Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36129 articles
Browse latest View live

Muuguzi asimamishwa kazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja

$
0
0

Mwenyekiti Baraza la Wauguzi na Wakunga  Zanzibar Profess Amina Abdul-qadir Ali akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na hatua ya kusimamishwa kazi kwa  Mfanyakazi wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.
Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya Maadili Baraza la Wakunga na Wauguzi Zanzibar (kulia) Zainab Hassan akitolea ufafanuzi juu ya maadili ya Ukunga na Uuguzi wakati wa mkutano wa Waandishi wa Habari uliohusiana na hatua ya  kusimamishwa kazi kwa Mfanyakazia wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar Salum Mohammed  Abdalla akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kwenda kinyume na Maadili ya kazi wakati wa mkutano wa Waandishi wa Habari uliohusiana na hatua ya kusimamishwa kazi Mfanyakazia wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.

Na Rahma Khamis Maelezo                      21/2/2023

Wauguzi na Wakunga hapa nchini wametakiwa kuwa na maadili mema na lugha nzuri wakati wanapowahudumia wagonjwa ili kuondoa malalamiko katika jamii.

Wito huo umetolewa leo katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja na Mwenyekiti wa Baraz la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Prof Amina Abdulkadir Ali katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na taarifa iliyotolewa na  mawiyo kuhusu Muuguzi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutowajibika ipasavyo kwa mzazi aliefika hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua.

Amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo si kitendo cha kiungwana kwani kimechafua mwenendo mzima wa wauguzi na kuitia doa hospitali jambo ambalo linarejesha nyuma jitihda za Serikali ya kuwapati huduma bora wananchi wake.

Amefahamisha kuwa miongoni mwa kazi za baraza la wauguzi na wakunga ni kupokea malalamiko kwa wananchi na kuyachunguza baadae kuchukua hatua ikiwemo kupewa onyo au kusimamaishwa kazi.

Prof Amina ameeleza kuwa katika hatua walizozichuka kwa mfanya kazi huyo ni kumsimamisha kazi kwa muda wa miezi sita bila ya malipo na endapo atafanya tukio jengine atachukuliwa hatua kubwa zaidi ikiwemo kunyang’anywa leseni ya kufanyia kazi sehemu yeyote.

Akizungumzia suala la nidhamu Prof huyo amesema baadhi ya wauguzi hawana maadili mazuri kwani lugha wanazotumia hazipendezi kwa mgonjwa kwani mgonjwa akenda kwake lazima amhudumie.

“iwapo mgonjwa ataletwa katika kitengo chako muuguzi au daktari alieyepangwa kazi ndie dhamana wa pale hivyo ni wajibu wake kumsaidia mgonjwa huyo kwa kumpatia huduma stahiki na endapo litatokea lolote juu ya mgonjwa basi atahusika,”alisema Mwenyekiti huyo.

Nae Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Salim Khamis Abdala amesema kuwa wamechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi hasa katika kada hiyo.

Aidha amefahamisha kuwa kwa mujibu wa sharia kifungu no 23 baraza limepewa uwezo wa kumsimamisha kazi au barua ya onyo mfanya kazi yeyote alienda kinyume na maadili na sharia ya kazi.

Kwa upande wake Mjumbe ambae pia ni Mwenyekiti wa Maadili katika Baraza hilo Zainab Hassan amewashauri wafanya kazi kubadilika na kushirikiana kwa pamoja kati ya wauguzi na wahudumu kwa Imani ili kufikia malengo.

 


Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Akutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Shakhboot Bin Nahyan, Ikulu Tunguu, Zanzibar

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mtukufu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 21, Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mtukufu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 21, Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mtukufu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan aliyeambatana na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 21, Februari, 2023.

ZMBF Inatekeleza kwa Vitendo Sera ya Uchumi wa Buluu

$
0
0

Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe,Mama Mariam Mwinyi (kulia) akisikiliza Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Rehema Omary Sombi,(wa pili kulia) alipokuwa akitoa shukurani baada ya mazungumza na Viongozi wa Ngazi ya Taifa UVCCM waliofika kujitambulisha katika Ofisi ya Taasisi hiyo Migombani Jijiji Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe,Mama Mariam Mwinyi (katikati) alipokuwa aki zungumza na Viongozi wa Ngazi ya Taifa UVCCM waliofika kujitambulisha katika Ofisi ya Taasisi hiyo Migombani Jijiji Zanzibar  wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Rehema Omary Sombi,(wa pili kulia)
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe,Mama Mariam Mwinyi (kulia) akisikiliza Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Rehema Omary Sombi,(wa pili kulia) alipokuwa akitoa shukurani baada ya mazungumza na Viongozi wa Ngazi ya Taifa UVCCM waliofika kujitambulisha katika Ofisi ya Taasisi hiyo Migombani Jijiji Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe,Mama Mariam Mwinyi alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa  mazungumzo na Viongozi wa Ngazi ya Taifa UVCCM waliofika kujitambulisha katika Ofisi ya Taasisi hiyo Migombani Jijiji Zanzibar  wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg.Rehema Omary Sombi (hawapo pichani).

Na Mwashamba Juma.                                                                                                            

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amesema taasisi hiyo inatekeleza kwa vitendo Sera ya Uchumi wa Buluu ya Serikali ya awamu ya nane ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo kwenye ofisi za taasisi hiyo, Migombani Wilaya ya Mjini alipozungumza na ugeni kutoka jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM waliofika kumtembelea.

Alisema tokea kusajiliwa kwa ZMBF Febuari 19 mwaka jana ambayo kwasasa imetimiza mwaka mmoja, wanajivunia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Sera za Serikali kwa vitendo hasa sera ya Uchumi wa Buluu.

Alisema dhana ya Uchumi wa buluu kwa taasisi ya ZMBF imejikita kwenye harakati za kuwasaidia na kuungamkono juhudi za kinamama wanaojitoa kupigania maendeleo ya kiuchumi kupitia matunda ya baharini.

Alisema ZMBF imefanikiwa kuwafikia kinamama wengi Unguja na Pemba wanaujishughulisha na kilimo cha mwani na kueleza asilimia 90 ya ukulima huo hushirikisha kinamama.

Alisema katika jitihada za kuwaungamkono, ZMBF imewasaidia vifaa mbalimbali vya uvuvi kinamama hao ikiwemo boti zenye mashine, viatu vya kuvalia baharini, mashine za kusagia mwani zenye uwezo wa kusaga mwani mwingi kwa wakati hali iliyowasaidia kinamama hao kuongeza ufanisi wa kazi zao na kuwaongezea kipato kwa kukabiliana vyema na soko la bidhaa hiyo.

“Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, siku hizi kinamama hufanya shughuli za kilimo cha mwani nje kidogo na usawa wa bahari kutokana na kina cha maji ya bahari wanayolimia tofauti na zamani walilima maeneo karibu hivyo, ZMBF imeona haja ya kuwasaidia vifaa kimama hao, hususani boti zenye mashine kwaajili ya kuvukia na shughuli zao za baharini pamoja na viatu kwa usalama wanapokua baharini” Alifafanua Mama Mariam.

Mama Mariam ambae pia ni Mlezi wa Matembezi ya UVCCM ya Mapinduzi ya Zanzibar aliwaeleza vijana hao kwamba pia ZMBF imejita kwenye harakati za utunzaji mazingira kwa kuishajihisha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha usafi.

Alisema katika harakati hizo, ZMBF inajishughulisha na utengenezaji wa taulo za kike za kufua na kuhifadhi baada ya matumizi, ambazo huwasaidia wasichana mashuleni hasa wale wanaotoka kwenye mazingira magumu ambao hawana uwezo wa kuhimili taulo za kawaida.

Aidha, alieleza taulo za kawaida ambazo hutupwa baada ya matumizi huchangia wimbi la uchafuzi wa mazingira na kueleza kwama nyingi husalia kutupwa baharini na kuathiri viumbe vya bahari.

Akizungumzia tatizo la magojwa yasiyoambukiza yanayoendelea kuiathiri jamii, Mama Mariam Mwinyi alieleza ZMBF imekua ikishajihisha jamii kufanya mazoezi na kuambatana nao kwenye makongamano mbalimbali yanayohusisha matembezi ya hiari ambayo husaidia jamii kufanya mazoezi ili kujiepusha na kujinginga na maradhi hayo yakiwemo, presha, kisukari matatizo ya moyo na saratani.

Kuhusu suala la udhalilishaji wa kijinsia, alieleza ZMBF inakerwa zaidi na vitendo hivyo ambavyo huwaathiri zaidi wanawake na Watoto, alisema licha ya harakati nyingi zinazofanya na taasisi hiyo kwa kuwagusa moja kwa moja kinamama, vijana, wasichana na Watoto suala la udhalilishaji wamekua wakilikemea kwa nguvu zote na kulipiga vita.

Katika hatua nyengine Mlezi huyo wa UVCCM aligusia matayarisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwataka vijana hao kufanya maandalizi ya aina yake kwani vijana ni sauti ya Chama hasa kwenye kuimarisha mustakabali wa maendeleo na mabadiliko kwenye nyanja zote za siasa, uchumi na jamii.

“Kuna haja ya kukaa chini na kufikiria namna kutakavyoadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe ya aina yake, muje na fikra tofauti, UVCCM ije na kitu tofauti sababu vijana ndio injini ya Chama” aliwashajihisha vijana hao.

Naye, Makamu Mwenyekiti UVCCM taifa, Ndg. Rehema Sombi Omari (MNEC) kwa niaba ya ugeni alioambatana nao, waliipongeza ZMBF kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa kwa kipindi cha muda mfupi pia waliahidi kuwa balozi wazuri wa kukitangaza Chama na kupaza sauti zao kwa umma kuyasemea mazuri yote yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dk. Mwinyi na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi imara wa Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akilizungumzia jengo la UVCCM, ofisi ya Jimkana, Zanzibar alisema wanatarajia kulifanyia maboresho makubwa ili kueka alama kwa vizazi vijavyo kwamba UVCCM 2022 – 2077 ilifanya makubwa wakati wake. 

 

Benki ya CRDB Yaingia Mkataba wa Makubaliano na ICTC na COSTECH Kuwezesha Biashara Changa (STARTUPS) Nchini Kupitia Programu ya Imbeju

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya IMBEJU iliyojikita katika uwezeshaji wa wa biashara bunifu za wanawake na vijana kiuchumi, katika hafla iliyofanyika leo 20 Machi 2023 hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
 
Dar es Salaam 20 Februari 2023 – Katika mwendelezo wa kusaidia jitihada za Serikali kukuza ujumuishi wa kiuchumi nchini, Benki ya CRDB leo imeingia mkataba wa makubaliano na Tume ya TEHAMA (ICTC), na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia programu yake ya ‘IMBEJU’ iliyojikita katika uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi.
 
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ushirikiano na taasisi hizo za Serikali utasaidia kufanikisha malengo ya programu kwa kiasi kikubwa kutokana na jinsi uzoefu wa taasisi hizo katika kuwawezesha vijana wabunifu katika sekta mbalimbali.
“Ili kuifanya programu hii kuwa yenye ufanisi na kufikia walengwa wengi, tumeona ni vyema kutafuta wadau ambao wana mawazo kama yetu yaani “like-minded partners”.

ICTC na COSTECH wamekuwa wakifanya kazi nzuri ambayo inaakisi utayari wa Serikali yetu katika kukuza biashara na mawazo ubunifu, hivyo tunajivunia kwa hatua hii muhimu,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema mkataba wa makubaliano waliongia na Benki ya CRDB utakwenda kusaidia upatikanaji wa mitaji wezeshi kwa biashara changa katika sekta ya TEHAMA, pamoja na kutoa usaidizi wa kuboresha mawazo na biashara bunifu, jambo litakalosaidia kukuza ajira nchini.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu amesema makaubaliano waliyoaingia na Benki ya CRDB yanakwenda kuoanisha IMBEJU na programu za taasisi hiyo zinazochochea ubunifu wa kibiashara ikiwamo MAKISATU jambo litakalosaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa biashara changa katika sekta mbalimbali.

Katika hafla hiyo, Benki ya CRDB pia  iliutangazia umma kuanzishwa kwa taasisi isiyo ya faida ya “CRDB Bank Foundation” yenye jukumu la kuanzisha na kutekeleza programu bunifu, endelevu, na shirikishi zinazolenga kuleta ustawi wa kijamii, na kiuchumi kama ‘IMBEJU’.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alimtambulisha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa kama Mkurugenzi Mtendaji mwanzilishi wa taasisi hiyo ya CRDB Bank Foundation.

Akizungumza kwa mara ya kwanza kama Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Bank Foundation, Mwambapa amewataka vijana wabunifu kuchangamkia fursa inayotolewa na benki hiyo kupitia programu ya IMBEJU inayotekelezwa kwa kushirikiana na ICTC, na COSTECH.
“Mkataba tulioingia leo unatupa uwezo wa kushirikiana na ICTC na COSTECH kufanya utambuzi wa biashara changa bunifu zinazohitaji usaidizi. Niwaombe vijana kutumia mifumo ya utambuzi ya taasisi hizi ili kunufaika na fursa hii,” amebainisha Tully.

