Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35931 articles
Browse latest View live

RC Makalla Aishukuru UN Kwa Misaada na Ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akielezea mipango aliyonayo ya kuinua uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia) nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: 'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.

Vijana Wakubali Maendeleo Endelevu, Waahidi Kuyapeleka Vijijini.

$
0
0
Wakati wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi. Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu ya watu wake ni vijana hivyo wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi kushawishi wengine kuhuisha maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku huku wakitunza mazingira. Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa mengi wakati yale ya Milenia yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema kwamba suala si uwingi wa malengo bali maana yake na haja ya utekelezaji. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema MDGs (Malengo ya Millennia) iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake kunahakikisha uwapo wa maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea sana mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Alisema ni matumaini yake kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto hizo za sasa za dunia. Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na wanachuo hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya sasa na kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo na mabadiliko.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.

Kwa kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa asilimia 75 ya vijana wanaishi vijijini, itakuwa heri kama walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa kupeleka salamu vijijini ili kukabiliana na tatizo la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanafumua misimu ya kilimo na upatikanaji wa mvua. Kushirikisha vijana ni suala la msingi sana, hasa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini ambako malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema Kidai Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia (Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Amesema amefurahishwa mno na mpango huo wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa basi atahakikisha anawaelimisha wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo hayo. Akirejea mazungumzo ya mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake. Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko wa vijana wa kutaka kujua malengo hayo na ni imani yake kwamba kwa kuwakujua wao basi jamii itaerevuka mapema zaidi.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya wakati wa semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro akiuliza swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni hapo, Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani) wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).



Mmoja wa washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Pichani juu na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (hayupo pichani).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Manafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss Mbeya 2016, Eunice Robert.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa mabalozi hao.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya wakiwa wameshikilia baadhi ya SDGs.

Amchoma Kisu Kaka Ake Hatimae Kufariki Dunia Akikimbizwa Hospitalini.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Pemba. 
MTU mmoja Massoud Amour Seif (54) mkaazi wa Mtambile wilaya ya Mkoani Pemba, amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu nje ya kituo cha Polisi cha Mtambile na ndugu yake wa damu, Kassim Amour Seif (43), baada ya kutokezea ugomvi wa wake zao.

Taarifa zinaeleza kuwa, wawili hao kabla ya mkasa huo, walianza kwa wake zao kugombana na kisha ugomvi huo kuhamia baina yao, na kupelekea marehemu kabla ya kufariki kupata majeraha na kupewa fomu ya Pf3 kwa ajili ya matibabu.

Imefahamika kuwa, baada ya kupata matibabu na kisha kwenda kituo cha Polisi kwa ajili ya maelezo ya kina, marehemu akiwa sambamba na mdogo wake, kisha walitakiwa warejee siku ya pili yake, na kujitokeza mkasa huo.

Mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kuwa, hatua chache kutoka kilipo kituo hicho cha Polisi, ndipo Kassim alipomrukia kaka yake na kumchoma kisu na kupoteza damu nyingi.

“Wakati Polisi wanamshughulika marehemu kwa tukio hilo, mpigaji kisu alichukua gari na kukimbilia eneo la barabara ya Wambaa, na mjeruhiwa kufarikia njiani akipelekwa hospitali”,alisema shuhuda huyo.

Aidha shuhuda Khamis Haji Omar, alisema tokea asubuhi ya tukio hilo, ugomvi wa wawili hao ulishaanza kwa muda mrefu, ikidaiwa kusababisha na watoto wao kuiibiana simu.

Nae shuhuda Mohamed Ali, alieleza kuwa baada ya kutokezea hali hiyo, iliosababishwa na watoto wao, ndipo wake zao nao walipoanza kutofahamiana na kisha kurukia na wanaume hao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba, Sheihan Mohamed Sheihan alisema, kwa sasa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo Kassim Amour Seif, na akipatikana atafikishwa mahakamani.

Alisema, kwa vile mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo alikimbia akitumia gari yenye namba za usajili Z 242 HI na kuelekea Wambaa, Jeshi lake lilivamia huko na baada ya kuona gari ya Polisi, mtuhumiwa aliamua kulitelekeza gari lake.

“Mtuhumiwa gari lake aliliawacha na kukimbia msituni, lakini sisi Jeshi la Polisi gari tunalo ambalo alilitumia Kassim, na sasa tumeshaweka mitego kila kona na akipatikana atajibu hoja’’,alifafanua.

Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi mkoani humo, amesema kwa sasa wanamshikilia kijana Mohamed Ali, ambae alikamatwa na pikipiki ikiwa na damu, akidaiwa kumsafirisha mtuhumiwa.

“Huyu kijana tunae na tunamuhoji, na tunamashaka nae kuwa ndie aliemsafirisha Kassim, ili kujihifadhi na hasa baada ya kulitekeleza gari lake, ili kuwakimbia Polisi’’,alifafanua.

Tukio hilo lilitokea Disemba 1 majira ya saa 12 :30 nje ya kituo cha Polisi cha Mtambile wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba, na likiwa la kwanza katika miaka ya hivi karibuni kuwahi kutokea.

