Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35810 articles
Browse latest View live

Mabaraza ya watoto, wazee kusaidia kuimarisha maendeleo yao

$
0
0
Na Asya Hassan
OFISA Tawala wilaya ya magharibi, Sabah Saleh, amesema kuanzishwa mabaraza ya watoto na wazee kutasaidia kuimarisha maendeleo yao.

Alisema hayo katika uzinduzi wa mabaraza hayo kwenye shehia ya Kiembesamaki katika hafla iliyofanyika  viwanja vya sheha wa shehia hiyo.

Alisema kuwepo kwa mabaraza hayo ni chachu ya kuwawezesha kujua haki zao pamoja na kuwajengea uwezo watoto hao kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji yanayowakumba.

Alisema kumekuwa na matukio mengi mabaya yanayofanywa kwa watoto na yanashindwa kufikia mwisho na kupata haki zao za msingi.


Alisema kutokana na kukua sayansi na teknolojia kunasababisha vijana kukumbwa na matukio mengi hali inayosababisha kukosa haki zao.

Hata hivyo, Ofisa huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wazee washirikiane na vijana wao katika kufanikisha maendeleo ya mabaraza hayo na wasione kama watoto wao wanapewa mzigo.


Nae sheha wa shehia hiyo, Mwinyi Khatib Juma, alisema watoto wamekuwa wakishawishiwa mara kwa mara juu ya kujishirikisha katika makundi maovu hali inayopelekea kuacha maadili yao.

Je vifo vya watoto vimepungua Afrika?

$
0
0
Na Mwandishi wetu
SEPTEMBA mwaka 2000, viongozi kutoka kote duniani walitia saini mkataba wa kutiumiza Malengo nane ya kimaendeleo ya Milenia (Millennium Development Goals (MDG).
Kila lengo likidhamiria kuimarisha maisha ya watoto wachanga kote ulimwenguni hasa kiafya, kielimu na hata katika kutoa nafasi za kujiendeleza.
Lengo muhimu zaidi kati ya haya ikiwa ni lile la kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaoaga dunia kabla ya kufikisha miaka mitano.
Mahimbo Mdoe kutoka Shirika la Kushughulikia Watoto (Unicef), anaelezea jinsi mataifa yanavyokazana kutatua tatizo hilo.
Hatua kadhaa zimechukuliwa lakini bado kunaendelea kushuhudiwa vifo vinavyoweza kuzuiliwa.
Kwa mujibu wa Unicef, mafanikio yanaendelea kupatikana katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga, kwani kwa sasa idadi ya vifo vya watoto inaendelea kupungua kwa kasi ya juu zaidi kuliko karne nyingine.
 Hata hivyo, watoto zaidi ya milioni 6 hufa kabla ya kufikisha miaka mitano hususan kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.
Mataifa ya Afrika yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara ndiyo yaliyo na asilimia kubwa ya vifo ya watoto wachanga wenye umri ulio chini ya miaka mitano.
Tangu 1990,MDG imekuwa ikilenga kupunguza vifo hivyo kwa thuluthi mbili 2/3 kufikia mwisho wa mwaka 2015.
Majuma manne ya kwanza tangu kuzaliwa kwa mtoto na hasa masaa ya kwanza ya kuwa duniani ndiyo hatari zaidi.
Ingawa idadi ya watoto wanaokufa katika muda huo imepungua, kasi yake imekuwa ndogo sana. Katika mwaka wa 2003, watoto milioni 2.8 walikufa katika muda wa siku 28 toka kuzaliwa.http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/736/amz/worldservice/live/assets/images/2014/09/25/140925103947_chart_complex_01_swahili.gif
Lini lengo la Umoja wa Mataifa litatimizwa?
Kati ya mwaka wa 1990 na 2003 watoto milioni 223 kutoka kote ulimwenguni walikufa kabla ya kutimiza miaka mitano.
Idadi hii ni kubwa sana hata kuliko idadi ya watu wote walio nchini Brazil.
Kwa mwendo huu, lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa thuluthi mbili 2/3 halitotimizwa kabla ya mwaka 2026.
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/736/amz/worldservice/live/assets/images/2014/09/25/140925104015_causes_of_death2-01_v2_swahili.gif


