Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 35936 articles
Browse latest View live

Kituo cha Huduma za Sheria Chawanoa Wasaidizi Wake Kutatua Migogoro Katika Jamii.

$
0
0
Na Salmin Juma ,Pemba
Katika muendelezo wa kutatua migogoro na changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ya Pemba katika maswala ya kisheria, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) upande wa Pemba kimezidi kuwanoa waajiri wake ambao ni wasaidizi wa sheria (parallegals) wa majimbo yote Pemba kwa kuwakumbushia sheria mbalimbali zinazotakiwa kutiiwa nchini ambazo zinagusana karibu na majukumu yao.

Hayo yamebainika jana katika Mkutano maalum uliyokusudia kutoa mafunzo kwa wasaidizi hao huko Wesha katika Hoteli ya Misali mkoa wa kusini Pemba.

Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa kituo hicho Pemba Bi Fatma Khamis Hemed amewataka wasaidizi hao kuwa makini zaidi kwa kile wanacho someshwa, lengo hasa ni kuwapatia elimu juu ya uelewa wa sheria mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyengine zinauhusiano wa karibu na kazi walizopangiwa kuzifanya.

Akiwasilisha mada ya Ufafanuzi wa sheria za Tawala za mikoa sheria nambari 08 /2016 Afisa mipango wa kituo hicho Bw: Khalfan Amuor Mohammed amesema lengo la sheria hiyo kwa serikali ni kukuza kipato cha wananchi na kuondosha umasikini hivyo kwa makusudi serikali imeona ni vyema kupitisha sheria hiyo kwakua katika ngazi za mikoa kujia chini ndiko kwenye umuhimu zaidi.

Muhammed amewataka wasaidizi hao kufahamu kua sheria hiyo moja kwa moja inampa mamlaka waziri husika wa kuweza kugawa mipaka au maeneo ya nchini kwa kushauriana na mkuu wa mkoa husika ikiwa wameona kuna haja ya kimsingi kufanya hivyo.

“ mukiona vile mipaka na maeneo kukatwa basi mujue inafanyika vile kwa mujibu wa sheria ndio iliyompa mamlaka waziri, hilo mulifahamu” alisema Muhammed
Katika sheria hiyo Muhammed amebainisha kazi za mkuu wa mkoa pamoja na mkuu wa wilaya kwa lengo la kuwaongezea taaluma wasaidizi hao ili kuzidisha ufanisi katika kazi zao.

Akiwasilisha mada ya ufafanuzi wa sheria ya usajili wa vizazi na vifo sheria nambari 10 / 2006 bw: Muhammed Ali Maalim kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Zanzibar (idara ya vizazi na vifo) amewataka wasaidizi wa sheria kufahamu kua mototo anapozaliwa anatakiwa kutambulishwa katika mamlaka ya vizazi na vifo ili kupatiwa haki zake za msingi ikiwemo cheti cha kuzaliwa, lakini hivyohiyo mtu kufariki inatakiwa kuwasilisha taarifa zake, amesema hiyo ni kwa mujibu wa sheria na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria wenyewe.

“ ingawa sheria hii ipo lakini hapa panashida, wananchi wengi hutoa taarifa za kuzaliwa kwa mototo lakini inapotokea mtu kufariki hupuuza kuleta taarifa na wanasahau kua taarifa hizo ndizo zinazoiwezesha serikali kufanya tathmini juu ya sababu za vifo nchini na kama ni maradhi serikali ipate kujipanga zaidi” alisema Maalim.

Maalim ametumia nafasi hiyo kuwashauri vijana nchini hasa wale wanaotaka kujiunga na vikosi vya ulinzi kwakua mara nyingi vikosi hivyo huhitaji umri maalum, imegundulika wapo baadhi ya vijana huchakachua vyeti vya kuzaliwa ili kukidhi matakwa ya mashrti hayo, amesema kunya hivyo ni kosa kisheria na ikigundulika mtu anaweza kuingia hatiani kujibu kosa hilo na sheria inaweza kumbana.

Katika mafunzo hayo pia mada ya sheria ya mototo nambari 6/2011 ilipata nafasi ya kuwasilishwa na mratibu wa kituo hicho bi Fatma Khamis Hemed na Bw: Hassan Abdalla Rashid mwanasheria kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za Zanzibar aliwasilisha mada ya sheria ya mamlaka ya serikali za mitaa ya 2014, ambapo mafunzo hayo yataendelea kesho.

