Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35852 articles
Browse latest View live

Makamu wea Rais Mhe. Samia Suluhu Ashiriki Dua ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Asha Bakari Makame.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja ya kumuombea aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja mbele ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakishiriki kubeba Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame kabla ya mazishi yake yaliyofanyika  leo Januari 22,2016 katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto akizungumza na kuwafariji wanafamilia wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame baada ya Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia akimfariji Mama Mzazi wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame, Bibi Mwanajuma Faki (90) wakati wa Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe Zanzibar, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto akizungumza na kuwafariji wanafamilia wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame baada ya Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. Wa pili kushoto ni Mama Salma Kikwete katikati Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuagana na Wananchi waliofika kwenye Msiba wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa marehemu Asha Bakari Makame wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo Januari 22,2016 katika kijiji cha kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. (Picha na OMR)

Zantel donates 20 million and adopts the classroom for students living with disability in Unguja

$
0
0


Telecom Company, Zantel Tanzania has today adopted the classroom for the visually impaired and donated stationery worth 20 million to Kisiwandui Primary School in Ugunja.

Speaking during the handover ceremony, Zantel Chief Executive Officer, Mr. Benoit Janin said supporting the students living with disability is part of Zantel’s commitment improving the quality of education offered in Zanzibar.

‘Our responsibility as members of the society is to give them the best support and get them ready for the journey ahead by treating them as if they were what they ought to be and helping them become what they are capable of becoming’ said Benoit.

The donated stationery comprises perking braille, embosser, A4 frame and braille papers are part of Zantel’s effort to address the needs of education and disability in Zanzibar.

We realized that we needed to help the students living with disability to get quality education and assist in developing their potential by purchasing and donating the stationery that they required’ said Mr Janin.

Also speaking at the event, School Headmaster, Ms Taifa Ahmed, thanked Zantel for their support to the school pointing out that the stationerywill go a long way in making a difference to quality of education that the students were getting.

We are pleased to receive this donation as we will see these students rise up to the challenge and accomplish many wonderful things,’insisted Ms. Taifa.

Ms. Taifa also noted that students living with disability are like any other students, and if well supported they can contribute more to the society.

The donation aims at improving education standards in local communities by ensuring that quality education is provided even for the students living with disability.



Kampuni ya simu ya Zantel yatoa msaada wa shilingi milioni 20/- kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui Unguja.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akisaini barua ya kampuni ya Zantel kwa ajili ya kuanza kulisaidia  darasa la walemavu wa uoni wa shule ya msingi Kisiwandui ambapo pia walikabidhi msaada wa jumla ya shilingi milioni 20. Waanaotazama kutoka ulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisiwandui, Bi Taifa Ahmed, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali, na mwisho kushoto ni Shinuna Kassim, Mkurugenzi wa Mipango ya Biashara wa Zantel.
Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa jumla ya shilingi milioni 20 kutoka kwa kampuni ya Zantel kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wa ulemavu wa macho.
Mkurugenzi wa Zantel, Benoit Janin akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa jumla ya shilingi milioni 20 kutoka kwa kampuni ya Zantel kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wa ulemavu wa macho.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi, mwalimu mkuu, Bi Taifa Ahmed mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya wanafunzi wenye ulemavu wa uoni wa shule ya msingi Kisiwandui.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akisaini barua ya kampuni ya Zantel kwa ajili ya kuanza kulisaidia  darasa la walemavu wa uoni wa shule ya msingi Kisiwandui ambapo pia walikabidhi msaada wa jumla ya shilingi milioni 20. Waanaotazama kutoka ulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisiwandui, Bi Taifa Ahmed, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali, na mwisho kushoto ni Shinuna Kassim, Mkurugenzi wa Mipango ya Biashara wa Zantel. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi Taifa Ahmed barua inayoonyesha nia ya kampuni ya Zantel kusaidia shule ya Kisiwandui. Anayetazama katikati ni Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali. Zantel pia walikabidhi shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya walemavu wa uoni.
Mwanafunzi, Mbarouk Nassor akitoa shukrani kwa kampuni ya Zantel baada ya kupokea msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya kuwasaidia kusoma.
Uongozi wa kampuni ya Zantel pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya Kisiwandui katika picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya walemavu wa uoni wa shule hiyo.

Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 20 kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho wa Shule ya Msingi Kisiwandui iliyopo Ugunja kwa ajili ya kununua vifaa vitakavyo wasaidia wanafunzi hao wawapo  shuleni.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zantel, Benoit Janin alisema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa  kampuni ya Zantel katika  kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu bora bila kujali tofauti zao.

‘Wajibu wetu kama wanajamii ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata msaada kama ilivyo kwa watu wengine na pia kuweza kuwaanda  kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama walivyo kusudia’ alisema Benoit.

Vifaa hivyo vipya ni sehemu ya jitihada za kampuni ya Zantel kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya elimu kwa wanafunzi wenye  walemavu ili kuhakikisha wanapata elimu bora kama ilivyo kwa wanafunzi  wasio na ulemavu .

‘Kama sehemu ya jamii tumedhamiria kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa wanavyovihitaji ili kuwasaidia kupata elimu bora, na kuanzia leo tutalichukua darasa hili kuendelea kuwasaidia mahitaji mengine’ alisema Benoit.

Naye Mkuu wa  Shule hiyo, Bi Taifa Ahmed, alitoa shukrani za dhati kwa Zantel kwa ukarimu wao  na kusema kuwa msaada huo ni wa kipekee na utarahisisha ufundishaji kwa wanafunzi hao, na hivyo kupelekea wanafunzi hao kupata elimu bora kama ilivyo kwa wengine wasio na ulemavu.

‘Tunawashukuru Zantel kwa kuziona changamoto tulizokuwa tunakabiliana nazo, na hakika kwa msaada huu utatatusaidia katika kuwafundisha wanafunzi hawa na pia kuwawezesha  kufikia malengo yao ' alisema Bi Taifa.

Katika hatua nyingine, Mwalimu Taifa aliongeza kwa kusema kuwa wanafunzi wenye ulemavu ni wanafunzi wa kawaida kama wanafunzi wasio na ulemavu hivyo wakiwezeshwa wanaweza kushika nafasi  yoyote katika jamii.

Shule ya msingi Kisiwandui ilianzishwa mwaka 1991, na mpaka sasa wanafunzi 199 wamepitia shuleni hapo.


Maonesho ya Biashara ya Esther Land Show Afrika Kusini Yavutia Wafanyabiashara Wengi Zaidi Kutoka Tanzania.

$
0
0
Na Emanuel Madafa,Mbeya,Mbeya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika kusini  (Esther Land Show) ambayo hufanyika kila mwaka nchini humo yameendelea kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kutoka nchini Tanzania.

Pia Maonesho hayo hufanyika  katika mji wa Johnsburg ambapo kwa mwaka huu yanatalaji kuanzia Mwezi Machi  23 hadi  April 03 mwaka huu huku idadi ya wafanyabiasahara hao waliojitokeza imetajwa kufikia  zaidi ya watu  100 ,hasa kutoka  katika mikoa ya Kanda ya Ntanda za juu kusini.

Katika kufanikisha safari ya wafanyabiashara hao  kampuni ya  Blue  Bird Buleau De Change iliyopo Jijini Mbeya imeamua kudhamini safari hiyo kwa kutoa usafiri wa kwenda na kurudi kwa basi  la Twiga Intarnational  ambapo kila mfanyabiashara atachangia kiasi cha shilingi laki nne na nusu  (450000).

Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Jankey Ndingo, amesema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa zilizomo kwenye maeneo yao.
“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.
  
Amesema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la kimataifa.

Amesema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza kusafirisha bidhaa hizo.
“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.

Aidha, amesema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi  kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.

Hata hivyo, amesema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa ya siku 13.