Mwandishi wa ZBC Mawio Zanzibar Hidaya Khamis Amefariki Dunia Asubuhi ya Leo Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

$
0
0
Mwandishi wa Habari wa ZBC Redio Kitengo cha Mawio Hidaya Khamis amefariki Dunia asubuhi ya kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kuugua hafla. Marehemu alikua mfanyakazi wa ZBC Redio akiripoti habari za Mawio Zanzibar. 
 Marehemu amezikwa leo kijijini kwao Unguja Ukuu mchana baada ya Sala ya Ijumaa.
Mwebnyenzi Mungu ampe malazi mema. 
Inalillah Waina Rajuhn.  

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Atia Saini Kitabu cha Maombolezi ya Rais wa Cuda Dar leo.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Bwana Fidel Castro kwenye ubalozi wa Cuba Mtaa wa Namanga Mjini Dar es salaam.
Kushoto yas Balozi Seif aliyesimama ni Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez.
Balozi Seif akitia saini kitabu hicho akishuhudiwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  Mh. Harus Said Suleiman pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga.
Balozi Seif Ali Iddi wa Pili kutoka Kushoto akimfariji Balozi wa Cuba Nchini Tanzania wa kwanza kutoka kushoto mara baada ya kutia saini Kitabu cha maombolezo ya Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Bwana Fidel Castro.
Kushoto ya Balozi Seif ni na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  Mh. Harus Said Suleiman , Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga pamoja na Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ  Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali.
Balozi wa Cuba Bwana Jorge Luis Lopez akiagwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  Mh. Harus Said Suleiman baada ya kumalizika kwa kazi ya utiaji saini.
Balozi wa Cuba Bwana Jorge Luis Lopez akiagwa na Naibu Waziri wa  baada ya kumalizika kwa kazi ya utiaji saini.Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga(Picha na Hassan Issa OMPR)

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametia saini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Marehemu Fidel Alejandro Castro Ruz  kilichotokea Tarehe 25 Novemba 2016 katika Mji wa Biran Nchini Cuba.

Utiaji saini huo wa Kitabu cha Maombolezo ameufanya katika Makaazi ya Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania uliopo Bara bara ya Ali Bin Said Mtaa wa Namanga Jijini Dar es salaam.

Balozi Seif  ameiwakilisha Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar katika utiaji saini huo akiambatana na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar  Mh. Harus Said Suleiman , Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga pamoja na Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ  Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali.

Marehemu Fidel Alejandro Castro Ruz  aliyefikia umri wa Miaka 90 alifanikiwa kuiongoza Jamuhuri ya Cuba akiwa na umri wa Miaka`32 kuanzia mwaka 1959 baada ya vugu vugu la kampeni ya kuuondosha Madarakani utawala wa Batista mwaka 1958 akisaidiwa na Kaka Yake Raul Castro pamoja na mwana harakati wa kupigania ukombozi wa wanyonge Kamanda Guavara.

Akimfariji Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Bwana  Jorge  Luis Loez baada ya saini hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Kifo cha Jemedari huyo wa Taifa la Cuba hakikuacha pengo kwa nchi hiyo lakini pia kimeigusa Tanzania kutokana na Mataifa hayo kufanana katika harakati zao za kupigania Uhuru kutoka makucha ya Kikoloni.

Balozi Seif alisema Jamuhuri ya Cuba ni kaka wa Tanzania katika njia ya kusaidia maendeleo na nyanja za uchumi zilizopata ufanisi mkubwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Wataalamu wa Nchi hiyo kuwawezesha Kitaaluma wananchi Wazalendo wa Tanzania.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Balozi huyo wa Cuba Nchini Tanzania amewataka Wananchi wa Taifa hilo lilioko katika Bahari ya Carribean kukubali kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi cha kuondokewa na Kipenzi Rais wao Mstaafu Kamanda Fidel Castro.

Akitoa shukrani zake  Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema Cuba itaendele kuwa mshirika mkubwa wa Tanzania katika azma yake ya kuona wananchi waliowengi wa ngazi ya chini wa Mataifa hayo wanafaidika na Uhuru walioupata kutoka katika makucha ya wakoloni.

Balozi Lopez alisema Cuba na Tanzania zimeshirikiana kwa muda mrefu uliobakia kuwa Historia kwa sasa hasa katika sekta za Afya, Kilimo, Viwanda na masomo ya Elimu ya Juu, ushirikiano uliowekwa msingi wake  na Waasisi wa Nchi hizo Mbili Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Bwana Fidel Castro. 

Marehemu Fidel Castro alizaliwa Mnamo Tarehe 13 Agosti mwaka 1926 ndani ya familia ya watoto Sita akiwa watatu  wa Mzee Angel aliyekuwa mfanyakazi wa mashamba ya miwa akiwa na asili ya Taifa la Hispania.

Marehemu Fidel Castro katika utoto wake alionyesha kipawa chake wakati alipoanza kupata elimu iliyomuwezesha kuonekana mwenye akili kubwa katika masomo yake Darasani tokea maandalizi,msingi, sekondari hadi chuo Kikuu.

Alipohitimu  masomo yake katika Chuo Kikuu cha  El  Colegio de Belen Mjini Havana Nchini Cuba Marehemu Fidel Castro aliamua kujiunga katika  harakati za Kisiasa zilizompelekea kukumbwa na misuko suko kadhaa  iliyomsababishia kuikimbia Cuba katika miaka ya 40.

