Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36095 articles
Browse latest View live

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Yakamata Shehena ya Mafuta ya Kupikia Yaliyoingizwa Nchini Kinyume na Sheria Yakiwa Karibu Kumaliza Muda Wake kwa Matumizi ya Binadamu.

$
0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua Godauni lenye mafuta ya kupikia yanayokaribia kumaliza muda wake wa matumizi ya kula binadamu, eneo la Amani magogoni Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Premium Enterprises Ndg.Humud Nassor Humud akiyakagua ili kuyatambua madumu ya kampuni yake ambayo yamekamatwa na Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar yakitumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kutia mafuta ya kupikia yanayokaribia kumaliza muda wake ili yaonekane kuwa ni mapya.
Shehena ya maboksi ya mafuta ya kula yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria.

Mkuu wa Idara ya Usalama na Ubora wa Chakula wa (ZFDB) Bi. Aisha Suleiman akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kukamatwa mafuta yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria yenye thamani ya miliono 40.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzuibar.)

Star Times yamleta nchini mchezaji Kanu kutoka Nigeria kuzindua duka jengo la Mkuki Mall

$
0
0
 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana usiku kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya StarTimes.
 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege.
 Hapa Kanu akihojiwa na wanahabari. Kushoto na kulia ni Mabaunsa waliokuwa wakimlinda baada ya kufika Uwanja wa Ndege kabla ya kuelekea Hoteli ya Serena.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be. Lanfang Liao (kulia), akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa StarTimes Tanzania,  William Masy.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI inayojihusisha na utoaji wa huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali, StarTimes Tanzania imepokea ugeni mzito wa aliyekuwa mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Bw. Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa kampuni hiyo kwa bara la Afrika ambamo imo kwenye takribani nchi zaidi ya 10.



Akizungumza mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jana usiku, mchezaji Nwankwo Kanu alisema kuwa anajisikia furaha kubwa kuwasili Tanzania salama kujumuika na kmapuni ya StarTimes katika shughuli mbalimbali kwa ndani ya kipindi cha siku tano atakazokuwepo.



‘’StarTimes ni kampuni kubwa barani Afrika na imeleta mapinduzi makubwa katika upande wa matangazo ya luninga kwa dijitali kwani imeweza kutoa huduma zake kwa ubora mkubwa na gharama nafuu ambazo kila mtu anaweza kuzimudu.’’



Kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo mchezaji Kanu amebainisha kuwa kampuni ya StarTimes imepiga hatua kubwa hasa kwa upande wa kupata na kuonyesha michezo ya ligi ya soka kubwa barani Ulaya kama vile za Bundesliga na Serie A za Ujerumani na Italia.



“Mimi kama balozi wa StarTimes barani Afrika nitajitahidi kawa kadiri ya uwezo wangu kuwa kiungo muhimu katika kuhakikisha ninaiwakilisha vema kwa wateja wake, hususani katika shughuli mbalimbali kama vile soka kama mjuavyo ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani na hata miongoni mwa waafrika wenyewe.” Aliongezea Kanu.



“Hivyo basi kwa muda wote nitakaokuwepo nchini Tanzania nitashirikiana na StarTimes kwa ukaribu katika shughuli za kikampuni na pia za kijamii kama vile za kielimu na afya. Kama mjuavyo katika mahala popote unapofanyia shughuli zako ni muhimu sana kuijali jamii inayokuzunguka kwani yenyewe ndiyo sababu kubwa ya wewe kuwepo.” Alihitimisha



Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa, “Uwepo wa Kanu Tanzania ni fursa ya kipekee na pia ni moja ya jitihada kubwa za kampuni yake katika kuimarisha na kuhudumia wateja wao hususani kwa vipindi vya michezo na burudani na ninaamini uwepo wake utaleta chachu kwetu sisi na wateja kwa ujumla.”



“Nwankwo Kanu alikuwa ni mchezaji wa kimataifa si tu aliiwakilisha nchi yake ya Nigeria kimatifa katika michuano mbalimbali lakini pia alifungua milango kwa vipaji vya Afrika barani Ulaya. Hivyo basi tunaamini bado ni maarufu na ana heshima kubwa miongoni mwa watanzania na wapenda soka barani Afrika. Kwa yeye kuwa balozi wetu ninaamini tutafaidika kwa namna gani tuboreshe huduma zetu ili kuiteka mioyo ya watanzania na waafrika kiujumla.” Alimalizia Bw. Liao

Skuli za msingi Wingwi zapatiwa vitendea kazi

$
0
0
 Mwalimu Yussuf Shoka Hamad alipokabidhi vifaa kwa Mwalimu mkuu shule ya msingi Simai, Wingwi, Mw. Muhammed Hamad pamoja na Walimu wengine wakiwa katika picha ya pamoja

 Mwalimu Yussuf Shoka Hamad akitoa maelekezo kuhusu vifaa alivyokabidhi kwa Walimu wa Shule za msingi Wingwi
Mwalimu Yussuf Shoka Hamad akikabidhi vifaa kwa Mwalimu Khamis Rashid wa Shule ya Msingi Wingwi


Na: Waandishi kutoka Pemba

Shule za msingi Mtemani, Wingwi msingi na Simai zote za Wingwi, wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, zimepatiwa msaada wa vifaa vya kisasa vya kutendea kazi kwa ajili ya kuleta ufanisi kazini.

Msaada huo uliotolewa na  mhadhiri kutoka chuo kikuu cha SOAS, London, nchini Uingereza  Mwalimu Yussuf Shoka Hamad, ulijumuisha mashine ya kompyuta za dawatini, mashine ya kutolea fotokopi, kupigia skani na kuchapishia barua na hati mbali za kiofisi.

Katika hafla fupi iliyoandaliwa na shule hizo jana (Jumatatu) mchana, Bwana Yussuf alisema kuwa lengo na nia yake ni kuzisaidia shule zote za  Wingwi kwa kuzipatia vitendea kazi vya kisasa ili kukuza ufanisi na kuendana na maendelea ya sasa ya dunia ya sayansi na teknolojia.

