Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35828 articles
Browse latest View live

NMB yachangia 10m/- Kibaigwa

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
BENKI ya NMB imetoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya skuli na hospitali katika kata ya Kibaigwa ikiwa ni jitihada za kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kuwaunga katika maendeleo ya kibenki.

Hayo yalibainishwa na Meneja Kanda ya Kati, Gabriel Ole Loibanguti,katika ufunguzi wa tawi jipya la benki hiyo.

“Kwa kutambua nia ya kuendelea kuchagangia huduma mbalimbali, benki ya NMB imetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili  kuchangia  maendeleo ya wanachi wa Kibaigwa  kama shukrani zetu,” alisema.


Alisema fedha zitakabidhiwa pale uongozi wa benki hiyo utakapokaa na wa wilaya ya Kongwa.

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa tawi hilo, wananchi walikuwa wakifuata huduma za kibenki makao makuu ya wilaya Kongwa na wengine kusafiri hadi Dodoma mjini.

Alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kunatokana na wananchi na wafanyabiashara wa soko la mahindi Kibaigwa kuhitaji huduma hiyo kutokana na kutembea na fedha zao mkononi na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Aidha alisema kufunguliwa kwa tawi hilo, NMB inafikisha jumla ya matawi ya benki hiyo kufikia 150 na zaidi ya mashine 500 za ATM kwa nchi nzima.

Akizindua benki hiyo, Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai,aliishukuru benki hiyo kwa kutambua umuhimu wa kuwapelekea wananchi huduma hiyo.

Alisema  awali usalama wa fedha za wananchi na wafanyabiashara wanaouza mazao na matrekta zilikuwa mashakani kutokana na wezi  na majambazi.

Alisema tawi hilo litawasaidia wananchi wa eneo hilo kufaidika na mikopo inayotolewa na benki hiyo jambo ambalo litasaidia kuinua vipato na  uchumi wa eneo hilo.


Aliiomba benki  hiyo kuwapunguzia wananchi  masharti ya mikopo inayotolewa kwao pamoja  na  riba zinazotozwa ili kujenga uhusiano mzuri kutoka idara hizo.

Waathirika wa ubakaji watoa kauli

$
0
0
Na Haji Nassor, Pemba
Waliobakwa na kisha kuozwa waume katika wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, wamesema ndoa za mkeka zinazofungwa kama sulhu, zinachangia kwa kiasi kikubwa kasi ubakaji katika jamii.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umeonesha jamii imekuwa na uharaka wa kuwafungisha ndoa mara wanapobaini kuwepo vitendo hivyo,wakidhani ndio sulhu ya kuvitokomeza badala yake vimekuwa vikichangia kuongezeka.

Uchunguzi umebaini imekuwa na kawaida kuharakia sulhu ya ndoa, hata kama shauri hilo limeshafikishwa katika vyombo vya sheria, jambo ambalo huwapa jeuri na kiburi wabakaji.

Mmoja kati ya waathirika wa ubakaji na kisha kuolewa mwenye miaka 17, mkaazi wa shehia ya Mchangamdogo wilayani humo, alisema binafsi baada ya kujihisi ameshapewa ujauzito, alikimbilia kituo cha polisi na kisha muhusika kukamatwa.

Awali, alimueleza mpenzi wake huyo kwamba, ameshampa ujauzito na alipokataa, ndipo alichukua uamuzi wa kukimbilia kituo cha polisi Wete,inagwa kesi hiyo haikufikishwa mahakamani.


Nae muathirika mwengine wa vitendo hivyo, mkaazi wa shehia ya Mchangamdogo (18) ambae alikatisha masomo alisema, mara baada ya kubainika na wazazi wake kwamba ameshapata ujauzito, harakati za kuolewa zilianza.

Aliwekewa mkazo na wazazi wake na hata baadhi ya marafiki, kwamba ni vyema akakubali kuolewa na baada ya kujkifungua aliachwa.

