Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36091 articles
Browse latest View live

ZIRPP Monthly Lecture: "Europe-Africa Relations: A Pan-Africanist Perspective

$
0
0

There will be another ZIRPP Monthly Lecture.
Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf
Speaker: Ambassador Andebrhan Giorgis
Subject: "Europe-Africa Relations: A Pan-Africanist Perspective"
Date & Time: Saturday 02 April 2016; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office; Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK)

Abstract: Europe and Africa have been in constant contact since time immemorial, through the ancient world to the present. The Euro-African or Afro-European relationship has not always been a happy one, especially in its modern version. Deeply rooted in the troubled historical legacies of the slave trade, territorial conquest and partition, and the colonial and neocolonial experience, Europe-Africa relations, about half a century after decolonisation, is undergoing radical transformation from one characterised by dominance and dependence to one aimed at strategic partnership and cooperation.

The lecture would highlight the salient features of the historical evolution of the Euro-African relationship, interrogate the EU’s push for the replication of its model of regional integration in Africa and the AU adoption of the EU model underpinning the of the Joint Africa-EU Strategic Partnership (JAESP), and assess the feasibility of such duplication.Tea, Coffee and Snacks will be served freely.

Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.

Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.

All are welcome.
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania; 
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475; 
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info



Wizara ya afya yalifanyia ukarabati tanuri la kuchomea takataka za Hospitali Chakechake

$
0
0

WIZARA ya Afya Pemba, imeanza kazi ya ukarabati wa Tanuri maalumu la kuchomea takataka zinazotoka katika Hospitali ya Chake Chake, kilio ambacho Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, kilimsikitisha sana kutokuwepo kwa tanuri hilo wakati alipotembelea kisiwani Pemba Mwanzoni mwa mwezi huu.

(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Muonekano wa Jengo la Mahkama Kuu Pemba

$
0
0


JENGO la Mahkama kuu ya Pemba, likiwa katika monekano mpya baada ya kumaliza kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu, jengo hilo linasubiri fanicha mpya, ili liweze kuhamiwa na kurudi kufanya kazi zake za kama zamani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Spika mpya BLW ala kiapo na aahidi uadilifu na umakini mkubwa ili kupata ufanisi

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 

Spika mpya wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amesema kuwa atakiongoza  chombo hicho, ambacho ni muhimili wa tatu wa Dola, kwa uadilifu na umakini mkubwa ili kuona  wajumbe wanafanyakazi ya kuwatumikia wananchi majimboni na kuisaidia Serikali katika kuleta maendeleo.

Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi mara baada ya kula kiapo cha nafasi  ya Spika kufuatia  kuchaguliwa kwa kura zote za wajumbe 76 waliokuwepo barazani hapo.

Amesema kazi hiyo ataifanya kwa kufuata Katiba ya Zanzibar, sheria na kanuni  zinazoongoza  Baraza la Wakilishi.

“Nitakitumikia chombo hichi  kwa uadilifu na kufuata sheria na taratibu zote za baraza ili kuhakikisha kinapata ufanisi katika utekelezaji wa kazi zake”, alisema Zubeir.


Aidha Spika huyo aliwataka Wakilishi kuwatumikia wananchi wao Majimboni bila ya kuangalia itikadi zao za kisiasa ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa jumla.

Spika huyo aliwashukuru wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kumchagua kwa kura nyingi na kusema kuwa ni wazi amekubalika,hivyo atakuwa msikivu na muadilifu katika kusimamia zake.

