Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35889 articles
Browse latest View live

Article 11

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                                                         30.11.2016
---
RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Kenya na kuahidi kurejeshwa utamaduni wa safari za meli kati ya Zanzibar na Mombasa kwa kutumia meli yake mpya ya MV Mapinduzi II.

Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa  Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Chirau Ali Mwakwere.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Mwakwere kuwa mbali ya ujirani wa mipaka kati ya Zanzibar na Kenya pande mbili hizo pia, zina udugu wa asili  ambao ulikuza uhusiano wa kiuchumi na kiutamaduni, hivyo ipo haja ya kuuendeleza.

Aidha, Dk. Shein amelipokea mikono miwili ombi la Balozi huyo la kuimarisha ushirikiano katika usafiri wa baharini kwa kuanzisha safari za meli kati ya Zanzibar na Mombasa, jambo ambalo Rais alisema kuwa limo katika mipango ya kutekelezwa.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kurejesha safari za meli zilizokuwepo hapo siku za nyuma baina ya Mombasa na visiwa vya Zanzibar na si muda mrefu safari hizo zitaanza huku akieleza kuwa safari za Tanga, Mtwara, Dar-es-Salaam na hata Comoro nazo zitajumuishwa.

Mbali na hilo, Dk. Shein aliunga mkono wazo la Balozi Mwakwere la kubadilishana uzoefu wa kitaalamu kati ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar na vyuo vikuu vya nchini Kenya na kueleza kuwa hatua hiyo itazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya pande mbili hizo sambamba na kuinua sekta ya elimu.

Dk. Shein alimueleza Balozi Mwakwere kuwa kumekuwa na uhusiano wa kidugu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Kenya hatua ambaye imeipelekea kuwepo kwa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko mjini Mombasa.

Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa nchi mbili hizo zimekuwa na historia ya kusaidiana pale nchi moja wapo inapopata matatizo, hivyo ana imani kubwa utamaduni huo utaendelezwa kwa manufaa ya pamoja.

Nae Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chirau Ali Mwakwere alimueleza Dk. Shein kuwa Kenya inajivunia uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Zanzibar na kuahidi kuukuza na kuuendeleza.

Katika kuendeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano huo, Balozi Mwakwere alitoa ombi maalum kwa Dk. Shein kurejeshwa utamaduni uliokuwepo hapo siku za nyuma za kuwemo usafiri wa baharini kati ya Zanzibar na Mombasa.

Aidha, Balozi Mwakwere alimueleza Dk. Shein haja ya kuwepo kwa uhusiano na ushirikiano wa kubadilishana uzoefu na utaalamu  wa wanafunzi kati ya vyuo vikuu vya Zanzibar na vile vya kenya ili vijana waweze kuutambua na kuukuza uhusiano uliopo.

Balozi Mwakwere alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kuendelea kuiongoza Zanzibar kwa amani, utulivu na maendeleo na kuahidi kuwa Kenya chini ya uongozi wa Rais Uhuru Kenyata  itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake hizo.

Alisema kuwa kwa vile Kenya hasa maeneo yake ya ukanda wa pwani tamaduni, silka na desturi zake zimeshabihiana na Zanzibar ni vyema uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo ukaimarishwa zaidi hasa katika sekta ya biashara na utalii.

Aidha, alisema kuwa Serikali ya Kenya imechukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha maeneo ya ukanda wote wa Pwani ya nchi hiyo unaendelea kutunza utamaduni, silka na desturi zao za asili.

Sambamba na hayo, Balozi Mwakwere alipongeza hatua za kuendelea kuyalinda na kuyatunza Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambayo yaliondosha unyonge na kuleta utu na demokrasia na kuifanya Zanzibar iweze kujisimamia mambo yake wenyewe.

Balozi Mwakwere alitoa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu wake kwa kuendelea kuilinda na kuitunza lugha ya Kiswahili ambayo imekuwa lugha maarufu ndani na nje ya Bara la Afrika na kusema kuwa wananchi wa Kenya wamekuwa wakikizungumza na kukipenda Kiswahili cha Zanzibar ambacho ndicho cha asili.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA KENYA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Chirau Ali Makwere alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Chirau Ali Makwere alipofika Ikulu Mjini Unguja leo
[Picha na Ikulu.]30/11/2016.