Magazetini Tz Bongo leo

Makamu wa Rais Dkt. Bilal Ahudhuria Kongamano la Biashara la Kimataifa kwa Nchi za Afrika Jijini Dubai

$
0
0
 Mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa Afrika Aliko Dangote katika mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kuhusu uwekezaji wake katika kiwanda cha simenti mkoani Mtwara. Dangote alisema kazi ya ujenzi inakwenda kama ilivyopangwa na kwamba kiwanda hicho kitakuwa kikubwa kabisa kwa uzalishaji simenti katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake baada ya mazungumzo yayo kumalizika walipofika Ofisini kwake jana.(Picha na OMR) 

ZSSF Yakabidhi Msaada wa Mabati kwa Ajili ya Kituo cha Afya Kinuni.

$
0
0
Jengo la Kituo cha Afya Kinuni kilichojengwa kwa Nguvu za Wananchi wa Shehia tatu za Kinuni, Mwera na Mtofaani, kikiwa katika hutua kubwa ya Ujenzi wake, Wanaomba msaada kwa swafadhili mbalimbali ili kuweza kutowa misaada yao kukamilisha uchenzi wake na kuwapunguzia mwendo wananchi swa maeneo hayo ambao hufuata huduma ya Afya ya Mama na Mtoto huduma hiyo mbali na maeneo hayo. juwa kituo hicho hakikukamilika ujenzi wake.Hutoa huduma ya Kliniki katika kjengo hilo kwa kinamama na Watoto katika sehemu hiyo ilioezekwa nusu mabati. Wanaomba msaada wenu Wadau wa Maendeleo ya Afya.     
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF) Ndg. Mussa Yussuf akimkabidhi mabati Sheha wa Shihia ya Mtofaani Bi Kijakazi Ferouz, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la kituo hicho kinuni Unguja.
 Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg.Mussa Yussuf, akizungumza na Wanakamati wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni wakati wa hafla ya kuabidhi mabati 150 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake kituo hicho kinahitaji mabati 187 ili kukamilisha ujenzi huo.
 Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni Ndg.Husein Ali akizungumzia ujenzi huo wakati wa kukabidhiwa mabati na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ili kuweza kuezeka kituo chao hicho na kuwataka Wananchi wengi kutowa msaada wao kuweza kumalizia ujenzi huo na kuaza kutowa huduma ya Afya kwa Wananchi swa Shehia hizo. Amesema kituo chao kitakuwa na sehemu ya Kliniki ya Watoto, Chumba cha kujifungulia Wazazi na kupata huduma nyengimu muhimu zinazotolewa kwa wananchi.Na kusisitiza kuwaomba Wananchi kuwapatia msaada ili kuweza kukimaliza kwa wakati muwafaka. 
 Sheha wa Shehia ya Mtofaani Bi. Kijakazi Ferouz, akitowa neno la shukrani kwa uongozi wa ZSSF kwa msaada wao wa mabati kukamilisha ujenzi huo wa kituo cha Afya Kinuni, ili kupunguza kero za wananchi wa maeneo hayo kufuata huduma ya afya mbali na makaazi yao, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la kituo hicho huko kinuni.    
 Wanakamati wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg. Mussa Yussuf, akitowa maelezo ya Mfuko wa ZSSF, wakatri wa kukabidhi mabati 150 kwa ajili ya kuezekea kituo hicho cha Afya kilichojengwa kwa nguvu za Wananchi wa Shehia tatu za Kinuni. Mwera na Mtofaani kwa ajili ya kupata huduma za afya kituo hapo kupunguza mwendo wa kufuata huduma hizo mbali na makazi yao..   


Polisi wakanusha kupanga kuwafanyia kitu kibaya CHADEMA

$
0
0
Na Rose Chapewa, Mwanza
JESHI la polisi mkoani Mbeya limeelezea kusikitishwa na habari ya uchochezi  iliyoandikwa na  chombo kimoja cha habari, ikidai jeshi hilo litakifanyia kitu kibaya Chama cha Demokrasi na Mendeleo na kudai habari hizo zina lengo la kuligombanisha jeshi hilo na chama hicho.

