Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35847 articles
Browse latest View live

Waziri Makamba afanya ziara Wilaya ya Kaskazini Pemba

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea  mara baada ya kupokea taarifa  ya Mkoa wa  Kaskazini Pemba alipokua ziarani Mkoani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka Wananchi wa Zanzibar  kuulinda na kuuheshimu Muungano pamoja na mapinduzi tukufu ya Zanzibar. Ameyasema hayo alipokua ziarani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aliongeza kuwa anaipongeza Serikali ya Mkoa kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha  wanasimamia usalama kwa raia wote . Akiwasilisha  taarifa kwa Mh Waziri, Katibu tawala wa Mkoa wa Kasazini Pemba Mohamed Ali alitaja changamoto zinazowakabili ni uchakavu wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  hivyo kuomba Waziri awsaidie.

 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba yupo katika ziara mkoani Kaskazini Pemba pamoja na Unguja.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Yusuf Mohamed Ali akisoma taarifa ya Mkoa wakati akiiwasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea mkoa huo huko Pemba
 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  (aliyenyoosha mkono)  akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Wete- Pemba Bwana Rashid  Hadid Rashid wakati alipokua ziarani mkoani Kaskazini Pemba.
 Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akikagua mazingira ya jengo ala Ikulu ndogo ya Ofisi ya Mh Makamu wa Rais lililopo Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi  ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia kingo za uzio wa  jengo la makazi ya  Makamu wa Rais huko Wete- Pemba.

Umuhimu wa kuanzisha Shirika la Ndege la Zanzibar wagusiwa BLW

Waziri Amina akutana na wazalishaji chumvi kisiwani Pemba

$
0
0
 
Kufuatia Tanzania kuelekea kua nchi ya viwanda na hatimae Zanzibar nayo ipo mbioni na hatua mbalimbali zimeanza kutekelezwa ili kufikia huko ifikapo 2020. 

Mh Waziri wa biashara , viwanda na masoko Zanzibar Amina Salum Ali jana alikua na maongezi maalum baina yake na wazalishaji chumvi kisiwani Pemba ambapo kwa namna moja ama nyengineyo nao ni wadau miongoni mwa wataokaofanikisha kuifikisha Zanzibar huko. 

Pia waziri huyo alikua na ziara maalum ya kuwatembelea wakulima wa mbogomboga na wakulima wa mazao ya karafuu pamoja na viungo vyengine mbalimbali,ambapo katika ziara hiyo alitoa miongozo kwa walima hao ili kufanikisha uzalishaji bora na upatikanaji wa soko la uhakika. 

 Sikiliza mahojiano maalum baina ya waziri huyo na mwandishi wa habari Salmin Juma aliyetaka kujua ni kwa kiwango gani Zanzibar inakwenda kufanikiwa kua nchi ya viwanda ifikapo 2020.

Serikali Yapiga Marufuku Kusoma Degree Bila Kupitia kidato cha sita - Form Six

$
0
0

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katikals mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.


Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako

Waziri Makamba atoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa mbunge wa Dimani - Hafidh Ali Tahir

$
0
0
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano Mazingira Mh. January Makamba akiwa pamoja na mjane wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani Zanzibar(CCM) Bi. Shekha Said alipoenda kuwapa pole wanafamilia huko nyumbani kwa Marehemu Maungani Kisiwani Zanzibar. Mheshimiwa Waziri hakuwepo Nchini wakati msiba wa Mbunge huyo unatokea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwapa pole wanafamilia wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani(CCM) alipowatembelea nyumbani kwa Mbunge huyo huko Maungani Zanzibar. aliyekaa kushoto ni ni baba mlezi wa Marehemu Mzee Kombo M. Kombo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwapa pole wanafamilia wa Marehemu Hafidh Ali Tahir aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani (CCM) alipowatembelea nyumbani kwa Mbunge huyo huko Maungani kisiwani Zanzibar. Aliyekaa wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Mh. Ayoub Muhammed Mahamoud.