Uzinduzi wa Baraza la Vijana Wilaya ya Chakechake Pemba.

$
0
0

 Na Salmin Juma Pemba
MKUU wa Wilaya Chake Chake Mhe: Salama Mbarouk Khatib amewataka vijana kuyatumia mabaraza ya vijana kwa kuhakikisha wanafanya shughuli walizojipangia , ili kujikomboa na umasikini na kuweza kujiletea maendeleo kiuchumi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Chake Chake katika uwanja wa Tenis amesema, lengo la kuwekwa mabaraza ya vijana ni kuwa, mategemeo makubwa ni kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.

Mkuu huyo amesema kuwa, kila kijana anatakiwa atimize wajibu wake, hivyo ni vyema wakafuata muongozo wa mabaraza, ili kuweza kuleta mabadiliko mbali mbali kiuchumi, kijamii, kisiasa na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Khadija Khamis Rajab amewataka vijana hao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita suala la udhalilishaji katika jamii na kuweza kuviripoti vitendo hivyo kwa haraka pindi vinapojitokeza.

Akisoma risala Mjumbe wa baraza hilo Ibrahim Salum Rashid amesema, kuna changamoto nyingi zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na kukosa ofisi maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji, ambazo zinawasaidia kujikwamua na umasikini.

Hata hivyo mwenyekiti wa Baraza hilo, Bakar Hamad Bakar amewataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii zitakazowaletea mapato yatakaweza kuwakwamu hali ngumu ya maisha.

Barabara ya Fuoni Ikiwa Imekamilika Ujenzi Wake na Kutowa Huduma kwa Wananchi.

$
0
0
Ujengi wa Barabara mpya ya fuoni ukiwa umekamilika ujenzi wake uliojengwa na Kampuni ya MECCO Tanzania na kuaza kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar kwa wanaotumia barabara hiyo kuelekea maeneo ya Mkoa wa Kusini Unguja kama inavyoonekana picha ikiwa katika hali ya kisasa.  

Article 12

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                                                                                            3.12.2016
---
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kubadilisha mitaala katika Skuli za Sekondari sambamba na kuimarisha vyuo vya amali ili somo la ujasiriamali liweze kuchukua nafasi kubwa katika mitaala na kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza elimu ya Sekondari wanafaulu vyema ujasiriamali.

Dk. Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kongamano la siku mbili na maonyesho ya Wajasiriamali linalofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni mjini Unguja.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kwa utaratibu huo wanafunzi watapata eimu itakayowasaidia kujiajiri wenyewe na kutumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kuhakikisha kuwa inaongeza kasi katika kulishughulikia suala hilo.

Dk. Shein aliwakumbusha vijana kuwa elimu waliyoipata katika Vyuo Vikuu na Taasisi mbali mbali zinazotoa mafunzo ya kazi na ufundi ni mtaji muhimu katika kuendeleza shughuli za ujasiriamali.

Hivyo, aliwataka wasijenge dhana kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara ndogo ndogo za bidhaa zinazoonekana katika masoko lakini wajifunze kutokana na uzoefu wa nchi mbali mbali hasa India ambapo vijana wengi waliosoma wamekuwa wakijiajiri wenyewe baada ya kumaliza masomo yao.

Alisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa kuwaendeleza wajasiriamali katika kuyafikia malengo ya kupambana na umasikini wa kipato na kupunguza tatizo la ajira hasa miongoni mwa wanawake na vijana.

Alisema kuwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kipindi hiki cha pili cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba  ameamua kuyaweka makundi ya vijana na wanawake katika wizara moja na masuala ya uwezeshaji ili shughuli za uwezeshaji kupitia ujasiriamali ziweze kukuza kipato cha wananchi na kuondoa umasikini.

Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya Mfuko wa Uwezeshaji ambao katika kipindi cha miaka miwili na miezi minne tangu mfuko huo ulipoanza kazi zake ambapo jumla ya mikopo 998 yenye jumla ya Tsh. Bilioni 1.6 imeshatolewa Unguja na Pemba ambapo tayari marejesho ya asilimia 96 yameshafanyika.

Alisema kuwa jambo la kufurahisha zaidi ni kuwa taarifa zinazonesha kwamba asilimia 67 ya watu waliopewa mikopo ya Mfuko huo ni vijana wenywe umri kati ya miaka 18 hadi 35 huku akiwataka wanasiasa kutowadanganya vijana kuhusiana suala la ajira kwani vijana hivi sasa hawadanganyiki.

