↧
Tangazo la Ajira DIRA TV
↧
Zanzibar inahitaji watalamu zaidi katika fani ya Sayansi
↧
↧
Former Kirkcaldy head boy’s big Zanzibar challenge
A former head boy of Kirkcaldy High School has spent three months helping rural farmers in Zanzibar. Alasdair Pilmer (22), who was head boy at KHS in 2012 before going on to complete an Honours degree in Geography at Aberdeen University, travelled to the African country with Voluntary Service Overseas (VSO).

Alasdair contributed as part of a group of British and local Tanzanian volunteers who organised Community Action Day events for isolated communities, with representatives from the Tanzanian Ministry for Agriculture and youth employment advisors.
As part of his trip, for which he had to undergo a selection process, he raised £885 for VSO to help pay for the equipment he needed. He lived and worked with local families and even managed to learn to speak some basic Swahili so he could communicate with them.
Alasdair, whose parents and younger brother live in Cluny, said: “I decided to volunteer with VSO because I wanted to put the volunteering skills I learned with the 14th Fife Scout group, and the practical skills gained from my degree, to good use and to make a positive impact in a developing country.
“During my time in Zanzibar I learned a wide range of things. Working and living cross-culturally has given me a new, fresher outlook and I was able to discover the similarities as well as the differences between Fife and an African/Islamic culture.
“I also learned plenty of useful employment skills such as leadership, confidence, teamwork and project management. From a personal point of view, I feel that the programme humbled me, and made me appreciate many of the things we take for granted in our everyday life in Scotland.
“When I was at Kirkcaldy High School, I never expected to spend time working in Zanzibar. Volunteering has allowed me to make a positive impact in communities facing rural poverty. “I would like to thank the 14th Fife Scout Group for the skills and development they provided which helped my selection and for their help with my fundraising.
“During my placement I gained a new appreciation of a different culture and lifestyle which allowed me to develop both personally and for my future employability skills. “I would strongly encourage any young person considering volunteering abroad to do so, it is a fantastic opportunity they will never forget.”
Read more at: http://www.fifetoday.co.uk/news/former-kirkcaldy-head-boy-s-big-zanzibar-challenge-1-4300006
↧
Rais Dk Magufuli amwandalia dhifa ya kitaifa mgeni wake Rais Edgar Lungu Ikulu Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume
Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Wimbo wa Taifa
Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa
Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa
Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama
Viongozi wakiwa wamesimama
Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia
Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa
Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria
Wageni mbalimbali
Mabalozi mbalimbali
Mabalozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje
Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali
Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje
Viongozi wa taasisi mbalimbali
Viongozi wa kidini na wageni mbalimbali
Makatibu wakuu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuma
Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia
Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza
Mrisho Mpoto akighani wimbo maalumu
Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi
Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi
Rais Edgar Lungu akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
Rais Edgar Lungu akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Rais Edgar Lungu akisindikizwa na mweyeji wake Rais Dkt Magufuli
Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakiondoka baada ya dhifa
Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU
↧
Prof. Ndalichako Akanusha Taarifa ya Wanafunzi wa Diploma Kuzuiliwa Kujiunga vyuo Vikuu

