Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36103 articles
Browse latest View live

Wanachama ‘tufaane’ wakopa sh/= 239 milion

$
0
0
Na.Haji Nassor  PEMBA
WANACHAMA 135 wa ushirika wa ‘tufaane saving and credit’ wa wizara ya ardhi, makaazi, maji na nishati Pemba, wameshakopeshwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 239, hadi kufikia mwezi disemba mwaka 2014 kwa wanachama wake.
Kati ya fedha hizo shilingi milioni 122.5 tayari zimesharejeshwa na wakopaji, wakati shilingi milioni 150.3 bado ziko mikononi mwa wanachama, wakiendelea kurejesha taratibu.
Akisoma risala ya ushirika huo, kwenye mkutano mkuu uliofanyika ofisi ya mamlaka ya maji ‘ZAWA’ Machomane Chakechake, Katibu Khamis Hamad Hassan, alisema hayo ni miongoni mwa matunda ya uhsirika wao.
Alieleza kuwa, pia ushirika umefanikiwa kukopesha shilingi zaidi ya milioni 6.5 kama mikopo ya dharura na shilingi milioni 143.8 mikopo ya kawaida miongoni mwa wanachama.
Katib huyo alifafanua kuwa, iwapo wanachama waliochukua mikopo hiyo wameekeza kwenye mitaji mbali mbali, itakuwa wameshapiga hatua ya kimaendeleo.
“Ushirika wetu umefikia pahala pazuri, maana wapo wanachama 135 hadi kufikia mwaka juzi, wameshachukua mikopo, na ndio miongoni mwa malengo yetu’’,alifafanua.
Akifungua mkutano huo Katibu tawala wilaya ya Chakechake Abdalla Rashid Abdalla, aliwashauri wanachama hao kuwa makini wanapochukua mikopo, ili faida ya kukopa kwao ionekane.
Alieleza kuwa, wapo wanachama katika vyama vyengine vya ushirika, wamekuwa wakikopa fedha na kisha kujinunulia chakula badala kuanzisha mitaji yenye thamani.
Katika hatua nyengine, Katibu huyo Tawala aliwasisitiza wanachama wa ushirika huo, kuendelea kutoa michango na ada zao, wakiamini kwa njia hiyo inaweza kukuza ushirika wao.
Afisa ushirika Yussuf Seif Yussuf, alisema lazima uongozi wa ushirika huo, ujiwekee malengo ya kutoa mikopo mikubwa kwa njia ya kuongeza hisa za wanachama.
Mshika fedha wa ushirika huo Juma Ali Juma, alisema kiujumla ushirika huo, umepiga hatua ya kimaendeleo na ndio maana, umefikia kutoa hadi mikopo yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 239.

Ushirika wa ‘Tufaane saving and credit’ ambao umeanzishwa mwaka 1992, ukiwa na waanchama 45 na sasa ukiwa na wanchama 201, bado unaendelea kukumbwa na changamoto ya uhaba wa mitaji.

MGODI WA ACACIA BULYANHULU WALIPA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1 YA USHURU WA HUDUMA HALMASHAURI YA MSALALA NA NYANG'WALE

$
0
0


Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umekabidhi hundi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga na halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.


Hafla fupi ya kukabidhi hundi hizo imefanyika Alhamis Machi 2,2017,katika ukumbi wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama na kuhudhuriwa na viongozi wa halmashauri na mikoa ya Shinyanga na Geita pamoja na viongozi mbalimbali kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu. 


Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew alisema fedha hizo ni malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2016. 
Alisema fedha hizo ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma ya mgodi huo kwa kipindi cha miezi sita katika awamu ya pili kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2016. 
“Mgodi umelipa shilingi za kitanzania 1,135,178,526/= na malipo hayo yamegawanyika katika halmashauri mbili kwa mujibu wa makubaliano na serikali ambapo halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 760 sawa na asilimia 67 na Nyang’wale shilingi milioni 374 sawa na asilimia 33”,alisema Crew. 
Aidha alisema mpaka sasa mgodi huo umelipa jumla ya shilingi bilioni 4.3 tangu mwaka 2014 kampuni ya Acacia ilipoanza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika. 
“Katika kipindi cha miaka hiyo minne halmashauri ya Msalala imelipwa zaidi ya shilingi bilioni 3.7 na Nyang’wale imelipwa shilingi bilioni 1.1”,aliongeza Crew. 
Katika hatua nyingine Crew alisema mgodi huo unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo ili kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma endelevu za kijamii na miundombinu katika jamii hususani katika elimu,barabara,umeme,maji na huduma za afya.
Wakipokea hundi hizo,mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela waliushukuru mgodi huo kwa kutimiza wajibu wa kulipa kodi na kuongeza kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri za Msalala na Nyang'wale.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa hafla hiyo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri,tazama hapa chini 
Wa pili kutoka kulia ni Mtaalamu wa Mawasiliano Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Mary Lupamba akiwakaribisha viongozi wa mkoa wa Shinyanga na Geita wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Msalala na Nyang’wale.Wa kwanza kushoto ni Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew,akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela 
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akiangalia hundi ya shilingi milioni 374 kabla ya kuikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa ajili ya halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale .Kushoto ni Kiongozi wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Teri 
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 374 kwa mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma ya mgodi kwa halmashauri ya Nyang'hwale iliyopo mkoani Geita 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni 374 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga na halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita. Alisema halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 760, Nyang’wale shilingi milioni 374 
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akikabidhi hundi hiyo ya shilingi milioni 374 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Carlos Gwamagobe 
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni 374 kwa ajili ya halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale ambapo alisema fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri hiyo 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Carlos Gwamagobe (kulia) akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama akishikana mkono na Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 374 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 760 kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma ya mgodi kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga. Katikati ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi milioni 760 kwa ajili ya halmashauri ya wilaya ya Msalala iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo ambapo alisema halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 760 sawa na asilimia 67 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ya hundi ya shilingi milioni 760 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige 
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 760 ambapo alisema aliushukuru mgodi huo wa malipo ya ushuru na kuongeza kuwa tayari fedha hizo zimeshaingizwa kwenye bajeti ya halmashauri ya Msalala kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri hiyo. 
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na Mweka hazina  halmashauri ya Msalala Masatu Mnyolo aliyemwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala wakati wa kukabidhi hundi hiyo 
Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambapo aliuomba mgodi huo kuendelea kulipa kodi kama inavyostahili huku akiomba mgodi kuyabana makampuni yanayofanya kazi zake mgodini ili yalipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya Msalala 
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambapo alisema Acacia imetimiza wajibu wa kulipa ushuru na kufanya tukio la kukabidhi hundi hizo kwa uwazi zaidi ili kuepuka minong'ono kuwa pengine mgodi huwa haulipi kodi 
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kodi iliyolipwa imetokana na uzalishaji wa mgodi kwa kipindi cha miezi sita na hiyo ni awamu ya pili,utaratibu wa Acacia ni kulipa kwa miezi 6 na tayari awamu ya kwanza walishalipa na sasa wamemalizia kipindi cha pili katika mwaka 2016 
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kampuni ya Acacia imekuwa ikifanya kazi zake kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka migodi yao
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akishikana mkono na mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akiagana na katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Wakulima wa Kilimo cha Mbogamboga Wametakiwa Kuzalisha Zaidi Bidhaa Hizo.

