Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tani 22 za karafuu zanunuliwa wiki moja

$
0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
TANI 22.521 za karafuu kavu zenye thamani ya shlingi milioni 315, 039,000 zimenunuliwa na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kisiwani Pemba katika kipindi cha wiki moja tokea kufunguliwa kwa msimu mpya wa ununuzi wa zao hilo.

Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Hemed Suleiman Abdalla alisema karafuu hizo zimenunuliwa katika vituo vyake vitatu vilivyopo Wete mjini, Mkoani na Chake Chake.

Aidha alisema shirika limetoa nafasi kwa masheha kutoa taarifa kwa Wakuu wa Wilaya wakati wanapohitaji kufunguliwa vituo katika maeneo yao na baada ya taarifa hizo kufika ofisini watakuwa tayari kufungua vituo kwa ajili ya ununuzi wa karafuu.

"Tayari tumefanikiwa kununua tani zaidi ya 22 katika kipindi hichi kifupi tokea kuanza msimu mpya wa ununuzi wa karafuu, na kwa sasa tumefungua vituo vitatu maeneo ya mijini na kwamba vituo vynegine vitafunguliwa kulingana na ongezeko la karafuu,” alisema.

Akizungumzia suala la magendo ya karafuu, alisema serikali haitakuwa na muhali juu yawatakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Alisisitiza kuwa kila mwananchi atakayepeleka karafuu zake ZSTC atapata asilimia 80 huku asilimia 20 inakwenda kwa serikali ambazo zitatumika katika huduma mbali mbali za maendeleo.

Alisema serikali imepandisha bei ya karafuu hadi shilingi 14,000 kwa kilo lengo likiwa ni kuboresha hali za maisha za wakulima na kuwataka wananchi kupeleka karafuu zilizo safi katika vituo vya ununuzi.

Baadhi ya wakulima waliozungumza na mwandishi wa habari hizi walisema kitendo cha Serikali cha kupandisha bei ya karafuu kimelenga kuwapunguzia ukali wa maisha ya kuongeza kipato chao.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles