Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36137 articles
Browse latest View live

Serikali na Washirika wa Maendeleo Wateta Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya, wa pili kulia ni Balozi wa Uingereza na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. David Concar, na kulia ni Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas, aliyekuwa akitoa mada.

Baadhi ya Wajumbe kutoka Jumuiya ya Kimataifa na Tanzania, wakifuatilia majadiliano wakati wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM-Dar es Salaam

Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo wamefanya majadiliano ya uboreshaji mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini illi kuwavutia wawekezaji.

Hayo yamelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa ngazi ya juu wa Majadiliano ya kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali imesema itaendelea kuwekeza nguvu kwenye maeneo yanayohitaji uwezeshwaji fedha kama vile kilimo, uvuvi na mifugo ili kukuza uchumi, ajira na maendeleo ya jamii.

 

Aidha, alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi na kutoa wito kwa wawekezaji wote kuja kuwekeza nchini na kutumia fursa zilizopo kupata faida yao na nchi kwa ujumla.

 

“Miaka  kadhaa iliyopita kulikuwa na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu utitiri wa kodi, Rais Samia alipoingia madarakani alifuta tozo na kodi zaidi ya 114,  katika sekta za uzalishaji,”, alisema Dkt. Nchemba.

 

Alisema moja ya hatua ambazo Serikali ya Awamu ya Sita pia imechukua ni kurekebisha sheria za kikodi na sheria za uwekezaji ili kuwepo na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara nchini.

 

Dkt. Nchemba alisema kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo kumewezesha ufanisi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Washirika hao wa Maendeleo wamekuwa wakiifadhili.

 

“Tulisaini makubalinao kwenye ziara ya Rais Samia nchini China kuhusu samaki, parachichi, kwenye ziara yake ya Ulaya makubaliano yalisainiwa katika masuala ya nafaka ambapo mchele wa Tanzania unauzwa mpaka Ubelgiji, pia tulisaini na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na nchi nyingine zinazotuzunguka,”alisema Dkt. Mwigulu.

 

Kuhusu uzalishaji katika kilimo, mifugo na uvuvi, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 mchango wa sekta hizo uwe umezidi asilimia 10 ili Pato la Taifa linapopanda na pato la mtu mmoja mmoja nalo lipande.

 

Alisema mpaka sasa vijana zaidi ya 27,000 wamejiandikisha kwa ajili ya kutaka kwenda kuwekeza kwenye mashamba maalumu ambayo serikali imepanga vijana wawekeze.

 

NayeWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya, alisema pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi na namna bora ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na kuishirikisha Sekta Binafsi.

Dkt. Mkuya aliongeza kuwa katika majadiliano hayo walisistiza suala la utunzaji mazingira ambayo yatawezesha kufanya kilimo endelevu kwa ajili ya utunzaji mazingira na upatikanaji wa chakula.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe Balozi wa Uingereza David Concar, alisema washirika wa maendeleo wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuhakikisha uchumi wan chi na wananchi unaongezeka.

Alisema washirika wa maendeleo pia wanaipongeza Serikali kwa kuwa na uongozi bora unao zingatia haki za binadamu pamoja na jitihada mbalimbali inazochukua kuboresha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kusimamia vizuri uchumi wa nchi.

Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha Mawaziri, Mabalozi, Makatibu Wakuu, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Viongozi Mbalimbali wa Serikali.

Mwisho


Tanzania Mwenyekiti wa Sekta ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika Jumuiya ya Nchi za Afrika,Karibiani na Pasifiki

$
0
0

Dodoma, 15 Februari 2023

Tanzania imekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Sekta ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) kwenye hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo yaliyopo jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 13 Februari 2023.

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, kwenye Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya OACPS, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga alikabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Sekta hiyo kwa ngazi ya mabalozi na Balozi wa Ghana nchini Ubelgiji, Mhe. Harriet Sena Siaw-Boateng ambaye nchi yake imemaliza muda wa uenyekiti.

Uamuzi wa Tanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa sekta hiyo ulifikiwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa OACPS uliofanyika Brussels, Ubelgiji, Mwezi Juni 2022. Uenyekiti wa Tanzania utakuwa kwa ngazi mbili ambazo ni za Mabalozi wa Jumuiya waliopo Brussels na Mawaziri wenye dhamana ya sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu ndani ya Jumuiya na utadumu kwa miaka miwili hadi Februari 2025.

Tanzania katika kipindi cha uongozi wake imejipanga kikamilifu kusimamia utekelezaji wa masuala mbalimbali katika Jumuiya ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati madhubuti na mazingira ya kuwezesha wananchi kupitia nchi zao kunufaika ipasavyo na uchumi wa buluu ikiwemo uvuvi na rasilimali zingine za majini; kuchochea uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu; kujenga uwezo na matumizi bora ya sayansi na teknolojia; kuongeza wigo wa masoko kwa bidhaa zitokanazo na uvuvi na uchumi wa buluu; kupambana na uvuvi haramu; na kuendeleza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, katika kipindi husika, Tanzania itakuwa na jukumu la kuandaa  Mkutano wa Mawaziri wa OACPS wenye dhamana ya masuala ya Uvuvi ambao unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania mwaka 2024.

Miongoni mwa sababu zilizopelekea Tanzania kuchaguliwa katika nafasi hiyo ni kutokana na kuongozeka kwa ushawishi wake ndani ya Jumuiya ya OACPS na kuthamini utayari, dhamira na hatua thabiti zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuchochea na kusimamia masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo yale yanayohusu sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu kwa ujumla.

                                                      Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.     