Hayo yalibainishwa na Kamanda wa polisi mkoa huo, Ahmed Msangi,  wakati akizungumza na waandishi wa habari  na kuwashukuru kwa kufika  ofisini kwake kupata ufafanuzi na hivyo kuzingatia misingi na maadili ya uandishi ya kuandika habari sizoegemea upande mmoja, baada ya uongozi wa Chadema mkoa wa Mbeya, ukiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi, kulalamikia kauli hiyo.

Alisema habari hizo ni za uchochezi na zenye lengo la kuharibu uhusiano uliopo kati ya viongozi wa vyama vya siasa ikiwemo Chadema.

Alifafanua kuwa yeye ni kiongozi anayewatumikia wananchi wote na kwamba kiongozi yeyote mwenye maadili ya utumishi hawezi kusema kitu kama hicho huku akiwapa pole viongozi wa Chadema kwa habari hiyo ambayo imewaumiza.

“Hiyo habari nami pia nimeisoma kwenye gazeti, na baada ya kuiona nilimpigia simu mwandishi aliyeiandika na nikamwambia sijapenda kuandika kitu ambacho sikukisema, na pia hata bosi wake wa hapa Mbeya naye nilimweleza,” alisema.


Awali uongozi wa Chadema  mkoa wa Mbeya,  uliitisha mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, ukimtaka Kamanda Msangi, kukanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku la Kiswahili nchini, kuwa atakifanyia kitu kibaya chama hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, John Mwambigija, alisema kutokana na kauli hiyo chama kimejipanga kuhakikisha kinakabiliana na tatizo lolote litakalosababishwa na jeshi la polisi.

Alisema wanachama wa Chadema hawaliogopi jeshi la polisi, na kutoa siku tatu kwa kamanda wa polisi mkoa huo, kukanusha taarifa hizo.

“Sisi tuna taarifa za kiusalama kama wao wanavyosema tunapata taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, na tayari tumeshawaagiza vijana wetu, wanawajua polisi walioko uraiani, kama hatafuta kauli yake tutawaambia polisi walioko uraiani waende wakakae nyumba za polisi,” alisema.

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, alisema anasikitishwa na kauli ya kiongozi huyo aliyepewa dhamana na jeshi la polisi, na kumuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu, kumfuta kazi mara moja.


Alisema kauli hiyo ya vitisho si kwa ajili ya  wanachama wa Chadema tu bali inaathiri wananchi wote wa mkoa wa Mbeya, huku akijigamba kuwa  wakazi wote wa Mbeya ni wanachama wa Chadema.

Polisi wajipanga kuwashughulikiwa wauza ‘unga’

$
0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, amekiri baadhi ya maeneo ya visiwa vya Zanzibar yanatumika kuingiza dawa za kulevya.

Alisema mwarubaini pekee  wa kukabiliana na tatizo hilo ni jamii  kuwafichua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo.

Alisema jamii inawatambua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao na kuwataka kuondoa muhali kwa kutoa taarifa polisi ili wachukuliwe hatua.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kisiwani Pemba, alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa kupitia falsafa ya polisi jamii, bado uingizaji, usambazaji na utumiaji wa madawa hizo unaendelea.


Aidha alikiri baadhi ya maeneo katika kisiwa cha Pemba kuwa kitovu ya uingiaji wa dawa za kulevya na kuongeza kwamba wamejipanga kuyadhibiti maeneo yao hasa yenye bandari bubu kwa kuimarisha ulinzi na doria.

Aliwataka wananchi kuacha fikira hasi ya kwamba biashara ya dawa za kulevya ni hahali kwa kuwa inawapatia fedha.

Alisema vijana wengi ambao wamejiingiza katika wimbi la utumiaji wa dawa za kulevya wameishia jela kutokana na kushiriki uhalifu.


Maeneo ambayo yanaonekana kukithiri vitendo vya uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya katika mkoa wa kaskazini Pemba ni Mtambwe ambapo kuna bandari bubu nyingi na sheha ya Bopwe.

Oman kulijengea uwezo ZBC

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Oman
OMAN imeahidi kuliimarisha Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) kwa kulipatia vifaa vitakavyoliwezesha kukusanya na kurusha matangazo yake na kuonekana vyema katika nchi za Mashariki ya Kati. 