‘Lengo langu si kujijenga kisiasa. Mimi si mwanasiasa, naruadia kusema hivi na naisitiza tena kwamba sitoi misaada hii kwa madhumuni ya kisiasa. Mimi ni mzaliwa wa Wingwi na ari  ya uzawa na mchango nilioupata kwa jamii yangu ya Wingwi ni miongoni mwa misukumo inayonipelekea kutoa misaada hii bila kuchoka na bila kujali thamani, ukubwa au udogo wa vitu hivyo ninavyotowa’.


Bwana Yussuf pia aliongezea kwa kusema nia yake hasa ni kuzibadilisha shule zote za Wingwi na kuzifikisha katika kiwango cha ubora wa shule za kisasa kivitendea kazi ifikapo mwaka 2020. Moja kati ya mikakati yake ya kufikia lengo hilo ni kuhakikisha kila shule inapata mashine za kutolea kopi (photokopi) zenye uwezo wa kuchapisha mitihani ya ndani ya wanafunzi, kujenga maktaba za ndani ya shule hizo na kuzipa uwezo wa vifaa vya asili na vile vya kisasa ili kukuza kiwango cha elimu nchini.

Katika hafla hiyo, Bwana Yussuf aliahidi kuzipatia shule hizo mashine za kutolea photokopi (kubwa) ifikapo mwakani ambapo kila shule itaweza kujitegemea kwa vitendea kazi  vyenye uwezo na ubora wa kisasa.

Wakitoa shukrani zao kwa Mwalimu huyo, Walimu wakuu wa shule  hizo walimpongeza Mwalimu Yussuf kwa uzalendo na moyo wake wa kujitolea na  hasa katika kusaidia sekta ya elimu ya shule hizo za Wingwi.

‘Kwa kweli msaada huu ni mkubwa kwetu kiasi ambacho hatujui jinsi gani tufikishe shukrani zitakazofikia thamani ya msaada huu. Tunashukuru sana na tunakutakia heri na fanaka katika kazi zako ili uweze kusaidia zaidi katika sekta hii ya Elimu ya shule zako za Wingwi.’ Aliema Mwalimu Mohammed Hamad wa Shule ya Msingi Simai.

Naye Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya msingi Wingwi, Bwana Khamis Rashid alimshukuru na kumpongeza Bwana Yussuf Shoka kwa hatua yake hiyo ya kukumbuka kusaidia shule za Wingwi ambako yeye (Yussuf) alisomea hapo.


Msaada huu wa zawadi uliotolewa ni moja ya sehemu za ahadi alizitowa Bwana Yussuf wakati wa hafla ya kuwazawadia wanafunzi waliofaulu mitihani yao ya darasa la saba mwaka jana ambapo kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo kimeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Dk Shein awaongoza wananchi kwenye kisomo maalum kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume

$
0
0
 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                   7.4.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaongoza viongozi na wananchi mbali mbali katika kisomo maalum cha kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ikiwa pia, ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo chake.

Marehemu Mzee Karume ambaye pia, alikuwa Kiongozi wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuawa siku ya Ijumaa tarehe 07 April, 1972 saa 12:05 jioni katika Makao Makuu ya ASP ambayo sasa ni Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyopo Kisiwandui mjini Unguja.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya CCM ambako ndipo alipozikwa marehemu, Dk. Shein na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi walishiriki kisomo maalum cha kumuombea dua kiongozi huyo ambaye kifo chake kiliushitua ulimwengu mzima.

Baada ya kisomo hicho viongozi hao walizuru kaburi la marehemu wakiambatana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ambao walipewa fursa za kumuombea dua marehemu wakiwa kaburini hapo.

Kisomo hicho cha kumuombea dua Marehemu Mzee Karume kilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Sita, Mhe. Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine walihudhuria katika hitma hiyo ni  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mufti Mkuu wa Tanzania Bara Sheikh  Abubakar Zubeir, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es- Salam Sheikh Mussa Salum.


Aidha, Mama Mwanamwema Shein alihudhuria katika tukio hilo akiungana na akina mama wengine akiwemo, Mama Fatma Karume na Mama Asha Balozi na viongozi wengine wanawake wa Kitaifa pamoja na viongozi wa serikali zote mbili na wakiwemo viongozi wastaafu, viongozi wa vyama vya siasa, Masheikh kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, Wabunge, Wawakilishi, Mabalozi wadogo wanaofanya kazi zao hapa Zanzibar na wananchi kutoka sehemu mbali mbali.

Kisomo hicho cha kumuombea dua marehemu Mzee Abeid Amani Karume pia, ni miongoni mwa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, kilitanguliwa na Qur-an tukufu iliyosomwa na Ustadh Sharif Muhidin na kuongozwa na Sheikh Jafar Abdallah kutoka Masjid Noor Mohammad,iliopo Kwa Mchina Mwanzo.

Mara baada ya hitma hiyo, Sheikh Hamid Masoud Jongo kutoka Tanzania Bara, alitoa mawaidha yalioendana na maudhui ya kumbukumbu hiyo na kumuelezea marehemu mzee Abeid Amani Karume kuwa ni kiongozi bora kutokana na kuwafaa watu waliowengi hapa nchini na kumuombea MwenyeziMungu ampe makaazi mema Peponi.

Sheikh Jongo alisema kuwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano zimefaidika na Muungano huo ulioasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pamoja na Marehemu Julius Kambarage Nyerere huku Sheikh Jongo akishangazwa na wale wanaoupinga Muungano huo.

Katika mawaidha yake hayo alisisitiza umuhimu wa kumuombea dua kiongozi huyo kutokana na msisitizo na msimamo wa kiongozi wa Waislamu, Mtume Muhammad (S.A.W) wa kupita makaburi kwa kila mwaka kwa ajili ya kuwaombea dua wale wote waliouhami Uislamu na kutoa mchango wao mkubwa katika dini hiyo.

Sambamba na hayo, Sheikh Jongo alieleza kuwa kutokana na juhudi zake Mzee Karume ndio zilizopelekea kupatikana uhuru sambamba na kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu hapa nchini.

Mara baada ya tukio hilo, tukio lililofuata lilikuwa ni kuweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Mzee Karume kitendo kilichofanywa na viongozi wakuu pamoja na muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Issa Nassor, wawakilishi wa familia, muwakilishi wa wazee waasisi Mzee Suleiman Omar pamoja na  muwakilishi wa Mabalozi wadogo wanaofanya kazi zao hapa Zanzibar.

