Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35810 articles
Browse latest View live

Wapiga Picha Zanzibar Washahijishwa Kuunda Jumuiya Yao.

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Kamesheni ya Michezo Zanzibar Ndg, Mustafa Omar, akizungumza katika mkutano huo na Wapiga picha kuwataka kuunda Jumuiya yao kuweza kushiriki katika matamasha mbalimbali ya maonesho ya Picha Duniani Zanzibar inayo nafasi hiyo katika maonesho ya picha. 
Katibu wa Bodi ya Filamu na Sanaa Zanzibar Ndg. Suleiman Mbarouk akizungumza na Wapiga picha za Matukio mbalimbali Zanzibar kuwahamasisha kuazisha Jumuiya yao kuwakutanisha pamoja ili kuweza kufaidika na kazi zao kupitia kuzitangaza katika maonesho ya Kimataifa baada ya kujisajili na kutambulikana kuweza kushiriki katika maonesho hayo yanayofanyika Nchini China kila mwaka na kushirikisha Nchi wanachama wa jumuiya ya Sanaa. 
Wapiga Picha Zanzibar wakiwa makini kumsikiliza Taibu wa Bodi ya Filamu na Sanaa Zanzibar Ndg Sulreiman Mbarouk akizunhgumza nao katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rahaleo.
Wapiga picha za Matukio na sherehe Zanzibar wakimsikiliza Katibu wa Bodi ya Filamu na Sanaa Zanzibar Suleiman Mbarouk, akiwahasisha kuazisha Jumuiya yao ili kuweza kufaidia bna Sanaa nao ya Picha katika jumuiya za Kimataifa kushiriki katika maonesho ya picha zao yanayofanyika Nchini China kupitia Jumuiya ya Wapiga picha Nchini China.

Dkt. Bilal Aiwakilisha Tanzania katika Kongamano la Kimataifa.

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA PILI LA KIMATAIFA LA BIASHARA KWA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DUBAI
OKTOBA 03, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Oktoba Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika kongamano la pili la Kimataifa la Biashara kwa nchi za Afrika lililofanyika katika jiji la Dubai, Falme za Kiarabu.

Kongamano hili limehudhuriwa na washiriki wapatao 800 kutoka nchi mbalimbali duniani na limelenga katika kukuza uwekezaji katika nchi za Falme za Kiarabu na kufungua fursa za kibiashara barani Afrika. Kongamano la kwanza la namna hii lilifanyika pia jijini hapa  mwaka jana na kushirikisha  washiriki wapatao 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Baadhi ya Viongozi wa Afrika waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais John Dramani Mahama wa Ghana na Rais Mulatu Teshone Watu wa Ethiopia.

 Viongozi hawa kwa nyakati tofauti walizungumzia umuhimu wa utengamano barani Afrika na wakaeleza kuwa hiyo ndiyo fimbo pekee ya kukuza uwekezaji wenye tija Afrika.

Pia walizungumzia mabadiliko makubwa ya Afrika huku wakiwakumbusha wawekezaji na wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo kuwa Afrika ya sasa siyo bara la giza na kwamba ni bara linalokuwa kimaendeleo kwa kasi huku likiwa na fursa ya kukuza maendeleo yake kwa haraka. Kongamano hili pia lilihudhuriwa na Mfalme Sheikh Mohammed Bin Rashid Al-Makhtoum ambaye alialikwa na wenyeji wa kongamano hili yaani Kituo cha Biashara cha Dubai. Sambamba na hao pia kulikuwa na wafanyabiashara wakubwa akiwemo Aliko Dangote, ambaye sambamba na kuwa na uwekezaji mkubwa katika Afrika pia anawekeza mkoani Mtwara katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti kuliko vyote Afrika Mashariki.

Mfanyabiashara huyo mara baada ya mijadala ya ufunguzi wa kongamano hilo, pia alipata nafasi ya kukutana na mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kubadilishana naye mawazo kuhusu uwekezaji wake Tanzania ambapo aligusia nia ya kutumia mkaa wa mawe uliopo Mbinga katika uzalishaji wa nishati kiwandani kwake pamoja na kutanua sekta ya usafirishaji ili kumudu kusafirisha saruji kwa matumizi ya nje ya nchi.

Mfanyabiashara huyo alifafanua kuwa, katika sekta ya usafirishaji pekee anatarajia kuchangia ajira zipatazo 3000 na pia anakusudia kuwapa mafunzo wafanyakazi wa kiwanda chake nchini Nigeria ili waendane na teknolojia ya sasa katika uzalishaji.

