Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35874 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amsimamisha kazi mkuu wa Uhamiaji na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia fedha

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

SUZA yatia saini mkataba wa mashirikiano na Chuo Kikuu cha Comoro

$
0
0





CHUO KIKUU CHA TAIFA (SUZA)
Sanduku la Posta 146, Zanzibar - Tanzania
Simu: + 255 24 2230724/2233337/2234063    Nukushi: + 255 24 2233337
Barua pepe: vc@suza.ac.tz                        Tovuti: http://www.suza.ac.tz




Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano juu ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro mjini Moroni katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 19 Januari, 2016  na kuhudhuriwa na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Komoro, Balozi wa Komoro nchini Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Bw Mudrik Ramadhan Soragha.

Makubaliano kati ya vyuo hivi ni moja ya matokeo ya ziara ya nchini Komoro ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya hivi karibuni.


Profesa Idris Rai, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Dkt Said Bourhani, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Komoro wakisaini Mkataba wa makubaliano ya mashirikiano baina ya vyuo vyao.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Profesa Idris Rai, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar aliwaeleza wahudhuriaji kwamba ametembea nchi nyingi duniani lakini Komoro ni nchi ya kwanza ambayo amekuwa akijisikia kama kwamba yuko nyumbani tokea alipoingia nchini humo. Alisema kwamba kuna uwiano mkubwa sana baina ya watu wa Zanzibar na watu wa visiwa vya Komoro katika kila nyanja za maisha.

Makamu Mkuu huyo wa SUZA aliwaeleza wana Chuo hao kwamba makubaliano baina ya vyuo hivyo viwili ni tofauti kabisa na mashirikiano ambayo SUZA imekuwa ikiweka saini na vyuo vingine mbali mbali kwani hayo yanahusisha vyuo vya nchi ndugu ambazo zinashabihiana kihistoria, kimazingira, kidini na kiutamaduni. Aliwahakikishia wanachuo waliohudhuria hafla hiyo kwamba SUZA kwa upande wake itahakikisha mashirikiano ya makubaliano yaliyofikiwa yanapewa kipaumbele na yanatekelezwa kama yatakavyopangwa.


Mkataba huo wa mashirikiano umeainisha mambo ya mashirikiano kama ifuatavyo:
-         kusaidiana kuendesha mafunzo ya lugha za Kiswahili na Kiingereza kwa upande wa Komoro na lugha ya Kifaransa katika ngazi ya Shahada kwa upande wa SUZA.
-         Kufanya tafiti za pamoja kwenye maeneo ya sayansi jamii na historia, tamaduni, lugha, dini kwa upande mmoja na masuala ya mazingira, rasilimali asilia na bahari kwa upande mwingine.
-         Kubadilishana walimu na wanafunzi baina ya SUZA na Chuo Kikuu cha Komoro.
-         Kusaidiana kujenga uwezo wa wanataaluma wa vyuo viwili hivi kwa maeneo ambayo Chuo kimoja kina uwezo zaidi.
-         Kuandaa mapendekezo ya kuazisha taasisi ya pamoja inayohusu masomo ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Komoro.

Ilibainika kwamba moja ya kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa mashirikiano haya kitakuwa ni lugha ambapo lugha kuu ya taaluma inayotumika katika Chuo Kikuu cha Komoro ni Kifaransa wakati lugha inayotumika SUZA ni Kiingereza na Kiswahili. Mafunzo ya lugha katika makubaliano haya yataweza kuondosha kikwazo hicho hivyo kuwawezesha wanafunzi na wafanyakazi wa vyuo hivi kutembeleana kwa masomo na kushirikiana katika kufanya tafiti za pamoja.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Komoro, Dkt Said Bourhani aliwaambia wanachuo wa Chuo Kikuu cha Komoro kwamba utekelezaji wa mashirikiano haya ni tofauti na mashirikiano na vyuo vingi kwani safari ya Tanzania, Zanzibar kutoka Moroni ni fupi na rahisi. Pia aliwashukuru marais wa Zanzibar na Komoro kwa kufikiria na kutaka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Chuo Kikuu cha Komoro kuanzisha mashirikiano haya.