$
0
0
Na.Haji Nassor Pemba.
Wakulima wa mboga mboga na migomba kisiwani Pemba, wametakiwa kuvitumia vifaa vya umwagiliaji wa matone walivyokabidhiwa na serikali, kwa lengo la kuongeza uzalishaji ili watunishe pato lao.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, Mifugo, Maliasili na Uvuvi Zanzibar kwa niaba yake, wakati Mkuu wa Mradi wa kuimarisha Kilimo na Ufugaji ASSP, dk Talib Saleh Suleiman akizungumza na wanavikundi hao mjini Chakechake.
Mkuu huyo wa program ya ASSP, alisema kwa wanavikundi hao vya mboga mboga na mtu mmoja mmoja, lazima kuwe na tofauti kabla na baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.
Alisema, vifaa hivyo vya umwagiliaji kwa njia ya matone, kama wakiyatumia vyema, anaamini uzalishaji wao utapanda sambamba na pato lao.
Dk Talib alisema, walipokea maombi ya wananchi kadhaa wanaohitaji mipira na matangi ya kuhifadhia maji kwa ajili ya kuimarisha kilimo chao, hivyo kwa hao waliobahatika, lazima wazingatie kuwa kilimo bora.
“Leo tunawakabidhi matangi na mipira maalumu kwa ajili ya kuendeleza kilimo chenu cha mboga mboga, sasa sisi tunachosubiri ni kuona mnaongeza pato lenu, ili kupunguza umaskini’’,alisema.
Aidha dk Talib, alieleza kuwa baada muda mfupi atatuma maofisa wao, kuwakagua na ikitokeza yupo mkulima au kikundi wanasita sita kwenye kazi zao, watapaswa kuyarejesha.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo wa ASSP-ASDP-L Pemba Asha Omar Faki, alisema kilimo cha mboga mboga na migomba, kinaweza kuwakombo wakulima pindi wakipatiwa vifaa kama hivyo.
“Sisi kama watu wa kuimarisha kilimo na ufugaji, tunaamini sana kuwa, wakulima wakikabidhiwa vitenda kazi kama mipira ya maji na matangi ya kuhifadhia maji, wanaweza kuukimbia umaskini’’,alifafanua.
Hata hivyo alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi yalivyojitokeza na kuwaathiri wakulima hasa wanaotegemea mvua, ndio maana serikali kupitia wizara yake ya kilimo ikakabidhi vifaa hivyo.
Wakulima mmoja mmoja waliokabidhiwa vifaa hivyo, kwa wilaya ya Wete ni Msanifu Ali Faki alipewa mipira ya maji ya matone seti mbili na tanki la maji lenye ujazo wa lita 1000.
Wengine Salim Kombo Hamad seti mbili za mipira, Kombo Hamad Yussuf seti mbili za mipira, Mohamed Rashid Ali tanki la lita 1000 na mipira seti mbili, wakati kwa wilaya ya Mkoani ni Salim Hamad Mohamed (seti mbili mipira), Said Omar Mohamed tanki la lita 5000, Issa Mohamed Ussi tanki la lita 1000, mipira seti mbili.
Kwa wilaya ya Micheweni ni ushirika wa ‘tujali wakati’ seti mbili za mipira, ushirika wa ‘vikunguni’ mipira seti mbili, wakati kwa wilaya ya Chakechake ni Rashid Salum mipira seti mbili, ushirika wa ‘mwisho wa ubaya’ tanki la lita 5,000 na mipira yake, mkulima Khamis Juma Kheir takini la lita 1,000 na mipira.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Tibina Issa Maligha kutoka Kiwani, alisema watahakikisha vifaa walivyokabidhiwa vinaongeza pato lao.
Hata hivyo walisema, bado wapo wenzao kadhaa wanahitaji vifaa kama hivyo, kutokana na mashamba yao kukauka na kuhatarisha vilimo vyao.

Wizara ya Kilimo, Mifugo, Maliasili na Uvuvi imeshatumia zaidi ya shilingi milioni 130 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya mipira ya maji ya umwagiliaji kwa njia ya matone, matangi (simtank) kwa ajili ya wakulima mmoja mmoja na vikundi vilivyowekeza kwenye kilimo.

Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma Akabidhi Uwanja wa Mao Kwa Wajenzi wa Uwanja Huo Kuanza Mradi Huo.

$
0
0
Mchoro wa Uwanja wa Kisasa wa Mao Zanzibar kama unavyoonekana katika picha hiyo jinsi utakavyokuwa baada ya ujenzi wake utachukua miezi 14 hadi kukamilika kwake unaofanywa na Kampuni ya Kichina. 
Hili ndilo eneo la uwanja wa Mao Zanzibar lililokuwa na uwanja miwili wa mpira wa miguu na mpira wa hoki kwa wale waliokuwa na kumbukumbu ya uwanja huu wataufahamu ulivyokuwa kabla ya kuvunjwa kwa majenzo yaliokuweko ndani ya uwanja huu.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akimkabidhi hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Mao kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi wa Mradi huo Ligen Zhang, kutoka China Kampuni ya Zhengtal Group Limeted hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya uwanja huo Mao Tse Tung Zanzibar leo.akishuhudia Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Ndg Omar Hassan King katikati.  
Waziri wa habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe Rashid Ali Juma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi uwanja huo kwa Mkandarasi leo katika viwanja vya mao.
Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na MichezoNdg Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya uwanja huo utakavyokuwa katika kukamilika kwa Mradi wa Ujenzi huo wa Uwanja wa Kisasa na  wa aina yake kwa Zanzibar na Afrika Mashariki. utakuwa wa mfano.  

Kijana Paul Mwilombwa Mlemavu wa Viungo Anaomba Msaada Wako Ili Aweze Kutimiza Malengo Yake Kupitia Shughuli Anayoifanya.

$
0
0
Ndg.Paul Ibrahim Mwilombwa ni Kijana anayeishi Mkoa wa Geita Wilaya ya Chato, ni mlemavu wa viungo na mwenye kujishughulisha na maswala ya upigaji picha na mambo ya 'Graphic Design'.  hapa anaelezea historia yake na kuwaomba msaada watanzania ili apate kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Ziara yaNaibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Kisiwani Pemba.

$
0
0
 
NAIBU katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Mhez:Abdullghafar Idrisa Juma, akimkabidhi bati muwasisi wa CCM Michakweni Kiwani, Amina Juma Heri ili kumaliza ujenzi wa nyumba yake, wakati alipotembelea nyumba ya mwana CCM huyo
NAIBU katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Mhez:Abdullghafar Idrisa Juma, akimkabidhi bati muwasisi wa CCM Michakweni Kiwani, Amina Juma Heri ili kumaliza ujenzi wa nyumba yake, wakati alipotembelea nyumba ya mwana CCM huyo
NAIBU katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Mhe:Mhe:Abdullghafar Idrisa Juma, akishiriki Ujenzi katika Tawi la CCM Mkungu Kengeja, kwa kuweka Tufali na Udongo katika ziara yake ya siku nne Kisiwani Pemba


NAIBU katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Mhe:Abdullghafar Idrisa Juma, akizungumza na vijana wa CCM katika tawi la CCM lililopewa jina la Balozi Seif Ali Iddi, wakati alipowatembelea vijana hao katika ziara yake ya siku nne Kisiwani Pemba.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein Azungumza na Balozi wa Singapore Ikulu Zanzibar.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Balozi wa Singapore Tan Puay Hiang alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi wa Singapore katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Tan Puay Hiang alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,
[Picha na Ikulu,]

Wadau wa Elimu Waiunga Mkono Programu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Kwa Vijana na Wazee.

$
0
0
Na Ismail Ngayonga. Maelezo Dar es Salaam
RIPOTI ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya mwaka 2015 inaonyesha kuwa takribani watoto Milioni 58 wameshindwa kujiunga na shule na milioni 100  kati yao wameshindwa kuhitimu anagalau elimu ya msingi.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa ukosefu wa usawa katika elimu umeongezeka, huku watoto maskini na wale walioko kwenye mazingira magumu ndio wanaobeba mzigo mzito zaidi wa uwezekano wa kutokwenda shule, mara nne zaidi ya watoto matajiri zaidi duniani.

Aidha ripoti hiyo ya dunia ya ufuatiliaji wa Elimu kwa wote inaendelea kueleza kuwa ubora mdogo wa elimu ya msingi kuwa ni miongoni mwa ni changamoto zinazosababisha mamilioni ya watoto kuhitimu shule bila ujuzi wa msingi. 

Hadi kufikia mwaka 2015 Jumuiya ya Kimataifa na Serikali mbalimbali duniani zimekuwa mstari wa mbele zimekuwa mstari wa mbele katika kuyafikia makundi ya walio pembezoni na walio kwenye mazingira magumu, yasiyo­kika kirahisi na ambayo bado hayajanufaika na haki.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, mwaka 1992 Taasisi ya Elimu ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzisha programu ya Elimu ya Sekondari kwa vijana na watu wazima waliokosa nafasi ya kuendelea na elimu ya Sekondari kwa sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa takwimu za TEWW za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya vijana wa umri wa miaka 7-17 Milioni 3.5 waliopo nje ya shule, ambapo kati yao Milioni 2.5 wanahitaji elimu ya Sekondari na Milioni 1 wanahitaji Elimu ya msingi.

Naibu Mkurugenzi wa TEWW, Dkt. Kassimu Nihuka anasema tatizo la vijana na watu wazima waliokosa elimu ya sekondari ni kubwa sio kwa Tanzania pkee bali kwa nchi zote zilizopo katika ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara.

“Vijana wanaomaliza elimu ya msingi na kupata alama ufaulu chini ya 100 (kati ya 250) wamekuwa wakiachwa kwenda sekondari katika mikoa mbalimbali isipokuwa wale ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwapeleka shule za sekondari za binafsi ambazo gharama zake ni za juu” anasema Dkt. Nihuka.