Marehemu Mzee Karume aliongoza harakati za kupigania uhuru wa Zanzibar hadi kuongoza Mapinduzi yaliyoung’oa utawala wa Kisultani uliokuwa ukihamiwa na Serikali ya Kingereza baada ya watawala hao kufanya kila njama za kuwanyima uhuru wananchi wa Zanzibar.
Mzee Karume anakumbukwa sana na wananchi wa Zanzibar kwa namna alivyoweza katika kipindi kifupi cha utawala wake kuleta mageuzi makubwa katika jamii ya Wazanzibari ambapo alisimamia haki na usawa katika umiliki wa njia za uchumi kama ardhi na kuondoa kabisa ubaguzi katika elimu, afya, ajira na kuwapatia wananchi makazi bora sambamba na mambo mengine muhimu ya kimaendeleo na kimaisha.
Mwenyezi Mungu alilaze roho ya marehemu mahala pema peponi-amin

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


Dua ya kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Karume

$
0
0

 Mjukuu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Ahmed Amani Abeid Karume akichukua shada la mauwa kwaniaba ya wenzake kuliweka katika kaburi  baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Babu yao,  iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na  uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]

 Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na  uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na  uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akifuatana na wasaidizi wake akitoka eneo la kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume liliopo nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika hafla ya dua na uwekaji wa mashada ya mauwa iliyofanyika leo,na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  akiwapungia mkono viongozi na wananchi walihudhuria katika hitma ya  Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo baada ya kumalizika katika  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar   na uwekaji wa mashada ya mauwa  ambapo  Viongozi na Wananchi mbali mbali walihudhuria,[Picha na Ikulu.]
Wake wa Viongozi wakiwa nje ya Ofisi Kuu wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwaanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeeid Amani Karume iliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.]

Balozi Seif akagua maendeleo ya ujenzi wa kuimarisha kiwanda cha upigaji chapa

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Nd. Mohammed Suleiman Khatib akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi changamoto zinazokabili uendelezaji wa miundombinu ya uimarishaji wa Kiwanda hicho hapo Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif alifanya ziara hiyo fupi ili kujionea harakati za kukamilisha Awamu ya Pili ya uimarishaji wa Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi uliopata ufadhili kutoka Serikali ya Oman kwa gharama ya Shilingi Bilioni 12.5.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Kiwanda cha upigaji chapa na Mpiga chapa Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba kazi ya kukamilisha miundo mbinu ya uwekaji Umeme pamoja na majengo kwa ajili ya ufungaji mashine kubwa za Kiwanda hicho inamalizika katika kipindi kifupi.

Alisema kudorora kwa kazi hizo kunakotokana na upatikanaji finyu wa fedha za kuwalipa wakandarasi wa ujenzi wa miundo mbinu hiyo ikiwa ni muendelezo wa ukamilishaji awamu ya Pili ya Mradi Mkubwa wa uimarishaji wa Kiwanda cha Uchapaji lazima upatiwe ufumbuzi wa haraka.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua ujenzi wa Miundombinu hiyo ambao umesimama kutokana na ukosefu wa fedha hapo katika Majengo ya Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif aliutaka Uongozi wa Taasisi hizo mbili kuhakikisha kwamba lile agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alilolitoa mapema mwaka huu la kutaka machapisho yote ya vitabu vya Bajeti ya Mwaka huu yanafanyika katika kiwanda hicho cha Serikali.

Alisisitiza kwamba Mradi huo mkubwa wa Serikali wa awamu ya Pili ya uimarishaji miundombinu ya Kiwanda hicho  uliopata ufadhili kwa kuungwa mkono na Mataifa rafiki na Zanzibar lazima ukamilike kwa wakati uliopangwa ili utoe huduma zilizolengwa.

“ Huu ni mradi mkubwa wa Serikali  uliopata baraka ya kusaidiwa  nguvu za vifaa na wenzetu wa Mataifa rafiki tena kwa gharama kubwa ya fedha lazima ukamilike kwa wakati uliopangwa kama alivyoagiza Kiongozi wetu wa Nchi ”. Alisema Balozi Seif.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliutanabahisha Uongozi wa Kiwanda cha Uchapaji na Mpiga Chaka Mkuu wa Serikali kwamba atatembelea tena kuangalia  ukamilishaji wa ujenzi huo ndani ya kipindi cha Wiki mbili ili kuona harakati alizoziagiza zimechukuliwa hatua zinazofaa mara moja.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Nd. Mohammed Suleiman Khatib alisema mitambo pamoja na vifaa vyote  vinayokusudiwa kufungwa katika awamu ya Pili ya uimarishaji wa Miuondombinu ya Kiwanda hicho vimeshawasili hapa Nchini.

Nd. Mohammed alisema kinachosubiriwa kufungwa kwa mitambo hiyo ni kukamilika kwa ujenzi wa Banda pamoja na miundombinu ya umeme itakayokidhi mahitaji halisi ya kiwanda kutoka Kilowats 200 ziliazokuwa zikitumika hivi sasa hadi Kilowats 500 ili viendane na vifaa vikubwa vitakavyofungwa.

Mkurugenzi huyo wa Idara ya Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kazi za uzalishaji Kiwandani hapo zitakwenda kwa ufanisi baada ya kukamilika kwa usambazaji wa umeme, huduma za maji kwa ajili ya mashine kubwa pamoja na milango mikubwa.

Hata hivyo Nd. Mohammed alielezea changamoto zinazokwaza kudorora kwa kazi hiyo akizitaja kuwa ni pamoja na ufinyu wa fedhakwa ajili ya Taasisi za uwekaji Umeme na wajenzi wa majengo ya kuwekea mashine hizo.

Alisema Jumla ya shilingi Milioni 252,000,000/- zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha kazi ya usambazaji wa huduma ya Umeme kwenye kiwanda hicho pamoja na shilingi Milioni 185,000,000/- kumalizia majengo na miundombinu mengine.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim alisema kinachosubiriwa kwa sasa ili kufungwa kwa mashine hizo ni ukamilishaji wa miundombinu ya huduma za Umeme katika eneo hilo la Kiwanda cha Uchapaji.