Uwekezaji wa Aliko Dangote katika Tanzania unatokana na nchi yetu kuwa na sera nzuri za uwekezaji na anafafanua kuwa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake yanakwenda kama alivyopanga na ujenzi utakapokamilika na uzalishaji kuanza, ni wazi eneo la Kusini mwa Tanzania litaanza kubadilika kiuchumi kufuatia uwekezaji huo mkubwa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akichangia katika mjadala ambao pia ulimshirikisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Richard Sezibera, alisema nchi za Afrika na hususani Tanzania zimepiga hatua katika kuweka mazingira ya uwekezaji licha ya kuwa changamoto ya uduni wa miundombinu na urasimu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, Tanzania imeunganika katika mtandao wa barabara hivyo kwa wawekezaji ni rahisi kwao kuwekeza huku pia nchi yetu inategemea kuwa na ziada ya umeme katika miaka michache ijayo hali itakayohakikishia uhakika katika uzalishaji hasa wa viwanda vikubwa vinavyohitaji nishati kubwa ya umeme ili kuzalisha.

Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa nchi za Afrika kuungana ili kurahisisha matumizi ya miundombinu sambamba na kutanua masoko katika nchi za Afrika na akaeleza kuwa Tanzania iko mstari wa mbele kuhakikisha inachangia uwezo wake katika kuhamasisha nchi kuungana kwa lengo la kukuza mahusiano, kuimarisha amani na kutanua fursa za uwekezaji.

 “Sisi Tanzania tupo katika uhusiano na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na zile za Kusini mwa Afrika. Ushiriki wetu katika jumuiya hizi unasaidia pia hasa sasa ambapo tunazungumzia kuweka mashirikiano na nchi za Magharibi ya Afrika na hivyo kuwa na mfumo mmoja wa biashara barani Afrika,” Mheshimiwa Makamu wa Rais anasisitiza.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Makamu wa Rais alikutana na Makamu wa Rais wa Sychelles Mheshimiwa Danny Faure ambaye alimuelezea Mheshimiwa Dkt Bilal kuwa, Sychelles inakusudia kuanza safari ya ndege zake kuleta watalii Tanzania sambamba na kununua mazao ya kilimo na ufugaji na hivyo kuwa fursa mpya kwa wakulima wa mbogamboga, vitunguu na wafugaji wa ng’ombe.

Mheshimiwa Faure alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, uhusiano baina ya Tanzania ni Sychelles ni mkubwa na hivyo ili kuuwekea msingi imara upo umuhimu wa kushirikiana katika biashara hasa kwa bidhaa ambazo hazipatikani Sychellles. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alipokea taarifa hiyo na kumueleza Makamu wa Rais Faure kuwa, Tanzania itatoa taarifa kwa wafanyabiashara wake ili waweze kuchangamkia fursa hiyo kupitia Bodi ya Biashara za Nje (Tantrade).

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Oktoba 3, 2014 Dubai, UAE

Ujenzi wa Utanuzi wa barabara ya kupitia ndege Ukiendelea kwa Kasi.

$
0
0
UJENZI  wa utanuzi wa  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ukiendelea na ujenzi wake katika barabara  za kupitia ndege, kama inavyoonekena pichani mafundi wakiwa katika harakati za ujenzi huo eneo la VIP, kuegeshea ndege 

Dk. Shein ateua Wenyeviti wa Bodi

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Ali Mohammed Shein, amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi katika taasisi mbali mbali za serikali.

Uteuzi huo ulitangazwa mjini Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ambapo alieleza kuwa ulianza rasmi Septemba 30 mwaka huu.

Walioteuliwa ni Dk. Issa Haji Ziddy, anaekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni Wakfu na Mali ya Amana, ambapo uteuzi huo umefanywa chini ya sheria namba 2 ya mwaka 2007 kifungu cha 5 (2) iliyounda taasisi hiyo.

Kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Mwenyekiti anakuwa Kombo Hassan Juma, ambapo uteuzi wake umefanywa chini ya sheria namba 3 ya mwaka 2011 kifungu cha 4 (1)(a).

Dk.Mohammed Mwinyi Mzale, ameteuliwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi (ZIPA) chini ya sheria namba 11 ya mwaka 2004, kifungu cha 6(2) (a).


Kwa upande wa Shirika la Meli na Uwakala chini ya sheria namba 3 ya mwaka 2013 kifungu cha 10 (2)(a),Dk Shein, amemteua Kepteni, Abdulla Yussuf Jumbe, kuwa Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo.

Kwa upande wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Dk. Shein amemteua, Ahmeid Sheikh Abdulrahman kuwa Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo.

Bodi ya Ushauri ya Mambo ya Nyaraka na Kumbukumbu, alieteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ni Amour Abdalla Khamis.


Aidha alimteua Mwalimu Haji Ameir, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara na Salmin Senga Salmin kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari.