Chuo Kikuu cha Komoro na SUZA ni vyuo vichanga lakini vimekuwa kwa kasi kubwa katika miaka ya karibuni. Wakati Chuo Kikuu cha Komoro kilianzishwa mwaka 2003 na kikiwa ni Chuo Kikuu pekee nchini Komoro kikiwa na wanafunzi karibu 9,500 katika masomo ya fani mbali mbali, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kilianzishwa mwaka 2001 na sasa kina wanafunzi karibu 4,000 waliojiunga na masomo kwenye karibu fani 40 katika ngazi za cheti hadi shahada ya uzamivu.

Mara tu baada ya ziara yake nchini Komoro, imekuwa ni hamu kubwa ya Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuona Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinashirikiana kwa karibu sana na Chuo Kikuu cha Komoro.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli Aonesha Umahiri wake wa Kushona

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

Tigo Wapata Ugeni wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard.

$
0
0


Mkurungezi  mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez akizungumza na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Harvard, Marekani waliopo nchini kwa ziara ya kimasomo na walitembelea leo makao makuu ya Tigo Kijitonyama kupata taarifa za uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Tigo katika sekta ya mawasiliano.
Mkurungezi  Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi toka chuo kikuu cha Harvard cha Marekani waliopo nchini kwa ziara ya kimasomo na walitembelea leo makao makuu ya Tigo Kijitonyama kupata taarifa uwekezaji uliofanywa na kampuni ya Tigo katika sekta ya mawasiliano.

Ligi Kuu ya Zanzibar JKU na Kijichi Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya JKU Imeshinda 2---1

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Kijichi na JKU wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2--1
Mshambuliaji wea timu ya Kijichi akimpita beki wa timu ya JKU wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya Kijichi akimpita beki wa timu ya JKU.
Mshambuliaji wa timu ya Kijichi akiwatoka mabeki wa timu ya JKU. 
Mchezaji wa timu ya Kijichi akiwa chini huku beki wa timu ya JKU akiokoa mpira huo.
Mshambuliaji wa timu ya Kijichi akipiga mpira golini kwa timu ya JKU huku kipa wa JKU akijiandaa kuokoa mpira huo. 

Kipa wa Timu ya JKU akiondoa mpira golini kwake huku mshambuliaji wa timu ya Kijichi akijiandaa kuchukua mpira huo.





UBA Tanzania Trains IFM (INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT) Students on Customer Service Management.

$
0
0
uba 1
Service Quality Manager, Queen Odunga during the training session at IFM (Institute of Finance Management).
Saturday, 16 January 2016 UBA trained IFM students on customer service management. Taking on the session was the Service Quality Manager, Queen Odunga, who explained how to handle a difficult customer. And after the session, the students tried to create a situation where the customer is complaining and doesn’t want to listen to the CSO. This came out so well as the one who was acting as CSO resolved the situation and the one acting as the client was happy that his problem was solved.
One happy student commended the UBA Team for taking them through the session “This has been a great session that we cannot easily get from our daily lectures. We thank UBA team especially Madam Queen who has highlighted on the importance and tactics of how to handle a difficult customer”, She concluded.
Queen Odunga the Service Quality Manager thanked the IFM Management for giving UBA the platform to share the knowledge on Customer service. She also applauded the students being attentive. “I would like to thank the IFM Management for providing UBA Tanzania with this platform and I would also like to thank the students for attending in numbers and being attentive throughout the session, it was quite interactive”. She continued by advising the students to take heed of the knowledge they have achieved in this session as “customer service is very vital for any business as it leads to customer retention and business development”.
Other UBA team members present at the session were also able to interact with the students giving them advise on the dos and don’ts in the finance and banking industry at large.
uba 2
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 3
A student ask a question during the training session with UBA Team on customer service management.
uba 4
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 5
Some of the students present at the training.

Wageni Watembelea Mji Mkongwe wa Zenj.

Ligi Kuu ya Zanzibar Jangombe Boys na Mafunzo Uliofanyika jana Usiku Uwanja wa Amaan.Timu hizo zimetoka sare ya 1--1

$
0
0
Mchezaji wa timu ya Kijichi na Mafunzo wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa kiporo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika jana usiku uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Mshambuliaji wa timu ya Jangombe Boys akimpita beki wa timu ya Mafunzo wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Mchezaji wa timu ya Jangombe Boys akimiliki mpira huku beki wa timu ya Mafunzo akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wao huo uliofanyika uwanja wa Amaan jana usiku. 
Wachezaji wa timu ya Jangombe Boys na Mafunzo wakiwania mpira.
Wachezaji wa timu ya Mafunzo wakimzonga muamuzi wa mchezo huo baada ya kutoa kadi ya njano kwa mchezaji wao kwa kitendo cha utovu wa nidhamu wakati akishangilia bao la kuzawazisha kwa kutowa sehemu yake ya siri kwa mashabiki wa jukwaa la urusi.
Mchezaji wa timu ya Jangombe Boys akimpita beki wa timu ya Mafunzligi wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika jana usiku uwanja wa amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1. 






