Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35810 articles
Browse latest View live

Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile Afungua kipya Mji Mwema Kigamboni cha Fursat Dhahabiyya.

$
0
0

  Mbunge we jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile akifunguaRasmi (Wa Pili Kulia)kiota kipya Mji Mwema Kigamboni kinachoitwa Fursat Dhahabiyya.

 Wadau mbalimbali wakijivinjari ndani ya kiota kipya cha Fursat Dhahabiyya Kilichopo Mji Mwema Kigamboni
 Mwonekano wa Ndani wa Kiota Hicho

Kikoao cha Baraza la Wawakilishi Kupitisha Miswaada Miwili

$
0
0

TANGAZO
Katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kitakachofanyika Tarehe 22/10/2014, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar linatarajia kupitisha Miswaada miwili ambayo ni; Mswaada wa Sheria ya Madaili ya Viongozi wa Umma na Kuanzisha Tume ya Maadili ya Viongozi na Mambo mengine yanayohusiana na hayo. 

Serikali imeamua kuwasilisha Mswada huu ambao utasimamia Maadili ya Viongozi wote hapa Zanzibar waliotajwa kwenye Jadweli la Mswada huu.

Katika  Mswaada huu Kiongozi yeyote wa Umma aliyetajwa katika Sheria atatakiwa ndani ya kipindi ambacho  kimeelezwa katika Mswaada huu kuwasilisha kwa Mwenyekiti tamko la mali kwa maandishi kuhusu mali zake anazomiliki na alizonazo wakala wake, madeni anayodaiwa pamoja na mali na madeni ya mwenza wake, watoto wake au watoto walio chini ya uangalizi wake.

Kwahivyo, Tume ambayo itaanzishwa kwa mujibu wa Mswaada huu itakuwa na majukumu mengi mbali mbali ikiwemo kupokea na kuhifadhi tamko la mali ambalo limetolewa na Kiongozi wa Umma chini ya Sheria hii, Kupokea tuhuma na taarifa za uvunjwaji wa maadili kutoka kwa wananchi, Kufanya uchunguzi juu ya madai au tuhuma za uvunjwaji wa maadili kwa kiongozi yeyote wa Umma.


Mswaada mwengine ni Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Wauguzi na Wakunga (Uanzishwaji wa Baraza la Usajili wa Wauguzi na Wakunga) Nam. 9 ya mwaka 1986 na kuanzisha badala yake Sheria mpya ya Wauguzi na Wakunga na mambo yanayohusiana na hayo.
Madhumuni ya kutungwa sheria hii mpya ni kuleta pendekezo la kufuta Sheria ya Wauguzi na Wakunga, Sheria Namba 9 ya 1986 ambayo imeonekana kwamba imepitwa na wakati na kupendekeza kuanzishwa kwa Sheria mpya ya Wauguzi na Wakunga ambayo itaweza kusimamia vyema misingiya taaluma na maadili ya fani hii kuendana na mabadiliko ya nchi kisiasa, kijamii na kiuchumi. Aidha mswaada huu unakusudia kuanzisha Baraza la na Wakunga litakalokuwa na wajibu ya kusimamia fani ya wauguzi na wakunga. Miongoni mwa sababu za msingi zilizopelekea kufuta Sheria hiyo ni Mabadiliko ya Sera ya Afya; Mabadiliko ya ukuaji wa kiuchumi na kuongezeka mahitaji ya kijamii yanayotokana na ongezeko la watu na mabadiliko ya kimazingira; Kutanuka kwa taaluma ya Wauguzi na Wakunga katika taasisi binafsi na za serikali.  
 Kwahivyo tunakaribisha michango na maoni kwa wananchi wote katika miswaada hiyo na kwa mtu yeyote anaehitaji nakala ya Mswaada tunawakaribisha katika Ofisi zetu za Baraza la Wawakilishi zillizopo Chukwani kwa Unguja na kwa waliopo Pemba tunawakaribisha kwenye Ofisi yetu iliypo Wete  au unaweza kuupata kupitia kwenye mtandao wetu www.zanzibassemly.go.tz.

Mwisho wa kupokea maoni hayo ni Tarehe 12 – 10 – 2014.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MENEJIMENTI YA BENKI YA NBC IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Bi. Mizinga Melu  (wa tatu kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi Rukia Mtingwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimsindikiza  Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa Bi. Mizinga Melu  alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo.


 Rais Jakaya Kikwete  katika picha ya kumbukumbu na  Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Bi Mizinga Melu  (wa pili kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi Rukia Mtingwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  NBC, Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
 Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Bi Mizinga Melu (wa pili kushoto), alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi. Rukia Mtingwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa NBC, Bw. Pius Tibazarwa na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Bw. William Kallaghe. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi mkurugenzi wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni. PICHA NA IKULU

Hutuba ya Rais wa Zanzibar Dk. Shein Baraza la Eid Alhajj

$
0
0
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI, MHESHIMIWA AL-HAJ DK ALI MOHAMED SHEIN,
KATIKA BARAZA LA IDD EL HAJJ, OKTOBA, 2014
 (Mwezi 10 Mfunguo Tatu: 1435)

Bismillahi Rahmani Rahim,

Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu; Mola wa viumbe wote.  Mwenyezi Mungu ndiye anayestahiki kukusudiwa na viumbe wote kwa kumuabudu, kumuomba msamaha na kumtegemea. 

Sala na salam zimshukie Mtukufu wa daraja, Mtume wetu na kigezo chetu; Nabii wa Mwenyezi Mungu, Sayyidna Muhammad (S.A.W) pamoja na wafuasi wake wote hadi kitakaposimama kiama.  Mwenyezi Mungu atujaalie na sisi tuwe miongoni mwa wenye kufuata mwenendo wao na kupata malipo mema hapa duniani na huko akhera twendako. AMIN!

Ndugu Wananchi,
Mheshimiwa Sheikh Khamis Haji Khamis;
Kadhi Mkuu wa Zanzibar,

Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad;
Makamu wa Kwanza wa Rais,

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi;
Makamu wa Pili wa Rais,

Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho;
Spika wa Baraza la Wawakilishi,

Mheshimiwa Omar Othman Makungu;
Jaji Mkuu wa Zanzibar,

Waheshimiwa Mawaziri,

Waheshimiwa Mabalozi,

Wageni Waalikwa,


Mabibi na Mabwana,


Assalamu Aleikum Warahmatullah Wabarakatuh


IDD MUBARAK


Nimeanza kwa kushuhudia kuwa hapana Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (SW) na kumsalia mbora wa waja; Mtume wetu Seyyidna Muhammad (S.A.W) pamoja na wafuasi wake.  Hapana shaka ni uwezo wake  Subhana Wataala kutujaalia neema ya uhai tukaweza kuidiriki siku hii na kuiadhimisha kwa Takbira nyingi.

Kwa mapenzi yake Mola wetu kwetu, tumeweza kuungana na Waislamu wenzetu walioko katika Mji Mtukufu wa Makka wanaoendelea kutekeleza Ibada ya Hija ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu.  Waislamu wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla tunaungana na wenzetu duniani kote kumuomba Mwenyezi Mungu awatakabalie ibada zao zote, awawezeshe kuzingatia mafunzo ya Hija na kuyaendeleza na awarudishe nyumbani salama ili waweze kuungana tena na familia, jamaa, marafiki na wananchi wenzao.