Alisema kuwa lengo la viongozi hao wa kisiasa ni kutaka kuwagombanisha vijana na Serikali yao na kuwataka viongozi hao kusema ukweli katika suala zima la ajira.

Dk. Shein aliwahakikishia wananchi na wajasiriamali kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko imejipanga ili kuona kwamba wajasiriamali wanafikia malengo waliyoyakusudia kwa kuwatafutia masoko.

Dk. Shein aliwaeleza wajasiriamali hao kuwa watu matajiri na maarufu duniani kote ikiwemo Zanzibar ni wajasiriamali hivyo, aliwahimiza kuendelea kukuza vipaji na elimu walizonazo wakiamini kwamba nao wanaweza kufanikiwa kama walivyofanikiwa wao.

Pia, Dk. Shein alisema kuwa Serikali itaendelea kuzitatua changamoto zinazowakabili wakulima na wajasiriamali katika suala zima la kuongeza ubora wa bidhaa na mazao yanayolimwa.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alitoa pongezi kwa Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kwa mafanikio yaliopatikana katika kituo cha Kuleta na Kukuza Wajasiriamali kilichopo Mbweni kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo na kusisitiza haja ya kuharakishwa ujenzi wa kituo kama hicho huko Pemba.

Mapema Dk. Shein aliangalia maonyesho ya Wajasiriamali ambapo alipata fursa ya kukagua bidhaa zao mbali mbali wanazozizalisha. Pia katika hafla hiyo alitoa vyeti maalum kwa wachangiaji wa kongamano hilo.

Nae Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Maudline Castico alisema kuwa kongamano hilo ni la kwanza la aina yake kufanyika hapa nchini na kueleza kuwa mchango wa Sekta binafsi kupitia wajasiriamali wakubwa na wadogo ni muhimu sana ili kufikia lengo la Zanzibar kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati ifikapo 2020.

Alisema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kuhamasisha kuwaelimisha wajasiriamali ili kuendeleza shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Wajasiriamali katika risala yao iliyosomwa na Aziza Saleh, walieleza kuwa wanafahamu kwamba wakati huu wa mabadiliko ya uchumi duniani kote ni wajasiriamali watakaosaidia kuzalisha ajira kupitia ujasiriamali, ili kusaidia Serikali kukuza uchumi wake.

Walieleza kuwa wajasiriamali wabunifu na wavumbuzi wanauwezo wa kuanzisha mambo tofauti kulingana na mahitaji ya soko yaliopo ili kuweza kuchangia pato la Taifa na ukuaji wa uchumi hapa nchini iwapo tu wataelekezwa na kupatiwa utaalamu unaohitajika.

Nao Wawakilishi wa Shirika la kujitolea la Kimataifa (VSO), pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kushirikiana na  Serikali katika kuwasaidia wajasiriamali ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Mwalimu Afariki Katika Mkutano wa Chama cha CWT Jijini Dar es Salaam.

$
0
0

 Mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula enzi za uhai wake.

 Jeneza lenye mwili wa mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula likiwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Wazo Hili Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa ibada ya kuuaga mwili huo.
 Mume wa marehemu, Samuel Mwakatumbula akimbusu mke wake wakati wa ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wake. Kushoto ni mtoto wake Kelvin.
Binamu wa marehemu, Nobert Nselu (kulia) akimsaidia rafiki wa karibu wa marehemu mama Malugu wakati mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake.
 Rafiki wa marehemu mama Malugu (katikati) akisaidiwa.
 Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu 
Wazo Hill.

 Ni huzuni kubwa 
 Wakina mama wakiwa na maua wakati wakisubiri mwili wa marehemu kuingizwa ndani.
 Geneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa nyumbani kwake. 

 Mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula akimuaga mke wake
 Mtoto mkubwa wa marehemu Nico Mwakatumbula (katikati), akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
 Waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu katika Kanisa la KKKT Usharika wa Wazo Hill.
 Mwili ukiwa kanisani.
 Mume wa marehemu akiwa na watoto wake. Kutoka kulia ni Gloria, Kelvin na Nico.
 Wanafamilia wakiwa katika ibada hiyo ya kumuaga mpendwa wao.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.N a Dotto Mwaibale

MWALIMU Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula wa Shule ya Msingi Kumbukumbu katika Manispaa ya Kinondoni amefariki dunia wakati akiwa katika mkutano wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) na viongozi wa Idara ya Elimu wa manispaa hiyo.

