Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35995 articles
Browse latest View live

Serikali yaainisha vipengele vyake kwa Serikali

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam hawapo pichani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam wanaonekana mbele katika picha

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na wajumbe wa menejimenti wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na baadhi ya waheshimiwa Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi za Ulaya na Amerika wanaoziwakilisha nchi  zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi za Afrika wanaoziwakilisha nchi  zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi za Mashariki ya Kati wanaoziwakilisha nchi  zao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  wawakilishi wa Mashirika ya Kimatifa  wanaowakilisha mashirika yao hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na  waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi za Asia na Australasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanisha vipaumbele vyake vya mwaka 2023 kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao nchini.

Vipaombele hivyo vimeainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2023.

“Misimamo ya Tanzania ni kuwa hatufungamani na upande wowote lakini pia Tanzania ni muumini wa uendelezaji wa ushirikiano wa kimataifa na kikanda. Tumeelezana vipaumbele vya Serikali hususani utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na kuona ni jinsi gani mabalozi wanaweza kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa manufaa ya pande zote,” alisema Dkt. Tax

Dkt. Tax aliongeza kuwa amesisitiza umuhimu wa maboresho yanayofanywa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ili kuboresha shughuli za kiuchumi, ambapo Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wameridhika na maboresho yanayofanywa na Serikali na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za kipaumbele zaidi ambazo Tanzania imeziainisha.

Kwa upande wake kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed ameishukuru Serikali kwa kuainisha vipaumbele vyake kwa mwaka 2023 na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa inafika malengo yake iliyojiwekea kwa mwaka 2023.

“Kwa niaba ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa, napenda kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wizara na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha inafikia viapombele na malengo yake iliyojiwekea kwa mwaka 2023,” alisema Balozi El Badaoui Mohamed

Mkutano huo ulilenga kufahamiana, kukumbushana na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Tanzania katika masuala ya Diplomasia na mahusiano yake na nchi na taasisi mbalimbali kwa wana jumuiya hao wa kidiplomasia wanaowakilisha hapa nchini.

Mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar viwanja vya Maisara

$
0
0

WANANCHI wakiangalia burudani katika mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar. 
MSANII wa kizazi kipya, Angela Amos (Wike) akitoa burudani wakati wa mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59  ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.
MSANII wa kizazi kipya, Muslih Mmanga (Musloe)akitoa burudani wakati wa mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59  ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar. 
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman akiwa na viongozi wengine katika mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.
MSANII wa kizazi kipya, Rico Single akitoa burudani wakati wa mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59  ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar. 
MSANII wa kizazi kipya, Warid Said (Honey Ella) akitoa burudani wakati wa mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 59  ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar. 

Serikali yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko ya maji Mkoani Mbeya

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akikabidhi Mablanketi  ya Msaada kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko ya Maji Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera (katikati) na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akikitembelea moja ya nyumba ya watu walioathirika na mafuriko ya maji katika kata ya Igawilo Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na mama ambaye ni moja wa waathirika wa mafuriko ya maji katika kata ya Iduda Jijijini Mbeya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na Mkazi wa Kata ya Uyole (kushoto) ambaye ambaye ni mmoja wa waathirika wa mafuriko ya maji .

Na Mwandishi wetu

Serikali Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu imetoa msaada kwa wananchi walioathirika na Maafa ya Mafuriko ya Maji Mkoani Mbeya, yaliyosabisha nyumba kubomoka, kuharibika kwa vifaa, vyakula, uharibifu wa mifugo na mazao yaliyoko mashambani.

“Msaada huo unajumuisha Magodoro 300 kwa kuanzia, mablanketi 1200 ya wakubwa na wadogo, mikeka 600, madumu ya maji, sufuria bakuli sahani pamoja na vijiko kwa kila familia ambayo imeathirika.”

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea maeneo yaliyoathirika wa mafuriko ya mvua katika kata saba Mkoani Mbeya kutokana na Mvua zilizonyesha  terehe 07/01/2023.

“Kwa mujibu wa sheria no. 6 ya Maafa ya Mwaka 2022 sisi kama Ofisi ya Waziri Mkuu tunayo dhamana ya kuwaunganisha wadau ili kuwasaidia watu walioathirika na tutafanya hivyo kwa kutumia Ofisi zetu za Mkoa na wilaya, naomba wadau wote wa ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya kutusaidia ili kuhakikisha watu hawa wanarudi katika hali yao.”

Natoa pole kwa wote walioathirika, TARURA kwa kushirikiana TANROAD Halmashauri ya jiji  la Mbeya na Halmashauri ya Mbeya vijijini wahakikishe wanaenda kuona kwenye vyanzo kuangalia ni eneo gani maji yametoka kwenye mkondo wake wa asili.

Akimkaribisha Waziri wa Nchi, Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameishukuru serikali kwa mchango iliyoutoa kwa  waathirika wa mafuriko ya Mvua Mkoani Mbeya .

