Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Wananchi Katika Ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Forodhani Unguja Leo
Serikali Yataka Aliyemlawiti Mwanawe Achukuliwe Hatua.*Waziri Mkuu asema Serikali haitofumbia macho vitendo vya ukatili
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wahakikishe wanamfikisha katika vyombo vya sheria baba mzazi wa mwanafunzi wa darasa la pili (7) katika Kata ya Sokoni One mtaa wa Lonovono Jijini Arusha kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake.
Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inakemea vikali vitendo vya unyanyasaji, ubakaji na ulawiti kwa watoto, hivyo imewataka Wakuu wa mikoa na makamanda wa polisi nchini wahakikishe wanawasaka na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitofumbia macho na wala kukubaliana na vitendo vya ukatili kwa watoto, hivyo ameitaka jamii kushirikiana katika kupiga vita vitendo hivyo pamoja na kutowaficha wale wote wanaohusika na unyanyasaji huo.
Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Februari 17, 2023) baada ya kusambaa kwa taarifa kupitia vyombo vya habari vikimuonesha mtoto huyo ambaye anadaiwa kulawitiwa na baba yake mzazi. Mtoto huyo ambaye alisikika akielezea namna mzazi wake huyo alivyokuwa akimfanyia vitendo vya ukatili naye atafutwe na kupatiwa huduma ya matibabu kwa haraka.
Amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya wazazi, walezi na wanajamii kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti, hivyo kuwasababishia maumivu makali pamoja na msongo wa mawazo hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo. “Serikali haitosita kumchukulia hatua mzazi au mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivi vya ukatili.”
“Kumeibuka wimbi la ukatili wa kuwafanyia vitendo vya hovyo watoto wetu kwenye maeneo mbalimbali nchini, hivyo fanyeni uchunguzi na kubaini wanaohusika na vitendo hivyo. Wakuu wa Mikoa, Makamanda wa Polisi pamoja na Maafisa wa Ustawi wa Jamii hakikisheni mnawasaka watu wote wenye tabia hizo na kuwachukulia hatua.”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa jamii ishirikiane na Serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake. “Wananchi shirikianeni kuhakikisha watoto wote wanalindwa na kupatiwa haki zao za msingi, mtoto wa mwenzio ni wako.”
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 17, 2023.
ULEGA: Msomera Yazidi Kung’ara Miradi ya Wafugaji Yapaa
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akiendesha trekta mara baada ya kufika katika moja ya mashamba darasa ya malisho ya mifugo kwenye Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, katika ziara yake ya siku moja kwenye wilaya hiyo.
Mhe Othman ashiriki Hauli ya Maalim Seif Masjid Omar Bin khattab, Msumbiji
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , amejumuika na Viongozi, wafuasi wa na Wanachama wa Chama cha Act- Wazalendo pamoja na waumini wa Dini katika haluli ya kumuombea Dua aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.
Dua hiyo iliyofanyika katika Masjid Omar Bin khattab katika mtaa wa Msubiji ni kumbukumbu ya kutimia miaka miwili tangu kufariki kwa kiongozi huyo mashuhuri mnamo tarehe 17 Februari mwaka 2021.
Marehemu Malim Seif alifariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa kwa matibabu kwa kipindi cha takribani wiki mbali baada ya afya yake kodorora zaidi alipokuwa amelezwa awali kwa matibabu katika Hospitali ya Mnanzi mmoja.
Akitoa wasifu wa Kiongozi huyo baada ya kukamilika kwa dua hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT- Wazalendo Nd. Hassan Jani Masoud, amesema kwamba kiongozi huyo alikuwa na mwenendo bora na kuwa msamehefu kwa kila aliyemkosa.
Amesema kwamba maalim Seif aliwajali wanancho wote na hasa wanyonge na hakuwa mkachu wa tabia sambamba na kujitoa katika kutetea maslahi ya Zanzibar na watu wake bila kuchoka katika maisha yake yote.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu amewataka wananchi wa Zanzibar kuishi na sifa ya maalim Seif kwa kuwa alikuwa ni mtu mstahamilivu, msamehevu na aliyejiweka katika dara la kati aliyeishi vyema na watu wa aina zote hata wale waliomkosa.
Aidha amesema kwamba maalimu seif alikuwa kiongozi mwenye huruma aliefuata vigezo na maelekezo mema katika kusimamia na kuwaongoza wananchi na wafuasi wake jambo lilomfanya kupata mapenzi kwa watuwatu wengi ndani na nje ya Zanzibar.
Naye Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Nd. Salim Biman kwa niaba ya Viongozi wawakuu wa Chama hicho amesema kwamba anawashukuru watu wote waliokusanyika katika maeneo mbali nchini kumuombea dua marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.
Dua kama hiyo imesomwa katika misikiti mbali mbali ya Unguja na Pemba , Dar es Salama na kwengineko kwa nia ya kumkumbuka na kumuombea kwa mwenyezimungu amsamhe makossa yake na amuweke mahali pema Peponi.
Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe 17.02.2023.
Mhe Hemed ajumuika na waumini katika Sala ya Ijumaa Masjid Utapoa, Bububu
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Masjid Utapoa Bububu Wilaya ya Magharibi “A” katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Akiwasalimia waumini hao baada ya Swala Alhajj Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi inachukua jitihada mbali mbali katika kuleta unafuu wa bei za bidhaa ili wananchi waweze kujikimu kimaisha.
Amesema pamoja na jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wapo baadhi ya wafanyabiasha wanapandisha bei za bidhaa bila ya kuwa na sababu za msingi jambo ambalo wanaenda kinyume na jitihada za Serikali za kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi wake.
Pamoja na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewakumbusha waumini hao kuwa na tabia ya kupendana na kusaidiana kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu katika jamii wakiwemo mayatima,watu wenye ulemavu pamoja na wajane.
Aidha Alhajj Hemed amewahimiza waumini na wananchi kwa ujumla kuendelea kuitunza amani iliyopo ili Serikali iendelee kuwatumikia wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
Pamoja na hayo Mhe. Hemed amewakumbusha waumini hao kusimamia misingi ya dini katika maisha yao ya kila siku na kudumisha ibada hasa katika miezi hii mitukufu ili kupata radhi za Allah (S.W.)
Nae Maalim Omar Hamad ameiomba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kusimamia mila,silka na desturi ili kuepusha mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Ameeleza kuwa katika Jamii kumeibuka mambo mbali mbali yanayoashiria kupotea kwa maadili ya wazanzibari hali ambayo inapaswa kukemewa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo
Rais Dk Hussein Mwinyi afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi naMwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu
Makatibu wa Uenezi CCM Zanzibar wapigwa msasa
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni Zanzibar Ndg.Omsr Ibrahim Kilupi akizungumza na Makatibu hao.(PICHA NA IS-HAKA OMAR).
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MAKATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wametakiwa kuwa wabunifu na wachapakazi katika kueneza na kutangaza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Khamis Mbeto Khamis wakati akizungumza na makatibu hao wa ngazi za majimbo hadi mikoa huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Amewakumbusha makatibu hao kuwa wanatakiwa kutangaza utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 inayotekelezwa katika maeneo yao.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais Dk.Mwinyi inatekeleza kwa ufanisi mkubwa Ilani ya CCM.
Katika maelezo yake Mbeto,aliwambia watendaji hao kuwa wanatakiwa kubadilika kiutendaji na kufanya kazi kwa bidii ili waende sambamba na kasi ya CCM kiutendaji.
“Makatibu nyinyi ndio mdomo wa Chama chetu mliopewa dhamana ya kusema na kufafanua mambo yote mazuri yanayofanywa na Chama pamoja na Serikali zetu kwa ujumla.
Tuna kazi kubwa ya kueneza na kuwambia wananchi mafanikio yanayopatikana katika maeneo yenu kunajengwa barabara za lami,maji safi na salama,hospitali zenye hadhi ya kimataifa,shule za kisasa na mengine mengi yanayotakiwa kujulikana kwa umma.”,alieleza Mbeto,
Alisema wananchi wanatakiwa kujua kwa kina utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na CCM katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ili wajiridhishe.
Alisema Zanzibar inaendelea kupiga hatua kubwa katika sekta za utalii,afya,kilimo,uvuvi,maji safi na salama,miundombinu ya umeme,usafiri wan chi kavu na baharini,usafiri wa anga,uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na ustawi wa jamii.
Pamoja na hayo alieleza kuwa CCM itaendelea kufanya siasa za kisayansi zinazobeba dhana ya kumiza ahadi kwa vitendo badala ya maneno.
Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organaizeshe CCM Zanzibar Ndg.Omar Ibrahim Kilupi, alisema kipaumbele chake ni kutekeleza ibara ya tano ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022,kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo kwa kila uchaguzi.
Alisema ushindi wa CCM utapatika kutokana na juhudi kubwa za kutangaza fursa na maendeleo yanayofanywa na serikali ili wananchi wajue na kuendelea kujenga imani kwa Chama walichokipa ridhaa ya kuongoza dola.