Wamarekani waahidi kuwekeza Z’bar

$
0
0
Na Khamis Amani
MAMLAKA ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) imewaomba wafanyabiashara wa kigeni kuvitumia vizuri vivutio vya Zanzibar kwa kuwekeza miradi yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA,Ndg. Salum Nassor, alisema Zanzibar ni visiwa vilivyojaaliwa kuwa na vivutio vingi na vizuri kwa uwekezaji, ambavyo vinaweza kukuza biashara.

Aliyasema hayo katika hoteli ya Double Tree Shangani mjini Unguja, wakati wa mkutano na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchini Marekani wa VIP Safari.

Alisema vivutio vya Zanzibar vina mandhari nzuri kwa wawekezaji ambavyo vinasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza biashara ikiwemo utalii.


Alisema ujio wa wafanyabiashara hao utasaidia kuitangaza Zanzibar kiuchumi na kiutalii pamoja na kukuza urafiki wa muda mrefu baina ya Tanzania na Marekani.

Hivyo aliwaomba wafanyabiashara hao kukubali kuwekeza miradi yao ambayo itasaidia kuondoa umasikini kwa kuwapatia ajira vijana, kuitangaza nchi pamoja na kuinua pato la taifa.

Balozi wa Tanzania mjini Washington DC, Balozi. Suleiman Saleh, alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama na fukwe za bahari, ambazo vikitangazwa vinaweza kuwashawishi wawekezaji kuwekeza miradi yao.

Alisema, ubalozi wake umefanya jitihada kubwa za kuitangaza Tanzania ikiwemo Zanzibar kuvutia wawekezaji jambo ambalo linahitaji kuungwa mkono na serikali na wadau wote wa utalii.

Alisema katika kufanikisha hilo aliweza kuwafikisha wafanyabiashara wakubwa kukagua vivutio hivyo ambavyo vimeleta mafanikio katika suala zima la uwekezaji.

Alisema ujio wa wafanyabiashara hao unaweza kuleta tija katika sekta ya uwekezaji jambo ambalo linahitaji jitihada za Serikali katika kuimarisha ulinzi kwa wawekezaji, watalii na mali zao pamoja na kuweka miundombinu imara.

Nao wafanyabiashara hao walisema, wameridhishwa na vivutio vizuri vilivyopo Zanzibar na kuahidi kuwekeza miradi yao pamoja na kuitangaza nchi kiutalii.


Hiyo ni ziara ya tatu kwa wafanyabiashara wakubwa wa Marekani kufika nchini kwa ajili ya kukagua vivutio kwa ajili ya uwekezaji.

Finland yamwaga fedha kwa wabunifu

$
0
0
Na Mwanajuma Abdi, Dar es Salaam
SERIKALI ya Finland imekabidhi hundi ya shilingi milioni 150, kwa washindi 10 wa tunzo ya ubunifu wa mfumo wa habari na mawasiliano yanayorahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

Hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam, ambapo  Balozi wa Finland nchini Tanzania, Sinikka  Antila,  alikabidhi hundi hizo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Patrick Makungu, aliyemuakilisha  Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa.

Alisema fedha walizokabidhiwa vijana 10 kutoka kampuni mbali mbali za ubunifu waliotengeza ‘software’ kupitia mawasiliano ya kompyuta na smart phone, ambazo zinarahisisha upatikanaji wa bidhaa mbali mbali kupitia TEHAMA.

Alisema serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania, wameanzisha mfuko wa kuwasaidia wabunifu ikiwa ni mradi wa kukuza maendeleo nchini hususani kwa vijana wajasiriamali.


Alisema malengo hayo yanakwenda sambamba na dira ya maendeleo ya Tanzania ya ukuaji wa kati wa uchumi ifikapo mwaka 2025, katika kuimarisha  uzalishaji wa bidhaa katika sekta mbali mbali, hivyo kuwepo kwa wabunifu hao kutatoa fursa kwa wenzao kuajiri na kukabiliana na masoko katika ulimwengu wa utandawazi.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Patrick Makungu kwa niaba ya waziri wake, alisema ubunifu unasaidia kuzalisha ajira kwa vijana, ambapo fedha walizokabidhiwa zitasaidia kuzalisha ajira za heshima kwa wenzao.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Hassan Mshinda, alisema ubunifu huo utaisaidia jamii kununua bidhaa za biashara nje na ndani ya nchi kupitia sekta ya habari na mwasiliano (TEHAMA).


Nao washindi hao, walisema walijishindia fedha hizo baada ya kutengeneza software katika kompyuta na kuingiza taarifa za bidhaa kupitia teknolojia hiyo ambapo mtu aliyeko eneo lolote anaweza kujua habari ya bidhaa hiyo. 

Wananchi Kisiwani Pemba wakiwa katika harakati za Maandalizi ya Sikukuu.