Aidha, imesema kwa waliomaliza kupitia mfumo huo na wapo kazini ni wajibu wa waajiri wao kuhakikisha wana sifa za kazi wanazofanya na kutumia fursa hiyo kufanya mitihani ili kuwa na sifa zinazohitajika.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya alitoa ufafanuzi huo jana Dar es Salaam kutokana na taarifa za upotoshaji zilizoenea mitandaoni kwamba serikali imepiga marufuku watu wenye Stashahada kujiunga na vyuo vikuu badala yake watakaoingia ni wenye sifa za kidato cha sita.
Manyanya alisema kwa waliopo vyuoni kwa sasa wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na sifa za shahada kwa kusafisha vyeti vyao na wapewe fursa ya kufanya mitihani hiyo waliyofeli na kama wamefaulu kozi hiyo, pia wataweza kufaulu mitihani hiyo itakayowapa sifa ya kusoma vyuo vikuu.
“Ni vitu tunavyovifanya wenyewe ila vina madhara makubwa, unakuta mtu anakaa nafasi kwa sababu ana vyeti, lakini uwezo hana… uhakiki utafanyika kwa vyeti na wanaofanya hivyo ni Utumishi,” alisema Naibu Waziri.
Alisema kwa watakaobainika pia kuingia vyuoni kwa sifa ambazo zilikuwa hazitakiwi kwa wakati huo ni batili zitafutwa na kwa watakaoingia kwa sasa vyuoni kwa kutumia njia zisizo rasmi na kubainika hata ikifika mwaka 2020 watafutwa kwa kuwa taarifa tayari wanayo.
“Kilichoongelewa siku ile ni kuruhusu kidato cha nne na kidato cha sita waliofeli kuingia kwenye ‘foundation course’ na diploma haikutajwa pale kwa kuwa haikuulizwa na hakuna kauli iliyotajwa pale kukataza watu wa diploma kwenda chuo kikuu,” alieleza Manyanya akirejea kauli ya Waziri wake, Profesa Joyce Ndalichako hivi karibuni katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) yaliyofanyika mkoani Pwani.
Profesa Ndalichako alikaririwa akisema vigezo vya udahili vinatakiwa kuzingatiwa.
“Nami ningependa nizungumzie kwamba foundation course hazimuongezei mtu sifa. Kama sifa ya kujiunga na chuo kikuu ni kufaulu kidato cha sita, kama amefeli Baraza la Mitihani linaruhusu kurudia mtihani, kwa nini anakwepa kule? Kwa nini? Kwa nini tunataka tuendeleze uchochoro,” alieleza Waziri Ndalichako.
Naibu Waziri alisema kuna njia mbili za kwenda chuo kikuu ikiwemo njia ya moja kwa moja na njia ya mbadala ya kuwa na vyeti vinavyotambulika na kinasimamiwa na mamlaka husika ambayo ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na wawe na ufaulu mzuri.
“Tanzania imejiwekea mifumo yake ya elimu ambayo inaendana na ngazi za kimataifa katika utoaji wa elimu na hapo awali tulikusudia kuhakikisha elimu inatolewa kwa watu wengi zaidi na hizo fursa zinawafikia wadau wote katika ngazi mbalimbali kwa kupanua elimu ya msingi hadi vyuo vikuu,” alieleza Naibu Waziri.
Alisema walitambua kuna wadau mbalimbali walitamani kusoma vyuo vikuu, lakini hawapati hiyo fursa na ndiyo wakaanzisha mfumo huo wa Chuo Kikuu Huria na mtu anaweza kusoma alipo na mfumo umekuwa ukiboreshwa siku hadi siku.
Alisema iliwekwa mifumo ya vyeti na ngazi zake kulingana na vigezo na hivyo siyo kila cheti kinachotolewa kinaruhusu mtu kwenda ngazi nyingine na kila mamlaka imepewa jukumu ili kulinda ubora wa elimu unaotolewa nchini.
Naibu Waziri alisema kutokana na uanzishwaji wa vyuo mbalimbali kumejitokeza changamoto na watu kutoka katika mfumo rasmi uliopangwa na kujiwekea mifumo binafsi ambayo imeingiza hata wanafunzi wa kidato cha nne ambao hawana sifa kuingia vyuo vikuu.
“Jambo hilo limesababisha kuwepo kwa msuguano, haiwezekani mtu afeli kidato cha nne bila kuwa na cheti kingine chochote anaingizwa katika kozi hiyo halafu anaingizwa chuo kikuu, sisi hatujarasimisha mfumo huo wa ‘foundation course’ na hatuna vipimo vyake,” alieleza.
Alisema kwa kawaida mwanafunzi mwenye diploma inayotambulika wamewekewa usawa wa alama fulani na kidato cha sita hivyo wanakuwa na sifa ya kuingia vyuo, lakini siyo waliofeli hivyo wanatakiwa kufanya utafiti zaidi katika kozi hiyo.
“Haiwezekani kila mtu akajianzishia mfumo wake tu, tulifikia eneo ambalo si zuri kama nchi na sasa tutaimarisha ubora…ukifeli kidato cha nne unatakiwa kwenda kusoma na kupata cheti kwenye mtaala unaotambulika na ukaenda diploma na unapofaulu unaweza kwenda chuo kikuu,” aliongeza.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila alisema suala la ‘Foundation course’ limelenga kumuandaa mtu mwenye sifa ambaye amekuwa nje ya mfumo kwa muda mrefu ili kuingia chuo kikuu, lakini walichokuwa wakikifanya wengi ni kuwachukua waliofeli kidato cha nne na sita na kuwaingiza katika kozi hiyo na hatimaye kuwaingiza chuo kikuu.
↧
↧
Balozi Seif Akabidhi Mchango Wake Aloahidi Kuchangia Ujenzi wa Jengo la Siti Bint Saad.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.(Picha na – OMPR –ZNZ.)
Na. Othman Maulid. OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Visiwa vya Zanzibar vitaendelea kupata heshima Kimataifa kadri siku zinavyoaidi kuyoyoma katika Nyanja ya sanaa na utamaduni kufuatia kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa na Msanii mkongwe wa Visiwa hivi marehemu Sidi Binti Saad.