Wazazi wa vijana hao wa kike walikiri kufanya hivyo, kutokana na kuogopa usumbufu katika vyombo vya sheria.

Kwa upande wake Mratibu wa wanawake na watoto wa shehia ya Mchangamdogo, Mbeu Makame Bakari, alisema chanzo cha vitendo hivyo ni kwa wakosaji kukosa kutiwa adabu inayofaa.

Sheha wa shehia ya Kinyikani wilaya ya Wete, Mussa Rashid Said, alieleza kuwa, chanzo cha vitendo hivyo ni kuondoka kwa malezi ya pamoja ambayo yalikuwa katika miaka ya iliopita.


Nae Mratibu wa wanawake na watoto wa shehia ya Mjini Ole, Khadija Henop Maziku, alisema, bado jamii haijaona ubakaji kuwa tatizo kutokana na kupuza pale linapotokezea katika shehia zao.

Wauza kuku Darajani wapewa kifaa cha kuchujia manyoya

$
0
0
Na Zainab Anuwar
Mkurugenzi wa Manispaa Zanzibar, Abedi Juma Ali, wamewataka wafanyabiashara wa soko la kuku Darajani kufanya shughulia katika hali ya usafi.

Aliyasema hayo wakati akizindua kifaa cha kuchujia manyoa ya kuku kwa lengo la kuweza kudhibiti utapakaaji wa manyoa hayo ndani na nje ya soko hilo.
Alisema kifaa hicho kitasaidia kiwango kiasi kikubwa  kulinda  mazingira katika soko hilo.

Aidha aliwataka kushirikiana na manispaa kuhakikisha hali ya usafi inaimarishwa katika soko hilo.


Mwenyekiti wa Glitters Volunteer Group Zanzibar Cleaning, Mohamed Khamis,  alisema manyoa ni mali ambayo hutumika kutengenezea mambo mbali mbali kama vile nguo pamoja na kutumika kama ni mbolea.

Hata hivyo, alisema bado soko la manyoa kwa Zanzibar ni dogo kutokana na idadi ndogo ya kuku wanaochinjwa.


Alisema kifaa hicho kitasaidia kutunza mazingira ya soko hilo na utapakaaji wa manyoya uliozoeleka katika soko hilo.

Rais Kikwete Afungua Rasmin Barabara ya Mwenge - Tegeta Jijini Dar-es-Salaam.

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

  Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa tayari tayari kumrekodi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua  rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifurahia baada ya kufungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.(WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI.)

$
0
0
Na.Mwashungi Tahir Maelezo.
Iko haja kubwa jamii kuwaheshimu wazee kwani bila ya wao kutulea kwa kutupa malezi mazuri kwa kutusomesha tusingelikuwa leo tuko hapa.
Hivyo iko haja kuwatunza , kuwalea na kuwathamini kwa malezi mema yao waliyotupa .

Hayo ameyasema mkuu wa Mkoa mjini magharibi Abdullah Mwinyi Khamis wakati alipokuwa akizungumza na wazee huko Dole wilaya ya magharibi katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani .

Amesema wazee wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii katika ujana wao katika kushiriki mambo mbali mbali ya kiuchumi  kiutamaduni  na vile vile kijamii katika serikali.

Hivyo tunahitaji kuwalea wazee kwa kuwatunza kwa kuwapa huduma  zikiwemo malazi kivazi  pia ikiwemo huduma ya kuwapatia chakula waweze kuwa na siha nzuri katika maisha yao.


“Serikali inatoa mchango mkubwa katika kuwaenzi wazee hao mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu mzee Karume aliwashughulikia kwakuwajengea nyumba za kuishi wazee hao pamoja na huduma nyengine zote za jamii” alisema Abdullah Mwinyi 

Abdullah Mwinyi ametoa wito kwa jamii iachane kuwatelekeza Wazee  na kutoa msisitizo kwa kuwahifadhi na kuwapa huduma nzuri kama ilivyo kwa kawaida kwa binaadamu.