$
0
0
 Wananchi katika Mji wa Chake chake wakiwa katika harakati za maandalizi ya kutafuta mahitaji kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid Alhajj inayotarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa wiki hii kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislam Duniani baada ya kufanyika Ibadaa ya Hijja inayofanyika Nchi Saudi Arabian Makka. 
Mfugaji wa Mbuzi akiwa na mifugo yake akipeleka marikiti Chakechake katika marikiti hiyo mbuzi mkubwa aliouzwa kwa shilingi laki moja na zaidi, Eid Haljj Waumini wa dini ya Kiislam huadhimisha sikukuu hii kwa kuchinja kwa mtu m,wenye uwezo.
Hali ya Harakati katika Mji wa Chakechake Pemba wakiwa katika kukamilisha maandalizi ya Sikukuu ya Eid Alhaj.
                     Mambo ya maandalizi hayoo katika Mji wa Chakechake pemba.

Wananchi wakiwa katika mtaa wa miembeni Chakechake wakipata huduma ya bidhaa za nguo kwa ajili ya watoto wao kuweza kusherehekea kwa vizuri.

Changamoto za usafiri wa anga kufanyiwa kazi

$
0
0
Na Kauthar Abdalla
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha inazifanyia kazi changamoto zinazoikabili sekta ya usafiri wa anga ili kuimarisha usalama wa sekta hiyo.

Waziri wa Usafirishaji, Dk. Harison Mwakyembe, aliyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana Juma Mbwana, katika mkutano  wa kwanza wa jumuiya ya vyuo vya usafiri wa anga uliofanyika hoteli ya Ocean View Kilimani Zanzibar.

Alisema pamoja na kuimarika kwa sekta hiyo katika miaka ya hivi karibuni bado kuna mambo kadhaa yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuchochea kazi ya maendeleo ya nchi.

Alisema usafiri wa anga ni moja ya sekta zinazopelekea ukuaji wa uchumi kwa haraka hivyo ukuaji wake na uimara wa miundombinu ya sekta hiyo ni lazima iendane na mahitaji ya kazi ya ukuaji wake.


“Kwa kuzingatia umuhimu wa usafiri wa anga katika uchumi wa Afrika,Mawaziri wanaohusika na sekta hiyo waliazimia kuanzisha mikakati ya kitaifa,kikanda na bara zima ili kuhakikisha  usalama wake kwa lengo la kuchangia sekta nyengine za uchumi hivyo umoja huo ni lazima uzingatie utekelezaji wa majukumu yake,” alisema.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.James Diu, alisema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na wataalamu wa kutosha katika fani hiyo jambo ambalo linakwamisha harakati za kimaendeleo katika jumuiya na kushindwa kuendelea mbele.


Malengo mkakati ya mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania ni pamoja na kuwa na sauti ya pamoja ya vyuo wanachama na kuhimiza vyuo hivyo kuendeshwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

Afariki baada ya kugongwa na gari

$
0
0
Na Madina Issa
MTU mmoja amefariki dunia baada ya kufikishwa hospitali kuu ya Mnazimmoja, akipatiwa matibatu baada ya kugongwa na gari.
Marehemu alitambulikana kwa jina la Ali Faki Khamis (22) mkaazi wa Kinuni wilaya ya magharibi Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa mjini magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo lilitokea  Septemba 21 mwaka huu saa 2:00 za usiku Amani.

Alisema kabla ya kifo,marehemu alikuwa akiendesha baskeli maeneo ya Kibandamaiti kuelekea Amani na ndipo alipopatwa na ajali ya kugongwa na gari yenye namba za usajili Z752 AG iliyokuwa ikiendeshwa na Mbarouk Juma Khamis (53) mkaazi wa Amani.


Alisema marehemu alifikishwa hospitalI kuu ya Mnazi Mmoja kwa kupatiwa matibabu na alipofanyiwa uchunguzi aligundulikana kuwa alipata maumivu makali kichwani na kufariki dunia Septemba 22.

Hata hivyo, alisema katika operesheni ya usalama barabarani katika mkoa wake kwenye wiki iliyopita makosa 207 yalikamatwa ambayo yanavihusisha vyombo mbalimbali vya moto.


Washitakiwa baadhi yao tayari wameshapelekwa  mahakamani na kesi zao zimeshatolewa hukumu kwa mujibu wa sheria.

Wananchi 24,000 wa vijijini kunufaika na umeme

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, Arusha
WANANCHI zaidi ya 24,000 waishio vijijini wanatarajia kunufaika na mradi wa umeme wa j na upepo katika kipindi cha miezi 18 ijayo.