Alisema Mchango wa Siti Binti Saad enzi zake kupitia Taarab asilia umeweza kuleta faraja kwa wapenzi wa Muziki huo katika kudumisha Utamaduni wa Kiafrika ndani ya Mwambao wa Afrika Mashariki, Nchi za Ghuba pamoja na baadhi ya Mataifa ya Bara la Asia.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati wa kukabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- alizoahidi kutoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Alisema jitihada zilizochukuliwa na Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad ya katika azma ya kutaka kumuenzi Mwanamuziki huyo Nguli Afrika Mashairiki na Bara la Asia inafaa kuungwa mkono na wapenzi wote wa fani hiyo iwe ndani au nje ya Nchi.
Akipokea mchango huo wa Balozi Seif Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar alimshukuru kiongozi huyo kwa kutekeleza ahadi aliyotoa kiasi kwamba imeleta faraja kwa Uongozi wa Taasisi hiyo.
Bwana Mohammed alisema katika kuthamini michango ya watoa ahadi Taasisi hiyo imeamua kutoa cheti Maalum kwa wachangiaji hao ili iwe kumbu kumbu nzuri kwao na vizazi vyao kutokana na kuunga mkono jambo hilo muhimu.
↧
Mtanzania wa Kwanza Kupanda Mlima Everest Uliopo Nchi Nepal Katika Mwaka 2012. Na Muafrika wa Tatu Kupanda Mlima Huo Mkubwa Duniani
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mrefu Duniani wa Mt.Everest uliopo Nchi Nepal ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa ukubwa.
Ndg Wilfred Moshi akiwa Zanzibar kwa matembezi na kuangalia Utalii wa Zanzibar na kupata nafasi kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar kwa mualiko wa Mhe Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Ndg Wilfred Moshi akitambulishwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa Mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akisalimia Wajumbe wa Baraza wakati wa kutambulishwa kwake.
Mtanzania wa Kwanza kupanda Mt. Everest upo Nchini NeNdg Wifred Moshi akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said. akiwa katika sehemu ya wageni katika ukumbi huo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akimtambulisha Mgeni wake Ndg Wilfred Moshi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, alipofika kutembelea na kujionea shughuli za Baraza la Wawakilishi wakati wa Mkutano wake leo asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mtanzania wa Kwanza na Muafrika wa Tatu Duniani kupanda Mlima wa Everest Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la wawakilishi Zanzibar akiwa mgeni wa Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya mgeni wake Ndg Wilfred Moshi ambae ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Everest..
Ndg Wilfred Moshi akitowa historia yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mualiko wa Mhe. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Tunguu Zanzibar. akitowa historia yake ya kufanikiwa kupanda mlima huo mkubwa duniani na kuelezea tayari ameshapanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 100.
Ndg Wilfred Moshi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kumbukumbu yake alipofika kutembelea Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar leo. 29-11-2016 akiwa mgeni wa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.![]()
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya pamoja na Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Everest uliopo Nchini Nepal Ndg Wilfred Moshi alipofika katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com
↧
UN na EU Waendeleza Kampeni ya Uelewa wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.
UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani. Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Moblog)
Semina katika vyuo hivyo ni sehemu ya mpango madhubuti wa Umoja wa mataifa uliozinduliwa Arusha Mei mwaka huu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wenye lengo la kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia. Ujumbe huo wa EU na UN pia ulipata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na EU ukiwamo wa Boma la Kijerumani ambalo lilikarabatiwa kwa ruzuku ya EU kupitia 'fahari yetu – Southern Highlands Culture Solutions'. Boma hilo ni moja ya majengo ya zamani katika mji wa Iringa na lilijengwa na Wajerumani mwaka 1900 kama hospitali ya kijeshi. Baada ya vita ya Kwanza ya Dunia, jengo hilo lilibadilishwa matumizi na watawala wapya, Uingereza, na kulifanya kuwa jengo la utawala. EU imesema inaona fahari kuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa katika sekta ya sanaa na urithi wa kitamaduni nchini Tanzania, ikifadhili miradi 10 iliyo chini ya programu ya 10 ya EDF ya kusaidia masuala ya kitamaduni. ![]()