Kifo cha mwalimu huyo kimetokea Desemba 1, 2016 Siku ya Ijumaa majira ya jioni wakati viongozi hao walipokuwa wakimalizia ziara yao ya kutembelea shule mbalimbali katika manispaa hiyo.

Akizungumza na Jambo Leo mume wa marehemu Samuel Mwakatumbula alisema mke wake hakuwa na tatitizo lolote la kiafya na siku ya tukio hilo aliamka salama na kumuaga kuwa anawahi kwenye mkutano huo.

"Siku chache kabla ya kifo chake mke wangu aliniambia alikuwa hajisikii vizuri kwani alikuwa na uchovu wa kawaida" alisema Mwakatumbula.

Mwakatumbula alisema alipigiwa siku na kuambiwa kuwa mke wake alianguka ghafla wakati mkutano ukiendelea na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mount Mkombozi iliyopo maeneo ya Morocco ambapo waliambiwa tayari alikuwa amefariki.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa maziko yatakayofanyika leo marehemu ameacha mume na watoto watatu, Nico, Kelvin na Gloria.









Balozi Seif Azindua Kambi ya Siku Mbili ya Uchunguzi wa Maradhi Mbalimbali Yanayowahusisha Wananchi na Kupatiwa Dawa.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kuzindua Kambi la uchunguzi wa Afya  katika Kituo cha Afya Mahonda chini ya Watalaamu kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Baps Charities.Kushoto ya Balozi Seif Ali Iddi  ni Muweka Hazina wa Jmuiya ya Baps Charities Bwana Kapil Dave.
Daktari dhamana ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Macho Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Slim Mohammed Mgeni wa kwanza kutoka Kulia akimpatia maelezo Balozi Seif anayeshuhudia uchunguzi wa Macho katika Kambi ya afya iliyowekwa Kituo cha Afya Mahonda.
Balozi Seif akimvisha Miwani Mmoja wa Wananchi baada ya kumaliza kufanyiwa uchunguzi wa Afya na kubainika anahitaji kuwa na miwani ya kusomea.
Msongamano mkubwa wa Wananchi waliojitokeza kufanya uchunguzi wa Afya katika Kituo cha Afya Mahonda chini ya Madaktari na wataalamu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Baps  Charities.(Picha na – OMPR – ZNZ.)

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema utamaduni wa kupima afya kila baada ya kipindi ni jambo la msingi linalomuwezesha Mwanaadamu kuendelea kuishi vizuri kwa matumaini.

Alisema vipo baadhi ya vifo vya kushitua vinavyowashangaza watu katika maeneo mbali mbali lakini vikichunguzwa chanzo chake hubainika kuwa ni ukosefu wa utambuzi  wa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua marehemu ambayo wataalamu walikuwa na uwezo wa kuyatibu.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alisema hayo wakati akizindua  rasmi Kambi ya Siku mbili ya Uchunguzi wa maradhi mbali mbali yanayowasumbua wananchi pamoja na kutolewa dawa bure, miwani za kusomea kwa wale watakaobanika kuwa na matatizo ikiwemo pia operesheni za Macho.

Kambi hiyo iliyofunguliwa katika Kituo cha Afya Mahonda inaendeshwa chini ya udhamini wa Jumuiya ya Kimataifa ya kuhudumia jamii ya Baps Charities ikijumuisha wataalamu na Madaktari Bingwa wapatao kumi kutoka Nchini India na Dar es salaam.

Balozi Seif aliwaeleza wananchi hao waliojitokeza kufanya uchunguzi wa Afya zao kuwa na tahadhari ya kujiepusha na ongezeko la maradhi ya kisukari na shindikizo la Damu kwa kuwaona wataalamu wa afya pale wanaoanza kuona dalili za maradhi hayo.

Alisema vifo vingi vinavyotokea ndani ya jamii  kwa sasa vinaripotiwa kuhusisha maradhi ya Kisukari na sindikizo la Damu ambayo hatimae mgonjwa anaishia kukumbwa na maradhi ya kiharusi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza na kuishukuru Jumuiya hiyo ya Kimataifa ya kuhudumia Jamii ya Baps Charities kwa mchango wake mkubwa wa kusaidia jamii yenye kipato cha chini na mazingira magumu.

