Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36157 articles
Browse latest View live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amefungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Sekta ya Utalii "The Z Summit"

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati akitembelea maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Utalii “The Z Summit” baada ya kuyafungua maonesho hayo leo 23-2-2023,katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar  na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw.Rahim Bhaloo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Bw. Nicola Alessandro, wakati akitembelea maonesho ya Sektya ya Utalii “The  Z Summit” baada ya kuyafungua leo 23-2-2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw. Rahim Bhaloo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia fulana wakati akitembelea banda la maonesho la Zanzibar Padel, baada ya kuyafungua Maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Utalii “The Z Summit” yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharini”B” Unguja leo 23-2-2023, na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw.Rahim Bhaloo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Utalii “The Z Summit” baada ya kuyafungua leo 23-2-2023, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mhe. Rahim Bhaloo, wakati akitembelea maonesho hayo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kuyafungua maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Utalii “The Z Summit” na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe. Mohamed Omary  Mchengerwa na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Bw. Rahim Bhaloo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana
MSANII wa muziki wa Taarab Zanzibar  Siti Amina akitowa burudani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii “The  Z  Summit” uliofunguliwa leo 23-2-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi kumpongeza Msanii wa muziki wa Taarab Siti Amina baada ya kutowa burudani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii “The Z Summit” uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023, na (kulia wa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said na Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa na ( kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw. Rahim Bhaloo.
MWENYEKITI wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw.Rahim Bhaloo akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimtaifa wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii “The Z Summit” uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023.
WAZIRI wa Maliasi na Utalii Tanzania Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii “The Z Summit” uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, leo 23-2-2023, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii “The Z Summit” kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kuufungua mkutano huo uliofanyika  leo 23-2-2023, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali katika Sekta ya Utalii “The Z Summit” , uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023
WASHIRIKI wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali katika Sekta ya Utalii “The  Z  Summit” wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023
WASHIRIKI wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali katika Sekta ya Utalii “The  Z  Summit” wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Gazeti la “The Z Summit” baada ya kuufungua Mkutano Mkuu wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi ”B”Unguja leo 23-2-2023 Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Bw. Rahim Bhaloo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said na Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Gazeti la “The Z Summit” baada ya kulizindua rasmin wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi ”B”Unguja leo 23-2-2023 Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Bw. Rahim Bhaloo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said


 


Balozi Fatma akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini

$
0
0

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali hususani ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Qartar ambapo Balozi Fatma amemhakikishia Balozi wa Qatar kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Qatar kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda, biashara na uwekezaji.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimsikiliza Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al – Homaid yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Zoezi la kuwahamasisha wanawake kujitambua na kujiinua kiuchumi nchini laendelea

$
0
0

 Na Maulid Yussuf WMJJWW 

 

Katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto inaendelea na zoezi la kuwahamasisha wanawake kujitambua na kujiinua kiuchumi nchini.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto bi Siti Abbas Ali amefika katika kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi JKU Mtoni na kuwapa elimu juu ya masuala ya udhalilishaji pamoja na kujitambua kwa Wanafunzi wanaojifunza uzalendo na ukakamavu katika jeshi hilo.

Bi Siti amewataka wanawake kushirikiana na kusimama imara katika kuhakikisha wanafanya kazi zote bila ya kujali jinsia zao ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Amesema hakuna kazi maalumu za wanaume wala kazi maalumu za wanawake, ni lazima kuwa imara na kukubali kuwa kazi zote wanawake wanaweza.

Amesema Serikali ilipoamua kumuinua mwanamke katika ngazi mbalimbali sio kama imekosea,  bali inataka wanawake waweze kujitegemea kwa kujiajiri wao wenyewe bila ya kusubiri ajira kutoka Serikalini. 

"Wanawake shikamaneni, uganeni na shirikianeni kuona kila penye mwanamke kuhakikisha anafanikiwa, na msiwekeane choyo wala roho mbaya, kwani hamtafanikiwa" amesisitiza Mkurugenzi Siti.

Aidha amewataka wanaume kuwasaidia wanawake kuhakikisha wanafanikiwa kwani watu wote ni sawa kama katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

Naye Mwalimu katika Skuli ya Ufundi JKU na  Sekondari , Meja Halima Khamis Khatib ameiomba Idara kuwa na muendelezo wa kufika katika Jeshi hilo kuwapa elimu vijana kwani kila mwaka wamekuwa wakipokea  wanafunzi wapya na wa rika na tabia tofauti, hivyo imani yao elimu hiyo itaweza kuwasiadia vijana hao kwa kuondokana na ushawishi wa matendo ya udhalilishaji. 

Kwa upande wao Wanafunzi wa Jeshi la kujenga uchumi Zanzibar JKU wameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa uamuzi waliouchukua wa kuwapatia elimu ya kujitambua pamoja  na masuala ya udhalilishaji na kuwaomba waendelee ili kuwasaidia kujua mbinu za kukabiliana na matatizo mbalimbi katika maeneo yao.

Wamesema katika jamii wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali juu ya masuala ya udhalilishaji lakini elimu hiyo imewapa mwamko wa kujitambua pamoja na kujua namna gani watajikwamua na changamoto hizo.

Tangazo la kukosekana umeme kesho maeneo ya Mjini

Mhe Hemed: Tuiombee dua serikali

$
0
0


 Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuiombea Dua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili iweze kukamilisha azma ya kuwatumikia wananchi wake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipojumuika na waumini wa masjid Nurullah Magomeni Wilaya ya Mjini katika Ibada ya sala ya ijumaa.

 Alhajj Hemed ameeleza kuwa Azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuijenga Zanzibar yenye Maendeleo na kuwataka Wananchi kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha Zanzibar inafikia maendeleo hayo.