Nae Katibu Mkuu wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii , Vijana , Wanawake na Watoto Asha Ali Abdullah amesema serikali imepitisha sera ya hifadhi jamii ya kulinda na kuwahifadhi wazee kwa vizuri.

Siku hii ni siku muhimu  inasherehekewa Duniani kote kila ifikapo tarehe 1-10-2014 ambapo ujumbe wa mwaka huu (WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI).

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Katibu mkuu Mufti shekh Soraga na M kuu wa Wilaya magharibi Ayoub Moh'd Mahmoud .

Yaliojiri Dodomo leo Bunge la Katiba.

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Yahya Kassim Issa akiomba mwongozo leo Bungeni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kuhusu kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman kuja kupiga kura na kukataa baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati alijitoa kwenye Kamati ya Uandishi ambapo alitakiwa awepo akitetea maslahi ya Zanzibar, jambo ambalo limewachanganya baadhi ya wajumbe. 
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pamoja Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo. 
Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo na Mjumbe Wabunge hilo nje jengo la bunge Dodoma.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani viwanja vya Dole Unguja.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mhe. Abdallah Mwanyi Khamis akiwahutubia Wazee katika maaadhimisho ya siku ya Wazee Dunuiani(kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Wastawi wa jamii, Vijana Wanawake na Watoo Asha Ali Abdallah na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Ayubu Moh’h Mahmoud, zilizofanyika viwanja vya mpira dole wilaya ya magharibi unguja leo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Wastawi wa jamii, Vijana wanawake na Watoto Bi. Asha Ali Abdallah akimkaribisha Mgeni Rasmin katika maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani.
Baadhi ya wageni waalikwa katika siku ya wazee Duniani.wakiwa katika viwanja vya sherehe hiyo zilizofanyika katika viwanja vya dole Wilaya ya Magharibi Unguja imeadhimishwa kitaifa Unguja leo. 
 Baadhi ya Wazee waliohudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani iliyoazimishwa leo huko Dole Wilaya ya Magharibi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis mgeni Rasmin katika Maazimisho ya Siku ya Wazee Duniani zilizoadhimishwa katika viwanja vya mpira Dole,akiangalia Mkoba na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na wazee hao. maadhimisho hayo yamifanyika huko dole Wilaya ya Magharibi Unguja.(Picha na Miza Othman Maelezo-Zanzibar).

Magazetini Tz Leo Bongo.


DK.Shein Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza  Kuku  (Perdue)kutoka Marekani  Dk.David Elua akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja jana kwa mazungumzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza  Kuku (Perdue) kutoka Marekani unaoongozwa na  Dk.David Elua  katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja jana .[Picha na ramadhan Othman Ikulu.]

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                                                    1.10.2014
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa hatua ya Kampuni ya ZANCHICKS kuekeza Zanzibar zitaweza kufikisha malengo ya uekezaji hapa nchini  sambamba na kuinua soko la ajira na kukuza uchumi.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK huko Ikulu mjini Zanzibar. Kampuni ambayo kwa hivi sasa inajishughulisha na uagizaji wa malighafi zake kutoka nje ambazo ni nyama ya kuku na kuuza hapa nchini.

Katika maelezo yake Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa miongoni mwa azma na malengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuinua sekta ya uekezaji ni kuhakikisha wananchi wake wanapata ajira hatua ambayo pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Dk. Shein alisema kuwa kuanzisha biashara ya nyama ya kuku hapa nchini kunatoa fursa kwa wananchi kutumia chakula hicho ambacho kimekuwa na walaji wengi hivi sasa sambamba na kuimarika kwa wafanyabiashara hiyo hapa Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein aliueleza uongozi huo haja ya kutoa ushirikiano na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wa aina hiyo wazalendo hapa Zanzibar ambao nao pia, wanahitaji kuimarika zaidi kibiashara kama ilivyo kwa kampuni hiyo hivi sasa.