Nd. Ahmad alisema wataalamu wa ufunguaji wa mashine hizo ambao wengine watatoka nje ya Nchi watahitaji kupata wiki mbili tu kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo baada ya kukamilika kwa miundombinu ya usambazaji wa Umeme.

Mradi huo Mkubwa wa awamu ya Pili wa uimarishaji wa Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi ulioanza ujenzi wake mapema Mwezi wa Febuari mwaka huu umefadhiliwa na Serikali ya Oman kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 12.5.

Gharama hizo zilielekezwa katika ununuzi wa mashine 34 tofauti kwa ajili ya kuendeleza kiwanda hicho zikiwemo mashine za rangi, Mabango, mashine za kuchomea pamoja na Plate.


Mkutano wa ufuatiliaji habari za uchaguzi wafanyika Mtwara

$
0
0
 MTANGAZAJI wa Clouds Fm kutoka mkoani Kilimanjaro, Beatrice akielezea changamoto na namna walivyokabiliana navyo mkoani humo, wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana, kwenye mkutano wa siku mbili wa ufuatiliaji wa habari za uchaguzi, uliofanyika Mkoani Mtwara na kuandaliwa na shirika la internews (picha na Haji Nassor alipokuwa Mtwara).
 MWANDISHI wa habari wa gazeti la Nipashe kutoka Zanzibar, Rahma Suleiman akifafanua jambo, kwenye mkutano wa siku mbili wa ufuatiliaji wa habari za uchaguzi, uliofanyika Mkoani Mtwara na kuandaliwa na shirika la internews (picha na Haji Nassor alipokuwa Mtwara).
 AKINAMAMA wauza korosho kutoka mkoani Mtwara Tanzania bara, wakiwahudumiwa wateja wao katika eneo la Bima katikati ya manispaa ya Mtwara, ambapo bei ya korosho ni kati ya shilingi 1000 na shilingi 20,000 kwa ujazo wa kilo moja, (picha na Haji Nassor alipokuwa Mtwara).
AKINAMAMA wauza korosho kutoka mkoani Mtwara Tanzania bara, wakiwahudumiwa wateja wao katika eneo la Bima katikati ya manispaa ya Mtwara, ambapo bei ya korosho ni kati ya shilingi 1000 na shilingi 20,000 kwa ujazo wa kilo moja, (picha na Haji Nassor alipokuwa Mtwara).

Rais Magufuli arejea nyumbani akitokea Rwanda katika safari yake ya kwanza ya nje ya nchi

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange huku Inspekta jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisubiri zamu yake  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe Jaji Francis Mutungi mara baada ya kutua  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 


Nwanko Kanu azindua duka jipya la Star Times jijini Dar

$
0
0
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.
 Ofisa Mauzo wa StarTimes Tanzania na mshereheshaji wa uzinduzi huo, Tang Jing Yu 'Juma Shorabaro wa Kichina' (kulia), akiendelea na majukumu yake.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (wa pili kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaamleo mchana, baada ya kuzindua duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall wakati wa ziara yake aliyoianza jana  nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, Katibu wa mchezaji huyo, Kingstey Obiekwe na Makamu wa Rais wa StarTimes, Zuhura Hanif.
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (katikati), akitia saini yake katika jezi.
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa StarTimes na wa jengo la Mkuki Mall baada ya kuzindua duka hilo.
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akichukua picha na mchezaji huyo.

Na Dotto Mwaibale

Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Naijeria (Super Eagles) na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall Barabara ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za kijamii.

“Ni mara ya kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa, inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw. Kanu

“StarTimes wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu

“Michezo na burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji (Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.

“Leo tunayo furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi, antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.” Alimalizia Bw. Carter.


Hafla ya Kuapishwa Wajumbe Saba wa Baraza Walioteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein.

$
0
0

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha AFP Mhe Said Soud Said, akiwasili katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar cha ajili ya kula kiapo baada ya kuteuliwa Nafasi hiyo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Mwakilishi wa Nafasi ya Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar Mhe Said Soud Said akisalimiana na Mwandishi wa Kituo cha TV cha Channel ten Ndh Munir Zakari wakiwa katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukuwani Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Nafasi ya Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar Juma Ali Khatib wa Chama cha ADA-TADEA akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa ajili ya kuaza kazi ya Kuwawakilishi Wananchi wa Zanzibar. 
Mhe Juma Ali Khatb wa Chama cha ADA -TADEA , akisalimiana na Mhe Balozi Amina Salum Ali wa Chama cha Mapinduzi wakati walipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kuhudhuria hafla ya kuapishwa kuwa Wajumbe wa Baraza baada ya kuteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.













































Marekani Kusimamia Miradi ya Kijamii Pemba.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba,Mhe Hemed Suleiman Abdalla , akikata Utepe kuashiria kufunguwa jengo la madarasa sita huko katika Kijiji cha Matale , lilijengwa na Serikali ya Marekani kupitia Jeshi lake.
Msimamizi wa Miradi wa huduma za Kijamii inayosimamiwa na Jeshi la Marekani, LT. Ruben Lopez, akitowa maelezo juu ya ujenzi wa mradi wa skuli hiyo iliogharimu Dola za Kimarekani 226,000/=.
Msimamizi wa Miradi ya Huduma za Kijamii, inayosimamiwa na Jeshi la Marekani Kisiwani Pemba LT, Ruben Lopez, akikaguwa Ujenzi wa Mradi huo wa jenzi wa ukuta wa kuzuwia mmomonyoko wa ardhi katika Skuli ya Matale Pemba.(Picha na Bakar Mussa-Pemba.)

Wajumbe wa Baraza Wachangia Hutuba ya Rais wa Zanzibar Shein Siku ya Uzinduzi.

Hotuba ya Balozi Seif Ali Iddi kuahirisha mkutano wa kwa kwanza BLW

$
0
0
HOTUBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KWANZA WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI, TAREHE 08 APRILI, 2016
----------------------

1.  Mheshimiwa Spika, awali ya yote, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwingi wa Rehma kwa kuendelea kuweka nchi yetu hii katika hali ya amani, utulivu, umoja na mshikamano mkubwa. Hali ambayo imeiwezesha Serikali na wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila ya mtafaruku wa aina yeyote. Aidha, tunaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufanya uchaguzi katika hali ya amani na utulivu, jambo ambalo sote tuliomo humu Barazani pamoja na wananchi wote ni mashahidi wa hilo. Ninawaomba wananchi waendelee kuitunza na kuithamini amani iliopo nchini.