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (upande wa kushoto katikati) pamoja na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) alipotembelewa ofisini kwake na ugeni huo. Kulia ni Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever pamoja na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi.
Masuala yanayohusu urithi wa kitamaduni ni muhimu katika kuchagiza ukuaji wa uchumi, ajira na huku ikifuma mahusiano ya kijamii, na kutoa fursa ya kuboresha utalii endelevu mkoani Iringa huku ikileta faida kwa wakazi wa eneo hilo. Bw. Rodriguez, akizungumza katika kampeni hiyo alisema kwamba ajenda 2030 ambayo ni ajenda ya maendeleo endelevu inahitaji ushiriki wa kila mmoja.Aliwapongeza wanachuo hao na wanazuoni kwa kujikita kutambua malengo hayo ya dunia. Aidha aligusia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa, kwa taifa kama la Tanzania vijana ni asilimia 60 ya wananchi wote waliopo.Alisema kwamba vijana wanajukumu kubwa la kushiriki katika maendeleo hayo kwa lengo la kuipeleka nchi katika hatua nyingine ya maendeleo. ![]()

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameongozana na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu cha Iringa.
Hata hivyo alisema kwamba ni wajibu wa kila mtu hasa vijana, kuhakikisha kwamba malengo hayo ya dunia yanafanikiwa . Alisema Umoja wa Mataifa kwa kusaidiwa na wadau wake muhimu kama Umoja wa Ulaya, utaendelea kusaidia Watanzania kuwajibika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuunga mkono malengo hayo ya dunia. Mmoja wa washiriki alipongeza Umoja na wa Mataifa kwa kuwafikia vijana wa vyuoni na kuwapa semina hiyo. “Ninajisikia mtu mwenye bahati kupata nafasi ya kujifunza maendeleo endelevu kutoka kwa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini. Nikiwa kama kijana, naona faraja kuona kwamba viongozi wetu wanafuata maelekezo yaliyofafanuliwa kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu; naamini kama tukijitahidi kuyafikia ifikapo 2030, basi Tanzania na duniani kwa ujumla itakuwa eneo jema la kuishi. Na kwa kuwa sasa natambua kuhusu malengo hayo ya dunia, ninaweza kutoa mchango wangu kusaidia kuyafikia -najisikia kuwezeshwa sana.” amesema Mary, mmoja wa washiriki. ![]()

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akisoma taarifa fupi ya Chuo Kikuu cha Iringa mbele ya ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wakati semina kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwenye semina ya malengo ya dunia kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa ambapo aliwaasa wakawe mabalozi wazuri wa malengo hayo kwenye jamii zao na wanafunzi wenzao wa vyuo vingine.


Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akitoa salamu za Umoja wa Ulaya kwa niaba ya Balozi wa Umoja huo, Bw. Roeland Van De Geer wakati wa semina Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanachuo wa Iringa iliyowezeshwa na EU.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kuhusu Malengo ya Dunia katika semina iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.


Mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayechukua Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa, Sarafina Sayi akiuliza swali kwa mkufunzi wa malengo ya dunia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.

Mwanafunzi wa Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa, Geoffrey Kadori akiuliza swali kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati wa semina ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo hicho.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

Pichani juu na chini ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kutoka vitivo tofauti chuoni hapo waliohudhuria semina ya malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).





Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla makabrasha na majarida yenye ripoti na taarifa mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya pamoja na Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs Champion), Sabinus Paul (kushoto) nje ya ukumbi kulikofanyika semina kuhusu SDGs kwa wanachuo wa Iringa.

Picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa semina hiyo huku wakiwa na mabango ya SDGs.

