Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36103 articles
Browse latest View live

Gwiji wa Soka Duniani John Barnes Ainoa Timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Miaka 15 (SERENGETI BOYS)

$
0
0
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) katika siku yake ya kwanza nchini katika kuadhimisha miaka 100 ya benki ya standard Chartered tangu kuanzishwa kwake. “ni muhimu sana kwa kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huo ni wito kwa viongozi wa soka hapa Tanzania na wadau wote wa michezo kuweka nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni. ,,,,,, ni muhimu kama taifa kuwekeza kwa vijana kuwaweka mazingira na miundombinu ya kutosha kabisa ili kuweza kuinua vipaji vyao vya soka na ndio staili inayotumiwa na mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Barnes
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu nchini.
Katika siku yake ya tatu (leo) nchini gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambao watapambana vikali kuwania kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield mjini Liverpool nchini Uingereza. Barnes amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na kuwa tegemeo katika nchini yao. Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. “Tumeweza kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka 15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani, lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100 tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kwamba takribani timu 32 zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na timu mbili kutoka Uganda na Kenya. Mramba alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana wadogo. Kwa upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia. “hii ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana ni mastaa wa taifa wa baadaye,”
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa kwanza kushoto) wakionyeshana jambo kwenye viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Aidha, kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake. Aliongeza kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania. Gwiji hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati pia akimtambulisha gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpoool John Barnes (hayupo) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) iliyoendeshwa na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na miundombinu ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka nchini.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool, John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya miaka 15.
Pichani juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen wakiwatazama timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji huyo jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akibadilishana uzoefu na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen (kushoto) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.


Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Faida Mohammed Bakari Atembelea Wazee Waasisi wa CCM.

$
0
0

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Kisiwani Pemba Mhe. Faida Mohammed Bakari, akimsalimia Mzee Muasisi wa ASP na CCM Bi. Shinuna Salum Ali nyumbani kwake Wilaya ya Mkoani Pemba akiwa katika ziara yake kuwatembelea Wazee wa CCM kuwasalimia na kuwajulia hali zao
Picha na Habiba Zarali -Pemba.

Jitihada za Kimataifa Zahitajika Katika Kukabiliana na Uvuvi Haramu.

$
0
0

Na Ismail Ngayonga, Maelezo 
Dar es Salaam.

RIPOTI ya shirika la Chakula duniani (FAO) inasema asilimia 15 ya samaki wanaovuliwa duniani ambao ni sawa na tani Milioni 26 wanatokana na uvuvi haramu na hivyo kuleta tishio kwa uendelevu wa rasilimali za bahari na uhakika wa chakula.

Taarifa hiyo inazitaja nchi za Afrika Magharibi ikiwemo Guinea, Siera Leone, Morroco, Mauritania na Angola kuwa ni mataifa yaliyoshamiri vitendo vya uvuvi haramu kukiwa na idadi kubwa ya meli na makampuni yanayojihusisha na uvuvi haramu zinapofanya safari za majini.

Aidha utafiti uliofanywa na chombo cha Umoja wa Ulaya kilichoanzishwa kusaidia nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (CTA) unaonyesha kuwa  jumla ya hasara ya sasa inayotokana na uvuvi haramu duniani kote inakadiriwa kuwa kati ya dola bilioni tisa na 24 kwa mwaka.

Nchi zinazoendelea zipo hatarini zaidi kukumbwa na uvuvi haramu, huku jumla ya samaki wanaovuliwa kwa njia haramu katika Afrika Magharibi pekee ikifikia hadi juu ya asilimia 40 kuliko samaki wanaoripotiwa.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo mwaka 2016 FAO iliandaa mkataba wa kimataifa kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu ambao tayari umeridhiwa na nchi 30 na hivyo kuanza kutumika kisheria, ambapo unalazimisha nchi wanachama kuhakikisha boti zote zinazoingia bandarini nchini mwao zinaheshimu kanuni za uvuvi endelevu.

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa bahari, mito na maziwa imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za mashirika ya kimataifa katika kupiga vita tatizo la uvuvi haramu, ambao unaendelea kuathiri mazalia ya samaki sambamba na uchafuzi wa mazingira ya bahari.