Mwambapa alitumia fursa hiyo pia kuwaalika vijana kushiriki semina maalum ya uwezeshaji iliyoaandaliwa na Benki ya CRDB tarehe 11 Machi 2023 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo programu hiyo itaingizwa sokoni rasmi, na uwezeshaji kuanza kufanyika. Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu (wapili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa wakionyesha mikataba ya makubaliano iliyosainiwa kati ya Benki ya CRDB, ICTC, na COSTECH kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya IMBEJU iliyojikita katika uwezeshaji wa wa biashara bunifu za wanawake na vijana kiuchumi, katika hafla iliyofanyika leo 20 Machi 2023 hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu (wapili kulia), Mkuruegenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa (wakwanza kulia), na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Startups Association, Zahoro Muhaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano kati ya Benki ya CRDB, ICTC, na COSTECH kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya IMBEJU iliyojikita katika uwezeshaji wa wa biashara bunifu za wanawake na vijana kiuchumi, katika hafla iliyofanyika leo 20 Machi 2023 hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.

Watoto Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu Wenye Ulemavu Wanaoishi Kituo cha "HOPES DISIABILITIES CENTER" na Shule za Kata ya Miono Chalinze Pwani Wafutwa Machozi na "TETE FOUNDATION"

$
0
0

Watoto wenye ulemavu na wasiojiweza wa Kituo cha Hopes kilichopo Miono Chalinze mkoani Pwani, wamefutwa machozi na Taasisi ya Tete (Tete Foundation) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Reliance na Benki ya DTB Tawi la Dodoma kwa kupewa msaada wa vitu vilivyokuwa changamoto kwao.

Tete Foundation na wadau wake walifika kwenye kituo hicho na kuwapatia watoto hao msaada wa vitu mbalimbali ambavyo awali vilikuwa changamoto kwao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Tete Foundation, Suzana Senso alisema kabla ya kufikiria kupeleka msaada kwenye kituo hicho walifanya utafiti na kugundua vituo vingi kama hivyo vinavyohitaji msaada lakini kituo hicho kinahitaji msaada zaidi.

Suzana amesema baada ya kubaini changamoto hiyo aliwasiliana na Kampuni ya Bima ya Reliance Tanzania Limited ambayo kwa uzalendo wake nao hawakusita kukubali ombi la kuwachangia msaada huo.

Suzana aliendelea kusema kuwa wengine waliomchangia ni Benki ya DTB Tawi la Dodoma ambao wote kwa pamoja aliwashukuru sana. Aliendelea kusema Suzana;

“Tunamshukuru Mungu siku ya leo ambayo imekuwa ni siku ya kipekee tukiwa tunakamilisha kampeni yetu iliyoitwa ‘Tunaamini Katika wewe’  wewe huku maeneo ya Miono Bagamoyo Chalinze mkoa wa Pwani tuliyoianzisha tarehe 9 Januari mwaka huu.

“Tunaposema tunaamini katika wewe ‘buku’ yako moja inakwenda kumgusa mtoto mmoja anayeishi katika mazingira magumu kwa kumnunulia peni au penseli.

“Tumekuwa na hii kampeni kwa karibia mwezi mmoja na nusu na leo ndiyo tumefikia kilele huku Miono. Lakini kikubwa zaidi tumeweza kuwapatia watoto hawa msaada mkubwa zaidi ya tulivyotarajia.

“Tunawashukuru wote waliojitoa kwa moyo wao wa uzalendo lakini shukrani za kipekee ziwaendee Reliance Isurance Tanzania Limited kupitia Benki ya DTB waliotuunganisha nao na kutuwezesha kutimiza lengo letu.

Pia tunawashukuru sana wale wote waliokuwa wakichanga zile elfu moja moja zao kupitia zile lipa namba zetu tulizokuwa tumeziweka kwenye mitandao ya kijamii.

“Nipende kutumia nafasi hii kumshukuru Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Reliance Insurance Tanzania Limited, Madam Rukia Goronga na msafara wake kwa kuonesha kujali zaidi na kutumia muda wao kuhudhuria tukio hili pia Meneja wa DTB Benki mkoa wa Dodoma ambaye ametumwa mwakilishi wake baada ya kupatwa na dharura Mungu ambariki sana.

“Nachukua nafasi hii kuwasihi wananchi wengine popote walipo wawakumbuke watoto kama hawa kwa maana tulivyotembea sehemu mbalimbali maeneo haya tulikuta watoto wa wakiwa na mahitaji mbalimbali na wengine kutumia daftari moja kuandikia masomo yote.

“Naibu Mkurugenzi wa Reliance Insurance, Rukia Goronga akizungumza kwenye hafla hiyo baada ya kujionea yaliyokuwa yakiendelea aliipongeza kampeni hiyo na kuahidi kampuni yake kuiunga mkono kwa siku zijazo.

“Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Miono na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mheshimiwa Juma Ramadhani ameipongeza Tete Foundation kwa kuichagua kata yake kutoa msaada huo na kuimbea kwa Mungu taasisi hiyo izidi kustawi na kuzidi kusaidia kata hiyo na sehemu nyingine.





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Amekutana na Kuzungumza na Uongozi wa UWT.

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe. Zainab Shomari.(kulia kwake) walipofika Ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo na kujitambulisha.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kusaidia vikundi vya  kina mama ili viweze kupata mikopo na kujikwamua kimaisha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) waliofika kujitambulisha Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Mhe. Hemed ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amesema Serikali inatoa Mikopo ya gharama nafuu kwa vikundi vya wajasiriamali kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuwaahidi kina mama kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa wanawake ili waondokane na utegemezi.

Mhe. Hemed ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali ni kuweza kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa urahisi na kuweza kujikimu kimaisha.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameupongeza Uongozi wa UWT kwa kuandaa mpango kazi ambao umelenga kuiletea mabadiliko Jumuiya hiyo hasa mpango wa kuanzisha vitega uchumi kwa kila Mkoa hatua ambayo itasaidia Jumuiya hiyo kuacha utegemezi katika kuendesha shughuli za kila siku.

Amesema,  Chama Cha Mapinduzi kimeelekeza kuboresha vitega uchumi na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa Jumuiya zake ili kurahisisha  uendeshaji wa shughuli za Chama za kila siku.

Pamoja na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea maendeleo watanzania ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Aidha Mhe. Hemed amewasihi viongozi hao kuwa wavumilivu na kutovunjika moyo kwa changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania  Bi. Zainab Shomari  amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa UWT imejipanga kufanya mabadiliko kwa kujiimarisha kimaendeleo kiutendaji, kisiasa na kiuchumi.