Nae mwakilishi wa jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Mussa alisema kuwa atafanya kazi ya kuwatumikia wananchi wake jimboni bila ya mitazamo  ya kisiasa ,na kusema kuwa wananchi wote katika jimbo hilo ni wake na watafanyakazi pamoja

Masauni ziarani mkoani Kigoma

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi  Mkoani  Kigoma, Tonny  Samwel  Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo,Dost Yousafzai (kushoto), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), wakati ya ziara ya Naibu Waziri kutembelea ilipokuwepo kambi ya wakimbizi ya Karago, wilayani Kibondo. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi (hawapo pichani) wanaoishi katika kambi ya Mtendeli, iliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Dk Shein amuapisha Makamu wa Pili wa Rais Ikulu

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
RESS RELEASE
    Zanzibar                                                   30 Machi, 2016
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo  amemuapisha  Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Dk. Shein alimteua Balozi Seif Ali Iddi kushika wadhifa huo hivi karibuni kwa mujibu wa kifungu cha 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Uteuzi wa Balozi Seif Ali Iddi ni uteuzi wa pili wa Mheshimiwa Rais tangu alipoapishwa Alhamisi iliyopita kuanza kipindi chake cha pili cha uongozi wa Awamu ya Saba.

Sherehe za kumuapisha Makamu wa Pili wa Rais ambazo zilifanyika Ikulu Zanzibar zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu Mheshimiwa Said Hassan Said.

Wengine ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu Sheikh Omar Kabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi Abdalla Mwinyi Khamis na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib.

Balozi Seif Ali Iddi anashika wadhifa huo kwa mara ya pili. Mara ya kwanza aliteuliwa mwezi Novemba, 2010 na kuushikilia hadi kumalizika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya uongozi wa Awamu ya Saba kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016.
  
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

Prof Mbarawa aipongeza Halotel kwa mkakati wake wa kuboresha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano ya simu vijijini.

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa ametoa pongezi kwa kampuni mpya ya simu ya Halotel kwa juhudi zake inazofanya katika kutekeleza mkakati  wa  kuhakikisha  huduma ya mawasiliano inapatikana  maeneo ya vijijini.

Pamoja na ongezeko la zaidi ya asilimia 16 la idadi ya watumiaji wa simu za mikononi nchini bado tatizo la upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa maeneo ya vijijini imekuwa ni changamoto.

Prof Mbarawa alisema serikali imekuwa inafanya juhudi mbalimbali ili kuziba pengo la upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kati ya maeneo ya vijijini na mijini, na hivyo mwaka 2006 mfuko wa mawasiliano kwa wote ulianzishwa  kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini na mijini.

'Kulikuwa na mwamko mdogo kutoka kwa makampuni ya simu katika kupeleka mawasiliano vijijini kutokana na mazingira yake na  changamoto  kama vile kuwa  na  idadi ndogo ya wakazi, ndio maana serikali ikaanzisha mfuko wa upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote ili kusaidia katika zoezi la utekelezaji wa upanuzi wa huduma ya mawasiliano' alisema Mbarawa.


Hata hivyo, Prof Mbarawa amebainisha kuwa bado mwitikio wa uombaji wa zabuni kwa ajili ya jitihada za kupanua mawasiliano maeneo ya vijijini umekuwa ni mdogo sana na hivyo basi kusababisha maelfu ya vijiji kukosa huduma ya mawasiliano  na hivyo kuendelea  kukithiri kwa hali ya umaskini .

'Wakati kampuni ya simu ya Halotel ilipokuja nchini na mkakati wa  kuwekeza maeneo ya vijijini, sisi kama serikali tuliwapokea kwa mikono miwili na tukaahidi kuwasadia baadhi ya mambo ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo, lakini pia tukawapa masharti ya kuhakikisha wanaunganisha mawasiliano ya mtandao kwa ofisi za vijiji 150, hospitali za umma 150, vituo vya polisi 150, pamoja na ofisi za posta 65 na pia shule 450 'alisema Prof Mbarawa.

Hadi sasa, Kampuni ya simu ya Halotel kwa  sasa imeunganisha huduma ya mawasiliano kwa  vijiji 1800 ambavyo vilikuwa havina huduma hiyo, na kufikia mwishoni mwa mwaka huu kampuni ya simu ya Halotel itakuwa imeunganisha  vijiji vingine 1500 kwa mara ya kwanza ili kuhakikisha huduma bora ya mtandao wa 3G.