Hayo yalisemwa na Kamishana wa Nishati na Petroli, Hosea Mbise, wakati akikagua maonesho ya makampuni  57 mkutano wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) jijini Arusha.

Alisema kikubwa katika mkutano huo wanatarajia kuteuwa makampuni 20 kati ya hayo yalioshiriki maonesho hayo, baada ya kushinda, ili wapewe kazi ya kusambaza umeme vijijini ambako gridi ya taifa haipo.

“Umeme huo tunaamini utakuwa wa bei nafuu kwa wananchi wengi wa vijijini na utawaondoa katika lindi la umaskini,”alisema.
Aidha alisema makampuni hayo  ambayo yatateuliwa kwenye mkutano huo, yataanza kazi mara baada ya kuteuliwa na ndani ya miezi 18 wananchi watajionea umeme umesambaa kwa kasi maeneo yao.


Alisema gharama za mradi huo ni shilingi bilioni 4.6, ambazo tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia makampuni 20 yatakayoshinda kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

“Fedha hizi zitagawanywa kulingana na ukubwa wa kazi ya kampuni husika na kila kampuni itafanya kazi katika kijiji chake ili mradi wasambae maeneo tofauti nchi nzima,” alisema.

Naye mmoja wa washiriki wa maonesho hayo, Mkuu wa Idara ya Ufundi kwenye kampuni ya T&A Business Center Ltd, Mgogiley Fivawo, alisema endapo kampuni yake itashinda atasambaza umeme kwenye sekondari moja ya Rufiji na Vituo vya Afya viwili huko Rufiji.


Alisema eneo la Rufiji lina rasilimali nyingi za uchumi kama zao la biashara la korosho, samaki na minazi, lakini wananchi wengi hawana nishati ya umeme.

Mabaraza ya watoto, wazee kusaidia kuimarisha maendeleo yao

$
0
0
Na Asya Hassan
OFISA Tawala wilaya ya magharibi, Sabah Saleh, amesema kuanzishwa mabaraza ya watoto na wazee kutasaidia kuimarisha maendeleo yao.

Alisema hayo katika uzinduzi wa mabaraza hayo kwenye shehia ya Kiembesamaki katika hafla iliyofanyika  viwanja vya sheha wa shehia hiyo.

Alisema kuwepo kwa mabaraza hayo ni chachu ya kuwawezesha kujua haki zao pamoja na kuwajengea uwezo watoto hao kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji yanayowakumba.

Alisema kumekuwa na matukio mengi mabaya yanayofanywa kwa watoto na yanashindwa kufikia mwisho na kupata haki zao za msingi.

Alisema kutokana na kukua sayansi na teknolojia kunasababisha vijana kukumbwa na matukio mengi hali inayosababisha kukosa haki zao.


Hata hivyo, Ofisa huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wazee washirikiane na vijana wao katika kufanikisha maendeleo ya mabaraza hayo na wasione kama watoto wao wanapewa mzigo.


Nae sheha wa shehia hiyo, Mwinyi Khatib Juma, alisema watoto wamekuwa wakishawishiwa mara kwa mara juu ya kujishirikisha katika makundi maovu hali inayopelekea kuacha maadili yao.

RAIS KIKWETE AHUTUBIA KIKAO CHA KAZI KWA VIONGOZI WA MIKOA< WILAYA NA HALMASHAUR​I MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubuia Kikao cha Kazi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma(Picha na Ikulu)


Zantel yafungua Duka lake Mtaa wa Samora Dar. (SAMORA SHOP OPENING)

$
0
0
Dar-es- Salaam, Oct 02nd, 2014: In the effort to bring customer care services closer to its customers in the country, ZANTEL has opened its 19th customer care shop along Samora Avenue, Dar es Salaam.
The services to be offered in the new shop include SIM cards, SIM registration, Internet activation, device sales and configuration, EzyPesa and after sales support.
Speaking during the inauguration of the shop, the Chairman, ZANTEL Board, Mr. Essa Al Haddad, said that, the launch was the beginning of a new journey to open a lot more in the country. ZANTEL has several shop centers in various parts of the City and that the company will continue opening as many shops as possible so as to reduce congestion in the already existing shops.
cid:image001.jpg@01CFDF19.7E1474C0

The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad
“We want to follow customers where they are,” he said.
Some of the company’s shops in Dar es Salaam are situated at, among others, Dar Airport, Kariakoo, Buguruni, Shoppers Plaza, and ZANTEL Headquarters.
Over the few years, Zantel has been able to transform mobile communication in Tanzania by introducing various innovative platforms which have tremendously improved lives of Tanzanians and therefore looking for ways of bringing services closer to the people so as to evade crowding and loss of time.