Alirejea  Nchini Cuba Disemba 2 mwaka 1956  akiambatana na zaidi ya askari 80 wakiwa na silaha kwa ajili ya mapambano lakini nguvu za Kijeshi za Batista zilisababisha kushindwa kwa jeshi hilo na hatimae Castro, Raul, Guavara na baadhi ya askari wao waliamua kukimbilia katika milima ya Sierra Maestra.

Miaka miwili baadaye Marehemu Castrol alijiimarisha tena kijeshi kwa lengo la kupambana kwa mara nyengine na Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Batista ambapo mwanzoni mwa mwaka 1958 akaanza kampeni ya kujipenyeza tena Nchini Cuba.

Mbinu za kuimarisha majimbo sambamba  na kuyashawishi makampuni ya Kilimo na Viwanda kumkubali  zilimuwezesha Castrol na washirika wake kuongeza nguvu zilizoisambatarisha Serikali ya Batista iliyokosa nguvu za kiutawala na hatimae  Jeshi la Castrol likafanikiwa kuidhibiti Cuba Kijeshi.

Mwezi Januari mwaka 1959  Batista aliamua kukimbilia Jamuhuri ya Dominica baada ya Serikali yake kushindwa nguvu na Kikosi cha Castrol akisaidiwa na Kaka yake Raul na Mwanaharakati za kupigania uhuru wa wanyonge Kamanda Enersto Guavara.

Bwana Fidel Castro alilazimika kukasimu madaraka kwa  kumteuwa Kaka yake Raul Castro mnamo Tarehe 31 Julai 2006 kukaimu nafasi hiyo  baada ya  afya yake kutomruhusu kuendelea kushika wadhifa wa Urais wa Cuba.

Tarehe 24 Febuari mwaka 2008 Bwana Raul akashika rasmi nafasi hiyo ya Urais na kuendelea kuliongoza Taifa hilo hadi hivi sasa.

Wanasheria Pemba Wapata Elimu ya Sheria.

$
0
0
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Pemba, Fatma Khamis Hemed, akifunguwa mafunzo ya kupitia Sheria mbalimbali ikiwemo za Tawala za Mikoa Zanzibar  sheria namba 8 ya 2014 ,yaliofanyika Hoteli ya Misali-Pemba.
Wasaidizi wa sheria wa majimbo mbali mbali Kisiwani Pemba, wakiwa katika mafunzo ya kupitia sheria mbalimbali huko Misali, yaliodhaminiwa na Kituo cha huduma za Sheria Pemba.
Ofisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria , Khalfan Amour Moh'd,akitowa ufafanuzi wa sheria za Tawala za Mikoa namba 8/2014.

Wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Gando Bakar Khamis Faki na ShaabanJuma Kassim, wakichangia mada katika mafunzo ya kupitia sheria mbalimbali huko Misali Chake Chake Pemba.
Wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Gando Bakar Khamis Faki na ShaabanJuma Kassim, wakichangia mada katika mafunzo ya kupitia sheria mbalimbali huko Misali Chake Chake Pemba.(Picha na Bakari Mussa Pemba)

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Azindua Baraza la Vijana

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba,Mhe.Salama Mbarouk Khatib, Akizindua Baraza la Vijana Wilaya ya Chakechake Pemba,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Afisi ya Mkuu wa Wilaya Chake,kushoto Ofisa Mdhamini Wizara ya Uwezeshaji, Vijana Ustawi wa Jamii, Wazee Pemba,Bi Khadija Khamis Rajab (kulia ) na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Chake Chake Bakar Hamad Bakar.


Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa baraza la Vijana Wilaya , Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chake Chake baada ya kulizinduwa Baraza hilo huko katika kiwanja cha Tenis Chake Chake Pemba.(Picha na Bakar Mussa-Pemba.)

RC Aruhusu Mjane Kujenga Eneo Ambalo Polisi Wamemzuia Kujenga

$
0
0
Badhi ya watumishi wa halmashauri ya Mji Makambako wakimsikiliza mkuu wa mkoa alipo fika katika Halmashauri yao kujia shina ma matatizo yao (Picha Hapo Chini)

Mkuu wa mkoa wa njombe Dr Rehema Nchimbi Akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Makambako (Picha Hapo Juu)

SERIKALI mkoani Njombe imetoa ruhusa ya kujenga nyumba mama mjane ambaye amezuiriwa na Jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro baina yake na jeshi hilo kwa kuwa majirani wa mama huyo wameruhusiwa kujenga.

Kauli hiyo inatolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mkanganjiko wa kiwanja cha mjane huyo na kuwapo kwa mvutano mrefu baina ya yake na jeshi la polisi wakati akiwa na mkotano na watumishi wa halmashauri ya mji Makambako ambako yupo katika ziara ya kikazi mkoani humo.

Dr. Nchimbe anasema kuwa mama huyo ajenge kama majirani zake walivyo ruhusiwa kujenga maeneo hayo na wakati watakavyo bomoa kwa majirani wengine basi wabomoe kwa wao wote.

Alisema kuwa haiwezekani mama huyo akazuiliwa kujenga wakati wajirani zake wameruhusiwa kujenga na kuwa kwa kuwa watu hao walijenga kiholele basi hata mama huyo ajenge kiholela.