Anaongeza kuwa programu iliyoanzishwa na TEWW imekusudia kuwawezesha wanafunzi waliomaliza darasa la saba ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari na wanahitaji kumaliza elimu hiyo.

Akifafanua zaidi Dkt. Nihuka anasema programu hiyo inaendeshwa katika majengo ya shule za msingi na sekondari za Serikali 83 na wadau 337 nchini, ambapo hadi kufikia sasa jumla ya vijana na watu wazima 95,140 wameweza kunufaika na masomo hayo kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.

Aidha Dkt. Nihuka anaongeza kuwa programu hiyo pia imewalenga wanafunzi ambao wamemaliza masomo ya MEMKWA (Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa) na wale waliomaliza masomo ya sekondari lakini hawakufanya vizuri na wangependa kurudia mtihani wa taifa wa kidato cha nne.

Kwa mujibu wa Dkt. Nihuka anasema kupitia programu hiyo, masomo hutolewa katika hatua kuu tatu ambazo ni pamoja na masomo ya kidato cha I na II, masomo ya kidato cha III na IV na hatua ya mwisho inabeba masomo ya kidato cha V na VI.

“Katika hatua ya kwanza, mlengwa anasoma kwa kipindi cha mwaka mmoja na hivyo kuwa na sifa ya kufanya mtihani wa maarifa, yapo masomo yanayotolewa katika hatua hii ni Historia, Jiografia, Kiingereza, Kiswahili, Hisabati, Biolojia na Uraia” anasema Dkt. Nihuka.

Dkt. Nihuka anasema mlengwa wa hatua ya pili anatakiwa kusoma kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo ataweza kuwa na sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha nne uliondaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Kuhusu hatua ya mwisho ya programu hiyo, Dkt. Nihuka anasema masomo mahsusi yanayotolewa katika tahasusi za HGL (Historia, Jiografia na Lugha), HKL (Historia, Kiswahili na Lugha), HGK (Historia, Jiografia na Kiswahili) pamoja na HE (Historia, Jiografia na Uchumi), na mlengwa katika hatua hiyo anaweza kusoma kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi pale atakapokuwa amejindaa vya kutosha kufanya mtihani wa maarifa au ule wa NECTA.

Anaongeza kuwa masomo hayo yanatolewa kupitia mafunzo ya ana kwa wakati wa jioni kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni, ambapo mlengwa ataweza kujisomea moduli na vitabu na matumizi ya teknolojia za kujifunzia kama vile elimu mtandao kupitia machapisho huria ya kielimu.

Kuhusu gharama za masomo hayo, Dkt. Nihuka anasema viwango vya ada vinavyotozwa na TEWW katika elimu ya sekondari hutofautiana na vituo vinavyoendeshwa na wadau, ambapo kwa upande wa TEWW gharama za ada ni kati ya Tsh 150,000/- hadi 300,000 kutegemeana na mkoa husika na gharama zilizowekwa kwa mwaka.

Elimu na mafunzo bora ni mkakati wa kipaumbele kufikia malengo ya mipango ya maendeleo yaliyowekwa, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) pamoja na malengo ya Milenia vinaweka wazi umuhimu wa elimu  na mafunzo katika kufikia malengo ya mipango hiyo. 

Ni wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka vijana wao waliokosa alama za ufaulu katika mitihani wa darasa la saba kutumia fursa ya TEWW ili kuwawezesha kupata elimu ya Sekondari.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Azungumza ba Mabalozi Walioteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Hivi Karibuni Kuiwakilisha Tanzania Nchi za Nje.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Dkt. Pindi anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya akiwaongoza Mabalozi wengine walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania Nchi za Nje hivi karibuni wakiongozwa na Balozi Dkt. Pindi Kichana(wa pili kulia) anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kiwakilisha Tanzania Nchi za Nje hivi karibuni wakiongozwa na Balozi Dkt. Pindi Kichana(wa pili kulia) anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais,[Picha na Ikulu.] 03/03/2017

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Akutana na Balozi wa Singapore Ikulu Zanzibar na Mabalozi wa Tanzania Nchi za Nje.

$
0
0

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                                                          03.03.2017
---
SINGAROPE imeahidi kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza sekta za maendeleo hasa katika sekta ya utalii, pamoja na vipaumbele vyengine vilivyowekwa na Serikali ili Zanzibar izidi kuimarika kiuchumi.

Balozi wa Singapore nchini Tanzania  Tan Puay Hiang aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungunmzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.

Katika maelezo yake, Balozi Hiang alimueleza Dk. Shein  kuwa Singapore inathamini sana juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuziunga mkono hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar inalingana na Singapore kimazingira.

Balozi Hiang, alimuahidi Dk. Shein kuwa atakuwa Balozi mzuri wa kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii nchini mwake hasa kwa vile Singapore imepiga hatua kubwa katika sekta hiyo huku akiendelea kuahidi kuwa atahakikisha mashirikiano ya karibu katika kuimarisha sekta hiyo kwa pande mbili hizo yanaimarika.

Aidha, Balozi Hiang alisema kuwa nchi yake pia, itazidisha uhusiano na ushirikiano katika sekta ya usafirishaji, uwekezaji, afya na biashara pamoja na kubadilishana utaalamu hasa katika sekta ya afya na kuahidi kusaidia vipaumbele vilivyowekwa na Zanzibar.

Aliongeza kuwa nchi yake inaona haja na umuhimu wa kuwepo kwa mashirikiano katika kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa viongozi na wataalamu katika sekta ya afya na kuahidi kuwa Singapore italisiamaia hilo ili kukuza uhusiano mwema uliopo.