Dk. Shein alisisitiza kuwa hatua hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wazalendo kuweza kuimarika kibiashara hali ambayo itasaidia lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kupambana na umasikini pamoja na kufikia lengo la Dira 2020 katika ukuaji uchumi wa Zanzibar.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara pamoja na Taasisi zake husika zitaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Kampuni hiyo ili kuhakikisha inaendelea kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi.
  
Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa soko la biashara hiyo kwa hapa nchini ni kubwa sana hivyo, jambo kubwa linalohitajika ni kuendeleza na kupanua soko la biashara hiyo ili Kampuni hiyo iweze kupata mafanikio zaidi na kufikia lengo ililojiwekea katika biashara zake.

Sambamba na hayo, Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa katika biashara yoyote ile suala la ushindani wa kibiashara haliepukiki hivyo, ni jambo la busara kwa Kampuni hiyo kufanya biashara zake kwa kuwavutia watumiaji pamoja na kutoa ushirikiano kwa jamii.

Nae kiongozi wa Kampuni hiyo Dk. David Elua alimueleza Dk. Shein kuwa Kampuni yake imeweza kupata mashirikiano mazuri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara husika na Taasisi zake zote na kupongeza kwa hatua hiyo ambayo imeiwezesha Kampuni ya ZANCHICK kufanya shughuli zake kwa ufanisi mkubwa hapa Zanzibar.

Dk. Elua alieleza kuwa Kampuni yake kwa hivi sasa tayari imeshatoa ajira kwa vijana zaidi ya 300 wa hapa Zanzibar wakiwemo wanaofanya kazi kiwandani pamoja na wasambazaji wa bidhaa zake.

Aidha, kiongozi huyo, alimueleza Dk. Shein azma ya Kampuni ya ZANCHICKS ambayo imeanza shughuli zake hapa nchini mnamo mwaka 2011, kuanzisha Kiwanda cha kusarifu bidhaa za kuku na kusafirisha nje ya nchi sambamba na kupanua zaidi soko la ajira kwa wananchi wa Zanzibar.

Kiongozi huyo wa Kampuni ya ZANCHIKS yenye Makao Makuu yake nchini Marekani alieleza kuwa Kampuni hiyo inafanya biashara zake katika maeneo mbali mbali duniani pia, alieleza kuwa  taratibu za utayarishaji wa kuku hao ni halali.

Sambamba na hayo, Dk. Elua alieleza mafanikio yaliopo katika shughuli za Kampuni hiyo hapa Zanzibar na kueleza azma ya Kampuni yake kupanua zaidi soko la nje ya nchi licha ya baadhi ya changamoto zilizopo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa AATO Wafanyika Zanzibar.

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ndg, Mbwana J.Mbwana akifungua Mkutano wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, akihutubia wakati wa ufunguzi huo wa mkutano wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar. 
Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika Ndg. Tchagbele Sadamba, akizungumza na kutowa maelezo ya Umoja huo wakati wa Ufunguzi wa Mkutasno wa Kwanza uliotayarishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Afisa wa Civil Avation Training Centre Bi Margareth Kyarwenda akizungumza katika  mkutano huo kuhusiana na mafunzo yanayotolewa na Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar na kushiriki Nchi wanachama wa Umoja huo barani Afrika. 
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, akifungua mkutano huo Zanzibar. 

Mwakilishi wa ICAO/ESAF Ndg.Eyob Estifanor, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofunguliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA.Tanzania, katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View. 
Afisa wa kutoka EAC, Ndg. Eric Ntangengewa akizungumza katika mkutano huo wa kwanza wa AATO, uliofanyika Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kwa makini wakati wa ufunguzi wake uliofanyika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa AATO kutoka Tanzania wakiwa makini kufuatilia michango iliokuwa ikiwakiliwashwa baada ya ufunguzi wake uliofanyika Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar. 
                     Wajumbe kutoka Nchini Ethiopia wakifuatilia mkutano huo






Katuni wa leo na Ujumbe wake

Wadau Kumradhini kwa Tatizo lililojitokeza katika Mtandao kuingiliana. bila ya idhini yetu.