Uvuvi haramu unatajwa kushamiri zaidi katika maeneo mengi ya pwani kuanzia Dar es Salaam, Mtwara hadi Tanga, hatua inayoisababishia Serikali kukosa mapato ya fedha za kigeni pamoja na kudumaza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inasema sekta ya uvuvi inachangia asilimia 2.4 yapato la taifa wakati ukuaji wake ni wa kiwango cha asilimia 5.5 kwa mwaka na kutoa ajira ya kudumu kwa wavuvi 185,000.

Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwahimiza wavuvi kuzingatia sharia, kanuni na taratibu zilizopo, baadhi ya wavuvi wamekuwa wakitumia zana na vifaa vya uvuvi zisivyo rasmi ikiwemo nyavu, matumizi ya mabomu ya sumu na hivyo kupelekea tishio la kupotea kwa rasilimali hizo muhimu.

Hivi karibuni Serikali ilitangaza operesheni maalum kwa kuunda kikosi kazi maalum kinachojumuisha Wizara saba ikiwa ni mkakati maalum wa kupambana vikali na wavuvi haramu pamoja na waigizaji, wauzaji na watumiaji wa zana zisizoruhusiwa katika uvuvi.

Kikosi kazi hicho kinahusisha Wizara mbalimbali ikiwemo OfisiyaRais- TAMISEMI, Ofisi ya Makamu waRais-Mazingira, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa, Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea soko la kimataifa la samaki lililopo Feri Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo, Mifugo naUvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema hakuna namna nyingine ya kukabiliana na vitendo hivyo haramu zaidi ya kuweka adhabu kali kwa wanaotiwa hatiani.

“Baadhi ya makosa ya uvuvi haramu kuwa ni uhujumu uchumi au ugaidi wa silaha (terrorism) kwa vile wanatumia milipuko  au mabomu na kumaliza mazalio ya samaki na kutishia wafanyakazi wa Serikali wanaofuatilia masuala hayo” anasema Dkt. Tizeba.

Kwa mujibuwaDkt. Tizeba anasema Serikali imebaini mapungufu yaliopo katika  sheria zilizopo, hivyo imejipanga kuwasilisha mabadiliko Bungeni  ambapo, itaamuliwa  kwa kiasi gani wataweza kuwabana wavuvi walio waharibifu na wavunjaji sheria.

Anasema sekta ya uvuvi nchini inatawaliwa na sheria kuu mbili za Sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003 na Sheria ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 2009, ambazo hazimfanyi mtu kuacha uvuvi haramu lakini iwapo adhabu itaongezwa, wengi wataogopa.

Anaongeza kuwa mikakati hiyo ya Serikali imekuja baada ya sheria na kanuni zilizopo kushindwa kupambana kikamilifu na vitendo vya uvuvi haramu vinavyotishia ukuaji wa sekta ya uvuvi nchini.

Aidha anasema Serikali itafanya mabadiliko ya sheria zinazosimamia uvuvi kwa kuyaainisha baadhi ya makosa ya uvuvi haramu kuwa ni ya uhujumu uchumi, ili kuongeza adhabu iwe kali kwa watu wanaotiwa hatiani kwa makosa hayo.

Waziri Tizeba anaongeza kuwa Serikali inaendelea na operesheni zake za kudhibiti uvuvi haramu katika mnyororo wote wa thamani kwa maana kutoka kwa watengenezaji zana haramu, wanaoziingiza nchini, wasafirishaji na wavuvi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Yohana Budeba anasema Serikali imenunua boti nane za kisasa zenye thamani ya Tsh. Milioini 640 kwa ajili ya kuongeza nguvu ya doria na kupambana na uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali ya uvuvi nchini ikiwemo maziwa makuu ya Victoria, Nyasa na Tanganyika.

Dkt. Yohana Budeba anasema boti nne kati ya hizo zimenunuliwa nchini Afrika Kusini na nyingine zinaendelea kutengenezwa hapa nchini katika kituo cha kunduchi ikiwa ni jitihada za Serikali za kukabiliana na Uvuvi haramu ambao umeanza kutishia kutoweka kwa baadhi ya samaki katika Mito, MaziwanaMabwawanchini.

KuhusuuvuviwasamakikatikamajiyabahariKuu, Dkt. Budeba anasema Serikali imeanzisha kituo cha udhibiti wa uvuvi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari kuu ambacho kitasaidia nyendo za vyombo vya uvuvi wakiwemo wavuvi wa kimataifa wanaoingia kuvua samaki kinyume cha sharia na taratibu za nchi.

Mazao ya samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania wengine na taifa kwa ujumla, lakini pia samaki wanachangia katika kuwapatia lishe na kwa sababu hiyo matumizi endelevu ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana.