Ndugu Wananchi,
Mwenyezi Mungu ametujaalia Waislamu sikukuu mbili kubwa kila mwaka;  Sikukuu ya Idd el Fitri na Sikukuu ya Idd el Hajj, tunayoisherehekea leo.  Miezi miwili iliyopita na siku kidogo, tulisherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri baada ya kuikamilisha ibada ya swaumu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan na leo tena tupo hapa Micheweni katika Chuo cha Kiislamu hapa Kiuyu kwa ajili ya Sikukuu ya Idd Al- Adhha, ambayo tunasali  Idd na kuchinja kama ilivyoagizwa katika Suratul Kawthar,  aya ya  kwanza na ya pili zenye tafsiri isemayo:

“Hakika tumekupa kheri nyingi”. 
“Basi sali kwa ajili ya Mola wako na uchinje”.

Mbali na wajibu wetu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuzifikia sikukuu hizi tukiwa hai, vile vile, tuna wajibu wa kuzingatia mafunzo yanayotokana na ibada hizi na kuyaendeleza katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani.

Ndugu Wananchi,
Ibada ya Hija imekusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa Mola wake.  Hija ni mithili ya taasisi ya mafunzo ya malezi na maarifa kwa Waislamu katika misingi ya tawhidi kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu na huanza kwa kuweka nia safi na ikhlasi.  Mafunzo haya yana mchango muhimu kwa mja kuwa mcha Mungu kwa kujiepusha na vitendo vyote vitakavyomtoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na mafunzo ya Bwana Mtume Muhammad (SAW) aliyeletwa kwetu kutupa miongozo.

 Mwenyezi Mungu anatukumbusha kwenye Kurani katika sehemu ya aya ya 7 ya Suratul Hashir yenye tafsiri isemayo:

“…… Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho.  Na muogopeni Mwenyezi Mungu; kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu“.

Kwa mnasaba wa aya hii, Mwenyezi Mungu anatuasa kuzingatia mafunzo ya Bwana Mtume kwa kufanya yote tuliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (SW), likiwemo hili la kutekeleza ibada ya Hija na kuzingatia mafunzo yake na kutubainishia ubaya wa kushindwa kuitekeleza kwa wale waliojaaliwa kuwa na uwezo. Mtakumbuka katika hotuba yangu ya Idd el Fitri nilieleza kuwa mafunzo ya Saumu ya Ramadhani ni mfano wa mafunzo ya Chuo Kikuu. Mafunzo yanayohusiana na utekelezaji wa Ibada ya Hija  nayo ni  mafunzo ya daraja la juu. Mwenye kufuzu na kupata hio daraja ya juu, kwa hakika hupata fadhila kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hadhi na heshima hata ya kumtambua kuwa Al-Hajj kwa mwanamme na Hajjat kwa mwanamke.

Kwa hivyo, tunapaswa kuwapongeza Waislamu wenzetu waliofanikiwa kwenda kuitekeleza ibada ya Hija na tuwape heshima wanayostahiki.  Pamoja na hayo, tuzidi kuwaombea hija zao zikubaliwe. Wale watakaofuzu huwa wamefutiwa madhambi yao yote, kama inavyosema hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Sayyidna Abu Huraira (RA), Bwana Mtume (S.A.W) amesema:

Mwenye kufanya  Hijja bila ya kusema maneno machafu na bila ya kufanya vitendo vichafu, atasamehewa madhambi yake arudi kama siku aliyozaliwa na mama yake”

Tumuombe Mola wetu (SW) azikubali ibada za Waislamu wenzetu wote waliokwenda kuitikia wito Wake wa kwenda kufanya ibada hiyo.

Ndugu Wananchi,
Jambo jengine muhimu tunalojifunza katika Ibada ya Hija ni kubainisha hisia za Umoja wa Kiislamu na usawa wa wanaadamu mbele ya Mwenyezi Mungu.  Waislamu kutoka mataifa mbali mbali, wenye nyadhifa, uwezo na rangi mbali mbali hukusanyika pamoja katika mji mtukufu wa Makka na Madina, wakiwa na lengo moja la kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu wa kufanya ibada katika nyumba tukufu ili kupata uongofu.  Katika Surat Al- Imran aya ya 96 Mwenyezi Mungu amesema,

“Kwa yakini Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na yenye uwongofu kwa ajili ya walimwengu wote”.

Na katika aya ya 97 ya Sura hiyo Mwenyezi Mungu ameendelea kusema:

“Humo mna ishara zilizo wazi (za kuonesha utukufu wake na ukongwe wake.  Miongoni mwa hizo ni) mahali alipokuwa akisimama Ibrahimu, na anayeingia (nchi hiyo) anakuwa katika salama.  Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hija katika Nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko .……”.

Ni faraja iliyoje kwa Muislamu kupata wasaa katika uhai wake kujumuika katika mkusanyiko mkubwa wa Umoja wa Waislamu wa kila mwaka katika nyumba tukufu. Katika mazingira haya mahujaji hupata fursa ya kujadiliana masuala mbali mbali ya kuuendeleza Uislamu na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili katika ulimwengu wa leo. Kadhalika, mkusanyiko huu ni kielelezo cha umoja, udugu na mshikamano wa Waislamu kwamba wanafuata miongozo ya Kurani Tukufu na Hadithi za Bwana Mtume Muhammad (S.A.W).

Ndugu Wananchi,
Hapana shaka kwamba maarifa mapya wanayoyapata mahujaji wetu wanapofanya ibada ya Hija, yatakuwa na manufaa zaidi iwapo watakuja kuyaendeleza watakaporudi hapa nyumbani.  Ni dhahiri kuwa nchi yetu inahitaji sana kuzidi kuendelezwa kwa hali ya umoja na mshikamano wetu kwani ndio siri kubwa ya mafanikio tuliyoyapata katika kuimarisha amani tuliyonayo, ustawi wa uchumi na kukuza maendeleo ya jamii.


Kwa hivyo, kwa kuwa hali hiyo ya umoja na mshikamano, mtu anaweza kuihisi katika wiki chache tu za kukutana na watu kutoka nchi mbali mbali kwa mamilioni wakati wa Hija, ni vyema akaiendeleza wakati anaporudi hapa nyumbani tunapoishi siku zote. Hiyo itakuwa ndiyo namna bora ya kuyatumia mafunzo hayo yanayotakiwa yadumu katika maisha yetu ya kila siku na ndio kielelezo bora cha mtu aliyekwishahiji.

Ndugu Wananchi,
Vile vile, mahujaji wetu hunufaika katika kuziimarisha imani zao kutokana na kuyatembelea maeneo mashuhuri ya historia ya Uislamu, wakiwa na amani ya nafsi na ya kimazingira wakati wote.  Katika kipindi chote cha Hija ndugu zetu hawa huwa ni wageni wa Mwenyezi Mungu Mkarimu.  Katika hadithi iliyopokelewa na Sayyidna Anas bin Malik (RA), Bwana Mtume (S.A.W) amesema:
“Mwenye kufanya Hija na mwenye kufanya Umra ni wageni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.  Hupewa wanachoomba, na (Allah) anajibu dua zao, na hurudishiwa walivyotoa, dirham (au shilingi) moja kwa dirham (au shilingi) milioni moja” (Al baihaqiy).