$
0
0
Asalamu Aleykum.

 Kumradhini kwa kwa tatizo lililotokea kuingiliana na Mtandao na kupata simu kwa baadhi ya  Wadau wetu kuliona hilo tatizo na kutuarifu.Tunaomba radhi sana kwa wananchi waliokumbana nalo tatizo hilo wakati wakisoma habari kupitia mtandao huu.

Wadau walituarifu tatizo hilo na kupitia katika kutoliona. Tunamshukuru Mwananchi huyo kwa kuona picha haiendani na maadili yetu kuonekana katika mtandao wetu, Tunawaombeni radhi ena sana  wananchi waliokutana na tatizo hilo. 

Wako Msimamizi wa Mtandao huu.   

Malindi yalalamikia kadi za manjano

$
0
0
Na Ali Cheupe
Timu kongwe ya soka visiwani Zaznibar, Malindi ambayo inashiriki ligi kuu ya Grand Malt imelalamikia kitendo cha wachezaji wake kuonyeshwa kadi za manjano bila ya utaratibu.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu, kocha msaidizi wa Malindi Mohammed Shuberi almaarufu Babu Shube alisema kitendo cha kuonyeshwa kadi tano za manjano kwenye mchezo mmoja ni njama maalum iliyoandaliwa kwa lengo la kuidhoofisha timu yao.
 
"Yaani ni jambo la aibu mwamuzi anamuonyesha kadi mlinda mlango wetu eti kwa kutoa mpira nje ili mchezaji mwenzake atibiwe" alifoka Shuberi.
 
Babu Shube aliosema kufuatia kitendo hicho, uongozi wa timu hiyo umepanga kupeleka malalamiko kwa katibu wa Chama cha soka Zanzibar kwa lengo la kuangaliwa kwa kina kadhia hiyo.
 
Kwa mujibu wa Kanuni ya Soka visiwani hapa kifungu cha 16 d kinasema kuwa "Timu ambayo wachezaji wake wataonyeshwa kadi tano za manjano katika mchezo mmoja itatozwa faini ya Shilingi elfu hamsini (50,000/).
 
Katika msimu huu wa ligi wazee hao wa funguni tayari wameshatozwa faini ya Shilingi Laki mbili (200,000/) kufuatia kitendo cha kumuweka bench kocha mabye hana Leseni C inayotambuliwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF na lile la dunia FIFA.
 
Malindi imeshashuka kiwanjani mara tatu ikishinda mchezo mmoja na kupoteza miwili huku ikishika nafasi ya saba kwa kuwa na alama tatu.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI DAR LEO

$
0
0
   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi mbali mbali kukata utepe ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo
Sehemu ya Wageni kutoka nchi mbali mbali wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo
Sehemu ya Wageni kutoka nchi mbali mbali wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja baadhi Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania,ambao ndio waratibu wakuu wa Maonyesho hayo ya  Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014. PICHA NA IKULU

Magazetini Tz Leo Bongo


Matukio katika Picha Vivutio vya Watalii Wanaofika Pemba.

$
0
0
 PAMOJA na makumbusho haya ya msikiti wa wahindi jamii ya mabohora, uliopo kijiji cha Jambangome wilaya ya Mkoani Pemba, kusemekana kama ndio eneo la mwanzo kuhamiwa kisiwani Pemba tokea karne ya 18 hadi ya 20, bado serikali kupitia Idara yake ya makumbusho hawajaona umuhimu wa kuyahiafadhi na kusababisa kuzongwa na pori na kupoteza fedha za kigeni
 