“Naomba sisi kama Halmashauri tusitoe vibali vya ujenzi kwenye  maeneo ambayo ni mikondo ya maji, kwa sababu athari za mafuriko zinarudisha nyuma  maendeleo ya uchumi kwa wananchi”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera katika taarifa yake amesema watu waliopata athari za mafuriko ya maji, kaya 281 zenye watu idadi ya watu 1405 ambao wanahitaji chakula takribani tani 50 kwa miezi mitatu ili ziweze kuwasaidia.

Wanawake Zanzibar Watakiwa Kujifunnza Utengenezaji wa Batiki

$
0
0

Na Maulid Yussuf WMJJWW Zanzibar 

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma  amewataka wanawake wa Zanzibar kujifunza juu ya utengenezaji wa mabatiki ili kuweza kujiinua kiuchumi.

Amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya batiki Zanzibar  iliyofanyika katika viwanja vya maonesho Maisara Mjini Unguja.

Amesema wanawake wanapaswa kupewa mafunzo juu ya utengenezaji wa batiki ili kuwawezesha kujikwamua  na kuisaidia Serikali katika kuongeza mapato.

Waziri Pembe amesema ni vyema kupewa ujuzi kwa wwnawake hao ili kuweza kuwaunganisha  na kuwa wamoja kati ya Moro batiki na Zanzibar batiki ili kutengeneze batiki za  kiwango cha hali ya juu na zilizokuwa na ubora sawa.

Aidha Mhe.Riziki ameziomba  Tasisi za Serikali na binafsi  kuweka oda za Batiki wanapokuwa na shughuli zao mbalimbali kwa lengo la kuwaunga mkono wafanya biashara hawo wadogo wadogo na  kuweza kuletea maendeleo.

Nae Katibu  Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda bwana Ali Khamis Juma amesema, soko la batiki kwa Zanzibar ni kubwa kwa wafanya biashara watakao weza kutengeneza batiki.

Amesema wapo wafanya biashara wengi wadogo wadogo wanajiunga na ujasiriamali lakini wengi wao  si wajasiriamali kwani wanakuwa wanafuata mkumbo tu.

Hivyo amewataka wajasiriamali wadogo kujitahidi  kutengeneza mabatiki hayo na kuweza kuuza kwa watalii ili kujiingizia kipato wao wenyewe pamoja  na kuongeza pato kwa Serikali.

Hata hivyo amesema maazimio yaliyofikiwa katika maadhimisho hayo yatasaidia kufikia katika malengo yao waliyojiwekea katika kujikwamua na umasikini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Moro batiki Group Dr Herriet James Mkanga, amewataka wanawake kujishughulisha na ujasiriamali kwa kujiunga na vikundi ili kujikomboa na umasikini.

Amesema lengo lao ni kutoa ajira kwa wanawake na vijana ili kuweza kujikimu mahitaji yao ya kila siku.

Amesema wapo katika kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuitangaza Tanzania katika nchi za Kimataifa.

KVZ Mabingwa Kombe la Mapinduzi Cup 2023 Netiboli Kwa Kuifunga Zimamoto 50-39.

$
0
0

Na Maulid Yussuf WMJJWW  Zanzibar

Timu ya Netball ya kikosi cha KVZ imeibuka kidedea katika Fainali za mashindano ya Netbal  Mapinduzi Cup 2023 ulichozwa katika Viawanja vya Gymkhana, Mjini Unguja hapo jana.

Mchezo huo wa Fainali umeuhusisha timu za Wanawake kutoka Vikosi vya KVZ na Zimamoto, ambapo KVZ imefanikiwa  kuichapa Zimamoto magoli 50 kwa 39.

Mpaka kufikia mzunguuko wa tatu wa mapumziko katika mchezo huo, KVZ ilionekana kuongoza kwa magoli 37 dhidi ya Zimamoto kwa kuwa na magoli 27.

Akizubgumza baada ya kumalizika mchezo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma amewapongeza washindi pamoja na washiriki wote wa mchezo huo wa netball kwa kushiriki mchezo huo kwa mashirikiano mazuri pamoja na nidhamu ya hali ya juu.

Amesema michezo ni Afya, michezo pia inajenga mashirikiano na nidhamu, hivyo amewataka kuendeleza mashirikiano hayo pamoja na nidhamu katika sehemu nyengine, ili kufikia malengo yao.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi Makini wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi umeahidi kuweka kipaumbele katika michezo katika bajeti yake ya 2023-2024, kwa kuendelea kujenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa lengo la kuimarisha michezo hapa nchini.

Hivyo amesema changamoto yao ya ukosefu wa viwanja vya kisasa naamini Dkt Hussein ataitatua, na kuwaonba uwa na uvumilivu katika kufikia malengo hyo.

Pia Mhe Riziki ametumia fursa hiyo, kuwaomba wakuu wa Vikosi hivyo uangalia uwezekano wa  kuwapandisha vyeo wachezaji wake hasa Wanawake, kwani wamekuwa wakiwaletea sifa kubwa vikosi vyao katika michezo.

Nae Katibu wa Chama cha Netball Zanzibar CHANEZA ndugu Said Ali Mansab amesema mashindano hayo kikawaida hufanyika kila mwaka ikiwa lengo ni kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kuwa ni chachu ya kuinua  michezo Zanzibar pamoja na kuinua vipaji vya vijana katika kujipatia ajira kimichezo.

