Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Said Bakari Jecha kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 9(1)cha Sheria ya chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Namba 8 ya mwaka 1999
Aidha Dkt Shein amemteua Abdulrahman Rashid kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)
Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo alipewa chini ya kifungu Namba 8 (a) (1) cha sheria ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Namba 7 ya mwaka 1996 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 8 ya 2009.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee ,Uteuzi wa Said Bakar Jecha unaanzaa Julai 20,na uteuzi wa Abdulrahman Rashid unaaza Julai 18 mwaka huu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 19/07/2013