Ameeleza kuwa tayari miradui mbali mbali ya mendeleo imeanza kuzinduliwa na mengine inaendelea kwa hatua mbali mbali ya kukamilika ambapo kutazalikafursa za ajira kwa vijana wenye fani mbali mbali ili kupunguza changamoto ya ajira Nchini.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaeleza waumini hao kuishauri serikali kwa mambo mazuri na kukemea tabia ya baadhi kubeza yanayofanywa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .

 Kuhusu suala la utunzaji wa Amani ambayo ndio kinga ya nchi yetu Alhaji Hemed amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuilinda hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha matendo maovu ikiwemo udhalilishaji na madawa ya kulenya ambayo yamekuwa ni majanga makubwa nchini.

 Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema jamii ya sasa ni ya kutegemeana hivyo ni Vyema kuwasaidia wanaohitaji jambo ambalo litaongeza umoja, Mshikamano na Upendo katika Jamii.

Akitoa Khutba katika Sala hiyo Shekh Abdallah Hassan Ali amewakumbusha Waumini hao kutumia vyema mwezi huu Mtukufu wa Shaaban kwa kufanya matendo mema kama alivyokuwa Kiongozi wa umma huu Mtume Muhammad (S.A.W).

Amesema miongoni mwa sifa za Waumini ni kujipamba na tabia njema pamoja na kujikita katika Ibada hasa kuomba msamaha kwa Mola Mtukufu kwa yote waliyokosea.

CCM yakemea vitendo vya ukwepaji kodi

$
0
0


 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Khamis Mbeto Khamis, akionyesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitowavulia baadhi ya watu wanaokwepa kulipa kodi kwa makusudi na kuisababishia hasara kubwa serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Khamis Mbeto Khamis katika mahojiano maalum huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.

Amesema kila mwananchi ana jukumu la kupinga vitendo vya ukwepaji wa kodi kwani ni hujuma,usaliti na jinai katika maendeleo na ustawi wa uchumi wa nchi.

Mbeto, alieleza kuwa madhara ya vitendo hivyo ni makubwa kwani yanaikosesha serikakali fedha nyingi ambazo zingetumika katika kutatua kero na changamoto za wananchi.

“ CCM ikiwa ndio msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 lazima tukemee vikali baadhi ya tabia ya ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wafanyabishara na wawekezaji.

Fedha hizi zingetumika kujenga hospitali,maskuli,maji safi na salama na huduma za barabara za kiwango cha lami na huduma zingine muhimu za kijamii.”,.alifafanua Mbeto.

Katika maelezo yake Katibu huyo Mbeto, alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo endelevu lakini kuna baadhi ya watu wachache wanakwamisha juhudi hizo kupitia vitendo vya ukwepaji wa kodi.

Pamoja na hayo alizitaka taasisi zinazohusika na usimamizi wa masuala ya kodi nchini zikiwemo ZRA,TRA na manispaa  pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanachukua hatua kali kwa yeyote anayehusika na vitendo hivyo bila kujali cheo,dini,kabila na itikadi ya kisiasa.

Sambamba na hayo aliwasihi wafanyabishara nchini  kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo ukusanyaji wa kodi ni lazima, kwani ikilipwa wanaijengea serikali uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Alisema serikali zote mbili ya Zanzibar nay a Jamhuri ya muungano wa Tanzania zimetoa fursa kwa wananchi kufuata taratibu za kisheria pale wanapoamua kufanya biashara.

Alifafanua kuwa Ibara ya 47 hadi 49 za Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 imeeleza kuwa CCM inatambua kuwa biashara ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda na sekta nyingine za kijamii.

Alisema katika Ilani hiyo ya CCM imeelekeza namna ya serikali itakavyokuza uchumi wa nchi kupitia sekta za biashara na uwekezaji sambamba na kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi.

Kupitia mahojiamo hayo Mbeto, alitoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kukwepa kulipa kodi huku wakiendelea kuwa wazalendo,wachapakazi na waadilifu.

Aidha, akizungumzia changamoto ya mfumuko wa bei kwa Zanzibar alisema ulikuwa asilimia 7.8 na asilimia 8.1 kwa mwezi Novemba na Desemba 2022, ukilinganishwa na lengo la asilimia 5 ambapo mfumuko huo ulikuwa mdogo kuliko nchi nyingi wanachama wa EAC na SADC kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kupunguza athari za ongezeko la bei za bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi .

Katika hatua nyingine Mbeto, amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuthibiti suala la mfumuko wa bei kwa kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha.

Dkt.Nchemba : Ameitaka Benki ya CRDB Kuharakisha Matumizi ya Mfumo wa Malipo wa GePG-BURUNDI.

$
0
0

Meneja wa Benki ya CRDB nchini Burundi Bw. Fredrick Siwale akizungumza wakati alipotembelewa na ugeni kutoka Tanzania uliongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza katika kikao na Menejimenti ya Benki ya CRDB-Burundi alipotembelea benki hiyo mjini Bujumbura nchini Burundi, ambako Benki hiyo inatoa huduma za kibenki kwa miaka kumi sasa.

Na. Ramadhani Kissimba – Bujumbura Burundi

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameitaka Benki ya CRDB kuharakisha matumizi ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya kieletroniki (GePG) ili kuongeza na kuharakisha shughuli za kiuchumi kati ya Tanzania na Burundi.

 

Mhe. Dkt. Nchemba alitoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya kikao na  Menejimenti ya Benki hiyo mjini Bujumbura nchini Burundi, ambako Benki hiyo inatoa huduma za kibenki kwa miaka kumi sasa.

 

Mhe. Nchemba alisema kwamba amefarijika kusikia mchakato wa kuanza kwa matumizi ya ‘’control number’’ kwa ajili ya malipo ya ushuru kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uondoshaji mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam upo katika hatua za mwisho.