Kupitia kikao hicho Ndg.Kilupi, aliwataka wabunge,wawakilishi na madiwani kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi majimboni.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kujadili hali ya Usalama katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mkutano huo umefanyika katika Jengo la Amani na Usalama la Mwalimu Julius Nyerere lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama (PSC) la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kujadili hali ya Usalama katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo umefanyika katika Jengo la Amani na Usalama la Mwalimu Julius Nyerere lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa tarehe 17 Februari, 2023.Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmin katika ufunguzi wa Mradi wa Maduka ya Darajani Souk
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Kampuni Africab Group Tanzania wakati alipowasili katika ufunguzi wa Mradi wa Maduka ya Darajani Souk leo, yaliyojenga na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (mbele kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohamned wakifungua pazia kufungua Mradi wa maduka ya Darajani Souk leo, yaliyojenga na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Maduka ya Darajani Souk yaliyojengwa na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi katika hafla iliyofanyika leo(kushoto kwa Rais) Mama Mariam Mwinyi na (kulia) Mkurugenzi Mwenza wa Africab Bw.Yussuf Ezzi(kushoto kwa Rais) na Viongozi wengine .[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakati alipotembelea Maduka ya Darajani Souk mara baada ya kuyafungua rasmi leo, ambapo Mradi wa Maduka huyo yaliyojengwa na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,(kulia) Mkurugenzi Mwenza wa Africab Bw.Yussuf Ezzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohamned (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akiangalia asali katika Duka la Mama Batul Ezzi wakati alipotembelea Maduka ya Darajani Souk mara baada ya kuyafungua rasmi leo,Mradi wa Maduka hayo yaliyojengwa na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,(kushoto) Mkurugenzi Mwenza wa Africab Bw.Yussuf Ezzi.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (katikati)wakiwa na zawadi walizopokea kutoka kwa Fatma Yussuf Ezzi (kulia) na Mufaddal Aliasger Ezzi wote wa Africab Group, alipotembelea Maduka ya Darajani Souk mara baada ya kuyafungua rasmi leo, yaliyojengwa na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akitia udongo wakati alipopanda mche wa Mnazi kama ishara ya kumbukumbu yake ya ufunguzi wa Mradi wa maduka ya Darajani Souk yaliyojengwa na Kampuni ya Africab Group Tanzania katika Eneo la Darajani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,viongozi mbali mbali walishuhudia kitendi hicho .[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Baadhi ya majengo ya milango ya Mradi wa Maduka ya Darajani Souk yaliyojengwa na Kampuni ya Afiricab Group ya Tanzania katika eneo la Darajani Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi na Kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.[Picha na Ikulu] 18/02/2023.
Rais Dk Hussein Mwinyi afanya ziara ya kushtukiza Marikiti Kuu Darajani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia mchele wa Mbeya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023,na kuzungumza na Mfayabishara wa Bidhaa za Vyakula katika marikiti hiyo Bw.Seif Khamis Ali na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kusalimiana na Watalii wakitembelea Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kutembelea Wafanyabishara ya vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Unguja leo 18-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Mfanyabishara wa Nyama ya Ng’ombe katika Soko la Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti hiyo kuangalia hali ya bidhaa ya vyakula.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akilipia Nyama ya Ng’ombe baada ya kuinunua kwa Bw.Ali Hashim mmoja wa Wafanyabiashara katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo 18-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)
Uongozi wa CCM Zanzibar Kuweka Usimamizi Mzuri wa Mapato Yanayotokana na Mradi wa Maduka ya Darajani "The Darajani Souk"
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka uongozi wa CCM, kuweka usimamizi mzuri wa mapato yanayotokana na mradi wa maduka ya Darajani, “The Darajani Souk” pamoja na kufikiria miradi mengine yenye faida itakayokisaidia chama na jumuiya zake.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa mradi wa maduka ya Darajani Souk, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema mradi wa maduka hayo ya Darajani ni sehemu ya jitihada za kutekeleza ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuwaahidi wafanyabiashara wadogowadogo kuwajengea maeneo mazuri ya kufanyiabiashara.
Alisema maeneo hayo yameanzwa kujengwa yakiwemo maeneo ya wajasiriamali wadogo kwenye mikoa na wilaya zote, ikiwemo miradi ya ujenzi ya masoko makubwa kama Chuini, Jumbi, Mwanakwerekwe na Mombasa. Aidha alieleza CCM itaendelea kubuni miradi mikubwa ya kiuchumi na uwekezaji ili kukijenga chama kwa nguvu za kiuchumi.
Rais Dk. Mwinyi, aliwataka viongozi wa chama hicho, kutumia vyema mradi wa Darajani Souk ili kufanikisha dhamira ya chama kwa kubuni miradi mikubwa ya kiuchumi yenye kipato na kukikuza kiuchumi na kueleza ujenzi wa mradi wa maduka hayo utanufaisha ustawi wa uchumi wa chama.
Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi aliwanasihi wafanyabiashara takaobahatika kupata milango, kuzingatia masharti yaliyowekwa ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Aidha, aliwataka viongozi wa Chama kutumia busara ya ugawaji wa maduka hayo kwa kuwapa kipaumbe wafanyabiashara wote waliopisha mradi huo.
“Kipaumbele cha kwanza wapewe wale wote waliopisha mradi huu, ambao walilazimika kusitisha shughuli zao za biashara na kuacha ujenzi uenedelee” Alielekeza Dk. Mwinyi
Alisema Serikali imeruhusu eneo hilo kuuzwa biashara saa 24 na kuwahakikishia ulinzi wa mali zao pamoja na kuwataka kulitunza vyema eneo hilo kwa kuendelea kuitunza haiba ya mji kwa mazingira safi na salama.