Katika hadithi nyengine iliyopokelewa na yeye Sayyidna Anas bin Malik (RA) vile vile Bwana Mtume (S.A.W) amesema:

Kutoa kwa ajili ya Hijja ni sawa sawa na kutoa kwa ajili ya jihad; dirham moja kwa mia saba” (Tabrany)

Riwaya hii imetafsiriwa na baadhi ya Maimamu kuwa inamaanisha kwamba hata wale wasiokwenda Hija, lakini kwa namna mbali mbali hushiriki katika kuwaandalia safari Mahujaji wetu, vile vile nao Mwenyezi Mungu huwalipa malipo makubwa.  Napenda kutoa shukurani zangu kwa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, kwa kushirikiana vyema na taasisi zote zilizohusika katika kuwasafirisha Mahujaji wetu kwa kuwahudumia vyema tangu mwanzo hadi sasa na Inshaallah mpaka hapo watakaporudi hapa nyumbani. Tumuombe Mwenyezi Mungu sote atupe ilham, afya na uwezo wa kupata kuitekeleza nguzo hii ya tano ya Kiislamu  na kuwasaidia kwa kila namna wenzetu waliojaaliwa uwezo wa kwenda kuhiji ili sote tuweze kunufaika na fadhila  zake.

Ndugu Wananchi,
Napenda kutumia fursa hii kusisitiza umuhimu wa kuyaendeleza mafunzo yanayotokana na ibada zetu mbali mbali katika maisha yetu ya kawaida, hasa suala la kuhimizana kufanya mambo mema na kukatazana mambo mabaya.  Kufanya hivyo ni kuitii amri ya Mola wetu Mtukufu, kutekeleza mafundisho wa Bwana Mtume (S.A.W) pamoja na jamii inayozingatia misingi ya sheria na utawala bora.

Mwenyezi Mungu huongeza baraka na neema katika jamii ambayo huzishukuru neema zake kwa kuzitumia katika njia inayolenga kunufaisha watu walio wengi.

Kwa kutumia uwezo wa rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ametujaaliya nchini, Serikali inaendelea na jitihada zake kwa kushirikiana na washirika wetu wa maendeleo mbali mbali katika kuimarisha miundombinu ikiwemo barabara, usambazaji wa maji safi na salama, huduma za umeme na mengineyo.

Katika Mkoa huu wa Kaskazini Pemba, wenyeji wa Mkoa huu na hata baadhi ya wageni ni mashahidi wa kubainisha jitihada hizo ambazo naamini matunda yake yanafurahiwa na watu wengi kwani mambo haya ya maendeleo yaliofanywa ni ukombozi mkubwa wa hali ya maisha ya wananchi.

Serikali kwa kushirikiana na washirika wetu wa maendeleo imefanya juhudi kubwa ya kuimarisha miundombinu ya barabara katika Mkoa huu.  Ni dhahiri kuwa, kuimarika kwa miundombinu ya barabara kutasaidia sana katika kuimarisha sekta nyingine za kiuchumi.

Kwa kipindi kirefu miundombinu ya barabara ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi kwa ajili ya kuendesha maisha yao na kwa wawekezeji wengi waliokuwa na azma ya kuwekeza katika katika sehemu mbali mbali nchini. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitangaza maeneo huru ya uchumi katika mwaka 1992, ambapo ilitenga eneo la Fumba kwa upande wa Unguja na eneo la  Micheweni kwa upande wa Pemba; kwa ajili ya kazi hiyo. Ukosefu wa miundombinu ya barabara za kisasa kwa kipindi kirefu ulikwamisha jitihada zetu za kupata wawekezaji wenye viwango tunavyotaka katika maeneo huru yaliyotengwa hapa Micheweni na Mkoa wa Kaskazini, Pemba kwa jumla. Ni dhahiri kuwa, hatua tuliyofikia hivi sasa ya kuimarisha miundombinu, itasaidia sana katika juhudi zetu za kutafuta wewekezaji tunaowataka.

Ndugu Wananchi,
Kwa bahati mbaya, wapo baadhi ya wananchi wachache ambao wanaendelea kuweka mbele maslahi yao  kwa kuharibu maslahi ya wengi. Katika maeneo mengi ya Unguja na Pemba kumekuwa na uharibifu wa makusudi wa miundombinu mbali mbali, licha ya Serikali kutumia fedha nyingi katika kuiimarisha. Wapo baadhi ya watu wanaong’oa nguzo na mabati ya alama za barabarani. Kwa upande wa miundombinu ya umeme, wako wanaokata nyaya za transforma. Kesi za uharibifu wa transforma ni nyingi ikiwemo iliyotokezea mwezi Agosti, mwaka huu katika eneo la Mwembe Shauri, Unguja na kesi nyengine kwenye visima vya maji.  Kadhalika, funiko za chuma za makaro kwenye maeneo ya miji zinachukuliwa na kuuzwa kama vyuma chakavu.   Mambo haya hayatoi taswira nzuri katika jamii yetu. Kwa hivyo, sote  tunapaswa tushirikiane ili tuweze kuvizuwia vitendo hivi  kwani, vina athari kubwa kwa ustawi wa maendeleo yetu.


Ndugu Wananchi,
Wakati huu tunaposherehekea sikukuu hii ya Idd el Hajj tunaendelea na msimu wa mavuno ya karafuu katika mwaka 2014/2015 tuliouanza mwezi Julai, 2014. Hatuna budi tumshukuru Mwenyezi Mungu (SW) kwa kutujaalia neema hii kubwa.  Kadhalika, napenda kutoa shukurani za dhati kwa wakulima wote wa karafuu nchini kwa kuendelea kuziuza karafuu zao katika vituo vya Shirika letu la ZSTC.  Nimearifiwa kuwa hadi kufikia tarehe 2 Oktoba 2014 tani 1,347.65 za karafuu zenye thamani ya Tsh.Milioni 18,862.7  zimeshanunuliwa katika vituo vyetu vya ZSTC Unguja na Pemba.  Haya ni mafanikio ya kutia moyo.