2.  Mheshimiwa Spika, kwa mara nyengine tena, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha hapa tukiwa katika hali ya uzima na afya njema na kutuwezesha kufanikisha vizuri Mkutano wa Kwanza wa Baraza hili Tukufu la Tisa la Wawakilishi, ulioanza tarehe 30 Machi, 2016. Nimefarijika kuwa kazi zote zilizopangwa katika ratiba yetu tumezikamilisha kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

3.  Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kwa niaba yangu na Waheshimiwa Wawakilishi kutoa pongezi za dhati kwako wewe Mhe. Spika pamoja na Naibu Spika, Mhe. Mgeni Hassan Juma kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuliongoza Baraza letu hili Tukufu. Vile vile, nampongeza Mhe. Riziki Pembe Juma, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Viti Maalum na Mhe. Shehe Hamad Mattar, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Mgogoni, Pemba kwa kuchaguliwa kuwa Wenyeviti wa Baraza letu hili. Hii inaonesha imani kubwa waliyonayo Waheshimiwa Wajumbe juu yao. Ni mategemeo ya Waheshimiwa Wajumbe kwamba mtaliongoza Baraza hili Tukufu kwa hekima, busara, uadilifu na umakini mkubwa ili kuliwezesha Baraza kutekeleza majukumu yake yakiwemo ya kuisimamia Serikali kwa ufanisi na kupeleka maendeleo endelevu kwa wananchi wetu na nchi yetu kwa ujumla. 


Aidha, nachukua fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Hamza Hassan Juma, Salha Mohamed Mwinjuma, Rashid Ali Juma, Lulu Msham Abdulla na Hamad Abdulla Rashid kwa kuchaguliwa kwao kuwa Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi.  Kuchaguliwa kwao kunadhihirisha imani kubwa ambayo Waheshimiwa Wajumbe aliyonayo juu yao, kwani Kamati hii ni muhimu sana kwa maendelezo ya Baraza letu.

Aidha, napenda kuwapongeza wenzetu saba walioteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na hivi karibuni tu uliwaapisha.  Wajumbe hao wakiwa Mhe. Mohamed Aboud Mohamed, Mhe. Amina Salum Ali, Mhe. Maudline Castico, Mhe. Ali Abeid Karume, Mhe. Hamad Rashid, Mhe. Juma Ali Khatib na Mhe. Said Soud Said.  Kuteuliwa kwao kunaonyesha imani kubwa ambayo Mheshimiwa Rais anayo juu yao na kwamba michango yao italisaidia sana Baraza lako Tukufu.

4.  Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuchaguliwa kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 91 kushika wadhifa huo katika muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Saba kupitia uchaguzi wa marejeo uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016.  Aidha, pamoja na pongezi hizo, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa imani kubwa aliyoionesha kwangu kwa kuniteua kuwa Makamu wa Pili wa Rais kwa mara nyengine tena.  Namuomba Mwenyezi Mungu atubariki na kutujaalia afya njema na nguvu ya kuwatumikia wananchi wote hapa Zanzibar bila kujali rangi, jinsia, dini au itikadi zao za kisiasa.

5.  Mheshimiwa Spika, aidha, kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, napenda kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi sana.  Hii imeonyesha imani na upendo kwa wananchi wa Tanzania walioayo juu yao.  Pia nampongeza Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo.  Hii inaonyesha imani ambayo Mhe. Rais Magufuli aliyonayo juu yake.

Ni matumaini yetu kwamba viongozi wetu hao watalitumikia Taifa letu kwa hekima na busara ili kuwapatia wananchi wetu maendeleo ya dhati.  Tunampongeza Rais Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo.

6.  Mheshimiwa Spika, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein tarehe 05 Aprili, 2016 alilituhutubia Baraza hili Tukufu kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba. Pamoja na mambo mengine, katika hotuba yake amefafanua kwa kina kuhusu wajibu wetu kama Wajumbe wa Baraza hili, na ameeleza masuala muhimu katika kuijenga Zanzibar yetu.

7.  Mheshimiwa Spika, hotuba ya Mheshimiwa Rais itakuwa dira na mwongozo wetu katika kutekeleza majukumu yetu ndani na nje ya Baraza hili kwani hotuba hiyo iligusa kila Sekta ya maendeleo yetu.  Wajumbe mlipata nafasi ya kuijadili hotuba hiyo kuanzia tarehe 6 Aprili, 2016 hadi leo hii.

Michango ya Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza lako tukufu ilijikita zaidi juu ya uwepo wa amani na utulivu, kuboresha na kuimarisha maeneo huru hasa ya Fumba na Micheweni, vita dhidi ya rushwa na udhalilishaji wa kijinsia, wanawake na watoto, uendelezaji wa elimu na Vyuo vya Amali, mazingira, ajira kwa vijana, ukusanyaji wa mapato na ulipaji wa kodi kwa kutaja machache.  Naliahidi Baraza lako tukufu kuwa Serikali itachukua hatua ya kuyashughulikia mapendekezo yote yaliyotolewa.  Kama Mwanasheria Mkuu alivyosema, michango yote hiyo itawekwa kwenye jeduali maalum (Bango Kitita) na kusambazwa kwa Mawaziri wote watakaohusika.

8.  Mheshimiwa Spika, Baraza hili Tukufu la Wawakilishi lina jukumu muhimu na kubwa la kutunga Sheria. Napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wawakilishi kwamba hiyo itakuwa ndiyo kazi yetu ya msingi, inayotakiwa kufanywa kwa busara, hekima na umakini mkubwa.  Pia, tunalo jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali ili kuhakikisha kuwa matatizo na kero mbali mbali za wananchi zinatatuliwa kwa ufanisi na mafanikio makubwa.  Tunapaswa kuhakikisha kuwa Serikali inatoa mchango wake kikamilifu katika kuyafanya maisha ya wananchi wetu kuwa bora zaidi kwa kutumia nguvu kazi na rasilimali tulizonazo. Ni matarajio ya Serikali kuwa itapata taarifa na ushauri kutoka kwa Waheshimiwa Wawakilishi juu ya maeneo yanayohitaji kupewa msukumo ili kuongeza kasi ya maendeleo ya Zanzibar. Kwa upande wake, Serikali itaifanyia kazi taarifa na ushauri utakaotolewa na Baraza hili Tukufu.