Magazetini Tz Bongo

Wizara ya Maji na Umwagiliaji Yapokea Maoni ya Wadau wa Maji katika Mji Mdogo wa Himo.

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao cha wadau wa maji cha kupokea maoni kilichofanyika ukumbi wa KKT -Himo.
Mkurugenzi mkuuu wa MUWSA,Joyce Msiru akizungumza jambo na DC Makunga pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa mamlaka za maji mijini,Mhandisi Amani Mafuru na Mwanasheria mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji Saimoni Nkanyemka.
Mkurugenzi wa MUWSA,Joyce Msiru akimuongoza Mkuu wa wilaya ya Moshi na wageni wengine kutoka wizara ya maji kuingia ukumbini.
Mwenyekitiwa Bodi ya wakurugenzi MUWSA,Sharry Raymond (MB) (Katikati) akiwa na Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein Jamal (Kulia) pamoja na Afisa mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo,William Mseo (Kushoto).
Baadhi ya Viongozi kutoka Menejimenti ya MUWSA pamoja na wawakilishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa mji mdogo wa Himo na Madiwani wakiwa na mwanasheria wa Wizara ya maji na Umwagiliaji.
Afisa mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo,William Mseoakizungumza wakati wa utambulisho wa wageni katika kikao hicho.
Baadhi ya wananchi na wajumbe wa mji mdogo wa Himo wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na uSAFI WA mazingira mjini Moshi ,MUWSA,Joyce Msiru akizungumza katika kikao hicho wakati anawasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa Mamlaka hiyo katika mji wa Himo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Sharry Raymond akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya wananchi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akichangia jambo katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa KKKT Himo. NaDixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao cha wadau wa maji cha kupokea maoni kilichofanyika ukumbi wa KKT -Himo.
Mkurugenzi mkuuu wa MUWSA,Joyce Msiru akizungumza jambo na DC Makunga pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa mamlaka za maji mijini,Mhandisi Amani Mafuru na Mwanasheria mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji Saimoni Nkanyemka.
Mkurugenzi wa MUWSA,Joyce Msiru akimuongoza Mkuu wa wilaya ya Moshi na wageni wengine kutoka wizara ya maji kuingia ukumbini.
Mwenyekitiwa Bodi ya wakurugenzi MUWSA,Sharry Raymond (MB) (Katikati) akiwa na Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein Jamal (Kulia) pamoja na Afisa mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo,William Mseo (Kushoto).
Baadhi ya Viongozi kutoka Menejimenti ya MUWSA pamoja na wawakilishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa mji mdogo wa Himo na Madiwani wakiwa na mwanasheria wa Wizara ya maji na Umwagiliaji.
Afisa mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Himo,William Mseoakizungumza wakati wa utambulisho wa wageni katika kikao hicho.
Baadhi ya wananchi na wajumbe wa mji mdogo wa Himo wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na uSAFI WA mazingira mjini Moshi ,MUWSA,Joyce Msiru akizungumza katika kikao hicho wakati anawasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa Mamlaka hiyo katika mji wa Himo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Sharry Raymond akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya wananchi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akichangia jambo katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa KKKT Himo. NaDixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
.

Katuni na Ujumbe Wake Huuooo.......

DC Kinondoni Kuongoza Upimaji wa Magongwa ya Moyo Bure Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam Kesho Kutwa January 23,2016

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa mwito kwa wananchi hasa wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupimwa maradhi ya moyo bure katiza zoezi litakalofanywa na madaktari kutoka taasisi hiyo litakalofanyika viwanja vya leaders kesho kutwa January 23, 2015. Kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Meneja wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga (kushoto), akimuelekeza jambo DC Makonda. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Dk.Peter Kisenge.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

 Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kesho kutwa anatarajia kuongoza wananchi wa wilaya yake na wakazi wengine wa jiji la Dar es Salaam katika upimaji wa magonjwa ya moyo utakaofanywa bure na madaktari kutoka Taasisi  ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),  katika viwanja vya Leaders Club. 