Aidha ameeleza kuwa Umoja wa Wanawake Tanzania umefurahishwa kwa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga Hospital zenye huduma za Mama na Mtoto hatua ambayo itasaidia kumaliza changamoto ya usumbufu wa kina mama wanapofata huduma hizo na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Dr Dimwa asisitiza mshikamano kati ya viongozi na wanachama

$
0
0

KADA wa Chama Cha Mapinduzi Ibrahim Raza(upande wa kulia), akimkabidhi kompyuta Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’ (upande wa kushoto), makabidhiano hayo yamefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa',amesema umoja na ushirikiano baina ya wanachama,viongozi na watendaji utasaidia kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya Chama.

Hayo ameyasema mara ofisini kwake Kisiwandui Mjini Unguja mara baada ya kupokea vifaa vya kompyuta kutoka kwa kada wa CCM Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza.

Alisema Chama Cha Mapinduzi kinaendeshwa kwa misingi ya kujitolea hivyo kila mwanachama ana haki na wajibu wa kutoa mchango wake wa hiari kwa nia ya kuimarisha chama.

Alieleza kuwa misingi hiyo imejengwa na waasisi wa CCM toka enzi za Chama Cha Afro-Shiraz Party(ASP),waliotoa michango mbalimbali kwa lengo la kujiimarisha kisiasa,kiuchumi na kijamii.

“Komputa hii itasaidia katika shughuli zetu za kiutendaji na tunakuahidi itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Tumeupokea msaada na tunaamini kuwa Ibrahim Raza ni kada mwaminifu wa CCM na kutupa msaada huu ni kwa mapenzi yake tu ya kuisaidia ofisi hivyo tunamshukuru sana”,alisema Dkt.Dimwa.

Alisema, kukiwa na makada kama hao na wakashirikiana kwa pamoja ni jambo zuri lakini vile vile chama kitawatumia kila mtu kwa nafasi yake na kila mtu kwa uwezo wake.

Kwa upande wake Kada huyo Ibrahim Raza, alisema kompyuta hiyo itakuwa ni chachu ya kuimarisha utendaji wa shughuli za Chama kwa wakati.

Raza ambaye ni mbunge wa zamani wa jimbo la Kiembesamaki, alimuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa, yupo tayari kufanya kazi na yeye na kwamba majukumu yoyote atakayopangiwa na Chama cha Mapinduzi.

Pamoja na hayo alisema ataendelea kuwa muumini wa kushiriki katika mikakati ya kuandaa mazingira ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2025.

 

Malezi kwa Watoto Yanahitajika ili Kuwasaidia kukua Katika Makuzi Bora

$
0
0

Na.Maulid Yussuf. ZANZIBAR

Mashirikiano ya malezi kwa watoto yanahitajika ili kwasaidia watoto kukua katika makuzi bora pamoja na kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji nchini. 

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Siti Abbas Ali ameyasema hayo katika muendelezo wa utoaji wa elimu juu ya masuala ya udhalilishaji katika shehia mbalimbali nchini.

Akizungumza katika shehia ya Mnarani Kijitoupele, Mkurugenzi Siti amesema bado wazazi wanaume wamekuwa wakiwaachia ulezi kina mama pekee hali ambayo inapotokea tatizo lawama pia zinawakuta wao.

Aidha amewataka wazazi kupunguza kuwakaripia ovyo watoto na badala yake kuwaweka karibu ili wanapofikwa na tatizo waweze kusema na kuweza ufuatilia.

Pia amewataka kupunguza hasira kwa kutowapa adhabu kubwa watoto wanapofanya makosa kwani baadhi yao wamekuwa wakiwachoma moto watoto jambo ambalo linaweza kumsababishia ulemavu wa maisha Mtoto huyo.

Hata hivyo amewanasihi wanaume kuwaunga mkono wanawake katika shughuli zao mbalimbali za kimaendeleo na hata wanapohitaji kugombea nafasi za uongozi ili kuleta mafanikio zaidi katika jamii.

Nae Sheha wa shehia ya Mnarani bwana Ramadhan Abdallah Rajab amewataka wananchi wa shehia hiyo kuwa karibu na ofisi zao za shehia kwani matukio mengi yanayofanyika yanatokea katika shehia, huku akiahidi kuendelea kutoa huduma bora katika shehia yake.

Kwa upande wao baadhi ya  wakaazi wa Shehia ya Mnarani wamewanasihi wazazi wenzao kutowapa simu watoto wao kwani ni miongoni mwa vichocheo vya kuwepo matendo ya udhalilishaji.

Vijana Watakiwa Kuzitumia Fursa Zilizopo na Zitakazotolewa na Serikali na Wadau wa Maendeleo - Dk.Hussein

$
0
0

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Mkurugenzi Mkaazi wa USAID Nchini Tanzania Bi. Kate Somvongsiri na (kushoto kwake) Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya T-Marc Bw.Alex Mgongolwa, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Kijana Nahodha Tanzania, uliozinduliwa viwanja vya mpira Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja leo 22-2-2023.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka vijana kuzitumia fursa  zilizopo na zitakazoletwa na Serikali na Wadau mbalimbali wa Maendeleo kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wao na Taifa kwa ujumla.

Alisema vijana ni nguvu kazi kwa taifa lolote duniani, ambayo inahitaji kuandaliwa vema kwa faida za baadae.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo huko Maisara Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi alipozungumza na vijana wa makundi tofauti kwenye uzinduzi wa mradi wa “Kijana Nahodha” unaofadhiliwa na Shirika la USAID la Marekani.

Alisema mradi huo unaunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kitaifa ikiwemo dira ya 2050, mpango wa taifa wa maendeleo 2026 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 -2025.

Alisema kundi kubwa la vijana duniani kote limekuwa likikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, mimba na ndoa za umri mdogo, UKIMWI, Afya ya Akili, ukatili na udhalilishaji wa kijinsia pamoja na matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Dk. Mwinyi alizitaka Wizara zote zinazoguswa na mradi huo kushiriki na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kuwaandaa na kuwasimamia vijana kuhakikisha shughuli watakazozianzisha zinakua endelevu hata baada ya kukamilika Mradi.

Akizungumzia mabaraza ya vijana Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasimamia uendeshaji wa Baraza la Vijana la Zanzibar kuanzia ngazi ya Shehia hadi taifa pia alisema baraza hili ni chombo kinachowaunganisha vijana nchini ili kupaza sauti zao kwenye masuala mbalimbali yanayohusu maslahi yao pamoja na kuchochea maendeleo ya jamii.