Amesema mashindano hayo  ya Netball Mapinduzi Cup, yalianza tarehe 4 January mwaka 2023 ambapo jumla ya timu saba zilishiriki, ikwemo KVZ, Zimamoto, Bandari, Mafunzo, Afya, Ztalent na timu ya Worious.

Katika mchezo huo wa Fainali,  KVZ ilijinyakulia Kombe la ushindi, fedha taslim shilingi milioni moja, pamoja na medali, huku zimamoto iliyoshika nafasi ya pili ilipata medali na fedha taslim shilingi laki tano na mshindi wa tatu timu ya Bandari ilijinyakulia kombe la nidhamu pamoja na medali.

Michuano ya 17 Kombe la Mapinduzi Cup 2023 Mchezo wa Fainali Kati ya Timu ya Mlandege na Singida Big Star Uwanja wa Amaan Unguja 13-1-2023

Wananchi wa Mkwajuni kuitumia na kuitunza vyema misikiti yao kwa kuendelea kutoa sadaka mara kwa mara ili kuwapa nguvu wasimamizi

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi wa Mkwajuni kuitumia na kuitunza vyema misikiti yao kwa kuendelea kutoa sadaka mara kwa mara ili kuwapa nguvu wasimamizi wa misikiti hiyo.

Al hajj  Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa msikiti wa masjid Istiqama, uliopo Mkwajuni njia ya Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema licha ya uzuri wa misikiti na uimara wake lakini itafikia hatua misikiti itahitaji ukarabati, huduma za maji na umeme ambavyo vyote vinahitaji usimamizi mzuri na gharama za kuhudimiwa, hivyo aliwaasa wananchi na waumini wa Kiislamu kutoa sadaka ambazo zitasaidia gharama za uendeshaji pamoja na kuwalipa wasimamizi wa misikiti hiyo

Aidha, aliwaasa waumini hao kuitumia misikiti hiyo kwa sala na ibada nyengine pamoja na kumshukuru mfadhili wa msikiti huo.

Akihutubu kwenye sala ya Ijumaa msikitini hapo, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Khalid Ali Mfaume alizungumzia fadhila za sadaka kwa muumini mwenye kuitoa na kueleza kuwa sadaka humuweka mtu huru kwa Mola wake.

Aidha, aliongeza sadaka kuleta tahfifu na shifai kwa muumini mgonjwa na kueleza kwamba swadaka huwa sababu ya mja kusamehewa makosa yake kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo aliwanasihi waumini hao kushajihika na kuendelea kutoa sana sadaka misikitini mwao.

Mapema, akisoma risala ya ufunguzi wa msikiti huo, Ustadhi Maulid Nafasi Juma alisema ujenzi wa msikiti huo ulitokana na uhitaji wa waumini wa eneo hilo ambao kwa mda mrefu walitumia msikiti mdogo uliokua haukidhi haja ya mahitaji ya eneo hilo.

Ustadhi Nafasi alieleza awali walikua na msikiti uliojengwa tokea mwaka 1983 lakini kutokana na changamoto kadhaa walizokumbana nazo ikiwemo kuongezeka kwa waumini kutokana na kutanuka kwa vijiji kwenye eneo lao, ndio iliwalazimu kutafuta mfadhali kwaajili ya ujenzo mpya hadi kufunguliwa kwake mwaka huu.

IDARA YAMAWASILIANO,

IKULU

Tangazo la Utumiaji wa Soko la Samaki Malindi Unguja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.

Uzinduzi wa Baraza la Chuo Cha KIST Zanzibar .

$
0
0

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Lela Mohamed Mussa akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Baraza la tatu – kipindi cha Pili la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), na kuwaaga Wajumbe waliomaliza muda wao, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mkutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija katika Taasisi hiyo Mbweni Zanzibar.

PICHA NA MARYAM KIDIKO- KIST.

Vijana wa Kitanzania Kupata Fursa Marekani

$
0
0

Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul leo Januari 13, 2022 jijini Dar es Salam, ameongoza kikao kati ya Wizara hiyo na Wadau wa Diaspora kutoka nchini Marekani kupitia NGO ya Global Youth Support Center, kujadili nia ya NGO hiyo kupata vijana wa kitanzania wa umri kati ya Miaka 14 hadi 15 wenye vipaji mbalimbali vya Michezo na Sanaa kwa lengo la kwenda nchini Marekani kuendeleza vipaji vyao.

Katika kikao hicho, Naibu Waziri Mhe.Gekul amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora kwa wadau wa Sekta za Wizara hiyo kuwekeza kwa vijana wenye vipaji, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuongeza elimu itakayowasaidia katika kukuza uchumi wao na jamii.

"Hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wetu, Wizara yetu ipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu kwa Taasisi hii ili vijana wa Kitanzania waweze kunufaika na mpango huu wa kuendeleza vipaji” amesisitiza Mhe. Gekul.

