Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36091 articles
Browse latest View live

Hafla ya Kuapishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.

$
0
0
Spika wa Baraza loa Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitowa maelezo kwa Wajumbe Wateuli kwa ajili ya kuanza kula Kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi baada ya kuanza kwa Baraza hilo.
Waheshimiwa wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi kabla ya kuaza zoezi la kuapishwa Wajumbe wa Baraza kwa ajili ya kuaza kazi yao waliotumwa na Wananchi kuwawakilisha. wakwanza Mhe Rashid Ali Abdalla Jimbo la Amani na Mhe Mihayo Juma N'hunga. Jimbo la Dole.
Wajumbe wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza wakifuatilia utaratibu wa kuaza zoezi la
kuapishwa.wakwanza Mhe Amina Iddi Mabrouk (Viti vya Wanawake) Mhe NadirAbdul-latif Yussuf (Jussab) Mwakilishi wa Chaani na Mhe Abdalla Maulid Diwani wa Jimbo la Jangombe.
Waheshimiwa Viti vya Wanawake wakifuatilia zoezi hilo wakati wakimsikiliza Spika akitowa maelezo ya utaratibu wa kuapishwa.. 
Waheshimiwa wakiwa Ukumbi wa Mkutano wa Baraza wakimsikiliza Spika Mhe Zuberi Ali Maulid.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akimuapisha Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe Balozi Seif Ali Iddi, akishuhudia Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad.  
Spika Mhe Zuberi Ali Maulid akimkabidhi nyezo za kufanyika kazi Katiba ya Zanzibar, Katiba ya Tanzania na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi Mhe Balozi Seif Ali Iddi baada ya kula kiapo ya Utii cha Baraza la Wawakilishi. 
Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe Abdalla Ali Kombo akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar Mhe Said Hassan Said akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishin Zanzibar. 
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Mhe Abdalla Maulid Diwani akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbe Pemba,Mhe Ali Khamis Bakar akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid.  
Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe Ali Salum Haji akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubri Ali Maulid na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad.
Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar Mhe Ali Suleiman Ali (Shihata) akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Nungwi Zanzibar Mhe Ame Haji Ali, akila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.  
Mwakilishi wa Viti vya Wanawake Mhe Amani Iddi Mbarouk akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa zoezi hilo la kuapishwa Wajumbe wa Baraza kwa ajili ya kuaza kazi rasmin.
Mwakilishi wa Jimbo la Kiwengwa Mhe Asha Abdalla Mussa akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad. 
Mwakilishi wa Jimbo la Chamani Pemba Mhe Bahati Khamis Kombo akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake Mhe Bihindi Hamad Khamis akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakiolishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mhe Chum Kombo Khamis Mwakilishi kupitia Viti vya Wanawake akitia saini hati yake ya kiapo baada ya kuapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Zanzibar Mhe Haji Omar Kheri akila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. 
Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Pemba Mhe Hamad Abdalla Rashid akila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Nafasi za Wanawake Mhe Hamida Abdalla Issa akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo Zanzibar Mhe Hamza Hassan Juma akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mhe Haroun Ali Suleiman wa Jimbo la Makunduchi Zanzibar akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Wete Pemba,Mhe Harusi Said Suleiman akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidh akila kiapo cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar mbele ya Mhe Sipa wa Baraza la Wawakilishi Zuberi Ali Maulid na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad.
 Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi kupita Nafasi za Wanawake Hidaya Ali Makame akila kiapo chake mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid.
 Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Zanzibar Mhe Hussein Ibrahim Makungu, akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar mbele ya Spika wa Baraza Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Zanzibar Mhe Issa Haji Ussi (Gavu) akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi wakati wa zoezi la kuapishwa Wawakilishi wapya wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 
 Mwakilishi wa Jimbo la Paje Zanzibar Mhe Jaku Hashim Ayoub, akitia saini hati yake ya kiapo baada ya kuapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad.
 Mwakilishi wa Jimbo la Kijini Zanzibar Mhe Juma Makungu Juma akila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
 Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe Zanzibar Mhe Khadija Omar Kibano, akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Malindi Zanzibar Mhe Mohammed Ahmada Salum akila Kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad. 
 Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Mohammed Said Mohammed Dimwa akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar mbele ya Mhe Spika Zuberi Ali Maulid. 
Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Zanzibar Mhe Mtumwa PayaYussf akila kiapo cha Utii wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Kupitia Nafasi za Wanawake Mtumwa Suleiman Makame. akila kiapo chake cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Ole Pemba  Mhe Mussa Ali Mussa akilia Kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
 Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani Pemba,Mhe Mussa Foum Mussa akila kiapo cha Utii mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
 Mwakilishi wa Jimbo la Chukwani Zanzibar,Mhe Mwanaasha Khamis Juma, akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
 Mwakilishi kupitia Nafasi za Wanawake Mhe Mwanaidi Kassim Mussa, akila kiapo cha Utii.
 Mjumbe wa Wawakilishi Kupitia Nafasi za Watu Wenye ulemavu Mhe Mwantatu Mbaraka Khamis akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. 
 Mwakilishi Jimbo la Dimani Zanzibar Dk Mwinyihaji Makame Mwadini akila kiapo cha Baraza la Wawakilishi mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
 Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdul-latif Yussuf (Jussab) akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa zoezi hilo la kuapishwa Wajumbe wapya wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salim Ali Jazira akiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid.
Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba Mhe Omar Seif Abeid akiapa mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid. 
 Mwakilishi wa Viti Vya Wanawake Mhe Panya Ali Abdalla akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Amani Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid. 