Alieleza mabaraza hayo yamechangia kuanzishwa vituo vya mafunzo ya vijana maeneo ya Bweleo na Pangeni kwa Unguja na Weni na Mjini Ole kwa Pemba kwa kuwaandaa vijana kupata maarifa na  umahiri wa kukabiliana na changamoto kwenye makuzi yao.

Akizungumzia fedha za  ahueni ya Uviko isiyo na riba, Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali ilitoa fedha hiyo kwaajili ya mikopo ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, kujenga vituo maalumu vya wajasiriamali kwa kila Wilaya pamoja na kuwapatia wananchi vifaa vya uvuvi zikiwemo boti na vifaa vyengine vya uvuvi wa kisasa, vifaa kwa wakulima wa mwani kwa vijana na kinamama. Alisema Serikali imeongeza uwekezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya binafsi, uimarishaji wa shughuli za uchumi wa buluu ikiwemo kuendeleza sekta ya utalii, kukuza uchumi wa nchi na kuongeza fursa za ajira ambazo vijana ni miongoni mwa walengwa wakuu.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita aliwaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuiungamkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwekeza zaidi kwenye miradi inayowahusisha vijana ili kuwakomboa na changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira wapate kujitegemea.

Naye, Mkuu wa Mradi wa Kijana Nahodha, Dk. Tuhuma Tuli alieleza mradi ni sekta mtambuka amabao utahusisha ajira kwenye sekta za elimu, kilimo, utawala bora na afya kwa unalengo la kuwajengea uwezo vijana wenye umri kati ya miaka 15-25.

Alisema mradi pia imelenga kuwajengea uwezo vijana, kuwasaidia upatikanaji ubora wa stadi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya ufundi, kuboresha uelewa wa afya ya akili kupitia zana za elimu ya kidijitali zinazoongozwa na watu binafsi na kuimarisha njia za wazi za mawasiliano kati ya vijana na serikali ili kuinua sauti za vijana katika maisha ya kiraia, siasa, na utungaji sera.

Kwa upande wake Mkururgenzi Mkazi wa USAID, Kate Somvongsiri alisema, kupitia mradi wa Kijana Nahodha, vijana watakuwa na uwezo wa kujifunza masuala mbalimbali, kuongeza maarifa na stadi za kuendesha biashara, misaada kutoka kwa familia zao, jamii, na serikali ili wapate fursa kupitia elimu.

Mradi wa Kijana Nahodha wenye kaulimbiu “Kijana Nahodha mpango mzima”. Unatarajia kuwafikia vijana 45,000 kwa Tanzania nzima ambapo kwa Zanzibar unatarajiwa kuwafikia vijana 15,000 Unguja na Pemba.

IDARA YA MAWASILIANO  IKULU, ZANZIBAR.

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA BWENI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MARY MAJALIWA WILAYANI RUANGWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akikagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondary Mary Majaliwa wilayani Ruangwa mkoa wa lindi Februari 21, 2023. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na wa nne kulia ni mkewe Mary Majaliwa.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokagua ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondary Mary Majaliwa wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi,
Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari, Mary Majaliwa wilayani Ruangwa  baada ya kukagua ujenzi wa bweni la wasichna shuleni hapo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango Azungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifanya Mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Manfredo Fanti, Mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2023. Kesho tarehe 23 Februari 2023 Makamu wa Rais anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya litakalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifanya Mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Manfredo Fanti, Mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2023. Kesho tarehe 23 Februari 2023 Makamu wa Rais anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya litakalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya Afrika Mashariki Manfredo Fanti mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2023. Kesho tarehe 23 Februari 2023 Makamu wa Rais anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya litakalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya Afrika Mashariki Manfredo Fanti mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 22 Februari 2023. Kesho tarehe 23 Februari 2023 Makamu wa Rais anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya litakalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

 

Wanafunzi wa KIST Wakiendelea na Mitihani ya Vitendo

$
0
0

Wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), wanaosoma fani ya Mechanical Engineering Diploma mwaka wa Pili, wakifanya Mtihani wa Vitendo  jinsi ya kuchoma vyuma ili kutengeneza maumbo mbali mbali  ikiwa ni miongoni mwa mitihani inayoendelea  katika Taasisi ya karume .


Wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), wanaosoma fani ya Automotive Engeering Diploma mwaka wa Pili, wakifanya Mtihani wa Vitendo  jinsi ya kutengeneza Gari ikiwa ni miongoni mwa mitihani inayoendelea  katika Taasisi ya karume .


CCM Zanzibar Yawasihi Wananchi Kuendeleza Utamaduni wa Kusoma Vitabu na Machapisho

$
0
0

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Ali Salum pamoja na Maafisa wa idara hiyo  wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani katika Maktaba Kuu ya Zanzibar iliyopo Maisara Unguja.
MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim, akieleza namna wanavyotoa huduma ya usomaji wa vitabu mbalimbali katika taasisi hiyo.
MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim, akieleza namna wanavyotoa huduma ya usomaji wa vitabu mbalimbali katika taasisi hiyo.

MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim(kulia), akizungumza juu ya muundo wa utendaji wa Maktaba hiyo baada ya Katibu wa Mkuu wa Idara ya SUKI Khadija Ali Salum (upande wa kushoto) kufika ofisini kwake kwa ajili ya ziara maalum ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar(SUKI) Khadija Ali Salum,amewasihi wananchi kuendeleza utamaduni wa kutembelea maktaba mbalimbali nchini ili kujifunza na kusoma vitabu ,machapisho,nyaraka na taarifa zitakazowaongezea maarifa na uelewa yakinifu.

Wito huo ameutoa katika ziara yake ya kutembelea Maktaba Kuu ya Zanzibar iliyopo mtaa wa Maisara Unguja.

Alisema wananchi wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu na machapisho mbalimbali ili wawe na uelewa juu ya mambo tofauti yanayohusu Zanzibar, Tanzania bara,Afrika na duniani kwa ujumla.

Katika maelezo yake Katibu huyo wa SUKI Khadija,alieleza kuwa Maktaba Kuu ya Zanzibar imehifadhi nyaraka,machapisho na vitabu mbalimbali vinavyosaidia kuwajengea uwezo wa kitaaluma wanafunzi wa ngazi mbalimbali za kitaaluma na kwamba wananchi nao wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

Kupitia ziara hiyo Khadija, aliahidi kuwa Chama Cha Mapinduzi kitatafuta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto za kiutendaji zinazoikabili taasisi hiyo ambayo ni chimbuko la kuhifadhi nyaraka muhimu za kitaaluma.

Alieleza kuwa licha ya kuwepo na changamoto za kiutendaji wafanyakazi wa taasisi hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waende sambamba na kasi ya utendaji wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.

