Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36158 articles
Browse latest View live

Mafunzo elekezi kwa viongozi vijana yafanyika

$
0
0


 Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Ndugu Muhammed A. Abdalla akiwa kwenye picha ya pamoja na viiongozi mbali mbali pamoja na viongozi Vijana kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar  na viongozi kutoka Braza la Vijana Vijana mara baada ya kuyafunga mafunzo elekezi kwa viongozi vijana yaliyoandaliwa na Uongozi wa Raha Tv Online yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Zanzibar School Of Health kilichopo kwa Mchina Mwanzo                                                 

Mstahiki Meya wa jiji la Zanzibar Mahmoud M, Mussa   amewasisitiza vijana kuwa wazalendo na kuwacha kujishirikisha na vitendo viovu vikiwemo vya udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya ili taifa lipate viongozi bora.

 

Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi vijana yalioyoandaliwa na Raha Tv Online Mahmoud amesema viongozi vijana wanamchango mkubwa katika kuchochea maendeleo kwa taifa lao hivyo si vyema kutumika katika vitendo viovu ambavyo vinarejesha nyuma maendeleo ya taifa   na hatimae kushiriki kikamilifu katika kuinua uchumi wa nchi.

 

 Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Suzan Peter Kunambi amewataka.vijana kutokata tamaa  katika kuzisimamia ndoto zao ili zikamilike   sambamba  na kuutaka uongozi wa Raha Tv Online kuwa wabunifu ili  jamii ifaidike na habari mbali mbali ikiwemo  za kuelimisha na kuburudisha .

 

Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdullah amesema Tume kwa kushirikiana na TCRA zitaendelea kuvisimamia vyombo vya habari nchini ili kuona vinafuata utaratibu na maadili ya utangazaji.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Raha Tv Online ndugu Raya Hamad Mchere amesema Raha Tv Online inalengo la kuwapasha habari vijana na wanawake na jamii kwa ujumla kuhusu mambo mbali mbali ikiwemo kuhabarisha, kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha

 

Mafunzo hayo yaliyobeba ujumbe ‘MIMI NI WA THAMANI’ yana lengo la kuwajengea uwezo Viongozi vijana na kuwawezesha kujua thamani yao na umuhimu wao kwa nchi, kwa vile wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanathamini jitahada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwainua kiuchumi na hatimae malengo yao kufanikiwa.

 

Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi vijana kutoka Baraza la Vijana Zanzibar, Vyuo Vikuu viliopo Zanzibar na wengine kutoka taasisi zisizo za kiserikali ambapo Mkurugenzi huyo amaesema mafunzo elekezi yatakuwa chachu ya kufahamu kwa kina changamoto za vijana na njia za kuwajengea uwezo ili wawe vijana wazalendo na kufuata sheria za nchi hii bila kushurutishwa.

 

Mafunzo hayo yamefungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg Muhammed Ali Abdalla ‘teacher Muha’ ambapo ameupongeza uongozi wa Raha Tv Online kwa kuwa na malengo mazuri ya kuwajengea misingi imara kwa kuamsha ari na kujenga uwelewa wa masuala ya kiuchumi kijamii pamoja na masuala mtambuka katika kuleta chachu na kuwainua kitaaluma katika kuwainua Viongozi vijana hatimae kuwa tayari na wajibikaji

Ameuomba uongozi wa Raha Tv Online kutoishia bali mafunzo hayo yawe ni endelevu na kuwataka viongozi vijana kuwa wana jukumu kubwa na kuonesha mabadiliko katika jamii na kuonesha uzalendo wenu kwa vitendo kubadilisha akili za baadhi ya watu kwa kutambua Zanzibar ni moja kuikomboa kiuchumi ilipo na kuipeleka kwenye maendeleo zaidi ambayo Serikali yetu inakwendanayo

Amesema Raha Tv Online iwe ni chemchem ya kuwajengea uwezo vijana ili waondokane na utegemezi wawe wabunifu katika utayarishaji kwa uwezo waliokuwa nao kuendeleza vipaji vyao katika kuyasarifu mazingira tuliyonayo na fursa zilizopo.

 

Mada kadhaa ziliwasiliwa zikiwemo Uzalendo iliyowasilishwa na Bw Mwalimu Ali Mwalimu Katibu Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kujitambua na uongozi, Itifaki ndg Mussa Yussuf, uongozi na matumizi ya vyombo vya habari Dkt Mnemo mhadhir chuo cha Habari.

 

Mada nyengine zilihisu udhalilishaji na maadili Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa ndg Yunus Ali Juma, UKIMWI Mkurugenzi Tume ya UKIMWI Dkt Ahmeid M. Khatib, ushuhuda na historia ya maisha Dkt Rukaiya Wakif Kamishna Idara ya Mipango Zanzibar, mafunzo hayo ya siku mbili  yamefanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Zanzibar School of Health kilichopo Kwa Mchina mwanzo.

 

 

 

 


WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUJIVUNIE UVUMBUZI WA MBEGU MPYA YA MICHIKICHI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele na kujivunia utafiti uliofanyika hapa nchini na kupata mbegu mpya ya michikichi ambayo imeonesha mafanikio makubwa.

“Baada ya kukaa na kufanya tathmini ya zao la chikichi hapa Tanzania, na leo nimesikia michango ya wadau wote. Nimejiridhisha kwamba utafiti tulioufanya wa kuzalisha mbegu ya Tanzania ambayo inaota na kutoa matunda ndani ya miaka miwili hadi mitatu, ninayo furaha kutamka kuwa utafiti ule umefanikiwa,” alisema na kuamsha shangwe miongoni mwa wadau wa zao hilo.