Ujumbe wa Katuni huuuooo...

Ligi ya Sita Bora Daraja la Kwanza Taifa Kati ya Mundu na Idumu Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao 1--1.

$
0
0
Wapenzi wa Timu Idumu wakishangilia timu yao wakati wa Mchezo wao wa Ligi ya Sita Bora Daraja la Kwanza Taifa kuwania kupanda daraja kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.

















Bongo Magazetini Tz.

Mandhari ya Barabara ya Amani Kwerekwe Ikiwa imepamba na Taa za Solar.

Tanzania na Burundi Zatakiwa Kuregeza Msimamo Ndani ya EAC

$
0
0
Mwenyekiti wa shirikisho la waajiri la jumuiya ya Afrika Mashariki(EAEO),Rosemary Ssenabulya akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivikaribuni kuhusu mafanikio na changamoto za shirikisho hilo,kushoto kwake ni katibu wa shirikisho hilo,Agrey Mlinuka na kulia kwake ni mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la waajiri nchini Kenya,Jacqueline Mugo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Tanzania  na Burundi zimeombwa kulegeza misimamo yao kwa kuondoa gharama za vibali vya kufanya kazi kwa raia wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kama zilivyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya ambazo nazo ni wanachama wa jumuiya hiyo.

Akizungumza jijini Arusha hivikaribuni Katibu wa Chama cha Waajiri Afrika Mashariki (EAEO), Aggrey Mlinuka alisema kuwa hadi sasa nchi za Tanzania na Burundi ndizo nchi pekee zilizobakia katika kutoza gharama za vibali vya wageni hasa raia wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mlimuka alisema kuwa mbali na nchi hizo kuondoa utaratibu huo pia amependekeza kwamba utaratibu wa utoaji vibali hivyo usichukua muda mrefu kama ilivyo sasa kwa nchi za Tanzania na Burundi na kushauri muda wa kuchukua vibali hivyo haustahili kuzidi siku 30.

Katibu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) alisema kuwa  chama chao kiliwasilisha mapendekezo hayo mbele ya  Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera ambaye anamaliza muda wake April 20 mwaka huu.

“EAEO na Sezzibera tumefanya kazi kubwa kuhakikisha jumuiya inasonga mbele kwa kasi kubwa mbali na changamoto zilizopo katika nchi moja moja, lakini tuna uhakika tutazitatua kwa manufaa na maslahi ya wana jumuiya wote,” alisema Mlinuka.

Alisema kuwa Katibu Mkuu mpya Liberata Mfumukeko kutoka kutoka Burundi anatakiwa kuendeleza pale ambapo Dk Sezzibera anapoishia ambapo ni kuhakikisha kwamba unakuwepo utatu wa ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mbali na hilo pia amemtaka katibu mkuu huyo mpya kuhakikisha protokali ya soko la pamoja kipengele cha pili cha jumuia ya Afrika Mashariki kinatekelezeka ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya wananchi kuingiliana kutoka sehemu moja kwenda nyingine kibiashara pamoja na kutafuta ajira ndani ya nchi wanachama.

Awali Mwenyekiti wa chama cha waajiri Kenya(FKE) Jacqueline Mugo alisema kuwa nchi wanachama hazipaswi kuwa na uoga katika yale ambayo yanaonekana kuwa na manufaa na uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki yakiwemo masuala ya ajira na mengineyo. 

Mkutano wa siku moja ulikutanisha vyama vyote vya waajiri wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki vikiwa na malengo ya kuhakikisha wananchi wa jumuiya hiyo wanapata ajira popote pale wanapokwenda ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

SMZ kwa Kushirikiana na AFDB Kuimarisha Miundombinu ya Barabara Zanzibar.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua Warsha ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri { TSSP } iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibae Beacha Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kaimu Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja akifafanua hatua zitakazochukuliwa katika hatua za utekelezaji wa Mradi wa mpango wa uimarishaji wa sekta ya usafiri.
Balozi Seif aliyepo kati akti akiwa pamoja na Viongozi wa Warsha ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri iliyofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Miundombnu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio, Kaimu Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja na kulia ya balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unaguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Khamis Mussa.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri iliyofanyika huko Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Balozi Seif aliyepo kati kati ya waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja washiriki wa warsha ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Viongozi wa warsha ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri mara baada ya kuizindua rasmi hapo Zanzibar Beach Resort.(Picha na – OMPR – ZNZ.)

Na Othman Khamis OMPR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika { AFDB } inatarajia kujenga  Barabara  Nne zenye urefu wa Kilomita 51.78 katika azma yake ya kuimarisha sekta ya mawasiliano ya usafiri wa ardhini hapa Nchini.

Ujenzi wa Bara bara hizo Nne  za Zanzibar unajumuisha sambamba  na zile za Tanzania Bara  zitakazopata msukumo wa ufadhili kupitia Mfuko huo wa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika zote zikiwa na urefu wa Kilomita Mia 462.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo kwenye Warsha  ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri { TSSP } iliyofanyika  Zanzibar Beach  Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kushirikisha wataalamu wa sekta ya usafiri, watendaji wa Serikali pamoja na wawakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Balozi Seif alisema mradi wa Bara hizo ni pamoja na zile za Bububu – Mahonda – hadi Mkokotoni wenye  wenye urefu wa Kilomita 31, Pale – Kiongele Kilomita 4.6, Fuoni – Kombeni  Kilomita 8.6 na Matemwe – Muyuni Kilomita 7.6.