 

Alisema kuwa kukamilika kwa matumizi ya mfumo huo wa malipo ya Serikali kwa njia ya kieletroniki kutasaidia kupunguza usumbufu na hasara wanayopata wanafanyabiashara wa Burundi wanapotaka kulipia mizigo yao inayopita katika Bandari za Tanzania.

 

‘’Nimefarijika sana niliposikia hilo la ‘contorl number’ kuwa litafanyika huku huku Burundi kwa sababu litawezesha na kuharakisha shughuli za kiuchumi na hicho ndicho kitu kikubwa ambacho Viongozi wetu wamekuwa wakikitaka na kukitamani kifanyike haraka’’ alisema Mhe. Dkt. Nchemba.

 

Aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wamekuwa wakihimiza urahisishaji wa ufanyaji biashara kati ya nchi hizi mbili, hivyo ni vema matumizi ya ‘control number’ yakaanza haraka ili kurahisisha ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax ambaye aliongozana na Mhe. Dkt. Nchemba kwenye ziara hiyo, aliipongeza Benki hiyo kwa hatua waliyoichukua ya kutoa huduma za kibenki nje ya Tanzania jambo ambalo linaitangaza Tanzania na kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa Watanzania wanaokuja Burundi na Warundi wanaofanya biashara na Tanzania.

 

Mhe. Dkt. Tax ameisihi benki hiyo kupanua huduma zao ili zienee kote nchini Burundi na kuvuka mipaka hadi katika nchi ya Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na si kuishia katika jiji la Bujumbura pekee.

 

Awali akizungumza katika Mkutano huo Meneja wa Benki ya CRDB nchini Burundi  Bw. Fredrick Siwale, alisema kuwa pamoja na kufanya shughuli za Kibenki nchini Burundi pia wamekuwa wakifanya siasa ya Kidiplomasia ya Uchumi ili kuwavutia wawekezaji kutoka Burundi kwenda kuwekeza nchini Tanzania na pia kuwahimiza Watanzania kuangalia fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Burundi.

 

Bw. Siwale alisema kwamba katika kutekeleza suala zima la uwekezaji nchini Tanzania wamekuwa wakiwapatia mikopo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa Burundi ili kutumia mikopo hiyo kuwekeza nchini Tanzania ambapo wafanya biashara hao wamewekeza kwa kujenga kiwanda cha Mbolea Jijini Dodoma, kiwanda cha kutengeneza saruji mjini Kigoma na ujenzi wa hotel ya kitalii mjini Tanga.

 

Mhe. Dkt. Nchemba na ujumbe huo pia walipata fursa ya kutembelea ofisi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zilizopo nchini Burundi.

 

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax, Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi – Sekta ya Ujenzi Mhe. Mha. Godfrey M. Kasekenya, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geoffrey Mizengo Pinda na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Maleko.

 

Mhe. Dkt. Nchemba na baadhi ya Mawaziri kutoka Tanzania wapo nchini Burundi kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo katika Mkutano huo agenda mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa kuhusu mtangamano wa Jumuiya hiyo.

Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Lakutana Jijini Bujumbura – BURUNDI

$
0
0

Waziri wa Fenda na Mipango, Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Peter Mathuki kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaofanyika Jijini Bujumbura, Burundi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) wakipitia nyaraka mbalimbali wakayti wa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi– Sekta ya ujenzi, Mhe. Mha. Godfrey Kasekenya (Mb).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Bunjura nchini Burundi. Kushoto kwa Bi. Amina ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Edward Sokoine na anayefuatia ni Naibu Waziri wa Katika na Sheria Mhe. Geoffrey Mizengo Pinda (Mb).

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Yamungu Kayandabila wakiwasili katika Hotel club du lac Tanganyika kuhudhuria Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Bujumbura nchini Burundi.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM-Bujumbura)

Na. Ramadhani Kissimba, Bujumbura -Burundi

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameshiriki katika Mkutano wa 43 wa kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Bunjura, Burundi. Mkutano huo ambao umefanyika baada ya miaka nane (8) toka ulipofanyika kwa mara ya mwisho nchini Burundi umeshirikisha Mawaziri wanaosimamia masuala ya Afrika Mashariki na ushirikiano wa Kikanda pamoja na Mawaziri wenye agenda zinazojadiliwa na Baraza hilo.

Awali kabla ya Mkutano huo kulitanguliwa na vikao vya Wataalamu na Makatibu Wakuu kutoka katika nchi wanachama vilivyofanyika kuanzia tarehe 19 – 22 Februari, 2023 ambao walipitia agenda na mapendekezo mbalimbali ya Jumuiya. Aidha wataalamu hao walipitia taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita katika maeneo ya biashara, forodha, miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira, utawala na fedha.

Dkt. Nchemba ameshiriki Mkutano huo pamoja na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambapo watajadili na kupitisha mapendekezo ya agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuitangaza lugha ya Kiswahili kwa kuanzisha vituo vya utamaduni wa lugha hiyo katika Balozi za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa muelekeo wa kuanza kutumika kwa lugha ya Kiswahili na Kifaransa katika uendeshaji wa shughuli rasmi za Jumuiya.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa chini ya Uenyekiti wa Burundi na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchini Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Sudan Kusini umemalizika tarehe 23 Februari, 2023 na maazimio na agenda zilizopitishwa zitawasilishwa katika mkutano wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuridhia utekelezaji wake.  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Rais wa Benki ya ADB Ikulu Zanzibar

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Dkt.Akinwumi Adesina alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Dkt.Akinwumi Adesina, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo, akiwa na Ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jiji Zanzibar na kuhudhuriwa na Wizara ya Fedha Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Rais wa  Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB)Dkt.Akinwumi Adesina (wa tano kushoto) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao,katika mazungumzo hayo Viongozi wa Wizara ya Fedha Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walihudhuria.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Rais wa  Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB)Dkt.Akinwumi Adesina (wa tano kushoto) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao,katika mazungumzo hayo Viongozi wa Wizara ya Fedha Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walihudhuria.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Dkt.Akinwumi Adesina baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25/02/2023.