Ahadi hiyo imetolewa mjini Muscat, Oman na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Redio na Televisheni za Umma wa Oman, Dk.Abdullah Bin Nasser Al Harrasi, wakati akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Said Ali Mbarouk akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini humo.

Alisema mamlaka yake ina dhima kuimarisha uwezo wa matangazo ya shirika hilo na kuonekana vyema Oman na kwengineko na hivyo iko tayari kulipatia vifaa vya kurushia matangazo kwa njia ya satellite  na matangazo ya moja kwa moja kwenye matukio nje ya studio.

Alisema hatua hiyo itazidisha kuimarisha uhusiano uliopo kwa vile itawawezesha wananchi wa Oman kuangalia vipindi vinavyorushwa na ZBC kwa wepesi zaidi kama ilivyo kwa matangazo ya redio na televisheni ya Oman yanavyopatikana Zanzibar.


Alisema kwa kuanzia kutakuwa na utaratibu wa kubadilishana mafundi na watayarishaji vipindi ili kuweka misingi ya kuandaa kwa pamoja vipindi vitakavyotumia lugha ya Kiswahili na Kiarabu na  kuwawezesha wananchi wa Oman na Afrika ya Mashariki kwa ujumla kufaidika na  matangazo ya vituo hivyo.

Akitoa shukrani kwa mamlaka hiyo, Waziri Mbarouk, alipongeza hatua hiyo inayokusudiwa kuchukuliwa na Oman na kusema sio tu itawawezesha wananchi wa pande hizo mbili kuendelea kuelewana zaidi na kupatiwa taarifa juu ya masuala mbali mbali lakini pia itasaidia kukuza na kuinua kiwango cha utalii katika nchi zote mbili.         


Waziri Mbarouk yuko Oman kwa ziara ya siku nne kutembelea vyombo vya habari, utamaduni na utalii na michezo kwa mwaliko wa serikali ya Oman kwa madhumuni ya kutafuta njia za kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.  

Wagonjwa wa kisukari watembea kilomita 20 kutafuta matibabu

$
0
0
Na Kija Elias, Siha
WAGONJWA wa kisukari wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wanalazimika kutembea umbali wa kilometa 20,kutafuta matibabu kutokana na huduma hiyo kutolewa katika hospitali ya wilaya pekee.

Kufuatia hali hiyo, wameiomba serikali ya wilaya hiyo kuwasogezea huduma za afya katika maeneo yao.

Matibabu kwa wagonjwa wa kisukari inatolewa hospitali moja tu ya wilaya jambo ambalo limekuwa likisababisha wagonjwa kutembea umbali mrefu.

Katibu wa klabu ya wagonjwa wa kisukari wilayani hapa (DIABETIC), Halima Hamisi, alitoa ombi hilo katika hospitali ya wilaya ya Siha wakati akizungumza na umoja wa wanawake wa CCM.

Akizungumza na wagonjwa hao, Katibu wa UWT, wilayani hapa, Zeydani Mwamba, aliishukuru serikali kwa kuimarisha miundombinu katika hospitali hiyo ambayo imeanza kutoa huduma huku akiwataka wagonjwa hao kuwa  na subira  juu ya tatizo hilo.


Mratibu wa huduma za maabara wa wilaya hiyo, Zakaria Magoye, alikiri kuwepo tatizo hilo na kusema serikali itajitahidi kuweka kliniki za kisukari katika hospitali za wilaya.

Harakati za mwisho mwisho Maandalizi ya Sikukuu Mitaa ya marikiti ya chakechake Pemba yapamba moto.

Ligi Kuu Mafunzo na Hardrock Uwanja wa Gombani Pemba, Hardroch imeshinda 2--1

Fainal Kombe la Karume Basket Ball Polisi na Rangers.