Sambamba na hayo, Balozi huyo alipongeza azma ya ujenzi wa Bandari mpya ya Mapigaduri unaofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kueleza kuwa hatua hiyo itazidisha ukuaji uchumi na maendeleo na kuahidi kutoa ushirikiano wake katika kufanikisha juhudi hizo hasa katika sekta hiyo ya miundombinu.

Nae Dk. Shein kwa upande wake alipongeza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Singapore na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa kipindi kirefu na kusisitiza kuwa Zanzibar itazidisha uhusiano na ushirikiano huo uliopo.

Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itautumia uzoefu wa Singapore katika kuimarisha sekta zake za maendeleo kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika uchumi wake ambao unatajika duniani.

Aidha, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuimarisha sekta zake za maendeleo hasa katika vipaumbele vilivyowekwa kwenye Dira ya 2020 na kuwepo kwa azma ya Singapore kuunga mkono vipaumbele hivyo kutazidisha kufikia malengo yaliowekwa.

Dk. Shein alieleza hatua zinazochukuliwa na serikali katika ujenzi wa Bandari mpya ya Mpigaduri pamoja na juhudi katika kuimarisha sekta ya utalii huku akisisitiza kuwa mafunzo na ubadilishanaji wa utaalamu na uzoefu kwa wataalamu na viongozi wa sekta ya afya ni jambo muhimu katika kuimarisha sekta hiyo.

Wakati huo huo, Dk. Shein amefanya mazungumzo na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, mazungumzo yaliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Miongoni mwa Mabalozi hao ni Balozi Pindi Chana anaekwenda nchini Kenya, Balozi Abdalla Kilima, anayekwenda nchini Oman, Balozi Joseph Sokoine anaekwenda Ubelgiji, Balozi Silima Kombo Haji anaekwenda Sudan, Balozi Fatma Rajab anaekwenda Qatar, Balozi Batilda Masuka anekwenda Jamhuri ya Korea na Balozi Grace Mgovano anekwenda nchini Uganda.

Akizungumzo na Mabalozi hao, Dk. Shein aliwapongeza kwa kupata uteuzi wao huo walioupata kutokana na sifa maalum walizonazo katika utendaji wao wa kazi na kujidhatiti kwenda kuutumikia huku akiwataka kutekeleza Diplomasia ya uchumi ambayo ndio mbinu kubwa kwa Tanzania ambayo itaongeza ari katika kufikia azma ya kuimarisha sekta ya viwanda.

Dk. Shein aliwasisitiza Mabalozi hao kutilia mkazo zaidi sekta za maendeleo kwa kuitangaza vyema Tanzania ikiwemo Zanzibar kutokana na sifa zake njema hasa katika sekta ya uwekezaji, utalii, uvuvi, viwanda, usafiri na usafirishaji, kilimo pamoja na mashirikiano ya vyuo vikuu  na hospitali kati ya nchi wanazokwenda kufanyakazi na  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nao Mabalozi hao walimuhakikishia Dk. Shein kuwa watakuwa mabalozi wema wa Tanzania katika nchi wanazokwenda na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa na Rais Dk. Shein.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Aili Iddi Aliahirisha Baraza la Wawakilishi leo

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafungua tena kazi za uchimbaji  mchanga kuanzia Jumatatu ya Tarehe 6 Machi 2017 ikilazimika kuchukuwa uamuzi mgumu wa kusimamia moja kwa moja uchimbaji huo badala ya kuwaachia Wananchi.

Alisema maamuzi hayo ya Serikali yatakwenda sambamba na utolewaji wa bei elekezi ya mchanga ili kujaribu kuzuia uharibifu wa mazingira uliokwishaathiri maeneo mengi yaliyokwishachimbwa mchanga pamoja naulanguzi wa kupita kiasi kwa wauzaji wa rasilmali hiyo.

Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wizara ya Kilimo itaandaa  zamu za kuchimba mchanga ili kupunguza msongamano wa gari zitakazokwenda katika maeneo ya Mchanga.

Alisema zamu hizo zitawapa fursa ya siku Tatu  kwa Wiki Wananchi wa kawaida kupata rasilmali hiyo ya Mchanga na Siku Mbili kwa Wiki zitazingatiwa kwa Makampuni na Taasisi  za Serikali  zilizopata vibali vya Ujenzi wakati Jumamosi na Jumapili zitakuwa siku za mapumziko.

Balozi Seif alisema utafiti unaendelea kufanywa na Kamati ya Wataalamu kwa kushirikiana na ile ya Mawaziri inayoshughulikia suala mchanga kujua kiwango cha mchanga kiliopo kwenye eneo la Kiwanda cha Sukari Pangatupu, Kichwele na maeneo mengi ili kubaini wingi wake  na endapo utafaa kwa matumizi ya ujenzi.

Alisema Zanzibar si nchi ya kwanza kuwa na upungufu wa mchanga ambapo ipo mifano ya uhaba wa rasilmali hiyo iliyokwishajitokeza katika baadhi ya nchi duniani kama vile Malaysia, Singapore, Phillipines na Tuvalu.

Balozi Seif alieleza kwamba upo ushahidi wa wazi uliothibitisha kuzama kwa Visiwa vodogo vidogo Vitano Nchini Phillipines kufuatia wimbi kubwa la uchimbaji wa mchanga kiholela pembezoni mwa fukwe zilizokuwa zimevizunguuka Visiwa hivyo.

Alifahamisha kwamba ushibiti huo wa rasilmali ya mchanga unaweza kupelekea Wananchi katika maeneo mbali mbali Nchini wakavamia fukwe kuchota mchanga. Hivyo aliziomba mamlaka zote kupiga marufuku uchotaji huo ili kujiepusha na majanga na kuangamiza Visiwa hivi.

Alitahadharisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake itatoa adhabu kali kwa mtu ye yote atakayekwenda kinyume dhidi ya agizo lililotolewa na Serikali kuhusu suala zima la uchimbaji wa Mchanga.