 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumapili, Februari 26, 2023) wakati akihitimisha kikao chake na wadau wa zao la chikichi mkoani Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF. Mbegu hiyo bora ya michikichi aina ya TENERA inatoa mafuta mara tatu zaidi ya aina ya DURA ambayo inalimwa na wakulima kwa takribani asilimia 90.

 

Alisema mtu yeyote anayetaka kulima chikichi anaweza kufanya hivyo kwa sababu mbegu zipo. “Tulianza kuzalisha mbegu mwaka 2018 na ilipofika mwaka 2020 tukaanza kupanda miche na leo tunaona matunda yanapatikana.”

 

“Twendeni mashambani, tutumie miche yetu iliyozalishwa ama na taasisi zetu, Halmashauri zetu au vyama vya msingi (AMCOS). Tuna kazi ya kuhakikisha zao la chikichi linaenda kwa spidi kali zaidi.”

 

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuagiza kila mkoa, kila wilaya tutenge maeneo ya kilimo lakini kuna baadhi hadi leo hii bado hamjagawa maeneo, tena vijana wapo na wanataka kulima. Inasikitisha kuona wataalamu tupo, nia ya dhati ya Serikali ipo lakini watu hamchukui maamuzi. Tunataka sasa, tutoke hapo tulipo.”

 

Akifafanua kuhusu umuhimu wa kuwa na mashamba makubwa ya michikichi, Waziri Mkuu alisema si lazima mashamba hayo yalimwe au kumilikiwa na mtu mmoja. “Jiungeni watu kadhaa na mtenganishe hizo ekari zenu kwa barabara lakini lazima yawe sehemu moja,” alisisitiza.

 

Akitoa maagizo mahsusi kabla ya kufunga kikao hicho, Waziri Mkuu alizitaka Halmashauri zinazolima zao la chikichi, ziimarishe vitalu vya miche ya zao hilo. Pia alizitaka zitoe fedha zilizokuwa zinatengwa kwa ajili ya vitalu na kuzipatia taasisi zinazozalisha miche ikiwemo TARI–Kihinga, JKT Bulombora na gereza la Kwitanga ili zizalishe miche kwa ajili ya Halmashauri husika na kisha wazisambaze bure kwa wakulima katika maeneo yao.

 

Alielekeza ufanyike ufuatiliaji wa karibu wa miche ya michikichi inayopelekwa kwa wakulima ili miche hiyo ikue na kufikia hatua ya kuzaa.  Pia aliitaka Taasisi ya Utafiti wa Mbegu (ASA) iimarishe ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) ili kuzalisha miche mingi zaidi ya michikichi.

 

Akisisitiza kuhusu utoaji elimu, Waziri Mkuu alisema wadau wa zao la michikichi wakutanishwe mara kwa mara ili kutathmini na kujadiliana changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi. Pia alitaka waelezwe fursa zilizopo katika zao la michikichi na wananchi wataarifiwe ili waweze kutumia fursa hizo.

 

Aliitaka Wizara ya Kilimo iandae filamu ya Kitanzania inayoelezea vizuri kilimo cha zao hilo ili wakulima waone kwa uhalisia na kupata elimu kuhusu zao hilo.

 

Waziri Mkuu aliitisha kikao hicho ili kufanya tathmini ya zao la chikichi tangu Serikali ilipoanza mkakati wa kulifufua Julai, 2018. Alikutana na wadau hao ili kutafuta njia za kuliendeleza na kuhakikisha nchi inakuwa na kiasi cha kutosha cha mafuta ya mawese, hatua ambayo alisema itasaidia nchi kuepuka gharama kubwa zinazotumika kuagiza kiasi kikubwa cha mafuta kutoka nje nchi.

 

Kila mwaka, Serikali inatumia shilingi bilioni 470 kuagiza tani 360,000 kutoka nje ya nchi ili kufidia pengo la tani 650,000 za mafuta ya kula zinazohitajika nchini. Serikali ilichukua hatua za makusudi za kuliingiza zao la michikichi katika orodha ya mazao ya kimkakati ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa soko. Mazao mengine ya kimkakati ni pamba, tumbaku, kahawa, korosho, chai, mkonge, zabibu na alizeti.

 

Mapema, wadau mbalimbali walitoa maoni yao na kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji, kutokopesheka kwenye mabenki, ukosefu wa ardhi ili kufungua mashamba makubwa na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu mikopo. 


Wadau hao walijumuisha wakulima wadogo na wa kati, wazalishaji miche, wakamuaji mawese, viongozi wa vijiji, viongozi wa vyama vya ushirika, viongozi wa taasisi za fedha, viongozi wa wilaya, halmashauri na mkoa na Wabunge wa mkoa huo.

 

(mwisho)

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, FEBRUARI 27, 2023.


--
Irene K. Bwire

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Apiga Marufuku Matumizi ya Kipimo cha Bidoo

$
0
0

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kiwanda cha kuchakata mafuta ya mawese cha Trolle Messle Danieli Amulike  moja ya bidhaa itokanayo na zao la Chikichi wakati alipotembelea kiwanda hicho mjini Kigoma Februari 27, 2023.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kiwanda cha kuchakata mafuta ya mawese cha Trolle Messle, Danieli Amulike wakati alipotembelea kiwanda hicho hicho, kuona mtambo wa kukaushia mbegu za zao la Chikichi, mjini Kigoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kiwanda cha kuchakata mafuta ya mawese cha Trolle Messle, Danieli Amulike wakati alipotembelea kiwanda hicho hicho, kuona mtambo wa kukaushia mbegu za zao la Chikichi, mjini Kigoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa mtambo wa kukamulia mafuta ya mawese na Meneja wa SIDO mkoa wa Kigoma Gervas Ntahamba, alipotembelea viwanda vya kukamua mafuta hayo, kukausha mbegu za chikichi na kiwanda cha kusindika mafuta ya mawese cha Trolle Messle, mjini Kigoma.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Jumuiya ya Shia Tanzania