Usimamizi endelevu na ulinzi wa bahari na mazingira ya pwani na viumbe hai ni jambo muhimu ili kuiepusha jamii na athari mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Aondoka leo Nchine Kwenda Nchini Indonesia Kumuwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli Katika Mkutano wa (IORA).

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi  zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),[Picha na Ikulu.] 04/03/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo wakati alipokuwa akiondoka   Nchini  kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi  zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),katika safari hiyo akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Mawaziri na Viongozi mbali mbali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka Nchini leo kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi  zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi  zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA.

Rais wa Zanzibar Dk Shein Ameondoka Leo Kulekea Nchini Indonesia Kuhudhuria Mkutano waKwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA)

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                                                                            04.03.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anaondoka nchini leo kwenda nchini Indonesia kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA)

Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kuanza Jumaapili ya tarehe 05 Machi na kumalizikia tarehe 07 Machi mwaka huu, mjini Jakarta Indonesia ambao utatanguliwa na vikao vya Mawaziri na wadau wengine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA).

Malengo ya mkutano huo ni kuendeleza ushirikiano baina ya nchi wanachama kupitia maeneo ya vipaumbele ambavyo ni Biashara na Uwekezaji, Usafiri wa Bahari, Uvuvi, Menejimenti ya Udhibiti wa Majanga, Taaluma, Sayansi na Teknolojia, Utalii na Utamaduni ambapo mada mbali mbali zitajadiliwa.

Pamoja na vipaumbele hivyo, hivi karibuni Jumuiya imeongeza maeneo mawili mtambuka ambayo ni Uchumi wa Bahari na masuala ya Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.
Mbali ya kuhudhuria mkutano huo, Dk. Shein atashiriki katika utiaji saini wa Mkataba unaoainisha mikakati, mipango na maazimio yanayolenga kuongeza kasi ya maendeleo ya Jumuiya hiyo kwa kuanisha mafanikio na changamoto zake.

Miongoni wa Wajumbe wanaofuatana na Rais Dk. Shein katika mkutano huo, ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa, Haji Ussi Gavu, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Hamad Rashid Mohammed, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afika Mashariki, Dk. Susan Alphonce Kolimba.

Wengine ni  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi na Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa pamoja na watendaji wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurejea nchi tarehe 9 Machi, 2017.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Dk. Shein aliagwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Madiwani Kisiwani Pemba Wapewa Elimu ya Utendaji wa Kazi Zao Kujua Sheria Mbalimbali.

$
0
0
Mkurugenzi Uratibu wa Tamisemi Zanzibar, Khalid Omar Abdulla, akifafanuwa jambo kuhusiana na mambo mbali yanayohusiana na kukasimu madaraka kwa Madiwani Zanzibar na mabadiloko yake huko katika mafunzo ya Madiwani wa Pemba Chake Chake -Kisiwani humo.
Ofisa Mwandamizi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zanzibar, Abrahaman Mnoga, akisisitiza jambo kwa madiwani kuhusiana na sheria mbali mbali za Tawala za mikoa Zanzibar na majukumu ya madiwani  huko katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba.
Madiwani Kisiwani Pemba, wakisikiliza kwa makini mafunzo wanayopatiwa juu ya kukasimu madaraka kutoka kwa maofis wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Zanzibar, katika hafla iliofanyika huko katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba.
Madiwani Kisiwani Pemba, wakisikiliza kwa makini mafunzo wanayopatiwa juu ya kukasimu madaraka kutoka kwa maofis wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Zanzibar, katika hafla iliofanyika huko katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba.
Picha na Bakari Mussa Pemba.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Mabalozi wa Tanzania Nchi za Nje.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mabalozi Saba Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenda kuliwakilisha Taifa katika Nchi mbali mbali Duniani.
Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na Mabalozi wapya wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif waliokaa ni Balozi Pindi Chana anayekwenda Kenya, Balozi Grace Mgwano anakwenda Uganda na upande wa Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Matilda Masuka anakwenda Korea Kusini na Balozi Fatma Rajan anakwenda Nchini Qatar.
Waliosimama kutoka Kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji anakwenda Nchini Sudan Balozi Joseph Sokoine anakwenda Nchini Belgium na Balozi Abdulla Kilima anakwenda Nchini Oman.
Picha  na - OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR.
Mabalozi wanayoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mataifa Rafiki Ulimwenguni wataendelea kuwa na jukumu la kuitunza Heshima ya Tanzania katika misingi imara itakayoimarisha Uhusiano mzuri uliopo kati ya pande hizo mbili.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga wakati akiwaaga Mabalozi Saba wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Nchi katika Mataifa tofauti Duniani uliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Balozi Seif Ali Iddi alisema yapo mafungamano mazuri ya muda mrefu yaliyopo baina ya Tanzania na Nchi Rafiki ambazo Wanadiplomasia hao wa Tanzania  wana kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba uwajibikaji wao unaleta tija na faida kwa mafungamano hayo katika pande zote mbili.

