Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Jela miaka 15 kwa kubaka

$
0
0
Na Shemsia Khamis, Pemba
MAHAKAMA ya Mkoa ya Chake Chake Pemba, imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela, Issa Ali Mohamed (28) mkaazi wa Chanjaani, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo, Khamis Ramadhan Abdalla baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka.

Mbali ya adhabu ya kifungo gerezani, mshitakiwa ametakiwa kulipa faini ya shilingi 200,000 kwa mlalamikaji kutokana na maumivu aliyomsababishia.

Kabla ya mshitakiwa kupewa adhabu hiyo, aliiomba mahakama kwanza kumruhusu kurudi nyumbani kwenda kushughulikia mifugo yake ombi ambalo lilikataliwa na mahakama.

“Muheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu kunipa angalau wiki moja kwenda nyumbani kushughulikia mifugo yangu kwani haina mtu wa kuishughulikia hivyo nakwenda kumkabidhi mtu,” alidai.

Upande wa mashtaka kwa upande wake, uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani matukio ya udhalilishaji watoto yamekuwa yakiongezeka.

Ilidawa na Mwendesha mashtaka ,Ali Bilali Hassan, kuwa Mei 18 mwaka 2011 majira ya saa 7:00 mchana huko Chanjaani Chake Chake, mshitakiwa alimbaka mtoto huyo na kumsababishia maumivu na baadae kukimbia.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>