“Ndugu zangu taaswira tuliyonayo paha tunapaswa kuitunza, tuhakikishe sehemu hii inaendelea kuwa nzuri kila wakati, mufanye ukarabati kwa kila patakapohitajika, rangi ipakwe ikichakaa na kufanyiwa matengezo kwa sehemu itakayoharibika, ili maduka yaendee kudumu muda mrefu” Alishauri Dk. Mwinyi,
Akizungumzia haiba ya Mji Mkongwe Dk. Mwinyi alieleza licha ya mabadiliko ya mji yanavyoendelea alisema Serikali haina nia ya kubadili haiba halisi ya mji Mkongwe bali kuutunza na kuuendeleza udumu.
“Sote tunaimani njema ya kuutunza Mji Mkongwe, ni urithi wetu sisi na vizazi vijavyo, hatuwezi kuruhusu uharibike” Alisema Dk. Mwinyi.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Masoud Ali Mohammed alisema Serikali inatekeleza ahadi zake kwa vitendo, aliwasihi wananchi waache chuki, kebehi na lawama kwani hazijengi nchi na aliwaomba washirikiane kwa kupeana moyo ili kuendeleza uchumi na biashara.
Akizungumzaa kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu CCM - Zanzibar, Katibu wa Kamati Maalum NEC, Idara ya Uchumi na Fedha kutoka ofisi Kuu cha Chama, Kisiwandui, Afadhali Taibu Afadhali, alisema ujenzi wa mradi wa maduka hayo ni utekelezaji wa sera ya CCM, toleo la 2021 inayokitaka Chama kutekeleza miradi na uwekezaji na kuelekeza kazi zote za chama kujikita kwenye kujenga uchumi na uwekezaji.
Aidha, alita wito kwa wawekezaji wengine kujitokea zaidi na kuwekeza Zanzibar ambako alieleza kwamba nchi imebarikiwa kuwa na maeneo mengi ya kuwekeza hivyo aliwataka kutumia fursa hiyo vilivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrisa Kitwana alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikua na mipango mingi ya maendeleo na uwekezaji kwenye eneo hilo la Darajani, alieleza mafanikio ya mradi wa maduka hayo ni miongoni mwa miradi iliyoelekezwa kwenye eneo hilo, aidha alisema Serikali inaendeleza miradi mengine ya kisasa itakayotoa faida nyingi kwa Serikali na watu wake ikiwemo miradi ya maeegesho ya gari ya kisasa kwenye eneo la mji wa Darajani.
Mmoja wa mwakilishi kutoka kampuni ya Africab ambao ndio wajenzi wa mradi wa Darajani Souk, Yussuf Azzi alipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya nane kwenda kasi kimaendeleo na kueleza kwamba ni awamu yenye upeo unaoona mbali zaidi na kufikiria utekelezaji wa maendeleo ya miaka ya mbele zaidi nakuongeza kuwa eneo la maduka ya Darajani Souk ni sehemu yenye mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.
Eneo hilo la maduka ya Darajani Souk awali lilijuulikana kama eneo la makontena ambapo kwa wakati huo kulikuwa na makontena 58 yalibeba wafanyabiashara 168 na sasa eneo hilo limetolewa maduka 445 ambalo linatarajiwa kuhudumia wafanyabiashara wengi zaidi.
IDARA YAMAWASILIANO – IKULU, ZANZIBAR
Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Akabidhi Sadaka kwa Watoto wa Kituo cha Yatima Mwandaliwa Jijini Dar es Salaam
DC Mohammed Moyo Akabidhi Msaada wa Chakula Kilo 400 Kwa Wazee Wenye Ulemavu wa Kuona
Na Fredy Mgunda, Nachingwea
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametoa msaada wa chakula kilo 400 kwa wazee wenye ulemavu wa kuona katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati kutoka na kukabiliwa na uhaba wa chakula kwa wazee hao.
Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ametoa msaada huo kufuatia ombi la wazee wenye ulemavu wa kuona kumuomba awasaidie chakula.
Alisema kuwa akiwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea anapaswa kuchangia misaada pale inapowezekana hivyo aliguswa na wazee hao ndio maana akatafuta chakula hicho na kuwapelekea walemavu hao wa macho katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati.
Moyo aliishukuru benki ya NMB kwa kuchangia msaada wa chakula kwa wazee wenye ulemavu wa kuona kwa kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo kusaidia chakula ambacho walikuwa na uhitaji nacho.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alimazia kwa kuwaomba wadau wengine kuwasaidia wazee wenye ulemavu wa kuona chakula na huduma nyingine kwa kila mtu ni mzee ajaye .