Rais Magufuli ampokea Rais wa Zambia leo

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akikagua gwaride rasmi i mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

Rais Magufuli ampokea Rais wa Jamhuri ya Chad leo

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno akipokea shada ya maua  mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli amlaki  mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha  na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno kwa viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimzawadia ki9nyago cha Kimakonve cha "Umoja" na picha ya kuchora ya tembo na Mlima Kilimanjaro  na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili  kwa mazungumzo Ikulu  jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

Wizara ya ujenzi na Mawasiliano kuzifanyia ukarabati barabara za ndani jimbo la Mkoani

$
0
0
Na Salmin Juma , Pemba

Naibu Waziri wa ujenzi na mawasiliano Zanzibar, Mh Mohammed Ahmada Salum amesema wizara imepanga kuzifanyia ukarabati barabara za ndani katika jimbo la Mkoani ili ziweze kupitika.

Amesema lengo la Serekali ni kuona wananchi wake wanaondokana na usumbufu wanaoupata wakati wa kusafiri na kusafirisha bidhaa zao.

Mh Mohammed ameeleza hayo kwa nyakati tofauti alipozitembelea barabara za ndani zilizomo katika jimbo la Mkoani pamoja na jimbo la Chambani na kuona hali halisi za barabara hizo.

Amesema ni vyema kwa wananchi kuwa wastahamilivu wakati serekali ikijiandaa kuziboresha barabara hizo ambazo ni kiunganishi kikubwa cha uchumi.

Nae mwakilishi wa Jimbo la Mkoani, Mmanga Mjengo Mjawiri ameiomba Wizara kuziangalia vyema barabara hizo ili kuwarahisishia wananchi kuyafikia masoko na mahitaji yao mengine ya kijami.

Mapema wananchi wa jimbo la Mkoani na Chambani wameiomba serekali kuharakisha kuziboresha barabara hizo ili ziweze kupitika kwa urahisi zaidi.

Wafanyabiashara watakiwa kuwa makini na vitendo vya utapeli

$
0
0
Jeshi la polisi mkao wa Mjini Magharibi limewatajka wananachi hususan wafanya biashara hususan wafanya biashara kuwa makini na wimbi la vitendo vya utapeli vilivyoshamiri katika siku za karibuni. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Hassan Nassir ametowa rai hiyo kufuatia polisi kufanikiwa kuwakamnata watu wawili waliojipatia kiasi cha shilingi 31 milioni baada ya kufanya manunuzi na kutowa hundi bandia katika mitaa ya Amani na Mbuyuni. 

Amewataja watu hao kuwa ni Festo Kayange Masanja mkaazi wa Migombani na Othman Mohamed Suleiman mkaazi wa Kwarara 

Kamanda Hassan ameeleza pia kwamba Polisi imefanikiwa kukamata katuni kumi na nane za bidhaa ambazo tayari zilishachukuliwa kitapeli na watu hao. 

Katika hatua nyengine Jeshi la Polisi limegundua vituo sita vinavyotengeneza vyeti na vitambulisho bandia ikiwemo leseni, bima na vyeti vya kuzaliwa na linakusudia kufanya operesheni kubwa kudhibiti hali hiyo.

Source: ZBC

Naibu Waziri Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe:Antony Mavunde Azindua Tamasha la AMANI JOGGING jijini Dar es Salaam Leo.

$
0
0
Mhe:Naibu Waziri Antony Mavunde Mapema ya leo akiongoza Jogging ya KM 8 Iliyo anzia Mlimani City na Kuishia katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam
Mhe:Naibu Waziri Antony Mavunde Mapema ya leo akiongoza Jogging ya KM 8 Iliyo anzia Mlimani City na Kuishia katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam
 Vijana wa Club ya Jogging Temeke Wakiimba Nyimbo za Hamasa
 Jogging ikiendelea
Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi Vya Jogging Club Dar es salaam Charles P Malim Akisoma Risala Kwa Mgeni Rasmi
Naibu Waziri Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe:Antony Mavunde akihutubia katika Tamasha Hilo la Amani Jogging Katika Viwanja Vya Leaders Club

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),Watoa Msaada wa Komputa kwa Shule ya Sekondari Chalinze Mkoa wa Pwani.