Jamiimojablog

Dk Shein Ahudhuria Mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Bi. Asha Bakari Makame Kianga Zanzibar.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                            22.1.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein  leo ameongoza mazishi ya marehemu Bi Asha Bakari Makame aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Mazishi ya Marehemu Bi Asha Bakari Makame yalifanyika huko Kianga, Wilaya ya Magharibi ‘B’, Mkoa wa Mjini Magharibi kwa heshima zote za Chama Cha Mapinduzi, ambapo viongozi mbali mbali wa vyama na serikali walihudhuria  akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.

Wengine waliohudhuria ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk. Mohammed Gharib Bilal pamoja na Rais wa Zanzibar mstaafu Dk. Amani Abeid Karume na wananchi.

Mapema asubuhi, Alhaj Dk. Shein alifika nyumbani kwao marehemu huko Jangombe, mjini Unguja kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wana familia pamoja na kumuombea dua marehemu.

Baada ya hapo Alhaj Dk. Shein alishiriki katika dua maalum (hitma) pamoja na sala  ya kumsalia Marehemu Bi Asha Bakari Makame iliyofanyika huko Masjid Noor Mohammad, Mombasa kwa Mchina mjini Unguja.

Akisoma wasifu wa Marehemu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa Marehemu Bi Asha Bakari Makame alizaliwa Disemba 12 mwaka 1949 huko Mtambwe, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kwa mujibu wa maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Marehemu Bi Asha alipata elimu ya msingi huko huko kijijini kwao Mtambwe na baadae alijiunga na Skuli ya Sekondari ya Fidelcastro huko Kisiwani Pemba hadi Kidato cha nne ambapo baada ya hapo alienda nchini Bulgaria kwa ajili ya kujiendeleza kwa elimu ya Diploma ya Siasa na Utawala.

Vuai alieleza kuwa tokea uhai wake, Marehemu Bi Asha Bakari Makame, akiwa skuli na baada ya kumaliza skuli alikuwa akijishughulisha na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Afro Shirazi Party (ASP) na baadae alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pale kilipoanzishwa mnamo mwaka 1977.

Katika uhai wake Marehemu Bi Asha Bakari Makame, aliwahi kushika nyadhifa  mbali mbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali ikiwemo Naibu Waziri, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo ambapo pia, aliwahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto.

Marehemu Bi Asha Bakari, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa mnamo mwaka 1983 na baadae alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo nafasi aliyoendelea nayo hadi kufa kwake.

Naibu Vuai katika akisoma wasfu huo wa Marehemu alisema kuwa marehemu Bi Asha  katika maisha yake alikuwa muumini wa kweli wa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 pamoja na kuwa muumini wa kweli wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika mwaka 1964.

Marehemu Bi Asha Bakari Makame, katika kipindi chake chote alichotumikia chama cha CCM pamoja na serikali alikuwa kiongozi muaminifu, muadilifu, mchapakazi na asiyeyumba katika masuala ya msingi.

Naibu Vuai alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa wote wa marehemu. Nao wanafamilia walitoa shukurani Kwa wale wote waliohudhuria mazishi hayo.

Marehemu ameacha watoto watatu, wakiwemo wawili wa kike na mmoja wa kiume Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.

Rajab Mkasaba, Ikulu

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamedv Shein, Awafariji Ndigu wa Marehemu Asha Bakari.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika msiba wa Marehemu Asha Bakari Makame jangambe kutowa mkono wa Pole akisalimiana na Viongozi wa Chama na Serikali na Ndugu wa Marehemu.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akitowa mkono wa pole kwa Ndugu wa Marehemu Asha Bakari Makame alipofika kutowa mkona wa pole na kuwafariji wafiwa. nyumbani kwao Jangombe leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akijumuika na Viongozi na Ndugu wa marehemu kumuombea dua alipofika kutowa mkono wa pole kwa Jamaa wa Marehemu Jangombe Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimpa mkono wa pole Mama wa Marehemu Asha Bakari Makame alipofika kuwafariji na kutowa mkono wa pole Jangombe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwafariji watoto wa Marehemu na ndugu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mama wa Marehemu Asha Bakari Makame alipofika kutowa mkono wa pole leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimfariji Baba Mzazi wa Marehemu Asha Bakame Makame Mzee Bakari Makame alipofika nyumbani kwake Jangombe kutowa mkono wa pole leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Ndugu wa marehemu wakati alipofika kutowa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Ndugu wa marehemu wakati alipofika kutowa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa. 