Kwa upande wao baadhi ya wazee wenye ulemavu wa kuona walimshukuru mkuu wa wilaya ya Nachingwea na benk ya NMB kwa msaada wa chakula kilo 400.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Maryam Mwinyi aongoza matembezi ya kupiga vita vitendo vya udhalilishaji
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation. Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiongoza Matembezi ya Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na Kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, akiwa na baadhi ya Watoto wakishiriki matembezi hayo yaliyoazia katika eneo la Kendwa na kumalizika katika viwanja vya mpira vya Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi Omary na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud .(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akishiriki katika mazoezi ya pamoja ya viungo baada ya kumaliza kwa Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, mazoezi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 19-2-2023, na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli za Msingi za Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakiwa na mabongo yenye ujumbe wa “Udhalilishaji kwa Watoto haukubaliki” wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwahutubia katika viwanja vya mpira vya Nungwi, wakati wa Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Fujoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, akihutubia katika viwanja vya mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja, baada ya kumaliza Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwahutubia Wananchi katika viwanja vya mpira vya Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja, baada ya kumaliza kwa Matembezi ya Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto yalioazia katika eneo la Kendwa na kumalizia kwa mazoezi ya pamoja ya viungo na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli za Msingi za Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, iliyofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi leo 19-2-2023.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwake) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Lela Muhammed Mussa na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar.Mhe. Riziki Pembe,wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli za Msingi za Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, iliyofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi leo 19-2-2023.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwagaia zawada Wanafunzi wa Skuli za Msingi za Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji kwa Watoto na kuadhimisha Mwaka mmoja wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, yaliofanyika katika viwanja vya mpira vya Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja leo 19-2-2023.(Picha na Ikulu)
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Marais na Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Addis Ababa, Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 19 Februari, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa aliyeambatana na ujumbe wake Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 19 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 19 Februari, 2023.
Washindi wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari wa takwimu za wanawake na uongozi kujulikana 25 Febuari, 2023
ChamachaWaandishiwaHabariWanawakeTanzania,Zanzibar(TAMWA,ZNZ),kwakushirikiananaJumuiyayaWanasheriaWanawakeZanzibar(ZAFELA)naJumuiyayaMazingira,JinsianaUteteziPemba(PEGAO)Jumamositarehe25Febuari,2023zimeandaahaflaya utoajituzo maalum za umahiri wa uandishi wa habari za takwimuzinazohusu masuala yawanawakenauongoziZanzibarambayoitafanyikakatikaukumbiwaSheikhIdrissAbdulWakil
–Kikwajunikuanziasaa 1:00usiku.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DkHusseinAliMwinyikatikahaflahiyoambayoinategemewakuhusisha zaidiyawatu150.
Kaulimbiuyatunzohizoni“KALAMUYANGUMCHANGOWANGUKWAWANAWAKE”na ina lengo la kuimarisha kada ya habari katika eneo mahsusi la takwimu za wanawake hivyokuwashajiisha waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuandika kwa weledi na umahirimasuala yawanawakenauongozi.
Waandishi wa habari ni watumuhimu katika kuleta mabadiliko, hivyo wana nafasi kubwa yakushajihisha kufikiwa kwa usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi ikiwa wataandikahabari zatakwimunauchambuzimfululizo.
Kazi zilizopitiwa zilikuwani 421 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti,redio,televisheni pamojamitandao yakijamii.
KazizilizowasilishwazilitakiwaziwezimetolewaaukurushwahewanikuanziaJanuari2022hadiDisemba 31, 2022 na ziwe zimezingatia umahiri wa uandishi na uandaaji bora wa vipindi namakala ikiwemo ubunifu, vyanzo vingi na tofauti vya habari, zenye kuweza kuleta mabadiliko,kutoasuluhishopamoja na kupanga kwa umakinitakwimuza wanawake na uongozi.
Jumla ya washindi 12 wanatarajiwa kutunukiwa zawadi katika usiku huo maalum; mshindi wakwanza, wa pili na wa tatu baada ya kupitiwa na jopo la majaji watano wataalamu wa masualambali mbali yakiwemo, habari za magazeti, kielektroniki, mitandao ya kijamii, masuala yawanawake nasheria.
Shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbali mbali kutoka katika taasisi za Serikali,habari,vyuovikuu,vyamavya siasa,asasiza kiraiana wadauwamasuala ya wanawake.
Kazi za washindi zitatangazwa na kuoneshwa kwa lengo la kuwahamasisha waandishi na wadauwa habarikujifunza na kutafuta njia za kuimarisha kazizawanwake na uongozi.
Hii ni mara ya pili kufanyika kwa tuzo hizo za takwimu za wanawake na uongozi chini ya mradiwa KuinuaWanawawake katika Uongozi (SWIL)Zanzibakwa mashirikiano na Ubalozi waNorwaynchini Tanzania.