Alisema ushirikiano wa karibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na washirika wa maendeleo umeiwezesha miundombinu ya bara bara  zenye urefu wa Kilomita 90 kuimarika  ndani ya kipindi cha miaka Mitano iliyopita zikiwa katika kiwango kinachokubalika Kimataifa .

Alifahamisha kwamba Serikali kupitia mfuko wa Bara bara Zanzibar {ZRF } iliongeza bajeti  yake kwa ajili ya matengenezo ya Bara bara kutoka shilingi Bilioni 5 mwaka 2011 hadi shilingi Bilioni 7.3 mwaka uliopita wa 2015.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba kuanza kwa miradi hiyo ya ujenzi wa Bara bara za Zanzibar kwa upande mwengine kutatoa fursa za ajira  1,500 kwa baadhi ya wananchi hasa Vijana.

Alisema fursa hizo pia zitaibua ajira  za muda zipatazo 3,000 katika kazi za matengenezo ya bara bara zinazoharibika kutokana na matumizi mbali mbali ikiwemo kuharibika kwa mvua.

Balozi Seif aliupongeza Uongozi na Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika chini ya usimamizi wa Mwakilishi wake hapa Nchini Dr. Tonia Kandiero kwa juhudi wanazochukuwa katika kusaidia Maendeleo ya Nchi changa hasa zile zilizomo katika ukanda wa jangwa la sahara.

Alisema mbali ya kuunga mkono nguvu za uimarishaji wa sekta ya Bara bara lakini pia Benki hiyo imeonyesha nia yake thabiti ya kusaidia uendelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo na ustawi wa jamii nchini.

Balozi Seif alisema ipo miradi ya Afya, Elimu, Kilimo, Huduma za Maji safi na salama pamoja na mafunzo ya kuijengea Jamii namna ya kuishi katika misingi ya utawala  Bora ambayo imepata msukumo wa Benki hiyo kupitia Mpango wa kuunga mkono Sekta ya Usafiri { TSSP }.

“ Benki ya Maendeleo ya Afrika imeanza kutoa huduma zake  Zanzibar tokea mwaka 1998 kwa kusaidia ujenzi wa Bara  bara Tano zenye urefu wa Kilomita 88.3 ambazo ni Kinyasini – tunguu, Paje – Makunduchi, Mazizini – Fumba na Amani – Dunga ”. Alifafanua Balozi Seif.

Mapema kaimu mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja alisema Taasisi hiyo ya kifedha kwa maendeleo ya Mataifa ya Bara la Afrika imejikita zaidi katika kuona mipango ya Mataifa hayo kama ile ya kupunguza Umaskini { MKUZA na MKUKUTA } inafanikiwa vyema.

Bibi Minja alisema Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri { TSSP } umeanza kubuniwa rasmi Tarehe 26 Novemba mwaka 2015 na kufikia hatua ya kuwekwa saini mkataba wake mnamo tarehe 4 Disemba mwaka 2015.

Kaimu Mwakilishi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja alifahamisha kwamba mradi mzima wa ujenzi wa bara hizo unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 270.95 sawa na shilingi Trilioni 1.3za Kitanzania.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Mradi  huo wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri { TSSP } Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio alisema kwamba maendeleo ya Taifa lolote duniani hutegemea kuimarika kwa Sekta ya mawasiliano ya usafiri.

Dr. Malik alisema Wizara anayoisimamia imepewa jukumu la kusimamia jukumu hilo kazi ambayo imekuwa ikipata  mafanikio kutokana na nguvu ya pamoja kati ya Serikali  na washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi.

Warsha  hiyo ya siku moja  ya uzinduzi wa  Mradi  wa Mpango wa uimarishaji  wa  Sekta ya Usafiri imejadili mada Nne muhimu miongoni mwake ni pamoja na sheria na taratibu za manunuzi, ujenzi wa bara bara zilizomo ndani  ya mradi huo pamoja na ripoti ya fedha  na ukaguzi wake.

Magazetini Bongo Tz.


Rais wa Zanzibar Dk Shein Alizindua Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.

$
0
0

Balozi Mdogo wa China Zanzibar akiwasili katika Jengo la Baraza la Wawakilishi kuhudhuria Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohanmed Shein, 5-4-2016. Chukwani Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China Zanzibar akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilisahi Zanzibar wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 
Balozi wa Heshima wa Uingereza Zanzibar akiwasili katika Jengo la Baraza la Wawakilishi kuhudhuria Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohanmed Shein. Chukwani Zanzibar.
Balozi Mdogo wa Msumbiji Zanzibar akiwasili katika Jengo la Baraza la Wawakilishi kuhudhuria Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohanmed Shein, Chukwani Zanzibar.
Spika Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho akiwasili katika jengo la Baraza kuhuduria Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakiliashi Zanzibar.
Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame na Katibu wa Baraza Dk Yahya Hamah Khamis, wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kulizindua Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid wakati akiwasili katika viwanja vya Baraza kuhudhuria Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakiolishi akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea saluti ya bwarifde Maalum lililoandaliwa kwa ajili ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikagua bwaride Maalum la Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiingia katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi akiongozana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid, kwa ajili ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.  
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakisimama wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, akiingia katika Ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya Uzinduzi wa Baraza jipya la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akizungumza na Wajumbe kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar kulihutubia na kulizindua Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid wakiwa katika ukumbi wa Mkutano.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akiwa katika ukumbi wa Baraza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa. 
Wajumbe wa Baraza wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid wakiwa katika ukumbi wa Mkutano.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akilihutubia na kulizindua rasmin. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar akilihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo. 
Mabalozi Wadogo wa Nchi za India, Msumbiji, na China wakiwa katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi wakifuatilia hutuba ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia uzinduzi wa hutuba ya Rais wa Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Tisa. 
Waziri Jamuhuri Makamba, Spika Mstaaf wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakifuatilia hutuba ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar ikitolewa na Rais wa Zanzibar  Dk Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa katika picha ya pamoja na Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar baada ya kuliozindua na kulihutubia. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar baada ya kuliozindua na kulihutubia. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kulihutubia na kulizindua rasmin kuaza kazi yake ya Kutunga Sheria Zanzibar.