Balozi Seif aliwaomba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaporudi Majimboni kuwaelimisha Wananchi wao juu ya uhaba uliopo wa mchanga unaovikabili visiwa hivi.

Aliwashauri Wajumbe hao kuandaa utaratibu maalum wa kuwapangia Wananchi wao ziara mahsusi za kwenda kuangalia hali halisi ya uharibifu wa mazingira uliokwishafanyika katika maeneo yaliyochimbwa mchanga.

Alisema Serikali kupitia Wizara  ya Kilimo  kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi pamoja na Wiara ya Ujenzi,Mawasiliano na Ushafirishaji zitaandaa muongozi wa uingiza wa bidhaa za ujenzi ikiwemo mchanga, kokoto, kifusi na Mawe kutoka nje ya Zanzibar.

Alisema muongozo huo utakwenda sambamba na kufuatilia utaratibu uliotumika katika uuzaji wa maeneo ya Kilimo kwa ajili ya kuchimbwa mchanga ili kubaini kwa kina ujanja unaotumika kuyabadilisha matumizi ya maeneo ya Kilimo.

Akizungumzia vita dhidi ya Dawa za kulevya vilivyotangazwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alionya kwamba Zanzibar haitakua kimbilio la waendelezaji wa biashara hiyo haramu na badala yake itakuwa gereza lao.

Balozi Seif  alisema vita hivyo ni vya Nchi nzima ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar. Hivyo wale wanaofikiria kwamba vita hivyo ni kwa Tanzania Bara pekee wanaelezwa bayana kuwa wamepotea njia.

Alisema Takwimu kutoka Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya zinaonyesha kwamba mwaka 2016 jumla ya kesi 37 ziliripotiwa kwenye Mahakama za Unguja na Pemba na ni Mtu Mmoja tu ndie aliyetiwa hatiani.

Alieleza kwamba kutokana na Takwimu hizo inaonyesha  wazi ukubwa wa janga hilo hauendani na kasi za kuwakamata wanaoingiza dawa za kulevya nchini na kuwapa adhabu stahiki.

Balozi Seif  alisema janga la Dawa za kulevya linaweza kumalizika endapo jamii mitaani itakuwa tayari kushirikiana kwa kina na Jeshi la Polisi, vyombo vyengine vya ulinzi chini ya usimamizi wa Tume ya Uratibu wa Udhibiti wa Dawa za Kulevya.

Akigusia vita dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema bado lipo ongezeko kubwa la vitendo hivyo vinavyoshinda kutoa matunda mazuri yaliyokusudiwa.

Alisema takwimu za vitendo hivyo viovu zilizoripotiwa kuanzia mwezi Julai hadi Septemba Mwaka 2016 zinazonyesha jumla ya matukio 218 yamewasilishwa katika vyombo vinavyohusika Unguja na Pemba.

Balozi Seif alitahadharisha kwamba hali hiyo bado inatisha na kutoa ujumbe kuwa bado Jamii inahitaji kushirikiana kwa karibu kujaribu kutokomeza vitendo vya udhalilishaji vya Kijinsia hapa Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  kwa umahiri wao wa kujadili Miswada Mitatu na baadae kupitishwa na Baraza hilo.

Aliitaja Miswada hiyo kuwa ni Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Tume ya Uchaguzi nambari 9 ya Mwaka 1992, Mswada wa Sheria ya kufuta sheria ya Nembo nambari 1 ya mwaka 1985 na Sheria ya Bendera ya Zanzibar nambari 12 ya mwaka 2004 na kutunga sheria inayoweka masharti bora yanayohusiana na Bendera ya Zanzibar, Nembo ya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar na Wimbo wa Taifa wa Zanzibar ya Mwaka 2016 na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Mswada mwengine ni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sheria nambari 2 ya mwaka 2006.

Baraza la Wawakilishi lilipokea Ripoti 7 za Kamati za Kudumu za Baraza hilo ambazo ni Ripoti ya Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya mwaka 2016/2017, Ripoti ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala  ya Mwaka 2016/2017 na Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Mwaka 2016/2017.

Nyengine ni Ripoti ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ya Mwaka 2016/ 2017,  Ripoti ya Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari ya Mwaka 2016/2017,Ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Mwaka 2016/2017 pamoja na Ripoti ya Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti  Hesabu za Serikali na Mashirikia {PAC} ya Mwaka 2016/2017.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi halkadhalika pia walijadili Hoja Binafsi Mbili zilizoletwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mh. Mohammed Said {Dimwa} inayohusu Dawa za Kulevya na ile ya Mwakilishi wa Jimbo la Kiwengwa Mh. Asha Abdalla Mussa iliyohusu uimarishaji wa mfumo mzima wa Kisheria unaoshughulikia uendeshaji wa Kesi za udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.

Baraza la Wawakilishi Zanzibar  limeahirishwa hadi Jumatano ya Tarejea10 Mwezi Mei mwaka 2017.

Wananchi wa Mkoa Arusha Wajitokeza Kwa Kasi Kupitia Huduma ya Kupima Afya Zao Bure Katika Wiki ya Wanawake Duniani.