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Atoa Tuzo Katika Hafla ya NACTVET. Serikali Itaendelea Kushirikiana na Sekta Binafsi - MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela tuzo baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi wa pili katika Mafunzo ya Uanagenzi kwenye kundi la makampuni makubwa kwa mwaka  2023. Makabidhiano hayo yalifanyika  katika hafla kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na wadau kutambua mchango wa uazalishaji rasilimaliwatu yenye ubora kwa soko la ajira, kwenye hoteli ya Hyatt Kempisk  jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi wa makampuni makubwa walioshiriki  katika hafla kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na wadau kutambua mchango wa uazalishaji rasilimaliwatu yenye ubora kwa soko la ajira, kwenye hoteli ya Hyatt Kempisk  jijini Dar es salaam, Februari 24, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na Sekta Binafsi katika utoaji elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kutosha unaohitajika katika sekta mbalimbali.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa waajiri wote nchini waendelee kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha malengo ya kukuza ujuzi na kuongeza soko la ajira yanafanikiwa kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Februari 24, 2023) katika hafla kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na wadau kutambua mchango wa uzalishaji wa rasilimaliwatu yenye ubora kwa soko la ajira. ”Maendeleo ya uchumi wa nchi yoyote yanategemea sana ngazi ya ujuzi wa nguvukazi uliyokuwa nayo. Hivyo, mchango wa wadau ni muhimu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewapongeza waajiri kwa kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo (field practical), uanagenzi,  utarajali pamoja na namna wanavyoshiriki wenu katika kuandaa mitaala inayotumika kwenye vyuo na taasisi za Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Amesema ushirikiano huo ni muhimu sana katika kuendeleza ujuzi kwa ajili ya kujenga uchumi wa viwanda. “Nataka nitumie fursa hii kuwapongeza lakini Serikali inatambua na inathamini juhudi mnazozifanya katika utoaji wa ajira kwa wahitimu wetu, tunawapongeza sana.”

Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Uzalishaji wa Wafanyakazi Wenye Ujuzi Nchini Tanzania”, Waziri Mkuu amesema kauli hiyo ni thabiti kwani inaweka msisitizo katika ujenzi wa rasilimali watu yenye ujuzi.

Ni ukweli usiopingika bila ujuzi hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana. Ujuzi unahitajika kwenye nyanja mbalimbali za uzalishaji hapa nchini kwani mataifa yote yaliyopiga hatua kubwa za maendeleo yamefanikiwa kwa kuweka kipaumbele katika kuongeza rasilimali watu yenye ujuzi.”

Amesema maeneo yaliyowekewa msisitizo ni sekta za kipaumbele, kuimarisha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kati ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanapata maarifa na ujuzi wa kazi utakaowawezesha kujiajiri na kuajirika. “Hii ni pamoja na kuimarisha mifumo na kuongeza kasi ya kurasimisha ujuzi ili nguvukazi ya Taifa itumike ipasavyo katika soko la ajira la ndani na nje.”

Amesema kwa kutambua umuhimu wa kukuza na kuendeleza ujuziSerikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suhulu Hassan inatekeleza kwa vitendo dhamira yake ya dhati ya kuwasaidia vijana hapa nchini kupitia mipango na mikakati mbalimbali ukiwemo Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/2022 - 2025/2026), unaolenga kukuza ujuzi kwa Watanzania wapatao 681,000.

Waziri Mkuu amesema kulingana na utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2021, nguvu kazi ya vijana ni milioni 14.2 sawa na asilimia 55 ya nguvu kazi yote nchini, ambapo vijana milioni 12.5 sawa na asilimia 87.8 ya nguvu kazi ya vijana nchini wameajiriwa au kujiajiri.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kupitia utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya Kukuza Ujuzi Nchini, vijana 22,899 wamepatiwa ujuzi unaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa. Kati ya hao, vijana 14,440 wakiwemo vijana wenye ulemavu 349 wamepatiwa mafunzo ya uanagenzi katika fani mbalimbali.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Makakati wa Taifa wa Uendelezaji wa Ujuzi wa Mwaka 2016/17-2025/26 ambao moja ya malengo yake ni kuwa na ushirikiano kati ya waajiri, wadau na vyuo au taasisi za elimu.

“Ushirikiano huu uteleta tija kubwa na kuondoa dhana ya kwamba wahitimu wetu hawana ujuzi unaohitajika katika ulimwengu wa kazi”

Kwa uoande wakeMtendaji  Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba-Doran amesema ili Tanzania iweze kushiriki kikamilifu katika soko shindani la Afrika Mashariki na dunia ni lazima hatua za maksudi zichukuliwe katika kukuza ujuzi hususani kwa vijana. “Katika kutimiza adhma hii, Chama Cha Waajiri tunaamini waajiri wana nafasi kubwa katika kufikia malengo tuliyojiwekea kama nchi.”

Mfano, kupitia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano, awamu ya tatu (“the National Five-Year Development Plan-Phase three), tumelenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka asilimia 9 (mwaka 2019) kufikia asilimia 8 ifikapo mwaka 2025/26. Kukuza ujuzi ni kati ya mipango iliyobainishwa na Serikali ili tufikie lengo na kuongeza idadi ya wahitimu waliopata mafunzo mahala pa kazi ni njia mojawapo ya kukuza ujuzi nchini kwa vijana wetu.”

Amesema wao wanatarajia kuongeza idadi ya wahitimu wenye mafunzo ya uanagenzi kufikia 231,000 ifikapo mwaka 2025/26 kutoka 46,000, mwaka 2019/20, vivyo hivyo na kwa mafunzo tarajari, lengo ni kufikia wahitimu 150,000 ifikapo mwaka 2025/26 kutoka 30,000, mwaka 2019/20.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Amefungua Kikao cha Kamati ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania

$
0
0

Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensaya Watu  na Makazi, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Hemed Suleiman Abdulla wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kikataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam kushiriki katika Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi.


Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 25-2-2023.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza Kikao cha Tisa cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar-es-salaam.

Akifungua Kikao hicho Mhe. Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 ameeleza kuwa kukamilika kwa zoezi la Sensa mwaka jana limetokana na kamati hiyo kusimamia miongozo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo walifatilia kwa ukaribu muendelezo wa zoezi hilo kwa kila  hatua.

Sambamba na hayo Mhe. Majaliwa ameishukuru Kamati hiyo kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kuandaa na kusimamia zoezi hilo hadi kukamilika kwake.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na Bunge Mhe. George Simbachawene ameeleza kuwa matokeo ya awali ya Sensa ya watu na makazi ya mwezi Agosti 2022 yamechanganua takwimu kuanzia ngazi ya Kata kwa Tanzania Bara na Shehia kwa Tanzania Zanzibar.

Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Anwani za Majengo Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali ameeleza kuwa Zoezi hilo ni la mara ya kwanza kufanyika Tanzania ambalo linasaidia kukamilisha mipango kazi ya maendeleo ikiwemo utungaji wa Sera.

Akiakhirisha Kikao hicho Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewashukuru wajumbe wa kikao hicho kwa kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Aidha, Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa takwimu za zoezi hilo zinaakisi mahitaji ya watanzania na amewataka watendaji wote Serikalini kuwa kuhakikisha  takwimu hizo zinaendana na mipango ya sahihi ya Serikali ili watanzania wanufaike.

Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya sensa ya watu na makazi kimejumuisha Mawaziri na Makatibu Wakuu, Watakwimu wakuu, na makamisaa wa sensa ya mwaka 2022, na watendaji wa taasisi na sekta mbali mbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe Hemed amkagua Raza

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla  amefika kumjulia hali aliekuwa Mwakilishi  wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammed Raza Hassanali, huko Nyumbani kwake Ali Abbas Tower Mtaa wa Jamhuri  Jijini Dar es Salaam.

 

Katika ziara hiyo, Mhe. Hemed ameongozana na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbali mbali.

 

Mhe. Hemed amemueleza Mhe. Raza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi zake anazoendelea kuzichukua hasa maamuzi yake ya kusaidia ujenzi wa Vyoo Kumi na mbili vya wanafunzi wa Kike Skuli ya Madungu Kisiwani Pemba pamoja na ahadi yake ya kuendelea kuinua vipaji na kuendeleza michezo Zanzibar

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kufurahishwa kwake kuona hali ya Kiongozi huyo inazidi kuimarika siku hadi siku na kumfikishia   salamu za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo anamuombea kwa M/Mungu Mtukufu apone haraka ili kuendelea na majukumu ya kuijenga Zanzibar.

 

Nae aliekuwa Muwakilishi wa Jimbo la  Uzini Zanzibar Mhe. Muhamed Raza Hassanali amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na ujumbe aliofuatana nao kwa kufika  kumjulia hali hatua ambayo inaonesha wazi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea inathamini jitihada zake katika kuiletea maendeleo Zanzibar.

 

Aidha Mhe. Raza amemuomba Mhe. Hemed kumfikishia salamu zake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kuwatumikia wazanzibari kwa miradi mbali mbali ya maendeleo na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

 

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiambatana na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walifika Hospitali ya Saifee Mtaa wa Osterbay Dar - es - Salaam kumjuulia hali Muwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (ACT Wazalendo) Mhe. Habib Ali Muhamed anaeendelea kupatiwa Matibabu Hospitalini hapo.

 

Mhe. Hemed amewataka wanafamilia kuwa wamoja hasa katika kipindi hichi wanachomuuguza Mzee wao pamoja na kumuombea Dua ili apone haraka aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe.

 

……………………….

Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar


 

NAIBU WAZIRI KHAMIS AHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis akipanda mti katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kilichopo Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Soma na Mti” iliyofanyika chuoni hapo jana.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, Amina Makilagi akipanda mti katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kilichopo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Soma na Mti” iliyofanyika chuoni jana.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) jijini Mwanza mara baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Soma na Mti” iliyozinduliwa jana.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis akipata maelezo kuhusu matumizi ya majiko rafiki katika uhifadhi wa mazingira kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Jiko Janja, Wilson Atukuzwe mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya “Soma na Mti” iliyozinduliwa katika Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) jijini Mwanza.
 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa rai kwa wizara na taasisi katika sekta za umma na binafsi kutumia nishati mbadala ili kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa

Mhe. Khamis amesema hayo Februari 25, 2023 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Soma na Mti’ katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira katika taasisi za elimu ya juu nchini.

Amesema zoezi la upandaji katika maeneo mbalimbali nchini ni ajenda ya kitaifa inayoongozwa na viongozi wa kitaifa akiwemo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe.Dkt Philip Mpango na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na hivyo kuzitaka taasisi za umma na binafsi kuunga mkono juhudi hizo.

“Tupo hapa kutekeleza mpango wa Serikali juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni muendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na viongozi wetu wakuu wa kitaifa. Nitoe rai kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha tunasimamia maelekezo ya Serikali ya kuzuia ukataji miti, tuanze kutumia nishati mbadala kama gesi kwa ajili ya kupikia kama anavyosisitiza Rais wetu,” amesema Mhe. Khamis

Aidha naibu waziri huyo ametoa maagizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia na kuendeleza kampeni hiyo kwa kuhakikisha kila shule na kila mwanafunzi anakuwa na mti wake na kuhimiza utamaduni wa kila Kaya kupanda miti na kila mtu anayenunua eneo kuhakikisha amepanda miti katika eneo lake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi amesema suala mazingira ni moja ya kipaumbele vya msingi kinachotekelezwa na taasisi zote za umma na binafsi zilizopo katika Wilaya hiyo na kukusudia kulifanya Jiji la Mwanza kuendelea kuwa Jiji la kijani.