 

Tukague Utekelezaji wa Miradi - MAJALIWA *Lengo ni kujiridhisha kama inalingana na kiasi cha fedha kilichotolewa

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi ya mkoa huo, Februari 15, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, hivyo ni jukumu la viongozi kuikagua na kujiridhisha kama utekelezaji wake unafanyika kwa viwango vilivyokusudiwa na unalingana na thamani halisi ya fedha iliyotolewa.

Ameyasema hayo jana (Jumanne, Februari 14, 2023) wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Kakozi wilayani Momba akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili.

Akiwa katika kijiji hicho kabla ya kuzungumza na wananchi, alikagua ujenzi wa mradi wa kimkakati wa soko la Kimataifa la mazao ya kilimo na mifugo pamoja na maghala sita ambapo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikia na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 8.6 unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, pia unahusisha ujenzi wa mnada wa kuuzia mifugo, josho, kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na hivyo kuwezesha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma za jamii.

Kwa upande wake, Mbunge wa Momba Condester Sichalwe alitumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha nyingi kupelekwa jimboni kwake katika kipindi cha miaka miwili kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo zikiwemo shilingi bilioni 7.8 zinazojenga miradi ya maji.

Mbali na mafanikio hayo mbunge huyo ameiomba Serikali ikamilishe usambazaji wa umeme vijijini pamoja na ujenzi wa hosteli katika shule za sekondari, ambapo Waziri Mkuu alimueleza kuwa vijiji 22 kati ya 72 vitapatiwa umeme kwani Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania ikipata umeme.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi katika Mji wa Tunduma ambapo aliwaeleza kuwa Serikali itaendelea kuwapelekea miradi ya maendeleo kulingana na mahitaji yao, pia alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji huo kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.

Naye, Mbunge wa Tunduma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, David Silinde aliipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kufanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 11 kwenye jimbo hilo katika kipindi cha miaka miwili.

Aliitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Songwe kwa gharama ya shilingi bilioni nne, ujenzi wa vituo vitano vya afya shilingi bilioni 2.5, ujenzi wa miradi ya maji shilingi bilioni nne, ujenzi wa shule ya sekondari kata ya Maporomoko shilingi bilioni moja. Pia bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka shilingi bilioni moja hadi shilingi bilioni nne.

TIMU ya Majimaji bado kioo cha Mkoa wa Ruvuma

$
0
0

 

Kikosi cha timu ya majimaji enzi zake katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kikiwa na wachezaji nyota kama vile Stephen Mapunda Galincha na wengine.

Hayati Dkt.Lawrence Gama Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wa zamani ambaye ndiye mwanzilishi wa timu ya soka ya Majimaji  mwaka 1977,katika kipindi hicho Dkt Gama alichangia mafanikio makubwa ambayo timu hiyo iliyapata ikiwemo kuchukua ubingwa wa Jamhuri ya Muungano miaka miwili mfululizo mwaka  1985 na 1986
Baba wa Taifa na Rais wa Awamu ya kwanza wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwl.Julius Nyerere akikagua Timu ya soka ya Majimaji mwaka 1977 kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea,Timu ya majimaji ilikuwa ni miongoni mwa timu bora za soka hapa nchini na kuacha jina ambalo bado linautangaza Mkoa wa Ruvuma licha ya timu hiyo kushuka daraja miaka kadhaa iliyopita

MAJIMAJI ni miongoni mwa timu maarufu za soka hapa nchini ambayo ina historia ndefu ukiachia timu za Simba na Yanga ambazo zimedumu kwa muda wote zikicheza ligi kuu bara na kuwa na wapenzi lukuki kila kona ya nchi yetu.

Hakuna ubishi Timu ya Majimaji inafuatia kwa kuwa na washabiki na wapenzi wengi hapa Tanzania.Majimaji katika kipindi chake imepita  katika vipindi vya mafanikio na changamoto.

Licha ya kupata mafanikio makubwa katika mchezo wa soko hapa nchini,Majimaji pia imekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka daraja mara kadhaa katika vipindi tofauti.

Historia inaonesha kuwa,Klabu ya Majimaji ilianzishwa mwaka 1977 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wa zamani na Katibu Mkuu Mstaafu CCM hayati Dkt. Rawrence Gama  ambapo   Kikosi  cha kwanza cha Majimaji kiliweza kuundwa kwa kuichukua timu ya kombaini ya Mkoa wa Ruvuma na kupewa jina la Majimaji.

Kulingana na historia hiyo,Timu ya soka ya Majimaji ilipanda  daraja na kucheza daraja la kwanza kwa wakati huo sasa ligi kuu, mwaka 1982 ambapo walicheza msimu mmoja na kushuka kutokana na wachezaji wake wakati huo hawakuwa na uwezo wa kuhimiri mikikimikiki ya ligi hiyo ambayo ilikuwa na timu nane kwa nchi nzima katika kipindi hicho.

Mwaka 1984 Majimaji ilirejea tena kucheza ligi hiyo kwa kasi baada ya kujipanga na kuwa moja ya timu ambayo ilikuwa na sifa ya kuwalipa fedha nyingi na maslahi bora wachezaji wake ,hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji wa timu za Simba na Yanga kutoka Dar es salaam na kutimkia Songea kwa lengo la kujiunga na timu hiyo ya wanalizombe.

Wachezaji ambao walikuwa wakiwika kwa wakati huo kwa timu za Simba, Yanga na Pan African ambao walikuja kujiunga na timu hiyo yenye makao makuu yake mjini Songea, ni  Peter Tino, Zamoyoni Mogela,Malota Soma na Inocenti Haule.