MKUU wa kamisheni ya utalii Pemba mwalimu Suleima Amour, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo lenye makumbusho ya waanzilishi wa kisiwa cha Pemba, wahindi jamii ya mabohora kwenye karne ya 18 hadi 20, kijiji cha Jambangome wilaya ya Mkoani Pemba, ambapo kamisheni ya utalii inaendelea na kampeni yake ya utalii kwa wote 

ENEO la Tandauwa wilaya ya Chakechake Pemba, ambapo panasemekana palikuwa na kisima cha utafiti wa mafuta kwenye miaka ya 1961, kazi iliofanywa na kampuni ya BP Schell, ambapo kwa sasa limebakia bila ya kuhifadhiwa 

GATI iliko kijiji cha bahari ya Tundauwa wilaya ya Chakechake Pemba, ambayo kwenye miaka ya 1960 hadi mwaka 1962 ilikuwa ikitumiwa na kampuni ya BP Schell kwa ajili ya kushushia vifaa na magari yao wakati walipokuwa wakiendesha utafiti wa mafuta kisiwani humo, ambapo kwa sasa gati hiyo inayoweza kuingizwa kwenye makumbusho ya taifa imetelekezwa. 
 KATIKATI Mkuu wa Kamisheni ya utalii Pemba mwalimu Suleiman Amour akiwa na mzee Mohamed Bakari Juma (71) ambae alikuwa akiutembeza ujumbe wa waandishi wa habari na watendaji wa kamisheni ya utalii, ili kutoa historia halisi ya kujengwa kwa gati hiyo kwenye miaka 1960 ili kampuni ya BP Schell kupitishia vifaa wakati ikifanya utafiti wa uchimbaji mafuta kijiji cha Tundauwa Pemba.
 KATIBU wa ‘’Wawi spice farm’ Ali Mohamed Ibrahim akizungumza na waandishi wa habari, juu ya malengo ya kuanzisha kituo cha utalii wa ndani, wakati waandishi hao walioambatana na watendaji wa kamisheni ya Utalii, walipofika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya kutangaaza utalii kwa wote. 
MWENYEKITI ushirika wa ufugaji samaki ‘Sir Fish Firm’ uliopo Pujini kibaridi aliembele Ahmed Salim Issa, akiuongoza ujumbe wa waandishi wa habari na watendaji wa kamisheni ya utalii Pemba, ili kuangalia ufugaji wa samaki, ikiwa ni ziara maalumu ya kuimarisha sera ya utalii kwa wote.(Picha na Haji Nassor Pemba)

Katuni Leo na Ujumbe wake

MAJAJI WAENDESHA MAHAKAMA YA WAZI KUSIKILIZA NA KUPOKEA MALALAMIKO YA WAKULIMA WALIONYANG'ANYWA ARDHI,WAFUGAJI NA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI LEO