$
0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwakimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Kombe la Karume Nahodha wa timu ya Polisi Ndg, Mohammed Kassim, baada ya timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Rangers kwa vikapu 80--76.mchezo huo uliofanika uwanja wa gymkhana.na kuhudhuriwa na Mlezi wa michuano hiyo Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume ,amekuwa mfadhili wa michuano hiyo kwa muda mrefu. tgangu kuazishwa kwake. 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akitowa nasaha zake kwa washiriki wa michuano ya Karume Cup, baada ya mchezo wa fainali kati ya Rangers na Polisi uliofanyika uwanja wa gymkhana 
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar (BMZ) Bi. Shery Khamis akielezea michuano hiyo na kuzipongeza timu zilizoshiriki michuano ya mpira swa Kikapu Kombe la Karume wakati wa maadhimisho ya mchezo wa fgainali kati ya Rangers na Polisi. 
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Shery Khamis akimfahamisha kitu Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wakiangalia mchezo wa Fainal ya Kombe la Karume uliofanyika uwanja wa gymkhana kulia Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume wakifuatilia mchezo huo uliotoa Bingwa wa Karume Cup timu ya Polisi Zanzibar kwa ushindi wa vikapu 80--76.  
Washiriki wa michuano ya Karume Cup  wakifuatilia mchezo wa fainali kati ya Polisi na Rangers, uliofanyika uwanja wa gymkhana.


WEaandishi Washauriwa Kutumia Teknolojia Kuhifadhi Kazi Zao.

$
0
0
Na Mwashamba Juma, Dar es Salaam
WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kurahisisha kazi zao kwa kuziweka salama na kuzinusuru na athari za teknolojia hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari za magazeti ya Tanzania, Ofisa ruzuku wa Mfuko wa Vyombo vya habari Tanzania (MF), Dk. Dastan Kamanzi huko ukumbi wa ofisi hizo, Mhimbili jijini Dar es Salam wakati akiwapa taaluma ya kutumia mtandao wa “Google Drive” waandishi hao katika warsha ya ruzuku za vijijini.

Dk. Kamanzi alisema mtandao wa “google drive” ni kimbilio pekee kwa waandashi wa habari wasasa katika kuzinusuru kazi zao kuathiriwa na maendeleo ya teknolojia ikiwemo kuharibiwa na virusi kwenye komputa, kuibiwa ama kupotea.

Aidha alisema “goole drive” hurahisisha na kuepusha kutembea na “had ware” zikiwemo laptop, flash, recoders na asets nyengine kwa lengo la kuondosha usumbufu wa kubeba mizigo kila mahali.

“Ukiwa na “google drive” mwandishi huhitaji kuwa na matumizi ya ziada ya “flash disk,” CD au hardware yoyote hata ukiwa ya nje ya ofosi, hakuna ulazima wa kutembea na laptop kila mahala, simu yako ya mkononi inatosha hasa kwa waandishi wanaotoka nje ya mji” alifahamisha.


Alisifu uzuri wa taaluma ya “google drive” kwa kueleza kuwa hata mwandishi wa habari asipokuwa na huduma ya mtandao “internet”, bado anaweza kuhifadhi kazi zake na kuwa salama hadi wakati atakapokuwa nao nakuongeza kuwa kazi zake zitakuwa salama kwa ofisi na binafsi.

Mapema akiwasilisha mada ya “Uandishi wa makala”, msimamizi wa ruzuku za vjijijini katika warsha hiyo (Mentor), Burhan Khatib Muhunzi alisema bado kuna baadhi ya waandishi wa magazeti hadi sasa hawawezi kutofautisha baina ya makala na stori za kawaida katika uandishi wao.

Alisema makala lazima ifanyiwe utafiti wakina kabla ya kuandikwa kwake sambmba na kujitosheleza kuwa na vyanzo vingi vya habari vitakavyobeba wazo la stori husika sio mawazo ya mwandishi mwenyewe.

“Waandishi hakuna alisema kwenye makala wala huandiki mawazo yako, lazima ulifanyie utafiti wazo lako, muandike kilichozungumzwa chanzo chako cha habari, halafu uende ndani zaidi uibue yaliyojificha, ili umpe nafasi msomaji wako, sio alisema …alisema…” alifahamisha Mentor huyo.

Nae msimamizi Samson Kamalamo aliwataka waandishi hao kuzingatia maadili ya uandishi wahabari na kuongeza kwamba stori ilikuwa inamashaka na maadili, mwandishi anahaki ya kutoichapisha stori hiyo.

Kwa upande wa washiriki ambao ni waandishi wa habari za magazeti kutoka vyombo mbalimbali vya habari walikiri kwamba kuna baadhi ya vyombo vyahabari bado vinaendelea kukiuka maadili ya kiuandishi hususani mitandao ya jamii, zikiwemo globaz.