Pamoja na hayo alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatia maazimio ya kikao cha kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kilichofanyika februari 20,mwaka 2023 hapo Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Alisema kuwa pamoja na majukumu yanayoikabili taasisi hiyo wanatakiwa kuongeza juhudi katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya maktaba kuu yaliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Maana halisi ya maktaba ni sehemu ya jengo lenye nyaraka au machapisho ya kujifunza na kujisomea hivyo kwa maana hiyo kila mwananchi ana wajibu wa kujiongezea maarifa kupitia maktaba hiyo.”alisema Khadija.

Naye Mkurugenzi wa Maktaba Kuu Zanzibar Mkurugenzi wa huduma za Maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-aziz Ibrahim, amesema wanatoa huduma mbalimbali za kuwasaidia wanafunzi na wananchi kwa ujumla kupata vitabu ili wajifunze na kupata taaluma,elimu na maarifa juu ya mambo mbalimbali yaliyowazunguka.

Alisema kupitia taasisi hiyo inayofanya kazi zake Unguja na Pemba wanahifadhi vitabu mbalimbali vikiwemo vya maalum za uchumi,sayanzi,maarifa ya jamii,diplomasia na ujasiriamali na mambo mengine yanayohusu viumbe hai na visivyo hai.

Alizitaja changamoto zinazowakabili katika maktaba hiyo kuwa ni pamoja na udogo wa jengo la maktaba hiyo pamoja na ukosefu wa vifaa vya huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).

Dkt.Ulfat, alizitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa huduma ya mtandao ‘Internet’, upungufu wa wakutubi na ukosefu wa usafiri kwa watendaji wa taasisi hiyo hasa wakati wanapokuwa na majukumu ya nje ya ofisi hiyo.

Kupitia ziara hiyo Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuhakikisha huduma za maktaba zinatolewa katika mfumo wa kisasa.

“Tunatoa huduma bora na rafiki kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla hivyo wananchi,wageni na wanafunzi wa ngazi tofauti milango yetu ipo wazi tunawakaribisha waje kujiongezea maarifa,elimu,taaluma na uelewa”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa baada ya Waziri wa Elimu Tanzania bara kupiga marufuku baadhi ya vitabu visivyozingatia maadili na kwa upande wa Zanzibar katika maktaba hiyo walifanya uchunguzi na kubaini uwepo wa baadhi ya vitabu hivyo na kuhakikisha wanaviondoka katika mfumo na taratibu za huduma ya usomaji.

Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Wapendezesha Uzinduzi wa Mradi wa Kijana Nahodha Viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja

$
0
0

Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Abdullatif na Mastura wakiwa katika vazi la asili la Zanzibar,  wakisoma utenzi maalum wa Uzinduzi wa Mradi wa Kijana Nahodha ukiwa chini ya Ufadhili wa USAID ya Marekani uzinduzi huo uliofanyika leo katika viwanja vya mpira Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo.22-2-2023. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapongeza Wanafunzi Abdullatif na Mastura kwa usomaji wa utenzi maalum wa Uzinduzi wa Mradi wa Kijana Nahodha, uliofanyika leo 22-2-2023 katika viwanja vya mpira Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dkt.Nchemba Akutana na Mkurugenzi wa AfDB

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Bw. Jonathan Nzayikorera, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Na Ramadhani Kisimba, WFM, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Bw. Jonathan Nzayikorera.

 

Dkt. Nchemba amekutana na Mkurugenzi huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaamakiwa safarini kuelekea Bujumbura nchini Burundi, kuhudhuria Mkutano wa 43 wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Masharikiutakaofanyika tarehe 23 Februari, 2023.

 

Bw. Nzayikorera amewasili nchini leo tarehe 21 Februari, 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku nneambapo pamoja na mambo mengine atakagua maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Bw. Jonathan Nzayikorera, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku nne.


Mradi wa Kijana Nahodha Fursa kwa Vijana Kujikomboa Kiuchumi

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifungua mlango kuashoroa kuzindua Mradi wa Kijana Nahodha inaofadhiliwa na USAID ya Marekani, uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya mpira Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana 22-2-2023.  









 

Naibu Waziri Khamis atoa maagizo mazito kwa Kamati za Ulinzi na Usalama, NEMC

$
0
0

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis akikagua mradi wa dampo la kisasa mradi wa dampo la kisasa lililojengwa katika Kata ya Buhongwa Wilayani Nyamagana jijini Mwanza wakati wa ziara yake

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis akipata maelezo kuhusu mradi wa dampo la kisasa mradi wa dampo la kisasa lililojengwa katika Kata ya Buhongwa Wilayani Nyamagana jijini Mwanza kutoka kwa Meneja wa Mradi huo Desderius Polle wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza kwa ziara ya Naibu Waziri kukagua miradi ya sekta ya mazingira mkoani Mwanza iliyoanza

Serikali imezitaka kamati za ulinzi na usalama katika Mikoa na Wilaya zote nchini pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuanzisha operesheni ya kuwaibaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria waagizaji na wasambazaji wa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na Serikali.

Agizo hilo limetolewa Februari 22, 2023 Jijini Mwanza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa dampo la kisasa lililojengwa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza.

Naibu Waziri Khamis amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kutokana na athari za mazingira na pia mifuko hiyo kuwa hatarishi kwa afya za wananchi, hata hivyo wapo baadhi ya watu wamekuwa wakikiuka katazo la matumizi ya mifuko hilo lililotolewa na Serikali mwaka 2019.

“Tumeona katika dampo hili la Buhongwa limekuwa ni kituo cha mifuko ya plastiki, hii imeonesha kuwa huko mitaani kuna watu wanaojishughulisha na biashara ya uagizaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki isiyo na ubora. Naziagiza Kamati za Ulinzi, NEMC na Mabaraza ya Halmashauri ya Wilaya kusimamia mianya yote inayopenyeza mifuko hii” amesema.

Aidha Naibu Waziri Khamis amesema nadharia za kisayansi zimedhibitisha kuwa mifuko ya plastiki inaathari kubwa kimazingira kutokana na kuchukua kipindi kirefu kutekeleza na kuoza kuanzia miaka mitatu na kuendelea na hivyo kuleta tishio kwa kubwa kwa maisha na ustawi wa viumbe na binadamu.  

Akifafanua zaidi amesema Serikali ya Awamu ya Sita kamwe haitorudi nyuma katika katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na kuwataka watu wachache wanaojishughulisha na biashara ya uagizaji na usambazaji wa biashara hiyo kuacha mara moja kabla ya kukamatwa na kufikishwa katika na mkono wa sheria. 