‘Kampuni ya Halotel imeunganisha zaidi ya watumiaji wa huduma ya simu 1,800, ambao kabla walikuwa hawajaunganishwa,na  muhimu zaidi, wameunganishwa na mtandao wa kasi wa 3G kupitia fiba yenye kilomita 18,000 na hivyo kusaidia watumiaji wa huduma hiyo kupatikana mahali popote na kwa wakati wowote ‘ alisema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel, Le Van Dai.

Serikali ya Tanzania na mshirika wake Kampuni ya Halotel wamewekeza jumla ya dola za kimarekani billioni moja sawa na trilioni 2 za kitanzania katika kutekelezeka upanuzi wa huduma ya mawasiliano kwa mikoa  mikoa 26, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kuunganisha vijiji 1,500 kupitia mkonga wa mawasiliano unaovuka kilometa 2,500 pamoja na na kusambaza kilometa 18,000 za fiba nchini kote, na hivyo kuifanya kampuni ya simu ya Halotel kuwa mtandao ulionea zaidi nchini .


Uchaguzi wa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake Pemba Mhe Suleiman Rarahan Ussi, akiwasuili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi akiongoza na familia yake wakati wa hafla ya kuapishwa leo asubuhi.
Mwakilishi wav Jimbo la Jangombe Mhe Abdalla Maulid Diwani akiwasili katrika viwanja vya Baraza leo asubuhi kuhudhuria hafla ya kuapishwa na kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi.













Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakibadilishana mawazo aliyekaa kutoka kulia Dk Khalid Salum Mohammed Jimbo la Donge, Mhe Abdalla Ali Kombo Jimbo la Mwanakwerekwev na Mhe Hassan Khamis Hafidh wa Jimbo la Welezo, wakiwa katika ukumbi wa Baraza.
Wawakilishi Wateule wakijadiliana wakati wakisubiri kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Tisa kulia Mhe Zaina Abdalla Salum (Viti vya Wanawake) na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Rashid Makame Shamsi.
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakibadilishana mawazo kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliotanguliwa na Uchaguzi wa Spika wa Baraza. aliyesimama Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mhe Mohammed Dimwa waliokaa Mhe Amina Iddi Mabrouk (Viti Maalum) Mwakilishi wa Chaani Mhe Nadir Abdul-latif Yussuf na Mwakilishi wa Jangombe Mhe Abdalla Maulid Diwani. 

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk Yahya Khamis Hamad akiingia ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kuanza Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Tisa kwa kumchagua Spika na kuapishwa Wajumbe Wteule leo asubuhi.

Wajumbe wa Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wamesimama wakati akiingia Katibu wa Baraza kuaza kwa Kikao cha kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe wa Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wamesimama wakati akiingia Katibu wa Baraza kuaza kwa Kikao cha kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe wa Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wamesimama wakati akiingia Katibu wa Baraza kuaza kwa Kikao cha kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Katibu wa Baraza laWawakilishi Zanzibarv Dk Yahya Khamis Hamad akisoma Dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi uchaguzi uliofanyika leo asubuhi.
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakisimama wakati wa Dua kabla ya kuaza shughuli za Baraza Kumchagua Spika leo asubuhi.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akimtambulisha Mgombea Uspika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulidi kwa Wajumbe Wateule wa Baraza wakati wa uchaguzi huo uliofanyika leo asubuhi.katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.  
Mgombea nafasi ya Upika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiomba kura kwa Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi leo asubuhi wakati wa uchaguzi wa kumchagua Spika.  
Afisa wa Baraza la Wawakilishi akigawa kura za kumchagua Spika kwa Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakipiga Kura kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyogombewa na Mhe Zuberi Ali Maulid, na kuibuka mshindi katika uchaguzi huo. 
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakipiga Kura kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyogombewa na Mhe Zuberi Ali Maulid, na kuibuka mshindi katika uchaguzi huo. 
Maofisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitoka katika Ukumbi wa Mkutano na masanduku ya Kutra za Spika baada ya kufanyika kwa Uchaguzi huo wa kumchagua Spika wa Baraza alijitokeza Mgombea mmoja kwa tiketi ya CCM Mhe Zuberi Ali Maulid.  
 Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk Yahya Khamis Hamad akitoka katika Ukumbi wac Mkutano baada ya kuahirisha kwa ajili ya kuhesabiwac Kura za Spika wa Baraza la Wawakilishi baada ya kupigiwa Kura na Wajumbe Wateule. 