Hata hivyo mchezaji Innocent Haule baadaye aliamua kuachana na Majimaji na kutimkia  nchini Kenya kucheza ligi za huko baada ya uongozi wa Simba kudai wachezaji hao walikuwa wamehama bila kufuata utaratibu wa uhamisho kutoka katika vilabu vyao.

Katika kipindi hicho Timu ya Majimaji ilikuwa tishio kwa vilabu vingine vilivyokuwa vikishiriki ligi hiyo na hata kusababisha kuchukua ubingwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa miaka miwili mfululizo mwaka 1985 na 1986 ambapo ligi hiyo ilikuwa ikishirikisha timu sita kati ya hizo timu tatu kutoka Visiwani na tatu kutoka Bara.

Majimaji katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 1986 ilipangiwa na timu ya Dyanamo ya Zimbabwe, mchezo ambao ulifanyika mjini Harare makao makuu ya nchi ya Zimbabwe, katika mchezo huo Majimaji ilifungwa mabao 5-0.

katika mechi ya marudiano mchezo haukuweza kufanyika kwa sababu Timu ya Majimaji ilijitoa baada ya kupata ajali wakati ikitokea Songea  kuelekea Dar es Salaam na baadhi ya wachezaji wake waliumia vibaya akiwemo Athumani Maulid na ikawa mwisho wake wa kucheza mpira.

Historia inaonesha kuwa,Mwaka wa pili Timu ya Majimaji ilipochukua ubingwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilipangiwa mchezo wake wa kwanza kucheza na timu ya Shirika la Kilimo la nchi ya Madagasca(BTM)  na kushinda bao 2-1.

Katika mchezo wake wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Taifa(Uhuru),jijini Dar es Salaam,Timu ya Majimaji ilishinda tena mabao 2-1 hivyo kusonga mbele, na kutolewa na FC Leopard ya Kenya kwa jumla ya mabao 2-0.

Timu ya Majimaji  ilishuka daraja baada Muasisi wake,Hayati Dkt.Gama kuhama Mkoa wa Ruvuma na kuhamia Mkoa wa Tabora,hali ambayo ilisababisha timu hiyo kuanza kuyumba,baada ya viongozi wa Serikali ya Mkoa  kushindwa kuchangia masuala ya michezo.

Hayati Dkt.Gama alipenda michezo na alikuwa mstari wa mbele kushughulikia changamoto zilizokuwa zinawakabili wachezaji.Hata hivyo Dkt.Gama akiwa Tabora aliweza kuusaidia Mkoa wa Tabora kuunda timu ya Mirambo iliyokuwa tishio katika ligi kuu Tanzania Bara.

Harakati ya Timu ya Majimaji kurudi tena kucheza ligi kuu Tanzania Bara,zilipata msukumo kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea mjini,Dkt.Emmanuel Nchimbi ambaye alihakikisha kuwa  timu hiyo inarudisha heshima yake ya miaka ya nyuma ambapo alitoa hamasa kubwa kwa  kuwashirikisha  wadau mbalimbali wa soka mkoani Ruvuma na wale wanaoishi nje ya mkoa huo.

Timu ya Majimaji ilijiwekea mikakati iliyosababisha timu hiyo kupanda daraja na kucheza ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wa mwaka 2009/2010 baada ya kucheza ligi ya daraja la kwanza Taifa na kufanikiwa kuwa kati ya timu tisa zilizoingia fainali ya kucheza ligi kuu.

Katika fainali hiyo timu tatu zilifanikiwa kuingia ligi kuu kufuatia kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo,timu hizo ni Majimaji, Manyema na African Lyon.

Majimaji tangu ilipopanda daraja na kurudi ligi kuu Tanzania bara ilijitahidi kucheza.Hata hivyo kiwango cha Majimaji cha enzi zile bado hakijaonekana,hali ambayo imesababisha timu hiyo  kupotea kwenye ulimwengu wa soka baada ya kushuka daraja kwa muda mrefu sasa.

Hata hivyo  timu hiyo haina budi kuungwa mkono kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa wadau na wafadhili  wanaichangia timu hiyo ili hatimaye kurejea ligi kuu na  kurudisha heshima ya Majimaji ya enzi zile  katika mchezo wa soka nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Mkutano wa kumi wa baraza la kumi la wawakilishi umeanza leo tarehe 15/02/2023

$
0
0

Mkutano wa kumi wa baraza la kumi la wawakilishi umeanza leo tarehe 15/02/2023, pamoja na maswali na majibu pia  kumewasilishwa hotuba ya ripoti ya kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya mwaka 2022/2023 pamoja na kuchangiwa na wajumbe wa baraza hilo.





 

Rais Dk Hussein Mwinyi afanya mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya Puma Afrika

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Kampuni ya Puma Afrika Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) akiongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa  mazungumzo yanayohusu masuala  mbali mbali ikiwemo uwekezaji wa Biashara ya Mafuta hapa Zanzibar.[Picha na Ikulu] 15/02/2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa na mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya  Puma Afrika ukiongozwa na Kiongozi Mkuu Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar,mazungumzo hayo yanahusu masuala mbali mbali ikiwemo   Bishara ya Mafuta hapa Zanzibar.[Picha na Ikulu] 15/02/2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na  Ujumbe wa Kampuni ya  Puma Afrika ukiongozwa na Kiongozi Mkuu Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar,mazungumzo hayo yaliyogusa masuala mbali mbali ikiwemo uwekezaji   katika Bishara ya Mafuta hapa Zanzibar.[Picha na Ikulu] 15/02/2023.  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Kampuni ya Puma Afrika Bw.Fadi Mitri  akiongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo (hawapo pichani) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa  mazungumzo yanayohusu  masuala mbali mbali ikiwemo uwekezaji wa Biashara ya Mafuta hapa Zanzibar.[Picha na Ikulu] 15/02/2023.
 