Serikali imejiandaa vyema kuhakikisha kuwa karafuu zote zinanunuliwa pamoja na kuhakikisha kwamba wakulima wa karafuu wanapata vifaa vyote wanavyohitaji katika shughuli zao.  Aidha, kwa kushirikiana na vikosi vyetu vya ulinzi na usalama tutaendelea kupambana na magendo ya karafuu, ili faida inayopatikana kutokana na zao hili iendelee kuwanufaisha wakulima wetu na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Kwa kuzingatia hali halisi ya bei ya karafuu katika soko la dunia, Serikali haikuweza kupandisha bei ya karafuu kwa msimu huu wa mwaka 2014, lakini imefanya kila jitihada kuhakikisha kuwa bei inabakia kama ilivyokuwa katika msimu uliotangulia wa mwaka 2013/2014 ili kuwapa nguvu wakulima.  Siku ya tarehe 9 Julai, 2014 nilipozindua rasmi Msimu wa Karafuu wa mwaka 2014/2015 Serikali ilitangaza bei mpya ya karafuu kuwa kilo moja ya karafuu ya gredi ya kwanza kuwa ni TShs. 14,000 na gredi ya pili kuwa TShs. 12,000 na TShs. 10,000 kwa gredi ya tatu.  Nimearifiwa kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kwa wakulima katika kuutunza na kuimarisha ubora wa karafuu zetu, jambo hili limewawezesha wakulima kupata gredi ya kwanza kwa karafuu nyingi wanazoziuza na kuinua kipato chao.  Nawapongeza wakulima kwa kuwa na mwamko huu.

Kadhalika, nachukua fursa hii kwa mara nyengine, kuwataka wale wenye tabia ya kuanika karafuu kwenye barabara au kutumia njia mbaya za uanikaji na ukaushaji wa karafuu kuacha tabia hiyo, kwa kuwa ina athari kubwa katika kupata bei bora ya karafuu zetu katika soko la dunia ambalo hivi sasa limejaa ushindani mkubwa.

Katika jitihada za kulinda hadhi na sifa pekee za karafuu zetu, Serikali inakamilisha utekelezaji wa mpango wa kuzipa karafuu za Zanzibar utambulisho maalum (Branding).

Vile vile, Serikali inaendelea kutekeleza ahadi ya kuimarisha miundombinu ya barabara katika maeneo ambayo wakulima wanapata usumbufu kuyafikia mashamba yao ya mikarafuu.  Serikali tayari imeshatekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara ya Kuyuni – Ngomeni kwa kiwango cha kifusi yenye urefu wa kilomita 3.1.  Ujenzi wa barabara hii umegharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mfuko wa Barabara.  Hivi sasa tunakamilisha mipango ya kuanza ujenzi wa barabara ya Kipapo-Mgelema pamoja na barabara ya Mgagadu – Kwa Utao.  Lengo la Serikali ni kuzijenga barabara hizi kwa kiwango cha lami hapo baadae tutakapopata uwezo. Kumalizika kwa barabara hizo kutarahisisha vile vile utekelezaji wa shughuli nyengine za maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Jitihada za Serikali za kurudisha hadhi ya zao la karafuu zimesaidia sana katika kuinua hali za maisha ya wakulima katika sehemu mbali mbali hasa hapa Pemba. Zao la karafuu limechangia sana kuimarisha mzunguko wa fedha ambao umekuwa ukisaidia sana  kuimarisha biashara  na shughuli mbali mbali za kiuchumi.

Kwa mara nyengine tena, napenda kuwanasihi wakulima wetu wa karafuu waendelee na jitihada zao za kutumia huduma za benki kwa kuhifadhia fedha zao na kujiwekea akiba.  Uamuzi wao huo ni uamuzi wa kimaendeleo.  Wale ambao bado hawajachukua hatua, ni busara wakafanya uamuzi huo hivi sasa.

Ndugu Wananchi,
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya mvua ambayo tumeanza kuipata katika maeneo mbali mbali nchini.  Ni vyema tukaitumia neema hii anayoendelea kuturuzuku Mola wetu katika kuimarisha shughuli zetu za kilimo.  Tuzitumie mvua hizi kwa kupanda kwa wingi miti ya matunda, mboga mboga, mimea ya vyakula vya mizizi na miti ya misitu na biashara.



Aidha, tuutumie wakati huu kwa kuendeleza kilimo cha mikarafuu kwa kuyashughulikia ipasavyo mashamba yetu. Nimeelezwa kuwa idadi ya miche ya mikarafuu 686,854 itatolewa kwa wakulima katika msimu wa mvua za Masika wa mwaka 2014/2015,  ambapo miche 499,354 iliyoatikwa kwenye vitalu vya Serikali na miche 187,500 iliyoatikwa kwenye vitalu vya watu binafsi.  Natoa wito kwa wakulima wayatayarishe vyema mashamba yao kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu wa kilimo na misitu, ili juhudi zetu ziweze kuwa na tija zaidi. Tusiusahau msemo mashuhuri wa walimu wetu kwamba “Jitihada ndiyo ufunguo wa mafanikio”. Kwa hivyo, tuzitumie fursa zote zilizopo ili kuliendeleza zao la karafuu ambalo ni tegemeo kubwa kwa uchumi wetu.

Ndugu Wananchi,
Sote tunafahamu kwamba Hija ya mwaka huu kama zilivyokuwa Hija za miaka iliyopita, imekuja wakati dunia yetu ikiendelea kukumbwa na matatizo mbali mbali.  Matatizo hayo yanatokana na sababu mbali mbali za uwezo wa Mwenyezi Mungu na zikiwemo zinazosababishwa na binadamu.  Matukio ya vimbunga, matetemeko ya ardhi, kuripuka kwa volcano, mabadiliko ya tabianchi, na kadhalika, yameleta athari kubwa pamoja na kupoteza maisha ya watu mbali mbali na mali zao.  Aidha, yapo maafa mengine ya maradhi thakili yanayoendelea kuikumba dunia yakiwemo maradhi ya UKIMWI, Ebola na mengineyo. 

Nchi yetu inaendelea kukumbwa na maafa kadhaa zikiwemo ajali mbali mbali, hasa za barabarani, athari ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile maeneo ya kilimo kuvamiwa na maji ya bahari na visima vya asili vimeingia maji ya chumvi.  Jumla ya maeneo 145 yameathirika kwa kuingia maji ya chumvi.  Kati ya maeneo hayo, maeneo 123 yapo hapa Pemba. 

Tatizo jengine ni kupanda kwa kina cha maji ya bahari duniani kwa maeneo yaliyo chini ya mita tano kutoka usawa wa bahari.   Maeneo hayo yapo kwenye hatari ya kuathirika zaidi kutokana na hali hiyo.  Kwa upande wa Pemba maeneo ya aina hii yana ukubwa wa mita za mraba 286 na yanakaliwa na asilimia 54 ya watu na kwa Unguja yana ukubwa wa mita za mraba 328 na yanakaliwa na asilimia 29 ya watu.  Kadhalika, tunashuhudia namna misimu ya mvua inavyobadilika.  Baadhi ya wakati mvua zinachelewa kunyesha na zinapokuja kiwango chake hupungua au hunyesha kwa kiwango kikubwa sana.  Upepo unaovuma nao hautabiriki.  Pepo za Kusi na Kaskazi, nazo huvuma tafauti na viwango vilivyozoweleka miaka ya nyuma.

Matatizo ya uchafuzi wa mazingira mengine tunayasababisha sisi wenyewe.  Suala la utupaji taka ovyo, bidhaa chakavu za kemikali na mifuko ya plastiki pamoja na uchimbaji wa mchanga na mawe madhara yake ni makubwa na lazima tuhakikishe kwamba sheria inasimamiwa vizuri.  Aidha, hatuna budi tuendelee kuchukua hatua madhubuti kwa mujibu wa sheria kuzuia ujenzi kwenye vyanzo vya maji na kwenye mabonde yaliyotengwa kwa shughuli za kilimo.