Wawakilishi wachagua Tume ya Bajeti

$
0
0
Na Takdir Ali, Maelezo-Zanzibar

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi, leo wamewachagua wajumbe watano kuunda Tume ya Bajeti ya Baraza hilo.

Waliopita katika uchaguzi huo na kura walizopata zikiwa kwenye mabano, ni Hamza Hassan Juma (71), Salha Muhammed Mwinjuma (69), Lulu Msham Abdallah (72), Rashid Ali Juma (71) na Hamad Abdallah Rashid aliyepata kura 70.

Akizungumza kabla ya uchaguzi huo, Naibu Spika Mgeni Hassan Juma,  amewaambia wajumbe hao kwamba tume ya bajeti ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chombo hicho.

Kwa hivyo aliwataka kufanya kazi zao kwa umahiri, weledi na uaminifu ili kuisaidia serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo. 

Wakitoa shukurani zao, wajumbe hao wateule wamewashukuru wajumbe wa baraza hilo kwa kuonesha imani kubwa kwao, na kuahidi kutumia uzoefu walionao kuhakikisha masuala ya bajeti yanakwenda vizuri.

Hamza Hassan Juma, alisema kamati iliyo imara, italiwezesha baraza kuwa madhubuti na kuipitia vyema bajeti kabla ya kuwasilishwa vikaoni.

Aidha amewataka wajumbe hao wawape ushirikiano kikamilifu ili lengo la kamati hiyo liweze kufikiwa.


Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba ahimiza ukusanyaji wa mapato ya Serikali

$
0
0
Na Masanja Mabula –Pemba 
 
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na Baraza la Mji Wete, ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake , atatumia nguvu alizonazo  kisheria  kumuweka rumande masaa 24 , kwani atakuwa ni chanzo cha kukosekana mapato ya Serikali .
 
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mfanyabiashara kukata leseni za biashara yake ili aweze kuchangia mapato ya Serikali Kuu ambayo baadaye hurejea kusaidia miradi ya maendeleo ya wananchi .
 
Alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa na muhali, jambo ambalo alisema  serikali ya Mkoa haitalivumilia .
 
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Wete na Micheweni , watendaji wa Baraza ka Mji wete pamoja na watendaji kutoka Serikali za Wilaya juu ya kuimarisha suala la ukusanyaji wa mapato
 
Aidha aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya  na Baraza la Mji Wete kuondoa muhali katika suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha wafanya biashara wanakata leseni za biashara zao.
 
“Ninao uwezo na nguvu kisheria wa kumweka rumande mtumishi wa Serikali masaa 24 , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake, mimi sitangoja kutumbuliwa jipu nitaanza  na atakaye onyesha uzembe katika agizo hili ”alieleza.
 
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo amesema  haitalivumilia .
 
Pia aliwataka kutumia lugha nzuri kwa wateja wao kwa kuwaelimisha , na wakiendelea kukaidi wawafiishe ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa hatua zaidi .
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni  Abeid Juma Ali amewasisitiza watendaji wa Halmashauri na baraza la Mji kufuata sheria na miongozo wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi zao 

 Alisema kwamba iwapo sheria zitatumika ipasavyo kila mfanyabiashara atakata leseni yake bila ya usumbufu na kuwasisitiza kuwachukulia hatua wanaoendesha biashara bila ya kuwa na leseni .
 
“Sheria zipo lakini hazitumiki , zitumieni kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara abakuwa na leseni na ambaye anakiuka mchukulieni  hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani ”alifahamisha .
 
Akichangia katika Mkutano huo , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Wete Mmanga Juma Ali  alisema ili kuzipatiwa ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanahitaji kupatiwa askari watakaoongozana nao kupita madukani na kudai leseni .
 
Alisema kuwa kipindi cha vuguvugu la kisiasa , mapato ya Halmashauri yamepungua kutokana na wafanyabiashara wengi kuendesha biashara bila ya kukata leseni .

President John P. Magufuli to visit Rwanda 6-7 April

$
0
0
Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli will tomorrow, April 6, visit Rwanda-his maiden regional visit.

KT Press has established that President Magufuli, who has made global headlines for his rapid leadership changes in the East African nation, will be in Rwanda for a two-day working visit.

The visit will begin with his official opening of Rusumo one stop border post connecting the two countries, before holding a joint press conference with President Paul Kagame.

On his 2nd day, Magufuli will join Rwandans for the 22nd commemoration of the genocide against Tutsi on Thursday, April 7.

On the day when Rwandans mourn over 1 million Tutsi who perished during the genocide, Presidents Magufuli and Kagame along with the First Ladies, will lay a wreath and lighting the memorial flame.

Later on, they will join Rwandans in a ‘Walk To Remember’, before attending a night vigil at Amahoro National Stadium in the capital Kigali.

What does Magufuli’s presence mean to Rwanda?

Tanzania is one of Rwanda major trade partners and a close ally too. The port of Dar-es-Salaam is crucial for Rwanda’s trade routes, accounting for roughly 70% of all Rwandan international maritime trade. A healthy relationship must exist to maintain this economic partnership.