$
0
0
     
Jaji Mh. Richard Mziray Akitoa Hukumu katika Mahakama ya wazi  katika Kesi zote Mbili ya Kiteto na Kilosa ,ambapo katika Kesi ya Wilaya ya Kiteto alitoa Maamuzi kwamba kulikuwa na umuhimu wa utekelezeji wa Amri ya Mahakama na kuheshimu Amri za Mahakama kuwa Mahakama ilisha tamka kuwa ile ni Hifadhi hivyo inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa na ameongeza kuwa kama kungekuwa na kuzingatiwa kwa Sera za Ardhi basi kusingekuwa na Migogoro yote hiyo ametolea mfano pia maeneo ambayo yanatakiwa kulindwa ni pamoja na Bahari na Hifadhi.Katika kesi ya Kiteto alimalizia kuwa Maamuzi ya Mahakama yangeheshimiwa basi kungekuwa hakuna hii Migogoro yote.
Katika Kesi ya Kilosa Mh. Jaji Richard alisema kwamba Mgogoro uliopo ni juu ya Maji katika Mto wa Mkondoa na Muyombo ambao unagombaniwa wa wafugaji pamoja na wakulima na kwamba katika mgogolo huu Serikali inapendelea zaidi Wakulima na kuwaacha wafugaji alisema kwamba ikiwa wafugaji wangekuwa wanasababisha uharibifu wa Mazingira basi wasinge Ruhusiwa kutumia mito hiyo na hakuna sehemu inaonesha wafugaji wanaharibu Mazingira. Hivyo wafugaji wanahaki ya kutumia mto huo.
Mwisho katika kesi zote Mbili Mh. Jaji  Richard Mziray alitoa Tamko lifuatalo kuwa Wafugaji wanahaki sawa ya kutumia mito hiyo, pia wafugaji wanahaki ya kushiriki katika maamuzi ya wakulima , Wanao lazimisha mkondo wa mito hiyo uende sehemu ambayo sio yake hawana mamlaka ya kufanya hivyo Mwisho ameshauri kwamba ili migogoro hii isiweze kuendelea kuna umuhimu wa upendo kwanza Baina ya pande zote Mbili wakilima na Wafugaji, wakifanya hivyo kutakuwa hakuna migogoro kulipo kungoja Amri za Mahakama.
 Majaji wakiwa wanasikiliza Kesi kwa Makini juu ya migogoro ya Ardhi na wafugaji, Wawekezaji wanachukua maeneo ya wanavijiji, Unyang'anyi wa ardhi na Mazingira kwa ujumla  Kutoka kushoto ni Mh. Jaji msaidizi Jonas, wa katikati ni Mh. Jaji Richard Mziray, na Mh.Jaji Msaidizi Emma Lukumai
 Muwezeshaji wa Mkutano huu Jenerali Ulimwengu akiendelea kutoa Mwongozo
Mlalamikaji wa Kesi ya matukio makubwa katika hifadhi za Murtangos na Sulendo Wilayani Kiteto Bwana Lembulu Ole Kosyamlos  kushoto akitoma malalamiko juu ya hifadhi ya E-Murtangos iliyoundwa na vijiji saba ambavyo ni Kimana,Ndirkishi, Emarti,Nhati, Engusero,O-sidan na Loltepesi ambapo walianza mchakato huo mwaka 1996 na kurasimishwa rasmi Mwaka 2002 na hifadhi hiyo inaukubwa wa Hekta za Mraba 133,33.15, alieleza changamoto za wafugaji na wakulima ambapo watu wengi walipoteza maisha,Wavamizi kuingia bila utaratibu na kuharibu mazingira, na wimbi la uvamizi kuendelea siku hadi siku mpaka kufikia mwaka 2013. Pia katika Mashitaka hayo ameiomba mahakama ya wazi iwasaidie kutatua tatizo lao na Serikali iangalie upya eneo hilo Kisheria na zisiingizwe Sheria katika Jambo Hilo.
Mh. Diwani lairumbe Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akitoa Malalamiko yao Mbele ya Mahakama ya wazi juu ya Hifadhi ya Msitu wa Vijiji Lusendo ambapo alieleza kuwa hifadhi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1994/1995 ambapo vijiji 9 viliungana na kutengeneza hifadhi hiyo aliongeza baada ya kuanzisha hifadhi hiyo walipata mafanikio ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha kupitia uvunaji wa miti , mkaa endelevu na asali , pia walifanikiwa kupata Gari moja aina ya Land Cruzer Pick up na pikipiki . Alimalizia kwa kuleta malalamiko yake katika Mahakama ya wazi kuwa kuna uvamizi uliokithiri kwa maeneo ya Misitu Hususani Maeneo yote yanayozunguka mipaka ya Wilaya za Kilindi na Kiteto na Kuiomba Serikari wapate kurejeshewa maeneo yao.
Bwana Henry Parmeo akitoa mashitaka yake Mbele ya Mahakama ya wazi  juu ya mgogolo uliopo Kilosa kati ya wafugaji na wakulima hasa katika eneo la maji, na muwekezaji ambaye yeye amebadilisha Mkondo wa Maji kutoka katika eneo lake husika na kwenda katika Mashamba, Katika kesi hiyo amedai kwamba wakulima wamekuwa wakiwalaumu wafugaji hao kuwa ndio wenye makosa kwa kuwa wanaingilia wakulima kuwa Mifugo yao inakula mazao na kusahau kwamba Wakulima hao wamebadilisha mkondo huo kwenda mashambani, na aliongeza kuwa mgogoro huu huwa unajitokeza hasa wakati wa kiangazi miezi ya Nane,Tisa, Kumi, Kumi na moja na Kumi na Mbili katika mto Mkondoa na Myumbo. ameiomba Mahakama ya wazi pamoja na Serikali kumaliza Mgogoro huu.
Mama Shujaa wa  Chakula kutoka Mkoa wa Morogoro akielezea kwa kina zaidi juu ya Mgogoro wa wakulima na wafugaji hasa katika mito miwili ambapo wote wanagombania kupata maji hasa wakati wa kiangazi na amewapongeza Oxfam kwa Juhudi zao za kusaidia kutatua matatizo ya Mgogoro huo
Bi Vera F. Mugittu Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina zaidi Juu ya Kesi Mbili zilizotajwa Kesi ya Kilosa na Kiteto na kusema kuwa Migogoro yote ni Juu ya Lasilimali na kwamba Serikali pamoja na Mahakama wanatakiwa kujua Matatizo haya na kujua Jinsi gani wanaweza kuyatatua na kuwajengea uwezo watu wapate kujitambua ili kuepukana na migogoro hiyo, Alimalizia kwa kusema kuwa ucheleweshaji wa kusikiliza kesi ndio unao ongezea Migogoro.
Bwana Muro Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina juu ya kesi mbili za Kilosa na Kiteto
Baadhi ya Wachangiaji wakichangia Michango na mawazo mbalimbali wakati wa Mahakama ya Wazi iliyo andaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Mh. Emma akitoa ufafanuzi juu ya Vifungu mbalimbali vya Sheria wakati wa Hukumu hizo katika mahakama ya wazi leo
Mh.  Jonas akitoa ufafanuzi zaidi wa maamuzi katika kesi hiyo ya Mahakama ya wazi
 Michoro ambayo inaonesha matukio mbalimbali ya Mkutano huo
 Burudani ikiendelea wakati wa mapumziko mafupi
Baadhi ya watu wakiwa wanasikiliza kesi kwa makini katika Mahakama hiyo ya wazi ambayo iliandaliwa na Oxfam na Forum CC