Upimaji huo utatoa fursa ya kubaini wagonjwa wa wilaya hiyo kwa kuwa wananchi wengi hawajui magonjwa ya moyo yanaweza pia kusababishwa na shinikizo la damu na ni chanzo kikubwa cha   magonjwa ya macho,upungufu wa nguvu za kiume, kiharusi, figo na kutokuzaa.


 
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi alisema kutokana na umuhimu wa wananchi kujua afya zao na kupatiwa matibabu mapema kesho wataungana na Makonda katika kuwapatia vipimo wakazi wa kinondoni.
 
Alisema ugonjwa wa moyo ni hatari na asilimia kubwa ya wagonjwa hao wanatembea na kufanya kazi zao kwakuwa ugonjwa huo hauna dalili hivyo haja ya kila mmoja kupima na kujua afya yake ni muhimu.
 
“Pia wengi wanaougua shinikizo la damu hawajua wanaweza kuwa na magonjwa ya moyo na  kujikuta wakisababisha kuua figo,macho,nguvu za kiume,kuugua kiharusi na kukosa watoto upimaji huu ni hatua nzuri kwa wananchi wa kinondoni hivyo tumeridhia kuwapima na kuwapatia matibabu bure,”alisema.
 
Alisema taasisi hiyo itakuwa kamili katika kila sekta kesho kutwa viwanja vya Leaders Club ili wananchi wenye magonjwa yanayoshabihiana na moyo waweze kupewa tiba katika hospitali za wilaya hiyo ikiwemo Mwananyamala na wale walioathirika na ugonjwa wa moyo waweze kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Profesa Janabi alisema pia watahakikisha madaktari wa ushauri wanatoa elimu ipasavyo juu ya kuepuka ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu ambao hauna tiba na jinsi ya kuzingatia lishe.
 
“Ni muhimu kujua ongezeko la matumizi ya vyakula vya wanga kwa wingi pia ni hatari katika kuongeza uzito hivyo kusababisha shinikizo la damu,”alisema
 
Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi kuelewa kuwa ugonjwa wa moyo ni hatari na matibabu yake ni gharama hasa kwa wale wanaosafirishwa nje ya nchi hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo kesho.
 
Alisema serikali imeona haja ya kuboresha afya za wananchi ili kukuza uchumi na hatua hiyo ya kusaidia upimaji wa bure itapunguza hatari ya ugonjwa huo kwa watu wengi wanaopoteza maisha kila siku.

Mkutano wa Wadau wa Traffic Plan ya Mji Mkongwe wa Unguja. Kuzuiya Uingiaji wa Magari Stone Town.

$
0
0



Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Bi Mwanaidi Saleh akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa mkutano huo wa Wadau wa Mji Mkongwe Zanzibar. 
Waziri wa Ardhi Makaazi na Maji Nishati akifungua mkutano wa Wadau wav Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kuzungumzia kupunguza uingiaji wa magari katika mji mkongwe ambao kila siku huiingia magari 17500 kila siku.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Sariboko Makarani akiwasilisha ripoti ya Utafiti wa Uhifadhi wa Mji Mkongwe ili kuweza kuuhifadhi kimataifa ili kuweza kupunguza uingiaji wa magari na kueleza kila siku katika Mji Mkongwe huingia magari 17500.kila siku.

Wajumbe wa Mkutano wa Wadau wa Uhifadhi Mji Mkongwe wa Zanzibar wakifuatilia ripoti wakati ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Masmlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar Saliboko Makarani. 
Wajumbe wa Mkutano wa Wadau wea Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar wakati wakipitia Trafic Plan ya Mji Mkongwe kuweza kuhifadhi na kuzuiya uingiaji wa magari.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bandari Abdalla Juma akichangia wakati wa mkutano huo wa Wadau wa Mjini Mkongwe katika uhifadhi wake kupunguza uingiaji wa magari katika mji mkongwe. 
Mjumbe wa Bodi ya Mji Mkongwe Mhe Simai Mohammed Said akichangia wakati wa mkutano huo wa Wadau wa Mjini Mkongwe Zanzibar.
Mdau kutoka Kameshine ya Utalii Zanzibar Saleh Ferouz akichangia wakati wa Mkutano huo wa Wadau wa kudhibiti uingiaji wa magari katika mji Mkongwe wa Zanzibar.
Wadau wa Traficc Plan ya Mji Mkongwe kuzuiya uingiaji wa magari katika mji mkongwe ili kuweza kuuhifadhi. 
Mdau kutoka Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu akichangia wakati swa Mkutano huo wa kudhibiti uingiaji wa Magari katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Balozi Seif Aongoza Kikao cha Kamati ya Maafa Zanzibar.