Hata hivyo mkuu wa mkoa aliingia katika majibizano ya maswali na majibu na afisa mipango walipo kuwa akimuhoji afisa mipango wa halmashauri hiyo Ephahim Mkambo.

Mkuu wa mkoa: kwanini mama huyo haruhusiwi kujenga.
Afisa mipango: mama huyo yupo katika eneo la polisi na haruhusiwi kujenga eneo hilo.
Mkuu wa mkoa: Kwanini majirani zake waliruhusiwa kujenga, eneo hilo.
Afisa mipango: Hawa wengine walijenga kiholela na wenye eneo walishindwa kudhibiti mikapa yao.
Mkuu wa Mkoa: sasa naamuru naye huyu mama ajenge eneo hilo kihilele na watakapo kuwa wakibomoa wabomolewe wote haiwezekani akazuiwa mmoja na wengine wakaruhusiwa.
Mkuu wa mkoa baada ya kutoa ruhusa ya ujenzi kwa mjane huyo alimuonya mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala kuto saini karatasi za watu wa ardhi kwa kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa usahihi na kufanya kwa ujanja ujanja.
“Nakuonya Mkurugenzi wewe usisaini karatasi za watu wa ardhi watakuingiza matatani hawa ni wajanja wajanja kuwa majini nao,” alisema Dr. Nchimbi.

Katika mkutano wake huo na maafisa na wakuu wa Idara walitoa maoni yao mbalimbali na changamoto zao ambazo zinawakabili kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi za wananchi.
Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Frederick Kazikuboma alisema kuwa halmashauri hiyo inaupungufu wa magari, na rasisimali watu ambapo kuna idara zinawafanyakazi wacheche.
Hata hivyo Dr. Kyunga Ernest, ni Afisa afya na ustawi wa jamii Halmashauri ya Makambako alisema kuwa pamoja na kuwa na kituo cha afya katika halmashauri hiyo changamoto kubw ani kuto kuwapo kwa chumba cha upasuaji licha ya kuanza ujenzi wake na baadhi ya vifaa kuwanavyo.

Alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo halmashuri imekuwa ikipokea fedha za kituo cha afya huku huduma zinazotolewa zikiwa ni za hospitali kutokana na watu wanaofika Hospitalini hapo.


Alisema kuwa baada ya kufunga mfumo wa kielekroniki wa kukusanya mapato wamekuwa wakikusanya zaidi ya milioni 14 lakini watu wanaopata huduma za bure hupokea watu wanao hudumiwa kwa gharama ya Milioni 13 au zaidi ya milioni 14 kitu ambacho hushindwa kujiendesha kwa fedha za ndani.
Regards BY: Elimtaa Media, Headquarter Njombe Tanzania web; www.eliabu.blogspot.com Email; furahanews1@gmail.com furahanews@gmail.com Facebook; https://www.facebook.com/elimtaamedia Twitter; https://twitter.com/elimtaa Linkedin; https://www.linkedin.com/home?trk=nav_responsive_tab_home Mbl; +255 753 321 191, +255 656 049 045 More News Update your Mind

Article 10

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Nne wa Baraza la Tisa la Wawakilishi lililokuwa likiendelea kwenye Ukumbi wa Majengo yake yaliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.(Picha na Hassan Issa OMPR) 