$
0
0
Baadhi ya wananchi  wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani  ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide intantament
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa  ,Ukimwi na mengineyo
Mmojawa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani  viwanja vya Sheikh Amri Abeid

Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha  ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure

zoezi hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100 wamejotokeza kupima afya zao   bure katika viwanja hivyo

Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi 

Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao  hivyo ni jambo zuri mno 

Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na  tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi  kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
Zoezi hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Ahutubia Wananchi wa Lindi leo

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi(Wakwanza kushoto), Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa pamoja na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi kuhusu masula mbalimbali ya mkoa huo pamoja na Taifa kwa ujumla.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

Wanafunzi Wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo Marekani Watembelea Chuo cha Afya na Sayansi za Tiba Mweni.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni  kubadilishana uzoefu.
Mwanafunzi Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar  wakati wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA Mbweni.
Wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA  wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhayo Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
Wanafunzi wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
Picha ya pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa na baadhi ya walimu  na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Aongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri Mjini Dodoma.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi cha Mawaziri alichokiitisha kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 3, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Rais Dkt Magufuli Atoa Miezi Minne Mradi wa Maji wa Ng’apa Mkoani Lindi Umekamilika Pia Akutana na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Katika Ikulu Ndogo ya Lindi.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta visingizio.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza kushoto ni Kiongozi wa Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi kutoka Nchini Afrika Kusini na Wakwanza kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro ambaye ni Mtanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi wa Wakurugenzi hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmoja wa Wakurugenzi wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo mkoani Lindi. 
Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.PICHA NA IKULU

MISA TANZANIA YAWAJENGEA UELEWA WANAHABARI KUHUSU HAKI ZA BINADAMU.

$
0
0
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, Marie Engel, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuandika habari juu ya Haki za Binadamu hususani za kiafya.
#BMGHabari

Mafunzo hayo ya siku mbili tangu jana, yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, yakilenga kuwajengea wanahabari uelewa juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 ili kuwasaidia katika utendaji wa majukumu yao bila kukinzana na sheria na kanuni hizo.

Pamoja na mambo mengine, washiriki wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) Tanzania, wamefundishwa sheria na taratibu za kuandika na kuripoti habari/ makala kuhusu haki za binadamu kwa kuangazia sekta ya afya juu ya habari na makala za magonjwa ya kuambukiza kama HIV/Ukimwi ambapo wameahidi kuifikisha elimu hiyo kwa wenzao na pia kuitumia vyema katika kuboresha utendaji kazi wao.
Wanahabari washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa mkufunzi Marie Engel, kutoka shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS nchini Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. Aliyesimama ni Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva.
Mwakilishi wa Metro Fm Mwanza, Alphonce Kapela, akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo kwa vitendo yakiendelea nje ya ukumbi
Hii inaitwa noa bongo, ukirushiwa mpira unaeleza ulichojifunza kwenye mafunzo hayo
Mafunzo nje ya ukumbi yakiendelea
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Wakili James Marenga, akisimamia zoezi hilo
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akiteta jambo na mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Marie Engel, kutoka shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS nchini Tanzania.
Picha ya pamoja, waandaaji wa mafunzo, wakufunzi wa mafunzo pamoja na washiriki wa mafunzo ambao ni wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu.

Vuai aiagiza CCM Wilaya ya Mjini kushuhgulikia kwa haraka mgogoro wa jimbo la Jango'mbe

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai Akizungumza na Watendaji, Viongozi na wafuasi wa chama hicho katika mwendelezo ya ziara ya kuimarisha uhai wa Chama kuelekea uchaguzi wa  taasisi hiyo na jumuiya zake Katika Jimbo la Jang’ombe iliyofanyika katika Tawi la Matarumbeta.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,  Nd. Vuai Ali Vuai ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Mjini kichama kichama  kufuatilia  sababu za kufukuzwa kwa Viongozi Wawili wa Jimbo la Jang’ombe na kutafuta na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo haraka kupitia miongozo na kanuni za Katiba ya Chama hicho.

Alisema  ina utaratibu wa kushughulikia migogoro ndani ya Chama na Jumuiya zake kwa ngazi mbali mbali kwa kufuata misingi ya Katiba hivyo ni lazima kasoro zinazojitokeza ndani ya taasisi hiyo ni lazima zitatuliwe kwa utaratibu uliowekwa  na sio matakwa binafsi ya baadhi ya Viongozi.

Vuai alisema kwa mujibu wa Kanuni za masuala ya Uongozi Kamati za Siasa za Majimbo hazina mamlaka ya kuwafukuza ama kuwaondosha katika nafasi za uongozi kwa ngazi za Majimbo badala yake wanatakiwa kufanya vikao vya kikatiba kuwajadili watu wanaotuhumiwa na kuwasilisha mapendekezo yao kwa ngazi ya wilaya  ili  ijadili na kuchukua hatua stahiki kwa kuzingatia taratibu za CCM.

Agizo hilo limetokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa viongozi wawili waliovuliwa nafasi za uongozi  katika Jimbo hilo kumueleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Nd. Vuai Ali Vuai kuwa wameonewa kwani wamefukuzwa wakiwa hawajui kosa linalowakabili na  bila kupewa nafasi za kujieleza.




Akitoa ufafanuzi juu ya Malalamiko hayo Naibu Katibu Mkuu huyo aliutaka uongozi wa Wilaya hiyo kufuatilia kwa kina mgogoro huo ili umalize bila kuathiri uongozi wa Jimbo hilo, na kuwasihi Viongozi, Watendaji na Wanachama kusoma Katiba ya CCM na kanuni za chama hicho kwa lengo la kujikumbusha mambo ya msingi yatakayosaidia kuepuka kasoro zisizokuwa za lazima.

“Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa kwa misingi ya kikatiba na maamuzi mbali mbali yanayofanyika yanafuata muongozo huo na kila ngazi imepewa majukumu yake kulingana na kanuni zetu hivyo nakukumbusheni kuwa viongozi tuwe makini kuhakikisha tunasoma kwa makini Katiba na Kanuni zinazotuongoza.

Lakini tusikubali kugawanyika kwa tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza kama changamoto ndani ya Chama chetu na tunaposhutumiana hadharani  tunavunja utaratibu unaotuongoza ndani ya taasisi yetu”, alisema Vuai na kusisitiza kuwa Umoja, Upendo na ushirikiano ndani ya jimbo hilo na CCM kwa ujumla ndio siri ya mafanikio.