For example, the port handles 60% of Rwanda’s exports and imports, making it a key port in terms of handling Rwandan cargo.

Again, Rwanda regards Tanzania’s central corridor, which combines road and railway network, as an essential trade and transport route linking it with neighbouring Burundi, Uganda and the eastern part of Democratic Republic of Congo. This is a great assets for the two countries.

Socially, many Rwandans, particularly those where were boar there and others lived there, have for so many years regarded Tanzania as their second home.

President Kagame has expressed his admiration for the new Tanzania President, especially his immediate stance on corruption.

On Novemer 5 last year, Kagame flew to Tanzania’s capital Dar-Es-Saram to attend the swearing in ceremony of President Magufuli.

In just six months, President Magufuli has been reluctant to travel both abroad and inside Tanzania, since he was sworn in as the President.

He has so far been in Dar-es-Salaam Statehouse and only traveled to Arusha, Mwanza, Morogoro and Geita regions.

He has been assigning his Prime Minister Majaliwa Kasim to travel to other parts of the country in a move to solve various political and socio-economic problems.

His courtesy visit to Kigali sets a strong and positive precedence and also rings a resounding tone of cultivating a stronger bilateral relationship.

Kesi ya Kupinga Matokeo ya Ubunge Jimbo la Vunjo, Mrema Akubali Yaishe, Amtambua Mbatia Kama Mbunge Halali wa Jimbo la Vunjo.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MBUNGE wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP)  Augustine  Lyatonga Mrema .

Mbatia ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa mlalamikaji (Mrema) kuamua kufuta shauri hilo kwa hati maalumu iliyowasilishwa katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi huku akikiri kumtambua Mbatia kama mbunge halali wa jimbo hilo.

Mbali na utambuzi huo Mrema pia amekanusha maelezo pamoja na ushahidi wake aliowasilisha mahakamani hapo dhidi ya Mbatia,wananchi wa jimbo la Vunjo pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ambazo zilitajwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi wake.

Ukiwasilisha hoja mahakamani hapo mbele ya Jaji wa mahakama kuu Lugano Mwandambo , upande wa mlalamikaji ukiongozwa na wakili January Mkobogho ulieleza kuwa pande mbili katika shauri hilo wamefikia makubaliano nje ya mahakama.

 Wakili Mkobogho aliiomba mahakama kuona makubaliano hayo ambayo yako katika maandishi kama alama kwa mujibu wa makubalinao waliyoafikiana baada ya kuingizwa na kupokelewa mahakamani hapo kama madai.

 Alisema kwa kuwa kesi hiyo ya uchaguzi ikiwa na maslahi mapana ya umma na kwa kuwa mlalamikiwa wa pili na watatu waliunganishwa kwenye shauri hili kwa mujibu wa sheria aliomba kila upande ubebe gharama zao.

Wakili Mkobogho alieleza kuwa kutokana na pande  zilizokuwa zinakwaruzana  wameamua kukaa na kumalizana wenyewe na kwamba haoni sababu za mlalamikiwa wa pili na watatu kutokubeba gharama zao wenyewe.

Jopo la mawakili sita wa upande wa utetezi ukiongozwa  na wakili , Mohamed Tibanyendera uliileza mahakama hiyo kwamba wanaungana na mtoa maombi kwa maslahi ya umma na kwamba wanakubali kila upande kubeba gharama zake.

Wakili mkuu wa  serikali Mark Muluambo akisaidiana na wakili wa serikali Grayson Orcado , alisema wamesikia pande zote na wameafiki kuhusiana na uamuzi huo kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi kwa umma.

Alisema upande wao hauna pingamizi na maamuzi hayo na kwamba wamekili kupokea nakala na wataisoma na kuipitia vizuri, na kutokana na mlalamikiwa wa pili na watatu walitumia gharama katika kesi hiyo waliiomba mahakama  walipwe nusu ya gharama hizo. 

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande hizo mbili Jaji Mwandambo alieleza kupata maelezo kuwa mlalamikaji amekiri kwamba kesi hiyo hainafaida yeyote kwa wana Vunjo na kwamba amekubali kuwa tuhuma zake zote alizokuwa nazo juu Mbatia na watu wote aliokuwa anawahusisha na kesi hiyo kuwa amezitengua .

Jaji Mwandambo alieleza kuwa mlalamikaji  pamoja na yote aliyoyasema  pia amekiri kuwa mbunge wa sasa wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia alichaguliwa kwa  kura halali na alipata kura nyingi dhidi yake.

Nje ya mahakama Wakili Tibanyendera alisema haikuwa kazi rahisi kufikia maridhiano haya na kwamba ushawishi mkubwa umefanyika baada ya Wakili anyemtetea Mrema kumueleza ukweli mwenendo wa shauri hilo.

“Tumefanya kazi ya kuwashawishi wateja wetu ,Mrema amekiri katika maandishi yaliyosajiliwa leo mahakamani baada ya kuona kwamba kesi hii haina faida kwa wana vunjo,amekiri na kutengua tuhuma zake zote alizotoa dhidi ya Mbatia,wafuasi wake na taasisi nyingine.”alisema Tibanyendera.

“Hoja kubwa ilikuwa ni kupinga matokeo ya Ubunge,Mrema kwa maandishi amekiri kwamba Mbatia alichaguliwa kihalali na akapata kura nyingi kihalali,hayo yamo katika amri wa mahakama,”alisema Tibanyendera.