Katika hatua nyingine, Mhe.Khamis ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuanzisha mradi huo ambao utasaidia juhudi za Serikali za kutotumia fedha nyingi kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwa kuwa taka zinazozalishwa katika Jiji la Mwanza zitapelekwa kwa wakati katika dampo hilo na kunusuru magonjwa ya mlipuko.

Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa mapambano ya uharibifu wa mazingira na katika kudhibitisha kauli kwa vitendo ametoa sh.bilioni 3 kwa kila Halmashauri nchini kwa ajili ya kuanzia miradi ya ujenzi madampo ya kisasa ynayochakata taka kisayansi na kulinda afya za wananchi.

Akizungumzia ujenzi wa mradi wa dampo hilo, Meneja mradi wa dampo hilo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza Desderius Polle amesema ujenzi wa dampo lenye ukubwa wa hekta 34 uliokamilika mwaka 2020 una thamani ya sh.bilioni 8.9 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Programu ya Uendelezaji wa Majiji ya Kimkakati Tanzania (TSCP).

Polle amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa shimo la kuhifadhi taka ngumu lenye ukubwa wa mita za mraba 39,000, ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa Kilomita 0.7, ujenzi wa barabara ya changalawe yenye urefu wa kilomita 1.8, ujenzi wa bwawa la kuhifadhi maji ya mvua, ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua, upandaji wa miti na uwekaji wa taa za barabarani na maegesho ya mitambo na uchimbaji visima.

Naye Diwani wa Kata ya Nyamagana, Joseph Kabadi ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kusimamia vyema utekelezaji wa mradi wa dampo hilo la kisasa ambalo litakuwa suluhisho wa utunzaji wa mazingira kwa kuwa taka ngumu zitakuwa zikiteketezwa kwa wakati na hivyo kulinda za afya za wananchi wanaozunguka kata hiyo.

Naibu Waziri Khamis yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazohusu sekta ya mazingira nchini.

Benki ya CRDB yawapa ubalozi wachezaji wa Simba na Yanga kampeni ya Benki ni SimBanking

$
0
0
Mkurugenzi Mtenndaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Timu ya Yanga, Andre Mtine (wapili kushoto) na Afisa  Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba, Imani Kajura (wapili kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa makubaliano wa kuwatumia wachezaji Clatous Chama, Mohammed Hussein, Aziz Ki na Farid Mussa kutoka timu za Simba na Yanga kuwa mabalozi wa Benki ya CRDB katika kufikisha elimu ya fedha kwa jamii kupitia kampeni yake ya “Benki ni SimBanking”, hafla ya kusaini mikataba  hiyo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya  CRDB, jijini Dar es salaam. Wapili kulia waliosimama ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya  CRDB, Joseline Kamuhanda pamoja na wanasheria Hosea Samba (Timu ya Simba) , Simon Patrick (Yanga) na Danford Kisinda wa Benki ya  CRDB.
Dar es Salaam, Februari 22, 2023 – Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano na wachezaji Clatous Chama, Mohammed Hussein, Aziz Ki na Farid Mussa kutoka Simba na Yanga kuwa mabalozi wake wa kufikisha elimu ya fedha kwa jamii kupitia kampeni yake ya “Benki ni SimBanking.” Mikataba na wachezaji hao imesainiwa katika makao makuu ya Benki ya CRDB na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka Benki ya CRDB pamoja na vilabu vya Simba na Yanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki ya CRDB kwa muda mrefu imekuwa ikishiriki katika kusaidia jitihada mbalimbali za kimichezo kwa kutambua mbali ya kuwa michezo ni burudani, bali pia michezo ni biashara na uchumi pia. 
 
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Benki ya CRDB imeanzisha mbio za kimataifa za hisani za CRDB Bank Marathon, mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu ya CRDB Bank Taifa Cup pamoja na mashindano ya resi za Ngalawa ya CRDB Bank Ngalawa Race.
“Pamoja na juhudi zetu za kuwekeza katika michezo mingine lakini Benki ya CRDB pia imewekeza katika mchezo wa mpira wa miguu kupitia ufadhili ambao tumekua tukitoa kwa klabu ya Namungo lakini pia mwaka jana tulishirikiana na vilabu hivi vya Simba na Yanga katika maandalizi ya Simba Day pamoja na Wiki ya Mwananchi kama maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara” aliongeza Nsekela.

Benki ya CRDB imefikia hatua ya kusaini makubaliano na wachezaji hao wa Simba na Yanga ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza wigo wa ufahamu wa elimu ya fedha kwa wachezaji wa soka na jamii kwa ujumla lakini pia ikiwa pia ni sehemu ya kutambua viwango vizuri ambavyo vimeonyeshwa na wachezaji hao katika kusaidia timu zao kupata matokeo mazuri lakini pia nidhamu ambayo wameonyesha katika mchezo jambo ambalo ni muhimu sana kwa mafanikio ya mchezaji.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine ameishukuru Benki ya CRDB kwa kutoa ubalozi kwa wachezaji wao jambo ambalo litaleta hamasa kwa wachezaji wengine kuongeza juhudi jambo ambalo litaisadia klabu wakati huu inaposhiriki mashindao ya ndani nan je ya nchi. Mtine alisema Klabu ya Yanga inafarijika pia kuwa sehemu ya familia ya Benki ya CRDB kwa kusaidia kufikisha elimu ya fedha katika jamii, na kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tunaishukuru Benki ya CRDB kwa kuwatambua wachezaji wetu na kuwapa heshima hii kubwa ya kuwa mabalozi wao. Kwa kuwa mabalozi wa taasisi kubwa kama Benki ya CRDB kunaleta imani na hamasa hata kwa taasisi nyingine kutaka kushirikiana na wachezaji wetu jambo ambalo litanuifaisha sio tu wachezaji bali vilabu na soka letu kwa ujumla wake” alsema Mtine.
Akizungumza kwa upande wa klabu ya Simba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula na yeye amepongeza hatua ya Benki ya CRDB kuwatambua wachezaji wao na hasa kwa kuangalia mchango wao katika timu na nidhamu jambo ambalo ni muhimu kwa mafanikio yao na timu kwa ujumla. Aidha, aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo, na kuahidi kuendelea kushirikiana kupitia kampeni hiyo ya Benki ni SimBanking.

“Pamoja na kuwa mikataba hii inakwenda kuongeza kipato kwa wachezaji lakini kupata nafasi ya kupewa elimu ya fedha ambayo itawasaidia kwenye maisha yao wakati huu wanacheza soka la ushindani na wakati ambao watakua wamestaafu ni jambo kubwa na la kupongezwa kwani wachezaji wengi wameshindwa kunufaika na vipaji vyao kwa kukosa elimu ya fedha” aliongeza Kajula ambae amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za fedha nchini.