Muonekano wa nje wa jengo la Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni -Iringa Boma ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Kibao cha Makumbusho ya Mkoa wa Iringa kinachoratibiwa na Mradi wa Fahari yetu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Iringa

Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akielezea dhumuni la mradi Fahari Yetu unaolenga kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (mwenye suti) ambao ndio wafadhili wa jengo hilo la Makumbusho ya Mkoa wa Iringa. Wengine katika picha ni wahadhiri na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Iringa.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wangeni ndani ya Makumbusho ya mkoa wa Iringa.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa.

Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akitoa maelezo picha mbalimbali zinazoelezea historia ya mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa Chifu Mkwawa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro walipotembelea makumbusho ya mkoa wa Iringa

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma historia mbalimbali za enzi za utawala wa kichifu ndani ya Makumbusho ya Mkoa wa Iringa.

Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Jacob Shenyagwa (mwenye miwani) akitoa maelezo ya picha mbalimbali kwa ugeni huo wa UN na EU uliotembelea makumbusho hiyo iliyojengwa chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa kichifu kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini Iringa.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro wakitwanga mahindi kienyeji katika moja ya kinu kilichokuwa kinatumika enzi hizo za utawala wa kichifu kilichopo katika makumbusho hayo.

Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja kwenye sanamu maalum za mavazi ya kipindi cha utawala wa Chifu Mkwawa walipotembelea Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
↧
Dhifa ya Chakula cha Usiki Kilichoandaliwa kwa Wageni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Rais wa Zambia Edga Lungu,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa Rais wa Zambia jana,katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.28-11-2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta na Rais wa Zambia Edga Lungu wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni aliyoiandaa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa Rais wa Zambia Edga Lungu katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akifuatana na Rais wa Zambia Edga Lungu baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiagana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,iliyoandaliwa kwa Rais wa Zambia Edga Lungu akiwa nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.
↧
↧
Rais wa Zanzibar Dk Shein, Azungumza na Mwakilishi wa UNICEF
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo, [Picha na Ikulu.] 29/11/2016.
↧
Kama Matangazo Hamna Basi Tuige Mfano Huu Uwanjani Kwetu Kuvutia Uwanja.
Viwanja vingi sana vya michezo duniani hasa vile vya mpira wa miguu huonekana kupambwa na mabango mengi ya matangazo nje na ndani husu yale ya wadhamini wa mchezo husika.
Kuna yale ambayo huwekwa pembezoni mwa majukwaa ya watazamani na mengine hupita kwa mtindo wa kisasa(Electronics) kwenye eneo husika.
Miaka mitatu iliyopita viwanja vya Amaan na ule wa Gombani vilionekana kuwa na mabango hayo kupitia udhamini wa ligi kuu uliokuepo yaani Grand Malt.