Zantel’s Corporate Solutions Director, Mr. Ahmed Seif Mohamed promised customers of more innovations and quality services.
cid:image008.jpg@01CFDF1E.03CEA140

The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (left) exchanging views with the company’s Executive Director, Mr. Pratap Ghose (center) and the Director of Sales at Zantel, Mr. Sukhwinder Bajwa (in suit) during the inauguration of a new Zantel shop along Samora Avenue in Dar es Salaam yesterday.

cid:image002.jpg@01CFDF19.7E1474C0

ZANTEL team poses for a group photo after the launch



cid:image003.jpg@01CFDF19.7E1474C0

The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (center) going around the shop with Manager, Customer Care, Ms. Yasmeen Ismael (right) and the Supervisor, Samora Shop, Mr. Yassini Makwaruzo (left) during the inauguration of a new Zantel shop along Samora Avenue in Dar es Salaam yesterday.

cid:image011.jpg@01CFDF1E.03CEA140

Customers as were captured at the shop yesterday being serviced

cid:image014.jpg@01CFDF1E.03CEA140

The Chairperson, Zantel Board, Mr. Essa Al Haddad (center) giving a hand of applause to the Flash Mob (not in picture) during their performance. Looking on is Etisalat Group, Chief Procurement Officer, Mr. Obaid Bokisha (right) and Director, Customer Experience, Mr. Gabriel Kamukara (left)

cid:image004.jpg@01CFDF19.7E1474C0


cid:image005.jpg@01CFDF19.E687A720

The two photos above are Flash Mob Dancers as shot at the inauguration ceremony of the ZANTEL Samora Shop

OMANI NA UJERUMANI KUSAIDIA SEKTA YA HABARI ZANZIBAR

$
0
0


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na wana Habari kuhusu ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman ikiwa ni hatua ya kukuza mashirikiano ya Wizara yake na Nchi hizo. 
 Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Joseph Kilange akimkaribisha Waziri wa wizara hiyo azungumze na wandishi wa Habari kuhusu ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman.

Na Rahma Khamis –ZJMMC.
Serikali ya Omani imeahidi kuisaidia Sekta ya Habari Zanzibar kwa kuliwezesha Gazeti la Zanzibar Leo kupata Mtambo wa kuchapishia Magazeti yake ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha nchi hiyo pia Imeahidi kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kwa kuliunganisha katika Mfumo wa Satalite ili liweze kusikiaka na kuonekana Duniani kote.
Waziri wa habari utalii,utamaduni , na michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuhusiana na mafanikio ya safari yake nchini Omani na Ujerumani.
Amesema kwa muda mrefu Gazeti la Zanzibar Leo linakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuchapishwa kwa gharama kubwa nje ya Zanzibar na hivyo kama Omani italeta Mtambo huo wa uchapishaji itasaidia sana maendeleo ya Gazeti hilo.
Kwa upande wa ZBC Waziri Mbarour amesema Omani italeta Gari mbili za kurushia mtangazo ya moja kwa moja na kufanya maboresho ya Studio za ZBC ili kuwa za kisasa zaidi.
Akizungumzia kuhusu Utalii, Waziri Mbarouk amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii ya Omani watafanya matangazo ya pamoja ya kutangaza na kuimarisha Sekta ya Utalii katika nchi zao.

Ameongeza kuwa Omani itaruhusu ndege zake za Oman AIR kusafirisha watalii Wanaokuja Zanzibar kutoka nchi tofauti ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza Idadi ya Watalii nchini.
Kwa upande wa Ujerumani Waziri Mbarouk amesema nchi hiyo itaisaidia Zanzibar kupitia Chuo cha Habari cha Zanzibar kwa kuwapatia Vifaa vya kufundishia na kuboresha Mtaala wa Uandishi.
Aidha amefahamisha kuwa nchi hiyo pia itatuma Walimu kutoka Ujerumani ili kuja kufundisha masomo mbalimbali ikiwemo Lugha ya Kijerumani.

Katika Ziara hiyo ya kikazi ya Siku nane nchini Oman na Ujerumani Waziri wa Habari aliambatana na Viongozi waandamizi wa Wiazara yake ambapo waliweza kujadili na kuahidiwa misaada mbalimbali kutoka nchi hizo.