Ndugu Wananchi,
Wapo wananchi, walioathirika na kukabiliwa na shida na matatizo mbali mbali kutokana na maafa yaliyotokea.  Serikali zetu mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa na Washirika wetu wa Maendeleo, zinafanya kila jitihada ya kutekeleza mipango yetu na ya Kimataifa katika kukabiliana na maafa.  Masuala ya mazingira na tabianchi na yale yote yanayosababisha maafa na majanga katika nchi yetu, yanatekelezwa kwa kuzingatia sera na mipango iliyokwishaandaliwa.  Hata hivyo, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote hayo ambayo ni mitihani yake kwetu.  Ni wajibu wetu tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu katika sala zetu ili atulinde na atuepushe na maafa mbali mbali.

Kadhalika, tunapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu atusamehe makosa yetu mbali mbali, ambayo inawezekana mengine yalisababisha baadhi ya maafa,  kama vile uharibifu wa mazingira na kadhalika.  Tuendelee kumcha na kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dhati ya imani ya dini yetu kwa kufuata na kuzitekeleza amri zake na mafundisho ya dini tukiwa waumini wa kweli.


Ndugu Wananchi,
Pamoja na kwamba sherehe za leo zinadhihirisha furaha yetu baada ya kukamilika kwa ibada ya Hija, tusisahau kuwa bado maafa yanaweza kutokea wakati wowote na kuikumba jamii yetu.  Hali hio inapotokea, sote tunawajibu wa kutoa mchango wetu ikiwa ni pamoja na kuomba dua, ili kukabiliana na hali hio.  Kwani dua ndio silaha ya Muumini kama alivyosema Bwana Mtume (SAW).

Kwa hivyo, leo ni fursa nzima ya kujiuliza na kujikumbusha sababu zinazopelekea jamii yetu kukumbwa na mitihani ya Mwenyezi Mungu (SW).  Tunafahamu kuwa zipo sababu nyingi zinazofanya mitihani hio itokee na kuikumba jamii yetu.

Imani ya dini inatueleza kwamba binadamu anapofanya maovu na kusahau mafundisho ya dini, kwa hakika anakosa radhi za Mola wake.  Sote tunashuhudia kwamba katika jamii yetu siku hizi; vitendo viovu vimekithiri kwa kiasi kikubwa.  Baadhi ya vitendo hivyo, ni pamoja na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani, mauaji, ubakaji, udhalilishaji wa wanawake na watoto, ujambazi, ulevi, rushwa, dhulma, uhasama na chuki zisizokuwa na msingi, na kadhalika.  Kwa hivyo, sote tunakabiliwa na jukumu la kupambana na maovu hayo kwa nguvu zetu zote, ili tuweze kuinusuru jamii yetu na vitendo vinavyotokea kinyume cha maadili yetu.

Ndugu Wananchi,
Jukumu kubwa liko kwetu  na kwa viongozi wetu mbali mbali; la kutuhimiza waumini na wananchi, ili tuyawache mambo maovu ambayo ni ya kishetani.  Viongozi waendelee daima kukemea maovu katika jamii na kuwahimiza wananchi kuendelea kupendana na kuwasaidia wale wanaostahili misaada, hasa mayatima, walemavu, wazee, maskini na wengine wote wasiojiweza.

Ndugu Wananchi,
Napenda nisisitize kwa mara nyengine tena kuhusu suala la kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.  Nchi yetu imefikia kuwa nchi ya amani kutokana na misingi ya uongozi bora iliyowekwa na viongozi wa awamu zote zilizopita za nchi yetu na uwezo wake Mwenyezi Mungu.  Kila mmoja wetu ana wajibu wa kufurahia baraka alizotupa Mwenyezi Mungu na kufanya kila jitihada ili tuilinde hali hio ya neema na kheri.  Ni lazima tuhakikishe kwamba hapana hata mmoja atakayekuwa ni chanzo cha kuvurugika kwa amani katika nchi yetu, kwa visingizio vya harakati za kidini, kisiasa na nyengine zo zote zile.  Tuiendeleze sifa ya nchi yetu kuwa ni nchi ya amani kwa kujiepusha na mifarakano na mizozo isiyokuwa na faida yoyote.

Wito wangu ni kwamba ubinafsi usiingie na kupewa nafasi katika masuala yanayohusu jamii, hasa mambo ya siasa na dini.  Wale wote wanaofanya hivyo, watambue kuwa wanafanya makosa kwa kufikiri kwamba wana uwezo zaidi kuliko wengine wa kuondosha matatizo katika jamii kwa kutumia nguvu zao.  Ni vyema tukaelimishana juu ya mema na mabaya kwa busara, badala ya kiburi na dharau.

Tuendelee kujenga imani yetu na kumuabudu Mwenyezi Mungu hadi mwisho wa uwezo wetu, bila ya kuchoka au kutosheka; ili atukubalie sala na dua za kuitakia nchi yetu iendelee kuwa na amani, umoja, mshikamano na maendeleo.

Tusisahau kamwe kwamba amani na umoja ni misingi ya uhai wa nchi yetu.  Waumini na wananchi kwa jumla; hatuna budi kuepuka kushabikia mambo yanayokwenda kinyume na maadili mema.  Kwa hivyo, waumini na wananchi wote ni lazima tufanye bidii ya kuendeleza na kuimarisha amani, kwani kwa namna hio tutaendelea kujenga mazingira mazuri yanayofaa kwa waumini kuendelea kufanya ibada na kumcha Mwenyezi Mungu na wananchi sote kujiletea maendeleo yetu.  Kwa hivyo, hakuna mbadala katika suala la wa amani.  Serikali zetu mbili zitasimamia hali ya amani na utulivu kwa uwezo wetu wote.

Ndugu Wananchi,
Sikukuu ni furaha lakini kila sikukuu huwa na sababu zake kama hii ya leo. Kwa hivyo, tuitumie sikukuu yetu hii kwa kufanya mambo mema yenye mnasaba wa kuonesha furaha na shukurani zetu kwa Mwenyezi Mungu (SW) kwa kutujaalia kuifikia siku hii. Miongoni mwa mambo mema ya kuyatekeleza ni lile la kuchinja mnyama kwa matumizi ya familia zetu na kuwapa sehemu ya mnyama marafiki zetu, mayatima na wenzetu wengine.

Imepokelewa kutoka kwa Abu Rafii (RA) kwamba Bwana Mtume (S.A.W) alikua akichinja kondoo wawili; mmoja kwa ajili yake na familia yake na mwengine kwa ajili ya umma wake. Mambo mengine ya kheri baada ya kusali sala ya Iddi katika siku hii ni kula na kunywa vitu vizuri vya halali, kuvaa vizuri kama tunavyoonekana hapa pamoja na kutembeleana, kupeana zawadi, kuwakagua wagonjwa na kuombeana dua. Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa wafuasi wazuri wa mafundisho na sunna za Mtume wetu (S.A.W) ili tuweze kufanikiwa hapa duniani na kesho akhera.