Breeking News Tume ya Uchaguzi Zanzibar Yatangaza Tarehe ya Marudio ya Uchaguzi Zanzibar.

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jesha Salum Jecha atangaza Tarehe ya Marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar  utafanyika tarehe 20-3-2016. siku ya jumapili. 

Nakusema wagombea watakuwa walewale waliogombea kwa Nafasi ya Urais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani. Akitangaza taarifa hiyo leo huko Afisini kwake maisara Zanzibar.  

Ripoti ya Tathimini ya Mazingira ya Kisheria katika Mwitikio wa Ukimwi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam Leo.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (katikati), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa ripoti ya tahmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa ukimwi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi hao wakiwaonesha wageni waalikwa na wadau mbalimbali ripoti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tacaids, Elizabeth Kaganda na kilia ni Dk.Bwijo Bwijo kutoka UNDP.
 Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina, akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (kushoto), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (katikati) wakimpongeza Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina baada ya kuhutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
Wasanii wa Hisia Threatel Group kutoka Sandali Temeke jijini Dar es Salaam wakionesha igizo linalohusu ukimwi katika uzinduzi huo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

TIGO Wazindua Udhamini wa Mbio za Nusu Marathon Mjini Moshi.

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

 Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo   kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga, Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.


Wageni waalikwa ambao  ni wadhamini wa Kili Marathon wakifurahia jambo baada ya Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga kuzindua mbio za Kili Marathon kwa upande wa Moshi ambapo zitafanyika hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.

Mbio za Nusu Marathon 2016 zimezinduliwa jana mjini Moshi, huku ikiwa imebaki mwezi moja kabla za mbio hizo kufanyika.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habarialisema mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.
“Tumeonelea ni vizuri kuzindua mbio hizi rasmi hapa Moshi  ambako zitafanyika ili kuashiria kuwa mambo yamekamilika,” alisema.
“Tigo imeingia mwaka wake wa 2 kama mdhamini wa mbio za kilomita 21.2 hizi. Kwa mujibu wa Meneja huyo, wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Kilimanjaro beer 45, Gapco kwa km 10 viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt kwa km 5.
Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair na Keys Hotel.
Alisema Tigo imewekeza zaidi ya Sh Millioni 200 katika mashindano hayo na kuwa hapo badaye watatangazo mchanganuo mzima wa zawadi zitakazotolewa.
Alitoa shukrani za pekee kwa mkoa wa Kilimanjaro na chuo kikuu cha Ushirika MOshi (MoCu), zamani kikiitwa MUCCoBS kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Akizindua mbio hizo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makung, aliwapongeza Kilimanjaro Premium Larger,Tigo wadhamini wengine na wandaaji kwa kujielekeza vyema  kila mwaka, akiongeza kuwa mashindanoyametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo ndani na nje ya nchi.
“Mashindano haya pia yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii, kwani wanariadha wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo kufaidisha uchumi wan chi,” alisema Makunga.
Makunga aliawataka wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanajiandaa vyema ili watwae zawadi nyingi zaidi kwa kadiri zilivyopangwa kwa kila mbio. Aliongeza kwamba wizara yake inaunga mkono kabisa ubunifu kama huo na kuzitaka kampuni nyingine kufuata nyayo hizo kwa kudhamini mashindano hayo kila mwaka.

Aliwapongeza wandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT) na wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha siku zote kwamba tukio hili linafikiwa .
“Mbio hizi zimeleta mwamko mpya katika riadha hapa nchini kwa kuwapa fursa vijana wetu wanaochipukia kuweza kujipima na wanariadha mashuhuri kimataifa. Changamoto hii imekuwa na faida kubwa,ambapo vijana wetu wameweza kutambua uwezo wao na kuweza kujiamini  zaidi wanapokwenda kushiriki mashindano mbalimabli kwenye nchi za kigeni,” alisema.