Mratibu wa programu hiyo Bw. Oswald Bwechwa ameeleza kuwa, vijana takribani 40 watapata fursa ya kwenda nchini Marekani katika awamu ya kwanza ya programu hiyo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa na la Taifa Dkt, Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Neema Msitha na Waziri na Mbunge wa zamani nchini Kepten Mstaafu John Chiligati.

Rais Dk Hussein Mwinyi aufungua rasmi Masjid Istiqaamah Mkwajuni

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Mfadhili wa Ujenzi wa Masjid Istiqama Bw.Suleiman Mohamed Yahya mara alipowasili na kufungua Msikiti huo leo,uliojengwa  Mkwajuni  Mkoa wa Kaskazini Unguja.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa nne kulia) akifungua pazia kama ishara ya Uzinduzi wa Masjid Istiqama leo,Msikiti   uliojengwa  Mkwajuni  Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa  Bw.Suleiman Mohamed Yahya (wa nne kushoto)  katika sherehe iliyofanyika sambamba na    Swala ya Ijumaa .[Picha na Ikulu] 13/01/2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (kushoto) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati waliokaa mbele) kuzungumza na Waumini baada ya kiufungua Masjid Istiqama,Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja hafla iliyokwenda sambamba  na Swala ya Ijumaa leo.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Suleiman Mohamed Yahya akiwa Mfadhili wa Ujenzi wa Masjid Istiqama katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja,ambapo ujenzi wake umefanyika kwa kushirikiana na Nguvu za Wananchi na Mfadhili huyo.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.

Waumini wa Dini ya Kiislamu walioswali Swala ya Ijumaa sambamba na Ufunguzi wa Masjid Istiqama,Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo mara baada  Ufunguzi wa Masjid hiyo leo.[Picha na Ikulu] 13/01/2023. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake leo mara baada ya Swala ya Ijumaa sambamba na Ufunguzi wa Masjid Istiqama  katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja,ambapo ujenzi wake ulifanyika kwa ufadhili wa Sheikh,Suleiman Mohamed Yahya na Nguvu za Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  (katikati) pamoja na Viongozi wengine na Waumini wakiitikia dua iliyosomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kushoto)baada ya hafla ya  Swala ya Ijumaa sambamba na Ufunguzi wa Masjid Istiqama  katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.[Picha na Ikulu] 13/01/2023.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kulia) alipokuwa kimpongeza Ramadhan Omar Mcha Wanamadrasa waliokuwa wakisoma Qaswida kwa Kumshindikiza Rais baada ya hafla ya   Ufunguzi wa Masjid Istiqama  katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, hafla iliyofanyika leo ambapo Viongozi mbali mbali na Waumini walihudhuria katika sherehe hiyo. [Picha na Ikulu] 13/01/2023.

Mhe Hemed ajumuika na waumini wa Msikiti wa Bweleo katika Ibada ya Sala ya Ijumaa

$
0
0

 Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kutenga muda kwa ajili ya Kusoma Dini ili kujenga jamii iliyo njema.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipojumuika na Waumini wa Msikiti wa Bweleo Wilaya ya Magharibi B katika Ibada ya Sala ya Ijumaa. 

Amesema kuwepo kwa matendo maovu katika Jamii kunatokana na kukosa elimu ya Dini na Malezi ambapo jukumu la wazazi kuhimizana kuisoma Dini hatua ambayo jamii itafahamu mambo mema kuyafata na maovu kuyawacha.

Amesema Elimu ni jambo la muhimu ambapo ni vyema kwa waumini kutumia Misikiti kwa kuendeleza masuala ya Dini pamoja na kujadiliana masuala mbali mbali ya kijamii.

Aidha ameeleza kuwa Jamii inaposhikamana na Dini inakuwa na nafasi ya kumuabudu Mungu ipasavyo jambo ambalo litasaidia kupata kizazi inayomtambua Mungu na kusimamia maadili mema.

Mhe. Hemed amewasisitiza Waumini hao kuwa na umoja na mshikamano kwa kusaidiana katika masuala mbali mbali ili kuiweka jamii pamoja na yenye upendo.

Akitoa Khutba ya Sala ya Ijumaa Maalim Mussa Ali Kirobo amewataka Waumini hao kusimamia maadili mema hasa kukemea matendo maovu yaliyokithiri na kuwataka kurudi katika mafundisho ya Dini ili kupata kizazi kilicho chema.

Amesema Zanzibar kwa miaka ya nyuma ilisifika kwa kuwepo wasomi waliobobea katika Dini ambao walikuwa tegemezi kwa nchi za Afrika Mashariki na Falme za Kiarabu.

………………….

Abdulrahim Khamis

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Mabalozi pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2023 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika Sherehe za Mwaka Mpya (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2023 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax, viongozi wengine katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Sherehe za Mwaka Mpya 2023 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa walioshiriki katika Sherehe za Mwaka Mpya 2023 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Januari, 2023.