Balozi Seif aliwaeleza Mabalozi hao kwamba Mataifa ya Qatar, Oman, Uganda, Kenya, Belgium na Korea Kusini yamekuwa mshirika mkubwa na Tanzania katika kuimarisha Sekta za Maendeleo zinazosaidia kustawisha maisha ya Wananchi.

Alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inahitaji kuendelea kuungwa mkono na Mashirika na Taasisi za Mataifa hayo ambapo Mabalozi hayo watakuwa na jukumu la kufanya ushawishi utakaopelekea azma hiyo inafanikiwa vyema.

Akigusia Nchi ya Sudan   ambayo Tanzania imeamua kufungua tena Ubalozi wake baada ya kuufunga katika miaka ya 90 kutokana na hali ngumu ya uchumi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtaka Balozi atakayesimamia Ofisi hiyo kufanya juhudi katika kuhakikisha fursa za masomo zilizokuwa zikitolewa na Nchi hiyo zinarejea kama kawaida.

Alisema Sudan ni Nchi iliyokuwa ikiifadhili na kuisaidia sana Tanzania na Zanzibar kwa jumla nafasi nyingi za masomo hasa katika fani za Elimu ya Dini ya Kiislamu na Historia.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake Balozi wa Tanzania Nchini Oman Balozi Abdulla Kilima alisema jukumu walilokabidhiwa na kukubali kulibeba watahakikisha wanalitekeleza kwa nguvu zao zote.

Balozi Kilima kwa niaba ya wenzake wamewaahidi Watanzania kwamba watazingatia kuilinda Heshima iliyopo ya Taifa lao inayoendelea kushamiri katika Nyanja za Kimataifa.

Mabalozi aliyozungumzao nao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kuwaaga ni pamoja na Balozi Pindi Chana anayekwenda Nchini Kenya, Balozi Silima Kombo Haji anayekwenda Sudan na Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Nchini Belgium.

Wengine ni Balozi Abdulla Kilima anayeiwakilisha Tanzania Nchini Oman, Balozi Matilda Masuka atakayekwenda fungua Ubalozi Mpya Nchini Korea Kusini, Balozi Grace Mgwano anayekwenda Nchini Uganda na Balozi Fatma Rajab anayekwenda Nchini Qatar.

Mkutano wa Kikao cha Baraza Kuu Maalum la UVCCM Taifa Kufanyika Marchi 09,2017 Mjini Dodoma.

$
0
0
Na.Fadhili Siraji.
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) , umepanga kufanya kikao cha Baraza kuu  Maalum , Machi 09, 2017  kitakacho tanguliwa na kikao cha kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu  UVCCMTaifa mjini Dodoma .
Taarifa iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka,imesema kikao hicho Maalum kinafanyika kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya marekebisho ya kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho yanayo tarajiwa kufanyika katika katiba ya Chama Cha Mapinduzi Toleo la 1977 marekebisho ya 2017.
Aidha Baraza kuu Maalum Litafanya mabadiliko ya Miongozo na taratibu za Umoja wa Vijana CCM.

Mabadiliko na Maboresho ya kanuni na Miongozo hiyo ni kuendana na matakwa ya katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

 Ifuatayo ni Taarifa rasmi, tafadhali isome upate taarifa kwa kina...



Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Gati Namba 2 Katika Bandari ya Mtwara Pia Afungua Jengo la Kituo cha Kibiashara Cha Benki ya NMB Mtwara.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa  Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa  Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko akitoa maelezo kwa Rais Dkt. John Magufuli kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Gati namba 2 litakalojengwa katika bandari ya Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Newala George Huruma Mkuchika mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari ya Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiaria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Biashara cha Benki hiyo mkoani Mtwara 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego wakipiga makofi mara baada ya kufungua kituo hicho cha Kibiashara cha NMB mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara baada ya kukifungua kituo hicho cha kibiashara mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma mara baada ya kufungua kituo hicho cha kibiashara cha Benki ya NMB mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mnolela ambapo pia amechangia kiasi cha Shilingi milioni 15 na akamuagiza Mbunge huyo kuchangia Shilingi milioni 10 kutoka fedha za jimbo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika kijiji cha Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mbunge mteule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimamishwa njiani na Wanakijiji wa Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU

Ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Mhe.Hamad Masauni.