“Katika Wilaya ya Nyamagana kila mradi unaotekelezwa unafungamanishwa na mazingira na kila tukio tunapanda miti na hivi karibuni taasisi zetu za TFS, Gereza la Butimba na wadau wengine tulipanda zaidi ya miti 7000 katika vyanzo mbalimbali vya maji ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Makamu wa Rais,” amesisitiza Makilagi.

Ameongeza kuwa kupitia kampeni ya “Soma na Mti” wilaya hiyo imejipanga kimkakati katika kuhakikisha kuwa inafikia lengo la kupanda miti 1,500,000 kwa kushirikisha shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu na kuhakikisha inarejesha hadhi ya Jiji la Mwanza kuwa kinara wa usafi wa mazingira nchini.

Naye Balozi wa Mazingira Nestory Mushi amesema kupitia taasisi yake ya Mweka Site wamefanikiwa kuotesha miti zaidi ya 358,000 na miti hiyo inatarajia kupandwa katika Mikoa yote inayokabiliwa na hali ya ukame. 

Taasisi yetu inahamisha jamii katika shughuli zote za usafi wa mazingira ikiwemo upandaji miti na usafi wa fukwe mbalimbali. Tunafundisha wanafunzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kuhusu vitalu vya miti, miradi ya samaki na utunzaji mazingira” amesema Mushi.

Mwakilishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Alex Julius amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha utunzaji wa mazingira ikiwemo upandaji, TFS imeanzisha kitalu cha miti ya matunda na vivuli ambapo kati ya Julai 2022 hadi Februari 2023, TFS imefanikiwa kuzalisha miche ya miti 67,310.

Wakati wa kuzalisha miche hii tunazingatia masuala mbalimbali ikiwemo miche inayokuwa haraka, miche inayohifandhi maji, miche inayozuia mmomonyoko wa udongo na kuanzia mwezi Julai 2022 hadi Februari 2023 miche ya miti 32,970 imegawiwa bure katika taasisi mbalimbali” amesema Julius.

Kampeni ya “Soma na Mti” ilizindiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais mwaka 2022 ikiwa imelenga kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kuona zoezi la upandaji miti kuwa sehemu muhimu ya maisha ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Haasan Amefanya Uteuzi na Uhamisho wa Viongozi

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Kisukari Zanzibar (DAZ)

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Nishati na Madini  Joseph Kilangi (aliyesimama) akiwapa nasaha Wanajumuiya ya Watu Wanaoishi na Kisukari (DAZ) huko katika Ukumbi wa Skuli ya Ben-Bella
Katibu wa Jumuia ya Watu Wanaishi na Kisukari Zanzibar (DAZ) Omar  Abdalla Ali akitoa rIpoti ya utekelezaji wa kazi ya Juumuiya ya Watu Wanaoishi na Maradhi ya Kisukari Zanzibar(DAZ) Januari hadi Disemba 2022, huko katika ukumbi wa Skuli ya BenBella
Baadhi ya Wanachama wa Jumuia ya Watu Wanaishi na Kisukari Zanzibar (DAZ)  wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Nishati na Madini Joseph kilangi (hayupo picha) huko katika ukumbi wa skuli ya BenBella.
Picha ya pamoja ya Mkutano Mkuu wa  Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Kisukari Zanzibar (DAZ) iliyopigwa katika ukumbi wa BenBella. Febuari 26,.2023..

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 26/02/2023/

Ugonjwa la Kisukari ni miongoni mwa Magonjwa yanayoathiri jamii kwa kiwango kikubwa na yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hapa nchini na hupelekea vifo na ulemavu wa viungo 

 

Akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watu Wanaishi na Kisukari  Zanzibar huko katika ukumbi wa Skuli ya Ben-Bella Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini  Joseph Kilangi kwa Niaba ya Naibu Wazara wa Maji Nishati na Madini Shaaban Ali Othman amesema

mwaka 2019 watu milioni kumi na tisa Barani Afrika wanaishi na ugonjwa wa kisukari kati ya umri wa miaka 20 hadi 70 ambapo kwa hapa Zanzibar ripoti  inaonyesha kuwa watu 4 kati ya watu mia 100 huugua ugonjwa huo .

 

Amesema ongezeko hilo linaendelea kukuwa siku hadi siku jambo ambalo huko nyuma halikuwepo na limekuwa  ni changamoto katika taifa  kutokana na kuutwika mzigo mkubwa Seriikali.

 

Aidha amefahamisha kuwa kundi la watu wanaishi na kisukari liko katika hatari zaidi kwa kushambuliwa na maradhi mengine hivyo ameitaka jamii kuzingatia lishe bora,  kufanya mazoezi kuachana na tabia za matumizi ya pombe ya kupitiliza na sigara pamoja na kujiepusha na msongo wa mawazo ambayo hupelekea kupata ugonjwa huo.

 

Alifahamisha kuwa elimu bado inahitajika kwa jamii ya kupambana na vichocheo vya maradhi hayo pamoja na kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kuipunguzia mzigo mkubwa serikali kutibu ugonjwa huo kwa kutumia fedha nyingi kwa matibabu fedha ambazo zingelitumika kwa mambo mengine

 

Nao Katibu wa Jumuia ya Watu Wanaishi na Kisukari Zanzibar (DAZ) Omar  Abdalla Ali na  Mjumbe wa Bodi ya Watu Wanaishi na Kisukari Dk Faiza Kassim wamesema Serikali ni vyema kuzidi kupambana na suala la dawa na shindano kwa wanaoishi na kisukari.