Akizungumza mara baada ya kufikiwa kwa uamuzi huo Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia alisema Chama chake kina aamini katika itikadi za utu na kwamba amemsamehe na hata dai gharama za kesi hiyo.

“Tungeweza kumdai Mrema gharama kubwa,tangu kuletwa kwa kesi hiyo mahakamani,mimi sitamdai Mrema hata senti moja,nimemsamehe Mrema kwa sababu ni mpiga kura wa jimbo la Vunjo,nisingependa kuona anadidimia zaidi lazima ni mlee vizuri mzee wngu Mrema,”alisema Mbatia.

“Gharama za mawakili talipia asilimia 50 za mawakili wa upande wetu,Mrema amekubali kulipa sehemu ndogo ya malipo ya mawakili wetu, tungeendelea tungeweza kuuza hata nyumba zake, sasa atalipa Milioni 40 na tayari kwa hatua ya kwanza mawakili watapewa Mil 15 ambazo tayari ziko mahakamani,mwezi ujao atalipa Mil 15 na kabla ya mwezzi wa sita atalipa Mil 10 “aliongeza Mbatia.


 Mbatia aliyekuwa amengozana na mawakili wake pamoja na baadhi ya wafuasi wa chama cha NCCR-Mageuzi  alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Vunjo waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo .

“Niwashukuru wananchi wa jimbo la Vunjo kwa ushirikiano  na muda mwingi uliopotea kwa ajili ya kufuatilia kesi hii ,yapo mengi ambayo tulitakiwa kuanza kuyafanya lakini muda mwingi tulitumia katika kushughulikia shauri hili “alisema Mbatia.

Upande wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa ukiongozwa na Mawakili Mohamed Tibanyendra, Faith Sadala ,Youngsevior Msuya na Mike Kavala huku Mawakili wa serikali wakiwa ni Mark Mluambo Helen Mwajage na Lilian Machange.

Katika uchaguzi huo Mbatia alitangazwa mshindi kwa kupata kura 60,187 huku Mrema akiambulia kura 6,416, na mgombea wa CCM, Innocent Shirima, kura 16,097.

Yaliyojiri Siku ya Uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Ujumbe wa Katuni Huuuooo......


Mhe. Omar Awataka Afisa wa Mji wa Wete Kukusanya Mapato.

$
0
0
Na Masanja Mabula –Pemba. 
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na Baraza la Mji Wete  , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake , atatumia nguvu alizonazo  kisheria  kumuweka rumande masaa 24 , kwani atakuwa ni chanzo cha kukosekana mapato ya Serikali .
 
Aliesema kuwa ni wajibu wa kila mfanyabiashara kukata leseni za biashara yake ili aweze kuchangia mapato ya Serikali Kuu ambayo baadaye hurejea kusaidia miradi ya maendeleo ya wananchi .
 
Alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo alisema  serikali ya Mkoahaitalivumilia .
 
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Wete na Micheweni , watendaji wa Baraza ka Mji wete pamoja na watendaji kutoka Serikali za Wilaya juu ya kuimarisha suala la ukusanyaji wa mapato
 
Aidha aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya  na Baraza la Mji Wete kuondoa muhali katika suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha wafanya biashara wanakata leseni za biashara zao.
 
“Ninao uwezo na nguvu kisheria wa kumweka rumande mtumishi wa Serikali masaa 24 , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake , mimi sitangoja kutumbuliwa jipu nitaanza   na atakaye onyesha uezembe katika agizo hili ”alieleza.
 
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo amesema  haitalivumilia .
 
Pia aliwataka kutumia lugha nzuri kwa wateja wao kwa kuwaelimisha , na wakiendelea kukaidi wawafiishe ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa hatua zaidi .
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni  Abeid Juma Ali amewasisitiza watendaji wa Halmashauri na baraza la Mji kufuata sheria na miongozo wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi zao 

 Alisema kwamba iwapo sheria zitatumika ipasavyo kila mfanyabiashara atakata leseni yake bila ya usumbufu na kuwasisitiza kuwachukulia hatua wanaoendesha biashara bila ya kuwa na leseni .
 
“Sheria zipo lakini hazitumiki , zitumieni kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara abakuwa na leseni na ambaye anakiuka mchukulieni  hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani ”alifahamisha .
 
Akichangia katika Mkutano huo , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Wete Mmanga Juma Ali  alisema ili kuzipatiwa ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanahitaji kupatiwa askari watakaoongozana nao kupita madukani na kudai leseni .
 
Alisema kuwa kipindi cha vuguvugu la kisiasa , mapato ya Halmashauri yamepungua kutokana na wafanyabiashara wengi kuendesha biashara bila ya kukata leseni .

Taarifa kwa Umma;Kufutwa kwa Safari za Ndege APRILI 2, 2016

$
0
0


Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba  idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa kufika kwenye maeneo  waliyokusudia  jioni ya Aprili 2, 2016.

Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa taa kwenye njia ya  kurukia  kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na hivyo kukosekana kwa usalama  ambao ungewawezesha marubani wetu  kutua.