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, alisema kwamba kampuni yake imefurahishwa kupata fursa ya kudhamini mbio za nusu marathoni kwa kilimota 21 kwa mwaka wa pili mfululizo.
“Natoa rai kwa washiriki wajiandae vizuri ili safari hiituweze kunyakua mataji mengi,” alisema Kinabo.

Meneja Masoko wa Gapco Tanzania, Caroline Kakwezi, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za kilomita 10 kwa wanaotumia viti vya magurudumu na wale wanaonyonga baiskeli kwa mikono ambazo wanazidhamini, alisema zimekua na mvuto mkubwa na ushindani mkubwa pia na kwamba katika mwaka wao wa tano katika udhamini wameshuhudia mbio hizo zikikua.

“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono, safari hii tutatoa usafiri, malazi na chakura kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam katika mbio hizi za walemavu na yote haya hayawezekani bila ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wateja wetu”alisema.


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Atangaza Marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar.

Mazishi ya Marehemu Asha Bakari Makame katika Kijiji cha Kianga Zanzibar

$
0
0
Viongozi wa Serikali wakijumuika na Wananchi mbalimbali wakimsomea hitma Marehemu Asha Bakari Makame iliofanyika katika Masjid Noor-Muhammad Kwamchina uliokosaliwa mwili wa marehemu na kuzikwa katika Kijiji cha Kianga nje kidgo ua Mji wa Zanzibar Wuilaya ya Magharibi B Unguja.wakwanza Waziri Kiongozi Mstaaf Shamsi Vaia Nahodha, Makamu wa Rais Mstaaf wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Msataa wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.   

Wakwanza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Khamis Mwinyi Naibu Kadhi Shekh. Mussa Ngwali, wakiitikia dua iliokuwa ikisomwa baada ya kumaliza kusowa hitma.katika Masjid Noor-Muhammad Kwamchina Zanzibar.
Wananchi wakiitikia dua baada ya kumsomea hitma marehemu Asha Bakari Makame.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakipokea jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame wakati wa kumsalia katika Masjid Noor-Muhammed Kwamchina Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Serikali na Wananchi wakikujumuika katika Sala ya kumsalia marehemu Asha Bakari Makame iliofanyika katika Masjid Noor-Muhammad Kwanchina.
Naibu Kadhi wa Zanzibar Shekh Mussa Ngwali akiongoza Sala ya kuusalia Mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame iliofanyika katika Masjid Noor-Muhammad Kwamchina na kuzikwa katika Kijiji cha Kianga Nje Kidogo ya Mji wa Zanzibar Wilaya ya Magharibi B Unguja. 


Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiusalia mwili wa marehemu Asha Bakari Makame katika Masjid Noor- Muhammad Kwamchina Zanzibar.
Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiitikiac dua ikisomwa na Naibu Kadhi wa Zanzibar Shekh.Mussa Ngwali. baada ya kumalizika kwa sala ya maiti.

Ndugu na Jamaa wakiitia dua 
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakijumuika katika Sala ya kumsalia marehemu Asha Bakari wakiitikia Dua baada ya Sala hiyo.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakijumuika katika Sala ya kumsalia marehemu Asha Bakari wakiitikia Dua baada ya Sala hiyo.
Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiitikiac dua ikisomwa na Naibu Kadhi wa Zanzibar Shekh.Mussa Ngwali. baada ya kumalizika kwa sala ya maiti.
Wananchi wakiwa wamebeka jeneza lenye mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame baada ya kumaliza Sala ya kuusalia mwili huo iliofanyika katika Masjid Noor-Muhammad Kwamchina Zanzibar,







Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi.
Makamu wa Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi la marehemu wakati wa mazishi hayo katika kijiji cha kianga Zanzibar. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho akiweka mchanga katika kaburi wakati wa mazishi hayo yaliofanyika katika kijiji cha kianga Zanzibar.
Baba Mzazi wa Marehemu Mzee Bakari Makame akiweka mchaka katika kaburi la mwanawe wakati wa mazishi hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Wananchi wakishiriki katika mazishi hayo katika Kijiji cha Kianga Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika kaburi la mareheme Asha Bakari Makame baada ya kumaliza kuzika na kuweka sawa kaburi hilo katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Naibu Kadhi Shekh. Mussa Ngwali akisoma dua baada ya kumalizika kwa mazishi hayo ya Marehemu Asha Bakari Makame yaliofanyika katika Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibu B Unguja. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akisoma wasifu wa Marehemu Asha Bakari Makame katika kukikutimikia Chama kwa nafasi mbalimbali hadi kifo kinamkuta alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania kwa Zanzibar.