 

Aidha wamesema kuwa ni vyema kwa jamii kujikinga na visababishi vya maradhi hayo na kuwataka kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kuweza kujigundua mapema na kupata huduma stahiki

 

Mapema akisoma Risala ya Jumuiya wa Watu Wanaishi na Kisukari Zanzibar(DAZ) ambae ni Mwenyekiti wa Vijana wa  Jumuia ya Watu Wanaishi na Kisukari Bi Nunuu Kheir Saleh  amesema ugonjwa wa kisukari unawapata hasa watu wazima, wajawazito na watoto ambapo kisukari cha utotoni imeonekana kuongezeka na kushika kasi na husababisha madhara na mzigo mkubwa kiuchumi kwa serikali na watu binafsi.

 

amesema miongoni mwa dalili kubwa za ungonjwa huo ni kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati, kwenda haja ndogo mara kwa mara, kusikia njaa kila wakati, kupata ganzi hasa sehemu ya miguu viganja vya mikono na vidole, pamoja na vidonda vya miguu vinavochelewa kupona.

 

Nae Mwanachama Omar Ahmada Ali ameiyomba  Jumuiya hiyo kuwapa msaada wa mahitaji ya lazima   kwa wale wanachama mwenye hali ngumu za maisha

 

Akitoa neno la shukrani Mrajis wa Jumuiya zisizo za kiserikali Bw Ahmed Gharib Abdalla ameipongeza jumuia hiyo kwa kufanya kazi za kupambana na ugonjwa wa kisukari pamoja na kutoa elimu kwa  jamii .

 

Amesema kuwa ni vyema kwa Jumuiya zinazoanzishwa ziwe na malengo ya kuisaidia serikali ili kuipunguzia mzigo na  lengo liweze kufanikiwa  


Ujumbe wa CPC Watembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar

$
0
0


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed akimkabidhi zawadi ya karafuu (kulia),Balozi wa China Tanzania Bi.Chen Mingijian (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed akimkabidhi zawadi ya karafuu (kulia),Balozi wa China Tanzania Bi.Chen Mingijian (kushoto).
UJUMBE wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed wakiwa katika eneo la historia ya watumwa katika Kanisa la Angilikana Mkunazini Zanzibar.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kuwa serikali ya China imekubali kuwekeza katika miradi mbalimbali inayobeba dhana ya uchumi wa bluu.

Hayo ameyasema Naib Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed 'Dimwa' wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamili ziara ya ujumbe wa Chama Cha Kikomunisti cha Chini visiwani Zanzibar.

Alisema  Serikali ya China imekubali kuwekeza katika bahari hasa katika mazao ya baharini ikiwemo mwani,uvuvi na ufugaji wa kaa.

Alisema mbali na kuwekeza katika miradi hiyo pia wamekubaliana kuwekeza ktika miradi ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar kwa kujenga nyumba za watumishi zitakazouzwa kwa gharama nafuu ili viongozi,watumishi na watendaji wa CCM wapate makaazi bora ya kuishi.

''Ziara hii imekuwa na mafanikio makubwa kwani tumejadili mambo mengi ya msingi yanayolenga kutatua kero za wananchi na wanachama wa CCM kwa ujumla''.alisema Dkt.Dimwa.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, alisema CCM inawakaribisha wawekezaji wa ndani ili waweze kuwekeza huku ikifungua milango kwa wawekezaji wa kimataifa.

 Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Khadija Ali Salum amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha Uhusiano katika nyanja za utamaduni,Siasa,diplomasia,Uchumi,jamii,michezo na burudani na  uwekezaji.

Alieleza kuwa kwa miaka mingi Chama Cha kikommunist Cha China(CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekuwa ni vyama vyenye urafiki na undugu wa kihistoria katika masuala ya kuimarisha Ilani za Uchaguzi za vyama hivyo.

Alisema ujumbe wa CPC ulipowasili Zanzibar wamevutiwa na mazingira ya Zanzibar na wakaweka wazi nia Yao ya kuja kuwekeza katika sekta ya bahari katika masuala ya usafiri,uvuvi na kilimo cha baharini cha mwani.

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa idara ya SUKI Khadija, amesema kuwa CCM inaendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplimasia na Vyama mbalimbali Duniani ili kwenda sambamba na Siasa ya kisayansi inayojikita katika masuala muhimu ya kuondosha changamoto na kero za Wananchi kwa wakati.

Alieleza kuwa Chama Cha CPC,kimekuwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha Serikali za nchi hizi mbili na China imekuwa ikipokea vijana wengi za Tanzania wanaoenda Kwa ajili ya masomo,biashara na utalii.

Khadija,akizungumzia ziara hiyo alisema baada ya ujumbe huo kuwasili Zanzibar majira ya 3:00 asubuhi ulienda katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo na kwa upande wa china ni Naibu Waziri wa idara ya mambo ya nje ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti LiMingxiang.

Baada ya kusaini kitabu walienda kutembelea maeneo ya kihistoria ya jumba la Wananchi katika mtaa wa forodhani na katika soko la watumwa lililopo katika Kanisa la Anglicana Mkunazini Zanzibar.

Mkuu huyo wa Idara ya SUKI,alisema ujumbe huo umekamilisha ziara yake kwa kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Rais Mhe Samia afanya uteuzi wa Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Akanusha Taarifa ya Ajali ya Moto Kuwa Sio ya Ukweli

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na uvumi wa  tukio la moto linalosambaa  mitandaoni likionyesha kuungua kwa  Hoteli za Nungwi ,huko Ofisini kwake Mkokotoni Kaskazini Unguja.
(PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

Na.Rahma Khamis Maelezo        26/2/2023

Jamii nchini imetakiwa kuacha kusambaza taarifa zisizo na uhakika katika mitandao ya kijamii ili kuepusha taharuki kwa wananchi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uvumi uliyotolewa siku ya Alhamis katika mitandao ya kijamii kuhusiana na  kuungua kwa Hoteli tatu za Nungwi huko Ofisini kwake Mkokotoni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amesema taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kupotosha jamii na kuwatia hofu wageni wanaotaka kuja kutembelea Zanzibar.