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa  Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Tanzania,(Tanzania Ithnashariya  Community)ulioongozwa Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, wakati wa mazungumzo na ujumbe huo leo ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa madhumuni ya kumpongeza Rais, wa Uongozi wake
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akimsikiliza Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Tanzania,(Tanzania Ithnashariya  Community)Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge wakati wa mazungumzo akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa madhumuni ya kumpongeza Rais, wa Uongozi wake
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa  Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Tanzania,(Tanzania Ithnashariya  Community)ulioongozwa Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge,(wa pili kulia)  wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar kwa madhumuni ya kumpongeza Rais, wa Uongozi wake wenye hekima
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na mgeni wake  Sheke Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Tanzania,(Tanzania Ithnashariya  Community)Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge,   baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao.

Masheha watakiwa kusimamia vyeti vya Mazao

$
0
0

Mkurugenzi Mwezeshaji Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Bakari Haji akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid kufungua Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la Karafuu ,katika  Ukumbi wa Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 febuari 2023. (PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid  akizungumza na Wadau na Wakulima wa Zao la  karafuu Wakati alipokua  akifungua mkutano wa Wadau hao   ulioandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa  Zanzibar ZSTC   huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati   Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 fubuari 2023.( PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR)
Katibu wa Shirika la Biashara laTaifa  Zanzibar ZSTC  Ali Hilal Vuai (alieshika kinasa sauti) alipokua akitoa tathmini ya utekelezaji wa kazi za Shirika wakati wa mkutano na Wadau na Wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa kusini Unguja, tarehe 26 so fubuari 2023 (PICHA NA FAUZIA MUSSA - MAELEZO ZANZIBAR).
Katibu wa Jumuiya  ya Wakulima wa zao la  karafuu (ZACPO)  Salim sleyum abeid alipokua akitoa salamu za Jumuiya katika mkutano wa wakutathmini zao Hilo Kwa mwaka 2022-2023 uliowashirikisha Wadau na Wakulima huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.(PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)
Wadau na wakulima  wa Zao la  Karafuu  walipokuwa katika Mkutano wa kutaathmini zao Hilo Kwa mwaka 2022-2023 ulioandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar ZSTC na kufanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 fubuari 2023.(PICHA NA FAUZIA MUSSA-ZANZIBAR)
Afisa kutoka Wizara  ya Kilimo Mussa Rajabu alipokua akihamasisha upandaji wa miche ya mikarafuu katika  Mkutano wa Wadau na Wakulima  wa Zao hilo uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.(PICHA NA FAUZIA MUSSA - MAELEZO ZANZIBAR)
Afisa masoko Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Aziza Baraka Omar   alipokua akitoa  elimu ya malipo na kutunza fedha  kupitia Benki hiyo wakati wa Mkutano wa wakulima na Wadau wa Zao la Karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)
Meneja wa Tigo pesa  Zanzibar Salum Nassor alipokua akitoa elimu kuhusiana na malipo kupitia Ezypesa -Tigopesa wakati wa Mkutano wa Wadau na wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini  Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.(PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)
Sheha wa Shehia ya Bambi Amour Mkombe  alipokua akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26,fubuari 2023.( PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)
Mkulima wa zao la karafuu Shehia ya Dunga bweni Abdalla Khamis Sadala akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26,fubuari 2023.( PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

Mkulima wa zao la karafuu Bungi Khamis Malik khamis  akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023( PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR) 

Mkulima wa zao la karafuu Shehia ya Koani Rukia Abdalla Mwinyi akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.( PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

 

Na Rahma Khamis Maelezo                      26/2/2023

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Masheha wa Mkoa huo kusimamia vizuri utoaji wa vyeti vya mazao hasa zao lakarafuu ili wakulima waweze kuuza bizaa zao kwa urahisi zaidi.

Wito huo ameutoa huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati katika mkutano wa wakulima na wadau wa karafuu wa kutathmini changamoto zinazowakabili wakati wanapokwenda kuuza karafuu zao katika Shirika la Biashara (ZSTC)

Amesema kuna baadhi ya masheha hawawajibiki ipasavyo katika kutoa vibali kwa wananchi jambo ambalo linawakosesha fursa wakulima kusafirisha bizaa zao kwa ajili ya mauzo ili kujikimu na maisha.

Aidha amefahamisha kuwa Serekali inaendelea kutegemea zao la karafuu katika kuongeza pato la nchi hivyo ipo haja ya kuliendeleza,kulitunza na kulithamini zao hilo kwa maslahi ya Taifa na wnanchi kwa ujumla.

Mkuu huyo ameinasihi Wizara ya Kilimo kuendelea kuvitunza vitalu vya miche ili wakulima wanufaike kwani miche hiyo ni muhimu katika kuendeleza kilimo cha zao hilo.

Akizungumzia suala la uaminifu kwa wakulima Mkuu huyo amesema kuwa kuna baadhi ya wakulma wanajitoa uamnifu kutokana na kuchanganya karafuu na makonyo wakati wa kuuza ili kujiongezea kipato jambo ambalo linapelekea kuondoa haiba ya zao hilo.

Hata hivyo amewashauri wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa makini katika kulilinda,kulitunza zao hilo kwani kuna baadhi ya watu wanaweza kuingiza karafuu kutoka nje ya nchi kinyemela na kushusha hadhi ya karafuu ya Zanzibar.

Nae Katibu wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Ali Hilali Vuai amesema kuwa miongoni mwa tathmini ya kazi zao ni kununua karafuu kutoka kwa wakulima ambapo kwa mwaka 2022/23 wamenunua tani 3785.000 zenye thamani ya Sh, 7151661000 za TZ.