Dt. Tax Aongoza Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo wakati wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, Mhe. Deng Dau Deng Malek katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen akijadili jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja 

Mawaziri mbalimbali walioshiriki Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023. 

 

Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 18-19 Februari 2023.

 

Pamoja na mambo mengine, mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya kimkakati yanayohusu Bara la Afrika ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika-AfCFTA, uhakika wa chakula, hali ya ulinzi na usalama, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

 

Akichangia katika mkutano huo, Dkt. Tax alisisitiza umuhimu wa Kamisheni na Taasisi za Umoja wa Afrika kusimamia vyema rasilimali za Umoja wa Afrika kwa kuchukua hatua za kuondoa mapungufu yaliyobainika kwenye taarifa ya ukaguzi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

 

Mhe. Waziri pia alieleza hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua katika kutekeleza Mikataba ya Uenyeji ya Taasisi za Umoja wa Afrika zilizopo Tanzania ambazo ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Umoja wa Posta Afrika na Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri dhidi ya Rushwa.

 

Awali akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendelea kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayowagusa wananchi wa Afrika ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za mabadiliko za kijamii, kiuchumi na kiusalama. Alisisitiza umuhimu wa Afrika kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za vyakula ndani ya bara la Afrika pamoja na kutumia fursa za mkataba wa AfCFTA katika kukuza Mtangamano wa Kiuchumi.

 

Bw. Faki aliongeza kuwa Umoja wa Afrika umeendelea kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika katika nchi za Ethiopia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Libya ambapo jitihada zilizofanyika zimelenga zaidi kupata suluhisho la amani kwa mataifa hayo.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen amesema Ethiopia ameshukuru Umoja wa Afrika kwa mchango na ushirikiano wake ambao umewezesha kupatikana amani na utulivu nchini Ethiopia na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka miwili. “Ethiopia inaamini kuwa kupitia Umoja wa Afrika amani, ulinzi na usalama vitailetea Afrika maendeleo zaidi,” alisema Mhe. Mekonnen.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Uongozi wa Kampini ya Puma Afrika

$
0
0

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na  Ujumbe wa Kampuni ya  Puma Afrika ukiongozwa na Kiongozi Mkuu Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar,mazungumzo hayo yaliyogusa masuala mbali mbali ikiwemo uwekezaji   katika Bishara ya Mafuta hapa Zanzibar.[Picha na Ikulu] 15/02/2023.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeitaka kampuni ya kimataifa, Puma Energy kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya mafuta ya ndege ili kuendana na soko la ushindani la kimataifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo, Ikulu Zanzibar amesema ongezeko la bei ya maputa kwa kampuni hiyo inaiathiri Zanzibar kwa baadhi ya kampuni kubwa za ndege kushindwa kutua nchini kwa hofu ya kukosa mafuta.

Aliishauri kampuni hiyo kushusha bei ili kuendana na soko la ushindani hasa kwa kampuni za usafiri wa anga na wadau wengine kwenye sekta ya usafirishaji.

Alisema kuna mgogoro mkubwa kwenye sekta hizo uliosababishwa na kupandisha gharama za mafuta ya ndege, hali inayosababisha baadhi ya kampuni kubwa za ndege kununua Dar es Salaam na Mombasa, aidha, Dk. Mwinyi alieleza wanaoathirika zaidi ni kampuni ndogo za ndege zinazofanya safari zake za ndani baina ya Pemba, Tanga na Dar es Salaam.

Hata hivyo, aliwashauri Puma Energy kutoridhika na hali hiyo, badala yake wakubaliane na hali halisi ya soko la ushindani lilivyo ili kutoa fursa ya soko la biashara kwa kila mwekezaji.

Aliwaeleza kampuni hiyo endapo watashindwa pungunguza gharama za mafuta na kukabiliana na ushindani wa kibiashara uliopo kwenye usafirishaji wa anga, Serikali tayari imeiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kuangalia uwezekano wa kampuni nyengine kupewa fursa ya kuhudumia eneo hilo.

Alidha, alisema Serikali ina dhamira njema kwa wawekezaji wote pia inaunga mkono jitihada wanazozifanya kwa Serikali katika kuwahudumia watu na mazingira mazuri ya biashara, hivyo aliwataka wawekezaji kukabiliana na ushindani kwa kuleta unafuu kwa kila mmoja.

Pia Dk. Mwinyi alieleza Serikali imedhamiria kufanya uwekezaji mkubwa wa kuhifadhi mafuta ya kutosha ili kujiweka tayari na tatizo lolote, kupata utatuzi wa haraka.

Aliishauri Kampuni ya Puma Energy kuangalia fursa za uwekezaji wa eneo hilo kwa bandari ya Mangapwaji kuweka chemba ya kushushia mafuta na ghala la kuhifadhia mafuta ya ndege.

“Kwa hali tuliyonayo sasa likitokea tatizo lolole ingawa hatuombi litokee, hatutokuwa na uwezo wa kulitatua kwa vile hatuna hakiba” alieleza Dk. Mwinyi.

Alisema Serikali inajipanga kuhifadhi mafuta ya ziada ili iwe na uwezo wa kukabiliana na changamoto itakayotokea kwa kuziba mianya ya athari za changamoto hizo.

Akizungumzia ujenzi mpya wa uwanja wa ndege wa Pemba, Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali imedhamiria kuweka uwiano sawa na mandhari ya kisiwa cha Unguja kwa uondoa utofauti wa maendeleo na uwekezaji baina ya visiwa viwili hivyo.