Nyota wa kikapu wa Malawi kuzikabili timu za Dar

$
0
0
 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.


 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.
Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.
Karabani ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji  vya vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.
 “Lengo letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu, ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Malawi
Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo huo.
 “Sote tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka alisema.

Magazetini Bongo Tz.

Matukio ya Picha Mitaani Zenj

$
0
0
Gari za kubebea mizingo zikiwa zimeegeshwa kando ya barabara zikisubiri wateja wakati wa kuingia kwa meli ili kuweza kupata mizigo, uegeshwaji wa magari kama hivi, Mamlaka ya Mji Mkongwe wakilifanyika kazi suala hili kwa maegesho ya aina hiyo na kuwa usumbufu kwa wananchi wengine wanaotembelea mji mkongwe. 

Askari wa Polisi Jamii katika Mji Mkongwe wa Zanzibar akimtaka dereva wa gari hiyo kuondoa gari yake ambayo imeegeshwa katika eneo halistahili kuegesha katika katika maeneo ya malindi ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo wakati wa kufika kwa male eneo hilo huwa na msongamano mkubwa wa magari.
Wachuuzi wa Samaki wakiwa katika ufukwe wa pwani ya Malindi Zenj wakisubiri wavuvi kurudi ili kuapa ta bidhaa hiyo ya samaki, katika kipindi hichi cha upepo samaki wamekuwa haba katika soko hilo la malindi na kufikia mtungo mmoja wa masaki katika mnada hapo hufikia kati ya shilingi 50,000 inategemea ukubwa wa samaki.

Katuni na Ujumbe Wake Huuuooo.....


Msimu wa Embe ukiwa Umetia Fora Zenj Mwaka Huu.

$
0
0
Mjasiriamali wa matunda aina ya embe katika mji wa Zanzibar akijitayarisha kuweka sawa bidhaa hizo ili kuweza kupanga fungu moja la embe dodo huuzwa kati ya shilingi 1000/= kwa embe tatu na embe tano huuzwa shilingo 2000/= katika maeneo ya Zanzibar.

Tz Bongo Magazetini leo.

Jengo la Mahakama ya Mkoa wa Kusni Pemba lafanyiwa ukarabati

$
0
0

MAFUNDI rangi wakiwa katika hatua za mwisho, kukamilisha kazi ya upakaji wa rangi katika jingo la Mahakama ya Mkoa wa kusini Pemba, ambayo imefanyiwa Ukarabati mkubwa mahakama hiyo, pichani mafundi wakimalizia upakaji wa rangi hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Hatuwezi kutenga sehemu maalum kuhifadhi historia ya magari yetu ya zamani?

$
0
0
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar inapaswa kutafuta sehemu maalumu ya kuhifadhi magari ya zamani, ambayo yalitembea kisiwani Pemba katika miaka ya 1970, gari hizo zinaweza kuwa moja ya vivutio vikubwa vya utalii, ni moja ya daladala za kisiwani Pemba ambazo zinaweza kuwa historia kubwa kwa vizazi vijavyo, pichani gari aina ya daladala za mbavu za mbwa, ambalo kwa sasa limekufa kabisa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Taasisi mpya ya kukabiliana na Vifo vya Wajawazito na Watoto Zanzibar ( KANGA) yazinduliwa

$
0
0
 Baadhi ya wageni waliohudhuria katika  uzinduzi wa Taasisi ya KANGA ambayo itahusika katika kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wadau kwa lengo la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi wa Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
 Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah Talib kushoto na Mwenyekiti wa Taasisi ya KANGA Dkt.Mohamed Hafidh kulia kwa pamoja wakiwakabidhi Viongozi kutoka Taasisi ya “DARAJA Foundation” KEKI waliyoinunua katika harambee ya kuichangia Taasisi ya Kanga kama njia ya kuiunga Mkono Taasisi hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