Baada ya mdhamini huyo kuondoka hakuna tena mabango hayo. Lakini mtandao huu unakuja na ushauri juu ya mfano ulioanza kuonyeshwa na baadhi ya mashabiki wa timu.
Kiukweli nafsi yangu ilivutika sana kuona mashabiki wa timu ya Taifa ya Jang'ombe, Jang'ombe Boys na baadhi ya siku Kilimani City wakipamba majukwaa kupitia mabango yao.
Ikiwa hali kama hiyo hapo juu itaigwa na mashabiki wa timu nyengine naamini hata taswaira ya viwanja vyetu itapendeza na itakua chachu ya kuwavutia wawekezaji na makampuni kusogea kwenye ligi yetu kwa lengo la udhamini.
Waswahili wanasema "Kuiga jambo jema si vibaya".
Kwanini basi mashabiki wa timu husika washindwe kufanya hivyo.
Kumbuka mjenga nchi ni mwananchi, na mvunja nchi ni mwananchi. Kama matangazo hamna basi tuupambe uwanja kwa mabango ya mashabiki.
↧
Ligi Kuu ya Zanzibar Jangombe Boys Yaipiku Mafunzo na Zimamoto.
MSIMAMO LIGI KUU YA SOKA ZANZIBAR (UNGUJA) 2016-2017 | |||||||||
POS | TIMU | P | W | D | L | GF | GA | GD | PTS |
1 | JKU | 12 | 9 | 3 | - | 20 | 5 | 15 | 30 |
2 | JANG’OMBE | 12 | 5 | 6 | 1 | 15 | 9 | 6 | 21 |
3 | MAFUNZO | 12 | 6 | 2 | 4 | 18 | 11 | 7 | 20 |
4 | ZIMAMOTO | 12 | 5 | 5 | 2 | 15 | 11 | 4 | 20 |
5 | POLISI | 12 | 5 | 5 | 2 | 10 | 7 | 3 | 20 |
6 | TAIFA J/MBE | 12 | 5 | 3 | 4 | 10 | 10 | - | 18 |
7 | KMKM | 12 | 5 | 2 | 5 | 14 | 8 | 6 | 17 |
8 | CHWAKA | 12 | 4 | 5 | 3 | 8 | 8 | - | 17 |
9 | MUNDU | 12 | 5 | 2 | 5 | 12 | 17 | -5 | 17 |
10 | B/ SAILOR | 12 | 3 | 7 | 2 | 10 | 8 | 2 | 16 |
11 | MIEMBENI | 12 | 4 | 3 | 5 | 11 | 13 | -2 | 15 |
12 | KILIMANI CITY | 12 | 4 | 3 | 5 | 10 | 17 | -7 | 15 |
13 | KIPANGA | 12 | 4 | 2 | 6 | 12 | 13 | -1 | 14 |
14 | KIJICHI | 12 | 3 | 4 | 5 | 14 | 15 | -1 | 13 |
15 | CHUONI | 12 | 2 | 6 | 4 | 7 | 10 | -3 | 12 |
16 | MALINDI | 12 | 3 | 2 | 7 | 6 | 10 | -4 | 11 |
17 | KVZ | 12 | 2 | 4 | 6 | 6 | 12 | -6 | 10 |
18 | KIMBUNGA | 12 | 1 | 2 | 9 | 7 | 21 | -14 | 5 |
Jumla ya mabao 205 yamefungwa kupitia michezo 108 |
↧
Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Chwaka Stars na JKU Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU Imeshinda 2--1.
Kizaazaa katika goli la timu ya Chwaka stars wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan unguja timu ya JKU imeshinda kwa bao 2--1
Vitendo vya imani ya ushirikina katika michezo vimeshamiri kama inavyoonekana hapa likiwa limevunjwa yai jirani na kibendera cha kona.
Mshambuliaji wa timu ya JKU akimpita beki wa timu ya Chwaka Stars wakati wa mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan Timu ya JKU imeshinda 2--1.
Viongozi wa Timu ya Kijichi wakifuatilia mchezo kati ya Chwaka Stars na JKU uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa bao 2--1.
Wachezaji wa Timu ya JKU wakishangilia bao lao la Pili na la ushindi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
↧
↧
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Alnajim Atembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili msaada wa moja ya mashine tatu za kupimia Presha alipotembelea Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili wakiwapa zawadi akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi ya Hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimbeba mtoto mchanga alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Dkt. Ali Salum Ali akimuongoza Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim alipotembelea majengo mapya ya Hospitali hiyo yaliyofunguliwa hivi karibuni.