Alisema tayari kuna wadau wengi wamejitokeza kuwekeza eneo hilo na kuwaeleza Puma Energy kuangalia fursa wa uwekezaji kwenye mradi huo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy kanda ya Afrika, Fadi Mitri aliiambia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba wana nia njema ya kuwekeza Pemba kwenye uwanja mpya wa ndege wa kimataifa kuwa wa kisasa na bora zaidi kwa Afrika nzima kuongoza kwa huduma za kimataifa na vifaa vyenye ubora wa uhakika.

Alisema kamuni ya Puma Energy itawekeza kwenye miundombinu ya kisasa ya uwanja huo, ipo tayari kutoa huduma za ndege za kimataifa kwenye uwanja huo kama ilivyo kwa kampuni ya Dnata ambayo inatoa huduma bora za viwanja vya ndege vya kimataifa kupitia mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Alisema licha ya Dnata kutoa huduma kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume, Kisauni Unguja, alisema kwa kisiwa cha Pemba, kampuni yake ya Puma Energy iko tayari kuhudumia na wameahidi kwa Serikali kwamba wataungamkono kwenye sekta hiyo.

Aidha, aliiahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuongeza ndege zaidi za kimataifa kuja moja kwa moja Zanzibar, alisema Puma Energy wanahudumia ndege zaidi ya 80 nchini Afrika Kusini. Hivyo, uwezo wa kuongeza ndege kufanya safari zake Zanzibar ni rahisi sana kwao.

Alisema watashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuifanya Zanzibar kuwa kituo bora zaidi kwa wageni kufikia na rahisi kufikiwa kwa kufurahia uzuri wa mandhari na haiba ya visiwa vyake.

Kampuni ya Puma Energy yenye makao makuu yake nchini Singapore, inafanyakazi kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 80 duniani kote pia ina vituo 740 kwa nchi 50 za Afrika, ni sehemu ya kampuni kubwa duniani ya Trafigura ambayo inafanyakazi kwa zaidi ya nchi 40 kutoka mabara Matano ya dunia.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR


Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awaapisha Viongozi Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Februari, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Mhe. Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 15 Februari, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Februari, 2023.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) akiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mb) Balozi Mhe. Pindi Hazara Chana, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Othman Yakub wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, 15 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb), Balozi Pindi Hazara Chana, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Othman Yakub mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 

Baraza la Madiwani Mafinga Mji Wapitisha Bajeti ya Bilioni 29.32.

$
0
0

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Reginant kivinge akiongea wakati wa kupitisha bajeti hiyo mbele ya wananchi,wadau na madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga
Baadhi ya madiwani, wataalam na baadhi ya wananchi wakifuatilia namna ya Baraza la madiwani lilipokuwa linaendelea

Na Fredy Mgunda, Iringa.

HALMASHAURI ya Mafinga Mji imepitisha bajeti ya shilingi bilioni 29.32 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi pamoja na matumizi ya ofisi.

Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Reginant kivinge alisema kuwa bajeti hiyo imejikitaka katika mishahara na matumizi mengine ya utendaji wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.

Kivinge alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Halmashauri ya Mji Mafinga inatarajia kupokea kiasi cha shilingi bilioni 6.35 kutoka serikali kuu, shilingi bilioni 1.81ni mapato ya ndani na shilingi bilioni 3.56 za mapato ya nje.

Alisema kuwa  rasimu bajeti hiyo imejielekeza pia katika kuboresha mtandao wa barabara za mjini na vijijini,  ngazi ya kata kwa kufanya matengenezo, utekelezaji wa makundi maalum kwa kuelekeza asilimia 10 ya makusanyi ya mapato ya ndani.

Kivinge alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika kukamilisha miundombini ya kutolea huduma kwa jamii katika sekta ya afya, elimu na utawala.

Alisema kuwa Halmashauri iataendelea kushirikiana na jamii,wadau, serikali kuu,ofisi ya mkuu wa mkoa na wilaya ya Mufindi pamoja na chama cha mapinduzi ngazi zote katika kuhakikisha wanachangia mpango wa bajeti ya Halmashauri hiyo.

Kivinge alisema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga hatua inayochochea maendeleo na utatuzi wa changamoto ya huduma mbalimbali ikiwemo Huduma za afya, Elimu na miundombinu ya kiuchumi.

Lakini pia chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kimelitaka baraza la madiwani Halmashauri Mafinga Mji kuhakikisha linashughulikia kwa wakati kero za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo Ilani ya CCM na kuwaonya viongozi wanaowakumbuka wananchi pindi uchaguzi unapokaribia

Akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga ,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke alisema kuwa suala la barabara,maji,afya,elimu na masoko imekuwa changamoto kubwa kubwa kwa wananchi hivyo viongozi wa serikali ya Halmashauri ya Mafinga Mji wanatatua changamoto zote hizo ili chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kuendelea kushika dola kama ambavyo ilivyo hivi Sasa.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Akijibu Maswali ya Wajumbe

$
0
0

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein akijibu swali namba 37 lililoulizwa na Mhe Abdallah Abass Wadi wakati wa Baraza la kumi la Wawakilishi mkutano wa kumi kikao cha kwanza, huko Chukwani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

SMZ Kuipa Lipaumbele Sekta ya Elimu kwa Kuongeza Ufaulu na Kufuta Divisheni Ziro

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said akizungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Pemba kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipa kipao mbele Sekta ya Elimu kwa kuongeza ufaulu na kufuta divisheni sifuri, mkutano huo uliofanyika katika Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba.
Walimu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Ndg. Khamis Abdallah Said wakati wa mkutano wake na Walimu uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba. 
Walimu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Ndg. Khamis Abdallah Said wakati wa mkutano wake na Walimu uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba. 

Katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said amewataka walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipa kipao mbele Sekta ya Elimu kwa kuongeza ufaulu na kufuta divisheni sifuri.

Ameyasema hayo katka Mkutano wa Kutathmini matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Darasa la nne uliowashirikisha Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi huko katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema matokeo ya mitihani ya Mwaka uliopita hayalingani na jitihada zinazowekwa katika kuimarisha Sekta ya Elimu hivyo amewataka Walimu Wakuu kujitoa kikamilifu katika kusimamia Uwajibikaji katika Skuli zao.
Aidha amesema kwa kua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi itajenga madarsa zaidi ya 2000,N yumba za walimu pamoja na Mabweni kwalengo la kuweka mazingira bora ya kufundisha na kujifunza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhan akijibu hoja za Walimu Wakuu kuhusu Tathmini ya Matokeo amewataka Walimu Wakuu kuwahamadisha walimu wao kufanya Tathmini kulingana na mazingira na rasilimali walizonazo.
Akifafanua zaidi amesema si vyema kuacha kuwapima wanafunzi kwasababu Skuli haina Mashine ya kutolea fotokopi na badala yake chaki na ubao zinaweza kutumika kuwapima Wanafunzi hao.
Aidha amesema Wanafunzi wa Maandalizi nirahisi mno kuwapima kwani upimaji wao unajikita katika maneno matatu ambayo ni Kusoma ,Kuandika,na Kuhesabu.
Wakati huohuo Bifatma amewataka Walimu Wakuu kutoa Mashirikiano ya kutosha kwa wazazi ili kubaini changamoto zinazowakabili watoto na kuweza kuzitatua.
Akiitoa ushauri wake Mwalimu Mkuu Skuli ya Kisiwa Panza Nd. Fatawi Mselemu Juma amesema ufaulu wa Wanafunzi katika kila Skuli Unawezekana iwapo Walimu , Wazazi na Kamati watatoa mashirukiano ya kutosha
Akifafanua zaidi Mwalimu Fatawi amewataka Walimu kuweka Utaratibu wa kuwashajihisha watoto kwa kuwapa Zawadi ndogo ndogo kwa lengo la kuwatengezea hamu na ari ya kujifunza.

ALIYEJIFANYA KATIBU WA IKULU MIKONONI MWA POLISI

$
0
0

Ndugu wanahabari,awali ya yote napenda Kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuamsha salama siku ya leo tukiwa na afya njema na kutuwezesha kufanya shughuri zetu za kujipatia riski kama kawaida.

 Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wasaidizi wao waandamizi kwa kuendelea kuongoza vyema nchi yetu. Mpaka sasa Amani na utulivu vimetamalaki  kwani wananchi wanafanya shughuli zao halali za kiuchumi bila ya bughuza wala tishio lolote la kiusalama.

Ndugu Wanahabari,hali ya Usalama kwa Visiwa vya Zanzibar ni shwari hakuna matukio makubwa yenye kuleta taharuki kwa jamii, matukio yanayojitokeza ni ya kawaida na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, tunakabiliana nayo.

Ndungu wanahabari,Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Zanzibar linafanya uchunguzi juu ya matukio mawili ya uhalifu ikiwemo tukio la kughushi nyaraka za Serikali na kuzitumia kuomba visa Ubalozi wa Marekani na tukio la pili ni kujifanya Mtumishi wa Serikali.

Ndungu Wanahabari, Mnamo tarehe 31/01/2023 ofisi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar ilipokea taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ofisi ndogo ya Zanzibar, ikieleza kughushiwa kwa nyaraka za Serikali na kuwasilishwa Ubalozi wa Marekani kwa lengo la kuomba visa.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi likishirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi pia na Kitengo cha Usalama Ofisi ya Ubalozi wa Marekani nchini imegundua watu 28 waliwasilisha barua wakijitambulisha na kujinasibisha kwamba wao ni watumishi katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibr. Hivyo kwa barua hizo ambazo zimepitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameomba kupatiwa Visa kwenda Marekani kufanya shughuli mbalimbali, zikiwemo kuhudhuria semina, masomo n ahata kushiriki michezo.

Ndugu wanahabari, Aidha katika uchunguzi huo watu 12 wamekamatwa na kuhojiwa ambapo baadhi yao wamekiri kutumia mbinu ambazo siyo halali kutaka kwenda Marekani.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi wa Marekani Kitengo cha Usalama na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaendelea na uchunguzi ubaini mtandao mzima unaohusika na mpango huu wa kusafirisha watu kwenda nje kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Napenda nitoe wito kwa vijana na watu wote wanaohitaji kusafiri kwenda nje ya nchi wasitumie njia zisizohalali kufanikisha safari zao na badala yake wafuate taratibu au njia sahihi za kufanikisha safari zao.

Ndungu wanahabari, Jeshi la Polisi vile vile linafanya uchunguzi wa tukio ambalo vijana wawili ambao ni KHATIB KONDO KHATIB miaka 39 mkaazi wa wa Mfenesini Shehia ya Kama Tarishi wa Baraza la Mji Kaskazini B na MDUNGI FADHIL MLEKWA miaka 32, mlinzi katika Wilaya ndogo ya Tummbatu  wamejifanya maafisa wa Serikali

Mnamo tarehe 02/02/2023 Jeshi la Polisi limepokea taarifa kutoka kwa kaimu Mkurugenzi baraza la mji Wilaya ya kaskazini B Mkoa wa Kaskazini UngujaMEMMY KOMBO MCHENGA kwamba alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa yeye ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Ikulu akimpa maelekezo ya utekelezaji akimwambia kwamba watumishi aliowaondoa katika nafasi zao awarudishe mara moja ni maagizo kutoka Ikulu.Pia aliongeza kuwa taarifa za Kaimu Mkurugenzi  ziko Ikulu kwamba amemdhibiti sana mkurugenzi kiasi cha kuwa Mkurugenzi hana nafasi na wala hana uwezo wa kutoa maamuzi Zaidi yake yeye.