$
0
0
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katikaeneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu
Katibu wa Kamati Maalumya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza naMkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma(kushoto), baada ya kutembelea eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo  ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika  ambapo Katibu huyo wa NEC  ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole, akimueleza Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea eneo la Mwanyanya Mikoroshini.Picha na Abubakari Akida

Taarifa ya Kuwatafuta Jamaa Zake Mzee Alinanoswe Anawatafuta Ndugu Zake Walioppotezana Miaka Kumi Iliopita

$
0
0
Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake  baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.
Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
 
Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.
Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,
Namba

0713 562954 Augustino Michael
0789682901 Lister Godfrey
0789421644 Frank Michael
0718 528632 Frank Michael
0769 56 2954 Augustino Michael.

Mchezo wa Ufunguzi wa Kombe la Karume Cup Uwanja wa Gymkhana Kasti ya Timu ya Mafunzo na African Magic Wanawake Mpira wa Kikapu. Timu ya Mafunzo Imeshinda kwa Vikapu 56-49.

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Mafunzo akimpita mchezaji wa Timu ya African Magic, wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Wanawake mchezo uliofanyika katika uwanja wa Gymkhana Zanzibar Timu ya Mafunzo imeshinda kwa Vikapu 56 - 49.

Katika mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika leo jioni timu hizo zimeonesha mchezo wa hali ya juu kwa mchezo safi na wa kujiamini kila upande kwa kuonesha umahili wa kujiandaa na michuano hiyo ya Karume Cup.kwa upande wa Wanawake.

Kipindi cha robo ya kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa na vikapu 15 - 14 Timu ya Mafunzo ilikuwa ikiongoza kwa kikapu kimoja   

Katika robo ya tatu timu hizo zilikuwa na Vikapu 25 - 27 Timu ya Mafunzo ilikuwa mbele hadi kipenga cha mwisho wa mchezohuo timu ya mafunzo imetoka kifua mbele kwa vikapu 56 - 49.

 Michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo saa 8 kati ya New West Vs KVZ  na saa 10 kutakuwa na mchezo kati ya Timu za Nyuki na African Magin zote kwa upande wa Wanaume.

Timu zinazoshiriki kwa Upande wa Wanawake ni Duma, Mafunzo,JKU,KVZ na African Magic.

Kwa upande wa Timu za Wanaume Kundi A litakuwa na Timu Beit El Ras, KVZ, Rangers, Polisi Mbuyuni na New -West 

Kwa upande wa Kundi B litakuwa na Timu za Nyuki, Usolo, African Magic, JKU, Stone Town na Zanzibar Kwerekwe.




















Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Afungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu (BOT) Pamoja na Nyumba za NHC Mkoani Mtwara.

$
0
0
Sehemu ya Nyumba hizo za Gorofa za Shirika la Nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha Leo mkoani Mtwara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kufungua rasmi Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma kabla ya kufungua rasmi Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya watoto  mkoani Mtwara waliomfata kumsalimia mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Picha na Ikulu.

Azania Kuwakilisha Afrika Mashariki England.

