Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zanzibar kuchimba mafuta bila kuingiliwa

$
0
0

Na Hamad Shapandu, Karagwe
RASIMU ya katiba mpya kama itapitishwa kuwa katiba, itatoa mamlaka kwa Wazanzibari kuchimba mafuta yao bila woga wala kuingiliwa.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Admund Mungi, alisema hayo wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati akizungumza na Wakurugenzi, Mameneja na Wajumbe wa Bodi za redio jamii Tanzania.

Alisema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linatarajiwa kukaa mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu kupitisha sheria ya mpito itakayotoa nafasi ya kupatikana serikali ya Tanzania Bara.

Aidha alisema migogoro mingi ambayo haikupatiwa ufumbuzi na tume mbalimbali zilizoundwa hapo kabla ina nafasi kubwa yakupatiwa ufumbuzi sasa iwapo rasimu ya katiba, itaidhinishwa kuwa katiba.

Alisema hiyo ni nafasi pekee kwa Watanzania kuijadili rasimu hio na kutoa michango yao kwa wajumbe wa mabaraza ya wilaya.

Alionya kwamba maamuzi ya serikali kwamba Tanzania iwe na katiba mpya yasipotumiwa vizuri, huenda ikachukua pengine miaka 50 mingine kupata katiba mpya.

Alisema rasimu hiyo,imebainisha wazi kuwa katiba itaenzi tunu za taifa ikiwemo utu,uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi,uwajibikaji na lugha ya taifa ili wananchi wanufaike na nchi yao.

Alisema kwa kuzingatia gharama kubwa za kuendesha serikali, Tume imeandaa rasimu yenye serikali tatu na kusisitiza kuwa wshiriki katika serikali ya shirikisho (Serikali ya Zanzibar na Tanzania Bara) hazitakuwa dola, badala yake dola itabaki kuwa serikali ya Shirikisho.

Dk. Mungi alisema redio jamii zina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii umuhimu wa katiba mpya ambayo ikipita italeta ufumbuzi wa kero nyingi ambazo Watanzania wa pande zote mbili wanakumbana nazo.

Mapema Mratibu wa Tume hiyo, Abdalla Mitawi alisema tume inakusudia kuonana na viongozi wa redio za jamii Tanzania kwa lengo la kuzitumia redio hizo ambazo ni tegemeo la wananchi kupata habari muhimu ili zitumike kuelimisha jamii juu ya mchakato mzima wa kupatikana katiba mpya.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>