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), Joseph Kilongola, (wakwanza kushoto-mbele), Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mhandisi Peter Ulanga, (wakwanza kushoto-nyuma), wakishuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, (mwenye tai nyekundu), Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (wakwanza kulia), Diwani wa Kata ya Bwilingu, Lucas Lufunga, (wane kulia), na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa, wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya kopyuta zilizotolewa na UCSAF kwa shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Mawasiliano kwa wote, (UCSAF), umetoa msaada wa kompyuta 10 kwa Shule ya Sekondari Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni moja ya jitihada za Mfuko huo kuwawezesha wananchi wa kada mbalimbali kupata fursa ya mawasiliano.
Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya msaada huo, shuleni hapo mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola alisema, mfuko ulipokea maombi kutoka shule hiyo ya uhitaji wa kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hiyo kupata fursa ya kujifunza teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta. 
"Ili kuwafundisha watoto wetu kupitia internet, ni vizuri shule iwe na kompyuta za kutosha, Mfuko ulikubali ombi la shule ili kuwapatia kompyuta 10  kuiwezesha maabara yao ya kompyuta kutumika kwa ufanisi zaidi, na ni matumaini yetu kuwa kompyuta hizi zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwaelimisha wananfunzi na kuwawezesha walimu kuzitumia kama nyenzo ya kupata maarifa ya ziada kwa ajili ya kufundisha na hivyo kuboresha maendeleo ya wananfunzi na jamii inayotuzunguka." Alisema na kuongeza.
 Baadhi ya kompyuta zilizotolewa na Mfuko kwa shule hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), Joseph Kilongola 
"nimeelezwa na mheshimiwa Mwalimu Mkuu, kuwa jumuiya inayotuzunguka Chalinze sekondari inakuja kujifunza hapa wakati mwingine namna ya kutumia komyuta kwakweli hili ni jambo zuri na ndio malengo ya mfuko kuhakikisha jamii inafikiwa zaidi na huduma za mawasiliano." Alifafanua Mwenyekiti huyo wa bodi.
Mfuko wa mawasiliano kwa wote ni taasisi ya serikali ambayo jukumu lake kubwa ni kuhakikisha sehemu ambazo wananchi hawafikiwi vilivyo na huduma za mawasiliano kama vile simu kutoka mitandao mbalimbali, Mfuko uhakikishe unahamasisha makampuni hayo kufikisha huduma hiyo kwa wananchi. "Serikali baada ya kugundua makampuni ya kutoa huduma za mawasiliano hayavitiwi kuwekeza maeneo ya vijijini, kwa kuhofian kutopata faida, ikaanzisha mfuko huu mwaka 2006 ili ksehemu kama hizo zikitambuliwa, taratibu zifanyike kuwahamasisha hao wawekezaji waweze kwenda huko ili kuhakikisha huduma za mawasuikliano zinawafikia watanzania, na wachangiaji wakubwa wa Mfuko huu ni serikali na makampuni yote yanayotoa huduma za mawasikiano yanachangia Mfuko huo na wadao wanaotakia mema nchi yetu kama vile Benki ya Dunia huchangia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga, akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, (anayeshughulikia mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwaasa wanafunzi kujifunza zaidi elimu ya kompyuta na sio kujifunza word, excel na access, kwa sasa mafunzo hayo hayatoshi, na hivyo aliwahimiza wanafunzi lkujifunza zaidi ya hapo na hususan kutengeneza nyenzo za kutumia kompyuta, (computer applications).

"Wenzetu huko nchi za nje ambako wametutangulia katika teknolojia hii ya mawasiliano ya kompyuta, tangu shule za vidudu watoto wanafundishwa jinsi ya kuandika programs, bila shaka sisi sote wenye simu za mikononi kwenye simu zetu tunazo nyenzo mbalimbali (applications),  tunazozi zitumia kupakua (dowload), vitu mbalimbali  kutoka Google play, kwa hivyo ni vema tukaanza kujiongeza ili kupata manufaa zaidi ya kompyuta." Alisema Profesa Kamuzora.