Amesema kitendo cha kusambazwa kwa taarifa hizo ni kwenda kinyume na sharia za matumizi ya mtandao hivyo ipo haja kwa wahusika kutafuta chanzo cha taarifa hiyo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha amefahamisha kuwa kuenea kwa taarifa hizo katika Mkoa wa Kaskazini kunapelekea baadhi ya wageni kuona kwamba Mkoa huo hauko salama jambo ambalo linakosesha ongezeko la pato la taifa.

Hata hivyo Mkuu huyo ametoa wito kwa wamiliki wa Hoteli na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari hasa wakati wa kiangazi ili kujilinda na ajali za moto.


CCM Zanzibar Yawasihi Wananchi Kuendeleza Utamaduni wa Kusoma Vitabu na Machapisho

$
0
0

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Ali Salum pamoja na Maafisa wa idara hiyo  wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani katika Maktaba Kuu ya Zanzibar iliyopo Maisara Unguja.
MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim, akieleza namna wanavyotoa huduma ya usomaji wa vitabu mbalimbali katika taasisi hiyo.
MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim, akieleza namna wanavyotoa huduma ya usomaji wa vitabu mbalimbali katika taasisi hiyo.

MKURUGENZI wa bodi ya huduma za maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim(kulia), akizungumza juu ya muundo wa utendaji wa Maktaba hiyo baada ya Katibu wa Mkuu wa Idara ya SUKI Khadija Ali Salum (upande wa kushoto) kufika ofisini kwake kwa ajili ya ziara maalum ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar(SUKI) Khadija Ali Salum,amewasihi wananchi kuendeleza utamaduni wa kutembelea maktaba mbalimbali nchini ili kujifunza na kusoma vitabu ,machapisho,nyaraka na taarifa zitakazowaongezea maarifa na uelewa yakinifu.

Wito huo ameutoa katika ziara yake ya kutembelea Maktaba Kuu ya Zanzibar iliyopo mtaa wa Maisara Unguja.

Alisema wananchi wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu na machapisho mbalimbali ili wawe na uelewa juu ya mambo tofauti yanayohusu Zanzibar, Tanzania bara,Afrika na duniani kwa ujumla.

Katika maelezo yake Katibu huyo wa SUKI Khadija,alieleza kuwa Maktaba Kuu ya Zanzibar imehifadhi nyaraka,machapisho na vitabu mbalimbali vinavyosaidia kuwajengea uwezo wa kitaaluma wanafunzi wa ngazi mbalimbali za kitaaluma na kwamba wananchi nao wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

Kupitia ziara hiyo Khadija, aliahidi kuwa Chama Cha Mapinduzi kitatafuta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto za kiutendaji zinazoikabili taasisi hiyo ambayo ni chimbuko la kuhifadhi nyaraka muhimu za kitaaluma.

Alieleza kuwa licha ya kuwepo na changamoto za kiutendaji wafanyakazi wa taasisi hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waende sambamba na kasi ya utendaji wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.

Pamoja na hayo alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatia maazimio ya kikao cha kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kilichofanyika februari 20,mwaka 2023 hapo Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Alisema kuwa pamoja na majukumu yanayoikabili taasisi hiyo wanatakiwa kuongeza juhudi katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya maktaba kuu yaliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Maana halisi ya maktaba ni sehemu ya jengo lenye nyaraka au machapisho ya kujifunza na kujisomea hivyo kwa maana hiyo kila mwananchi ana wajibu wa kujiongezea maarifa kupitia maktaba hiyo.”alisema Khadija.

Naye Mkurugenzi wa Maktaba Kuu Zanzibar Mkurugenzi wa huduma za Maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdul-aziz Ibrahim, amesema wanatoa huduma mbalimbali za kuwasaidia wanafunzi na wananchi kwa ujumla kupata vitabu ili wajifunze na kupata taaluma,elimu na maarifa juu ya mambo mbalimbali yaliyowazunguka.

Alisema kupitia taasisi hiyo inayofanya kazi zake Unguja na Pemba wanahifadhi vitabu mbalimbali vikiwemo vya maalum za uchumi,sayanzi,maarifa ya jamii,diplomasia na ujasiriamali na mambo mengine yanayohusu viumbe hai na visivyo hai.

Alizitaja changamoto zinazowakabili katika maktaba hiyo kuwa ni pamoja na udogo wa jengo la maktaba hiyo pamoja na ukosefu wa vifaa vya huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).

Dkt.Ulfat, alizitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa huduma ya mtandao ‘Internet’, upungufu wa wakutubi na ukosefu wa usafiri kwa watendaji wa taasisi hiyo hasa wakati wanapokuwa na majukumu ya nje ya ofisi hiyo.

Kupitia ziara hiyo Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuhakikisha huduma za maktaba zinatolewa katika mfumo wa kisasa.

“Tunatoa huduma bora na rafiki kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla hivyo wananchi,wageni na wanafunzi wa ngazi tofauti milango yetu ipo wazi tunawakaribisha waje kujiongezea maarifa,elimu,taaluma na uelewa”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa baada ya Waziri wa Elimu Tanzania bara kupiga marufuku baadhi ya vitabu visivyozingatia maadili na kwa upande wa Zanzibar katika maktaba hiyo walifanya uchunguzi na kubaini uwepo wa baadhi ya vitabu hivyo na kuhakikisha wanaviondoka katika mfumo na taratibu za huduma ya usomaji.

Rais Mhe Samia afanya uteuzi wa Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania

Viewing all 36157 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>