↧
Madaktari Nchini Wametakiwa Kuitisha Mikutano ya Kijamii Ili Kujadili Magonjwa
Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa Elihuruma Nangawe.
Dk. Manase Frank akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Profesa Andrew Swai akitoa mada.
Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia kwa karibu mada zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Dk. Andronicus Aloyce Rwelamila kutoka Hospitali ya Tumbi Kibaha (kushoto) na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Mary Gowele wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Usikivu katika kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA, Dk. Elihuruma Nangawe
Profesa Japhet Kileo (kulia), akiuliza maswali kwenye
kongamano hilo.
Dk. Mwanahamisi Magwangwara (kushoto), akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya afya katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mtoa mada, Profesa Andrew Swai.
Dk.Chilolo Edward (katikati), akijibu maswali kuhusu changamoto ya waendesha bodaboda. Kushoto ni Profesa Andrew Swai na Dk. Manase Frank.
Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matumizi ya pombe katika Manispaa ya Kinondoni.
Na Dotto Mwaibale
MADAKTARI nchini wametakiwa kufanya mikutano ya kijamii au wananchi ili kuwapa fursa ya kujua magonjwa yanayo wakabili.
Hayo yalielezwa na Dk. Manase Frank wakati akitoa mada katika kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi wengi kutojua magonjwa yanayowasumbua hivyo ni muhimu kwa madakatari kuitisha mikutano itakayowakutanisha na wananchi ili kuondoa changamoto hiyo" alisema Dk. Frank.
Alisema wagonjwa wengi wamekuwa wakikata tamaa kwa kuchangiwa na kauli za baadhi ya madaktari ambao wanashindwa kujua tatizo la mgonjwa husika hivyo wakati umefika wa madaktari kushirikiana kwa karibu na jamii, viongozi wa dini ili kuondoa changamoto hiyo.
Akitolea mfano wa kijana mmoja ambaye alifiwa na ndugu zake wote wa karibu kutokana na ugonjwa wa ukimwi na kuishi kwa kunyanyapaliwa lakini baadaye afya yake ilikuja kuimarika kufuatia ushauri uliotolewa na daktari kwa jamii iliyokuwa ikimzunguka wakati wa ugonjwa wake.
Mtoa mada mwingine Profesa Andrew Swai aliomba serikali wakati wa siku ya Jumamosi na Jumapili kufunga baadhi ya barabara ili zitumike kwa wananchi kufanya mazoezi ya kutembea ili kujenga afya za miili yako na kuepukana na magonjwa kama kisukari.
Akizungumzia changamoto ya matumizi ya bodaboda Dk.Chilolo Edward alisema kwa mwaka jana katika Hospitali za mikoa ya Morogoro, Tumbi Pwani na Shinyanga kulikuwa na ajali 895 huku majeruhi wakiwa 4813.
Alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali hizo walikuwa ni 4525, waliopewa rufaa kwenda hospitali za Bugando na Muhimbili walikuwa 71 na waliolazwa ni 702.
Alisema vifo vilikuwa 81 hivyo vilitokea baada ya kufikishwa Hospitalini ni 70 na vilivyotokea eneo la ajali vilikuwa 11.
Dk.Chilolo alisema ili kupunguza changamoto hiyo inapaswa watoa huduma za afya kutoa elimu kwa waendesha boda boda pale wanapofikishwa mahospitali kuhusu umuhimu wao katika familia na taifa kwa ujumla hivyo kuwa makini wanapoendesha vyombo hivyo vya moto badala ya kuacha kazi hiyo kufanywa na polisi au Sumatra.
↧
Dk Shein Azungumza na Mwakilishi wa UNICEF Ikulu Zanzibar.
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 29.11.2016