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi katika mchezo wa fainali Kombe la Mapinduzi kati ya Mlandege na Singida Big Boys

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha Timu ya Mlandege kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, mchezo uliofanyika jana usiku 13-1-2023 katika Uwanja wa Amaan Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha Timu ya Singida Big Stars,kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, mchezo uliofanyika jana usiku 13-1-2023 katika Uwanja wa Amaan Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Kocha Mkuu wa Timu ya Singida Big Stars Hans Pluijm kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, dhidi ya Timu ya Mlandege mchezo uliofanyika jana usiku 13-1-2023, katika uwanja wa Amaan.Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)
KIKOSI cha Timu ya Mlandege Mabingwa wa Timu ya Mapinduzi Cup 2023.mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja Wilaya ya Mjini.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Timu mbalimbali zilizoshirika michuano ya 17 ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, wakati wa mchezo wa Fainali kati ya Mlandege na Singida Big Stars mchezo uliofanyika jana usiku 13-1-2023 uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja.Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)
WACHEZAJI wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la pili dhidi ya Timu ya Singida Big Stars, katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatili mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja.Timu ya Mlandege imeshinda kwa bao 2-1, na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Singida Big Stars akiwapita mabeki wa Timu ya Mlandege wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, mchezo uliyofanyika katika uwanja wa Amaan.Timu ya Mlandege imeshinda mchezo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)

WAPENZI wa Timu ya Mlandege wakishangilia Timu yao baada ya kushinda bao la pili wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 13-1-2023.Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi mbalimbali wakishangilia Timu ya Mlandege baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali, kati ya Timu ya Mlandege na Singida Big Stars, uliofanyika jana usiku 13-1-2023, katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja.Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Kipa Bora wa Michuano ya 17 ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023,kutoka Timu ya Mlandege. Yussuf Abdul Ali, baada ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amani dhidi ya Timu ya Singida Big Stars, mchezo iliofanyika jana usiku 13-2023 katika uwanja wa amaan Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakishuhudia Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita akimkabidhi zawadi Mfungaji Bora wa Michuano ya 17 Kombe la Mapinduzi Cup 2023 kutoka Timu ya Singida Big Stares. Fancy Kazadi,baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup, kati ya Mlandege na Singida uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha Medali ya Dhahabu Mchezaji wa Timu ya Mlandege Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup 2023, baada ya kuifunga Timu ya Singida Big Stars katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku13-1-2023. Kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu)

WACHEZAJI wa Timu ya Mlandege wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi Cup 2023. Baada ya kuifunga Timu ya Singida Big Stars kwa mabao 2-1.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup 2023, Timu ya Mlandege baada ya kuwakabidhi Kombe la Ubingwa baada ya kuifunga Timu ya Singida Big Stars katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 13-1-2023,Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1.(Picha na Ikulu) 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mhe Samia aongoza Kikao cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa mwaka 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

$
0
0

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  wakiwa katika Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023. 
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipiga makofi wakati wa kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan kuongoza Kikao cha kwanza cha Kamati Kuu Mpya ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akisisitza jambo wakati alipokuwa akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati Kuu Mpya ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa katika Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.
 
Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji (Joint Investment Fund) kati ya Tanzania na Oman kuanzishwa

$
0
0

 Tanzania kwa kushirikiana na Oman zinatarajia kuanzisha Mfuko wa Pamoja wa Uwekezaji (Joint Investment Fund) mwaka huu (2023). Mfuko huo pamoja na mambo mengine, unategemewa kunufaisha sekta za uvuvi, kilimo na madini.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha pamoja kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema kuanzishwa kwa mfuko huo wa pamoja wa uwekezaji ni utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wakuu na kuongeza kuwa uanzishwaji wake utasaidia kuinua uchumi wa mataifa yote mawili. “kuanzishwa kwa mfuko huu ni utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wetu wakuu ambapo Hati ya Makubaliano (MoU) ya kuanzishwa kwa mfuko huo ilisainiwa mwezi Juni mwaka 2022 kwa lengo la kuinua uchumi wa pande zote mbili na kwa maslahi mapana,” alisema balozi Mbarouk.

Mkataba huo ulisainiwa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi nchini Oman mwaka 2022.

Kwa upande wake, Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan amesema kwa sasa hatua zote zimekamilika na mwaka huu 2023 mfuko huo unategemea kuanzishwa rasmi na kusaidia kuinua biashara na uwekezaji kwa maslahi ya mataifa yote mawili. “mfuko huu utaanza rasmi mwaka huu 2023 na tunategemea uwasaidie kuichumi wafanyabishara na wawekezaji wa mataifa yetu mawili,” alisema Balozi Al Shidhan

Mwezi Juni mwaka 2022, Tanzania na Oman zilisaini Hati sita za Makubaliano katika sekta za nishati, utalii, maliasili, elimu ya juu, mafunzo ya ufundi stadi na makumbusho. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na  Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan

Alhajj Dk.Hussein Amewataka Wananchi wa Mkwajuni kuitumia na kuitunza vyema misikiti yao kwa kuendelea kutoa sadaka mara kwa mara

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi wa Mkwajuni kuitumia na kuitunza vyema misikiti yao kwa kuendelea kutoa sadaka mara kwa mara ili kuwapa nguvu wasimamizi wa misikiti hiyo.