Walisema ni mwiko katika uandishi wa habari kuonesha sura za maiti ama watoto walidhalilishwa, lakini baadhi ya vyombo vya habari hufanya hivyo bila ya kutanguliza msamaha, hali ambayo inaitia dosari tathnia ya habari Tanzania.


Warsha hiyo ya wiki moja kwa waandishi wahabari za vijijini kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini imeandaliwa na kusimamiwa na Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania, TMF.

Wafanyakazi Uwanja wa Ndege Pemba Watakiwa kufanya kazi kwa Bidii na Uwajibikaji.

$
0
0
Na Bakar Mussa, Pemba
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa raslimali watu wa mamlaka hiyo, Rajab Talib Abdalla, wakati akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo katika hafla ya kuwazawadia wafanyakazi bora.

Alisema katika kipindi kifupi kijacho mamlaka itaweka vifaa vya usalama katika uwanja huo.

Bado abiria wanaosafiri katika uwanja huo wamekuwa wakipekuliwa kwa kutumia mikono hali inayosababisha migogoro baadhi ya wakati.

Alisema miongoni mwa mikakati ya mamlaka katika  kipindi cha miaka mitano ijayo ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake wanaokaribia kustaafu, ili wanapomaliza muda wa utumishi wasiwe na hofu juu ya maisha yao.


Nae Meneja wa mamlaka ya uwanja wa ndege Pemba, Rajab Ali Mussa, alisema kumekuwa na ushirkiano mkubwa katika uwanja huo kati ya wafanyakazi na mawakala wa mashirika ya ndege jambo ambalo limeongeza kiwango cha abiria kutoka 250 hadi 300 kwa siku sawa asilimia 11.6.

Alisema ongezeko hilo limekwenda sambamba na kuwepo ndege 14 kwa siku na mashirika 18 ya ndege yanayotoa huduma.


Mzee Ali Juma, kutoka Jumuiya ya Cotwu Pemba, aliwasihi wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuzidisha nidhamu katika kazi zao za kila siku.

Historia yaandikwa Rasimu inayopendekezwa yapita

$
0
0
Na Mwantanga Ame
Hatimae wajumbe wa bunge maalum la katiba, wamepitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa, baada ya kupata theluthi mbili ya kura kutoka pande zote mbili za Muungano.

Furaha na nderemo zilihanikiza ukumbi wa bunge, baada ya Naibu Katibu wa bunge hilo, Dk. Thomas Kashilila, kutangaza matokeo ya kura zilizopigwa.

Shughuli za bunge zilisimama kwa muda kutokana na wajumbe kuanza kuimba nyimbo mbali mbali kwa furaha, baada ya Naibu Katibu huyo kumaliza kusoma kura za upande wa Zanzibar.

Akitangaza matokeo ya kura hiyo, Kashilila alisema theluthi mbili ya kura za Zanzibar imepatikana na baadae kuanza kusoma kura za upande wa Tanzania Bara.

Wasi wasi mkubwa ulikuwepo kwa kura za Zanzibar kama zingetimiza theluthi mbili baada ya baadhi ya wajumbe kupiga kura ya hapana na wengine kukataa baadhi ya vifungu.

Alisema wajumbe wa Zanzibar,walipaswa kuwa 219 na waliopiga kura walikuwa  ni 154 huku wajumbe  65 wakikosa kupiga kura.

Alisema ili theluthi mbili ya Zanzibar iweze kupatikana kulihitajika kupatikana kura 146.

Akichambua matokeo hayo, Kashilila alisema katika sura ya kwanza yenye ibara ya 1 hadi 11, imepata theluthi mbili, sura ya pili yenye ibara ya 12 hadi 21 imepata theluthi mbili, sura ya tatu inayoanza na ibara 22 hadi 26 imepata theluthi mbili na hali kama hiyo ilijitokeza kwa sura nyengine zote.

Baada ya Naibu Katibu kusoma kura za ibara zote, ndipo Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, alipotangaza rasmi kupitishwa rasimu inayopendekezwa.