Mapema Mweka Hazina wa Jumuiya ya Baps Charities Bwana Kapil Dave alisema Taasisi yao imeamua kutoa huduma za Afya kwa jamii ya kipato cha  chini baada ya kubaini ongezeko kubwa la gharama katika upatikanaji wa huduma za afya.

Bwana Kapil aliwatoa hofu Wananchi kwamba huduma za Afya pamoja na Dawa zinazotolewa na Wataalamu na Mabingwa wa Taasisi hiyo hazina mashaka yoyote baada ya kufanyiwa uhakiki na vyombo vinavyohusika Kimataifa.

Mweka Hazina huyo wa Jumuiya ya Baps Charities aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na watendaji wote wa Sekta ya Afya waliochangia kuwajengea mazingira bora ya uchunguzi pamoja na utowaji wa huduma za Afya hapa Zanzibar.

Bwana Kapil alifahamisha kwamba ushirikiano huo wa pande mbili ndio uliowawezesha wataalamu wa Afya wa Baps kurejea kutoa huduma tena  Zanzibar baada ile huduma waliyotowa mwanzo katika Kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja kipindi kilichopita.

Wataalamu na Mabingwa hao wa Sekta ya Afya kutoka Baps Charities wanafanya uchunguzi wa maradhi mbali mbali pamoja na kutoa dawa bure ikiwemo miwani za kusomea kwa Wananchi wanaofika kwenye Kambi hiyo.

Zaidi ya Wananchi 1,000 kutoka sehemu mbali mbali za Majimbo na Shehia zilizomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” wamejitokeza kufanya uchunguzi wa afya zao na kupatia dawa pamoja na ushauri.

Mrembo Anna Nitwa Afanikisha Ukarabati wa Choo cha Wodi ya Kinamama Wanaojifungua Watoto Njiti Hospitali ya Dodoma

$
0
0
 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

Mrembo huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba 1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali ili kuweza kukarabati.

Aliendelea kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.

Kwa Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana. 

Kwa upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini hapo.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma 2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

Rais wa Zanzibar Dk Shein, Afungua Kongamano la Wajasiriamali.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja,kuzindua Kongamano la Wajasiriamali sambamba na maonesho ya wajasiria mali wa vikundi mbali mbali na taasisi za Serikali  leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali   katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Meneja wa Tawi la DTB hapa Zanzibar Mbarouk  Ramadhan Mbarouk katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar   katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Ofisa wa Taasisi ya 'Mchele Z'bar Foundation' hapa Zanzibar Eshe Haji Ramadhan  katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar   katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja. 
Mratibu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Afwa Mohamed akitoa hutuba fupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar   katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo,ambalo lilizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Wajasiriamali wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali hao lililofanyika  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo
Baadhi ya Wajasiriamali wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali hao lililofanyika  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo.
 Baadhi ya mabanda ya maonesho ya Wajasiriamali katika viwanja vya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea leo kabla ya kuzindua Kongamano la Wajasiriamali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya wajasiriamali wa Vikundi mbali mbali leo akiwa na Waziri wa Kazi Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watotio Mh,Moudline Cyrus Castico(kushoto) kabla ya kuzindua Kongamano la Wajasiriamali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya wajasiriamali wa Vikundi mbali mbali leo kabla ya kuzindua Kongamano la Wajasiriamali.
,[Picha na Ikulu.] 03/12/2016.​

Ligi Kuu ya Zanzibar Taifa ya Jangombe na Kijichi Mchezo Uliofanyika Amaan Timu ya Taifa ya Jangombe Imeshinda Bao 1--0.

$
0
0
Wachezaji w Timu ya Kijichi wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe kabla ya kuaza kwa Mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika jana usiku uwanja wa amaan, Timu ya Taifa ya Jangombe imeshanda mchezo huo kwa bao. 1--0.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakiomba dua kabla ya mchezo wao na Timu ya Kijichi mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Timu ya Taifa ya Jangombe imeshinda bao 1--0.