Watendaji wa Dawati la Kijinsia Kufanya Kazi Zao kwa Ushirikiano na Uaminifu - Bi.Siti
Na Maulid Yussuf WMJJWW. Zanzibar
Matukio 504 ya Udhalilishaji Yaliripotiwa Zanzibar
JUMLA ya matukio 504 ya udhalilishaji yaliripotiwa Zanzibar nzima kwa kipindi cha miezi mitatu, kutoka Novemnba 2022 hadi mwezi Januari, 2023 ambayo yalihusisha vitendo vya ubakaji, kulawiti, vipigo kwa watoto na udhalilishaji wa kijinsia.
Miongoni mwa matukio hayo 41 pekee yaliripotiwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kipindi hicho.
Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi alitoa takwimu hizo alipozungumza na watoto, wazazi, walezi, walimu na viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja alikojumuika nao kwenye matembezi ya kupinga vita dhidi ya udhalilidhaji.
Aliposhiriki matembezi ya kupinga vita dhidi ya udhalilishaji
Mama Mariam Mwinyi alisema matukio hayo ni mengi na yanazidi kila uchao hivyo, alivitaka vyombo vya sheria kutekeleza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutowaachia huru watuhumiwa wa makosa ya udhalilishaji nchini.
“Tunawaomba sana Jeshi la polisi wasiwatoe hawa watu wanaotuhumiwa kwa makosa ya udhalilishaji” Kwa hisia alisisitiza Mama Mariam.
Mwenyekiti huyo wa Zanzibar Maishabora Foundation, aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mashauri ya udhalilishaji, kuonhgeza mahakimu 10, majaji watatu ambao wameongeza idadi ya majaji kwa Majakama kuu kufikia 12 pamoja na kuajiri makaadhi wanne wanaoshughulikia mashauri ya familia.
Aidha, alipongeza hatua ya Serikali kwa kuzuia dhamana kwa watuhumiwa wote wa makosa ya udhalilidhaji.
Akizungumzia masuala ya vipigo kwa watoto, aliwasihi wazazi/walezi na walimu wa skuli na madrsa kutowaadhibu watoto kwa kipigo chenye kupitiliza na kuwataka watumie busara ya kuwapa adhabu zenye huruma badala ya kuwazuru kwa vipigo vikali.
“Hatupingi watoto kuchapwa wanapokosea, sababu ni sehemu ya ulezi na makuuzi yao lakini isiwe vipigo vyenye kupitiliza” alionya Mama Mariam Mwinyi.
Pia aliwasihi walimu na wazazi/walezi hao kuweka tabia ya kuwasikiliza watoto/wanafunzi kwani kunawengine hupitia ukatili mkubwa lakini kutokana na hofu kwa wanayoyapitia kwenye jamii zao huogopa kusema wanapokua majumbani ana skuli kwa walimu wao.
Mama Mariam Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwaeleza watoto kuvunja ukimya badala yake wawe jasiri kuzungumza kwa yanayowatokezea, ikiwemo vitisho, vipigo, kunyanyaswa kwa namna yoyote iwe na watu wazima au watoto wenzao wawe tayari kuzungumza badala ya kuweka usiri ili jamii iwasaidie.
Pia aliwataka kuwa makini na watu wakaribu na familia zao, wakiwemo walezi, jirani na jamii wanayoishi nayo hata kwenye mazingira wanayosomea kwa kutotoa fursa ya mtu yeyote kushika miili yao kwa namna yoyote.
Alisema matukio mengi ya udhalilishaji nayoripotiwa kwenye vyombo vya sheria yanahusisha watu wa karibu na familia na jamii ya watoto inayowazunguruka.
“Msiruhusu watu washike miili yenu, msiruhusu kukoshwa na mtu asiekua mama yako au kuvaa nguo mbele za watu, mujitahidi kuheshimu miili yenu, hata wakati wa kuvaa nguo jitahidi uwe peke yako kuutunza mwili wako.” alisihi Mama Mariam.
Pia Mama Mariam alikemea tabia ya baadhi ya wazazi/walezi kuwabusu watoto midomoni nakueleza kwamba tabia hiyo inachochea viashiria vya udhalilishaji nakuongeza ni chanzo cha maambukizi kwa baadhi ya maradhi.
Katika hatua nyengine Mama Mariam Mwinyi aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada ya kuimarisha sekta ya elimu nchini kwa kuongeza skuli mpya nchi nzima na kukarabati za zamani hali iliyopunguza msongamano wa wanafunzi mashuleni.
Naye, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia Wanawake na Watoto, Riziki Pembe Juma aliwataka wanaume kwa nafasi na dhamana zao kuungana na jamii kuendelea kuwalinda na kuwastahi watoto, kukemea na kuwa msatari wambele kupinga udhalilishaji wa kijinsia.
Alieleza matukio mengi ya udhalilishaji wa kijinsia yakiwemo ubakaji, kulawiti, kutelekeza na kutorosha wasichana wanaume ndio wahusika wakubwa wa vitendo hivyo.