WELCOME TO TANZANIAN NEW YEAR 2017 EVE PARTY IN CALGARY - ALBERTA - CANADA

ESRF Yafanikisha Mkutano wa 5 wa Mwaka Wajadili Uchumi.

$
0
0
Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Philemon Luhanjo katika mkutano wa siku moja wa kujadili sera za kijamii zinavyoweza kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania, mkutano ambao uliandaliwa na ESRF.

Luhanjo alisema ni vyema Serikali inapokuwa inatunga sera ihakikishe zinakuwa na faida kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kupata maendeleo na kuboresha maisha yao na hata wakati nchi ikielekea katika uchumi wa kati kila mwananchi ahusike na mabadiliko hayo.

"Sera zipo nyingi, zipo za maendeleo ya jumla, elimu, afya, kilimo, viwanda na kila kitu, sisi tunajaribu kuangalia tunapotengeneza sera mbalimbali tuhakikishe kwamba sera hizo zitamnufaisha binadamu, kwamba chochote unachofanya kiwe nikwa faida ya mwanadamu, mipango na malengo yote yawe yanamlenga binadamu kuondoa matatizo yake,


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)

"Serikali inapofanya mipango inatakiwa kupanga mipango ambayo inajaribu kujibu kero za mwananchi, kama ni elimu, kama ni afyaa au kama ni kilimo cha kisasa, tunapotengeneza sera tuwe tunauwianisha, hizo sera zikitekelezeka na mteja wa bidhaa awe ameandaliwa ili mkulima asiwe amepoteza nguvu bure," alisema Luhanjo na kuongeza.

"Tunazungumzia nchi ya viwanda, viwanda gani? na nchi yetu niya kilimo kwahiyo tunatarajia viwanda vingi vitakuwa ni vya kilimo, kwahiyo tunataraji mkulima mdogo aimalishwe ili aweze kuzalisha mazao yanayokwenda kiwandani ni lazima sera ziwe na uwiano mzuri."

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali inafahamu kuwa nchi haiwezi kupiga hatua bila kuhusisha mwananchi mmoja mmoja na inachofanya kwa sasa na kuwashawishi watu wenye viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili wakulima nchini wafaidike na uwepo wa viwanda nchini.

"Tunaamini hatuwezi kuwa na uchumi unaokua kama hali ya kijamii ya wananchi haikui na hata Rais Magufuli alikuwa akisema tangu akiwa katika kampeni kwamba Tanzania ya Magufuli niya viwanda, na viwanda hivi ni kwa ajili ya watu wetu,

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.

"Kwenye mpango wetu wa miaka mitano tumesisitiza maendeleo ya viwanda lakini vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini katika kilimo chetu, kwahiyo hatuwezi kuwa na viwanda kama kilimo hakijaendelea, hatuwezi kuwa maendelo ya kijamii kama kilimo chetu hakijaendelea, kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, kwahiyo tumejadili hilo ili kuona wananchi wetu wananufaika vipi," alisema Kijaji. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alizungumza kuhusu mkutano huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kusema,"ESRF kwasasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017, "Katika hiyo ripoti tumeweza kutaharisha ripoti 11 ambazo zitachangia katika utayarishishaji wa hiyo ripoti na dhumuni kubwa ni kuweza kuzijadili hizo ripoti na kupata uelewa mpana ni kwa kiasi gani sera za kijamii zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa Tanzania."
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF, na mashauri wa ufundi wa mradi wa THDR Profesa Marc Wuyts, akiwasilisha mada Situating social policy transformation: A conceptual framework, kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mhadhiri wa Masuala ya Afrika na Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Shule ya Sayansi ya Siasa nchini Uingereza Dk.Hazel Gray, akiwasilisha mada yake kuhusu mabadiliko katika sera za kijamii kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF.
Mchokoza mada kutoka taasisi ya Daima na Mtafiti mwandamizi mshiriki ESRF, Profesa Samwel Wangwe, akitoa maelezo yake kuhusu mada iliyowasilishwa mezani kwa wajumbe.
Profesa wa uchumi DoE, Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Mushi, akiwasilisha mada kuhusu historia ya sera ya jamii katika mkutano huo.
Mgeni rasmi Dk. Kijaji, (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida, (wa kwanza kushoto), Bi Anna, na mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya ESRF, Bw Philemon Luhanjo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha (wa pili kulia) wakipongeza wakati wa mkutano huo.
Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali kwa makini katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania
Picha ya pamoja ya washiriki, wakuu ESRF, wakiwa na mgeni wa heshima Dk. Kijaji.