 Aidha amefahamisha kuwa wamefanikiwa kununua karafuu ambazo hazijachanganywa na makonyo kwa mwaka huu kutokana na kununua mashine za kuchujia na kusema kuwa changamoto inayowakabili ni baadhi ya wakulima kupeleka karafuu ambazo hazijakauka vizuri jambo ambalo sio sahihi.

 Kwa upande wao wakulima wa zao hilo wamesema ukosefu wa visima katika maeneo ya mashamba ya mikarafuu imepelekea baadhi ya miti hiyo kufa kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.

Aidha wamiomba Wizara ya Kilimo kufanya utafiti wa ardhi ambayo itaweza kuota mikarafuu kwa ili zao hilo lipandwe kwa wingi Zanzibar

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Amemteuwa Dkt. Said Ally Mohamed

Maktaba kuu Zanzibar kwenda sambamba na Teknolojia

$
0
0


 Mtangazaji wa kipindi cha kumepambazuka katika Televisheni ya Zanzibar Calbe(ZCTV) Ndg.Homoud Abdallah(kulia),akiongoza kipindi cha kumepambazuka wakati akiwa na wageni kutoka Maktaba kuu Zanzibar ambao ni  Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar Ndg.Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim(wa pili kulia),pamoja na Mkuu wa Divisheni ya Maktaba Zanzibar Ndg.Mahfudha Abdallah(kushoto) jana tarehe 27/02/2023.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

WAZAZI na walezi nchini wameshauriwa kuwapeleka watoto wao katika maktaba mbalimbali nchini ili wajifunze masuala mbalimbali ya kitaaluma.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar Bi.Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim,katika kipindi maalum kinachorushwa mbashara na Kituo cha Televisheni ya Zanzibar Cable(ZCTV) iliyopo Migombani Zanzibar.

Amesema maktaba kuu nchini imeweka mazingira rafiki ya kuwajengea uwezo watoto mbalimbali ili wapate nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali kwa mujibu wa vipaji vyao.

Amesema vipindi hivyo vinajumuisha watoto kuanzia ngazi za nasari hadi kitado cha sita na kwamba hata watoto ambao umri wao bado sio wa kwenda skuli wanapata nafasi ya kujumuika na wenzao kwa nia ya kujifunza.

“Kila siku ya ijumaa tuna kipindi maalum cha watoto kunakuwa na huduma ya kusoma vitabu mbalimbali,michezo hata vipindi vya masomo vya elimu kwa njia ya luninga kwani mtoto kama hawezi kusoma basi atajifunza kwa njia ya Televisheni kupitia katuni na njia nyingine za kisasa”, alieleza  Ulfat.

Akizungumzia mipango ya taasisi hiyo kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 kuwa imeelekeza wajenge maktaba tatu za kisasa kwa Unguja na Pemba ili kuimarisha huduma za taasisi hiyo.

Bi.Ulfat, alisema wanajipanga kuhamia katika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), ili wananchi pamoja na wadau wengine waliopo nje ya nchi wapate huduma za taasisi hiyo kwa wakati.

Katika maelezo yake Mkurugenzi huyo Ulfat,alieleza kuwa wana dhamira ya kwenda na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuhakikisha maktaba zote za Zanzibar zinakuwa na vituo maalum ya ubunifu utakaowawezesha wanachama wa maktaba na wananchi kwa ujumla kuibua vipaji vya fani mbalimbali sambamba na kuendeleza vipaji hivyo.

Naye Mkuu wa Divisheni ya maktaba Zanzibar Mahfudha Abdallah,alisema kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa huduma nzuri na rafiki kwa wananchi wote.

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha machapisho,vitabu na taarifa mbalimbali za kitaaluma vinapatikana kwa wakati ili wanafunzi na wadau mbalimbali wanapata fursa ya kusoma na kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma,utamaduni,sayansi na saikolojia.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili katika maktaba kuu nchini kuwa ni udogo wa eneo la ofisi hiyo haliendani na mahitaji yao kwa sasa.

“Wananchi wengi bado wana dhana ya kuwa maktaba zipo kwa ajili ya wananchi jambo ambalo sio sahihi kwani taasisi hiyo ipo kwa ajili ya watu wote kulingana na mahitaji wanayotaka kujifunza”, alisema Mkuu huyo wa Divisheni ya Maktaba nchini bi.Mahfudha.

Bi.Mahfudha, alisema kwa sasa wananchi wengi wameanza kuelewa umuhimu wa maktaba na kwamba wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kupata huduma za kusoma machapisho ya vitabu na nyaraka.

EU yaridhishwa na uboreshwaji wa haki za binadamu, utawala bora nchini

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akichangia jambo wakati wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya. Majadiliano hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti akitoa mchango wake wakati wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya. Majadiliano hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti wakionesha makubaliano waliyosaini baada ya majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yakiendelea Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akichangia mjadala wa kisiasa kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya Jijini Dar es Salaam

Mabalozi wa Tanzania katika Nchi za Jumuiya ya Ulaya wakitambulishwa 

Picha ya pamoja 

Dar es Salaam, 27 Februari 2023

Jumuiya ya Ulaya (EU) imeonesha kuridhishwa na hatua ambazo Serikali ya Tanzania imekuwa ikizichukua katika kuboresha masuala ya haki za binadamu, demokrasia, uhuru wa kuongea na utawala bora.

Hayo yamebainishwa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania wakati wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na EU yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema katika majadaliano hayo EU imeoneshwa kuridhishwa na hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikizichukua kuboresha masuala ya haki za binadamu, demokrasia, uhuru wa kuongea na utawala bora.