$
0
0
WATANZANIA wamepata nafasi ya kuwakilisha Afrika Mashariki katika uwanja wa mpira wa Anfield unaotumiwa na Liverpool baada ya timu iliyokuwa inawakilisha ya Azania Group kutwaa ubingwa wa Standard Chartered 2017. Katika michuano hiyo iliyohusisha klabu zilizoingia fainali kutoka Tanzania, Kenya na Uganda mwakilishi wa timu ya Liverpool mchezaji Gwiji John Barnes na mabalozi wa Uingereza, Uganda na Kenya, Azania ilionesha kandanda safi . Azania imepata nafasi ya kutwaa kombe hilo katika Mashindano hayo ambayo yanajulikana kama ‘Standard Chartered-Road to Anfield Tournament’ kwa tofauti ya magoli katika kipute ilichokipiga na Capital FM katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam jana. Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (katikati) wakati wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)[/caption] Azania Group of Companies ambayo ilikuwa inawakilisha Tanzania ilijikusanyia pointi saba kama ilivyokuwa Capital FM kutoka Kenya lakini waliweza kupata nafasi kutokana na kujipatia magoli matatu zaidi dhidi ya Kenya ambao walikuwa na magoli mawili. Mpira huo ambao ulichezwa kwa dakika tano kila upande ulikuwa mkali na ambao ulishindwa kutoa utabiri wa wazi nani ataibuka mshindi na hivyo kupata nafasi ya kuingia uwanja wa Anfield Mei mwaka huu kuangalia mechi za Liverpool. Baada ya kila timu kuicheza mechi tatu katika raundi ya kwanza na kila mmoja kujipatia pointi tatu waliingia katika raundi ya pili. [caption id="attachment_624" align="aligncenter" width="1404"]Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (mwenye kofia) akizungumza na timu ya Capital FM baada ya kuwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.[/caption] Katika michuano hiyo Coca cola ya Uganda ilicheza dhidi ya Azania Group of Companies na kuondolewa mapema katika michuano hiyo pamoja na watu wake kuwa na miili ya soka. Kutokana na Uganda kuondolewa mapema, Azania waijikuta wakikabiliana na washindi wa mwaka uliopita mabingwa wa Kenya. Kenya walicheza mpira ambao ulileta taabu sana, mpira wa kujihami na hivyo kutibua mbinu waliyokuwa nayo Azania ambao walitaka kumaliza game mara moja. Unaweza kusema kwamba kipa wa Capital FM’s, Shafi Sudi ndiye alikuwa staa wa mechi kutokana na kufanikiwa kuzuia kasi ya mashambulizi kutoka Azania yaliyokuwa yakiongozwa na Nahodha Shabaka Hamis.Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na timu ya Coca cola kutoka Uganda mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park kushuhudia fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.[/caption] Kutokana na fainali hizo kutokuwa na mfumo wa penati timu ambayo inamaliza gemu ikiwa na pointi zaidi huwa ndio washindi na katika hilo Watanzania ndio wawakilishi wa timu za Afrika Mashariki katika uwanja wa Anfield. Kutokana na ushindi huo Capital FM wanakuwa wa pili na nafasi ya tatu inashikwa na Coca cola ya Uganda. Akizungumza baada ya gemu kumalizika, Rajab Ali ambaye ndiye aliyeibeba Azania Group alisema kwamba alikuwa na furaha kubwa kwenda kuishuhudia Liverpool FC ikikipiga katika uwanja wa Anfield kwani ndilo ilikuwa nia yao kubwa.Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes (katikati) akiwasili pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba walipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.[/caption] Naye nahodha wa Capital FM, Lassie Atrash alisema kwamba wameshindwa kufanya vyema kwa kuwa uwanja ulikuwa mdogo. Hata hivyo alisema ulikuwa ni mchezo safi na mshindi ilikuwa lazima apatikane na kusema kwamba ana matumaini kuwa Azania itawawakilisha vyema Afrika Mashariki huko England. Awali mchezaji John Barnes akizungumza kabla ya michezo hiyo alisema anafurahishwa na kutambua kwamba soka linatengenezwa Afrika Mashariki na hivyo kuondoa dhana potofu kwamba soka katika Afrika linapatikana Afrika magharibi pekee.Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akitambulishwa kwa Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza, Daniel Rathwell alipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.[/caption] Alisema kwamba amefurahishwa na kuona kwamba Liverpool imepata mashabiki wengi kutoka Afrika ambao wanatengeneza familia ya timu hiyo katika sera iliyoanzishwa miaka ya 1960 ya kuwa na wapenzi na mashabiki wa damu wa timu hiyo. Aidha alizungumzia uhusiano wao na walezi Standard Chartered na kutabiri kwamba Tanzania itaibuka washindi kutokana na yeye kuwapo Kenya mwaka uliopita na Kenya kufanikiwa kwenda England kuishuhudia Liverpool. Pamoja na mchezaji huyo mahiri wa zamani wa Liverpool kuzungumza katika fainali za tuzo hizo, wapenzi wa michezo pia walipata kusikia nasaha kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Balozi wa Uganda na mwakilishi wa Kenya. Meza kuu kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered Road to Anfield 2017, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza, Daniel Rathwell, Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande.Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akiwasalimia washiriki wa fainali mashindano hayo ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.Timu ya Coca cola Uganda ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano hayo.Timu ya Capital FM kutoka Kenya ikiimba wimbo wa Taifa kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es SalaamKikosi cha timu ya Azania Group of Companies wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es SalaamMtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa na vijana wake kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano hayo.Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha katika picha ya pamoja na timu ya Coca cola kutoka nchini UgandaMeza kuu ikisalimiana na wachezaji na kuwatakia kheri ya mchezo mwema.Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande katika picha ya pamoja na timu ya Capital FM kutoka Kenya.Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akijumuika na wadau wa soka kupasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi za fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth ParkMtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akibadilishana mawazo na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes wakati wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya JK Youth Park.Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017.[/caption] [caption id="attachment_640" align="aligncenter" width="1404"]Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akitoa salamu kwa washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwasalimu washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.Mwakilishi wa Ubalozi wa Uingereza, Daniel Rathwell akizungumza kwa niaba ya balozi wake kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield yaliyofanyika katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, akitoa salamu za TFF kwa wageni waalikwa na washiriki wa fainali za mashindano hayo.Wafanyakazi wa Standard Chartered Bank na wadau wa soka waliohudhuria fainali za mashindano hayoMtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akitazama vijana wake walipokuwa uwanjani.Benji la ufundi la Azania Group of CompaniesMechi ya utangulizi kati ya mashabiki wa timu ya Liverpool (tisheti nyeupe) na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered (vesti nyekundu) ambapo mashabiki wa timu ya Liverpool waliinyuka benki hiyo bao 1-0.Kiungo wa timu ya Azania Group of Companies, Rajabu Ali akiwatoka wachezaji wa timu ya Coca cola kutoka Uganda.[/caption] [caption id="attachment_649" align="aligncenter" width="1404"]Nahodha wa Capital FM, kutoka Kenya, Lassie Atrash akizungumzia mchezo ulivyokuwa kwa wanahabari mara baada ya fainali hizo kuisha na Tanzania kuchukua ubingwa.Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda (kulia) na watoto wake katika picha ya pamoja na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es SalaamMashabiki wa Liverpool wakiimba wimbo "You'll never walk alone" pamoja na Gwiji huyo John Barnes.Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (katikati) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa waamuzi wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyofanyika jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akiwavisha medali washindi watatu timu ya Coca cola ya Uganda katika mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.[/caption] [caption id="attachment_658" align="aligncenter" width="1404"]Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayoBalozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwavisha medali washindi wa pili wa Standard Chartered road to Anfield 2017 timu ya Capital FM kutoka Kenya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa pili kushoto) na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba wakiushuhudia tukio hilo.[/caption] [caption id="attachment_658" align="aligncenter" width="1404"] Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo.[/caption] [caption id="attachment_660" align="aligncenter" width="1404"]Picha ya pamoja na washindi wa pili wa mashindano hayo timu ya Capital FM kutoka Kenya.Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes akimvisha medali Nahodha wa Azania Group, Shabaan Hamis baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa 2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (kulia) akikabidhi kombe kwa timu ya Azania Group of Companies kutoka Tanzania, ambao ni mabingwa wa mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (aliyezibwa).Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akiselebuka pamoja na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania, mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana. Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (aliyezibwa)Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akifurahi pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania (walioko mstari wa nyuma) mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.Wengine pichani ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko Juanita Mramba (wa pili kushoto), Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (wa tatu kushoto), Balozi wa Uganda nchini Mh. Dorothy Hyuha, (wanne kushoto) na Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda na Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kushoto).Abdullah Zulu Lyana (katikati) katika picha ya pamoja na mashabiki wenzake wa timu ya Liverpool.