UN na EU Yawanoa Mabalozi 50 wa Malengo ya Dunia Iringa.

$
0
0
UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions). Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania. 

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akimkabidhi cheti Rais wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa Athman Waziri aliyehitimu kuwa balozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champion).
Picha juu na chini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na zoezi la kutunuku vyeti kwa mabalozi wa malengo ya dunia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champions) baada ya kuhitimisha semina maalum iliyoshirikisha vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Muazarau Matola
Baadhi ya Global Goals Champions katika picha ya kumbukumbu na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na wahitimu wa semina malengo ya dunia (Global Goals Champions) mara baada ya kuhitimisha semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa ambapo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Leo Bongo Magazetini

Ujumbe wa leo Katuni Huuuooo....

Madiwani Meru Wamkataa Mkurugenzi

$
0
0
 makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani Meru akiwa anachangia hoja katika baraza hilo
 baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia kikao
 mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza kumalizika
 mkurugenzi   wa halmashauri ya Meru  Christopher Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa meru
 baadhi ya madiwani wakifuatailia

 Habari picha na  Woinde Shizza,Arusha

BARAZA la madiwani  Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi wasema hana uwezo wa kuongoza  Halmashauri hiyo.


Akitoa  maazimio  ya kikao  cha baraza kilichokaa siku mbili kilichowajumuisha  madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.


" Tumejadili ajenda ya utendaji  usioridhisha wa Mkurugenzi wetu na tumeona  kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema Njau.


Aidha Njau alisema Mkurugenzi huyo ameonekana kukata mawasiliano na mwenyekiti wa Halmashauri jambo alilosema siyo sahihi.


Alisema pia ameweza kukata mawasiliano na madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na kusababisha hata wakuu wa idara kutokuwa na mawasiliano na madiwani jambo linalorudisha maendeleo nyuma.


Aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa  tangu  Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu  ya uzembe.


" Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na kuongeza.


"Tumeamua kuiomba mamlaka yake  na Uteuzi ichukue  hatua stahiki za kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya meru"


Vilevile alisema  kuwa  Mkurugenzi huyo amekuwa  akidharau maagizo yanayotolewa na  kamati mbalimbali za baraza hilo na Kushindwa kuzitekeleza ambapo ni kuvunja kanuni na taratibu za Halmashauri.


Hata hivyo alisema kitendo cha mkurugenzi kukata posho zamadiwani ni kinyume na utaratibu kwani ziliwekwa kisheria ambapo alisema  Kama kuna tatizo la kukatwa  posho ni lazima sheria hiyo ingebadilishwa kwanza.


" Mwenye dhamana ya kutangaza kuwa posho zinabadilika ni Waziri mwenye dhamana hiyo  lakini siyo mkuu wa mkoa, Wilaya au Mkurugenzi" alisema .

Naye Diwani wa Kikatiti  Elisa Mungure ambaye ni Mwenyekiti wa madiwani alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiendesha Halmashauri kisiasa jambo ambalo halifai.


" Ninasikitishwa na uongo unaoelezwa na Mkurugenzi ambaye kateuliwa na mheshimiwa Rais hii ni ajabu haiwezekani kuendelea kumuamini mtu wa aina hii" alisema Mungure.


Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa  akiwqhamisha watendaji wa kata  bila  kufuata taratibu huku akishinikiza ofisi ya kata ya Kikatiti kuwa ni ya CCM  huku ikiwa ni ofisi ya wananchi wala siyo ya chama chochote.


Kwa upande wake mkurugenzi  Huyo Christopher Kazer  alisema anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri  wanavyofikiri.


" Maelekezo ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi" alisema.


Alisema hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.