“EU wamefurahishwa na hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kuboresha haki za binadamu na demokrasia, …..tumeeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali na wenyewe hata kabla ya kuwafahamisha tayari walishaona na wameridhika kuwa tumepiga hatua katika eneo hili, kwa kuimarisha haki za binadamu, demokrasia, uhuru wa kuongea na mengine mengi waliyoeleza ambayo yanaonesha kuwa Tanzania tumepiga hatua kubwa kwenye eneo hili,” alisema Dkt. Tax  

Dkt. Tax amesema pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala ya uchumi wa buluu, mazingira, ushiriki wa Tanzania katika shughuli za Kikanda na Kimataifa na jinsi gani Tanzania inaweza kufanya kazi kwa pamoja na EU ili kuhakikisha yale yote yanayofanyika Kikanda na Kimataifa yanakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Aidha, Dkt. Tax ameongeza kuwa wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano wa Kimataifa, biashara na uwekezaji, kuboresha urari wa biashara kati ya Tanzania na EU kuwa chanya, mabadiliko ya tabia nchi, ushiriki wa Tanzania katika nyanja za kikanda na kimataifa, vita ya Urusi na Ukraine na athari zake.

Kwa Upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema kuwa mkutano wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na EU umekuwa muhimu kwa kuwa umetoa picha ya masula ya kisiasa zaidi na kupata uelewa wa kisiasa nchini Tanzania.

“Kupitia mkutano wa majadiliano ya kisiasa wa leo tumeridhishwa na mazingira ya siasa nchini Tanzania,” aliongeza Balozi Fanti

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Wizara. Ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga amesema katika mjadala wa kisiasa ulijikita katika makundi matatu ambayo ni ushirikiano wa uwili (bilateral cooperation) kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, masuala yanayohusiana na Kikanda (kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na mambo yanayoendelea duniani.

“Makundi yote matatu na agenda zake yalijadiliwa kwa kina, masuala yaliyojadiliwa kwa upande wetu Tanzania ni masuala ya mabadiliko ya mabadiliko ya tabianchi……………. biashara na uwekezaji, stratejia mbalimbali zinazotolewa nan chi za umoja wa ulaya,” Alisema Balozi Mindi

 


Wanahabari Mahiri Wa Habari Za Wanawake Na Uongozi Wapatikana

$
0
0

Mshindi wa kwanza kipengele cha magazeti Hussna Mohamed Khamis akikabidhiwa tuzo na Waziri wa habari Zanzibar Tabia Maulid Mwita.
Amina Massod kutoka Redio jamii mkoani Pemba alieibuka kuwa mshindi wa kipengele cha redio jamii.
Zuhura Juma Saidi kutoka mtandao wa Pembaportal alieibuka mshindi wa tuzo ya wanahabari kupitia mtandao wa kijamii akikabidhiwa zawadi na katibu mtendaji wa Tume ya utangazaji Zanzibar Suleiman Abdalla.


·         Radio jamii na mitandao ya kijamii zang’ara

 

Jumla ya waandishi wa habari 10 wameibuka kidedea katika tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi zilizoandaliwa na TAMWA, Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO).

Miongoni mwa vipengele ambavyo vilikuwa vinashindaniwa ni pamoja na mwandishi mahiri katika kipengele cha radio za kitaifa, radio za kijamii, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii, ambapo kwa upande wa magazeti kulikuwa na washindi watatu, mitandao ya kijamii watatu, radio za kijamii washindi wawili na washindi wawili kutoka katika radio za kitaifa.

 

Katika washindi hao 10 waliopatikana, jumla ya washindi wane (4) wa kwanza kutoka katika kila kipengele walipatiwa zawadi na cheki ya  milioni moja, tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki.

 

Washindi hao wanne kutoka katika kila kipengele ni pamoja na Husna Mohammed Khamis kutoka gazeti la Zanzibar Leo, Rehema Juma Mema kutoka radio Asalaam FM, Zuhura Juma Said wa mtandao ya kijamii wa Habari Portal na Amina Masoud Jabir kutoka radio Jamiii Mkoani kisiwani Pemba, ambapo washindi wa pili nao walijipatia vyeti pamoja na cheki ya shilingi laki tano (5) kwa kila mmoja, ambapo mshindi wa tatu katika kila kipengelke alizawadiwa cheti pamoja na cheki ya shilingi laki nne (4).

 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajauni, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein Ali Mwinyi ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita alisema kuwa kilio cha wanahabari kuhusu mabadiliko ya sheria ya huduma ya habari kuwa Serikali imewasikia na ipo njiani kuzibadilisha ili muifanye kazi yenu kwa umahiri zaidi na bila ya wasiwasi wowote.

 

“Tunataka kuwa na sheria ambayo imetokana na pande mbili yaani wadau wa habari na Serikali”, amesisitiza Waziri Tabia.

 

“Nimekuwa nikifuatilia vyombo vya habari na kuona kuwa  Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 na marekebisho yake ya mwaka 1997 na  Sheria No.8 ya 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2010 zikilalamikiwa zaidi kuwa na mapungufu na zinahitaji kurekebishwa pamoja na  sheria nyingine kadhaa zinazohusiana nazo” alisisitiza.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Zanzibar Dkt.Mzuri Issa aliiomba Serikali kuhakikisha kwamba ile asilimia 40 ya ushiriki wa wanawake inafikiwa katika kila nyanja ya vyombo vya maamuzi ikiwemo kamati, bodi za utendaji, hivyo hakuna budi kuwa na mazingira mazuri ya kuwewezesha wanawake kushiriki katika uongozi katika ngazi zote.

 

“Tunasisitiza pia kuandaa takwimu za wanawake na Uongozi jambo hilo litasaidia kujua hasa tuko wapi katika malengo hayo ambayo ni ya kimilenia, lengo nambari 5 la milenia (sustainable development goal, SDG), na sisi taasisi zetu tunaahidi kutoa mashirikiano ya kina”. Aliongeza Dkt Mzuri Issa.