Jengo la mahakama Mkoani Pemba lipo katika hali mbaya

$
0
0


Na Haji Nassor, Pemba
UONGOZI wa mahakama ya wilaya ya Mkoani Pemba, umeiomba serikali kuangalia uwezekano wa kulihami haraka jengo la mahakama hiyo, kutokana na kuvuja baadhi ya maeneo na kuwapa usumbufu wafanyakazi wakati mvua inaponyesha.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu, hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Nassor Suleiman, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, kwa Naibu waziri wa wizara nchi afisi ya rais, Katiba, sheria utumishi wa umma na utawala bora, alipofika hapo na jumbe wake, ikiwa ni sehemu za ziara yake ya siku mbili kisiwani Pemba.

Alisema kuvuja kwa jengo hilo, wakati wakiwa kazini huwapa mashaka ya kuhama hama na kusababisha kusita kwa kazi, kutokana na kukimbia maji kwa baadhi ya mapaa ya mahakama hiyo.

Hakimu huyo alisema, ingawa lipo paa walipata msaada wa kuezekewa na Baraza la mji Mkoani, wakati wakifanya matengenezo ofisi yao, lakini kwa yaliobakia yapo baadhi yanavunja na juhudi zinahitaji kuokolewa.

“Muheshimiwa Naibu waziri tumeshaona juhudi za serikali za kulifanyia matengenezo makubwa jengo letu la mahakama kuu Chakechake, lakini na hili la wilaya ya Mkoani, hali iko mbaya maana yapo mapaa yanavuja’’,alifafanua.

Aidha alisema changamoto nyengine inayowakumbuka wafanyakazai hao wa Idara ya mahakama Mkoani, ni ukosefu wa usafiri kutokana na kuwa na vespa moja pekee.

Akielezea changamoto nyengine inayowakabili, mfanyakazi wa mahakama hiyo Riziki Mohamed Makame, alisema wanapata ugumu wa kusambaa baruza za wito ‘smears’ kwa wahusika.

“Mahakama inapotoa barua za wito, inatubidi tutumie nauli zetu, na kumuomba mtuhumiwa au mlalamikaki ni kosa, sasa kama tukiwa na usafiri wetu, kazi itafanyika vyema.

Nae mfanyakazi Muhidin Mohamed Muhidin, amelalamika kutoingizwa kwenye orodha ya posho la shilingi 50,000 ingawa wenzao wa Unguja wameshaanza kupata.

Akilitolea ufafanuzi hilo, Afisa Utumishi wa wizara hiyo Chumu Khamis Omar, alisema lililojitokeza hadi wafanyakazi wa Pemba, kuchelewa kuingizwa kwenye posho hilo, ni kuchelewa kupewa taarifa kutoka makao makuu Unguja.

“Ni kweli wafanyakazi sasa kuna posho la mazingira magumo, kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 50,000, lakini kwa sisi wafanyakazi wa Pemba, tulichelewa maana taarifa zilichelewa kutufikia’’,alifafanua.

Mapema Naibu waziri wa nchi afisi ya rais Katiba, sheria Utumishi wa umma na utawala Bora Zanzibar, Khamis Juma Maalim, aliwapongeza wafanyakazi hao licha ya changamoto zinawazowakabili.

Kwa upande wake Naibu Mrajisi wa Mahakamu kuu Zanzibra Ali Ameir, alisema kutokana na changamoto zinazowakabili wafanayakazi hao, na kufanikiwa kufanya kazi, ile dhana ya hapa kazi imewadia.

Ujumbe huo wa Idara ya mahakama ikiambatana na Naibu waziri wa wizara hiyo, wamekamilisha ziara ya siku mbili kisiwani Pemba, ambapo walitembelea jengo la mahakama kuu Chakechake lililofanyiwa ukarabati, mahakama za Konde, Wete, Kengeja na Mkoani.

Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk: Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa jengo la mahakama kuu Chakechake lililofanyiwa matengenezo makubwa.

Rais Dk Shein atembelea kijiji cha Mgonjoni Kaskazini Unguja

Rais Dk Shein alipofungua kongamano la wajasiriamali

Turkish Airlines launches flights to Zanzibar

$
0
0


Already flying to 49 destinations in Africa, following the recent addition of Seychelles, Turkish Airlines is adding Zanzibar to its extensive flight network from December 13, 2016. This brings to 293 the total number of destinations that Europe’s Best Airline serves worldwide, and raise to 50 destinations in 31 African countries.

Turkish Airlines, the world’s 4th largest flight network that flies to more countries than any other airline, will now serve 244 international destinations- with the addition of Zanzibar which is best known for spices. Users of the airline will now enjoy great experiences with the new routes that include 20 wonderful city-destinations around the world such as Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, India, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, and Prague.