Serikali Kusaidiana na Taasisi ya Millen Magese Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa Endometriosis

$
0
0
Na. Andrew Chale.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari, Makurumla na zinginezo za Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada Millen Magese ni za kuungwa mkono hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, anatambua wanawake wengi duniani kote wanasumbuliwa na tatizo hilo ambapo gharama zake kwa kawaida ni kubwa huku bado wataalam wanaendelea kushughulikia namna ya upatikanaji wa tiba yake ili kuweza kuwa nafuu.
“Napongeza juhudi za dhati zinazofanywa na taasisi ya Millen Magese, katika kuunga mkono juhudi za serikali ya tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kuwasogeza wananchi karibu na huduma bora kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii yetu.
Tatizo la kutoshika mimba (kitaalamu Endomytiosis) hutokana na sababu mbalimbali, nyingi zikichangiwa na uelewa mdogo wa jamii inayomzunguka msichana au mama anayejianadaa kuanza kubeba mimba, lakini pia upungufu wa vifaa tiba hospitalini na kwenye vituo vya afya sambamba na kukosekana kwa wataalamu katika hospitali zetu, Hivyo tunapenda kuchukua fursa hii kupongeza juhudi kama hizi za kuandaa semina na warsha ikiwa ni hatua madhubuti na ya msingi katika kuikabiliana na changamoto ya uelewa wa tatizo hili katika jamii.
Kwani, tunaamini, limekuwa jambo la faraja sana, tangu Magesse alipojitokeza hadharani na kuihabarisha dunia juu ya tatizo hili linalomkabili yeye binafsi. Naomba kusema wazi kuwa, huo ulikuwa uthubutu wa pekee wa mrembo huyo, kiasi cha kuifanya jamii kubwa ya kimataifa kuanza kulifuatilia tatizo hili ili kusaidia mabinti wadogo ambao walikuwa hawajakumbwa na hali hiyo. “ alieleza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla katika hotuba yake hiyo.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, ni faraja kubwa kwa watanzania tangu Magese Foundation ilipoanzishwa ikifanya kazi kubwa ya kuhamasisha upatikanaji wa vifaa na pia ujenzi wa hospitali maalumu kwa ajili ya kutibu tatizo hilo. Jambo hilo linaendelea kuitia moyo serikali hususani Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufikia lengo la kumuwezesha mtoto wa kike kufikia malengo tarajiwa.
Kwa upande wake, Mwanadada Millen Magese amewaeleza vijana wa kike katika semina hiyo kuwa, wawe wazi pindi wajisikiapo dalili mbalimbali wakati wanapokuwa katika mzunguko wa siku zao ambapo na kubainisha kuwa, jambo hilo endapo litabainika mapema ni rahisi kulipatia tiba kuliko kuficha na kufika steji mbaya.
Mwanadada, Millen Magese pia alitumia wasaha huo kuishukuru Serikali kwa namna walivyokubaliana kushirikiana naye bega kwa bega katika mapambano dhidi ya tatizo hilo hapa nchini ambapo pia amewashukuru wadau wote kwa kuwa naye dhidi ya mapambano hayo.
Semina hiyo pia imeweza kukusanya watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu wasanii, wanamitindo na wabunigu wa mavazi, wafanyabiashara na wanaharakati wanawake katika maendeleo hapa nchini huku wanaume nao wakijumuika pamoja ilikusambaza ujumbe huo kwa wenza wao na marafiki zao.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
DSC_8330
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mwanadada, Millen Happiness Magese (katikati) pamoja na Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa.
DSC_8338
Mwanadada, Millen Happiness Magese.
DSC_8343
Baadhi ya wanafunzi, wadau wanaosaidiana na mwanadada Millen Magese wakifuatilia semina hiyo.