 

Tuzo hizi za uandishi wa habari za takwimu kwa wanawake na uongozi ni muhimu sana katika kushajihisha waandishi wa habari wa Zanzibar kuandika zaidi habari na makala kuhusiana na masuala ya wanawake na uongozi, lakini pia kutoa takwimu ya idadi sahihi ya wanawake walioko katika uongozi Zanzibar.

 

TAMWA, Zanzibar imeamua kuchukua juhudi mahasusi za kuandaa tuzo hizo ili jamii itambue mchango wa wanawake na uongozi katika sekta mbalimbali ili kuinua hali za wanawake na kuongeza ushiriki wao  katika masuala ya uongozi ili kufikia 50 kwa 50 katika katika ngazi zote za maamuzi kama inavyoelezwa katika katiba nchi yetu na mikataba na itifaki mbali mbali za kimataifa.

 

TAMWA, Zanzibar inatoa wito kwa waandishi wa habari wa zanzibar kuendelea kuandika habari zinazohusu wanawake, takwimu lakini pia vikwazo mbalimbali vinavyomzuia asifikie nafasi za uongozi na kuwa tayari kushiriki katika tuzo zijazo ambazo zitaandaliwa.

 

Tuzo hizo ambazo ni mara ya pili kutolewa zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) na Ubalozi wa Norway.

 

Jumla ya kazi 421 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio, televisheni pamoja mitandao ya kijamii, zilipitiwa katika kutafuta washindi hao katika  tuzo hizo zenye kauli mbiu “KALAMU YANGU MCHANGO WANGU KWA WANAWAKE” hivyo waandaji wa tuzo hizo zinawaomba waandishi wa habari kujitahidi kuandika habari za kina za wanawake na uongozi.

 

Dkt. Mzuri Issa

Mkurugenzi

TAMWA, ZNZ.

 

Tanzania kuanza safari za moja kwa moja Saudi Arabia

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Abdulwahab wakikabidhiana zawadi baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini akijadiliana jambo na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Abdulwahab katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Tanzania inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.

 

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

 

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.

 

DC Moyo Ameaza Ziara na Maagizo Mazito

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka viongozi wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wanatakiwa kuwatumikia wananchi wa Nachingwea.

Akizungumza wakati wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo sema kweli sio majungu ya ,Moyo alisema kuwa hataki kusikia habari za mchakato kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ya serikali.

Moyo aliwataka viongozi kutatua changamoto na kero za wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya hivyo kama kutakuwa na kiongozi hataendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita basi akae pembeni awapishe wengine wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kasi ya serikali ya awamu ya sita.

Akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo alitoa siku saba kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha wanawapa wazee kadi za matibabu kama ambavyo serikali ya awamu ya sita inavyotaka.

Moyo aliwataka viongozi wa TARURA kuwasimamia vilivyo wakandarasi wote ambao wamepewe kazi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo ili zijengwe kwa kiwango kinachotakiwa.

Aidha Moyo alimtaka Injinia wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha miradi yote inajengwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu pamoja na Halmashauri kwa faida ya Taifa na Wananchi wote.

Moyo alimazia kwa kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa walinzi wa amani ili kuondoa vurugu na migogoro mbalimbali ambayo imekuwa inahatarisha amani Taifa 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Nachingwea na watayafanyia kazi kwa faida ya wananchi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan apokea Hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Nchi 6, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Ukraine hapa nchini Mhe. Andrii Pravednyk, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Ukraine Mhe. Andrii Pravednyk mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Slovak hapa nchini Mhe. Katarina Zuffa Leligdonova, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Slovak mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Hungary Mhe. Zsolt Meszaros, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Hungary Mhe. Zsolt Meszaros mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Israel Michael Lotem, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Israel  Michael Lotem, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ghana Damptey Bediako Asare, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Ghana Damptey Bediako Asare, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ureno  Antonio Manuel Coelho Da Costa Moura, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Ureno  Antonio Manuel Coelho Da Costa Moura mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
 PICHA NA IKULU.

Rais Dk Hussein Mwinyi azungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, ikiwa ni kawaida yake ya kuzungumza na Waandishi wa habari na Wahariri wa vyombo vya habari kila mwisho wa mwezi, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-2-2023.(Picha na Ikulu)

WAANDISHI wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano wake wa kila mwisho wa mwezi na Waandishi uliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-2-2023.(Picha na Ikulu)

 MWANDISHI wa Habari wa kujitengemea Bw.Ligwa  Paulin akiuliza swali katika mkutano wa Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari viliopo Zanzibar, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-2-2023.(Picha na Ikulu)

MWANDISHI wa Habari wa Azam TV Bi. Mtumwa Said Nassir, akiuliza swali katika mkutano wa Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari viliopo Zanzibar, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-2-2023.(Picha na Ikulu)

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, ikiwa ni utaratibu wake wa kuzungumza na Waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-2-2023.(Picha na Ikulu)
 

Msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya mizunguko 22

Reja asisitiza kutunzwa vizuri nyaraka na kumbukumbu za CCM

$
0
0

KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,akikagua chumba maalum cha kuhifadhi nyaraka na machapisho mbalimbali katika taasisi ya kumbukumbu na nyaraka Zanzibar.
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,akikagua studio za kituo cha radio ya Bahari FM kilichopo Migombani Zanzibar.
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,wakikagua gari zilizotumia aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume zilizohifadhiwa sehemu maalum
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,wakikagua gari zilizotumia aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume zilizohifadhiwa sehemu maalum
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,wakiomba dua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume huko Kisiwandui.
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,pamoja na viongozi wengine na familia wakiomba dua katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania marehemu Aboud Jumbe.
KATIBU wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,wakiomba dua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume huko Kisiwandui.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),kimesema kitaendelea kutunza,kuhifadhi na kudhibiti zisiharibiwe kumbukumbu na nyaraka zake za kihistoria ili ziwanufaishe vizazi vya sasa na vijavyo.