Hata hivyo, aliipongeza Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation kwa kuungamkono juhudi za Serikali kwa kuendelea kuwa bega kwa bega kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika harakati zake.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mahmoud alisema, Mkoa huo wanaendelea kupambana na ongezeko la vitendo hivyo, kwa kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza na kutokomeza udhalilishaji, ikiwemo ya kuongeza uelewa kwa jamii yakiwemo makundi ya wavuvi ambao wanalalamikiwa sana kwa kutelekeza familia wanapokua dagoni, elimu kwa wakulima na vyombo vya ulinzi na usalama, madrasa na mashuleni.
Alieleza mkoa pia umewafikia watu wenye ulemavu kuwa nao karibu kuwalinda na kuwathamini na kutoa uelewa kwa jamii juu ya kushirikiana nao kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.
Alisema licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya mkoa huo kupinga udhalilishaji bado suala la muhali mkoani humo ni changamoto sugu, nakueleza kwamba wanawake na watoto wanaathiriwa zaidi na masuala ya ubakaji, kulawiti, kutorosha, shambulio la aibu, kukashifu, mvutano wa malezi, shabulio la kuumiza mwili, dawa za kulenya pamoja na mashambulio ya hatari
Aidha, alieleza ndoa za umri mdogo huongeza talaka nyingi mkoani humo, hali inayochangia kushindwa kuhimili familia na watoto, pia alieleza serikali ya mkoa imejitahidi kuzibiti maundi maovu na kufanya ziara za kustukiza maeneo yenye vichocheo vya mporomoko wa maadili.
Matembezi ya kupinga vita dhidi ya udhalilidhaji yaliandaliwa na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation yakiwa na kaulimbiu “Mimi ni shujaa, nitaulinda mwili wangu na kuutunza” yalikwenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tokea kuzinduliwa kwa taasisi hiyo.
Taasisi za Dini na za Kiraia Zinamchango Mkubwa kwa Serikali Katika Jukumu la Kuendeleza Amani
Alisema taasisi za dini zina jukumu la kutoa huduma za kiroho, zinasaidia kujenga taifa lenye amani, mshikamano na maadili kwa jamii jambo linaloimarisha amani na maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, jimbo kuu la Kusini mwa Tanzani, Dkt. Godwin Lekundayo aliyefika na uongozi wake kujitambulisha.
Alisema taasisi hizo zimekua na ushirikiano mzuri na Serikali katika ustawi wa jamii bora na kustawisha mshikamano wa imani za kiroho katika kukuza vijana waadilifu.
Amani utulivu, umoja na maridhiano ni mambo ya msingi katika nchi yoyote na kuongeza kuwa amani inapokosekana mambo mengi hushindikana kutekelezwa kwa wakati unaostahiki yakiwemo maendeleo hata uhuru wa kufanya ibada.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza viongozi hao kwa kuendelea kuhubiri na kuhamasisha amani kwa imani zao na kueleza licha ya taifa kuwa na mchanganyiko wa waumini wenye imani tofauti lakini linasonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo, alizitaka taasisi hizo za dini kuendelea kuisaidia Serikali kulea taifa lenye uadilifu na vijana watiifu ili kujenga taifa lenye viongozi bora.
Naye, Askofu Mkuu wa Kanisa la Sabato Tanzania, Dkt. Godwin Lekundayo alisifu juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyopiga ndani ya kipindi cha muda mfupi wa na kuzipongeza Serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwa kuimarisha umoja na mshikamano bila kujali tofauti za imani za wananchi.
Wakati huo huo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alishiriki halfa ya ufunguzi wa ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Zanzibar ambapo Balozi Mdogo wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Saleh Al Hemeir aliwakaribisha wananchi wa Zanzibar kwenye ofisi hizo kuhudumiwa masuala mbalimbali ya kidiplomasia.
Alisema taasisi za dini zina jukumu la kutoa huduma za kiroho, zinasaidia kujenga taifa lenye amani, mshikamano na maadili kwa jamii jambo linaloimarisha amani na maendeleo.
RaisDk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, jimbo kuu la Kusini mwa Tanzani, Dkt. Godwin Lekundayo aliyefika na uongozi wake kujitambulisha.
Alisema taasisi hizo zimekua na ushirikiano mzuri na Serikali katika ustawi wa jamii bora na kustawisha mshikamano wa imani za kiroho katika kukuza vijana waadilifu.
Amani utulivu, umoja na maridhiano ni mambo ya msingi katika nchi yoyote na kuongeza kuwa amani inapokosekana mambo mengi hushindikana kutekelezwa kwa wakati unaostahiki yakiwemo maendeleo hata uhuru wa kufanya ibada.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza viongozi hao kwa kuendelea kuhubiri na kuhamasisha amani kwa imani zao na kueleza licha ya taifa kuwa na mchanganyiko wa waumini wenye imani tofauti lakini linasonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo, alizitaka taasisi hizo za dini kuendelea kuisaidia Serikali kulea taifa lenye uadilifu na vijana watiifu ili kujenga taifa lenye viongozi bora.