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi Wanalalamikia Uvuvi Haramu Katika Bahari Yao na Kwenda Maeneo ya Mbali Kuvua.

$
0
0
Mwananchi Mvuvi swa Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya makampuni katika ukanda wao wa bahari ya nungwi kwa kutumia bunduki na mishare wakati wa uvuvi wao na kuwakimbiza samaki katika maeneo hayo na wao inawalazimu kwenda kuvua seheme ya mbali na eneo hilo kutokana na samaki kukimbilia maeneo mengine, wameitaka taasisi husika kulichunguza hili. ili mkuepusha uvuvi huo haramu katika pwani yao.
Mwananchi wa Kijiji cha nungwi Unguja akizungumza na waandishi wa habari kero yao kwa waandishi kutokana na kukithiri vitendo vya uvuvi haramu jua Serikali inapiga vita uvuvi huo bado kuna watu wanatumia bunduki na mishare katika uvuvi huo.Wao wameachana na uvuvi haramu wa kutumia nyavu za matundu madogo na kuendelea kuvua kwa uvuvi unaotakiwa na Serikali kwa kutumia nyavu za macho makubwa.  

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi wakiwa katika eneo la ufukwe wa bahari hiyo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika ukanda huo wa pwani ya nungwi wakiwa katika kazi zao za kawaida.


Kongamano la Baraza la Vijana wa Shehia ya Miembeni Zanzibar Kupinga Udhalilishashi wa Wanawake na Watoto Zanzibar.

$
0
0
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Dkt. Sira Ubwa Mwamboya akiwahutubia Vijana wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni Zanzibar katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 March. 
Mlezi wa Baraza la Vijana Miembeni Mhe Mgeni Hassan Juma akitowa nasaha zake wakati wa Kongamano hilo la Vijana wa Miembeni Zanzibar kupiga Vita Vitendo vya Uzalilishaji wa Wanawake na Watoto vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.


 Mratibu wa Kongamano Baraza la Vijana wa Miembeni kutoka Taasisi ya Wanasheria Wanawake Zanzibar ZAFELA Jamila Mahmoud akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mtoa Mada kutoka Jeshi la Polisi Kituo cha Nga'mbu Dawati la Wanawake na Watoto akitowa mada kuhusiana na vitendo vya uzalilishaji wanavyofanyiwa watoto na wanawake Zanzibar.

PBZ YAKABIDHI MSAADA KWA MADRASATUL ISLAMIA TARABBIYYA KIGONGONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo Mbalimbali Jijini Dar Leo.

$
0
0
Baadhiya Maofisa wa Serikali na Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati akitoa taarifa ya operesheni maalum ya kutokomeza pombe kali aina ya viroba mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba (katikati) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya operesheni maalum ya kutokomeza pombe kali aina ya viroba mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni. Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Mayungi na kushoto ni Kaimu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya.Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo

ZIARA YA KATIBU WA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC, IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA, MHANDISI HAMAD MASAUNI JIMBONI WELEZO ZANZIBAR

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Welezo, Mhe.Saada Salum Mkuya akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni (wa kwanza kulia), ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja
Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa ziara Jimboni Welezo, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, kufuatilia maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji.Kushoto ni Mstahiki Meya wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja, Hamza Khamis Juma. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja
 Mjumbe wa kamati ya Siasa Jimbo la Welezo, Ayub Saleh, akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji.Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Welezo, Saada Salum Mkuya. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja
Mwakilishi Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi, Shawana Buheti, akibadilishana mawazo na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa Jimbo la Welezo, Sada Salum Mkuya (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya Katibu huyo ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji, Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja. Picha na Abubakari Akida.


Fundo karibuni kupata Umeme Zeco yafunga Transfoma

$
0
0
 MAFUNDI wa shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakifunga Tansfoma katika kijiji cha Ndooni Kisiwani Fundo, ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha kisiwa hicho kinapata huduma ya Umeme ya uhakika.



(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAFUNDI wa Shrika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, wakipachika Tansfoma katika moja ya vituo huko katika kijii cha Kimeleani Kisiwani Fundo Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Na Mwandishi wetu

Zoezi la usambazaji wa nguvu ya umeme katika Kisiwa cha FUNDO linaendelea kwa kasi huku uongozi wa shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ukiahidi kulikamisha kwa wakati.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia maendeleo ya zoezi hilo afisa uhusiano wa ZECO Pemba Amour Salim Massoud amesema tayari wameshafunga trasfoma nne na kujenga line kubwa na kwasasa wanalenga kujenga line ndogo kwa ajili ya kuwashushia wananchi.

Amesema mafundi wa shirika kwa kushikiana na wananchi wa Fundo wamekuwa wakifanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha zoezi hilo linamalizika kwa muda uliopangwa.

Nao baadhi ya wananchi wa fundo wameelezea kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na kuwaomba mafundi wa shirika la umeme ZECO kujitahidi kukamilisha uwekaji wa line hizo ili waanze kukamilisha usajili na kujiungia huduma hiyo ya umeme.


Aidha wameuomba uongozi wa ZECO kutoa elimu kwa wananchi wa FUNDO juu ya matumizi salama ya umeme na kuepuka ajali zisizo za lazima.
Viewing all 36103 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>