Akitoa maelezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Endrew Chenge, alisema kutokana na matokeo hayo rasimu hiyo sasa itaitwa rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014, ambayo itakwenda kwa wananchi kupigiwa kura.

Alisema bunge hilo limezipigia kura ibara zote kwa kuzingatia uwepo wa theluthi mbili katika pande zote za Muungano na ni dhahirisha kwamba rasimu hiyo imeungwa mkono.


Akitoa shukurani, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, alisema kazi hiyo imemalizika ikiiacha Tanzania katika hali ya amani na utulivu licha yakujitokeza vitimbi vilivyokuwa vikiashiria kutaka kuvuruga amani.

Alisema wakati mchakato huo unamalizika, angetamani kuona serikali inawatengezea mazingira Watanzania wakati watakapopiga kura katika uchaguzi mkuu ujao, iende sambamba na upigaji kura wa katiba hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alisema Tanzania imefanikiwa kujenga historia na itakuwa busara kwa Watanzania kuiunga mkono kwa sababu imejali maslahi ya makundi tofauti wakiwemo wanawake.

Aidha aliwataka Watanzania kupambanua pale yanapojitokeza matamko ya baadhi ya watu wanaojiita Wazanzibari wanaokataa Muungano kwa sababu sio wote wanaoukataa.

Aliwaomba wananchi wa kuepuka propaganda zinazoendelea kutolewa kwamba wajumbe wa bunge hilo wamepoteza fedha za wananchi.

Nae mjumbe mkongwe wa bunge hilo, mzee Kingunge Ngobale Mwiru, aliwataka wajumbe wa bunge hilo, kuacha kulumbana na wabunge waliotoka ama makundi mengine yanayoipinga katiba hiyo na badala yake waende kufanya kazi ya kuwashawishi wananchi kuipigia kura ya ndio.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, alikanusha madai kwamba alikuwa akilipwa shilingi 7,000,000 ili kubadilisha kanuni za kuendesha bunge na kwamba hata angepewa angezikataa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anna Makinda, aliwataka Watanzania kutambua kwamba umasikini hauwezi kuondoka kwa kuvutana kila wakati badala yake wajenge tabia ya kupendana.

Mjumbe wa bunge hilo, Hamad Rashid Mohammed, alisema haoni haja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, kukubali kutumia katiba yenye viraka katika uchaguzi mkuu ujao na badala yake aharakishe kutumika kwa katiba mpya.

Nae John Cheyo, alieleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na atakuwa tayari kuhakikisha katiba hiyo inaungwa mkono.

Nae mjumbe kutoka Chadema, John Shibuda, alisema yuko tayari kuitwa msaliti lakini kazi aliyoifanya kwa ajili ya kuwatetea wakulima, wafugaji na wavuvi imekamilika.

Nao viongozi wa dini wakitoa shukrani zao akiwamo Sheikh, Nouman Juma Jongo, walisema wanakubaliana na maamuzi ya Mwenyezi Mungu na kuumaliza mchakato huo kwa usalama.

Askofu mstaafu Dornad Mtetemele, alisema ni vyema Watanzania kuipokea katiba inayopendekezwa.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wajumbe wa bunge hilo, Peter Serukamba, alisema kitendo walichokifanya kimewajengea historia kubwa kwa kuumaliza mchakato huo katika hali ya usalama na amani.

Upande wa kundi la 201, mjumbe Amon Mpanju, aliwapongeza wajumbe hao kwa kuandika katiba iliyozingatia haki za walemavu, wavuvi na wakulima mambo ambayo hayajawahi kuzingatiwa katika katiba iliyopita.

Nae Mjumbe Hawa Mchafu, akitoa shukrani kwa niaba ya wanawake na vijana,alisema ni vyemakwa vijana wa Tanzania kuiona katiba hiyo ni yao kwa sababu imezingatia Maslahi yao.

UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU CHA UDOM Inbox x MUHIDIN MICHUZI

$
0
0

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya  Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kuanzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dododma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.
Jengo kuu la  Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 
 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM
 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM
 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katuika ukumbi wa Chimwaga katika Cho Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.
src="http://3.bp.blogspot.com/-jF3X9lBirNY/VC_M2rFFVMI/AAAAAAAGnt8/Is69QJ1gjGE/s1600/u6.jpg" height="336" width="640" />
 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM
 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM
 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katuika ukumbi wa Chimwaga katika Cho Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.

