman Air mchana saa 3 kuaza safari ya kwenda India .
   



Rais Kikwete Azungumza na Wasanii Nyoka wa Marekani Iluku Dar.

$
0
0
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni   Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka  Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na  Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto)  na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

 

                   Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii Nyota kutoka Nchi Marekeni
Viewing all 36229 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>