Huu ni mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha  kufutwa kwa ndege mbili miongoni mwa ndege zetu kutua  usiku ule:

  • Ndege Na. FN157 iliondoka kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa  3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda  unaotakiwa  saa 4.40 usiku. Wakati ndegte ikikaribia  Uwanja wa Kilimanjaro marubani wetu walijulishwa  na mnara wa kuongozea ndege  kwamba taa zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege  zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa  muda usiokuwa mrefu. Ndege ilizunguka  uwanja wa Kilimanjaro  ikisubiri  ukarabati wa taa hizo kwa  takribani  dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi.
  • Ndege iliwasili tena Dar es Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye  ukumbi wa kusubiria ndege  wakati ndege  ikijazwa mafuta tena na marubani wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari  kurudi Kilimanjaro mapema kadri  iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia ndege  ukikamilika. Kwa bahati mbaya taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi  hadi kufikia saa  saa 7.00 usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016,  ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa  ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa walishakuwa  kazini kuanzia saa 12.30 jioni.
  • Hii inamaanisha kwamba  hatukuwa na mbadala wa kufuta  safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo ilikuwa  irudi  kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam.
  • Abiria wetu waliopata usumbufu walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia  na ilisafiri kutoka uwanja wa pili  kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira  walichukua mbadala huu lakini wengie waliamua kubaki  katika uwanja wa ndege  kusubiri ndege  iliyofuata.
  • Abiria wote  walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege iliyofuata walisafiri nasi kwa  kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016.

  • Tunaomba radhi kwa abiria  wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu  walioupata huku tukiwahakikishia kuwa tunaweka kipaumbele kikubwa  kwenye usalama wa abiria wetu na marubani.

John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet Tanzania

Spika wa Baraza la Wawakilishi Awaapisha Wajumbe Walioteuliwa na Rais leo.

$
0
0
Ali Issa Maelezo, Zanzibar.
Mwakilishi mteule wa Chama cha Alliance for Development Change (ADC) Hamad Rashid Mohammed, amemuomba Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, atakapounda serikali achague watendaji wenye utaalamu wanaoweza kuisaidia serikali kuinua uchumi wake.

Akichangia hotuba ya Rais baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Rashid amesema kupewa nafasi kwa wataalamu kutaisaidia serikali kufikia malengo inayojipangia kwa kuwaletea maendeleo wananchi.

Mwakilishi huyo aliyegombea urais wa Zanzibar kupitia ADC katika uchaguzi mkuu uliopita, amesema katika kipindi cha pili cha awamu ya saba, Dk. Shein anahitaji wataalamu wachumi na watakaotumikia nchi kwa uadilifu.

Aidha, alisisitiza vyombo vya sheria vitumie nafasi yao dhidi ya watendaji na viongozi watakaokiuka sheria na kujaribu kuikwamisha serikali kutimiza malengo yake.

Aliiomba serikali iache muhali kwa kulea watendaji wasiotimiza majukunmu yao ipasavyo, akisema ni lazima watu kama hao wachukuliwe hatua madhubuti vyenginvyo nchi itarudi nyuma kimaendeleo.

Rashid alieleza kuwa, kinachokwamisha nchi kupata maendeleo ni watendaji na viongozi wengi kutojali wakati na kupoteza muda mwingi kwa mambo yasiyokuwa ya msingi badala ya kufanya kazi.

“Tumeshuhudia watu wengi wakkinyimwa au kucheleweshewa huduma wakiwemo wawekezaji wanaoomba miongozo. Hili ni tatizo na lazima tufike wakati likomeshwe,” alisisitiza.

Aliitaka serikali kuiga mfano wa Tanzania Bara, ambapo amesema mtu anayeomba huduma hupangiwa mtendaji maalumu wa kumsaidia, na pia hujulishwa mapema tarehe atakayomaliziwa mchakato wake na kupewa majibu au kutumiwa kokote aliko.

Kwa upande mwengine, aliitaka serikali iwe makini katika kusimamia ukusanyaji wa mapato kwani kodi ndio msukumo wa kuharakisha maendeleo.

Mhe.Rashid aliwataka wananchi waondokane na fikra za kutegemea misaada kutoka nchi za nje, na badala yake wakaze buti katika kufanya kazi za uzalishaji na huduma kwa kutumia rasilimali zilizomo nchini.

Kwa upande wake,Mhe.Mohammed Aboud Mohammed ambaye pia ni mwakilishi wa kuteuliwa na Rais, amewaomba wajumbe wenzake waache siasa kwani  uchaguzi umekwisha na kilichobaki sasa ni kujenga nchi.

Amefahamisha kuwa katika suala la maendeleo, si vyema kuingiza itikadi za kisiasa, dini, ukabila au maeneo watu wanakotoka kwani Zanzibar ni nchi ya Wazanzibari wote.

Aidha aliwataka wananchi wawe watulivu, wavumilie na kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwao.

Salamu za Pongezi za CCM kwa Dk Shein

$
0
0
SALAMU ZA PONGEZI ZA CCM
KWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA
BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN
KWA HOTUBA YAKE ALIYOITOA KATIKA UZINDUZI WA
BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR
TAREHE 05 APRILI, 2016.

CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar kwa moyo mkunjufu kinampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kutokana na hotoba yake nzuri na dira kwa maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake, aliyoitoa jana Aprili 05, mwaka huu, wakati akizindua Baraza la Tisa (9) la Wawakilishi Zanzibar.

Ni hotuba iliyosheheni mambo kadhaa ya maendeleo kiuchumi, kisiasa na kiustawi wa jamii, mambo ambayo wananchi wanatarajia kuyaona yakitekelezwa na Viongizi wao wa Kitaifa kwa mustakbali wa Taifa na Wazanzibari wote.                                                                 

Chama Cha Mapinduzi, kimeelezea kufarajika kwake kutokana na hotuba ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Shein, alipoihakikishia jamii nzima ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla wake kwamba Serikali yake imekusudia kuwaleta maendeleo endelevu wananchi ndani ya maendeleo yao, na hivyo kuondokana na umasikini hasa wa kipato.

