Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Chini waliofika Zanzibar kuangalia Sekta ya kuwekeza Vitega Uchumi Zanzibar, Ujumbe huo umefika Zanzibar kwa ajili ya kuwekeza katika Sekta ya Hoteli na Viwanda .
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China ya Asia Economy League Bwa. Bian. Hongdeng, akizungumza wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha Zanzibar kujitambulisha na kufanya mazungumzo ya kuwa na nia ya kuwekeza Zanzibar katika Sekta ya Viwanda na Hoteli za Kitalii Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Ujumbe kutoka China wakiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha Zanzibar,mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mkutano wa Wizara hiyo Vuga.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee, akitowa maelezo ya Ujio wa Wafanyabiashara kutoka China waliofika Zanzibar kuangalia sekta ya kuwekeza Kiuchumi katika nyanda mbalimbali Zanzibar.