Naye, Askofu Mkuu wa Kanisa la Sabato Tanzania, Dkt. Godwin Lekundayo alisifu juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyopiga ndani ya kipindi cha muda mfupi wa na kuzipongeza Serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar kwa kuimarisha umoja na mshikamano bila kujali tofauti za imani za wananchi.
Wakati huo huo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alishiriki halfa ya ufunguzi wa ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Zanzibar ambapo Balozi Mdogo wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Saleh Al Hemeir aliwakaribisha wananchi wa Zanzibar kwenye ofisi hizo kuhudumiwa masuala mbalimbali ya kidiplomasia.
CCM Yaipongeza ZIPA
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema kimeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika eneo la uwekezajikupitia Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar(ZIPA).
Kauli hiyo ameitoa jana Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCMZanzibar Khamis Mbeto Khamis mara baada ya kufanya mazungumzo naMkurugenzi Mtendaji ZIPA,Shariff Ali Shariff ofisini kwake Maruhubi.
Alisema ZIPA imetekeleza kwa kiasi kikubwa azma ya Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ya kuwavutia wawekezaji ambapo miradi mingi tayari imekwishawekezwa kwa kipindi kifupi.
"Eneo la uwekezaji ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar hivyo niwapongeze ZIPA kwa kazi nzuri mnayoifanya na kasi kubwa mnayoitekeleza ya ilani ya chama chetu,"alisema
Katibu huyo aliitaka ZIPA kuendelea kufanya kazi kwa karibu na CCM ili kufikia malengo ya ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wazanzibari.
Naye, Mkurugenzi wa ZIPA Sharif Ali Sharif, alisema, mwekezaji anapotaka kuwekeza anapewa masharti kwa kuhakikisha anazingatia mazingira ya uwekezaji yenyewe.
Alisema kwa sasa ZIPA imekuwa na uwekezaji wa miradi mikubwa 226 ambayo inaweza kuzalisha dola za kimarekani bilioni 3.5 ambapo inatengeneza ajira zaidi ya 13000.
"Katika kipindi cha miaka hii miwili ya serikali ya awamu ya nane ZIPA kupitia serikali tumetekeleza ilani kwa vitendo jambo ambalo imeonyesha dhamira kwa serikali kuhakikisha uchumi unaongezeka,"alisema
Alisema katika kipindi cha miaka miwili wawekezaji wameongezeka kutokana na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Rais, Dk. Mwinyi kutokana na kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji.
"Rais Dk.Mwinyi ameiimarisha ZIPA kiutendaji kwani Mamlaka hii imekuwa na watendaji wenye uwezo mkubwa wa kitaalamu katika kuwavutiawawekezaji na pia wameweka sheria ambayo ni rafiki zaidi kwa wawekezaji,"alisema
Alisema kupitia miradi hiyo zimepatikana ajira mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha uchumi wa unaongezeka kwa asilimia kubwa.
Pia, alisema uwekezaji umeongezeka kutokana na serikali kuanzisha kituo cha pamoja ambacho kinatoa huduma zote kwa wakati mmoja ambapo wawekezaji wamekuwa wakirahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa
wakati.
Akizungumzia upande wa visiwa, Mkurugenzi Sharif, alisema, kibali kinachotolewa kwa muwekezaji hupewa masharti ya asilimia 10 ya eneo husika na asilimia iliyobakia hupewa masharti ya kujenga ndani ya eneo
la baharini ili kuona visiwa hivyo havihathiriki na uwekezaji huo.
Mkurugenzi huyo alisema katika uwekezaji huo,muwekezaji utanguliza fedha kabla ya kuwekeza ambapo kwa sasa serikali imeshaingiza dola za kimarekani milioni 14 ambapo katika miradi ya visiwa hivyo inatakiwa kuingiza dola za kimarekani milioni 19.
"Wawekezaji hawa wamekuwa wakilipa kwa awamu na fedha zilizoingia zipo na zitatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kulipwa fidia watu waliokuwepo katika bahari ikiwemo wavuvi, na wawekezaji ambao
hawakufikia vigezo tunavyovitaka," alisema
Akizungumzia suala la viwanda ndani ya visiwa vidogo alisema, katika uwekezaji huo kutotakiwa uwekezaji wa viwanda vikubwa na kwamba viwanda vinavyotakiwa ni vya kati na vyepesi ambavyo vitakuwa na
thamani kubwa.
Mbali na hilo,alisema ZIPA itaendelea kutekeleza ilani ya CCM katika utendaji wao wa kazi wa kila siku na kufuata miongozo ya Rais Dk.Mwinyi juu ya uwekezaji nchini.