Napenda kuwanasihi wazazi wenzangu tuendelee kusimamia malezi ya vijana wetu ili nao waige maadili mema na mafundisho ya dini kwa kuziepuka tabia mbaya  zisizoendana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu, utamaduni, silka na malezi ya jamii yetu. Tuwasimamie mavazi yao ili tuone kuwa wanavaa mavazi ya stara yaliyo muruwa na wanapokwenda kwenye viwanja vya sikukuu hawajisahau na wanarudi nyumbani mapema na wanayafikia malengo ya sikukuu zetu.

Ndugu Wananchi,
Kama kawaida yangu, nataka nizungumzie umuhimu wa matumizi mazuri ya barabara zetu kwa kuepusha ajali zisizo za lazima hasa katika nyakati hizi za sikukuu.  Sheria za usalama barabarani zimekuwa zikivunjwa kwa kupakia abiria na watoto zaidi ya wale wanaokubalika kisheria. Baadhi ya madereva huendesha gari zao kwa mwendo wa kasi, alama za usalama barabarani wanazipuuza na kusababisha ajali ambazo zingeweza kuepukwa iwapo wangekuwa waangalifu.

Taarifa kutoka katika Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuanzia mwezi wa Januari hadi Agosti mwaka huu wa 2014 kumeripotiwa ajali za barabarani 314 zilizohusisha magari na kusababisha vifo vya watu 53 na majeruhi 377. Matukio yaliyohusisha waendesha vyombo vya moto vya maringi mawili katika kipindi hicho ni 112 na kusababisha vifo vya watu 25 na majeruhi 161.

Katika hali kama hii, lazima Jeshi la Polisi liweke mikakati ya kukabiliana nayo na kushirikiana na taasisi zinazowasimamia madereva na ukaguzi wa vyombo vyao ili kuhakikisha kuwa madereva wanaokiuka sheria na vyombo vya usafiri wa barabarani ambavyo ni vibovu, na haviwi vyanzo vya ajali za barabarani. Wananchi wengi wananung’unika juu ya mwenendo mbaya wa madereva wa magari makubwa yanayobeba mchanga kwa kukosa hadhari barabarani, Unguja na Pemba. Naziagiza taasisi zote zinazohusika kuyafanyia kazi manung’uniko haya ya wananchi na wawachukulie hatua kali za kisheria madereva watakaobainika kuvunja sheria kwa sababu ya ukubwa wa vyombo wanavyoviendesha. Hatuwezi  kuwaruhusu madereva wasiojali utu kuendelea kukiuka sheria na kusababisha ajali.

Kadhalika, wananchi waendelee kuelimishwa juu ya masuala ya usalama barabarani na matumizi mazuri ya barabara, ili uzuri wa barabara zetu tunazoendelea kuzijenga ulete faraja kwa wananchi badala ya kusababisha madhara ya kupata ulemavu au kupoteza maisha.

Ndugu Wananchi,
Namalizia hotuba yangu kwa kutoa pongezi na shukurani zangu kwa Kamati ya maandalizi ya sherehe hizi kwa kazi nzuri ambayo sote tumeridhika nayo. Natoa shukurani kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana vyema na viongozi mbali mbali wakiwemo Maafisa Wadhamini wote katika kila hatua. Ni dhahiri kuwa kufanikiwa kwa sherehe zetu za leo kumetokana na michango ya kila mmoja wenu. Shukurani zangu za dhati kwa viongozi na wananchi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba pamoja na wananchi wote wa Pemba kwa mapokezi mazuri na mahudhurio makubwa katika sala ya Iddi leo asubuhi na kwenye Baraza hili la Idd-el-Hajj.

Kwa pamoja tuendelee kuwaombea dua Mahujaji wetu iwe Hijjah Mabrur  kwao  na Mwenyezi Mungu awarudishe nyumbani kwa salama. Mwenyezi Mungu (SW) atuzidishie amani, umoja na mshikamano ili tuweze kupiga hatua zaidi za maendeleo. Awape afya njema na subira wagonjwa wetu walioko majumbani na hospitalini.  Awarehemu wazee wetu na awasamehe makosa yao wote waliokwishatangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu atupe mvua zenye kheri na baraka na neema ya mazao. Atujaalie sote turudi nyumbani kwa salama na tusherehekee sikukuu hii kwa amani, furaha na utulivu.
         
Wassalamu  Aleikum Warahmatullah Wabarakatuhu
IDD MUBARAK, WAKULLU AAM WAANTUM BIKHEIR
Ahsanteni kwa kunisikiliza.


Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akimuika na Waumini wa Kiislam katika Viwanja vya Konde katika Sala la Eid Alhajj.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya kusalia Sala ya Eid Alhajj Konde Wilaya ya Micheweni Pemba, akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakari Khamis Bakari na 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharifu akiwasili viwanja Konde katika Sala ya Eid Alhajj. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuiya na Waumini wa Kiislam Kisiwani Pemba katika Sala ya Eid Alhajj iliofanyika katika uwanja wa Mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuiya na Waumini wa Kiislam Kisiwani Pemba katika Sala ya Eid Alhajj iliofanyika katika uwanja wa Mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.

Waumini wa Dini ya Kiislam kisiwani Pemba wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk, Ali Mohamed Shein, katika Sala Eid Alhajj wakiungana na Waumini wa Dini ya Kiislam Duniani kuadhimisha Eid Alhajj baada ya Ibaada ya Hijja kufanyika ikiwa ni moja ya Nguzo tano za Kiislam.  



Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Shein, akisalimiana na Wananchi waliohudhuria Sala ya Eid Alhajj katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Shein, akisalimiana na Wananchi waliohudhuria Sala ya Eid Alhajj katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba.

Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd. Yakabidhi nyama kwa Wazee Sebleni na Welezo na Watoto Yatima Kusherehekea Sikukuu ya Eid Alhajj

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Ndg. Seif Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la kugawa Nyama kwa Wazee Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo na Nyumba za Watoto yatima ili kuungana wa  Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Eid Alhajj inayoadhimishwa kwa Waislamu Wote duniani kwa Ibaada ya Hijja na kuchinja kwa mwenye uwezo.
Vijana wakiwa kazi klukamilisha kazi hiyo ya ugawaji wa nyama hiyo baada ya kuchinja

 Mtaalam wa Benjki ya Kiislam PBZ Islamic akizungumza n a Maofisa wa Pbz, katika Kijiji cha Kizimbani Unguja wakati wa zoezi hilo la uchinjaji lililofanyika kijiji hapo kwa ajili kutowa sadaka kwa Wazee wasiojiwe na Watoto yatima.PBZ hutowa moja ya faida yake kwa kusaidia jamii     

Kaimu Mkurugenzi wa PBZ Ndg. Seif Suleiman, akimkabidhi nyama Afisa Mdhamini wa Nyumba ya Wazee Sebleni kwa ajili hya Wazee wanaoishi nyumba hiyo kuungana n a Wanchi katika kusherehekea Sikukuu ya Eid Alhajj inayoadhimishwa na Waumini wa Kiislam Duniani makabidhiano hayo yamefanyika katika makaazi ya wazee hao sebleni

Wazee wanaoishi Nyumba ya Wazee Sebleni wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa PBZ Seif Suleiman, akikabidhi msaada huo kwa ajili ya kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam kusherehekea Sikukuu ya Eid Alhajj.