Hata hivyo aliwambia wanachama hao kuwa mabadiliko ya kimuundo yanayofanyika ndani ya Taasisi hiyo yanalenga kujenga Chama chenye nguvu za kiuchumi utakaotokana na matumizi mazuri ya rasilimali zake kwa maslahi ya wanachama wote.

Kupitia ziara hiyo aliwakumbusha viongozi na watendaji wa Chama hicho kusimamia vizuri miradi ya CCM  ili isaidie shughuli za kiutendaji na kuwanufaisha wanachama wote badala ya watu wachache.

Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini, Nd.  Juma Fakih Choum alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa baada ya kupata malalamiko ya kufukuzwa kwa viongozi hao Wilaya hiyo ilichukua hatua za kuuagiza uongozi wa jimbo kukutana pamoja katika kikao ili wajadiliane na kutafuta ufumbuzi wa kumaliza mzozo huo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema ndani ya Wilaya hiyo wamejiandaa kikamilifu kushiriki katika uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake ili kupata viongozi na watendaji imara wa ngazi mbali mbali watakaoweza kusimamia mikakati ya ushindi mwaka 2020.

ZECO waahidi kukamilisha wakati ufungaji umeme Fundo

$
0
0
Na Mwandishi wetu

Zoezi la usambazaji wa nguvu ya umeme katika Kisiwa cha FUNDO linaendelea kwa kasi huku uongozi wa shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ukiahidi kulikamisha kwa wakati.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia maendeleo ya zoezi hilo afisa uhusiano wa ZECO Pemba Amour Salim Massoud amesema tayari wameshafunga trasfoma nne na kujenga line kubwa na kwasasa wanalenga kujenga line ndogo kwa ajili ya kuwashushia wananchi.

Amesema mafundi wa shirika kwa kushikiana na wananchi wa Fundo wamekuwa wakifanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha zoezi hilo linamalizika kwa muda uliopangwa.

Nao baadhi ya wananchi wa fundo wameelezea kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na kuwaomba mafundi wa shirika la umeme ZECO kujitahidi kukamilisha uwekaji wa line hizo ili waanze kukamilisha usajili na kujiungia huduma hiyo ya umeme.

Aidha wameuomba uongozi wa ZECO kutoa elimu kwa wananchi wa FUNDO juu ya matumizi salama ya umeme na kuepuka ajali zisizo za lazima.

WanaCCM wasiwe na hofu ya kuwepo mabadiliko katika mfumo wa serikali

$
0
0
Na Muhammed Khamis

Wanachama wa chama cha mapinduzi CCM  visiwani Zanzibar wametolewa  hofu ya kutokuwepo aina yoyote ile ya mabadiliko katika mfumo wa Serikali.

Kauli hio imetolewa na makamo wa pili wa Rais Zanzibar ,Balozi Seif Ali Iddi wakati  akiwahutubia wajumbe wa baraza  la wawakilishi wakati wa ufungaji wa kikao cha tano cha baraza hilo.

Alisema wanaoendelea kusema taarifa zisizokuwa na ukweli kupitia mitandao  wataendelea kufanya hivyo huku Serikali ikiendelea na shughuli zake kama kawaida .

Balozi alisema kuwa kiongozi wa chama cha upinzani ( CUF) Maalim Seif hana uwezo wa kuwa Rais wa wananchi wa Zanzibar na ndio maana amekuwa akishindwa katika chaguzi zote tokea mwaka 1995.
‘’’Serikali hii itaendelea kuwepo mpaka mwaka 2020 msitishwe na mtu yeyote, yule Maalim Seif hana ubavu hata huo uchaguzi mwengine ukifika hataweza kushinda na kamwe Serikali hii haitatoka mikononi mwa chama cha mapinduzi’’alisema Balazi Seif.

Alieleza kuwa kinachoendelea kufanywa ni ''propaganda'' za kisiasa ili wananchi wao waendelee kuwaamini na kuwepo kwa mabadiliko jambo ambalo kiuhalisia halina ukweli wa aina yoyote hile.

Katika jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar Balozi alisema Serikali kwa sasa wanaendelea na jitihada mbali mbali kuwaletea maendeleo wananchi wote bila ya ubaguzi.

Pamoja na hayo kiongozi huyo aligusia uwepo wa changamoto kubwa visiwani Zanzibar ya rasilimali ya mchanga kutokana na kuadimika kwa kiasi kikubwa bidhaa hio.

Alieleza kuwa lengo la serikali sio kuwatesa wanachi lakini ifike wakati kila mmoja wetu kukubali ukweli kuwa mchanga visiwani hapa unakaribia kumalizika.

Katika kukabiliana na hilo tayari Serikali imeunda tume ya watalamu kufanya utafiti na hatimae kushauri njia na maeneo gani yanafaa kuchimba mchanga.

Aidha alieleza kuwa baada ya utafiti huo kufanyika na kwa sasa tayari serikali itazindua rasmi mashimo yanayopaswa kuvunwa kwa mchanga pamoja na kutoa bei elekezi ili kuzuia ulanguzi kwa wananchi.

Akiendelea kufafanua zaidi  kiongozi huyo alisema kuwa wameamua kuchukua jitihada hizo ili kuzuia athari  ambazo zingeweza kujitokeza iwapo rasilimali hio ingendelea kuchimbwa bila ya udhibiti.

Sambamba na hayo alisema Serikali haitolipa fidia maeneo yoyote yale ambayo yatalazimika kuchimbwa kwa mchanga kwa ajili ya wananchi wote wa Zanzibar.

Kiongozi huyo pia  alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika nyanja mbali mbali kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.

Kikao cha tano cha cha  baraza kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi visiwani hapa kimefungwa  jana na kinatarajiwa kufunguliwa tena mnamo tarehe 10 ya mwezi wa tano mwaka huu.
Viewing all 36103 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>