$
0
0
Kikao cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar chakutana chini ya mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwa Vuga Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akikiongoza Kikao cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wake kulia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad  aliyesimama akitoa Muhtasari wa Sheria ya Kamisheni hiyo kwenye Kikao cha kwanza Wajumbe wa Kamaisheni hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Moh’d  Khamis Ngwali akitoa ufafanuzi wa muelekeo wa mvuza zinazonyesha  za mwezi januari na febuari 2016 kwenye kikao cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR.
Kikao cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar kimeanza rasmi ambapo Wajumbe  wa Kamisheni hiyo wamekutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Kufutwa  kwa Sheria nambari 2 ya mwaka 2003 na kuanzishwa kwa sheria nambari 1 ya mwaka 2015 ya kukabiliana na maafa Zanzibar ndio iliyotoa mamlaka kwa kamisheni hiyo kutekela majukumu yake hapa Nchini.

Akiwasilisha Muhtasari wa sheria ya kukabiliana na maafa Zanzibar kwenye Kikao hicho, Mkurugenzi  Mtendaji wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad alisema mabadiliko ya sheria hiyo yamekuja kutokana na mapunugu kadhaa yaliyokuwa yakikwamisha utekelezaji wa shughuli za kujikinga na kukabiliana na maafa hapa Zanzibar.

Nd. Juma alisema kukosekana kwa muundo wa usimamizi, mfumo madhubuti wa utoaji wa Taarifa, ushiriki wa sekta binafsi pamoja na mbinu za kujiandaa, kujikinga na kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa ni  baadhi ya masuala  yaliyokuwa yakileta usumbufu katika kipindi kilichopita nyuma.

Alisema kwa mujibu wa sheria nambari 1 ya mwaka 2015, Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa itakuwa ni chombo cha juu kitakachotoa maamuzi yanayohusu masuala ya kukabiliana na maafa Zanzibar.

Alifahamisha kwamba  katika kukabiliana na maafa , kifungu cha 6 cha sheria hiyo kinaipa uwezo Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa kumshtaki mtu ye yote ambae atakataa kutoa au kupokea huduma wakati wa dharura au maafa.

“ Kwa kushirikiana na Taasisi zinazohusika, kufanya ukaguzi kwa mtu ye yote, jengo, eneo au chombo kwa lengo la kukinga, kupunguza na kukabiliana na maafa na hali za dharura ”. Alisisitiza Nd. Juma.

Akitoa ufafanuzi wa Taarifa ya muelekeo wa Mvua mkubwa kwa mwezi wa Januari na Febuari  mwaka  2016  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya  Zanzibar  Nd. Moh’d  Khamis Ngwali alisema changamoto za mvua zinazonyesha ni kiashirio kinachoweza kusababisha Mvua za Alninyo.

Nd. Ngwali alisema kwa mujibu wa miongo ya mvua miezi ya Januari na Febuari ni misimu ya vimbunga ambavyo vinaweza kuleta athari wakati wowote na mamlaka hulazimika kutoa tahadhari  pale mvua inapoendelea kunyesha wakati ikipindukia zaidi ya milimita arubaini.

Alisema  baadhi ya wakati mvua zinazoripotiwa kunyesha hapa Zanzibar  hufikia hadi milimita 83.5 kiwango kinachosababisha kutokea mafuriko na hatimae kuleta maafa hasa katika maeneo ya mabonde.

Naye Waziri wa Fedha Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee  alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshaandaa mfuko maalum wa Miundo mbinu        { Infrustructure Fund } ambao huchangiwa  na Kila Mgeni anayeingia Nchini  kwa Dola Moja ya Kimarekani.

Mh. Omar alisema matarajio ya makusanyo ya mkufo huo imekadiriwa kufikia shilingi Bilioni 25 ambapo asilimia 25% ya makusanyo hayo yamelengwa kwa Mifuko saba  iliyosajiliwa akatolea mfano kama ile ya Maafa pamoja na  ukimwi.