Hayo ameyasema Katibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa Salum Khatib Reja,wakati akitembelea na kukagua maeneo ya historia ya CCM yaliopo maeneo ya Unguja ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuyajua na kuyatambua maeneo yote ya historia ya chama.

Alisema kumbukumbu hizo zimebeba historia halisi ya CCM inayotakiwa kuenziwa na kulindwa kikamilifu.

Katibu huyo alieleza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2022 ibara ya 107(2)(f) inayotoa maelekezo kwa Idara ya itikadi na uenezi ina wajibu wa kutekeleza jukumu la kutunza kumbukumbu hizo za chama.

"Idara ya Itikadi na Uenezi ndio imepewa jukumu na chama la kuhifadhi na kuendeleza historia ya chama hivyo tuhakikishe tunatekeleza majukumu haya tuliopewa,"alisema

Mbali na hilo,Katibu huyo pia aliwataka watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Mkoa na Wilaya kuanza kutengeneza mifumo mizuri ya kutunza kumbukumbu za chama tangia kuzaliwa kwake.

Pamoja na hayo alisema Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ni sehemu ya mambo makuu yanayojenga historia ya CCM, hivyo kuna umuhimu wa jamii kujifunza historia hiyo.

Aliziagiza  ofisi ya CCM kuanzia mkoa hadi wilaya kuweka historia ya kuonyesha idadi ya makatibu wa ngazi hizo waliongoza tangu kipindi cha mwaka 1977.

 

"Lazima tuwe na ubao ofisi za chama ambao utaonyesha katibu wa kwanza wa CCM alikuwa nani alikuwa katibu kuanzia lini mpaka lini,"alisema

Katibu huyo alisema kuna baadhi ya kielelezo cha historia bado hakijahifadhiwa kwenye kumbukumbu ikiwemo eneo la Mbuzini ambalo lina historia kubwa kwa chama.

"Kwenye kumbukumbu eneo la Kilombero lipo lakini hili eneo la Mbuzini bado hatujaweka kumbukumbu licha ya kuwa lina historia kubwa kutokana na kuwa ASP ilinunua eneo hili kwa ajili ya kuzikana wanachama waliobaguliwa enzi za ukoloni.,"alisema

Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis alisema Idara yake itahakikisha inahifadhi na kuzitunza vielezo vyote vya kihistoria vya chama.

Alisema idara hiyo ina mpango wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama wake juu ya masuala mbalimbali ya historia ili kuwajenga kisaikolojia waendelee kuwa wazalendo.

Katibu huyo wa sekretarieti Taifa Roja, alitembelea maeneo mbalimbali ya CCM yakiwemo Ofisi ya CCM Wilaya ya Mjini iliyokuwa Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa ASPYL pia lilitumika kuwapokea wapigania uhuru wa Chama cha frelimo na katika jingo la Chama cha Shiraz Association lilipo Kijangwani.

Nyingine ni taasisi ya nyaraka na kumbukumbu kilimani Zanzibar, kituo cha radio bahari FM,iliyokuwa nyumba ya ASP katika eneo la Muembe Kisonge,iliyokuwa nyumba ya vijana wa chipukizi wa zamani(YASO) pamoja na iliyokuwa nyumba ya chama cha African Association iliyopo kikwajuni.

Maeneo mengine ni iliyokuwa nyumba ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Aman Karume iliyopo Kisima Majongoo Kikwajuni pamoja na nyumba ya Wananchi Forodhani na jingo la ASP lililopo Kijangwani.

Aidha, maeneo mengine yaliyotembelewa ni shamba la CCM lililopo Kilombero,eneo alipozaliwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume,shamba la ASP lililonunuliwa kwa ajili ya kuzika wanachama wake waliotengwa na wakoloni,kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Aboud Jumbe pamoja na kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume.

 


Mhe Hemed akutana na UVCCM

$
0
0



 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameupongeza Uongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa mipango yake madhabuti ya kuandaa vijana wenye nidhamu, na utii katika ngazi mbali mbali za Uongozi.

 

Mhe. Hemed ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jumuiya hiyo Ofisini kwake Vuga wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Muhamed Ali Muhamed (Kawaida).

 

Amesema ni jambo lililowazi kuwa Jumuiya hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kulea Vijana kuwa Viongozi Imara na wenye Maadili ambapo tokea kuasisiwa kwake mwaka 1978 tayari Viongozi wengi Nchini wamepitia katika Jumuiya hiyo.

 

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa amewahakikishia kuwapa mashirikiano ya kila namna kwa kuiunga Mkono Jumuiya hiyo ili iweze kufanikisha Shughuli zake za kila siku.

 

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameupongeza Uongozi wa UVCCM kwa kuandaa mpango mkakati ambao umelenga kuiletea mabadiliko Jumuiya hiyo kwa kufanya mapitio ya miradi na kutayarisha mpango mkakati ambao utakuwa na tija zaidi kwa jumuiya hiyo

 

Amesema kuboreshwa kwa vitega uchumi hivyo kutarahisisha  uendeshaji wa shughuli za Chama na Jumuiya zake pamoja na kupatikana ajira zitakazowanufaisha vijana nchini.