Na Othman Khamis OMPR. 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kulifanyia marekebisho makubwa ya Miundombinu eneo la Kijangwani ili liweze kutumika kama Kituo Kikuu cha magari ya Abiria katika azma yake ya kuendeleza uboreshaji wa haiba ya Mji wa Zanzibar Kibiashara.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Nne wa Baraza la Tisa la Wawakilishi lililokuwa likiendelea kwenye Ukumbi wa Majengo yake yaliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema Serikali haijawa na nia mbaya kama baadhi ya watu wanvyofikiria ya kuwahamisha Wafanyabiashara wanaouza mbao katika eneo hilo la Kijangwani na kuwatengea sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili yao katika Mtaa wa Daraja Bovu.
Balozi Seif aliwakumbusha  Wananchi kwamba  zoezi hilo la kudumu litaendelea kutekelezwa katika maeneo mengine ya  Mji na Vitongoji vyake  ambayo baadhi ya wafanyabiashara waliamua kuyavamia kwa kufanya biashara zao bila ya utaratibu na mpango maalum.
“ Kama nilivyoeleza katika Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Tatu, Serikali itaendelea na mkakati wake wa kuufanya Mji wa Zanzibart kuwa na haiba inayostahiki. Tunawaomba Wananchi waendelee kuyaunga mkono mazoezi ya aina hiyo ”. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia  kelele za Wananchi dhidi ya vilabu vya pombe vinavyoonekana kuzidi kufunguliwa katika maeneo ya makaazi ya Watu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisema taratibu za ufunguzi wa nyumba za biashara hizo lazima uzingatie sheria  zilizopo.
Alisema Serikali haikatazi watu au Mtu kufurahi baada ya saa za majukumu ya kazi, lakini  kinachokusudiwa kuzingatiwa zaidi kwa wahudumu wa nyumba hizo ni kuheshimu mila, utamaduni wa kutoudhi wakaazi wa maeneo husika ili kuendelea kuimarisha heshima ya Nchi.
Balozi Seif  aliwaagiza wamiliki wa nyumba hizo kudhibiti upigaji ovyo wa muziki katika maeneo ya makaazi ya wananchi kwani baadhi ya nyumba hizo zimekuwa zikiendeleza kelele kubwa wakati wa usiku.
Kuhusu suala la Amani ambalo limekumbwa na tabia iliyochipuka ya baadhi ya watu hasa vijana kuharibu mali, mimea na mali za Wananchi na Taasisi za Umma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alivitaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali wale wote watakaopatikana na hatia ya kuhatarisha amani na utulivu uliopo Nchini.
Balozi Seif  aliwapa pole Wananchi wa Kijiji cha Pwani Mchangani Kisiwani Unguja na Kikosi cha Vyuo vya Mafunzo Tungamaa Kisiwani Pemba kwa kuharibiwa mazao na vipando vyao.
Aliwaasa wazee na wazazi katika maeneo mbali mbali Nchini kuendelea kuwasihi watoto kutojiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani vikiwemo vile vya ufisadi wa kuharibu mali na mazao ya watu.
Balozi Seif  aliwahakikishia wananchi kwamba Serikali itaendelea kusimamia amani na utulivu uliopo nchini na wale watakaojitokeza  kuvuruga hali hiyo vyombo vya dola havitasita kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi.
Wajumbe wa Mkutano huo wa Nne wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar walijadili na kupitisha Miswaada Minne ya Sheria ambayo ni pamoja na Mswaada wa Sheria ya kufuta na kutunga upya Sheria ya Ushahidi Sura ya Tano na masuala yanayohusiana na nayo.
Mswaada mengine ni Mswaada wa Sheria ya kurekebisha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nambari 2 ya Mwaka 2005 kuweka masharti bora zaidi kwa ajili ya ufanisi na usimamizi imara wa Mfuko na mambo yanayohusiana nayo.
Uliofuata ni Mswaada wa Sheria wa kufuta sheria ya manunuzi na uuzaji wa mali za Serikali nambari 9 ya mwaka 2005 na kutunga sheria inayoanzishwa  mamlaka ya manunuzi na uuzaji wa mali za Umma na kuweka masharti mengine yanayohusiana nayo.
Ukamalizia mswaada wa sheria wa kutunga sheria ya usimamizi wa fedha za Umma kwa kuweka masharti bora ya udhibiti na kusimamia fedha za umma na kuweka mambo mengine yanayohusiana na hayo na kufuta sheria ya usimamizi wa fedha za Serikali nambari 12 ya mwaka 2005.
Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi Jumatano ya Tarehe 15 Febuari Mwaka 2017 mnamo saa 3.00 za Asubuhi.

MAKAMU wa Rais Mama Samia Aendesha Harambe ya Shs.Bilioni 1 Kusaidia Mfuko wa Ukimwi Nchini.

$
0
0
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF)  Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akihutubia kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Meza kuu.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Salum Mussa (kulia), akishiriki uzinduzi wa mfuko huo na wadau wengine.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Mkutano ukiendelea.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati), akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye kwa ushiriki wake katika kuchangia mfuko huo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko. 
 Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kampuni hiyo ilichangia sh.milioni 100.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga kwa ajili ya kuchangia mfuko wa ukimwi Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko.

Makamu wa Rais akipeana mkono na mdau aliyeshiriki uzinduzi huo. 

Meneja Mawasiliano Msaidizi  wa Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza baada ya kutoa mchango wa sh. milioni tano.


Na Dotto Mwaibale

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan ameendesha harambee ya sh. bilioni 1,036, 050,000 ahadi ikiwa ni sh. bilioni 5, 913,650,000 pamoja na ahadi ya serikali kwa ajili ya  Mfuko wa Ukimwi Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Ukimwi (ATF) ulioenda sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi  Duniani jijini Dar es Salaam juzi,  aliwaomba wadau mbalimbali  kuchangia mfuko huo ili kukabiliana na changamoto ya ukimwi nchini.

"Tunaomba wadau mbalimbali kusaidia mfuko huo kwani bado tunachangamoto kubwa ya ugonjwa wa ukimwi" alisema Makamu wa Rais mama Samia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama Sera ya ukimwi ya mwaka 2001 imeelekeza kuanzishwa kwa mfuko wa ukimwi ambapo serikali ilianza mchakato wa kuanzisha mfuko huo mwaka 2008.

Alisema mfuko huo umeanzishwa kwa kupitia marekebisho ya Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi namba 6 ya mwaka 2015.

"Madhumuni makubwa ya mfuko wa Ukimwi ni kuhakikisha uwepo wa rasilimali za kutosha na za uhakika katika kupambana na ukimwi zilizotokana na mapato ya ndani" alisema Mhagama.

Alisema kulingana na Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi uliothaminishwa, mahitaji ya Taifa kugharamia Ukimwi katika kutekeleza makakati huo kwa kipindi cha miaka mitano 2013/14 na 2017/18 yanakadiriwa kufika 6 Trilioni (USD 2.975 bilioni).

Alisema asilimia 93 ya fedha hizo zinatarajiwa kutoka kwa wafadhili na asilimia 7 kutoka vipato vyandani na kuwa sehemu kubwa ya asilimia 56 ya fedha zote katika miaka hiyo mitano ni kwa ajili ya manunuzi ya dawa za kufubaza VVU (ARV drugs)

Alisema mahitaji ya fedha katika kipindi cha mwaka 2016/17 ni Trilioni 1.258, fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 833 na hivyo kuwa na upungufu wa Bilioni 425.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2017/18 mahitaji ya fedha ni Tsh. Trilioni 1.260, fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 740 na hivyo kuwa na upungufu wa Bilioni 520.