Ndungu wanahabari, Sambamba na hilo mtu huyo aliyejitambulisha kama ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais alimueleza kaimu mkurugenzi kwamba yeye ana taarifa zake kuwa ni msomi aandae CV zake atakuja kuzichukua ili aangalie jinsi ya kumpatia nafasi kubwa Zaidi kwa sababu Mhe Rais atafanya uteuzi hivi karibuni.

MEMMY KOMBO MCHENGA mara baada ya kupata taarifa hizo aliripoti katika Jeshi la Polisi na uchunguzi ukaanza mara moja. Uchunguzi unaendelea watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi

Ndugu wanahabari, Wito wangu wananchi tuwe makini na matapeli wa mitandaoni, unapopokea simu au ujumbe wowote kwa mtu ambae humfahamu basi usitekeleze chochote unachoelekezwa na kama kuna mashaka ripoti haraka Jeshi la Polisi. Vijana tusitumie njia za mkato kijipatia kipato, uhalifu haulipi.

Ahsanteni.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Jijini Addis Ababa Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.

 

Rais Dk Hussein Mwinyi ameweka jiwe la msingi Jengo la Ofisi na Maabara ya Kituo cha Nguvu za Atomu Dunga Zuze

$
0
0

MUONEKANO wa Jengo la Kituo cha Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja lililoweka, Jiwe la Msingi la ujenzi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika viwanja vya Ujenzi wa Kituo cha Ofisi na Maabara  ya Tume ya Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kuweka la Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo hicho leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikilia Mshauri Elekezi Dkt.Justin Ngaile akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Jengo la Ofisi na Maabara ya Kituo cha Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja, wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo hicho leo 16-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikilia Mshauri Elekezi Dkt.Justin Ngaile akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Jengo la Ofisi na Maabara ya Kituo cha Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo hicho leo 16-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe.Omar Juma Kipanga na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadidi Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dungu Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadidi Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumaliza kuweka Jiwe la Msingi la Kituo cha Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hadidi Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi na Maabara ya Tume Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dungu Zuze Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)
MSANII wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Msechu akitowa burudani kwa wimbo maalumu wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023.(Picha na Ikulu)


Ratiba ya Ligi Kuu ya Zanzibar mzunguko wa 21

Umuhimu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kUSIMAMIA NA kUDHIBITI mATUMIZI sALAMA ya Vyanzo vya Mionzi

$
0
0

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Dunga Zuze Wilaya ya Kati Unguja leo 16-2-2023.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ni jambo muhimu kwa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya vyanzo vya mionzi nchini, ili vitoe mchango zaidi katika maendeleo ya Taifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ofisi na maabara ya Tume hiyo kwa Zanzibar, huko Dunga Zuze Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Dk. Mwinyi alisema Taifa linatumia teknolojia ya nyuklia katika nyanja mbalimbali na kueleza kuwa sayansi na teknolojia ya nyuklia ina manufaa makubwa ikitumiwa vizuri, itasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo kilimo, mifugo, nishati na afya.

Alisema Zanzibar imepata mafaniko makubwa kutokana na kutumika kwa teknolojia ikiwemo kutokomeza wadudu aina ya mbung’o ambao walikuwa wakiathiri afya na uzalishaji wa mifugo hususan ng’ombe.

Alieleza Tume iliwezesha upatikanaji wa mbegu bora ya mpunga aina ya “SUPA BC”, yenye sifa ya kustahamili ukame na maradhi na kuongeza sasa mkulima anaweza kupata tani saba badala ya nne za awali kwa hekta moja.

Akizungumzia faida ya atomu kwa sekta ya elimu, Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaidia kuimarisha uwezo na utaamu wa kudhibiti na kuongeza wigo wa matumizi ya teknolojia ya nyuklia nchini.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, inakamilisha utaratibu wa kufadhili vijana wa Kitanzania kwenda kusoma masuala ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia katika vyuo bora duniani” alieleza Dk. Mwinyi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwataka wadau na wafanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania kujituma kwa bidii na maarifa ili kuleta mchango mkubwa kwa Taifa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Omar Juma Kipanga kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda alieleza mipango ya wizara hiyo kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo.

Alisema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu imedhamiria kuongeza wataalamu zaidi kwenye eneo hilo na kuongeza kwamba tayari imekamilisha mitaala ya shahada tatu za uzamili kwenye Teknolojia ya nyuklia zitakazo tolewa kupitia taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Nelson Mandela, Arusha

Akizungumzia ufadhili wa masomo kupitia mpango wa (Samia Scholarship) Naibu Waziri huyo, alieleza Serikali inawahamisisha vijana kubobea kwenye masomo ya sayansi ili kunufaika na fursa nyengine za ufadhili za ndani na nje ya nchi. Pia alieleza juhudi nyengine zinazochukuliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuweka msukumo wa kutanua wigo wa matuizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia nchini.

Naye, Waziri wa Afya Ahmed Nassor Mazrui amesema, sekta ya afya Zanzibar inafanyakazi kwa karibu na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania, kutokana na miradi yake mingi kuhusisha mionzi.