Mbunge wa chalinze, Ridhwani Kikwete, aliushukuru mfuko wa UCSAF kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa kompyuta shuleni hapo. "Naamini msaada huu utatusaidia sana kuhakikisha wananfunzi wetu wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia internet lakini pia kujiongezea maarifa mbalimbali yatokanayo na kompyuta.

 Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, (aliyesimama), akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa kompyuta hizo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano), Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Edes P.Lukoa.

 Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola, (kulia), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga, wakijadiliana jambo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora, (aliyesimama), akitoa hotuba yake

 Mbunge wa Chalinze, Rizwani Kikwete, (kulia), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora, wakati wakitembelea maabara ya kompyuta ya shule hiyo
 Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Kamuzora, Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete, Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Ulanga, na viongozi wengine wakitembelea maabara hiyo.
 Mkuu wa Huduma za Manunuzi wa UCSAF, John S.Munkondya, (kushoto), akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chalinze, Emmanuel Kahabi
 Mbunge Kikwete, akiteta jambo na Mhandisi Ulanga
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta

Vijana Wakisenebuka kwa Furaha baada ya Kumaliza Mafunzo ya Ujasiriamali

$
0
0




Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.

Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.

Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akizungumza na Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Mafunzo ya Siku tano ya Ujasiliamali, Fursa na Taratibu za kufanya biashara kuelekea Soko la Jumuiya ya Afrika Mashari. Nasimi alifunga mafunzo hayo yaliyomalizika juzi Nov 25, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza.

Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akifurahia na Vijana hao wakati wakiimba wimbo maalum.

Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'The Foundation For Civil Society' Nasim Losai, akifurahia na Vijana hao wakati wakiimba wimbo maalum.

''Sasa Mafunzo yamefungwa rasmi'' .......

Waratibu wakiweka mabo sawa wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Mkufunzi Peninah akiwaelekeza baadhi ya Vijana kujaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakielekezana kujaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo. Ila wengine walikuwawakipiga chabo kama Class wakati wa Mtihani mwananguuuuuu........
Vijana wakijaza Fomu za Mpango kazi baada ya kumalizika mafunzo hayo.

Usafi Eneo la Kijangwani

$
0
0
Wafanyakazi wa Baraza la Manispa Zanzibar wakifanya usafi katika eneo la kijangwani baada ya kuhama wafanyabiashara za mbao katika eneo hilo ili kupita ujenzi wa kituo cha kisasa cha daladala katika eneo hilo zamani kulikuwa na kituo cha mabasi.   


Wanafunzi wa Darasa la Nne Zanzibar wafanya Mitihani yao ya Darasa la Nne.

Harakati Marikiti Kuu Darajani Zenj.

$
0
0
Wavuvi kutoka katika Kijiji cha Kizimkazi Unguja wakishusha samaki aina ya Nduaro katika marikiti Kuu ya Darajani Unguja kutoka katika gari ya abiria ya Kizimkazi 




Huduma ya maji yarudisha nyuma nguvu za akinamama

$
0
0

Na Salmin Juma, Pemba

Kufuatia msemo mashuhuri nchini  wa akina mama wakiwezeshwa wanaweza, imeonekana dhahiri kua wanaweza  kutokana na baadhi yao kuonekana wakijishuhulisha katika maeneo tofauti ya ukuzaji uchumi na maendeleo ikiwemo katika sekta ya kilimo, mifugo na hata uvuvi.