The first flight will be operated on Tuesday, 13 December and passengers will depart from Istanbul at 00:30 on board TK567 arriving at 09:30, with a return service on TK567 departing from Zanzibar at 10:25 to arrive in Istanbul at 17:45.

Wanancnhi watakiwa kuzitathmini skuli zao za karibu

$
0
0
Na Salmin Juma, Pemba

Wananchi wa wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba wametakiwa kuzijali na kuzithamini skuli za karibu yao badala ya kukimbilia kuwapeleka  watoto wao skuli za mbali  na zinazotoza ada kubwa za kusomeshea na gharama nyenginezo wakati skuli za karibu zipo na ubora wake ni sawa au umepindukia huko.

Hayo yamesemwa leo na mgeni rasmi wa katika  ya sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la sita  wa skuli  ya Akhalil English Medium school iliyopo Mtoni chakechake Pemba  sheikh Zahor Saleh Omar ambae ni katibu mkuu wa Zanzibar Children Fund (ZCF) na mkurugenzi wa skuli hiyo.

Kwa kulithibitisha hilo Sheikh Zahor amesema skuli hiyo imeshika nafasi ya tatu katika ya skuli zisizopungua ishirini na tano kiwilaya na kusema kua hiyo ni dalili tosha ya kuonesha  kua skuli ya Alkhalil ni bora na inayohitaji kuungwa mkono na wazazi na jamii kwa ujumla kwa kuwapeleka watoto katika skuli hiyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa kamati ya wazazi wa skuli ya Alkhalil Hafidh Mbarouk amesema wazazi na walezi wa watoto hakuna budi jumuku la malezi kulibeba kwa pmoja ili kujua maendeleo ya mtoto, ambapo amesema kua katika hali ya kawaida watoto muda mwingi huwa katika mikono ya wali, hivyo wazazi kujiona kua ndio wameshamaliza kazi

“Kuanzia asubuhi mtoto wako anakua skuli na akirudi anapumzika muda mfupi tu kisha anakwenda madrasa sasa muda mwingi anakua mikononi mwa mwalimu, hivyo wazee musiitumie fursa hiyo kama ndio mumeshamaliza kazi badala yake pia mutoe mashirikiano ya dhati kwa walimu kufanikisha ulezi wa watoto”alisema Mbarouk.

Haya ni mahafali ya nane kufanyika, Skuli ya Alkhalil inafundisha watoto katika ngazi ya Nursery hadi darasa la sita, inawalimubora wenye uzoefu wa hali ya juu. 

Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu kitaifa yafanyika Micheweni , Pemba

$
0
0
 Watu wenye Ulemavu wakiwa na mabango katika maandamano ya maadhimisho ya siku ya Watu wenye ulemavu Duniani yaliofanyika huko Micheweni Pemba.
 Waziri wanchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Moh'd Aboud Moh'd, akipokea maandamano ya watu wenye Ulemavu katika maadhimisho ya siku ya Waleamvu Duniani yaliofanyika huko Micheweni Pemba kwa Zanzibar.
 Watu wenye Ulemavu wakiwa na mabango katika maandamano ya maadhimisho ya siku ya Watu wenye ulemavu Duniani yaliofanyika huko Micheweni Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Wa Zanzibar, Moh'd Aboud Moh'd, akihutubiwa Wananchi mbali mbali na Watu wenye Ulemavu katika madhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu kitaifa iliofanyika huko

Micheweni Pemba.  Picha na Habiba Zarali, Pemba

WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko azungumza na wanahabari baada ya kutembelea vikundi vya wajasiriamali kisiwani Pemba

$
0
0
 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salim Ali, akiangalia aina maalumu za karafuu za Organic ambazo ziko tafauti na karafuu za kawaida, Organic huzwa pishi 17500 na karafuu za kawaida bei 14000, wakati alipotembelea vikundi vya wachumaji wa karafuu hizo huko Bagamoyo na Daya Mtambwe Wilaya ya Wete.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salim Ali, akionyesha aina mbali mbali za Viungo vinavyolimwa na wajasiriamali wa Bagamoyo na Daya Mtambwe Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salim Ali, akiwaonyesha waandishi wa habari bidhaa ya Vanilla, bidhaa ambayo ni ghali sana, huku ikiendelea kulimwa na kikundi cha Mataka Spices Kilichoko Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe:Balozi Amina Salim Ali, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali Pemba, mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Kisiwani Pemba, juu ya kutembelea vikundi mbali mbali vya wajasiriamali Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Ujenzi wa Jumba la Treni Darajani Waanza Maandalizi Yake Unaofanywa nma Kampuni ya Kichina.