Aidha pia alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa ujumla 

Alisema kuwa anaamini haya yote yanatokea kutokana na madiwani hawa kukatwa fedha za posho na usafiri ambao walikuwa wamejiwekea bila kufuata taratibu

"ivi jamani ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha wanataka walipwe  fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa Rais ya kubana matumizi sitakubali  wafanye vitu ovyo na ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema mkurugenzi  Kazer



Mtoto Anapaswa Kuandaliwa Katika Mazingira Maalum Yatakayomuwezesha Kutoa Ushahidi.

$
0
0
Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar  Jaji George Kazi Kulia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi namna Mahakama ya Watoto itakavyofanya kazi alipofika Mahonda kukagua ujenzi wa Mahakama ya Watoto.
Nyuma ya Balozi Seif Ali Iddi ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Issa Juma.
Mhandisi Mkuu wa Jeshi la Polisi Mrakibu wa Polisi Paschal Macorwa akimpatia maelezo Balozi Seif  hatua iliyofikia ya Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif kulia akiwa pamoja na Mhandisi Mkuu wa Jeshi la Polisi Mrakibu wa Polisi Paschal Macorwa wakifurahia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Mahakama ya Watoto Mahonda alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wake.
Mkuu wa Kituo cha Afya Mahonda Dr. Ramadhan Makame Khamis kushoto  akimueleza Balozi Seif  hatua iliyofikiwa ya matayarisho kwa ajili ya Kambi ya Uchunguzi wa Afya kwa Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini “B” inayotarajiwa kufanyika Kituoni hapo Tarehe 3 na 4 Mwezi ujao.
Balozi Seif  kati kati akishauri baadhi ya hatua zinazopaswa kukamilishwa kabla ya kuanza kwa Kambi ya uchunguzi wa Afya hapo Kituo cha Afya Mahonda mnamo Tarehe 3 na 4 Mwezi ujao.(Picha na – OMPR - ZNZ.)

Na Othman Khamis OMPR.
Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Jaji George Kazi alisema Mtoto anapaswa kuandaliwa mazingira maalum yatakayomuwezesha kutoa ushahidi ulio huru endapo atafanyiwa vitendo vya udhalilishaji au kujitetea kama amefanya makosa ya jinai akiwa chini ya Umri wa miaka 18.

Alisema Serikali imeanzisha Sheria ya Mtoto nambari 6  ya Mwaka 2011 kwa madhumuni ya kuipa mamlaka Mahakama kusikiliza na kuamua makosa ya Jinai dhidi ya Mtoto kwa kosa lolote linaloshukiwa kutendwa kabla ya Mtoto hajafikia umri huo isipokuwa makosa ya Uhaini, Kuua na Kubaka.

Jaji George Kazi alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto liliopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema mfumo sasa ndani ya Mahakama nyingi Nchini umekuwa na mchanganyiko wa Kesi kiasi kwamba inaleta usumbufu kwa zile kesi zinazowahusu Watoto jambo ambalo huwapa kigugumizi watoto wanaohusika na kesi hizo wakatiwa kutoa ushahidi au kujitetea.

Jaji George Kazi alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mfumo mpya wa uanzishwaji wa Mahakama za Watoto utawapa nafasi Majaji au Mahakimu waosikiliza Kesi zinazowahusu Watoto kuzihamisha kutoka Mahakama za kawaida na kuzipeleka Mahakama maalumu za Watoto.

Naye Mhandisi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anayesimamia ujenzi huo Mrakibu wa Polisi { S.P } Paschal  Macorwa akimkaguza Balozi Seif  kuangalia maeneo mbali mbali ya Jengo hilo alisema kazi halisi za ujenzi huo zinatarajiwa kukamilika kati kati ya Mwezi ujao wa Disemba.

Kamanda Paschal alisema ujenzi wa Kituo hicho unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kama Taasisi kwa kutumia vifungu vyake vya kawaida vya matumizi umechelewa kukamilika kutokana na  kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi.