Hayo yamejidhirisha wazi jana katika ziara maalum ya waandishi wa habari kisiwani Pemba walipowatembeela wakulima wa mbogamboga ambao ni wanawake kutoka Mchangamdogo Wilaya ya  Wete mkoa wa kaskazini Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi  Naibu mwenyekiti wa kikundi cha "TUNASONGMBELE"  wanaojishuhulisha na ukulima wa  Pilipili hoho, Tungule (nyanya) na Bilinganyi Bi Asha Khamis amesema kua, kutokana na hali halisi ya kimaisha ilivyokua ngumu kwa pamoja wameamua kujikusanya na kuunda kikundi kushikiriana katika sekata ya kilimo.

Amesema licha ya changamoto mbalimbali zinzowakabili ikiwamo soko la uhakika na kutokuwepo kwa huduma ya maji shambani mwao lakini mpaka hivi sasa nyota ya matumaini mema wameshaanza kuyaona.

 “kikundi chetu bado hakijakua na pia hatujaanza kugaiana faida, tunachokipata tunakiweka ili tuzidi kutanua mradi wetu kufikia malengo tuliyojipangia  na kwakweli tulichonacho tunashukuru” alisema Naibu huyo.

Akiitaja kwa mara nyengine tena  changamoto ya maji inayowakabili katika ushirika wao kwa hamasa amesema huwalazimu kuchukua huduma hiyo kutoka majumbani mwao na kumwagilia mazoa, hali ambayo inawatatiza na kuwapa usumbufu mkubwa.

Akijibu suala la mwandishi wa habari aliyetaka kujua uzalishaji wao ukoje pamoja na soko, amesema shamba lao ni la robo ekari na  tungule wanazozalisha kila msimu ni gari moja ya keri  hivyohivyo katika mazao mengine na soko bado ni tatizo  ambapo hutegemea  baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wanaojitokeza  kununua bidha hizo shambani kwao.

Bi Hadia Juma Hamad  mwanachama wa kawaida katika ushirika huo amesema kua, tokea kujiunga katika ushirika huo hali ya kiuchumi imekua afadhali ingawa bado hawajafika walipo pakusudia.

“lengo letu hasa na tukiwezeshwa kupatiwa huduma ya maji tulime eneo kubwa zaidi kwani eneo lipo ila maji tu ndio tatizo” alisema bi Hadia.

Ushirika wa "TUNASONGMBELE"  unajumla ya wanachama ishirini (20) kumi na nne katia yao (14) ni wanawake na sita (06) ni wanaume ambapo  wametoa wito kwa serikali  na taasisi binafsi kujitokeza kuwasaidia katika kutatua changamoto zao ili kufikia lengo walilolikusudia la kujikwamua kiuchumi na hatiame akinamama kupiga hatua za kimaendeleo zaidi.

Balozi Seif akikagua mipira inayozalishwa kisiwani Pemba

$
0
0

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe;Balozi Seif Ali Iddi,akiangalia moja ya mipira inayozalishwa na wafanya kazi wa kiwanda cha Mipira Kisiwani Pemba,(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Alloo avitaka vyombo vya habari kusaidia kulaani vitendo vya ubakaji

$
0
0
 Wanafunzi kutoka shule ya mandalizi ya Madrasatul Nasril Islamiyya ya mjini Zanzibar wakisoma utenzi mbele ya mgeni rasmi, Yasmin Alloo jana.Kutoka kushoto ni Hajra Suleiman, Asia Mharami na Hairat Hamad
Picha na Martin Kabemba.
 Yasmin Alloo akizungumza kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya mandalizi ya Kidutani mjini Zanzibar.
Picha na Martin Kabemba

Mjumbe wa zamani wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Yasmin Alloo amevitaka vyombo vya habari nchini kusaidia katika mapambano na kulaani vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto vikiwepo ubakaji na utumikishwaji wa ajira zisizo rasmi.