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ilianzishwa chini ya sheria ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nambari 7 ya mwaka 2003 kwa lengo la kusiumamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi pamoja na kusimamia vyanzo vyote dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na vyanzo hivyo. Pia ina jukumu la kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia nchini.

Ujenzi wa ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania kwa Zanzibar, utahusisha ofisi 27, maabara sita, kumbi tatu za mikutano, ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kuchukua watu 100, jiko na sehemu ya kulia, ukumbi wa bodi, ukumbi mwengine wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 21 pamoja na eneo la walinzi.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

TAMWA, |UNESCO kuwajengea uwezo waandishi kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto

$
0
0

 

Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa kushoto akikabadilishana hati ya makubaliano na mwakilishi mkaazi wa UNESCO Tanzania Michel Toto Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Na.Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanazibar) zimesaini mkataba wa mradi  kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Mradi huo wa miezi mitatu wenye thamani ya dola za Marekani 17,000, umesainiwa kati ya Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar, Dk. Mzuri Issa Ali na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Michael Toto, katika hafla iliyofanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja.


Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Mzuri alisema mradi huo  utaongeza nguvu mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto ambayo ni moja ya mikakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais, Dk. Hussein Ali Mwinyi.


Alisema hii ni mara ya kwanza kwa TAMWA na UNESCO kushirikiana, hata hivyo aliahidi kutekeleza mradi huo kwa kiwango ili kukidhi matarajio ya UNESCO.


Pamoja na hayo alieleza kuwa wanamatumaini makubwa na kwamba mradi huo utafanya vizuri na kuleta tija kwa kwa maslahi mapana ya Taifa.


Kwa upande wake mwakilishi mkaazi wa UNESCO Tanzania  Michel Toto, alisema mradi huo utalenga kuwajengea uwezo wanahabari katika kuondoa mila potovu kuhusu GBV visiwani Zanzibar.


Alipongeza mchango wa wanahabari na TAMWA kwa kujikita kuandika habari za udhalilishaji na kuahidi kwamba UNESCO itaendelea kushirikiana na TAMWA katika kukabiliana na udhalilishaji ikiwemo kupunguza mimba za umri mdogo.


Pamoja na hayo alisema mashirikiano hayo ya awali yatafungua mlango kwa mashirikiano mengine zaidi ya shirikika hilo na TAMWA-ZNZ.

Jakaya Kikwete announced as Africa Food Prize Chair

$
0
0

 2023 Nominations for Africa’s preeminent award for food security now open

 

ADDIS ABABA, 17 February 2023 - Former President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, has been announced as the new Chair of the Africa Food Prize (AFP). He will succeed former Nigerian President, H.E. Olusegun Obasanjo, who has been serving as the AFP Chair since 2016.

 

Welcoming the appointee, outgoing Chair, H.E. Obasanjo expressed enthusiasm noting that through his work, H.E. Kikwete has shown a genuine passion and dedication towards transforming Africa’s agriculture.

“I congratulate Dr. Kikwete on his appointment as Chair of the Africa Food Prize. Through his leadership, I am confident that the continent will continue to explore and implement food systems strategies that lift people from poverty through inclusive growth and sustainable development,” H.E. Obasanjo said.

 

Dr Kikwete has a commendable track record as a leading contributor to the transformation of Africa’s food systems. As President of Tanzania, H.E. Kikwete led the implementation of ‘Kilimo Kwanza’ (Swahili for Agriculture First), an initiative that unlocked productivity and profitability for the country’s smallholder farmers. He also spearheaded the implementation of the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), a public-private partnership aimed at unlocking more private sector investment in the country’s agricultural sector.

 

Upon his retirement, and through the Jakaya Mrisho Kikwete Foundation, H.E. Kikwete has been collaborating with farmers and researchers to develop initiatives and strategic interventions to increase yield and productivity in smallholder farming and agribusiness.

 

Dr. Kikwete’s appointment coincides with the 2023 call for nominations for the US$100,000 Africa Food Prize. The Africa Food Prize is the preeminent award recognizing the extraordinary women, men, and institutions whose contributions to African agriculture are forging a new era of sustainable food security and economic opportunity that elevates all Africans.

This year, Nestlé partnered with the Africa Food Prize, contributing CHF 100,000 (equivalent to US$ 108,400) which will go to the main award, and a special category focusing on innovations that advance regenerative food systems.

 

“We are excited to see how this year’s applicants for the Africa Food Prize are making a difference. Their research and innovation efforts will help drive the transformation of agriculture on the African continent, and we are proud to support this,” said Remy Ejel, Chief Executive Officer of Zone Asia, Oceania and Africa, Nestlé S.A.

 

In 2022, Eric Yirenkyi Danquah, a Ghanaian plant geneticist, won the award for his outstanding expertise, leadership and grantsmanship skills that led to the establishment and development of West Africa Centre for Crop Improvement (WACCI), a world class centre for training plant breeders in Africa for Africa. Through WACCI, Mr. Danquah’s innovations led to the creation of more than sixty improved seed varieties, including superior maize hybrid varieties, which continue to boost yield for farmers and contribute towards food and nutritional security in Ghana.

 

Organisations, institutions, businesses, and individuals who have created opportunities for Africa’s farmers to gain viable livelihoods from their trade can submit their nominations at www.africafoodprize.org/nominate before Monday, 16 May 2023.

 

Winners will be selected by the Africa Food Prize committee and will be announced at the AGRF, Africa’s Food Systems Forum 2023 to be held in Dar es Salaam, Tanzania, in September.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Addis Ababa, Ethiopia

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.

Viewing all 36137 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>