$
0
0
Maandalizi ya Ujenzi wa Jengo la Darajani Maarufu kwa jina la jumba la treni tayari maandalizi ya ujenzi huo yameanza baada ya kupatikana mkandarasi wa ujenzi huo. 

Jengo hilo liko chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kulifanyia matengenezo makubwa na kulifanya la kisasa na kuwa na maduka ya kileo.

Ujenzi huo unafanywa na kampuni ya ujenzi ya kichina.

Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi Kutumia Mapato Yake Kusaidia Jamii Wodi ya Wazazi na Watoto Hospitali ya Makunduchi Zanzibar.

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe Haroun Ali Suleiman akikabidhiwa Dawa na Vifaa vyengine na Kiongozi wa Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi ikiwa mchango wao kwa Jamii kusaidia Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Makunduchi Unguja ikiwa ni pato lao la kuunganisha Umeme wa nguvu ya jua Solar, Mafunzo ya kutengenmeza Umeme wa Jua wameipata Nchini India na kuendeleza utaalam huo kwa kuwaungia wananchi wa kijiji cha makunduchi na vijiji vya jirani kwa harama ndogo. Vifaa hivyo na Dawa vikiwa na gharama ya shilingi milioni moja. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali ya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.   
Mwakilishi wea Jimbo la Makunduchi Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman wakiwa katika picha ya pamoja na Wanawaki wa Kikundi hicho cha Solar ,Makunduchi. 
Wanawake wa Kikundi cha Solar Makunduchi wakiwa katika wodi ya Wazazi na Watoto wakigawa Maji na Biskuti ikiwa ni mchango wao kwa Jamiii na kuchangia dawa zenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Wananchi wa Kijiji cha makunduchi ikiwa ni jitihada zao za elimu waliopata Nchini India ya kutengeneza Umeme kwa kutumia nguvu ya jua Solar. Hutowa huduma hiyo kwa kuwaunganishia umeme wananchi wa makunduchi kwa gharama ndogo ya shilingi elfu sita na kuchangia kila mwezi.



TIB Corporate Bank Yatoa Shs.Milioni 20 Kuwasaidia Vijana Jijini Arusha.

$
0
0


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa(kushoto)akipokea mfano wa hundi wenye thamani ya Sh 20 milioni kutoka kwa Meneja wa TIB Corperate Bank Limited tawi la Arusha,Juliana Mwansuva(kulia)ukiwa ni mchango wa benki hiyo kwaajili ya kununua Pikipiki ambazo Waziri Mkuu amezikabidhi leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corperate Bank,Frank Nyabundege na Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe.

Meneja wa TIB Corperate Bank Limited tawi la Arusha,Juliana Mwansuva(kulia)akipongezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo baada ya kumkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa(kushoto) mfano wa hundi wenye thamani ya Sh 20 milioni kwaajili ya kununua Pikipiki .

Baadhi ya walionufaika na Pikipiki zilizotolewa na Waziri Mkuu ambazo zilichangiwa na wadau mbalimbali mkoani Arusha,mradi huo utawawezeha vijana kurejesha fedha zenye thamani ya Pikipiki kisha kuwa wamiliki halali.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo wakizungumza na mmoja wa watu wenye ulemavu walionufaika na msaada wa Pikipiki leo

Pikipiki mpya zaidi ya 200 zenye thamani ya Sh 400 milioni zilizotolewa kwa vijana jijini Arusha leo katika ziara ya Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com Arusha.

TAARIFA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KWA UMMA TAREHE 4/12/2016, DAR ES SALAAM.

$
0
0

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008.  Kinapenda kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.

Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya NMB na wadhamini wengine unatarajia kuanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa siku mbili mfululizo.

Katika mkutano huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine. 

Aidha katika mkusanyiko huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana Blogu. 

Mkutano huu ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.

TBN inaendelea kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake.

Lakini kwa namna ya pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF, NHIF, SBL, na Coca Cola kwa kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya. 

Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii. 

TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii. 


Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
0756469470
Viewing all 35936 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>