Akizungumza kwenye sherehe za wazazi wa shule ya mandalizi ya Madrasatul Nasril Islamiyya ya mjini Zanzibar jana, akiwa mgeni rasmi, Yasmin pia amewataka wazazi kufufua utamaduni wa kizanzibari katika malezi ya watoto kwa kufuata maadili ya kizanzibari badala ya kuwaacha wakiiga tamaduni za mataifa ya kigeni,

Tanzania to host High-level roundtable organized jointly by UN-OHRLLS and EnergyNet Ltd, 6 December 2016

$
0
0

LONDON, United Kingdom, November 28, 2016/ -- The United Nations Office of the High Representative for Least Developed Countries, Landlocked Developing Countries and Small Island Developing States (UN-OHRLLS) (http://UNOHRLLS.org), together with EnergyNet (www.EnergyNet.co.uk) will be convening a joint high-level roundtable on 6 December 2016, Dar es Salaam, Tanzania.

The event will bring together participants from the two sustainable energy events which are running back to back in Dar es Salaam during a week dedicated to sustainable energy. Roundtable participants will discuss practical ways for African countries to achieve the three universal goals on sustainable energy. With a particular focus on building durable partnerships and financing initiatives, contributors will draw on their experience working in the field of sustainable energy, sharing success stories but also highlighting challenges and lessons learnt in mobilizing investment and innovation.

Prior to the roundtable, UN-OHRLLS will host the 2 day meeting Regional Meeting on Sustainable Energy for Least Developed Countries, 5-6th December (http://APO.af/TIHR7b), which will bring together key stakeholders in the African energy sector, highlighting ways to put energy finance in motion for least developed countries and deliver life changing benefits to vulnerable communities. Sessions will offer practical, workable solutions in areas including access to finance for energy initiatives, energy investment and business plans, benefitting from global energy initiatives, project preparation skills to attract investment and partnerships for sustainable energy.

The Africa Energy Forum: Off the Grid Summit, taking place 6-8th December (www.AEF-OffGrid.com) will focus on project opportunities for mini- and off-grid technology providers working in Africa’s energy space. The Summit will bring together ministries of energy, rural electrification agencies, philanthropic business foundations, banks, regulatory bodies, multilateral organisations and off-grid businesses to discuss topical issues concerning rolling-out off-grid projects across Africa.

Registered participants at both the UN-OHRLLS and EnergyNet’s Africa Energy Forum: Off the Grid Summit are invited to attend and the event which will also be open for members of the press. A brief Q&A session will take place at the end of the roundtable for members of the press.

When:  3:30 pm – 5:30 pm, 6 December 2016

Where:  Conference Hall of Bank of Tanzania, 2 Mirambo Street, Dar es Salaam, Tanzania, 11884. Map Location: http://APO.af/X0sNov

Speakers:           

  • Mr. Gyan Chandra Acharya, Under-Secretary-General, UN-OHRLLS
  • Hon. Sospeter M. Muhongo (MP), Minister for Energy and Minerals, The United Republic of Tanzania (tbc)
  • Mr. Joseph Yado Howe, Assistant Minister for Energy, Ministry of Lands, Mines and Energy, Liberia (tbc)
  • Christopher Baker Brian, Co-Founder, BBOXX
  • Veronica Bolton-Smith, Regional Director, East and Southern Africa, EnergyNet Ltd.
Distributed by APO on behalf of EnergyNet Ltd.. 

Balozi Seif aagiza ukuta uliojengwa kinyumne na sheria uvunjwe Kazole ifikapo Novemba 30

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati aliyevaa miwani akiangalia ukuta uliojengwa na Mtu aliyetumia nyaraka za Kikoloni zilizofutwa kufuatia Tamko la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la Mwaka 1964 mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964.

Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Issa Juma akimpatia maelezo ya jinsi Serikali ya Wilaya hiyo ilivyochukuwa hatua dhidi ya Mtu huyo.

 Balozi Seif akizungumza na Wagonjwa na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Kitope akiwahamasisha kushiriki katika uchunguzi wa Afya zao utakaotolewa na Madaktari Mabingwa kutoka Nchini India katika Kituo cha Afya cha Mahonda.
 Balozi Seif akipokea maelezo kutoka kwa Muuguzi Stara Ali Moh’d wa Kituo cha Afya cha Kitope hayupo pichani kuhusu utatuzi wa changamoto zilizokuwa zikikikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na huduma za maji safi na salama.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameagiza kwamba uamuzi uliotolewa na Serikali ya Wilaya ya Kaskazini “B” kufuatia  Mtu aliyejenga ukuta kwa nia ya kuzuia eneo la Ardhi  katika Kijiji cha Kazole  wa kumtaka avunje Ukuta huo hadi ifikapo Tarehe 30 Novemba mwaka huu uko pale pale.