Tusome Tujifunze

$
0
0
Watoto hawa wamekuta katika moja ya duka la magazeti katika mji wa Chakechake wakipitia magazeti yaliokuwa katika duka hilo kupata habari na kujifunza kusoma kupitia magazetini kama wanavyoonekana pichani wakiwa dukani hapo wakiwa bizz kuagalia na kusoma magazeti.

Dk. Shein Awasili Kisiwani Pemba Kuhudhutria Baraza la Eid Kesho.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usdalima uwanja wa ndege Chake baada ya kuwasili kisiwani humo kuhudhuria sherehe Baraza la Eid Alhajj kesho.
 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid alipowasili uwanja swa ndege wa Chakechake Pemba kuhudhuria Sala ya Eid na Balaza la Eid Kitaifa linafanyika kisiwani Pembe kesho katika viwanja vya Wilaya Micheweni Pemba. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, awasili uwanja wa Ndege Pemba kuhudhuria Baraza las Eid na Sala ya Eid Alhajj kitaifa mwaka huu inadhimishwa kisiwani Pemba katika Wilaya ya Micheweni Pemba.akisalimiana na Wananchi na Viongozi wa Serekali alipowasili leo jioni.

Balozi Seif Akutana na Muwekezaji kutoka Marekani na Balozi wa Heshima wa Tanzania U S A.

$
0
0
 Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake akimtambulisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya maendeleo ya ujkenzi ya Detroit Nchini Marekani Bw. Andrew G. McLemore kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipokutana kwa mazungumzo VIP ya Uwanja wa ndege wa Pemba.Aliyepo kushoto na Balozi Seif ni Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh. Suleiman Saleh.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake kwenye uwanja wa ndege wa Pemba.(Picha na Hassan Issa OMPR)


Na.AOthman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi alikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ms Shimoja kutoka Jimbo la Michigan Nchini Marekani Dr. Robert Shumake.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika chumba cha watu mashuhuri { VIP } kilichopo kwenye uwanja wa ndege wa Pemba ambapo Balozi Seif aliwasili akitokea Mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba.
Katika mazungumzo yao Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake ambaye amepata heshima ya kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani alielezea kuridhika na mazingira mazuri ya uwekezaji kisiwani Pemba.
Dr. Shumake alisema Uongozi wa Kampuni yake utaangalia maeneo ambayo inaweza kuwekeza vitega uchumi kama alivyomuahidi Balozi Seif wakati wa ziara yake katika Jimbo la Seattle Nchini Marekani mwaka jana.

“ Muda wangu mfupi niliopata kutembelea maeneo tofauti ya Tanzania ikiwemo Zanzibar umenipa faraja na shauku ya kuangalia fursa zilizopo za uwekezaji na namna  uongozi wa Kampuni yangu utakavyochangamkia fursa hiyo “. Alisema Dr. Robert Shumake.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo ya Ms. Shimoja kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuupa msaada wakati unaohitaji kuwekeza hapa Zanzibar.
Balozi Seif alimueleza Dr. Shumake kwamba Zanzibar tayari imetoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza miradi na vitega uchumi vyao ili kusaidia kunyanyua pato la taifa sambamba na kuongeza soko la ajira.
Alisema yapo maeneo na sekta ambazo Kampuni ya Ms Shimoja inaweza kuyatumia kuwekeza akiyataja kuwa ni patoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Pemba, Bandari ya Wete, Sekta ya utalii pamoja na nyumba za mkopo nafuu.
Alifahamisha kwamba miradi ya nyumba za mikopo nafuu kwa kiasi kikubwa inaweza kuwasaidia zaidi vijana wenye ajira mpya  ili wajenge hatma bora ya maisha yao ya baadaye.
Dr. Robert Shumake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms. Shimoja ambae pia ni Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani alikuwepo Nchini Tanzania kutia saini mkataba wa uanzishwaji wa treni iendapo kwa mwendo wa kasi kati yake na Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania.
Treni hiyo itakapokamilika itakuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya Dar es salaamu na pugu kwa kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/10/2014.

4 Attachments

Magazetini Bongo Tz

Viewing all 35810 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>