 

Mhe. Hemed ameutaka Uongozi huo kuendelea kuwaelimisha Vijana dhamira ya uwepo wa Jumuiya hiyo ikiwemo kutekeleza na kutimiza shabaha na madhumuni ya Chama Cha Mapinduzi, kuhakikisha kuwa vijana wanaandaliwa katika misingi ya kuthamini umoja wa Taifa, kuwaanda vijana kuwa wanachama safi na Viongozi bora wa CCM na Serikali na kuwa raia wema wa taifa pamoja na kuendelea kuhamasisha Amani na Utulivu iliyopo Nchini.

 

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali katika ujenzi wa Miradi ya maendeleo ili Wananchi wafahamu dhamira Njema ya Serikali zao.

 

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amempongeza Mwnyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Bara Ndg. Abdulrahman Kinana kwa kuendelea kutoa maelekezo kwa lengo la kukijenga na kukiendeleza  Chama Cha Mapinduzi.

 

Akizimgumza kwa niaba ya Viongozi hao Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg. Mohamed Ali Mohamed (Kawaida) amemueleza Mhe. Hemed kuwa UVCCM inaimani na kasi ya Serikali zote mbili zinazoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya kuwaletea maendeleo watanzania na kuahidi kuendelea kuunga Mkono juhudi hizo kwa maslahi ya Taifa.

 

Aidha Ndg. Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kufanyika  Mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ikiwa ni sehemu ya kupanua wigo wa demokrasia nchini  na kueleza kuwa fursa hiyo itumike kuhamasisha umoja na mshikamano na kuepuka kuwagawa watanzania.

 

Katika kikao hicho Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amekabidhi Kompyuta kwa Wilaya zote kumi na mbili za Zanzibar Kichama ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa kwa Jumuiya hiyo kwa lengo la kuimarisha utendaji.

 

…………………………

Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

01/03/2023

Dk Hikmany ateuliwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar

Shule ya Sekondari Coastal ya Jijini Tanga Kiaza Kunifaika na Mkonge

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akizungumza wakati wa maafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga yaliyofanyika kwenye Hotel ya CBA Jijini Tanga.

Na Oscar Assenga,Tanga.

Shule ya Sekondari Coastal ya jijini Tanga,itaanza kunufaika na uwekezaji wa sekta ya mkonge baada ya Bodi ya Mkonge Tanzani (TSB) kuahidi kuiingiza katika majaribio ya klabu za vijana watakaoendelezwa.

Pia shule hiyo imeahidiwa kupewa ekari 100 kwa ajili ya kilimo cha mkonge ikiwa ni sehemu ya kuiongezea kipato .

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mko n ge nchini,Saad Kambona alitoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita walioanza mtihani ya kitaifa.

Alisema bodi hiyo imeandaa programu maalumu itakayowawezesha vijana kujiinua kiuchumi kuptia kilimo cha mkonge na bidhaa zitoakanazo na zao hilo.

Alisema kama inavyofahamika Bodi ya Mkonge ni taasisi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni kama imekufa sasa imeshafungua rasmi ofisi katika jengo lake na kuwezesha kuinua sekta ya mkonge kwa ujumla wake.

“Lakini tunategemea tunapokwenda mbele vijana wengi sana kutoka kwenye shule za Tanga ndiyo wahusike kwenye mpango mzima wa kuleta mapinduzi kwenye zao la mkonge kwani sasa hivi tunapozungumzia mkonge tunazungumzia bidhaa moja tu ya nyuzi za mkonge zitengeneze vikapu, makapeti, magunia, kamba na bidhaa nyingine zitokanazo na zao hilo ,lakini kuna bidhaa nyingti zinahitajika kama sukari,mbolea mvinyo na hata vyakula vya kunenepesha mifugo” alisema Kambona

Mkuu wa shule hiyo,Joseph Gaspar alisema ilianza rasmi mwaka 2000 na kwamba kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikitoa ufaulu wa daraja la kwanza A na pili kwa wanafunzi wote wa kidato cha sita wote katik a mitihani ya kitaifa ya mchepuo wa sayansi.

“Hadi sasa shule hii imetimiza miaka 22 lakini kwa kipindi cha miaka miatatu mfululizo i mekuwa ikitoa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na la pili katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita...tunatarajia mitihani hii ufaulu utakuwa wajuu zaidi”alisema Gasper.

Makamu mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George alisema kuwa miongoni mwa mambo yanayotiliwa mkazo ni masomo ya sayansi wakiamini kuwa jukumu lao ni kupata wataalamu watakaoiendeleza nchi katika sekta ya uhandisi,udaktari na utafiti mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo na ufugaji.

WAZIRI MKUU AKAGUA HALI YA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo ,Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam



Waziri Mkuu Kassim akifafanuliwa jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakub wakati akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana.
Waziri Mkuu Kassim akifafanuliwa jambo na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Balozi Pindi Chana, wakati akikagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakub.
Waziri Mkuu Kassim akuzungumza na Viongozi wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Baraza la Michezo Tanzania, wakati alipokagua hali ya Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa, baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo Machi 1, 2023 jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar awasilisha muelekeo wa Mpango wa maendeleo na Bajeti ya Serikali 2023/2024

$
0
0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar  Dr Sada Mkuya Salum amewasilisha muelekeo wa  Mpango wa maendeleo na Bajeti ya Serikali 2023/2024 na kueleza kwamba kutakua na mazingatio mahsusi ikiwemo ongezeko la Bajeti ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, pensheni ya Wastaafu na Pensheni Jamii, kuanza kulipa asilimia 3.5 ya mshahara kwa ajili ya mfuko wa huduma ya Afya, Ununuzi wa Vitendea kazi ikiwemo magari na ujenzi wa ofisi za serikali pamoja na kutoa kipaombele katika malipo ya madeni ya Wazabuni, Wakandarasi na Watumishi wa Umma.

Viewing all 36158 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>