Alisema kitendo cha Mtu huyo aliyetambuliwa kwa Jina moja la Bibi Fadia cha kudai  umiliki wa eneo hilo kwa kutumia nyaraka za zamani za Utawala wa Kikoloni zinakwenda kinyume na Tamko la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la kufuta nyaraka zote za kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua ukuta uliozunguushwa katika maeneo mawili tofauti  zikiwemo nyumba za baadhi ya Wananchi pembezoni mwa Bara  bara katika kijiji cha Kazole Wilaya ya Kaskazini “B”  Mkoa wa Kaskazini Uanguja.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kukabiliana na vitendo vya ghilba vinavyoonekana kuibuka katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba ambapo baadhi ya watu wanajitokeza kudai maeneo ya ardhi kwa kutumia hati na nyaraka zilizofutwa rasmi na Serikali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  aliuagiza Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Kaskazini “B” kuhakikisha kwamba agizo lililompa muhusika huyo la kuvunja kuta zake analitekeleza kabla ya Serikali kuchukuwa mkondo wake wa Sheria ikiwemo kuvunja kuta hizo kazi ambayo muhusika huyo atalazimika kulipia gharama hizo.

Balozi Seif aliwaonya baadhi ya Wananchi wanaopewa maeneo ya Kilimo au ujenzi wa Makaazi kupitia Mamlaka zinazohusika na Ardhi kuacha tabia ya kurubuniwa na Watu wanaotumia  fedha kuwahadaa katika kutaka kuwapokonya kijanja maeneo yao.

Alisema Serikali Kuu haitasita kuwafutia hati na nyaraka Wananchi hao wakionekana kwenda kinyume na makubaliano waliyopewa na badala yake   watapewa wale watakaohitaji maeneo hayo kwa kuyatumia kwa lengo lililokusidiwa.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Issa Juma  alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Serikali ya Wilaya hiyo kupitia Halmashauri yake ilimpa barua ya kusitisha ujenzi wowote mtu huyo baada ya kukosa vielelezo vinavyotambulika na Wizara inayohusika na masuala ya Ardhi.

Nd. Issa alisema Uongozi huo wa Serikali ya Wilaya ulilazimika kutoa agizo la kumtaka avunje kuta zake kabla ya Tarehe 30 Novemba 2016 baada ya kubaini kukiuka amri aliyopewa na Serikali ya Wilaya.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwaomba wananchi wa Wilaya ya Kaskazini B na vitongoji vyake  kujitokeza kwa wingi ifikapo Tarehe 3 na 4 Mwezi Disemba kuangalia afya zao katika Kituo cha Afya Mahonda.

Akizungumza na wagonjwa pamoja na watendaji wa Kituo cha Afya Kitope Balozi Seif alisema ujio wa Wataalamu Mabingwa kutoka Nchini India utatoa fura kwa wananchi kupata muda wa kuchunguza afya zao yakihusishwa  maradhi ya macho, Kisukari pamoja na sindikizo la damu { Blood Pressure }.

Alisema wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo katika uchunguzi huo hasa yale matatizo ya macho wataandaliwa utaratibu maalum wa kupatiwa tiba katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.

Kambi hiyo awali ilikuwa imepangwa kufanyika katika Kituo cha Afya Kitope lakini kutokana na sababu za kimsingi Wataalamu wa Sekta ya Afya wamependekeza kambi hiyo kufunguliwa katika Kituo cha Afya cha Mahonda  kwa vile kimebahatika kuwa na vifaa vingi vya uchunguzi vitakavyorahisisha kazi zao.
Viewing all 35847 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>