Dk. Shein Ahutubia Baraza la Eid Al Hajj Ukumbu wa Chuo cha Kiislam Kiuyu Pemba.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Kiislam Kiuyu kuhudhuria Baraza la Eid, Kitaifa limefanyika katika Wilaya ya Micheweni Pemba,  
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Kiislam Kiuyu micheweni Pemba kuhudhuria Baraza la Eid lililofanyika Kisiwanin Pemba  katika Wilaya ya Micheweni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Kiislam Kiuyu kwa msafara wa mapikipiki ya Polisi yakimshindikiza kuhutubia Baraza la Eid Alhajj Kitaifa limefanyika katika Wilaya ya Micheweni Pemba. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed.Shein, akipokrea Bwaride rasmin lililoandaliwa kwa ajili yake katika Baraza la Eid Al Hajj lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Kiislam Kiuyu Micheweni Pemba, Baraza la Eid Kitaifa mwaka huu limefanyika katika Wilaya ya Micheweni Pemba. 


Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Abubakary Khamis Bakar, akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kulihutubia Baraza la Eid katika ukumbi wa Chuo cha Kiislam Kiuyu Wilaya ya Micheweni Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Baraza la Eid Al Hajj, katika ukumbi wa Chuo cha Kiislam Kiuyu Micheweni Pemba na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serekali,
Wananchi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akilihutubia Baraza la Eid AlHajj katika ukumbi wa Chuo cha Kiislam Kiuyu Micheweni Pemba.
Kutoka kulia Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume, Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mama Mwanamwema Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Abubakary Khamis Bakar, wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar wakati akihutubia Baraza la Eid Al Hajj katika ukumbi wa chuo cha kiislam kiuyu micheweni Pemba,
    Waheshimiwa Mawaziri wakiwa katika ukumbi wa chuo cha kiislamu wakihudhuria Baraza la Eid.


Rais wac Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) akizungumza na Makamu wa Kwanza na wa Pili kulia Maalim Seif Sharif Hamad na kushoto Balozi Seif Ali Iddi wakibadilisha mawazo nje ya ukumbi wa baraza wakipata viburudishaji vilivyoandaliwa kwa wananchi waliohudhuria baraza la Eid Kiuyu Micheweni.  


Mchezaji wa Timu ya Zimamoto Atakosa mechi tatu za ligi Kuu Zanzibar.

$
0
0
Klabu ya Zimamoto inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Grand Malt Zanzibar imezidi kupata doa kufuatia mchezaji wake Ali Salum Bakar maarufu Kibata kufungiwa kutoshuka kiwanjani kwa michezo mitatu.

Kifungo hicho kimetolewa na Chama cha Soka ZFA kufuatia mwanandinga huyo kumpiga ngumi kiwanjani mchezaji wa timu ya Malindi Abdalla Said Hamad kitendo kilichosababisha kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

kwa mujibu wa kanuni ya kuendeshea ligi kuu ya soka Zanzibar kifungu cha 16 c "Mchezaji atakaetolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga au kupigana atakaa nje na kutocheza michezo mitatu(3) inayofuata ya klabu yake pamoja na kulipa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/)

Klabu hiyo ya Zimamoto tayari imeshapata aibu kutokana na rekodi za mchezaji huyo kwani kwenye pambano la ufunguzi wa ligi September 15, 2014 dhidi ya timu ya Chuoni pia alionyeshwa kadi nyekundu.

JK Awajulia hali Wakuu wa Mikoa ya Kilimanjaro, Simiyu na na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Waliolazwa Muhimbili

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Paschal Mabiti aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe. Dkt Henry Mwijarubi Nyamubi aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo. 


Magazetini Tz Bongo Leo

Uzinduzi wa Maonesho ya Stemp za Zamani na za Sasa katika Viwanja vya Forodhani Beit Ajaab.

$
0
0
 Meneja Mkaazi Zanzibar Shirika la Posta Tanzania Bi Mwanaisha Said, akitowa maelezo ya maana ya Stemp wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Stemp Zanzibar ikiwa ni kujumuika na Mashirika ya Posta Duniani huadhimisha kila mwaka 9-10-2014, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Jumba la Makumbosho ya Taifa Forodhani Beit Ajaab. Zanzibar.
 Wafanyakaazi wastaafu wa Shirika la Posta Tanzania wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Ndg. Tahir Abdalla Khamis, akizindua maonesho hayo uanayofanyika katika viwanja vya Beit Ajaab Forodhani Zanzibar yatakuwa kwa muda wa siku nne  
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Ndg. Tahir Abdulla Khamis, akikata utep[e kuashiria kuzinduwa maonesho hayo katika viwanja vya beit lajab forodhani. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Ndh. Tahir Abdullah Khamis, akihutubiwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya kuadhimisha Siku ya Stemp Duniani huadhimishwa kila mwaka October 9,ni Siku ya Stemp Duniani. 
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania Bi Khadija Said, akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Siku ya Stemp Duniani katika viwanja vya Jumba la Makumbusho Forodhani Zanzibar.,
Mkusanya Stemp Zanzibar Profesa Shariff akizungumzia  maana ya Stemp kwa niaba ya wakusanyaji wa Stemp Zanzibar ambae ameshirika wakati huo kukusanya Stemp za mataifa mbalimbali na kuchangia katika maonesho hayo ya stemp yanayofanyika katika viwanja vya jumba la makumbosho ya taifa forodhani Zanzibar.Akizungumzia Stemp ni utambulisho wa Nchi na kuitangaza katika sekta ya utalii duniani. 

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika viwanja vya maonesho wakifuatilia hafla hiyo.
Wafanyakazi Wastaaf wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika viwanja vya maonesho wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmin akihutubia wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya beit ajaab forodhani.


Afisa wa Shirika la Posta Tanzania Bi. Sharifa Rashid, akitowa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Tahir Abdullah Khamis,akiangalia stemp hizo 



 Wananchi wakiwa katika banda la maonesho ya Stemp za zamani na za sasa wakati wa maonesho hayo yanayofanyika forodhani Zanzibar
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Tahir Abdullah Khamis, akionesha moja ya stemp ya zamani baada ya kupata maelezo kutoka kwa Kaimu Msaidizi Meneja Bi.Hawa Daruwesh Chande,mwenye kilemba cheusi, 
 Wananchi waliofika katika maonesho hayo wakiangalia baadhi ya Stemp za Zamani wakati wa maonesho hayo huko forodhani.

Vikosi vya SMZ vyakamata Mafuta ya Magendo Kisiwani Pemba yakingizwa yakiingizwa kisiwani huo.

$
0
0

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Pemba, ambae pia ni Kamanda wa opreretion Karufuu Kanda ya Pemba, Msaidizi Kamishna wa Zimamoto Zanzibar , Iddi Khamis Juma , akitowa maelezo kwa Waandishi wa  Habari huko Bandarini Uchangani Wesha .