Kupitia hotuba yake hiyo, wananchi walio wengi hasa wapenda amani, utulivu na maendeleo, wamejenga matumaini makubwa kutokana na kauli ya Mhe. Rais, na hasa pale alipowaahidi  kwa kusema Serikali yake iliopo madarakani na kupitia Mkuza II, itafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na ustawi wa jamii, ili kuwawezesha Wazanzibari kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2020.

Akifafanua zaidi, Dkt. Ali Mohamed Shein, alisema huo miongoni mwa mikakati Serikali ya kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi yetu na pia kukuza pato la Taifa. Ili kufika azma hiyo, kipaumbele cha mwanzo cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kukuza uzalishaji kupitia sekta za kilimo, utalii, viwanda vidogo vidogo, pamoja na kuimarisha raslimali watu, ubora wa huduma za jamii ikiwemo Elimu, Afya, Mazingira, Utawala bora, nk,  jambo ambalo linapaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo wa Taifa hili.

Akizungumzia kuhusu uimarishaji wa sekta ya biashara, Mhe. Dkt. Shein, amewataka Wazanzibari kutambua umuhimu wa zao la karafuu ambalo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar na kutoa wito kwa wananchi kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali yao za kuimarisha zao hilo, ili liweze kuwaletea tija zaidi.

Kama hiyo haitoshi,  kauli ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, ya kukubali kuwalipa wakulima wa karafuu kwa asilimia 80 ya bei ya zao hilo kwenye soko la dunia, inatoa matumaini mapya kwa wakulima wa zao hilo wa Unguja na Pemba.

Kuhusu suala la uwekezaji, Mhe. Dkt. Shein, amewaeleza Wazanzibari kuwa Serikali anayoiongoza imekusudia kushajiisha vyema wawezeshaji wa nje kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii na utoaji wake wa huduma ya fani hiyo, jambo ambalo kila Mzanzibari anatakiwa kuliunga mkono kwa nguvu zote.

Kauli ya Mhe. Rais wa Zanzibar  ya kuwahakikishia wananchi kutekeleza ahadi mbali mbali alizozitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya kuimarisha maslahi ya wafanyakazi wa kima cha chini nchini kufikia Tsh. 300,000 kwa mwezi, pamoja na Idara Maalum za SMZ ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani, sio tu imeleta faraja kwa wananchi, bali pia itainua utekelezaji wa majukumu yao na kuleta tija kubwa kwa Taifa letu.

Sambamba na hilo, kauli ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanza kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuwapatia pencheni maalum wazee wote waliofikia umri wa miaka 70 bila kujali historia ya kazi walizokuwa wakizifanya, nayo CCM linaunga mkono kwani zitawapunguzia kwa kiasi fulani ugumu wa maisha kwa wazee wetu hao pamoja na walio karibu na wazee hao. 

Kauli ya Rais wa Zanzibar kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini, kwa kuimarisha mashindano mbali mbali Maskulini, Wilayani, Vikundi vya Mazoezi, pamoja na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Mao Tse Tung, ni jambo jema kwa wananchi hasa wanamichezo wa Taifa hili.

Wazanzibari walio wengi wamefarajika kwa kiwango cha juu na kauli ya Rais wao mpendwa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuwaahidi tena bila ya kigugumizi kwamba wakati umefika kwa Serikali yake wa kutumbua majipu kwaviongozi na watendaji wote wanaoonekana kuwa ni majipu kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, kinachukua nafasi hii kumpongeza tena Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa uongozi wake mzuri ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tangu alipoingia madarakani (Awamu ya Kwanza) hapo Novemba 03, 2011.

Kwa mnasaba huo, katika Awamu ya Pili ya Uongozi wake, CCM inajenga matumaini makubwa yafuatayo :-

·        Mhe. Dkt. Shein, ataweza kuwaunganisha vyema Wazanzibari Ndani ya Serikali na Nje ya Serikali kwa kutekeleza kikamilifu Katiba na Sheria za nchi.
·        Mhe. Dkt. Shein, ataweza kusimamia kwa kiwango kikubwa na kuwaletea maendeleo ya haraka Wazanzibari jambo ambalo litawezesha kuimarisha ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbali za jamii.
·        Mhe. Dkt. Shein, katika kipindi kijacho cha uongozi wake, ataweza kusimamia suala zima la amani na utulivu ndani ya visiwa vyetu vya Unguja na Pemba, jambo ambalo litawawezesha Wazanzibar wote kufanya shughuli zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii, bila ya kuwa na hofu yoyote.
·        Mhe. Dkt. Shein, ni kiongozi anayependa watu wa rika na jinsia zote na hana chembe ya ubaguzi, anawapenda watu wote na atawatumikia wananchi kwa umakini na uadilifu mkubwa sana.

Mwisho, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pongezi za pekee kwa Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuunda Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, itakayosimamia masuala ya maadili ya viongozi na nidhamu makazini.

Mwisho kabisa, Chama Cha Mapinduzi kinatoa wito kwa Jamii nzima ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla wake, wawe tayari kumpa kila aina ya mashirikiano, ili aweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake aliyokabidhiwa na Taifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

(Vuai Ali Vuai),
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
ZANZIBAR.
06/04/2016.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Afungua Kongamano la 21 kwa Watafiti wa Uchumi wa Viwanda.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, kabla ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoanza leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa  leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki, Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa washiriki hao inayojadili kuhusu uendelezaji wa Utafiti wa Uchumi wa Viwanda Nchini. Warsha hiyo imefunguliwa leo katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda leo April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)
Viewing all 36091 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>