Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mama Shein asaidia ‘sober house’

$
0
0

Na Mwantanga Ame
MKE wa Rais wa Zanzibar, mama Mwanamwema Shein, amewataka vijana wanaoishi katika nyumba za kubadilisha tabia (sober house), kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kujifunza mambo mema zaidi ili waweze kubadili maisha yao.

Mama Shein, aliyasema hayo jana wakati akikabidhi msaada wa chakula cha futari kwa ajili ya nyumba tisa za vijana wanaoacha kutumia dawa za kulevya, makabidiano ambayo yalifanyika nyumbani kwake Mazizini.

Nyumba za kurekebisha tabia zilizokabidhiwa msaada huo ni ya Bububu, Nyarugusu, Zanzibar Youth Forum, Tawabina , Women sober house, Bombay sober house, Betroit sober house kwa Unguja na Pemba ni Chake Chake sober house na Wete sober house.

Msaada waliokabidiwa ni pamoja na unga, sukari, tambi, mafuta na tende ambao thamani yake ni shilingi 1,554,000, ikiwa msaada uliotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Mama Shein, alisema umoja wa wake wa viongozi umeamua kutoa msaada huo kwa kuthamini vijana wanaoishi katika nyumba hizo kwani na wao wanahitaji huduma nzuri katika mwezi Ramadhan.

Alisema mwezi wa Ramadhani umejaa mafunzo yatakayoweza kuwaweka sawa vijana wa nyumba hizo kurudi katika maadili na kufuata misingi ya dini na kuacha kufanya vitendo viovu.

Aliwataka vijana wa nyumba hizo kuendelea kushirikiana na serikali yao iko tayari kuwasaidia kumudu maisha yao.

Mapema mke wa Makamu wa Pili wa Rais, mama Asha Suleiman Iddi, alisema umoja wao utahakikisha unachangia kubadili maisha ya vijana wanaoishi katika nyumba hizo kwa kuwapatia misaada mbali mbali ya kijamii.

Aliwata vijana hao kutumia ushawishi wao kuwashauri vijana wengine ambao bado wanatumia dawa hizo kuachana na kujiunga katika nyumba hizo.

Alisema vyakula hivyo vitachangia kuwapunguzia makali ya kusaka futari katika mwezi wa Ramadhani ili kuwawezesha kuwa watulivu kumudu saumu zao.

Nae Msimamizi wa nyumba hizo, Fatma Sukwa, alimshukuru mama Shein kwa mchango anaoutoa wa kusaidia nyumba hizo kwani umewawezesha vijana kuwa karibu na serikali yao.

Alisema wengi wa vijana wanaoishji katika nyumba hizo bado wamekuwa wakipata unyanyasaji kutoka kwa jamii kutokana na kujengewa hofu ya kuwa bado ni wezi jambo ambalo ni tofauti.

Nae Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Zainab Mohammed, alisema ipo haja kwa serikali kutenga fungu maalum la kuzisaidia nyumba hizo.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>