Waandishi wa Habari Ziarani Nchini India.

$
0
0
Waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali wakitembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Mbele kulia ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR). (Picha zote kwa hisani ya Hassan Hamad, India).

Muongozaji watalii, akitoa maelezo kwa waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali waliotembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Katikati ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR).
Muongozaji watalii, akitoa maelezo kwa waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali waliotembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Wa pili kulia ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR).

Waandishi na maafisa habari kutoka baadhi ya nchi za Afrika, Asia na Latin America wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la kihistoria la Taj Mahal nchini India, wakati wakiwa katika ziara ya kimasomo. Taj Mahal ilijengwa na mtawala Shah Jahan wa India katika karne ya 17 kama kumbukumbu ya mke wake mpendwa aliyefariki kabla yake aliyejulikana kwa jina la Mumtaz Mahal. Likiwa na wafanyakazi wa ujenzi 22,000 ilichukua miaka 22 hadi kukamilika kwake.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal ahudhuria Kongamano la Biashara la Kimataifa kwa Nchi za Afrika Jijini Dubai.Farme za Kiarabu.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji Katibu  na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania < dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na baadhi ya viongozi, Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai


 Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia) akijadiliana jambo na Prof. Ahmada Ktahib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati walipohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis nchini Dubai. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Viongozi na wawekezaji baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo. Picha na OMR
Viewing all 35828 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>