Hata hivyo kamanda Paschal alieleza kuwa juhudi zinafanywa na jeshi hilo kuhakikisha kwamba ujenzi huo unakamilika ifikapo Tarehe 15 Disemba  kwa kumalizia kazi za uwekaji wa huduma za Umeme pamoja na Maji ili Mahakama hiyo ianze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alilipongeza Jeshi la Polisi Nchini kwa kazi kubwa inalochukuwa licha ya ulinzi wa Raia lakini pia kujihusisha na Miradi inayotoa huduma kwa Jamii akiutolea mfano Ujenzi huo wa Mahakama ya Watoto Mahonda.

Balozi Seif alisema udhalilishaji wa Watoto kwa sasa umekuwa tishio kwa Jamii kiasi kwamba Serikali kupitia Taasisi mbali mbali imefikia hatua ya kuanzisha Mahakama ya Watoto kwa lengo la kukabiliana na vitendo hivyo vinavyovuruga ustawi wa Jamii Nchini.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikitembelea Kituo cha Afya cha Mahonda kinachojitayarisha kupokea Wataalamu wa Afya kutoka India watakaopiga kambi kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi  Wananchi kwa maradhi ya Meno, Kisukari pamoja na sindikizo la damu { Blood Pressure }.

Kambi hiyo awali ilikuwa imepangwa kufanyika katika Kituo cha Afya Kitope lakini kutokana na sababu za kimsingi zilizotolewa na Wataalamu wa Sekta ya Afya wamependekeza uchunguzi huo ni vyema ukafanyika katika Kituo cha Afya cha Mahonda  kutokana na kubahatika kuwa na vifaa vingi vya uchunguzi vitakavyorahisisha kazi zao.

Balozi Seif katika mazungumzo yake ya awali na  Wagonjwa na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Kitope juzi aliwahamasisha Wananchi wote wa Wilaya ya Kaskazini “B” kushiriki katika kufanya uchunguzi wa Afya zao utakaotolewa na Madaktari hao Mabingwa kutoka Nchini India.

Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Yaangamiza Zaidi ya Tani 62 za Bidhaa Zilizoharibika kwa Matumizi ya Binaadamu.

$
0
0
Wafanyakazi wa gari ya mizigo wakishusha bidhaa zilizoharibika katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja tayari kwa kuangamizwa katika zoezi ililosimamiwa na Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar.
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika maandalizi ya kuharibu chakula na dawa zilizoharibika na kupitwa na wakati katika dampo la Kibele.
Magari ya mizigo yakishusha shehena za bidhaa mbovu zilizokamatwa na maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi katika maghala na maduka Zanzibar.
Mkuu wa operesheni wa uangamizaji wa bidhaa mbovu wa ZFDB ndugu Abdulaziz Shaib Mohd akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuangamiza bidhaa hizo katika dampo la Kibele
Kijiko cha Manisapaa ya Zanzibar kikiharibu bidhaa mbovu na zilizomaliza muda wake wa matumizi katika dampo la Kibele Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.  30.11.2016
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib  Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa  bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.
Amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.
Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.
Mkuu wa Idara ya Chakula wa ZFDB bibi Aisha Suleiman amesema  mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika  bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.
Hata hivyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi  ili hatua  za haraka ziweze kuchukuliwa.
Wakati huo huo Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi wa ZFDB Ndugu Mwadini Ahmada Mwadini amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vinakemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu.
Amewashauri wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara ya dawa na vipodozi kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa  mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tania tatu.

UNESCO-Tanzania Yawajengea Uwezo Maafisa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika Kutekeleza Mpango Mkakati wa Wizara Mwaka 2016/2017

$
0
0
 Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigueas, (kulia), akiendesah semina ya mafunzo ya siku tatu kujenga uwezo kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makao makuu ya UNESCO, Oysterbay jijini Dares Salaam, leo Novemba 30, 2016. Kushoto ni Mwanasheria wa Wizara, Bw.Evordy Kyando.