9.  Mheshimiwa Spika, sambamba na majukumu hayo, naomba kuwashauri Waheshimiwa Wawakilishi tuwe karibu na wananchi waliotuchagua. Sisi ndio macho na masikio ya wananchi hao. Tumepewa heshima kubwa na wananchi hao kwa kutuchagua kuwa Wajumbe wa Baraza hili.  Wananchi hao wana mategemeo makubwa kwamba tutawasaidia kutatua changamoto zao mbali mbali za maendeleo zinazowakabili. Ni wajibu wetu kufikisha mawazo ya wananchi hao Serikalini kwa kupitia mikutano na vikao vya Baraza hili pamoja na njia nyengine zinazofaa. Aidha, tunapaswa kuwaeleza wananchi wetu kile ambacho Serikali imepanga kukifanya na jinsi ya kutumia fursa, rasilimali, mipango na taratibu zilizopo za Serikali ili kuweza kuboresha maisha yao.

10.    Mheshimiwa Spika, napenda kuwaomba kwa mara nyingine tena, wananchi wote kuendelea kudumisha amani na utulivu katika visiwa vyetu na nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla. Bila ya kuwepo Amani na Utulivu, hakuna maendeleo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kusimamia suala la amani na utulivu kwa nguvu zake zote ili kutekeleza mipango yetu ya kujiletea maendeleo zaidi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.  Hakuna haja tena ya kukumbusha mambo yaliyopita, ila Serikali inatambua wapo baadhi ya wananchi wakorofi wanaojihusisha na vitendo vya kuvuruga amani na utulivu uliopo.

Kwa mfano, wakati tukielekea katika uchaguzi wa marejeo uliomalizika hivi karibuni, wakorofi hao walijihusisha kutega miripuko inayosadikiwa kuwa mabomu na kuchoma moto mashamba ya mikarafuu, nyumba na makaazi na maskani za CCM. Vyombo vya Dola vinaendelea na hatua za uchunguzi wa matukio hayo na baadae kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria.  Hakuna mtu atakayepona kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa atabainika kutishia amani na utulivu tulionao.


11.    Mheshimiwa Spika, tunasikitishwa na mambo yanayotokea huko Pemba ambapo baadhi ya wafanya biashara kuwanyima wananchi wenzao huduma za kibiashara kama vile kuwauzia bidhaa au kuwapa huduma za usafiri kwa sababu za kiitikadi za kisiasa.  Jambo hili siyo zuri na ingefaa liachwe mara moja.  Serikali inalifuatilia kwa karibu sana suala hili na haitasita kumchukulia hatua mfanya biashara yoyote atakaye liendeleza jambo hili ikiwa ni pamoja na kumfutia leseni yake.

12.    Mheshimiwa Spika, kuhusu uchaguzi wa marejeo uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016, nachukua fursa hii kuipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kazi nzuri ya kusimamia na kufanikisha uchaguzi huo kwa mafanikio makubwa. Uchaguzi huo ulikuwa huru na haki, na ulipelekea ushindi mkubwa kwa Chama cha Mapinduzi kupitia kwa aliyekuwa mgombea wake, Dkt. Ali Mohamed Shein, ambaye kwa sasa anaendelea kuiongoza nchi yetu akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha miaka mitano (2015 – 2020).

13.    Mheshimiwa Spika, kwa vile uchaguzi umekwisha, tunapaswa tuzidishe ushirikiano, mshikamano na umoja wetu katika kuijenga nchi yetu. Kwa upande wetu Waheshimiwa Wawakilishi turudi Majimboni mwetu ili tukashirikiane na wananchi kusukuma gurudumu hili la maendeleo.  Aidha, napenda kutumia fursa hii kuwaomba watumishi na watendaji wote wa Serikali watakaoteuliwa hapo baadae, kuwatumikia wananchi wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inahimiza uwajibikaji zaidi na usimamizi mzuri wa fedha na rasilimali nyengine za umma katika ngazi zote.   Wafanyakazi kujituma na siyo kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo Rais wetu alilipigia kelele sana katika kipindi kizima cha kwanza.  Na hata hotuba yake aliyoitoa wakati akilizindua Baraza hili alisisitiza jambo hilo.  Nikimnukuu alisema:
“wapo baadhi ya watumishi wenye tabia ya kutoroka kazini, kuchelewa na hawazijali kanuni ziliopo za utumishi wa umma.  Wao hujifanya wababe mbele ya viongozi wao.  Wafanyakazi wenye sifa mbaya nilizozielezea katika kipindi hiki tutawachukulia hatua watakapobainika na kama hapana budi tutawafukuza kazini.  Hatuwezi kuwa na wafanyakazi waliokuwa hawana nidhamu.  Sasa basi, imetosha.
Waliopewa dhamana ya kuziongoza Idara mbali mbali za Serikali watapaswa watekeleze wajibu kwa kuwasimamia wafanyakazi walio chini yao.  Pindi kama hawatawawajibisha wafanyakazi wao, basi watawajibishwa wao.  Lengo letu liwe kutoa huduma kwa wananchi, kwani sote tunawajibika kwao; kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.”

14.    Mheshimiwa Spika, mimi najua ziko Idara na Mashirika ya Umma ambayo hayako vizuri kiutendaji na ambayo yanalalamikiwa sana na wananchi kwa sababu ya kutowajibika kwa watendaji wao.  Nawaomba Watendaji watakaoteuliwa pamoja na kazi zao za Maofisini, watenge muda kuzitembelea  Taasisi zilizo chini yao ili waone uwajibikaji wa viongozi wanaozisimamia Taasisi hizo.  Naahidi kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kuyatumbua majipu yatakayojitokeza.  Nitamuomba Mhe. Rais aniunge mkono kwa uamuzi wowote nitakao uchukua dhidi ya mtendaji yeyote ambaye ataonekana hawajibiki vipasavyo, kwa sababu ya ama uvivu, uzembe, dharau au ubadhirifu.  Wako watendaji, Mhe. Spika, wanakatazia jambo la maendeleo kwa sababu ya ubinafsi. Watendaji hawa nao hatutawavumilia.