Mhagama alisema licha ya kupungua kwa ahadi ya wafadhili bado hakuna uhakika kama fedha zilizoahidiwa zitapatikana zote kwa mantiki hiyo hivyo kuongeza fedha zinazotoka ndani ya nchi ni suala la muhimu sana.



Leo Tz Bongo Magazetini

Ujumbe wa Katuni Huuuoooo....

Ligi Kuu ya Zanzibar Zimamoto na Kilimani City Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Zimamoto Imeshinda 3--0.

$
0
0
 Wachezaji wa Timu ya Zimamoto na Kilimani Cty wakiwania mpira, wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika jioni leo Timu ya Zimamoto imeshinda 3--0. dhidi ya Timu ya Kilimani City. 
Beki wa Timu ya Kilimani City Nurdin Bakar akimiliki mpira huku mshambuliaji wa timu ya Zimamoto akijaribu kumfuata. 
 Golikipa wa Timu ya Zimamoto akiokoa moja ya hatari golini kwake huku mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Ibrahim Ali akiwa tayari kuchukua mpira, katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Zimamoto imeshinda 3--0


 Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Ibrahim Ali akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani.wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Zimamoto imeshinda 3--0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Ibrahim Ali akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani.
 Benchi la ufundi la Timu ya Kilimani City wakiwa na simanzi baada ya timu yao kufungwa katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa bao 3--0. mchezo uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar.
 Beki wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani akimzuiya mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City mwenye mpira Juma Abdallah, Timu ya Zimamoto imeshinda bao 3--0 
Mshambuliaji wa timu ya Kilimani City akimpita beki wa Timu ya Zimamoto wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan jioni hii. (2-12-2016) 

Bei ya Fedha za Kigeni Zenj leo.

Taarifa ya Tanzania Blogges Network (TBN) Kwa Waandishi wa Habari 02 DESEMBA, 2016 Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

$
0
0




Ndugu Mwakilishi kutoka Benki ya NMB,
Waandishi wa habari,

Kwa niaba ya Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) napenda kuwashukuru kwa kujitokeza katika mkutano huu muhimu. TBN inajua kuwa mnamajukumu mengi ya kuujuza umma masuala anuai, lakini mmechagua kuja kwetu ili kutusikiliza tulichowaitia na baadae tunaamini mtaujuza umma juu ya tukio letu.

TBN iliosajiliwa rasmi na Serikali mwezi Aprili, 2015 kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' itakayofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hii maalumu ambayo itajumuisha mafunzo ya siku mbili yaani tarehe 5 na 6 ya Mwezi Desemba, 2016 kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania nzima (Bara na Visiwani) itafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima ya mitandao ya jamii.

Ndugu Wanahabari,
Katika mkusanyiko huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine. Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.

TBN inapenda kutoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Nne na Tano chini ya Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa ushirikiano alioanza kuuonesha hasa kwa kutambua mchango wa mitandao hii ya kijamii na hata kuitumia katika utoaji wa taarifa zao. Kimsingi hii ni hatua nzuri na ya kuigwa hasa katika ulimwengu huu ambapo dunia imekuwa kama kijiji kutokana na hatua ya maendeleo ya habari na mawasiliano.

Ndugu Wanahabari,
Kwa kulitambua hili mnaweza kuona hata taasisi nyeti kama Ikulu nayo ina Blogu maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma, Idara ya Habari Maelezo nayo ina Blogu kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma juu ya masuala mbalimbali yanayopaswa kutolewa kitaarifa kwa jamii. Jambo la kujivunia zaidi kwa maendeleo ya mitandao hii hata Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape M. Nnauye amekuwa mstari wa mbele kuona umuhimu wa mitandao ya kijamii hasa blogu na hata kuzitumia katika kupasha habari umma. Hata katika mkutano wetu wa kesho kutwa ndiye tunayemtarajia kuwa mgeni rasmi atakayetufungulia mkutano huo.

Ndugu Wanahabari,
Kwa namna ya pekee TBN inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Benki ya NMB kwa kukubali kuwa wadhamini wa kuu wa mkushanyiko huo wa 'bloggers' kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa yetu. Kitendo cha kujitolea kufanikisha jambo hili kinaonesha namna gani NMB inavyowajali wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo hili la upashanaji habari kwa jamii.

Kama hiyo haitoshi tunapenda kuwashukuru wadhamini wengine ambao ni NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola ambao wamejitolea kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers na kutoa mafunzo kwao. Tunaamini tutakuwa nao siku zote katika masuala mengi ya maendeleo ya tasnia ya mitandao ya kijamii.
Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi

0756469470

TANESCO Yatangaza Kuwepo kwa Katizo la Umeme kwa Baadhi ya Mikoa Ilioungwa Kwenye Gridi ya Taifa.

$
0
0
 Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.
SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.