DSC_8349
Baadhi ya wageni waalikwa, wakiwemo waliowahi kushiriki mashindano ya ulimwende hapa nchini ..wakiwa wamejumuika pamoja kuungana na taasisi ya Millen Magese.
DSC_8353
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo
DSC_8366
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo.
DSC_8370DSC_8388
Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa akitoa hotuba fupi katika semina hiyo
DSC_8382
Baadhi ya wadau walioungana kwa pamoja kusaidiana na taasisi ya Millen Magese wakifuatilia semina hiyo. Mustafa Hassanali pamoja na Rio Paul ambao wote ni wabunifu wa mavazi hapa nchini.
DSC_8478DSC_8394
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,akitoa hutuba yake
DSC_8454
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika semina hiyo.
DSC_8380DSC_8401
Mmoja wa madaktari bingwa wa wanawake wa Hospitali ya Muhimbili akitoa maelezo machache .
DSC_8548DSC_8421DSC_8493DSC_8502DSC_8497
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiendeshwa kwenye semina hiyo..
DSC_8398
Mwanadada Doris Mollel ambaye alikuwa akiongoza semina hiyo akieleza machache wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Dk. Kigwangalla.
DSC_8543
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo machache wakati wa kufunga mkutano huo.
DSC_8606
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Happiness Magese wakipata picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za Sekondari mara baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
DSC_8593
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na Mwanadada Millen Magese.
DSC_8492DSC_8606
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wanafunzi hao.
DSC_8611
Mwanadada Millen Magese akipata 'Selfie' na wanafunzi pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri Dk. Kigwangalla
DSC_8614
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Magese wakifurahia jambo na wanafunzi
DSC_8623
Mwanadada Millen Magese akipata picha ya 'selfie' na wanafunzi waliojumuika katika semiana hiyo
DSC_8576
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata picha ya pamoja na waandaaji wa semina hiyo pamoja na wadau wengine kutoka Serikalini. Semina hiyo imefanyika mapema leo Machi 30.2016, jijini Dar es Salaam.

Kuapishwa kwa Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid.

$
0
0

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akiingia katika Ukumbi wa Mkutano kutangaza Matokeo ya Kura ya Spika wa Baraza baada ya kumalizika kwa Uchaguzi na kuhesabiwa kura. zilizopigwa na Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe Wateule wakiwa wamesimama wakati wa Kuingia kwa Katibu wa Baraza kuendelea na Kikao hicho kutowa matokeo ya Uchaguzi wa Spika. 
Mgombeav Uspika wa Baraza la Wawakilishi akiingia Ukumbini baada ya kutangaza mshindi wa nafasi hiyo ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid kwa ushindi wa kura 75 na kura moja imeharibika.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akitowa maelezo kabla ya kumuapisha Spika mteule Mhe Zuberi Ali Maulid kwa kushinda katika uchaguzi huo kwa kura nyingi. zilizopigwa na Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk Yahya Khamis Hamad akimuapisha Spika Mpya wa Baraza la Tisa Mhe Zuberi Ali Maulid baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo ili kuliongoza Baraza la Wawakilishi kwa Kipindi cha Miaka Mitano.
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akikata utepe Katiba ya Zanzinar na Tanzania na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha. 
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani kwa Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi kwa kumpigia Kura kuweza kuliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano. 

Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano. 
Makamu wa Pili wa Rais Mteule na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe Balozi Seif Ali Iddi na wajumbe wengine wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani zake na kuahidi ushirikiano na Wajumbe wa Baraza katika Kazi zake za Vikao vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani zake kwa Wajumbe hao baada ya kumpa ushindi wa kishindo.

Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad akiwa na wasaidizi wake katika ukumbi wa mkutano wakati Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani kwa Wajumbe wa Baraza.

Magazetini Bongo Tz.

Ujumbe wa Katuni huoooo.....

Tutafika kweli?

$
0
0
Pichani tuiite foleni ya kupata tiketi za MV Mapinduzi 2 Chakechake, Pemba

Miaka ya zamani ilikuwa kila kitu kwa kibiru, ukitaka tiketi ya Sinema kibiru, tulipokuwa tukihangaika na mikate siku za shida ya miaka hiyo kibiru, pia kuliwa na wataalamu wa kibiru, ukiwapa tenda tu wanaingia kazini na kukupatia tiketi yako.

Utaratibu wa foleni ilikuwa ni msamiati usioeleweka.

Kinachoudhi hata ukileta ustaarabu wa foleni atatokea mtu eti anaingia moja kwa moja ndani na kudharau wote mlioko kwenye fulani kisa ana ujamaa na mhusika au na mfanyakazi wa hapo na wakati mwengine bila ya hata kuwaomba.

Tutafika kweli?


Uwanja wa Mao: Lini Utaanza ujenzi wake?

$
0
0



Mchoro wa Uwanja Mpya wa Mpira wa kisasa katika viwanja vya Mao Tse Tung, uliowakilishwa na kampuni ya Uchoraji ya Kichina kwa aliyekuwa Waziri Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Ali Mbarouk, wizarani ili kuona kama kuna mapungufu ili kufanyiwa marekebisho zaidi kabla ya kuanza kwa ujenzi wake.  Kama unavyooonekana pichani

Mchoro huu uliwasilishwa tokea mwaka jana 2015 mwezi Machi.

Takukuru Imewapandisha Kortini Wabunge Hawa Leo

$
0
0
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Lupa Mh. Victor Mwambalaswa.
Wakijadiliana jambo

Dar es Salaam


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewaburuza kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar, wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotuhumiwa kwa rushwa.



Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Mh.Victor Mwambalaswa.



Taarifa zaidi za tukio hilo zitawajia kadri tutakavyozipata.

GPL

Balozi Seif awataka watendaji wawe makini katika kusimamia matumizi ya fedha

$
0
0
 Watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakimpokea na kumkaribisha kuanza kazi Ofisini kwake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar kuendelea kushika wadhifa huo katika kipindi cha Pili cha Awamu ya Saba.
 Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Abdullah Ali Abdullah { Kitole } aliyeinama akinong’onezana kitu na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim kwenye hafla ya kupokea Balozi Seif kuanza rasmi majukumu yake Vuga Mjini Zanzibar.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim akimpongeza Balozi Seif kutokana na juhudi zake zilizopelekea watendaji wa ofisi yake kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano iliyopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwashukuru watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake baada ya kufanyakazi pamoja atika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Picha na – OMPR – ZNZ

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Watendaji wa Taasisi za Umma Nchini wanapaswa kuwa makini katika kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha kwenye Taasisi zao ili kuipa nguvu Serikali kuu kuvuka vyema katika kipindi hichi cha mpito.

Alitahadharisha kwamba kipindi hichi hali ya fedha si nzuri kutokana  na mambo mengi yaliyofanywa katika kipindi kifupi kilichopita ikiwemo suala la uchaguzi Mkuu ambalo limelazimika kutumia fedha nyingi.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wawakilishi wa watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake walipompokea rasmi kuingia ofisini kwake na kuanza kazi mara baada ya kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kushika wadhifa huo katika kipindi chengine cha miaka mitano ijayo.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuendesha Taasisi zake za Umma kwa kutumia fedha inazokusanya kupitia vianzio vyake mbali mbali chini ya usimamizi wa watendaji watakaoonyesha uadilifu kwenye usimamizi huo.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kuchukiwa kwake na baadhi ya watendaji wa Umma wenye tabia mbaya ya kuwekeana chuki katika utekelezaji wa majukumu yao yanayowakabili ya kila siku.