Ufungajim wa Mkutano wa Umoja wa AATO Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocein View Kilimani.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Tahir M.K. Abdullah akitoa hutuba ya ufungaji wa Mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika.Mkutano huo ulifanyika huko Ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika Ndg. Tchagbele Sadamba, akitoa Shukrani kwa Washiriki wa Umoja huo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufunga Mkutano huo wa Kwanza uliotayarishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) wakimsikiliza Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Tahir M.K. Abdullah(hayupo pichani) katika hafla ya Kuufunga Mkutano huo,huko Ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mgeni rasmini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe.Tahir M.K. Abdullah akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa watendaji wakuu wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika mara baada ya kufungwa kwa Mkutano huo uliofanyika huko Ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania ambae ni Katibu Mteule wa (AATO) Bi. Margareth Kyanwenda akizungumza na wandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika uliofanyika Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

Ligi Kuu Mtende na Shaba Gombani Pemba Timu Hizo zimetoka sare ya 1--1

$
0
0


Kikosi cha timu ya Shaba yas Kojani Pemba Maarufu (Wazee wa Dago) kilichoilazimisha timu ya Mtende Rangers kutona nao sare ya mabao 1--1katika mchezo uliofanyika uwanja wa gombani Pemba 
Kikosi cha timu ya Mtende Rangers kilichoendesha mchakamchaka na timu ya Wazee wa Dago Shaba katika uwanja wa gombani Pemba kulazimishwa sare ya 1--1
Beki wa timu ya Shaba Hassan Suleiman, akikimbilia mpira huku mchezaji wa timu ya Mtende Rangers, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt mchezo uliofanyika uwanja wa gombani Pemba, timu hizo zimetoka sare ya 1--1.
Beki wa timu ya Shaba akiondoa mpira galini kwa huku mshambuliaji wa Mtende Rangers Ali Rajab akimkimbilia wakati wa mchezo wao uliofanyika uwanja wa gombani Pemba timu hizo zimetoka sare ya 1--1
Golikipa wa timu ya Shaba Bakari Hassan akiwa hewa akidaka mpira huku mshambuliaji wa timu ya Mtende Rangers akiwa hewani. 


Mchezaji wa timu ya Shaba akiondoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt iliofanyika uwanja wa gombani Pemba leo jioni timu hizo zimetoka sare ya b ao 1--1.
Beki wa timu ya Shaba Hemed Bakari, akikokota mpira huku mchezaji wa timu ya Mtende RangersJumanne Seif, akijiandaa kumzuiya katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Grand Malt uliofanyika uwanja wa gombani leo jioni timu hizo zimetoka sare ya 1--1.   
Wachezaji wa timu ya Mtende na Shaba wakiwania mpira katika mchezo wao wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa gombani Pemba.


Mashabiki wa timu ya Wazee wa Dago Timu ya Shaba kutoka kujani wakishangilia timu yao wakati wa mchezo huo uliofanyika uwanja gombani Pemba leo jioni.







Kocha wa timu ya Mtende Rangers Madundo kushoto na Kocha wa timu ya Shaba o Mbarouk Chande, wakipongezana baada ya mchezo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1--1. 
Kocha Mkuu wa timu ya Shaba Mbarouk Chande, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalikiza kwa mchezo huo, na kusema timu yake imecheza mchezo mzuri lakini bahati haikuwa kwao kwa kukosa mabao mengi katika mchezo huo na kuahidi kurekebisha ubutu huo wa wachezaji wake kukosa mabao. 
Kocha Mkuu wa Timu ya Mtende Rangers Madundo akizungumza na waandishi wa habari za michezo baada ya mchezo wa timu yake dhidi ya wapizani wao timu ya Shaba kutoka sare ya bao 1--1, mchezo uliokuwa mzuri lakini umaliziaji wa wachezaji wangu walifanya makosa kutotumia nafasi walizozipata na kuwa  na upinzani mkubwa dhidi ya wachezaji wa Shaba.    

Jamii yahimizwa kushirikiana kwenye malezi

$
0
0
Na Kauthar Abdalla
IPO haja ya  kurejeshwa malezi ya pamoja katika jamii pamoja na kuimarisha ndoa ili kutunza familia na watoto kuepukane vitendo vya udhalilishaji.

Mjumbe kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Zanzibar, Sharifa Maulid, alisema hayo katika kongamano la wazee juu ya hifadhi ya mtoto na mapambano ya udhalilishaji katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani mjini Unguja wakati  akiwasilisha mada ya udhalilishaji.

Alisema mfumo wa malezi kwa watoto umebadilika tofauti na ilivyokuwa zamani na kwamba ongezeko la talaka kwa wanandoa linachangia kwa kiasi kikubwa kudhalilishwa watoto kwani wanakosa matunzo yanayostahiki.

Aidha alisema vitendo vya udhalilishaji kwa watoto vinawaathiri kiakili, kimwili na kisaikolojia hali ambayo inampelekea mtoto kukosa haki zake za msingi.


Kaimu Mkurugenzi kijiji cha kulelea watoto yatima (SOS) Salum Abrahman Salum, alisema ni wakati sasa kwa taifa kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji.