Matengenezo hayo yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
  
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu


Kampuni ya Puma Energy Tanzania yajivunia kuutangaza Utalii wa Tanzania

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi, Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya marubani wa ndege za kizamani mara baada ya kuwasili Zanzibar.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy  Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza  katika hafla maalum baada ya kuwasili  jumla ya ndege 22 za kizamani  zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na  1930 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana.
 Mwenyekiti wa bodi ya Puma Energy  Tanzania,  Dk Ben Moshi (wapili kushoto)  akisalimiana na rubani pekee wa kike  katika mashindano ya kurusha ndege za  kizamani zilizotengenezwa kati ya mwaka  1920 na 1930 mra baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid  Amani Karume, Zanzibar, wa kwanza kushoto  ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya  Utalii Zanzibar, Dk Miraj Ussi na wa pili  kulia ni Meneja Mkuu wa Puma Energy  Tanzania, Dk Ben Moshi.
 Moja ya ndege ya kizamani iliyotengenezwa  kati ya miaka 1920 na 1930 ikiwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika moja ya
mashindano ya ndege hizo yajulikanayo kwa jina la "Vintage Air Rally"
yaliydhaminiwa na Kampuni ya Puma Energy  Tanzania.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya  Utalii ya Zanzibar, Dk Miraj Ussi  akizungumza katika hafla ya kuzipokea  jumla ya ndege 22 za kizamani  ziliyotengenezwa kati ya miaka 1920 na  1930 mara baada ya kuwasili kwenye uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika moja ya mashindano ya ndege  hizo yajulikanayo kwa jina la "Vintage Air  Craft Rally"
 Baadhi ya ndege za kizamani  zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na
1930 zikiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana.
Mkurugenzi wa Vintage Rally, Sam Rutherford akizungumza mara baada ya
kuwasili kwa ndege za kizamani zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na
1930 zikiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana. Rutherford aliipongeza kampuni ya Puma Energy kwa kufanikisha mashindano  hayo




Kampuni ya Puma Energy Tanzania yajivunia kuutangaza Utalii wa Tanzania

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imesema itaendeleza jukumu la kuutangaza Utalii wa ndani ya Tanzania nje ya mipaka yake ili kuwawezesha wataalii wengi kuja nchini na kuongeza pato la taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti mara baada ya kuwasili jumla ya ndege 22 za kizamani zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na 1930 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana.

Corsaletti alisema kuwa jukumu la kuutangaza utalii wa Tanzania halipo kwa serikali pekee, kwani hata wadau wanafursa ya kufanya hivyo ili kuendelea kuleta tija nchini.

Alisema kuwa jumla ya marubani 48 kutoka ndege 22 wameshiriki katika mashindano ya ndege za zamani maarufu kwa jina la “ Vintage Air Rally” yenye lengo la kuutangaza utalii nchini na ushiriki wao mbali ya kujitangaza, pia ni sehemu ya kushiriki katika kazi za kijamii kwani mashindano hayo pia yanachangisha fedha kwa ajili ya shughuli za Unicef, Bird Life International na Seed Bombing.

“Mbali ya marubani na waongoza ndege, pia kuna washiriki wengine ambao wameambatana na ndege hizi kwa ajili ya kazi mbalimbali, hao wote watashindana katika hifadhi na kuona vivutio vya utalii na kwenda kuvitangaza nje ya nchi, hii ni fursa pekee ya kuvitambulisha duniani,”

“Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeshiriki ipasavyo kuhakikisha ndege zote zinapata mafuta ya kutosha aina ya Avigas mbayo kampuni yetu pekee ndiyo inazalisha mafuta haya ambayo ni ya ubora wa hali ya juu, mbali ya kupita katika mbuga ya Ngorongoro na kujionea utititiri wa wanyama na vivutio mbalimbali, baada ya hapo watapita Dodoma, Songwe (Mbeya) kabla ya kuelekea Zambia,” alisema Corsaletti.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Puma Energy Tanzania, Dk Ben Moshi aliipongeza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukubali ndege hizo kutua na kupata huduma ya mafuta huku maribani wake wakijionea vivutio mbalimbali vya utalii.

“Tumefarijika na ushirikiano tulioupata kutoka viongozi na kuwezesha tukio hili la kihistoria kufanyika kwenye uwanja wa ndege na watu mbalimbali kujionea ndege hizi za kizamani lakini bado zinauwezo wa kuruka umbali mrefu, kampuni yetu imefurahia sana nahasa jukumu la kuwa wadhamini wa mashindano haya,” alisema Dk Moshi.

Dk Moshi alisema kuwa mashindano hayo yamefungua ukurasa mpya kwa kampuni ya Puma Energy kwa upande wa biashara na hasa ubora wa bidhaa zake ambazo mpaka sasa zimewavutia na zinaendelea kuwavutia wateja wengi.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar, Dk Miraj Ussi aliipongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kuchagua Zanzibar kuwa moja ya kituo cha mashindano ya ndege hizo ambazo zenyewe ni kivutio pekee.

Dk Ussi alisema kuwa mashindano hayo ya Ndege za zamani yataendelea kuutangaza utalii wa Zanzibar na kuwendelea kuwa maarufu zaidi na kuwafanya watalii wengi zaidi kutembelea kujionea utajiri mkubwa wa nchi.