Al hajj  Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa msikiti wa masjid Istiqama, uliopo Mkwajuni njia ya Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema licha ya uzuri wa misikiti na uimara wake lakini itafikia hatua misikiti itahitaji ukarabati, huduma za maji na umeme ambavyo vyote vinahitaji usimamizi mzuri na gharama za kuhudimiwa, hivyo aliwaasa wananchi na waumini wa Kiislamu kutoa sadaka ambazo zitasaidia gharama za uendeshaji pamoja na kuwalipa wasimamizi wa misikiti hiyo

Aidha, aliwaasa waumini hao kuitumia misikiti hiyo kwa sala na ibada nyengine pamoja na kumshukuru mfadhili wa msikiti huo.

Akihutubu kwenye sala ya Ijumaa msikitini hapo, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Khalid Ali Mfaume alizungumzia fadhila za sadaka kwa muumini mwenye kuitoa na kueleza kuwa sadaka humuweka mtu huru kwa Mola wake.

Aidha, aliongeza sadaka kuleta tahfifu na shifai kwa muumini mgonjwa na kueleza kwamba swadaka huwa sababu ya mja kusamehewa makosa yake kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo aliwanasihi waumini hao kushajihika na kuendelea kutoa sana sadaka misikitini mwao.

Mapema, akisoma risala ya ufunguzi wa msikiti huo, Ustadhi Maulid Nafasi Juma alisema ujenzi wa msikiti huo ulitokana na uhitaji wa waumini wa eneo hilo ambao kwa mda mrefu walitumia msikiti mdogo uliokua haukidhi haja ya mahitaji ya eneo hilo.

Ustadhi Nafasi alieleza awali walikua na msikiti uliojengwa tokea mwaka 1983 lakini kutokana na changamoto kadhaa walizokumbana nazo ikiwemo kuongezeka kwa waumini kutokana na kutanuka kwa vijiji kwenye eneo lao, ndio iliwalazimu kutafuta mfadhali kwaajili ya ujenzo mpya hadi kufunguliwa kwake mwaka huu.

IDARA YAMAWASILIANO,

IKULU.

Waziri Mhe.Aweso Atua Tanga Kufuatilia Tatizo la Maji Maelekezo kwa Tanga Uwasa,Bonde la Mto Pangani

$
0
0

Waziri wa maji Jumaa Aweso  akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi.

Na Oscar Assenga,Tanga                                                                                                            
Waziri wa maji Jumaa Aweso amelazimika kutua Mkoani Tanga kwa ajili ya kufuatilia uwepo wa changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji huku akiitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) kuhakikisha taarifa zinatolewa kwa wakati kwa wananchi inapojitokeza hitilafu ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu ili kuondoka malalamiko kwao.

Sambamba na hayo aliagiza Bonde la Maji la Mto Pangani kufanya ufuatiliaji kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vya watu kufanya shughuli zao

Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wananchi kufuatia changamoto ya ukosefu wake kwa baadhi ya wananchi kwa siku nne mfufulizo chanzo kikitajwa ni uchafuzi wa mazingira uliofanywa na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji vya Mto Zigi hali iliyopelekea maji kuwa katika hali ya uchafu usio kawaida na hivyo kuifanya mamalaka hiyo kusitisha huduma kwa wananchi ili kutatua changamoto hiyo.

Waziri Aweso alisema jukumu la utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa jiji la Tanga ni la Tanga Uwasa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni kwa nini wananchi walipata huduma ya maji isiyo ya kawaida baada ya kuona maji katika hali ile waliamua kuzima mitambo kwahiyo kelele za watu kukosa maji yaliyokuwa yanapatikana zilileta taharuki pamoja na changamoto iliyojitokeza watu wa maabara na wataalamu wameweza kuyatibu na sasa hivi yapo katika hali yake na tumepita kwa wananchi baadhi ya nyumba maji yapo.

Alisema kubwa ambalo alitaka kusisisitiza kwao ni kwamba inapotokea changamoto kukosekana kwa maji sio jambo baya lazima watoe taarifa kwa wakati na hivyo kutokuitoa kunapelekea tahatuki kwa wananchi hivyo jambo hilo waangalie na lisiitokeze tena .

“Lakini Tanga Uwasa utoaji wa huduma ya majisafi na salama ni wajibu na majukumu ya mamlaka yenu kwahiyo lazima mjipange kuhakikisha mnatoa huduma ya maji safi na salama wakati wote “Alisema Waziri Aweso

“Ndugu zangu maji hayana mbadala lakini pamoja na kurejea huduma hii lazima iundwe timu maalum ya kupita kila mtaa kuona huduma ya maji inarejea kama kawaida yake nina imani hili jambo haliwezi kutokea tena"

Aidha waziri Aweso ameitaka bodi ya mamlaka hiyo kukaa na kujadili namna watakavyoweza kupambana na kutatua changamoto zinazopelekea kukosekana kwa maji akiitaka pia kufanya kikao cha pamoja na madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwaeleza hali halisi ya utekelezaji wake hii ikilenga hasa kuweka wazi taarifa za kiutendaji zitakazosaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Akieleza changamoto iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa siku kadhaa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa Geofrey Hilly alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo uchimbaji wa madini katika chanzo kibwa cha Mto Zigi kinachotegemewa na mamlaka hiyo hali iliyopelekea kuchafuka kwa maji.

"Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa maji tangu mwezi wa 10 mwaka 2022 changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa umeme katika maeneo yetu ya kuzalisha maji lakini hivi karibuni ikatokea changamoto ya kuchafuka sana kwa maji na imetokana na hali ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo chetu kikubwa cha mto Zigi na hata usafishaji wake ulikuwa ni wa hali ngumu kwahiyo tukazima kwanza maji yasije tuyatibu na tumefanikiwa na hivyo tayari maji yameshaanza kutoka kwa baadhi ya maeneo"

Hilly alisema kuwa Mamlaka hiyo ipo mbioni kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara ambapo wamejipanga kununua mitambo maalumu ya kudhibiti changamoto ya kupungua kwa umeme , kupatikana kwa mradi mkubwa wa kujenga tanki la kuhifadhia maji ambapo hata itakapotokea changamoto ya umeme bado maji yatakuwa yanapatikana kwa uhakika.

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule amekiri uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji licha ya jitihada wananzozifanya akiahidi kupokea na kwenda kutekeleza maagizo ya waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Alisema bonde hilo ndio lenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wenzao wanaochukuwa maji kwenye vyanzo yana kuwa kwenye ubora stahiki hivyo wamezingatia maelekezo ya viongozi na wameshajipanga kutekeleza na wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani serikali za wilaya na mikoa.

Akizungumza Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameipongeza Tanga Uwasa kwa jitihada za haraka ilizozifanya kutatua changamoto ya kuchafuka kwa maji hali iliyoleta kwa wakazi wa jiji la Tanga kwa siku nne mfululizo huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo.

Akizungumza mmoja wa madiwani wa Jiji la Tanga Salimu Perembo ameishauri mamlaka hiyo kupanua huduma zake kwa upande wa majitaka hii ikienda sambamba na ongezeko la wananchi na makazi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira inazihudumia wilaya za Tanga Pangani pamoja na Muheza ikiwa inazalisha lita zaidi ya 30 za maji kwa siku ambapo sasa inatekeleza mradi unaogharimu shilingi Billion 9.18 ambao mara baada ya kukamilika utaiwezesha Tanga uwasa kuwa na uhakika maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi. 
Waziri wa maji Jumaa Aweso  akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi 
Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule  akizungumza wakati wa ziara hiyo
KATIBU wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akieleza hatua walizochukua kuondosha changamoto hiyo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika mwenye kofia akikagua maji katika mtambo wa kusafishia maji wa Mowe Jijini Tanga wakati wa ziara yake 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa kwenye mtaa wa Chumbageni Jijini Tanga akikagua upatikanaji wa maji kwa wananchi wakati wa ziara yake.

Na Oscar Assenga,Tanga                                                                                                            
Waziri wa maji Jumaa Aweso amelazimika kutua Mkoani Tanga kwa ajili ya kufuatilia uwepo wa changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji huku akiitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) kuhakikisha taarifa zinatolewa kwa wakati kwa wananchi inapojitokeza hitilafu ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu ili kuondoka malalamiko kwao.

Sambamba na hayo aliagiza Bonde la Maji la Mto Pangani kufanya ufuatiliaji kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vya watu kufanya shughuli zao

Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wananchi kufuatia changamoto ya ukosefu wake kwa baadhi ya wananchi kwa siku nne mfufulizo chanzo kikitajwa ni uchafuzi wa mazingira uliofanywa na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji vya Mto Zigi hali iliyopelekea maji kuwa katika hali ya uchafu usio kawaida na hivyo kuifanya mamalaka hiyo kusitisha huduma kwa wananchi ili kutatua changamoto hiyo.

Waziri Aweso alisema jukumu la utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa jiji la Tanga ni la Tanga Uwasa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni kwa nini wananchi walipata huduma ya maji isiyo ya kawaida baada ya kuona maji katika hali ile waliamua kuzima mitambo kwahiyo kelele za watu kukosa maji yaliyokuwa yanapatikana zilileta taharuki pamoja na changamoto iliyojitokeza watu wa maabara na wataalamu wameweza kuyatibu na sasa hivi yapo katika hali yake na tumepita kwa wananchi baadhi ya nyumba maji yapo.

Alisema kubwa ambalo alitaka kusisisitiza kwao ni kwamba inapotokea changamoto kukosekana kwa maji sio jambo baya lazima watoe taarifa kwa wakati na hivyo kutokuitoa kunapelekea tahatuki kwa wananchi hivyo jambo hilo waangalie na lisiitokeze tena .