Clouts Chama ambae ni mmoja kati ya wachezaji waliosaini mkataba wa ubalozi wa Benki ya CRDB amesema kuwa mkataba huo utakua chachu ya kumfanya aongeze juhudi zaidi kukuza kipaji chake lakini pia kufanya yale yanayotakiwa katika mkataba kwani bila hivo ni ngumu kuendelea kuwapa sababu makampuni mengine kuvutiwa kufanya kazi naye.

Wadau wa Sekta ya Utalii Watakiwa Kuboresha Huduma Ziendani na Mazingira ya Wakati Uliopo Kukidhi Haja. - Dk.Hussein

$
0
0

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali katika Sekta ya Utalii “The Z Summit” , uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wadau kwenye sekta ya utalii kuboresha huduma ziendane na mazingira ya wakati uliopo ili kukidhi haja na mahitaji ya wageni wanaoitembelea Tanzania.

Dk. Mwinyi alieleza hayo alipofungua tamasha la utalii na biashara “The Z- Summit” huko ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa Ndege wilaya ya mjini.

Alisema sekta ya utalii Zanzibar nyenye vivuti vingi ni sekta muhimu inayochangia asilimia 30 ya pato la taifa.

Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanazibar imechukua jitihada mbalimbali kuimarisha sekta hiyo yenye lengo la kuongeza watalii kufikia 850, 000 ifikapo mwaka 2025 ambapo tayari imeimarisha miundombinu ikiwepo kutanua barabara za kisasa, kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume ambapo alieleza kwa sasa unatoa huduma za kimataifa zenye kukidhi haja ya mahitaji ya wageni chini ya uongozi wa taasisi ya kimaifaifa ya DNATA inayotoa huduma za kimataifa za viwanja vya ndege.

Alisema ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba unaotarajiwa kuifungua Pemba kiutalii ni miongoni mwa juhudi za sreikali kwenye kukuza sekta ya utalii nchini.

Alisema Zanzibar ni kituo cha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali ya dunia kilivyopambwa na magofu yaliyohifadhi historia pamoja na mji mkongwe uliokwenye hifadhi ya UNESCO inawavutia wageni wengi kupitia fukwe angafu, ubuluu wa bahari pamoja na ukijani wa visiwa vyake vilinavyopambwa na michezo ya baharini

Alieleza milango ya serikali ikowazi kuwakaribisha wawekezaji kuekeza kwenye michezo ya baharini ikiwemo gamu za baharini na michezo ya fukwe za bahari ikiewemo volleyball.

Akizungumzia Sera ya uchumi wa bluu na utalii Dk. Mwinyi alieleza Serikali imechukua jitihada kubwa kuitekeleza sera hiyo kwa vitendo iliwa pamoja na kutilia mkaazo suala la endelevu kupitia sera yake ya “utalii kwa wote”.

Aliahidi kuwa serikali itaendelea kuwawekeza mazingira mazuri wadau wote wa utalii na kuwaomba mkutano huo uwe chachu ya kutoa firsa nyingi kwa watalii na wadau wake. Hivyo alisema ni imani kwamba mkusanyiko huo ulioshirikisha wadau mbalimbali wa sekta utatoa mafanikio mazuri katika kuikuza sekta nchini.

“Sote kwapamoja tuungane kubadilishana uzoefu, kufanyakazi pamoja tutachangia kuikuza sekta ya utalii, Tanzania

Akizungumzia suala la kutunza mazingira endelevu, Rais Dk. Mwinyi alisema utalii ni chachu ya uchafuzi wa mazingira, hivyo aliitaka jamii, wadau wa utalii pamoja na wawekezaji kwenye sekta hiyo, kutunza mazingira na viumbe vya bahari, kuepuka ujaribifu wa ikolojia, uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa hew na maji kwa kuweka mazingira na utalii endelevu.

Mapema Waziri wa Utalii na Maliasili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Muhamed Omary Mchengerwa alieleza hali ya utalii ilivyo duniani, Tanzania inakazi kubwa ya kuitangaza nchini kimataifa kupitia sekta ya utalii.

Alisema kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usjirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanalengo la kuongeza watalii wengi kutoka mataifa makubwa duniani ikiwemo bara Ulaya, Asia, Mashariki ya Mbali na Amerika

Aidha alieleza serikali pia zina nia ya kuliteka soko la utalii kutoka China ambao wanaongoza dunia kutoa watalii wengi hadi kufikia milioni moja na nusu kwa kila nchini.

Naye, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Muhammed Said alisema wakati umefika kwa Zanzibar kubadili mtazamo kupitia misimu ya utalii kuondokana na dhana msimu mdogo na mkubwa badala yake wawetayari kuutangaza utalii misimu yote iwanufaishe wao na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa ZATI ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii, Rahim Baloo alisema mkutano huo umelenga kuitambulisha dunia na kuitangaza Zanzibar kiutalii na kiutamaduni pamoja na kuwa kuwakaribisha wawekezaji zaidi. Aidha, aliipomgeza serikali awamu na nane na wizara kwa ujumla kwa kuziungamkono sekta binafsi mchango mkubwa wanaoutoa kwa uchumi wa Zanzibar.

IDARA YA MAWASILIANO – IKULU, ZANZIBAR

Balozi Mbarouk Ateta na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje – EU

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya (EU), Bi Helena Konig katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) amekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya (EU), Bi Helena Konig katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambapo Balozi Mbarouk amemhakikishia Bi. Konig kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika nyanja za biashara na uwekezaji, utunzanji wa mazingira hususan uchumi wa buluu, nishati, miundombinu pamoja na ushirikiano wa kikandaa na kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili. 

“Napenda kukuhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika sekta za biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, nishati, miundombinu kwa maslaahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Mbarouk

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya kuimarisha maeneo muhimu hususan biashara na uwekezaji kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu kwa kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje Umoja wa Ulaya, Bi. Konig amesema licha ya changamoto ya uviko 19 kuikumba Dunia na vita ya Urusi na Ukraine, Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Afrika, hususan Tanzania kuimarisha na kuendeleza sekta za biashara na uwekezaji.

“EU tunaendelea kushikamana na kuimarisha nguvu zetu kwa pamoja ili kuhakikisha tunaendelea kuwekeza na kukuza biashara kati yetu na Tanzania kwa maslahi ya mataifa  yote,” alisema Bibi Konig.

Viongozi hao pia wamejadili masuala ya jinsia, digitali, ulinzi na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kijamii na kisiasa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimsikiliza na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya (EU), Bi Helena Konig wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya (EU), Bi Helena Konig

Viewing all 36129 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>