NA K-VISBLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , (UNESCO), limeendesha mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ili kuwajengea uwezo wa kutekeelza mpango mkakati wa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 30, 2016, na kuendeshwa na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, nchini, Bi. Zulmira Rodrigues yanafanyika kwenye ofisi za shirika hilo, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Tumekusanyika hapa kwa mara ya kwanza kuisaidia wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuboresha uwezo wawafanyakazi wake, wafanyakzi kutoka idara tofauti tunao hapa, wapo kutoka idara ya Habari, Utamaduni, michezo pamoja na idara za kiusaidizi kama vile fedha, sheria, ICT na kadhalika.” Alianza kwa kusema Mkuu huyo wa UNESCO.
Alisema, Mpango unaweza kusaidia kufanya tathmini na marekebisho kwa mahitaji ya wizara au taasisi yoyote ile na kwa kuzingatia hilo, Shirika hilo limeona upo umuhimowa kuwajengea uwezowatendaji katika wizara hiyo ili kutekeleza vema mpango mkakati wa wizara. “Kama huna mpango wowote ule uliouweka, utajikuta unatumia nguvu nyingi na kuishia patupu bila mafanikio yoyote yale.” Alisema.
Alisema, wafanyakazi katika taasisi yoyote ile ni wajibu kushirikiana ili kuwa na lengo moja kufikia malengo mahsusi yaliyopangwa na Wizara au taasisi. “Kabla ya kuweka mpango wowote ni lazima kufanyike utafiti wa hali halisi ya jambo linalotaka kushughulikiwa.” Alifafanua Bi. Zulmira.
Washiriki walianza kujifunza mambo mbalimbali ama vile, namna ya kutambua tatizo la msingi, uwezo, udhaifu, fursa na tishio mambo yote hayo yanayojulikana kitaalamu kama (SWOT Analysis), ndiyo yatakayotoa picha halisi ya namna ya kupanga mkakati na namna ya kuutekeleza mkakati huo.



Aidha washiriki wa warsha hiyo wamefurashiswa na mafunzo hayo kwani yatasaidia kuwajengea uwezo wa kutekeelza kikamilifu malengo ya kiofisi na binafsi.
“Mafunzo haya yatanisaidia sana katika kutekeleza malengo yaliyopangwa kwani nimejifunza njia mbalimbali za kimkakati katika kutekeleza malengo yaliyopo.” Amesema mshiriki Lorietha Lawrence, afisa habariwizara ya Habari, Utamaduni, Sanaana Michezo.
Kupitia mafunzo haya, ninahakika yatasaidia kutekelza majukumu yangu ya kila siku, na nitakachojifunza nitashirikiana na wenzangu kwenye kitengo chetu katika kutekelezaipasavyo majukumu yetu.” Alisema Afisa mwingine wa habari, Lilian.

 Baadhi ya washiriki
Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, Sefania Molela, akizungumza
 Mshiriki kutoka idara ya Habari akizungumza
 Bi. Zumlira Rodrigues, (kulia), akiteta jambo na Afisa Mpango wa Utamaduni wa UNESCO, Rahma Sudi
 Afisa Mpango wa UNESCO, Michaela Konopikova
 Mtaalamu wa masuala ya ICT wa UNESCO, Leonard Kisenha, (katikati), na Afisa Mpango, Utamaduni wa Shirika hilo, Michaela, (kushoto0, wakitazama kitu kwenye kompyuta
 Mkufunzi wa UNESCO, Deirdre Prins-Solan
 Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, akizungumza

 Mshiriki kutoka idara ya Michezo akizungumza
 Bi.Zulmira akiendesha mafunzo
 Maafisa mpango-Utamaduni wa UNESCO, Rehema (kulia) na Michaela wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo
 Bi.Zulmira akiendesha mafunzo
Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Evordy Kyando, akizungumza jambo

Mandhari ya Eneo la Biashara Maarufu kwa Jina la Pinda Mgongo Saateni.

$
0
0
Wafanyabiashara katika eneo la sebleni wakifanya biashara zao baada ya kuhamia eneo hilo lililotengwa kwa ajili yao baada ya kuhamishwa katika eneo la jua kali darajani na kuhamishiwa sehemu hiyo eneo la saateni ili kuendelea na biashara zao kama inavyoonekana pichani wakiwa katika eneo hilo.


Mwanafunzi wa Kidatu cha Tatu Anusurika Kufa Mara Baada ya Kubakwa na Kutelekezwa Korongoni.