15.    Mheshimiwa Spika, naamini siyo baada ya muda mrefu Mheshimiwa Rais atateua Baraza lake la Mawaziri.  Ni imani yangu kwamba tutashirikiana pamoja na Watendaji watakao teuliwa ili kulisukuma gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya wananchi wetu.  Natoa wito kwa watakaoteuliwa kuwa Mawaziri nao wasikae maofisini tu, wakipepewa na mafeni na viyoyozi, bali watenge siku waende vijijini wakaangalie wananchi wenye matatizo na waone namna gani wataweza kuwasaidia.  Kila Waziri kwa eneo linalomhusu.

16.    Mheshimiwa Spika, migogoro ya ardhi imekuwa changamoto kubwa kwa Serikali yetu katika kipindi kilichopita.  Migogoro mingi imekuwa ikisababishwa na baadhi yetu viongozi kwa sababu za kitamaa.  Kama hiyo haitoshi, baadhi ya wananchi wanaendesha ujenzi wa nyumba kiholela bila ya vibali vya kujengea na wakati mwingine katika maeneo yasiyo ruhusiwa kama vile kwenye maeneo ya vianzio vya maji na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa miji ya kisasa.  Tunawatahadharisha waliojenga katika maeneo hayo.  Katika hotuba yake aliyoitoa wakati akilizindua Baraza hili, Mheshimiwa Rais alilizungumzia sana suala hili.  Niwakumbushe aliyosema, namnukuu:
“Napenda nitoe indhari kuwa Serikali haitomvumilia kiongozi wa ngazi yoyote ambae atajijengea tamaa na akajiingiza katika migogoro ya ardhi au akashindwa kutatua migogoro iliyopo katika dhamana yake.  Si siri kwani wapo baadhi ya viongozi waliojiingiza katika matatizo ya ardhi na kusababisha mzozo mkubwa kwenye jamii.  Migogoro ya ardhi ni kadhia ambayo tunataka tuimalize katika kipindi hiki cha miaka mitano ijayo.  Kwa hivyo, nawatahadharisha viongozi watakaopewa dhamana ya kushughulikia masuala ya ardhi wayazingatie maelezo yangu haya.”

17.    Mheshimiwa Spika, mnamo siku za hivi karibuni kumekuwepo na upandaji wa bei za bidhaa bila ya sababu za msingi.  Serikali inalifuatilia suala hili kwa karibu sana, na atakaye gundulika kupandisha bei kiholela atafungiwa leseni yake ya kuendeshea biashara mara moja.
18.    Mheshimiwa Spika, ninachukua nafasi hii kutoa wito maalum kwa Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza lako Tukufu kushirikiana na wananchi katika kuendeleza usafi wa mazingira na kutekeleza maelekezo yote ya Wataalamu wa afya ili kujikinga na maradhi ya miripuko kikiwemo Kipindupindu kwani ugonjwa huo bado upo, na namna moja ya kuuepuka ni kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi.
Pia, ninaomba niwakumbushe Waheshimiwa Wawakilishi na wananchi tuzitumie vizuri mvua zinazoendelea nchini kwa kuendeleza shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara kwa lengo la kupata mavuno mengi zaidi na kujiongezea kipato. Sambamba na hayo, Serikali inaendelea kuwataka wananchi wanaoishi sehemu za mabondeni waendelee kuchukua hadhari wakati huu wa mvua zinazoendelea ili tuweze kuepuka athari na majanga yasiyo ya lazima.  Tunawasihi wananchi hao wahame kutoka mabondeni humo na kuhamia sehemu za juu ili kuepuka uharibifu wa mali zao na hata upotevu wa maisha yao.

19.    Mheshimiwa Spika, mwisho, ingawa si kwa umuhimu, napenda kumshukuru sana Spika wetu Mstaafu, Mhe. Pandu Ameir Kificho kwa kuliongoza Baraza hili kwa umahiri mkubwa kwa mudakwa miaka 20 mfululizo.  Mhe. Kificho aliliongoza Baraza hili kwa hekima, busara na uvumilivu mkubwa.  Ninamtakia kila la kheri na mafanikio mema katika shughuli zake za baadae. 
Lakini pia niwashukuru Mhe. Ali Abdulla Ali, Naibu Spika Mstaafu, Waheshimiwa Mgeni Hassan Juma na Mahmoud Mohamed Mussa ambao walikuwa Wenyeviti wa Baraza hili.  Ni dhahiri kuwa wote walituongoza vizuri katika kipindi chote cha miaka 5 iliyopita.  Nao nawatakia kila la kheri na mafanikio mema.

20.    Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru wote waliotuwezesha kukamilisha shughuli zilizopangwa kwenye Mkutano huu wa Kwanza wa Baraza la Tisa la Wawakilishi kwa ufanisi mkubwa. Pongezi hizo zaidi ziwafikie watendaji wote wa Baraza hili la Wawakilishi wakiongozwa na Katibu, Dkt. Yahya Khamis Hamad.  Ni ukweli usiofichika kwamba tumeanza vizuri na ninaamini tutaendelea vizuri.  Mungu libariki Baraza hili, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.  Lakini pia niwapongeze wakalimani wetu wa lugha ya alama ambao wamewawezesha Waheshimiwa Wawakilishi wenye ulemavu wa kusikia kufuatilia yote yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Baraza.  Pia nawashukuru wanahabari kwa kufanya kazi ya kuwahabarisha wananchi wetu yale yaliyokuwa yakiendelea Barazani hapa.

21.    Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Mahonda kwa imani kubwa walionipa kwa kunichagua kuwa Mwakilishi wao.  Nawaahidi kuwa nitawapa utumishi ulio bora na kutekeleza ahadi zote nilizozitoa wakati wa Kampeni.  Nawaomba wanipe ushirikiano wao ili tuweze kuendeleza Jimbo letu na kujiletea maendeleo.