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Watoto Duniani (UNICEF) limepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika suala zima la kuwahudumia watoto na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ili Zanzibar ifikie malengo iliyoyakusudia.
Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Maniza Zaman aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Mwakilishi huyo wa UNICEF hapa nchini alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kupata mafanikio makubwa katika kuwahudumia watoto sambamba na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi ikiwemo kupata elimu na afya bora.
Alieleza kuwa Shirika hilo linathamini juhudi hizo na limeweza kushuhudia mafanikio na mabadiliko makubwa katika sekta za maendeleo hatua ambazo zimewawezesha watoto wa Zanzibar na wao kuweza kupata haki zao za msingi pamoja na mahitaji yao muhimu ya kimaisha.
Bi Zaman alizipongeza hatua za Serikali ya Mapinduzi za kujenga majengo mapya yatakayowahudumia wanawake na watoto katika hospitali ya Manzi Mmoja na ujenzi wa hospitali mpya ya Abdalla Mazee ni miongoni mwa mafanikio katika sekta ya afya ambayo watoto nao watafaidika.
Vilevile, Mwakilishi huyo alimpongeza Dk. Shein kwa juhudi zake kubwa anazozichukua katika kupiga vita vitendo Ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto kupitia Kampeni aliyoianza mnamo mwaka 2014, kwa ajili ya kukomesha vitendo hivyo.
Alieleza kuwa hatua za Serikali katika kuhakikisha vifo vya akinamama na watoto vinapungua hapa Zanzibar sambamba na kukabiliana na tatizo la mtapiamlo kwa watoto navyo vimepata mafanikio ambapo UNICEF pia, imeahidi kuendelea kuziunga mkono juhudi hizo.
Mwakilishi huyo alieleza kuwa UNICEF tayari imeshaanzisha programu mbali mbali mpya pamoja na kuziendeleza zile za zamani katika suala zima la kuwahudumia watoto na kueleza azma yake ya kwenda ngazi za chini zaidi katika jamii kwa kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili watoto.
Nae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa upande wake amelipongeza Shirika la UNICEF kwa juhudi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kuahidi kuimarisha uhusiano na mashirikiano yaliopo.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Shirika la UNICEF lina historia kubwa na mashirikiano kati yake na Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta za maendeleo zikiwemo sekta ya afya, elimu sambamba na kuimarisha ustawi wa akinamama na watoto.
Dk. Shein alisema kuwa Shirika hilo limeweza kutoa misaada yake mbalimbali na kuweza kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya afya kwa kushirikiana na Shrika la Afya Duniani (WHO).
Aidha, Dk. Shein amesema kuwa licha ya changamoto kadhaa zinazowakabili watoto katika Bara la Afrika lakini bado Shirika hilo limeendelea kutoa ushirikiano wake na misaada mbali mbali kwa watoto walio ndani ya nchi za bara hilo.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza juhudi zilizochukuliwa katika kupambana na vifo vya akinamama na watoto, ambapo Zanzibar imepiga hatua kubwa hasa pale ilipoanzisha mapambano dhidi ya Malaria jambo ambalo limefanikiwa.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo, kutoa pongezi kwa Shirika hilo kwa kuungana na Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye Ofisi zake hapa Zanzibar kuunda ‘One UN’ iliozipelekea ofisi hizo kukaa katika jengo moja na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuzisimamia vyema, Sera, Kanuni na Sheria zinazowahusu watoto katika kupata haki zao za msingi na huduma za kijamii.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
↧
Tz Bongo Magazetini leo.
↧
↧
Katuni na Ujumbe Wake Huuuooo......
↧
Rais Dk Shein alipokutana na Mwakilishi wa UNICEF nchini
↧
Wananchi watakiwa kuupokea utafiti mpya wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kisiwani Pemba
Na Salmin Juma, Pemba
Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kuwa tayari kuupokea utafiti mpya juu ya viashiria na matokeo ya ukimwi Tanzania wa mwaka 2016/17 utakaonza hivi karibuni kisiwani Pemba.
Nasaha hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Bi Mwanajuma Majid Abdalla huko katika ukumbi wa mikutano Gombani katika hafla ya mkutano wa wadau wa utafiti huo kisiwani Pemba.
Kupitia mkutano huo uliyojumuisha wadau mbali mbali wakiwamo waandishi wa habari walitakiwa kwa umoja wao wafikishe taarifa na elimu kwa jamii juu ya kuupokea utafiti huo ili jamii iweze kutoa taarifa sahihi kwenye utafiti huo muda utakapowadia na hiyo itakuwa kwa kaya ambazo zitachaguliwa kushiriki katika utafiti huo.
Mapema mwakilishi na mjumbe kutoka shirika la kimataifa lisilo la kiserekali ambalo ni mdau na mfadhili wa mradi huo ICAP bi Mihayo Lupamba amesema ni vyema wananchi wakauona umuhimu wa utafiti huo na kuupokea kwa mikono miwili kwani ni njia moja wapo ya kulisaidia taifa kuweza kupanga mipango yake ya maendeleo na hasa katika suala zima la afya na mapambano ya maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI humu nchini.
Amesema mradi huo utakuwa na utafiti mpana zaidi kwani hautaangalia tu maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI bali utakwenda mbali zaidi kuona pia viashiria vya maradhi mengine mbali mbali katika jamii kama vile kaswende na homa ya ini ili kujuwa ukubwa wa matatizo hayo na hio itakuwa kwa kila rika ikijumuisha watoto wa kuanzia miaka 10 kujia juu.
Aidha amesema utafiti huo utakuwa katika ngazi za mikoa na wilaya na kuzitaja shehia nane zitakazoshiriki katika utafiti huo kwa upande wa Pemba kuwa ni Mtambwe kaskazini na Maziwani kwa wilaya ya Wete na kwa upande wa wilaya Micheweni amezitaja shehia za wingwi mapofu na maziwa ng'ombe aidha wilaya ya chake amesema shehia ya kilindi pekee ndio itakayowakilisha katika mpango huo na kwa mkoani shehia ya KP, Stahabu, Ng'ombeni zitawakilisha eneo hilo
↧