Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kikundi cha Taifa Taarab wamfurahisha JK, awatunza laki 5

$
0
0
 Na Mwandishi Wetu.
VIWANJA vya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, juzi usiku vilimeremeta na kugeuka kiota cha burudani kutokana na mirindimo  maridhawa ya muziki wa taarab asilia ulioporomoshwa na kikundi cha Taifa katika kusherehekea nusu karne ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk, Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Kikwete, waliungana na wananchi mbalimbali kuwashuhudia magwiji hao wa  taarab wakishusha kibao kimoja baada ya chengine, huku wakipulizwa na upepo mwanana uwanjani hapo.
Katika staili ya aina yake, kikundi hicho kilikuwa kikiongozwa na washereheshaji (MC) wawili, Chimbeni Kheri wa klabu ya Culture pamoja na Ali Masoud wa Nadi Ikhwan Safaa.
Pazia la burudani lilifunguliwa na mwimbaji Hilda Mohammed aliyeanza kwa wimbo maalum, Miaka 50 ya Mapinduzi, huku bibiye Fauzia Abdallah akihanikiza kwa kibao chake, Mapenzi yako matamu.
Waimbaji wengine waliotamba na kulitikisa eneo hilo ambako Mapinduzi ya 1964 ndiko yalikoanzia na nyimbo walizoimba zikiwa kwenye mabano, ni Khamis Nyange 'Profesa Gogo' (Lulu namba 2), Sihaba Juma (Faida za Mapinduzi na Mtumwa Mbarouk (Mpewa hapokonyeki, ombi la Rais Shein na Tunapendana).
Wengine ni Iddi Sued (Tusherehekee Mapinduzi), Khofu yako iondoe (Rukia Ramadhan) na Bahati (Fatma Issa) ambayo ilighaniwa baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis.
Kutokana na umahiri waliouonesha katika kucharaza vinanda na kuimba, sambamba na ufundi wa MC Chimbeni katika kulitawala jukwaa, wasanii hao walifanikiwa kumfanya Rais Kikwete atie mkono mfukoni na kuwadondoshea bahasha 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>