22.    Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia niwatakie Waheshimiwa Wawakilishi kila la kheri na mafanikio mema katika kuwatumikia wananchi wao Majimboni mwao.  Aidha, nawatakia safari njema na ya salama ya kurudi Majimboni mwao, na hasa Wawakilishi wenzetu kutoka Pemba kwa sababu wao wana safari ndefu zaidi kuliko wenzao wa Unguja.

23.    Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naomba sasa kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu liahirishwe hadi siku ya Jumatano tarehe 18 Mei, 2016, saa 3.00 barabara za asubuhi.

24.    Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.



Sehemu ya kufanyia Tawaaf ya muda Msikiti wa Makkah yaanza kubomolewa

$
0
0


Hatua ya kwanza ya kubomoa eneo la kufanya Tawaaf lililojengwa kwa muda imeanza ndani ya Masjid Al Haraam, Makkah, Saudi Arabia. 

Kazi hii inatarajiwa kumalizika Mei 25 kabla ya kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhaan.


Yanga ikijifua Uwanja wa Gombani kukabiliana na Al Ahly Jumamosi

$
0
0
 Timu ya Yanga ikiendelea na mazoezi ya mwisho Ijumaa kabla ya kukabiliana na Al Alhly Jumamosi katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam
Timu ya Yanga wakiwa katika mazoezi ya mwisho kabla ya kukutana na timu nguma ya Al Ahly Jumamosi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Kocha Plum ndfani ya Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba walipopiga kambi kwa ajili kukabiliana na waarabu.

Picha na Abdi Suleiman, Pemba

BREAKING NEWS: Dkt Shein atangaza baraza lake la mawaziri

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza jipya Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.
Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo la Mapinduzi kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7 na taasisi za wizara alizozivunja amezihamishia ambapo  katika baadhi ya wizara za sasa.
mawaziri hao watawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
      Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.

2). Wizara nchi Afisi ya Rais Katiba  Sheria Utumishi wa Umma na utawala bora – 
     Mhe. Haroun Ali Sleiman.
    Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Katiba .Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora 
      Mhe. Khamis Juma Maalim.  

3). Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ 
      Mhe. Haji Omari Kheir.

4). Wizara ya nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa  Rais 
      Mhe. Mohammaed  Aboud. Mohammed

5). Waziri wa Fedha na Mipango 
      Mhe. Dk. Khalid Salum Mohd.

6). Wizara ya Afya
      Mhe Mahmoud Thabit Kombo.
Naibu Wizaya ya Afya .
      Mhe.Harusi Said Suleiman.

7). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
      Mhe.Riziki Pembe Juma 
Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali.
      Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri.

8). Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
      Mhe. Balozi Amina Salum Ali.

9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji
     Mhe Balozi Ali Karume 
Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji 
Mhe.Mohamed Ahmed Salum.

10). Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo 
         Mhe.Rashid Ali Juma 
Naibu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo.
          Mhe.Chumu Kombo Khamis.

11).Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi
        Mhe.Hamad Rashid Mohd 
Naibu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
   Mhe.Lulu Msham Juma.

12).Wizara ya  Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
        Mhe.Mauldine Castiko.

13). Wizara ya Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Salama Aboud Talib.
 Niabu Waziri Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
       Mhe.Juma Makungu Juma.

Mhe Said Soud na Juma Ali Khatib wateuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum:

i.            Mhe. Said Soud Said – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

ii.          Mhe. Juma Ali Khatib – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
 
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 9 Aprili 2016.
    
Waheshimiwa wote waliotajwa wanaombwa wafike Ikulu Mjini Zanzibar kesho Jumapili tarehe 10 Aprili 2016
saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.



(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee),
KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.


                                                               
9 APRILI, 2016


Dk Shein, Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar Wakati wa Kutangaza Baraza Jipya la Mawaziri Wake.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakati wa kutangaza Baraza lake Jipya la Mawaziri Ikulu leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakati wa kutangaza Baraza lake Jipya la Mawaziri Ikulu leo.


Waandishi wa habari wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza nao katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Farouk Karim alipata fursa ya kuuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi uliofanyika Ikulu Zanzibar leo.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha TV cha Chanel Ten Munir Zakari akiuliza swali katika mkutano huo na Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu Zanzibar.
Mwandishi wa Kituo cha TV cha Star Tv Ndg Abdalla Pandu akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar Leo Ndg Hafsa Golo akiuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi wa kutangaza Baraza la Mawaziri Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijibu maswali ya baadhi ya waandishi waliopata fursa ya kuuliza. 
Waandishi wa habari wakiwa makini wakifuatilia maelezo ya Rais wa Zanzibar Dk Shein, wakati akizungumza na Waandishi Ikulu Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandishi katika kutangaza baraza jipya la Mawaziri Zanzibar Ikulu leo.asubuhi Zanzibar.
Waandishi wa Habari Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Waandishi wa Habari Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari Zanzibar, baada ya mkutano wake na Waandishi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kingozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee na Washauri wa Rais Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari baada ya mkutano wake na Waandishi Ikulu Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wakichangia Hutuba ya Rais wa Zanzibar Alipolihutubia Baraza Wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Tisa.

$
0
0

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdul-latif Yussuf akichangia wakati wa mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake Mhe Mgeni Hassan Juma akichangia hutuba ya Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Maalim Rashid Makame Shamsi. akifuatilia michango hiyo wakati wa Baraza la Tisa lililofanyika katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar. 
 Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mhe Moudline Castico akichangia Hutuba ya Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliomaliza kikao chake jana na kuahirishwa hadi mwezi wa tano mwishoni.
Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake Mhe Shadya Mohammed Suleiman akichangia hutuba ya Rais wa Zanzibar. wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Azindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege Msasani Beach Waterfort Leo.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Leo Aapril 09,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Kuli Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang,  Leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront akikabidhi Mfano wa hundi yenye jumla ya Tshs. 10,000,000. Kwa Uongozi wa Shule Msingi Mbuyuni kwa ajili ya kuendeleza Shule hiyo. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wapili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang wa pili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Pazia kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo, Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront, Leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Afisa Muandamizi wa Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wakati wa ghafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Gropu 6 ya China zinazojengwa Msasani Beach Waterfront. (Picha na OMR).
Viewing all 36095 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>