“Lakini Tanga Uwasa utoaji wa huduma ya majisafi na salama ni wajibu na majukumu ya mamlaka yenu kwahiyo lazima mjipange kuhakikisha mnatoa huduma ya maji safi na salama wakati wote “Alisema Waziri Aweso

“Ndugu zangu maji hayana mbadala lakini pamoja na kurejea huduma hii lazima iundwe timu maalum ya kupita kila mtaa kuona huduma ya maji inarejea kama kawaida yake nina imani hili jambo haliwezi kutokea tena"

Aidha waziri Aweso ameitaka bodi ya mamlaka hiyo kukaa na kujadili namna watakavyoweza kupambana na kutatua changamoto zinazopelekea kukosekana kwa maji akiitaka pia kufanya kikao cha pamoja na madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwaeleza hali halisi ya utekelezaji wake hii ikilenga hasa kuweka wazi taarifa za kiutendaji zitakazosaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Akieleza changamoto iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa siku kadhaa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa Geofrey Hilly alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo uchimbaji wa madini katika chanzo kibwa cha Mto Zigi kinachotegemewa na mamlaka hiyo hali iliyopelekea kuchafuka kwa maji.

"Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa maji tangu mwezi wa 10 mwaka 2022 changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa umeme katika maeneo yetu ya kuzalisha maji lakini hivi karibuni ikatokea changamoto ya kuchafuka sana kwa maji na imetokana na hali ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo chetu kikubwa cha mto Zigi na hata usafishaji wake ulikuwa ni wa hali ngumu kwahiyo tukazima kwanza maji yasije tuyatibu na tumefanikiwa na hivyo tayari maji yameshaanza kutoka kwa baadhi ya maeneo"

Hilly alisema kuwa Mamlaka hiyo ipo mbioni kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara ambapo wamejipanga kununua mitambo maalumu ya kudhibiti changamoto ya kupungua kwa umeme , kupatikana kwa mradi mkubwa wa kujenga tanki la kuhifadhia maji ambapo hata itakapotokea changamoto ya umeme bado maji yatakuwa yanapatikana kwa uhakika.

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule amekiri uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji licha ya jitihada wananzozifanya akiahidi kupokea na kwenda kutekeleza maagizo ya waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Alisema bonde hilo ndio lenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wenzao wanaochukuwa maji kwenye vyanzo yana kuwa kwenye ubora stahiki hivyo wamezingatia maelekezo ya viongozi na wameshajipanga kutekeleza na wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani serikali za wilaya na mikoa.

Akizungumza Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameipongeza Tanga Uwasa kwa jitihada za haraka ilizozifanya kutatua changamoto ya kuchafuka kwa maji hali iliyoleta kwa wakazi wa jiji la Tanga kwa siku nne mfululizo huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo.

Akizungumza mmoja wa madiwani wa Jiji la Tanga Salimu Perembo ameishauri mamlaka hiyo kupanua huduma zake kwa upande wa majitaka hii ikienda sambamba na ongezeko la wananchi na makazi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira inazihudumia wilaya za Tanga Pangani pamoja na Muheza ikiwa inazalisha lita zaidi ya 30 za maji kwa siku ambapo sasa inatekeleza mradi unaogharimu shilingi Billion 9.18 ambao mara baada ya kukamilika utaiwezesha Tanga uwasa kuwa na uhakika maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi.

Uongozi wa Bajaji Iringa Wapinga Vikali Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia

$
0
0

Mwenyekiti wa madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele akiwa katika ya madereva Bajaji wa Manispaa ya Iringa alipowatembelea katika vituo vya Bajaji kutoa elimu ya kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Na.Fredy Mgunda, Iringa.
MWENYEKITI wa chama cha madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele amewataka madereva Bajaji kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa abiria ambao wanawapakia.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vituo vya Bajaji Manispaa ya Iringa, mwenyekiti huyu Melabu Kihwele alisema kuwa uongozi wa Bajaji Manispaa ya Iringa hautamvumilia Dereva Bajaji yoyote yule ambaye anafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kihwele alisema kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupinga vikali vitendo vya ukatili kwa Watoto na wanawake ambavyo kwa siku za hivi karibu vimezidi kuongezeka.

Alisema kuwa Dereva Bajaji yoyote atakaye baka au kulawiti hawatamfumbia macho kwa kuharibu taswira ya madereva Bajaji Manispaa ya Iringa.

Kihwele alisema kuwa kubaka, kulawiti na kuaafanyia ukatili wanawake hukumu take ni kifungo cha miaka 30 jela hivyo madereva Bajaji Manispaa ya Iringa wanatakiwa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Hivi karibuni si kuna Dereva Bajaji wa hapa Manispaa ya Iringa amefungwa miaka 30 jera kwa kosa la ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike si ndio hivyo serikali ikitaka ushirikiano na uongozi wa Bajaji Manispaa ya Iringa sisi tupo tayari"alisema Kihwele

Mwenyekiti wa madereva Bajaji Manispaa ya Iringa Melabu Kihwele alimazia kwa kusema kuwa jamii ya watanzania hawajazoea vitendo vya ukatili wa kijinsia kufanywa na madereva Bajaji hivyo Dereva Bajaji yoyote atakaye kutwa na tuhuma au kesi hiyo uongozi hauwezi kumsaidia.
Viewing all 35995 articles
Browse latest View live

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>