$
0
0
Image result for KAMANDA WA POLISI ARUSHA MKUMBO
Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo
Meru mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kuteketezwa
kwenye  korongo la mchanga na kusababishiwa  maumivu makali
yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo  mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12.30
alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.
"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimejipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyoo  alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus  alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifkra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson  Elias ambae ndie  aliyehusika na ukatili huo  na kumfikisha katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa  polisi  Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo limesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016  na atafikishwa mahamani upelelezi ukikamilika.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Akabidhi Vifaa na Dawa Hospitali ya Makunduchi kwa Ajili ya Wodi ya Wazazi.

Rais wa Zanzibar,Dk Shein Amuapisha Kaimu Jaji Mkuu.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                          1.12.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Mkusa Issac Sepetu, kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hafla ya kumuapishwa  kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman.

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Wajerumani Watengeneza Filamu Ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Tanzania.

$
0
0
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (katikati) akizungumza na Mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon ya nchini Ujerumani,Mona Lessnick alipotembelea eneo la Kogatende jirani na  Mto Mara ambapo kulikuwa kukifanyika shughuli za uchukuaji wa picha za video kwa ajili ya Tamthiliya ya Dream Boat.kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mratibu wa uzalishaji wa Filamu wa kampui ya Polyphon Studio,Mona Lessnick (kulia) akiwa na Mpiga picha mkuu wa kampuni hiyo ,Manuel Schroeder na Jorg Gariel  wakati wakizungumza na wanahabari  (hawapo pichani) juu ya tukio la uchukuaji wa picha za video katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo picha za video za sehemu ya Tamthiliya ya Dream Boat zimepigwa hapo.
Moja ya gari lililotumika katika tukio hilo likitoka eneoo la tukio kando ya Mto Mara unopita katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Uchukuaji wa picha za video kando ya Mto Mara ukiendelea.
Magari yakiwa yamebeba sehemu ya vifaa kwa ajili ya uchukuaji wa picha za Video.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiteta jambo na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA,Ibrahim Musa( katikati) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Jorg Gabriel walipoktana eneo la Kogatende katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akisaidia kubeba moja ya Kamera kubwa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uchukuaji wa picha katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Moja ya Kamera kubwa iliyokuwa ikichukua matukio katika upigaji picha wa Tamthiliya ya Dream Boat katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii akiitizama Kamera ambayo ilikuwa iktumika kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo.
Wataamu wakifunga Kamera katika ndge ndogo ya Shirika la ndege la Costal Airline kwa ajili ya upigaji wa picha za juu . 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

SEKTA ya Utalii nchini inatarajia kupiga hatua baada ya wasanii maarufu wa filamu kutoka nchi za nje kuanza kutumia baadhi ya maeneo katika vivutio vya Utalii vilivyoko nchini kuandaa sehemu za tamthiliyaa zao.

Kampuni kubwa ya utengezaji wa filamu ya Polyphon Group  ya Humburg  nchini Ujerumani imekuwa ya kwanza kupiga picha za video za sehemu ya tamthiliya maarufu nchini Ujerumani ya Dream Boat ambayo imekuwa ikiooneshwa katika vituo mbali mbali vya televisheni kwa nchi zinazozugumza lugha ya Kijerumani.

Maeneo ambayo picha za video zimechukuliwa ni pamoja na Kogatende na Lobo ndani ya Hifadhi za Taifa za Serengeti ,huku picha nyingine zikipigwa katika Hifadhi ya taifa ya Arusha pamoja na Pori la akiba Endumeti.

“Tumefanya Sehemu moja ya Tamthiliya yetu Botswana,moja Zambia na nyingine Kenya katika muendelezo wa tamthiliya hii inayooneshwa kwa mika 30 sasa,Sehemu ya mwisho ya muendelezo wa filamu hii iliyochukuliwa Afrika ilikua mwa 2007,ni muda mrefu na tuliangalia wapi tunaweza enda,na tukafanya utafiti ,tukaja Tanzania,Tumeona hii nchi ni nzuri tukaamua kuleta filamu yetu hapa”.alisema Manuel Schroeder mpiga picha wa kampuni ya Polyphon Studio.

Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa amesema hatua hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii kimataifa huku mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon,Mona Lessnick akieleza utalii utaongezeka kupitia tamthiliya hiyo.