 
 Mwenyekiti wa Taasisi ya KANGA Dkt.Mohamed Hafidh akitoa maelezo ya Taasisi hiyo ambayo itahusika katika kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wadau kwa lengo la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi wa Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah Talib akitoa hutuba yake kabla ya kuizindua Taasisi ya KANGA ambayo itahusikana ukusanyaji wa michango mbalimbali kutoka kwa wadau kwa lengo la kupambana na Vifo vya Wajawazito na Watoto nchini.Uzinduzi wa Taasisi ya KANGA ulifanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar.


Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 23/01/2016

Katika kukabiliana na Vifo vya Wajawazito na Watoto Zanzibar Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama KANGA imezinduliwa rasmi ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo nchini.

Uzinduzi wa Taasisi hiyo umefanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar.

Akitoa ufafanuzi wa kuanzishwa kwake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Dkt.Mohamed Hafidh amesema Serikali na Taasisi binafsi zinawajibu wa kuzidisha mikakati ya kukabiliana na Vifo kwa akinamama na watoto ili kuwa na taifa endelevu.

Amebainisha kuwa wapo baadhi ya watu wenye uwezo wa kuchangia lakini wanashindwa kujua wapi watapeleka Misaada yao ili kuokoa maisha ya watoto na akinamama.


Dkt. Mohamed ameongeza kuwa hata Serikali kupitia Wizara ya Afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali za matibabu nakwamba uwepo wa Taasisi ya KANGA kutasaidia kwa kiasi kikubwa juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo hilo nchini.

“Ukweli nikwamba wapo wasamaria wema wanaguswa na hali ya vifo vya Wajawazito na Watoto lakini wanashindwa wapi kwa kupeleka misaada yao lakini kupitia Taasisi hii ya KANGA basi itakuwa ni sehemu muafaka ya kupeleka misaada yao na bila shaka lengo litafikiwa”Alisema Dkt. Mohammed Hafidh

Dkt Mohamed amesema hali ya Vifo nchini bado inatisha na kufafanua kwamba kati ya Kinamama Wajawazito Laki moja,wastani wa 460 hupoteza maisha yao nchini ambapo kwa nchi za Ulaya Idadi kama hiyo ni wastani wa watu sita wanaopoteza maisha.

Ameongeza kuwa Wastani wa Watoto 29 kati ya Elfu moja wanaozaliwa hufariki dunia nchini Tanzania ambapo kwa nchi za Ulaya ni Wastani wa watoto watatu wanaopoteza maisha miongoni mwa watoto Elfu moja.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdallah Talib amewaomba Viongozi na wananchi kwa ujumla kuiunga mkono Taasisi hiyo kwa kuchangia jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazowakabili wazazi na Watoto katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.

Amesema kutokana na umuhimu wa jambo lenyewe ameahidi kukwata kiasi Fulani cha Mshahara wake kila mwezi ili kuchangia harakati za Taasisi ya KANGA.

“Kwa namna ambavyo nimeguswa na Malengo ya Taasisi ya KANGA na kwa namna ambavyo Tatizo la Vifo kwa Wajawazito na watoto linavyoendelea naahidi kukatwa Mshahara wangu kila mwezi kusapoti Taasisi hii”Alisema Shekh Talib

Taasisi ya KANGA ambayo imezinduliwa imejikita katika kujitolea kupambana na tatizo la Vifo kwa watoto na akinamama wakati wa ujauzito ambapo pia malengo ya baadae itaratibu uwepo wa Madaktari Wanawake wa kutosha ili taratibu za Uzazi zote Hospitalini zifanywe na Wanawake wenyewe badala ya Wanaume kama ilivyo sasa.

Katika uzinduzi huo Taasisi mbalimbali zilihudhuria na kutoa michango yao ikiwemo Mfuko wa Huduma za jamii Zanzibar ZSSF, Bank ya Watu wa Zanzibar, Taasisi ya Daraja Faoundation. 

Viewing all 35852 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>