“Ni faraja kuwa miongozi mwa mashindano haya, kwa kweli yametuvitia sana kwani yataendelea kututangaza nje ya mipaka yetu, tuna vivutio vingi sana hapa, tunawaomba mashindano mengine yaanzie hapa,” alisema Dk Ussi.

Mkurugenzi wa Vintage Rally, Sam Rutherford aliipongeza kampuni ya Puma Energy kwa kufanikisha mashindano hayo huku akivutiwa na vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania. “Tumependa sana Zanzibar, tumeona vivutio kadhaa vya utalii, bado tutaendelea kuona, kwani mashindano yanaendelea,” alisema Rutherford.

Vintage Air Rally inahusisha ndege za zamani za kati ya miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika kutoka katika visiwa vya Crete nchini Ugiriki hadi Cape Town Afrika ya Kusini.

Shindano hili lilianza tarehe Novemba 12, Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35 wakipita katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania na kuendelea Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika ya Kusini.

Watakaokwamisha Maboresho ya Sekta Binafsi Kukiona – MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inahitaji ushirikiano mkubwa na wafanyabiashara, hivyo haitakubaliana na mtumishi yeyote wa umma atakayefanya urasimu kwa lengo la kukwamisha uboreshaji wa sekta binafsi.

Amesema miongoni mwa maboresho yanayofanywa na Serikali katika sekta binafsi ni pamoja na kuimarisha utendaji wa watumishi na kuondoa urasimu katika utendajikazi wa kila siku baada ya eneo hilo limelalamikiwa sana.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Desemba 2, 2016) wakati akizungumza na wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda mkoani Arusha kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Ziara hiyo inalenga kuangalia utelelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,Utendaji wa Serikali, kusikiliza na kujionea kero zinazowakabili wananchi  wa Mkoa huo na kushirikiana na viongozi wa Mkoa ili kuweza kuzipatia suluhisho.

“Serikali inafanya jitihada kubwa katika kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi yetu. Pia mapambano dhidi ya rushwa yanayofanyika ndani ya Serikali na nje yanalenga kuleta maboresho makubwa katika sekta binafsi ,” alisema.

Alisema Serikali inawataka watendaji wake wote watumie lugha nzuri na rafiki katika kutoa huduma kwa wafanyabiashara na wananchi kwa jumla na haitamvumilia mtumishi yeyote atakayefanya urasimu ili mfanyabiashara atoe rushwa.

“Hatuwezi kuzungumzia maendeleo katika sekta za maji, madini na viwanda bila ya kutaja wafanyabiashara kwa sababu hata viwanda wao ndiyo wamiliki. Wafanyabiashara wameondoa vijana wengi waliokuwa wanakaa vijiweni na kujadili mambo yasiyokuwa na tija na kuwaajiri kwenye viwanda vyao,” alisema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itaimarisha mipaka yake na  kuzuia uingizwaji holela wa bidhaa kutoka nje ambazo nyingi zinazalishwa hapa nchini huku lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani.

“Hatuwezi kuwalinda wazalishaji wetu wa ndani bila ya kuweka doria ya nguvu  kwenye mipaka yetu ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa, hususan zinazozalishwa nchini. Lazima Serikali isaidie kulinda masoko ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu,” alisema.

Aliongeza kuwa “Mfano Jiji la Arusha linajenga mradi wa maji na kisha mzabuni anaagiza mabomba kutoka nje wakati viwanda vya ndani vinatengeza kwa viwango sawa au bora zaidi ya yanayoagizwa nje, huko si kutaka kuongeza gharama ya mradi”? Alihoji.

Alisema Serikali haitakubali kuruhusu viwanda vya ndani vife kwa kukosa soko baada ya uingizwaji wa bidhaa za nje. “Ni lazima mitaji ya wafanyabiashara iheshimiwe na ilindwe ili iweze kuleta tija inayokusudiwa,”.

Waziri Mkuu alisema Serikali na sekta binafsi zimefanya jitihada kubwa katika  kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji kwenye sekta ya viwanda nchini. Na sekta hiyo ndiyo inategemewa katika kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati.

Kwa upande wao wafanyabiasha wengi walilalamikia kuwepo kwa wingi wa kodi ambapo wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuzipunguza ili kuwaondolea usumbufu.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAMOSI, DESEMBA 3, 2016.

Jezi Mpya za Zanzibar Zaingia Mitandaoni

$
0
0
Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar, ZFA kimepata mkataba wa jezi kwa ajili ya timu za taifa za visiwa hivyo.
                         JEZI YA UGENINI
Jezi hizo mpya zimetengenezwa na kampuni ya AMS Clothing ya nchini Australia na zitatumiwa na timu za taifa za Zanzibar katika michuano mbali mbali.
Mbali na Zanzibar, kampuni ya AMS Clothing ina mkataba wa kutengeneza jezi za timu za mataifa ya Rwanda, Sierra Leone na Sudani ya Kusini.
                        JEZI YA NYUMBANI
Mwakilishi wa AMS Clothing alisema wanatarajia kuuza jezi hizo katika mtandao huku lengo lao likiwa kuuza jezi hizo visiwani katika siku za usoni.
” Tulifanya kazi na Mzee Zam Ali wa ZFA kufanikisha kila kitu. Jezi ziliwasili Zanzibar wiki iliyopita. “

Mkutano Mkuu wa TBN Dar.

Viewing all 35931 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>