Balozi Seif alisema tabia hiyo potofu  inayolaaniwa hata katika imani  na Vitabu vya  Kidini ikiachiliwa kuendelea hatma yake inaweza kuzaa uadui utakaoleta hasara kubwa hapo baadae.

Aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi pamoja na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kwa kazi kubwa waliyoifanya iliyomuwezesha kutekeleza majuku yake ya ufanisi mkubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Balozi Seif aliwanasihi Viongozi na watendaji hao kuendelea kushirikiana na kushikamana kwa kufanya kazi kama ndugu wamoja ili kazi ya Utumishi waliokabidhiwa na Taifa ifikie malengo yaliyokusudiwa.

Alisema zipo kasoro, changamoto na hata mikwaruzano iliyojitokeza na kupelekea kukoseana baina ya baadhi ya watendaji na Viongozi hao akiwemo na yeye pia ndani ya kipindi kilichopita cha miaka mitano. Hivyo njia pekee ya kuzishinda changamoto na kasoro hizo ni kusameheana ili kufuta kasoro hizo.

Mapema Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim kwa niaba ya watendaji wa Ofisi hiyo amempongeza Balozi Seif kwa kuteuliwa tena kushika wadhifa huo.

Nd. Ahmad alisema ndoto na dua za Viongozi na Watendaji wa Taasisi za Ofisi hiyo zimesibu kwa Mwenyezi Muungu aliyempa ilham Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kumteua tena Balozi Seif kuendelea kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Alisema ahadi waliobeba Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni kushirikiana nae bega kwa bega kadri ya uwezo wao kiutendaji ili kufanikisha majukumu yao kwa upeo mkubwa zaidi.

Nyumba inauzwa!

$
0
0







Ipo Maungani ina vyumba vinne na vyoo vitatu. Ni ya kisasa na ipo katika hali nzuri. 

Pia katika uzio (fence) kuna banda la mtumishi au mfanyakazi ambalo lina chumba, choo, jiko na stoo.

Bei ni shs 95,000,000 kwa maelezo Zaidi au kuiona piga simu namba 0777275551 ulizia Khalid

Makamu wa Rais, Mhe Samia akutana na naibu Waziri wa Katiba na Sheria leo

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Ndugu Amon Mpanju wakati Naibu Mpanjo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo March 31, 2016.(Picha na OMR)

Hafla ya Kuapishwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ikulu Jana.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akisalimiaiongozi wa Dini alipowasili Ikulu Zanzibar kuhudhuria hafla ya kuapisha na Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Makamu wa Rais Mteuli Balizi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mshauri wa Rais Utamaduni Mhe Chimbeni Kheri alipowasili Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kuapisha kushika nafasi hiyo kwa mara ya Pili.cha miaka mitano.
Balosi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib Ikulu Zanzibar wakati wa hafla hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi akipitia hati ya kiapio kabla ya kuahafla hiyo ya kuapishwa kushika nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mara ya Pili, akiwa na Mkewe Mama Asha Balozi Seif.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid wakihudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
Waheshimiwa Washauri wa Rais wa Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Ikulu Zanzibar.
Viongozi wa Dini Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ikulu Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwasili katika ukumbi wa hafla ya kumuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Ikulu Zanzibar.,  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizi Seif Ali Iddi,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar, 30-3-2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizi Seif Ali Iddi,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar, 30-3-2016.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada kumaliza hafla ya kumuapisha Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na familia yake baada ya hafla hiyo ya kuapishwa jana 30-3-2016 Ikulu Zanzibar. 

Magazetini Bongo Tz.

Viewing all 36091 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>