 Mapipa ya Mafuta ya Disel ambayo yalikuwa yanaingizwa kisiwani  Pemba kwa njia ya Magendo na kukamatwa na Vikosi vya SMZ, Vilivyoko Mkumbuu wakati vikiwa katika Doria ya Kawaida.katika maeneo hayo. 
Wapiganaji wa Kikosi cha Zimamoto Pemba, wakipeleka Tangi la Mafuta yaliokamatwa kwenye Boti , inayofanya Doria huko katika Bandari ya Uchangani Wesha.

Dk Jakaya Mrishio Awataka Mabalozi Msiingize Dini katika Siasa.

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi wa dini alipowasili katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam kufungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi wa dini alipowasili katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam kufungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi wa dini alipowasili katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam kufungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea machapisho toka kwa mwandaaji wa Mkutano wa viongozi wa dini chini ya taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na washiriki wa Mkutano wa  viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika pich ya pamoja na wafanyakazi wa hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam wanaowahudumia washiriki wa Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence. PICHA NA IKULU

Msiingize dini katika siasa, Rais awaambia mabalozi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na siasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.
Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”
Rais Kikwete alikuwa anazungumza usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, wakati wa chakula cha usiku ambacho alikula na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands ya Dar Es Salaam.
Mkutano huo wa siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka juzi, 2012 kwenye Hoteli hiyo hiyo.
Aidha, Mkutano huo ambao moja ya wadhamini wake ni taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na mashirika kadhaa ya kimataifa likiwemo lile la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, ... [Message clipped] View entire message Click here to Reply, Reply to all or Forward

Breeking Newss Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein Amteua Mwanasheria Mkuu Zanzibar.

$
0
0

Mhe Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya  Kifungu 55(1)cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.     

Katuni na Ujumbe wake Huooo,,,,,,,,,,,,,,,


Makamu wa Rais Dkt. Bilal Asaini Kitabu cha maombolezi ya Msiba wa Profesa Kivisa.

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Rogath Kivasi, wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Goigi jijini Dar es Salaam, leo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa ,marehemu Prof. Amelia Kivasi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Goigi jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waombolezaji  wakati akiondoka baada ya kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Professa Rogath Kivasi, Goigi jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2014. (Picha na OMR)

Watoto Wakifurahia Sikukuu ya Eid Al Hajj katika Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zenj.

Tiba ya mgonjwa mmoja wa Ebola Sh. 520m

$
0
0
Mwandishi wetu na mitandao
WAKATI Zanzibar ikichukua juhudi kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini kwa kuwapima abiria wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege na bandarini, imebainika tiba ya mgonjwa mmoja wa Ebola ni dola za Marekani 315,000 sawa na shilingi milioni 520.4.

Hata hivyo, hakuna dawa mahasusi wala chanjo ya ugonjwa huo hatari ambao tayari umeanza kuingia nchini Uganda baada ya mtu mmoja kufariki kwa kupatwa na virusi vya homa ya Marburg, ambavyo vinashabihiana kwa sehemu kubwa na Ebola.

Badala yake madaktari katika kliniki zinazowahudumia wagonjwa wa Ebola wanamsaidia mgonjwa kwa kumuongezea maji, kupunguza shinikizo la damu, kumuwekea mashine ya oxygen, kumuongezea damu na kutibu magonjwa mengine nyemelezi.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, umegundua gharama kubwa za kuwatibu wagonjwa wa Ebola na upungufu wa wataalamu ni miongoni mwa sababu zinazopelekea nchi za Afrika kushindwa kudhibiti ugonjwa huo.


Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, ugonjwa huo unaweza kudhoofisha uchumi wa Afrika kwa sababu ya gharama kubwa za kuwatibu wagonjwa.

Shirika hilo limewanukuu wanasayansi wakisema kuwa kuna hatari kubwa ya ugonjwa huo kusambaa katika mataifa ya magharibi hasa Uingereza na Ufaransa kutokana na safari nyingi za ndege zilizopo kati ya nchi hizo na mataifa yaliyoathiriwa na ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) halijazuia safari za ndege katika mataifa yaliyoathiriwa na ugonjwa huo badala yake imekuwa ikiyahamasisha mashirika ya ndege kuchukua tahadhari.


Mashirika ya Ndege ya Uingereza na Emirates, yamesimamisha safari zake katika nchi za Afrika Magharibi zenye visa vya Ebola.

TAMWA kuzindua ripoti kuhusu unywaji pombe, unyanyasaji

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) leo kitazindua  taarifa ya  utafiti kuhusu kiwango cha unywaji pombe na ukatili wa kijinsia.

Taarifa ya utafiti huo inaonesha  kiwango cha unywaji pombe, sababu zinazopelekea watu kunywa kupita kiasi, madhara, kiwango cha upatikanaji pombe, ufahamu kuhusu matumizi na uhusiano kati ya matumizi ya pombe na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Kinondoni.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya pombe na tabia ya kufanya vurugu, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu Tanzania (TDHS) ya mwaka 2010, matokeo yalionesha wanawake ambao waume zao ni walevi wako katika hatari ya kufikwa na ukatili wa kihisia, kimwili au kingono mara mbili zaidi ya wanawake ambao waume wao hawanywi pombe.


Uzinduzi wa utafiti huo ni sehemu ya mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokana na matumizi ya pombe dhidi ya wanawake na wasichana, unaofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya IOGT wenye lengo la kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na pombe ili kupambana na ukatili unaotokana na pombe.


Mradi wa IOGT una miaka mitatu ya mafanikio tangu umefanya kazi na TAMWA.

Watoto 81 wazaliwa mkesha wa sikukuu

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga
Jumla ya watoto 81 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Idd el Hajj katika hospitali ya Mnanzimmoja na Muembeladu.

Kati ya watoto hao, 61 wamezaliwa hospitali ya Mnazimmoja wakiwemo wanawake wakiwa 34, ambapo wawili walifariki dunia baada ya kuzaliwa wakati mama zao  wakiwa njia kuelekea hospitali kwa ajili ya  kujifungua.

Katika hospitali ya Muembeladu walozaliwa watoto 20 katika ya hao wanawake 8 na wanaume 12.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa hospitali ya Mnazimmoja, Hassan Makame, alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito wa juu ni kilo 3.5 na uzito wa chini ni kilo 2.

Alisema watoto hao wako salama na hawana matatizo yoyote ya kiafya na kwamba wameruhusiwa kurudi nyumbani.


Msaidizi Muuguzi Dhamana wa hospitali ya Muembeladu, Mgret Sylveter Tayari, alisema uzito wa watoto waliozaliwa hospitali hiyo ni baina ya kilo 4.2 na 3.

Akizitaja changamoto wanazokumbana nazo katika kuwahudumia mama wajawazito wakati wanapofika kituoni kujifungua ni pamoja na kuchelewa kufika hospitali wakisubiri waumwe na uchungu.

Aidha, alisema wengine wanatumia dawa za asili kuongeza uchungu hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao na watoto.


Aliitaka jamii kuhamasika kuvitumia vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Viewing all 35810 articles
Browse latest View live