Wakichangia katika Mkutano huo  baadhi ya wajumbe wa Kikao walisema bado ipo haja ya kuandaliwa njia mbadala kwa watu wanaoishi katika maeneo hatarishi itakayokuwa ya kudumu katika kudhibiti maafa wakati yanapotokea.

Walisema mipango ya muda mrefu na mfupi inahitajika kufanywa licha ya juhudi kubwa inayochukuliwa na Serikali Kuu katika uchimbaji wa mitaro katika baadhi ya maeneo  kwa kudhibiti maji yanayotuwama pamoja na wale  waathirika kuhifadhiwa kwenye majengo ya Skuli.

Kuhusu Kikosi cha Zima moto na Uokozi  Zanzibar  Wajumbe hao waliiomba Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi za Kitaifa na Kimataifa kukijengea uwezo zaidi wa Vifaa Kikosi hicho ili kiwe na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Walisema yapo mapungufu mengi ya ufinyu wa vifaa vinavyoweza kukisaidia kikosi hicho katika kukabiliana na maafa hasa yale ya moto kwenye baadhi ya maeneo kama  Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Akitoa nasaha zake Mwenyekiti wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Umoja wa Mataifa tayari umeshatoa onyo la kuziasa Nchi wanachama kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi wakati wowote yanapotokea.

Balozi Seif alisema  utafiti wa Wataalamu wa Umoja huo umethibitisha na kutoa tahadhari kwamba zipo nchi nchi zenye uwezekano wa kukumbwa na vimbunga ikiwemo Tanzania kutokana na mabadiliko makubwa ya mzunguuko wa hali ya hewa Duniani.

Kikao hicho cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar kilijumuisha wajumbe  mbali mbali wakiwemo Mawaziri, wakuu wa Mikoa na Vikosi vya ulinzi pamoja na watendaji wa taasisi zinazohusiana na maafa hapa Nchini.

Mwili wa Marehemu Asha Bakari Wawasili Zanzibar kwa Mazishi Kesho Saa nne Jangombe

$
0
0
Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea matibabuni Nchini India.Mareheme anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi kesho saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni
Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja huo leo jioni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar leo jioni tayari kwa mazishi kesho katika kijiji cha kiyanga. 

Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu leo jioni 



Wananchi wakishiriki katika kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea Nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kaka wa marehemu kwa ajili ya matayarisho ya mazishi kesho katika mtaa wa jangombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi kesho saa nne asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwao jangombe Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndg wa c na mareheme baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Jangombe kwa nduga zake kwa mazishi kesho
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KIKULETWA WILAYA YA HAI LEO

$
0
0
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kuzalisha umeme na kutoa mafunzo cha Kikuletwa ambacho nchi yake imetoa dala za Marekani milioni 5 kwaajili kukifufua kwaajili matumizi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,Anthony Mtaka,Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakikagua vyanzo vya maji eneo la Chemka vitakavyotukika kuzalisha umeme na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya Uandisi Umeme wa Chuo hicho.

Mhandisi wa Umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha,Merchior Urbanus(kushoto)akimwelekeza jambo Balozi wa Norway wakati akitembelea eneo la Kikuletwa.

Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akifurahia madhari ya Kituo cha Kikuletwa, amehaidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati hapa nchini.

Moja ya mitambo zamani iliyopo kwenye kituo cha Kikuletwa iliyowekwa na Mmisionari wa Kijerumani mwaka 1935 na baadaye kukabidhiwa kwa shirika la umeme nchini Tanesco kisha Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kutotumika kwa muda mrefu.

Moja ya chanzo cha maji ambacho pia hutumika kama sehemu ya utalii kutokana na maji yake kuwa ya vuguvugu muda wote.

Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad(wa tatu kutoka kulia)Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wakuu wa Chuo hicho na maafisa wa Ubalozi wa Norway nchini katika picha ya pamoja leo.

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

SSRA kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii

$
0
0
Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi na kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. 
Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Baadhi ya wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua picha na taarifa iliyokuwa ikitolewa na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza na kuchukua taarifa iliyokuwa ikitolewa na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakichukua maswali ya waandishi wa habari, walipokuwa wakitaka ufafanuzi kuhusu mamlaka na mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mamlaka hiyo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii. Katikati ni Ofisa Tehama wa SSRA, Ernest Masaka na kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi (kushoto), akijibu maswali ya waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mamlaka hiyo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii. 

Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema imeanzisha utaratibu mpya wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Ofisa wa Tehama wa mamlaka hiyo, Ernesti Masaka amesema hayo, leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.

Alisema kuwa kwa sasa mwanachama yoyote mwenye malalamiko kuhusu huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii au maoni yake mbalimbali anaweza kufanya mawasiliano na mamlaka kwa urahisi kupitia njia ya kieletroniki  inayopatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi na kwenye simu hizo huduma hiyo inapatikana kwenye Google play kwa jina la SSRA.

"Mlalamikaji pia anaweza kutuma malalamiko yake kupitia kwenye tovuti ya mamlaka ya www.ssra.go.tz na kwenda sehemu iliyoandikwa malalamiko na maoni. Uanzishwaji wa mfumo huo ni moja ya hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii namba 8 ya mwaka 2008 iliyoboreshwa kwa sheria namba 5 ya mwaka  2012 alisema".

Aliongeza utaratibu huo umeanzishwa ili kurahisishia mwanachama yoyote kutoa malalamiko yake kuhusu masuala ya sekta hiyo ambapo anaweza kufanya hivyo akiwa mahali popote.

Alisema mwanachama yoyote anaweza kupakua mfumo wa malalamiko kwenye simu yake kupitia google play  kwenye simu yake na kuanza kutuma malalamiko yake au kupitia kurasa ya kwanza ya tovuti ya mamlaka.

Ambapo ataweza kuingia katika mfumo huo wa malalamiko na maooni na utampeleka moja kwa moja katika kurasa itakayomuwezesha kuingiza taarifa binafsi za mwanachama mwenye lalamiko kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya wanachama.

"Mfumo huu wa malalamiko umezingatia uwekaji mzuri wa kumbukumbu kwa upande wa mamlaka ambapo huonesha ripoti kwa ufupi za jumla ya malalamiko yanayoendelea  kufanyiwa kazi, yaliyokamilika kufanyiwa kazi na mfuko husika wenye malalamiko hayo.Pia  mfumo huo hutoa taarifa za malalamiko ya wanachama kwa vigezo vya aina ya malalamiko kwa idadi na hatua ya utekelezaji  iliyofikiwa,"alisema Masaka.

Aliongeza kwa ujumla mawasiliano kati ya wananchi na mamlaka yameimarishwa kwa matumizi ya simu za mkononi kwa njia ambazo zimeorodheshwa hapo juu.Pia mamlaka hiyo ina utaratibu wa kuwasiliana na wadau kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu na barua pepe.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yalitaka Gazeti la MwanaHALISI kuiomba radhi Ukurasa wa Mbele katika toleo lake lijalo.

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE 

 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko Zanzibar ni miongoni mwa Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25, oktoba,2015. 

Hata hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano. 

Tume imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18, 2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni mwa Wananchi. 

 Kwa ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,

Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao: 

• Tarehe 13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo. Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume. 

• Katika Taarifa hiyo, Tume ilieleza wazi kuwa Majimbo ya Zanzibar yataendelea kuwa hamsini (50), ingawaje Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeongeza majimbo manne na kuwa Hamsini na Nne (54). 

• Tulieza sababu ya kubaki na Majimbo hamsini (50) ni kutokana na matakwa ya Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ili kuongeza idadi ya wabunge kutoka Zanzibar inahitaji theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono mabadiliko hayo.

 • Tulieza kuwa, kipindi hicho Tume isingeweza kuandaa na kuwasilisha Muswada Bungeni kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa linamaliza muda.

 • Katika taarifa hiyo, ilifafanuliwa kuwa, ili kubaki na majimbo Hamsini (50), kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, majimbo manne yaliunganishwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabuge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoka Zanzibar. 

• Majimbo yaliyounganishwa ni: 1. Jimbo la Bububu liliunganishwa na Jimbo la Mtoni, likaitwa jimbo la Bububu 2. Jimbo la Mwera liliunganishwa na Mto pepo likaitwa jimbo la Mwera 3. Jimbo la Kiembesamaki liliunganishwa na Chukwani likaitwa jimbo la Kiembesamaki 4. Jimbo la Pangawe liliunganishwa Kijitoupele likaitwa Kijitoupele 

• Kwa mantiki hiyo Jimbo la Kijitoupele ni mojawapo ya Majimbo hayo (50) ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisimamia na kuratibu Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge. 