Alisema kutokana na hali hiyo taifa halitakuwa na mtetezi na siku zote litakuwa tegemezi hali ambayo itapelekea kukosekana maendeleo endelevu nchini.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya taasisi na familia kuchukua madaraka waliyonayo kutatua kesi hizo kwa njia ya kienyeji.


Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo, walisema ni bora wakarudishwa walimu wenye hisia za kidini katika skuli za serikali na binafsi na katika vyuo vya madrasa ili wawafahamishe watoto juu ya mwenendo mzima wa maisha unavyokwenda.

Wanyama 21,000 wapatiwa chanjo kujikinga na kichaa cha Mbwa

$
0
0
Na Salama Salim, ZJMMC
ZAIDI ya wanyama 21,000 wamepatiwa chanjo ya kuwakinga na maradhi ya kichaa cha mbwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maabara na Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Wanyama Zanzibar, katika Ofisi za Idara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo, Dk. Warid Abdalla Musa, alisema kampeni ya kuchanja wanyama hao inatekelezwa  kwa ufadhili wa Shirika la Kutetea Wanyama Duniani na Serikali Zanzibar.

Alisema maradhi ya kichaa cha mbwa yamekuwa yakiathiri mifugo kama vile mbuzi,ngo’mbe na paka na wakati mwengine kusambulia binaadamu.

Maeneo yaliyoathirika zaidi na maradhi hayo ni Ubago, Caheju na Koani kwa wilaya ya kati pamoja na Fuoni na Chuini kwa upande wa wilaya ya magharibi.


Aidha alisema maeneo mengine yalioathirika zaidi ni Donge na Zingwezingwe kwa upande wa mkoa wa kaskazini Unguja.

Alisema maradhi hayo yanasabishwa na virusi vinavyojuilikana kama NYSA vinavyoshambulia mishipa ya fahamu, tezi za mate na viungo vya uzazi ambapo dalili zake ni kubadilika tabia na mnyama kuwa mkali.


Alisema juhudi mbali mbali zinachukuliwa ili kudhibiti maradhi hayo ikiwa ni pamoja na kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa inayojuilikana kama ‘rabies vaccine’, ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka pamoja na kutoa elimu juu ya udhibiti wa maradhi hayo.

Wanahabari watakiwa kuibua udhalilishaji

$
0
0
Na Khamisuu Abdallah
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuibua masuala mbalimbali ya udhalilishaji wa kijinsia ili kuongeza uelewa kwa jamii.

Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari yaliyofanyika Ofisi ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (ZANAB), Msimamizi wa vipindi vya redio kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kanda ya Dar es Salam, Judica Losai, alisema ikiwa waandishi wa habari wataongeza uelewa na kuibua mambo mbalimbali ya udhalilishaji itawawezesha watunga sheria kutoa sheria madhubuti ambayo itatoa haki kwa wafanyaji wa vitendo hivyo.

Alisema ni vyema kwa wanahabari kujikita zaidi katika kuelimisha jamii masuala ya udhalilishaji ili jamii iweze kujitambua.

Aidha alisema lengo la mkutano huo ni kuimarisha zaidi masuala ya udhalilishaji na kutoa muamko kwa jamii kuhusu vitendo hivyo.


Kwa upande wake mwanachama wa chama hicho kanda ya Zanzibar, Sophia Ngalapi, alisema ni vyema kwa waandishi hao kuyafanyia kazi ipasavyo mafunzo watakayopewa na kuitumia vyema taaluma yao kwa kuandika habari za udhalilishaji ili vitendo hivyo viweze kuondoka.

Nao wanahabari wakichangia mada, walisema masuala ya udhalilishaji wa kijinsia yapo zaidi katika maskuli na vyuo vya madrasa huku sheria ikiwa ndio changamoto kubwa ya kuzorotesha uendeshaji wa kesi hizo.


Mafunzo hayo yameandaliwa na TAMWA na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbali mbali.

Kandwi wapelekewa huduma za afya

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga
KITENGO cha Elimu ya Afya kimeandaa mpango maaalum wa kutoa huduma za afya kwa watoto katika shehia ya Kandwi ili kuwapunguzia masafa ya kufuata huduma za afya.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakaazi wa eneo hilo kufuata huduma hiyo katika kijiji cha Pwani Mchangani na Chaani hali ambayo inawaletea usumbufu.

Abdulrahman Mussa, alisema masafa ya kufuata huduma za afya ni marefua na yanasababisha baadhi ya wakati watoto kukosa haki yao ya kupatiwa chanjo.


Alisema wakazi wa eneo hilo, wamehamasika kupata huduma hizo lakini umbali wa vituo vya afya umekuwa kikwazo hasa kwa watu wenye umri mkubwa.


Hata hivyo, waliiomba serikali kuwajengea kituo cha afya ili tatizo hilo liondoke kabisa.
Viewing all 35810 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>