“Kutokana na uzoefu ,watu wametuamini sisi , tumefanya hii kazi kwa miaka 30 sasa,hivyo baada ya kurusha sehemu ya tamthiliya ilichukuliwa hapa itaongeza soko la wageni kutoka nchi zinazozungumza kijerumani,kwa sababu wanajua tunafanya utafiti,tmekwisha fka hapa mara mbili na kukutana na mtaalamu na kutuonesha maeneo ,wanajua tunachukua maeneo mazuri,hoteli nzuri,tuna taarifa  na vifaa vya kutosha,hivyo kutakuwa na matokeo makubwa katika Utalii “alisema Lessnick.

Kuhusu Maudhui ya Tamthiliya hiyo ambayo inaoneshwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa ,Mona Lessnick amesema imebeba maudhui ya aina tatu ambayo ni Vichekesho,Mahusiano pamoja na Drama.
“Ni Burudani kwa familia,tuna hadithi tatu,katika hadithi kuu watu wanasafiri kwa meli kuizunguka nchi,wakasafiri kuja Tanzania ,kuna hadithi nzuri za mahusiano ambazo vipande vyake vimechukuliwa Tanzania “alisema Lssnick.

“Katika muongozo tuna aina tatu ya hadithi,tuna hadithi ya mapenzi,tuna hadithi ya vichekesho na drama hii tunayofanya leo ni vichekesho,tuna watu wawili ,katika muongozo wa kwanza inaonesha watu haw wamepata tatizo katika gari lao hapa  Serengeti,lakini tulipaa ugumu kupiga picha ndio tukapata mahala hapa pazuri kwa kufanya video,tukafanya Drama hapa ya gari kukwama ndani ya maji na gari nyingine ikaja nyuma kuoka watu hawa wakiw wamekaa juu ya gari lao na kuondolewa katika maji”alisema Schroeder.

Tamthiliya ya Dream Boat imefikisha miaka 35 sasa tangu kuanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya Televisheni nchini Ujerumani na kwamba sehemu mbili zenye urefu wa dakika 90 kila moja za tamthiliya hiyo ,picha zake hupigwa katika nchi moja ya kiafrika .

Mwisho.


Rais wa Zanzibar Dk Shein, Amuapisha Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Mkusa Sepetu leo.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimuapisha Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu baada ya kumuapisha kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akipena mkono na Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu baada ya kumkabidhi hati ya kiapo  alipomuapisha kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
Viongozi waliohudhuria  katika hafla ya kuapishwa Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar (kutoka kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akimpongeza Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu kwa kuteuliwa kwake kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla ya kiapo iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali ,[Picha na Ikulu.] 01/12/2016. 

Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Azungumza na Uongozi wa Hospitali ya Chake.

$
0
0
Daktari Dhamana wa Hospitali ya Chake Chake, Ali Habibu Ali, akitowa maelezo ya kiutendaji katika Hospitali hiyo kwa mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, huko katika ukumbi wa Hospitali hiyo Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Hospitali ya Chake Chake ,kujitambulisha na kukumbushana baadhi ya majukumu ya kiutendaji.
Kamati ya Uongozi ya Hospitali ya Chake Chake Pemba, wakiwa katika kikao cha pamoja baina yao na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake.Bi.Salama Mbarouk Khatib, huko katika ukumbi wa Hospitali hiyo.(Picha na Bakari Mussa) 

Kuelekea Tanzania ya Viwanda

Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Chapata Viongozi Wapya.

$
0
0
 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake Dk.Elihuruma Mangawe (katikati), akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick Goodluck.
 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi uliompa nafasi hiyo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano huo.
Usikivu katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.

Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.

Katika nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey Swai aliibuka kidedea dhidi ya Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura tisa zilikataa ambapo katika nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa wawili Elizabeth Nchimbi aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.

Katika nafasi ya Mtunza Fedha licha ya kuwepo na ushindani makali aliyeibuka mshindi ni Mwanahamisi Hassan ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya mgombea mwenzake Violeth Shirima aliyepata kura 24.

Nafasi ya Katibu wa Mipango ilikwenda kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata kura 38 dhidi ya Othman Shem aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi na Dismas Vyagusa wakishinda nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.





Viewing all 35889 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>