• Tarehe 28 Oktoba, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Umma kuwa, ilishapokea Matokeo ya Kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kutoka Majimbo yote ya Zanzibar na siyo “siyo Matokeo ya Ubunge” 

 • Tarehe 19 Desemba, 2015 Tume ilitoa orodha ya Majimbo ambayo hayajafanya Uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hililafu mbalimbali, mojawapo ya majimbo hayo nane (8), jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni miongoni.

Ni vema wananchi wakafahamu kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haianzishi na haijaanzisha Jimbo jipya la Uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015. 

Hii inaonesha ni kiasi gani Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alivyodhamiria kuupotosha Umma kwani katika Makala/Taarifa hiyo hiyo ambayo anadai hakuna Jimbo la Kijitoupele (Unguja); anaeleza kuwa tarehe 25 Oktoba 2015 wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele walikosa fursa ya kumchagua Mbunge. 

Amemtaja Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI kuwa ni Wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele, ambalo anadai eti Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeliibua miezi mitatu baada ya Uchaguzi. Huu ni uongo na upotoshwaji wa makusudi kabisa. 

Tume inapenda wananchi waelewe kuwa, hata kabla Tume ya Uchaguzi haijafuta matokeo wa Zanzibar, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imesha tangaza kuahirisha Uchaguzi katika Majimbo nane (8) likiwemo la Kijitoupele kwa sababu za Vifo vya Wagombea na hitilafu mbalimbali.

Jimbo la Kijitoupele la Zanzibar ni miongoni mwa majimbo nane (8) ambayo yaliahirishwa kufanya uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo majimbo sita (6) ambayo ni Lushoto, Ulanga Mashariki, Masasi Mjini, Ludewa, Handeni Mjini na Arusha Mjini yaliahirishwa kutokana na vifo vya wagombea na majimbo mawili (2) ya Kijitoupele - Zanzibar na Jimbo la Lulindi – Masasi yaliahirishwa kutokana na hitilafu mbalimbali.

 Hoja nyingine iliyotolewa na gazeti hilo ilihusu uteuzi wa Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum. Ifahamike kwamba katika maamuzi yake kuhusiana na viti maalum, Tume imezingatia matakwa ya Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoeleza kuwa, ili chama kilichoshiriki Uchaguzi Mkuu kipate Viti Maalum ni lazima kiwe kimepata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge.

 Hivyo, Viti Maalum vilivyobaki haviwezi kugawanywa hadi hapo Jimbo la Kijitoupele litakapofanya Uchaguzi katika tarehe ambayo itaitangazwa na Tume hapo baadaye.

 Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alipaswa kufanya uchunguzi na uchambuzi wa kina kuhusu habari aliyoiachapisha ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Viongozi wa Tume ya Uchaguzi ili wapate ufafanuzi wa Majimbo ya Uchaguzi na siyo kutoa Taarifa za uongo, uchochezi na upotoshaji kama walivyofanya. 

Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI atambue uandishi wa habari ni zaidi ya kushika kalamu na kuandika, unahusisha uwezo wa kutafuta habari pande zote mbili ili kupata mizania ya habari anayoiandika, kufanya utafiti, kujiridhisha pasipo shaka kuwa habari anayoitoa ni sahihi. 

Kwa kuwa Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alikusudia kuupotosha umma kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe kwa kutoa Taarifa zisizo sahihi, za uongo na uchochezi Tume ya Taifa ya Uchaguzi inamtaka Mhariri wa Mwanahalisi kuiomba radhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ukurasa wa mbele wa Toleo Lijalo kama alivyofanya katika gazeti hilo. 

Kama wasipofanya hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi italichukulia Gazeti la MwanaHALISI hatua za Kisheria. 

 Imetolewa na Kailima,R.K 
Mkurugenzi wa Uchaguzi. 

Ligi Kuu ya Zanzibar Mtende na Zimamoto mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan leo Jioni.

Maalim Seif aifariji familia ya Marehemu Asha Bakari Makame

$
0
0
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akimfariji Mama mzazi wa marehemu  Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.


 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akibadilisha mawazo na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, pamoja na kaka yake Bw. Mbarouk Makame (mwisho kushoto), alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Viewing all 35874 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>